Starting a Christadelphian (CBM) Ecclesia Kuanzisha Iklezia ya Kristadelfiani (CBM) Dibaji. (Hiki kitabu kidogo kimechapishwa kwa minajili ya pande zote mbili kwa iklezia lililokwisha anzishwa na hao Ndugu & wa-Dada. wanaotaka kuunda iklezia mpya. Yafuatayo yasomwe kulingana na Katiba na baadhi ya mambo yafuatayo yamewekwa wazi katika Katiba.) “Iklezia” ni neno lenye maana ya mkusanyiko au kikundi cha watu wenye imani moja iliyo katika Biblia; neno hili halina maana jengo. Iklezia ni kwa ajili ya kuwasaidia hao wanohusika nalo, na wengine ambao wanavutwa kujiunga nalo, kusoma Biblia na kujifunza kweli ya Biblia. Linafanya mikutano kwa ajili ya washirika wake waweze kumcha Mungu na kushiriki mkate na divai kwa ukumbusho wa kifo na ufufuo wa Bwana Yesu. Kila juma linakuwa na shule ya Biblia kwa kujifunza Biblia. Iklezia linakuwa na Shule ya Jumapili (Sunday School) kwa ajili ya kufundisha watoto. Linatoa msaada kwa njia yo yote ikiwezekana, kwa walio na shida. Ni jamii mahali ambapo washiriki wake wote ni ndugu na dada katika Yesu Kristo. Kuanzisha Iklezia Idadi ya ndugu na dada waishio karibu vya kutosha kila mmoja waweza kuunda iklezia kwa kumwarifu anayewaunganisha katika CBM pande mbili, yaani, (CBM Linkman) matakwa yao. Tendo hili halina haki ya pesa yo yote kwao ya kujiendesha toka CBM. Iklezia nyingine zitaarifiwa ni nini kinatokea. Wanaweza kukutania katika nyumba ya mmojawapo, iwapo chumba chenye nafasi kubwa zaidi hakitapatikana. Chini ya sheria ya Tanzania hairuhusu kutumia chumba cha shule kwa lengo la kufanyia ibada. CBM imesajiliwa na serikali ya Tanzania kuwa ni kundi la dini. Hao wanaounda iklezia hawanabudi kuhakikisha kuwa kwa kila hali wanatii sheria za nchi. Kikundi ni lazima kikubali kufuata mafunzo na desturi za iklezia za CBM. Washiriki wa Iklezia. Waliopokea mafunzo ya Biblia, na wakiwa wamefanyiwa usaili (interview) na mmisionari wa CBM nao wamekwisha batizwa na Iklezia la CBM wanakuwa ni washiriki kamili wa iklezia linalowahusu. Wanajulikana kuwa ni ndugu na dada. Hakuna mtu anayeweza kusailiwa na kubatizwa na awaye yote ambaye hakutakiwa kufanya hivyo na Linkman. Ubatizo halisi hauwezi wala haununuliwi kwa pesa. Wanaotaka kubatizwa ni lazima . wawe wameelimika katika mafundisho ya kweli ya Biblia nao wapende kuiendeleza kwa kujifunza zaidi ili kuielewa Biblia . waweze kumthibitishia mmisonari ya kuwa wanajua majibu ya maswali na kuamini Biblia inavyofundisha . waonyeshe kwamba lengo lao kuu katika maisha ni kufahamu wokovu ambao Mungu ametoa kwa njia ya Bwana Yesu na kuwa na tumaini thabiti la kuwa na sehemu katika Ufalme wa Mungu. Ni washirika tu waliokwisha batizwa na CBM wanaoweza kuchukua mkate na divai wakati wa ibada ya Ukumbusho. Ni ndugu (brothers) tu wanaotakiwa kuendesha mikutano, kutoa maonyo na hotuba mbele ya halaiki, kusoma Biblia kwenye mikutano na kutoa sala mbele ya watu wote. Akina dada waweza kusaidia kufundisha watoto na watu wazima na kushiriki wakati mambo ya ikilezia yakijadiliwa kwenye mikutano ya shughuli. Marafiki wanaweza kuwapo katika mikutano ya CBM kuangalia kinachoendelea na kujifunza katika Biblia. Wao si washirika wa iklezia na hawatakiwi kushiriki mkate na divai, kutoa maonyo, maombezi, hotuba, kusoma katika mikutano, kuchukua nafasi yoyote ya uongozi katika iklezia k.m. kuwa mtunza hazina au kushiriki kwa njia yoyote katika kufanya maamuzi ya iklezia. Utaratibu wa Iklezia. Watumishi wa