_____________________ Ni Kwa sababu gani Mungu Anaruhusu Mateso? Why does God allow suffering? _____________________ Kufasiri: Simon Uswegi Kuumba: Carl Hinton Biblia inalojawabu kwa Msiba wa Mwanadamu Kwa nini Mungu Anaruhusu Mateso? - Biblia inalojawabu kwa msiba huu MATESO ni jambo gumu katika maisha yanapomjia kila mmoja. Mtoto anazaliwa kipofu, kilema au kuwa na mtindio wa ubongo; swali linajitokeza: Ni kwa sababu gani? Mtoto hajafanya lolote baya. Mwanamume au mwanamke mwenye sifa njema, aliye na maisha bora lakini maumivu yanamtesa sana kwa ugonjwa unaokatisha tamaa, hatimaye anaishia katika mauti tu. Kwa nini mwanamume au mwanamke ateseke? Hawa ni watu ambao wanaweza kuachwa wasidhurike. Watu mamilioni wanateseka, nusu kwa njaa na maradhi katika nchi zenye idadi kubwa ya watu na ardhi iliyo na rutuba duni. Wengine wanaangamia au wanakosa makazi kutokana na mafuriko na matetemeko ya ardhi. Ni kwa nini wateseke? Maumivu, kuteswa kikatili na mauti vimekuja kwa mamilioni ya watu wasio na matumaini kutokana na usultani wa binadamu na uharibifu unaoletwa na vita vya sasa. Maisha ya watu wengi yanapotea kutokana na vitendo vya kigaidi, kwa ukatili na utekaji nyara. Ajali zimekuwapo siku zote, lakini kiwango cha majanga na misiba mikubwa ya asili siku hizi mara nyingi inaangamiza: ndege za abiria zinaanguka; mashini za kuchimbia mafuta zinapasuka, moto unawaangamiza mamia katika treni inayosafiri chini ya ardhi. Watu wanauliza: Kwa nini Mungu anayaruhusu haya yatokee? Maswali yanazuka haraka sana katika akili na kwa upande mmoja yanaonekana ni ya maana: lakini yakitazamwa kwa unyoofu yanaonyesha kwamba yanachukuwa vidokeso fulani. Yanadokeza kuwa mateso katika maisha ya mwanadamu hayalingani aidha kwa nguvu au kwa upendo wa Mungu: kwamba kama ni Mungu mwenye upendo aidha hana uwezo wa kuzuia mateso, au ikiwa ana nguvu, basi hana nia, naye si Mungu mwenye upendo. Imesadikika kwamba kuzuia mateso kama ilivyo sasa ni dhahiri yanadhuru wasio na hatia ni jambo lingine tutarajie toka kwa Mungu mwenye upendo ambaye pia ni muweza yote. Je! kusadiki hivi kuna haki ? (1) Mambo Hakika ya Maisha Mambo mengine ya hakika juu ya maisha ni lazima yaangaliwe kabla ya kujaribu kufanya uamuzi 1.Maisha ya mtu ni ya kusudi la watu wote na matokeo na sababu fulani kubwa zisizoepukika. Moto huunguza, maji yanagharikisha, vijidudu vya magonjwa vinaangamiza. Mambo haya ya vidokezo vya uadilifu.Watu wanaishi katika ulimwengu ambao ndani yake matokeo ya mambo wanayoyafanya hayaepukiki, na kwa sababu hiyo wajibu wao kwa wafanyayo hayaepukiki sawia. Pasipo mzigo huu wa ‘sheria ya asili’ mwanadamu anaweza kufanya apendavyo bila hofu ya kuogopa kupata adhabu, na hakutakuwa na kuwajibika. Mungu alifanya ulimwengu jinsi hii kwa sababu ni Mungu mwadilifu awafanyaye watu kuwa viumbe wenye kuwa na wajibu na hiari kuchagua jinsi gani watatenda. 2.Kutotunza na kutumia vibaya mwanadamu maisha yake mwenyewe ameharibu mtiririko wa maisha yenyewe ya mwanadamu, ameacha maovu yanayoangukia katika vizazi vinavyofuata. Tena, hizi kama sehemu ya sheria ya asili, zenyewe zaweza kudhihirika kama udhaifu uliorithiwa na kuelekea katika ugonjwa. Jambo kabisa la maisha laweza kudhihirika kama lilivyopita toka kizazi hadi kizazi. 