_____________________ Fungu Lako Katika Ahadi za Mungu Fundisho la Biblia kuhusu “Tumaini la Israeli” Your Share In God’s Promises _____________________ Kufasiri: Simon Uswegi Kuumba: Carl Hinton KATIKA mazungumzo ya kila siku tunaongea kuhusu tumaini. Tunasema “Natumaini utapona haraka” au “Tunatumaini kwenda nchi za nje mwaka huu” au “Natumaini mgomo utakoma juma lijalo”. Tuna maana kuna jambo fulani wakati ujao tungependa sana litokee, na tunaona kwa makini kwamba matumaini yatakuwa hivyo. Maisha yasiyo na tumaini yatakuwa magumu sana. Hata katika mazingira mabaya sana, watu hupendelea kutazama upande unaong’aa. Mtunga mashairi aliandika: “Tumaini huchipuka milele katika moyo wa mwanadamu. Tumaini linaweza kuwapa watu kushikilia kauli- kama wachimba madini walionaswa mgodini, au mabaharia walichukuliwa na mkondo wa maji juu ya ubao, mara nyingi watapigana na mauti kwa siku kadhaa, huku wakisadiki ya kwamba rafiki zao watafika kutoa msaada kabla ya kuangamia. Kwa huzuni, kwa kweli, mara nyingine wanapata kile wasichokitarajia. Inawezekana kutokea ya kuwa mwamba unaanguka katika shimo refu la kupenya ndani kwenda chini kabisa, au hakuna mtu anayejua merikebu ikiingia maji na kuzama. Katika suala hili nafasi ambayo wanaishikilia inapotea, na tumaini lao linakuwa ni ndoto. Tumaini lililo na msingi Taraja ni jambo la kuzungumziwa linalochipuka mara nyingi katika Biblia. Sehemu zote mbili Agano la Kale na Jipya, waandishi wamejaa na matarajio kwamba mambo yatakuwa mazuri. Wanatazama katika ulimwengu unaochosha na usio na haki mahali ambako mara nyingi mateso huwajia wasio na hatia na watu waovu huwa washindi, hata hivyo wana ujasiri wa ajabu wa kuwa siku moja Mungu Muumbaji atageuza mambo yawe sawasawa. Si hivyo tu, bali waonekana kusadikishwa ya kwamba wao wenyewe watashiriki katika kuistawisha hali itakayokuja. Msikie mwandishi wa Zaburi: “Wewe uliyefanya mambo makuu; Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe? Wewe uliyetuonyesha mateso mengi mabaya, utatuhuisha tena….. Nitakuimbia wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli. Midomo yangu itafurahi sana nikuimbiapo” (Zab. 71:19-23). Hapana shaka juu ya tarajio la mtu huyu kuhusu wakati ujao Au Paulo Mtume, kwa moyo mtulivu, katika fungu hili la maneno toka barua yake kwa Timotheo: “Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, imani nimeilinda”. Ona ni jinsi gani alikuwa na hakika kama anavyoendelea:- “Baada ya hayo nimewekewa taji ya haki ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake”(2Tim.4:6-8). Fungu hili la mwisho hasa ni la kuvutia kwa kuwa liliandikwa akiwa kifungoni. Mfalme wa Kirumi aliwajia juu Wakristo, na Mtume aliye na umri mkubwa alikuwa katika jaribu la maisha yake. Mara ya kwanza kesi yake ilisikilizwa mahakamani, alikuwa anasubiri kesi ya kusikilizwa mara pili. Tayari alijua matokeo alipomwandikia kijana Timotheo toka jela isiyo na furaha. Alielekea kufariki. Mbali na matazamio haya yenye huzuni, amejaa tumaini kabisa. Si kama wachimbaji madini walionaswa ardhini au mabaharia waliovunjikiwa merikebu, hashiki bahati finyu ya kwamba hati nyingine ya muhimu itatokeza bahati ya kufunguliwa, au