Iklezia, yaani Mwenyekiti, Katibu, Mtunza Hazina na Mkaguzi wa Hesabu. Iklezia mpya watahitaji ndugu wanne ili kutenda kazi wakiwa ni “watumishi wa Iklezia” na kushika kazi mahususi. Watumishi wa Iklezia hawatakiwi kutawala iklezia, bali watende kazi kama watumishi wa Bwana na wa ndugu zao na dada. Hawatakiwi wao wawe madikiteta katika mambo ya Iklezia bali kama watumishi wa Bwana na wa Iklezia. Hawatakiwi kuishi kwa pesa za Iklezia au kujiona wenyewe ni wachungaji au watu wa kuheshimiwa sana kama Padri n.k. Ni lazima wachaguliwe na ndugu na akina dada wa iklezia na wawe wamekwishaonyesha ya kwamba wanaweza kutoa ushauri wa busara na kwamba ni waaminifu kabisa. Wawe na sifa njema miongoni mwa washirika wa iklezia. Iwapo hawapo ndugu wanaofaa kushika nafasi ya kazi ya Mtunza Hazina na Mkaguzi wa Hesabu, ndipo kazi hizi zaweza kushikwa na akina dada, ila Katibu na Mwenyekiti inabidi wawe ndugu nao hawana budi kutenda kama wasemaji kwa ajili ya Iklezia. Watumishi wa Iklezia wakutane mara moja kwa mwezi kuamua ni mikutano gani ifanywe, ni nani anahitaji msaada katika Iklezia na ni jinsi gani pesa itumike. Ni lazima wahakikishe kuwa mafunzo ya kweli ya Biblia yanadumishwa na washirika wote na kwamba mshirika anakuwa na mwenendo mzuri. Iklezia lote likutane kila juma la kumi na tatu kujadili kuendesha mkutano na kuthibitisha au pengine maamuzi ya watumishi wa Iklezia. Huu umejulikana kama Mkutano wa kutathimini. Mara nyingi yanaweza kufanywa majadiliano ya Iklezia, iwapo jambo la kupimwa linahitaji kuangaliwa haraka. Muhutasari wa haya na mikutano ya shughuli yote itunzwe katika kitabu na Katibu na muhutasari wa mkutano uliopita ukubaliwe kama taarifa ya kweli kila muda Iklezia likutanikapo kwa ajili ya Mkutano wa jinsi hii. Mwenyekiti Ndugu anayeshika kazi hii, tena amechaguliwa na idadi kubwa ya kura ya iklezia, awe amejulikana kwa uaminifu wake kwa kila mwelekeo wa maisha. Awe na ujuzi wa kuratibu na awe na sifa ya kujali kwake na huruma. Anashika wadhifa huu ili ahakikishe:- kwamba Iklezia lina utaratibu mzuri ya kwamba Ibada ya kumega mkate inafanyika kila juma. Kwamba Injili inaelezewa waziwazi katika maelekeo yake yote, kwa hao watu waitwao na Bwana kusikia ujumbe wake wa wokovu. Ya kwamba Biblia inasomwa na kujifunza kila mara na washirika wote wa Iklezia. Ni kwa njia hii tu washirika wataongezeka katika maarifa na kuishi kwa namna ya kama kuleta tumaini katika Injili waikiriyo kuishika. Katibu Ndugu anayechaguliwa kushika kazi hii, kwa kura nyingi za Iklezia, inampasa kuonekana kuwa mwaminifu na mnyoofu katika kudumisha utendaji wa iklezia na kufundisha kweli ya Biblia. Wajibu wa Katibu unajumuisha:- Kuwa na kitabu ambacho majina yote ya washirika wa Iklezia yanakuwa kwa namna ya daftari yenye orodha. Kila mwongofu mpya aliyebatizwa karibu aorodheshwe. Mtu akifa au akiondoka katika Iklezia, akihamia iklezia lingine au akiacha kuja kwenye mikutano kwa sababu zo zote, habari zao ziingizwe juu ya majina. Daftari ya orodha ya majina itiwe alama, kama taarifa iliyo na tarehe, kila kipindi mshirika akihudhuria ibada ya Kumega Mkate. Iwapo mshirika anahamia eneo lingine lenye Iklezia, Katibu atume barua kwa Katibu wa Iklezia lingine akimpa tarehe na mahali alipobatizwa huyo mtu na kumkabidhi kwao katika ushirika wa Iklezia mpya. Kuandika barua kwa niaba ya washirika wa Iklezia kwenda kwa Linkman (angalia chini Ustawi wa Jamii). Mtunza Hazina Ndugu au dada