3.Matokeo ya vitendo vya mwanadamu si moja kwa moja vya mwili tu. Maovu ya jamii na katika siasa ambayo yameumbika katikati ya historia nzima yameacha mkusanyiko wa mzigo juu ya vizazi vilivyofuata. Leo watu wamenaswa katika wavu wa maatokeo ya historia iliyopita, na hata wanapojaribu kusahihisha jambo baya moja,lingine linazaliwa: “viumbe vyote pia vinaugua pamoja, navyo vina utungu pamoja hata sasa” ( Warumi 8:22 ) Je! Watu Wanajiokoa Wao Wenyewe ? Kwa kuangalia mambo haya , inabidi kuuliza, Kwa kweli tunafanya nini tunapotaka Mungu aondoe mateso? Je! hatumwombi Mungu ya kwamba (a) asimamishe kwa muda sheria ya asili, (b) ageuze matokeo ya urithi, na © kugeuza pembeni matokeo ya ukatili kwa binadamu ? Je! tuna haki kutarajia Mungu kuwaokoa watu toka katika matokeo ya vitendo vya kibinadamu ? Je! utakuwa ulimwengu wa uadilifu kama angefanya hivyo? (2) Maswali haya yanaweza kuulizwa tu kwa mazingira wakati mkono wa mtu ukihusika. Matetemeko ya ardhi, tufani, njaa na mafuriko ya maji yanaitwa ‘matendo ya Mungu’ kwa kuwa mara nyingi hakuna maelezo mengine kwa ajili ya kutokeo kwao. Hivyo kama tukitazama kupita matendo ya mwanadamu kwa ma-baa ya asili, tunaona ya kwamba ma-baa yanawakumba wote, wasio na makosa na wakosaji vile vile. Mara tukianza kuhoji mateso ya wasio na makosa kwa misiba hii mashaka mengine yanazuka. Je! tunasema ya kwamba misiba itakuwa ya kuchagulika katika utendaji kazi wake, itawatafuta tu hao wanaostahili kuteswa ? Ubaya au Dalili ? Kutokeza ubaya wote wa kufikiri juu ya mada ambayo imechunguzwa hadi hapo ni msingi mmoja unaojitanguliza: ni hayo mateso yana ubaya ndani yake yenyewe. Ni hii imani ya kwamba mateso ni uovu wa lazima ambao umelala kwenye shina la dini ya Budha. Mtazamo wa Biblia kimsingi upo tofauti: uovu au ubaya ndani yake wenyewe si mateso, bali ni dalili ya ubaya wa ndani kabisa.Maandiko yanaonyesha mateso kama matokeo ya dhambi: sio lazima ni dhambi ya mtu mmoja anayeteseka, lakini dhambi katika historia ya mwanadamu na katika jamii. Asili ya dhambi imeelezwa bayana na kwa kifupi na Mtume Paulo: “Kwa hiyo kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi” ( Warumi 5:12 ). Hukumu iliyotamkwa kwa mwanamke baada ya kuasi katika Edeni inasema: “Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala”. Kwa mwanamume Mungu akasema: “Kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maaana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” (Mwanzo 3:16,19 ). (3) Fundisho ni jepesi kueleweka. Kutokana na uasi wa Adamu, ukaja mvurugiko katika uhusiano kati ya Muumbaji na viumbe; uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu upo nje ya muunganiko. Dhambi ya kwanza ilileta badiliko kubwa ambalo limedhuru vyote kwa mabaya ambayo ni ya kawaida kwa mwanadamu. Mauti ni ya watu wote: Mungu harekebishi kifo kwa mtu mmoja mmoja katika kuchagua. Biblia inafundisha ya kwamba watu wameachwa katika njia zao wenyewe na sheria za asili, ingawa panaweza kuwepo nyakati hapo ma-baa ya asili yanaelekezwa na Mungu kama hukumu kwa mwanadamu na kwa kuisafisha nchi. Mfano wa kuonekana dhahiri ni gharika katika siku za Nuhu. Wakati uo huo ni kweli kwamba katika Biblia, kwa hao watafutao kumtumikia Mungu, kuteseka kunachukua maana nyingine; wao wapo katika uhusiano mpya na Muumbaji, watajifunnza