atapatikana shahidi rafiki, labda, wa kumtetea afutiwe mashitaka. Matarajio yake yalikuwa bora kuliko kifo chake. Ana uhakika kabisa kuwa hata baada ya kufa kwake, Mungu wa Mbinguni atamfufua kupata maisha mapya yaliyo bora, siku ya mwisho. (1) Uthibitisho Kamili Tarajio la Waandishi wa Biblia ni la wazi jambo fulani lenye nguvu kuliko matarajio ya watu waangalifu. Wana mawazo dhahiri juu ya kile kinachoenda kutokea wakati ujao, na kwa kweli wanatazama mbele katika utimilifu wake. Labda unamwonea wivu Mtume Paulo kutokana na uthibitisho wake, hasa kama unapita katika maisha yako yakiwa machungu na kuhuzunisha.Unaweza kuwa na shaka zamani ya kuwa ulikuwa na hakika lilikuwepo jambo lingine la kutumainia zaidi ya kaburi.Pia unaweza kustaajabu ulimwengu unaelekea wapi, watoto wako na wajukuu watarithi nini ukiondoka. Vema, jipe moyo. Biblia inakufungulia mambo yajayo, pande zote mbili ya ulimwengu na ya kwako. Inakuonyesha mpango ambao Mungu amekuwa akiufuatia wa kupatana tangu mwanzo, msingi wake juu ya ahadi alizoahidi. Habari kidogo ya mambo , inaanza na Ibrahimu, baba wa Israel, na kupanuka katika Manabii ndani ya maandishi ya Agano Jipya, ipo wazi na iliyo na hoja kamili ambayo mtoto mdogo aweza kuielewa. Inaweza kukupa ujasiri ambao utakupitisha katika bonde lenye giza nene la mateso, na Mungu ametoa ushahidi kuitegemeza imani yako iwe na nguvu ambapo ni upumbavu wa kiburi unaweza kupofusha macho yako tu. Soma na uone ni jinsi gani habari inavyofuatana sawa sawa. Ahadi kwa Ibrahimu Mwanzo wa masimulizi yetu yamo katika Agano la Kale. Kitabu cha watu wa Israeli. Masimulizi haya yasikufanye kutopenda. Agano la Kale sio kuwa halihitajiki wala kuwa limepitwa na wakati. Eneo la nchi laweza kutofahamika, lakini kuna hazina ya kweli inayopatikana katika vitabu hivi vya kwanza vya Biblia. Kwa mfano, ni watu wachache waliowahi kusikia ahadi alizoahidiwa Ibrahimi, lakini ndizo zimefanya msingi kamili katika mpango mkuu atakaoufanikisha Mungu. Hebu tusimulie kwa ufupi. Ibrahimu alikuwa na sifa ya kuangaliwa aliyeishi karibu miaka 3000 K.K. katika mji ulioitwa Uru uliokuwa katika nchi tunayoijua sasa kuwa Iraki. Siku moja alitembelewa na mjumbe toka kwa Bwana, aliyekuja mwambia aondoke na aiache nchi ya kuzaliwa kwake. “Toka”, Bwana alisema, “uende mpaka nchi nitakayo kuonyesha” (Mwanzo 12:1). Kwa kuwa alimwamini Mungu, Ibrahimu akauza yote aliyokuwa nayo na kuondoka safari ya kuvuka jangwa akiwa na jamaa yake. Wakafika katika nchi tunayoijua leo kuwa ni Israeli. Kwa kifupi baada ya kuichunguza nchi, BWANA akamtokea tena, akamwambia “Uzao wako nitawapa nchi hii” (Mwanzo 12:7). Wema huu aliopewa Ibrahimu na Sara mkewe ulimfurahisha hasa, kwa sababu mbali na kudumu ndoa yenye furaha, hawakuwa na watoto. Inaonekana BWANA alikuwa anawaahidi kuwa jamaa, na vile vile kuwa na mahali pa kuishi. Miaka mingi ilipita Ibrahimu aliendelea kuishi katika hema, akisubiri kwa saburi jambo lingine litokee, lakini hapakuwa na dalili ya kupata mtoto, nao wenyewe wenyeji wa nchi waliendelea na shughuli zao. Jioni moja mjumbe wa BWANA alimtokea tena. Ibrahimu alichukua nafasi hii kuuliza maswali mawili muhimu. “Tazama”, aliuliza taratibu, “hukunipa