iwapo hakuna ndugu wa kufaa, asiwe na tabia ya mapato ya aibu kabisa. Hawa mmojawapo achaguliwe na idadi kubwa ya Iklezia. Ni jukumu la Mtunza Hazina:- Kuhesabu changizo kila juma. Kutunza taarifa ya kawaida ya kiasi cha changizo kila juma kilichokusanywa katika kitabu cha hesabu. Kuhakikisha kwamba mahesabu si ya upotoshaji. Kuwa na hesabu ya benki inayotumika iwe imefunguliwa kwa jina la Iklezia na kuwa na kitabu cha benki au kadi,na majina yaliyokubalika kuwa ni watia saini. Kuweka pesa iliyokusanywa na Iklezia kila juma. Kutoa pesa katika Account, ikiishatolewa maelezo vema idadi na matumizi yake katika kitabu cha hesabu kama kilivyokubalika na Iklezia. Kulipa madeni ya Iklezia na kutoa pesa kwa ajili ya ustawi wa jamii ikikubalika tu na Iklezia lote. Kuonyesha mahesabu yaliyopigwa kwenye Iklezia kila juma la kumi na tatu katika mkutano wa kutathimini. Mkaguzi wa Hesabu. Mkaguzi, tena aliyechaguliwa na idadi kubwa ya wana-Iklezia, inabidi ahakikishe kuwa mahesabu yametunzwa vema na kwamba mahesabu yanaoana na pesa zilizo benki katika jina la Iklezia. Ni lazima mkaguzi atie saini mahesabu kila muda ambao yamethibitishwa na Iklezia katika mkutano wa tathimini. Changizo. Iklezia lililoanzishwa na CBM haliwi na wachungaji au watumishi wanaolipwa. Kwa hiyo inaonekana ni jambo lenye maana kwamba washirika wa Iklezia watoe changizo kila muda wakutanikapo kukumbuka kifo cha Yesu. Hii changizo halina kiwango kilichopangwa bali kiendane na namna ambayo Bwana amewabariki. Pesa yo yote isichukuliwe toka kwa wanafunzi ambao hawajabatizwa, wanaosoma bado Injili. Pesa itumike kwa kununulia mkate na divai na kutoa kusaidia hali njema ya washirika, yakiwapo makubaliano kamili ya Iklezia nzima. Hali ya Ustawi wa Washirika. Iwapo suala la kushughulikia hali njema ni kubwa mno kwa Iklezia, Katibu atatakiwa kumwandikia Linkman wa CBM, kwa kutumia muhuri wa Iklezia kwenye barua, ikionyesha dhahiri shida.Linkman ataliangalia hilo jambo na kuamua ikiwa linaweza kupelekwa mbele zaidi. Kwa namna iwayo yote uamuzi unavyokwenda hauna budi Iklezia liukubali. Hakuna mshirika wa Iklezia anaruhusa kuwaandikia Wakristadelfiani wengine wo wote penginepo ulimwenguni, kuomba msaada. Barua zote hizi hurudishwa kwa Linkman ni kupoteza muda wa bure. Mikutano ya Kumega Mkate Wakati wa Ibada ya Kumega Mkate, akina dada wafunike vichwa vyao. Hawatakiwi kuketi wamejitenga na ma-brothers-wandugu. Matakwa makubwa mawili ya ibada hii ni mkate na divai. Mkate waweza kutengenezwa kutokana na nafaka yo yote- Mchele, mahindi au ngano. Kila mmoja unaweza kukandwa katika umbo la keki, mkate au chapati. Umbo hasa si kitu cha kuzingatiwa. Biskuti zaweza kutumika iwepo ni vigumu kupata kitu cho chote kingine. Lengo kubwa ni kwamba uweze kumegwa na kugawana. Kwa njia hiyo tunaonyesha kwa vitendo kuwa sisi ni mwili mmoja wanaoamini, tukigawana alama ya mwili wa Yesu. Divai au maji ya zabibu yanapatikana popote mijini na divai nyekundu inapatikana katika miji mingi. Inafanyika kazi kidogo ili kupata duka linaliouza divai. Patana basi na muuza divai. Angalia kununua chupa zaidi ya moja. Ikiwezekana, nunua chupa ya “Ushirika Mtakatifu au divai yenye nguvu.” Hii inadumu, hata wakati wa hali yenye joto. Divai nyekundu inaonekana kama damu, nayo yatukumbusha kuwa tunashiriki mfano wa damu ya Yesu, kama alivyotuagiza kufanya . Mifano ya mkate na divai itawasaidia kutafakari juu ya lengo la kukutana. Kama akina