kuona msiba kwa mwanga mpya. Ni nini ? Mtu wa Mungu Yaliyompata Jawabu linaweza kuonekana katika mfano wa Ayubu. Hapa ni mtu mcha Mungu aliyekumabana na janga la hasara ya mifugo yake - chanzo aha utajiri wake; na msiba wa kutisha wa kupotea watoto wake wote kwa mpigo; na halafu akapigwa na maradhi ya kuumiza yaliyomtenga na watu. Hata hivyo akasema: “Nini? Je! tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate mabaya ?” ( Ayubu 2:10 )Alitambua jambo kuu la asili kwamba hawezi kudai mema kama haki: si juu yake kuamua Mungu atafanya kitu gani. Shida ya Kuumiza Sana Kipindi kinakuja, ingawa hivyo, wakati mateso hayavumiliki hivyo kwamba kifo kinaonekana kupendelewa sana. Katika uchungu na kufadhaika akahoji, kwa matokeo: ni kwa sababu gani mtu aishi ikiwa ni kwa kuteseka tu ? Je ! Mungu anaweza, aliyemfanya mtu, anamwangamiza kama kitu cha kutupwa ? Rafiki wa Ayubu wakasema kwa kusisitiza kwamba upo muunganiko moja kwa moja kati ya kosa la mwanadamu na mateso yake na kwa sababu hiyo walishindana ya kwamba kuteseka mno Ayubu ni lazima alifanya dhambi kubwa. Ayubu akathibitishiwa unyoofu wake mwenyewe: ni binadamu, lakini anajua ya kwamba hana kosa la dhambi wanazojaribu kumshutumu. Hata hivyo anayo ya kutosha mawazo ya rafiki zake kuona sasa kuwa anateseka isivyo haki. Je! Mungu alimchagua awe shabaha yake ? Kwa sababu kulinganisha na wengine, mateso yake yaonekana makubwa kwa makosa yoyote anayoweza kukiri. (4) Kwake inaonekana kwamba maumivu yake yanaweza tu kuwa na maana ya kwamba Mungu amegeuka juu yake, na shida ya uadilifu wake inaongeza uchungu wake. “Hema za wanyang’anyi” zinafanikiwa: kwa sababu gani mwenye haki ateseke ? Kama Mungu anamhukumu ni haki kwamba ahukumiwe kwa kusudi ambalo hali ya mwanadamu hawezi kufikia ? Marafiki wakashindwa kabisa kutikisa uthabiti wa Ayubu katika haki yake na hatimaye wakakoma kubishana naye. Lakini shauri la Ayubu linalojitokeza ni imani ya mwisho kwa Mungu, mbali na maswali yote, na imani iliyo katika haki ya Mungu; na hivyo Ayubu anafikia katika tumaini ambalo ni maisha mengine, kama si sasa, Mungu akiwa ni Mkombozi wake atamthibitishia haki yake na kuwa upande wake. Hivyo akaingiza jambo jipya kwa kuthibitisha ukweli anapotazama mbele kupita kaburi hadi kwenye ufufuo na kupatanishwa. Imani hiyo, ilidokezwa kwa Ayubu, imeelezwa kabisa kila mahali sehemu zote mbili Agano la Kale na Jipya, nayo inatoa uhusiano mpya katika shida. Lakini yenyewe haielezi ni kwa nini wanaume na wanawake wateseke katika maisha haya Mungu akanena na Mwanadamu.. Marafiki waliponyamaza na Ayubu alipotoa hotuba yake ya mwisho, kijana Elihu akaingia katika mjadala. Akaonyesha ya kwamba Ayubu katika kikomo chake amenenea haki ya Mungu, lakini vile vile akatoa mwanga mpya juu ya tatizo. Mungu ananena na watu ( a ) kupitia ufunuo, na ( b ) katika mateso. Mungu, kwa njia zake mwenyewe, anazungumza na wanaume na wanawake na kuwavuta kwake ( soma Ayubu 33: 14-18 ). Mungu ananena na watu, amesema Elihu, kwa kuelimika kwao kiroho, mwongozo wao katika maisha na kulindwa kwao toka katika kuangamia. “Humwondoa mtu katika makusudio yake , na kumfichia mtu kiburi”’ Humwongoza mbali katika mwendo wa maisha ya kujidai mwenyewe binafsi, maana kiburi ni chanzo cha dhambi. Kama kwa njia zingine za