dada wanataka, wanaweza kutumia ujuzi wao wa kushona vitambaa vya mezani, ambavyo vitatumika kwa ajili ya kufunika na nguo safi ya kufunika mkate na divai. Mkate uwekwe katika sahani na divai katika kikombe au bilauri. Yesu alisema kwamba atakuwepo katika roho, wawili watatu wakikutana pamoja katika jina lake. Kwa sababu hii inabidi ibada ifanyike kwa heshima kabisa kwa hicho kinachofanyika. Kwa hivi,Iklezia likubaliane muda wa kuanza ibada ya kukumbuka nao huo muda uzingatiwe. Vitu kimoja-kimoja ambavyo vinakuwamo katika ibada ya kukumbuka vimeorodheshwa katika Katiba. Mambo muhimu zaidi kuhusiana na kutwaa mkate na divai ni kwamba anayeendesha ibada ya meza:- Asome katika Mathayo 26:27-28 au 1Kor.1125-26 kama utangulizi. Amtake ndugu kutoa maombi mafupi ya shukurani kwa ajili ya mkate. Aumege mkate vipande viwili na kila ndugu na dada aliyebatizwa amege kipande kidogo na ale. Sahani yenye Mkate ipite toka kwa mshirika mmoja hadi kwa mwingine, kuonyesha kwamba tunagawana mfano wa mmoja. Amtake ndugu mwingine atoe sala fupi ya kutoa shukurani kwa ajili ya divai. Amtake kila ndugu aliyebatizwa na kila dada anywe tone dogo kabisa la divai katika kikombe. Tafadhalii kumbuka kwamba ni waumini waliobatizwa tu wanaruhusa kushiriki mkate na divai. Wao peke yao, wamefanya agano na Bwana kwa ubatizo na ni hilo ambalo wanalifanya upya kila muda wakishiriki mifano.Hiyo ndiyo sababu ni muhimu mno kwamba ifanyike hivyo mara kwa mara na kicho jinsi hii. Mkutano wa Tathimini Lengo la kuendesha mikutano ya tathimini limeelezwa kinaganaga katika katiba, unatakiwa kuisoma. Kushughulikia Matatizo. Katika jambo hili, unahitaji kukumbuka kwamba Bwana anajua ni sababu gani kuna shida, nani anasababisha matatizo na jinsi gani yatatuliwe na Iklezia. Mara nyingine ndugu au dada anaweza kuwa na mwenendo mbaya sana, kwa kuvunja amri za Kristo kwa njia ya bila kufikiri. Wakati mwingine ndugu au dada aweza kufunza mafundisho potofu. Tafadhali kumbuka kuwa sisi sote tunakosa kwa namna tofauti. Utaratibu wa Bwana wa kushughulikia mambo ya jinsi hii ni kama ifuatavyo:- Mkabidhi hii shida Mungu kwa maombi. Katika Mathayo 18:15-17 Yesu anatushauri ni jinsi gani tumkabili mtu aliye na matatizo. Mshirika aliyegundua tatizo yeye binafsi amwendee mtu anayeonekana kusababisha shida, kwa unyoofu na mwenendo wa upole. Iwapo huko kumwendea hakusaidii, basi mshirika huyo achukue ndugu wawili wengine wamwendee tena huyo aliyeonekana kuleta shida.Hii ifanyike tena katika roho ya upatanishi. Ikiwa hii haisaidii, ndipo jambo liwekwe mbele ya Iklezia zima, huku akiwapo aletaye shida, kama anataka kuwapo kwenye mkutano huo. Kama bado haisaidii, wakati huo kadhia aambiwe Linkman wa CBM ili kupata mtazamo uliojitegemea. Kama huo utaratibu unashindwa kutatua hiyo shida na imeonekana kubwa vya kutosha, ndipo mtu aletaye kikwazo inabidi kuondoa ushirika na kutoweza kushirikiana katika mkate na divai kwenye ibada ya Ukumbusho. Inatakiwa awepo Linkman Kufuatia tendo hili kubwa, huyo hana ruhusa kurudia ushirika kwa kadiri ya mwaka mmoja, hapo tena akiwapo Linkman. Muhutasari. Tukumbuke kwamba ni kwa neema ya Mungu hata tunaokolewa, Wakristadelfiani wote wakumbuke kwamba Bwana ajua kila mtu alivyo na Iklezia linavyofanya. Anawajua waletao shida wenye husuda na wachafuzi wa watu. Vile vile anawajua wanaomtumikia kwa uaminifu, naye Bwana atawapa thawabu “kila mtu kwa kadiri ya matendo yake” (Ufunuo 20:13).