kuwasiliana, Elihu anasema: “Yeye hutiwa adabu kwa maumivu kitandani mwake, na kwa mashindano yaendeleayo daima mifupani mwake; hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri. Nyama ya mwili wake huliwa, isionekane; na mifupa yake isiyoonekana yatokea nje. Naam, nafsi yake inakaribia shimoni, na uhai wake unakaribia waangamizi” (Ayubu 33:19-22 ). (5) Maelezo ya mateso kikamilifu yamfaa Ayubu, naye Elihu anasema ya kwamba hata akihitaji kutiwa adabu, kukaripiwa, kuadibishwa na Bwana - si kwa dhambi dhahiri walizodai rafiki zake kuwa za kweli, maana Elihu hazitaji, bali kwa makosa zaidi ya hila. Tayari Elihu amedokeza, maana ni dhambi ya kiburi cha kiroho, na kuona mateso tu kunaweza kuleta katika nuru hivyo kama kuthibitisha hatia ya kosa kwake. Kutenda Kazi Mungu na Mwanadamu Kwa hiyo, mateso yanaweza kuwa ni sehemu ya njia za Mungu akitenda kazi na watu kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe na kwa kuwaleta katika kumjua Yeye Mwenyewe; na matokeo ya Ayubu: yakawa mapya na habari ya maarifa ya Mungu. Aliweza kusema: “Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; Bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu katika mavumbi na majivu” ( Ayubu 42:5 - 6 ). Huku kutenda kazi Mungu na mwanadamu inabidi kwa hali yake kuwa na mtu mmoja mmoja: mwanadamu tu anayeteseka anaweza kupata hii nafasi kama kwa kuona mwenyewe. Shida kubwa ya mateso inabakia pale pale, na jawabu pekee la kubandua katika Kitabu cha Ayubu ni kwamba mwanadamu hawezi kumhoji Mungu mwenye enzi na hekima: Yeye ni Muumbaji na Mwenye kuvihifadhi vyote, na matendo yake yanapita maarifa ya mwanadamu. Ni jawabu hili linaloelezewa na uweza huu na uzuri wa sauti toka katika upepo wa kisulisuli mlango wa 38-41. Mwanadamu anaweza tu kufahamu ya kwamba njia za Mungu zinazidi uamuzi wake. “Je! Huyo Ayubu yu amcha Mungu bure ?” Kwa hiyo, wakati Kitabu cha Ayubu hakitoi jawabu rahisi kwa tatizo la mateso, kimezusha usawa mpana. Ni kwa hasara tu na kuteseka Ayubu aliweza kujua ya kwamba hakumtumikia Mungu kwa ajili ya nyumba, viwanja, wanyama na mifugo, au hata watoto. Hata hakumtumikia kwa ajili ya ngozi yake mwenyewe, afya yake na maisha bora. Alimwabudu Mungu mwenyewe, na mbali na maneno yote ya kinyama yaliyokuja toka katika mkazo wa akili yake na mwili alikuwa na imani ya kipeo katika haki ya Mungu na uaminifu. Hapo ilipokuwa kila kitu kilipoondolewa kwake ambacho alikijua kweli Mungu alikuwa ni kimbilio lake tu, na kwa uvumbuzi huo ushindi wake ukathibitishwa juu ya kisingizio cha Adui aliyeelezewa kwa marafiki watatu. (6) Mungu aliijaribu imani ya Ayubu, na kwa majaribu imani ikawa ngumu kama chuma. Ilikuwa kwa kufahamu yeye mwisho hekima ya Mungu, na kwa kujifunza kwamba imani inaweza kukua kwa njia ya mateso, hata Ayubu hatimaye akafikia maarifa tele ya Mungu. Maneno Mengine ya Mwisho Maneno ya mwisho kuchukuliwa toka katika kile tulichoona hadi hapo kinaweza kuelezewa kwa ufupi kama ifuatavyo:- 1. Mwanadamu anayeishi katika ulimwengu wa kulazimisha na matokeo ni lazima akubali matokeo yake; na maadamu dhambi iliingia katika maisha ya mwanadamu matokeo haya ni lazima yahusishe mateso. Ingawa hivyo, mateso hayawezi moja kwa moja kuhusiana na dhambi za mwenye kuteseka ila yaweza kuwa sababu toka matendo ya vizazi vya kwanza. 2. Wakati uo huo ni ulimwengu wa Mungu mwenye hekima na upendo awezaye kuongoza na kusimamia mateso kwa hao wanaomtafuta ili kwamba waingie katika kumjua kwa kina. Malezi ya Ki-Mungu Ni kwa mwangaza huu wa shauri hili la pili kwamba tuweze kufahamu fungu la maneno katika Barua kwa Waebrania ambayo msingi wake ni katika misemo ya Kitabu cha Mithali: “Tena mnayasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, Mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, wala usizimie moyo ukikemewa naye; maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, Naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili, Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama hamna kurudiwa ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba wa roho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tumshiriki utakatifu wake.Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa ni kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani. Kwa hiyo inyoosheni mikono iliyolegea na magoti yaliyopooza” ( Waebrania 12:5-12; Mithali 3:11-12 ). (7) Ukisoma kwa maneno yake,fungu la maneno linajieleza wazi lenyewe. Mateso na hasara ni vya kawaida kwa mwanadamu, lakini kwa watoto wa Mungu mateso na hasara yanaelekezwa kwa Baba yao wa Mbinguni kama malezi ya kiroho, na kama hivi ni njia ya kueleza upendo wake. Je! Mungu Huteseka ? Hatua moja zaidi inaweza kifikiwa katika kuelewa mateso. Ni Mungu mwenyewe amekuwemo katika mateso ya mwanadamu, maana katika upendo wake alimtoa Mwana wake mwenyewe kufa kwa ajili yao, na kuingia naye kuteseka pia. Yesu hakuwa na kosa kabisa, hakuwa na doa la dhambi ya aina yoyote, hata hivyo kwa hiari aliutoa uhai wake, akateseka isivyo halali na kwa ukatili kwa ajili ya rafiki zake: “Na kama vile Musa alivyomwinua yule nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa; ili kila mtu aaminiye awe na uzima wa milele katika Yeye. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika Yeye” ( Yohana 3: 14 - 17 ). “Hakuna upendo mkubwa kuliko huu, wa mtu kutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake”. Upendo mkubwa hata Mungu asingekuwa nao kuliko kumtoa Mwanawe wa pekee kuteseka msalabani kwa ajili ya ukombozi wa watu.” Ni kweli, kwa sababu hii kusema ya kwamba hata Mungu anahuzunika, basi inawezekana kuelewa msemo wa nabii kuhusiana na uhusiano wa Mungu kwa Israeli: “Katika mateso yao yote Yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa” ( Isaya 63:9; tazama vile vile Waamuzi 2:16 ). Ni kwa sababu gani Mungu haingilii kati ? Mungu wa Israeli hajajitenga mbali sana, asiyeonyesha ishara ya kusababisha kwanza kuona: Roho wake Mtakatifu anaweza kuhuzunika, anaweza kuingiwa na huruma ya kututamani sana. Anaweza kupenda kwa upendo usiokoma. Yote haya ni njia ya maandiko katika kuelezea jambo, yanadhihirisha Mungu kuwa ni Mkuu sana ambaye toka katika utakatifu wake anapitia mbali kuingia katika maisha ya wanaume na wanawake aliowaumba. (8)Mara nyingi watu huuliza: Ni kwa sababu gani Mungu haingilii kati kuzuia mateso, kukomesha vita, kuzuia magonjwa, n.k. ? Kwa kweli Mungu anaingilia mambo ya wanadamu; Ameonyesha uweza wake mara nyingi katika historia.Lakini kipo kikomo cha huku kuingilia kati: Ameruhusu hiari ya mwanadamu, na amemruhusu mwanadamu atumie mapenzi ya hiari hiyo - - kwa mema na mabaya. Mungu aliwahi kuingilia kati katika historia ya watu wake aliowachagua wa-Israeli na kuwapa nafasi mahususi katika kumwabudu. Yeye na kuwa mashahidi wake. Aliwagawia ufunuo na ahadi na unabii wa kuja Masihi. Mungu alimtuma Mwanawe Hivyo ikawa, karibu miaka 2000 iliyopita, Mungu aliingilia kati katika maisha na historia ya mwanadamu kwa kuwapa Mwanawe Yesu Kristo kushiriki mateso ya mwanadamu zaidi ili kuleta ukombozi toka katika dhambi na mauti. Kristo alikuja katika maisha na um,bile la kibinadamu; aliyashiriki yanayotukabili na kuvumilia majaribu toka ndani ya moyo na maumivu toka nje ambayo ni kawaida kwa wanadamu wote: “Kwa kuwa ilimpasa yeye…. Kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso….Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa Kuhani Mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasidia wao wanaojaribiwa” ( Waebrania 2: 11-18 ). “Ingawa ni Mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata” ( Waebrania 5: 8 ). Katika kukubali mateso kwa kutii mapenzi ya Mungu aliinua katika anga mpya, na alionyesha si ubaya mkubwa zaidi tena bali kama njia hadi mwisho: maana kwa njia ya mateso, katika utii wake kikamilifu kwa Mungu, akaishinda nguvu ya dhambi katika mwili wa mwanadamu, na hivyo kuwezesha ufufuo katika wafu na kuingia katika uzima wa milele na Baba. Kwa hivi akakamilishwa, imani iliyojaribiwa na kupimwa, kwa utiifu na ukamilifu, upendo wote kwa Mungu na utumishi wa mwanadamu - ni mfano kwa wafuasi wake wote. (9) Kuakamilika kwa njia ya Mateso “Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kieleleza, mfuate nyayo zake: Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake: Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakuogofya; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumiwe kwa haki: Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa” ( 1 Petro 2: 21 - 24 ). Naye “akiisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote ambao wanamtii” ( Waebrania 5:9 ). Yeye ni sababu, chanzo, mwanzilishi wa wokovu watu wasioweza kuufikia wao wenyewe, maadamu kwa kuingiza dhabihu yake wanaume na wanawake wamjiao kwa ajili ya kupata uzima, wao kwa neema ya Mungu wanakubalika kuwa washirika wa Kristo. Na hivyo, kama Kristo alivyofufuka siku ya tatu, upo ufufuo wa kiroho kuingia maisha mapya sasa kwa hao wabatizwao katika jina lake, na tumaini la ufufuo wa mwili na kubadilika kuwa kutokufa siku atakapo kuja “Washirika wa tabia ya Uungu” Ikiwa wamaume na wanawake walikuwa wawe “washirika wa tabia ya Uungu” ( 2 Petro 1:4 ), na kufufuliwa toka katika dhambi hadi kuingia usawa ambao kwa kweli wanaweza kumjua Mungu, kufurahia ushirika wa milele pamoja naye na kushiriki maisha yasiyoharibika, basi ni Mungu pekee alijua ni namna gani jambo hili lifanikishwe kwa kuwemo na ukuu wa utakatifu wake mwenyewe. Ilikuwa ni njia iliyohitaji kipawa cha Mwanawe kufa msalabani. Kama, wakati ule, Mungu aliteswa, na ikiwa, kwa kumtii Baba, Kristo aliteseka hadi kifo chake, shida yote ya mateso ya mwanadamu yameinuliwa kwenye usawa mpya. Pasipo kumwamini Mungu, mateso ni ubaya wa kuustahimili. Kwa imani, na kielelezo cha Mwana wa Mungu, mateso yaweza kutakasa na kuwa mwenye tabia nzuri, na kuwa njia ambayo kwayo Mungu humleta mtesekaji karibu naye. Kweli inaweza kuwa elimu ya kufundishwa na Mungu, kurudiwa na Bwana. (10) “Mambo yote Upya” Ikiwa Mwana wa Mungu aliteseka, je! watu wanatarajia kukwepa ? Lakini mbali na mateso ukaja ufufuo, na zaidi ya ufufuo utakuja Ufalme wa Mungu Kristo atakaporudi kutawala, na kuwatwaa kwake mwenyewe hao ambao tayari wamejiweka wenyewe kuwa wafuasi wake. Hiki kipindi cha kuanzisha Ufalme kimekaribia sana. Lakini maneno yake mwenyewe Bwana na unabii mwingine mwingi unaeleza bayana kwamba kuja Kristo kutatanguliwa na dhiki kubwa kwa ulimwengu, na bila shaka vile vile kwa wafuasi wake: “Kwa kuwa wakati huo kutakuwepo dhiki kubwa, ambayo haijatokea namna yake tangu mwanzo wa ulimwengu hata sasa, wala haitakuwapo kamwe. Na kama siku hizo zisingalifupizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitafupizwa siku hizo” ( Mathayo 24: 21, 22 ). Lakini Bwana Yesu Kristo anapotokea, ataondoa ubaya wote, weka chini dhambi yote na uchoyo, ataondoa magonjwa - na hatimaye mauti. Atatawala kwa ajili ya Mungu na kuondosha mateso. Ndipo yatatimia maneno ambayo Yohana aliyasikia kule Patmo: “Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya” ( Ufunuo 21: 3 - 5 ). Kwa hao wanaojibu mwito wa upendo wa Mungu, njia ya mateso inaweza kuwa njia ya uzima, na hilo ni kusudi la mwisho la kuwepo mateso ulimwenguni. Bado mwito unatoka; bado kuna nafasi kwa wote wanaotafuta tumaini zaidi kupita ubaya wa ulimwengu wa sasa, na kuona ni ‘habari njema’ ya Injili. (11) Tena: 1 902059 00 - X Matayarisho ya Ubatizo 1 902059 01 - 8 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 1-4 1 902059 02 - 6 Ukimwi 1 902059 03 - 4 Mshitaki Wenu Ibilisi 1 902059 04 - 2 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 5-8 1 902059 05 - 0 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 9-11 1 902059 06 - 9 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 12-15 1 902059 07 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 16-19 1 902059 08 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 20-23 1 902059 09 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 24-27 1 902059 10 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 28-31 1 902059 11 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 32-36 1 902059 12 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 37-40 1 902059 13 - 1 Ufunuo Mlango wa Kwanza 1 902059 14 - X Ni kweli Yesu Kristo alishuka kutoka mbinguni? 1 902059 15 – 8 Nyimbo za ndugu wa Kristo 1 902059 16 – 6 Ufunuo Mlango wa Pili 1 902059 17 – 4 Katiba ya Makanisa 1 902059 18 – 2 kitabu-mwalimu wa kristadelfiani 1 902059 19 – 0 Kuanzisha Kristadelfiano (CBM) Eklesia 1 902059 20 – 4 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura moja 1 902059 21 – 2 Ni kwa sababu gani Mungu Anaruhusu Mateso? Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya Biblia kaitka somo hili muhimu. Lina itwa Kuishi katika Ukweli. Unaweza kupata nakala kutoka Kanisa la Christadelphian, au kutoka anuani iliyoandikwa katika kijitabu hiki. ? CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW ISBN 1 902059 21 -2 Registered Charity Number: 248979 / 1020558 Company Number: 2796412 Telephone +44 (0) 1604 765068 Email: CarlHinton@hotmail.com Web: http:\\www.cbm-tz.org