uzao”. Kwa kujibiwa, alimleta nje, akasema, tazama sasa mbinguni. “Kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu”, aliambiwa. “Ndivyo utakavyokuwa uzao wako!” Kipengele kingine kilichokuwa kinampa shida Ibrahimu ilikuwa jambo la nchi. “Mimi ni BWANA niliyekuleta toka Uru wa Wakaldayo nikupe nchi hii ili urithi, malaika alimkumbusha. Ee Bwana MUNGU”, alijibu, “nipateje kujua ya kwamba nitairithi ?” (Mwanzo15:3-8) (2) Agano la Heshima Kwa kumjibu BWANA aliendelea kufanya mapatano ya heshima na Ibrahimu, kwa desturi ya siku zile, liliitwa “agano”. Akaagizwa kukusanya kwa uangalifu aina ya wanyama na ndege, waliotolewa kuwa dhabihu. Mwili uligawanywa na kulazwa sawa sawa. Kwa kawaida, pande mbili katika agano walipita katikati ya vipande vya nyama, kwa hivi kulihalalisha agano, Katika jambo hili, kama Mungu alivyokuwa anaahidi kwa Ibrahimu, alipita katikati ya vipande. Ibrahimu alichoona katika giza zito, tanuru ya moshi na mwenge uliowaka, katika mfano ambao mara nyingi Mungu alijifunua mwenyewe kwa watu wake. Ibrahimu aliridhika. Agano likithibitishwa namna hii halitanguki. Miaka ilisonga mbele. Kwa kipindi Ibrahimu aliongezeka kumjua Mungu, ahadi zilirudiwa na kupanuliwa. Mambo mawili yanapita ndani yake bila kubadilika- kumiliki nchi, na wazao wake wakati ujao.Ni vizuri kufuatilia maendeleo katika kitabu cha Mwanzo 13,15,17 na22. Ahadi ya kuvutia moyo zaidi kati ya zote ni ile ya mwisho. Hii ilianza na kiapo “Nimeapa kwa nafsi yangu”, asema BWANA. Kiapo kiliendelea katika msemo uliozoeleka: “Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani”, Kiliishia katika siri: “Uzao wako utamiliki mlango wa adui zao, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibariki” (Mwanzo 22:17,18). Ona badiliko katika mtu kwa wingi, “Uzao”. Vile vile ona umuhimu wake “Kumiliki mlango” wa mtu mwingine ni msemo maalumu katika Kiebrania. Zamani mlango ulikuwa sehemu ya kuingilia katika mji ulio na ngome. Pia palikuwa sehemu ambapo watawala walifanya baraza kuhukumu. Kumiliki mlango wa adui yako ni kuwa na mamlaka kabisa. Uzao wa Ibrahimu ilikuwa uwe ni wenye kushinda na kuleta furaha kwa watu wote. Ni yupi ambaye alikuwa moyoni mwa Mungu ? Ibrahimu aliweza kukisia tu na kuamini. Miaka ishirini na tano baada ya kufanya maagano, Sara alimwambia Abrahamu kwa mshituko mkubwa kuwa alikuwa anaelekea kuwa na mtoto. Mungu alikuwa akitunza neno lake. Kwa muda wote huo Abrahamu hakuwa na shaka ikiwa Mungu atampa mwana. Mtume Paulo alifafanua kuhusu yeye katika Warumi: “Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa Imani,…huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi” (Warumi 4:20,21). Imani ya Abrahamu haikuyumba. Wala hakumpa Urithi…. Maelezo mafupi pekee yanayohangaisha katika maisha ya huyu muasisi mkuu ni ukweli wa kwamba alipofariki, wala hakumiliki nchi. Mungu alikuwa na Nyakati kadhaa zilizoahidiwa kwake yeye mwenyewe, vile vile na uzao wake. Lakini kama mfia dini Stefano alivyosimulia, Mungu “hakumpa urithi humu, hata kiasi cha kuweka mguu” (Mdo 7:5). Alifariki katika hema lake bila kuwa na nyumba iliyo na jina lake. Lakini tumaini la Abrahamu kwa Mungu lilipita juu hata kwenye kizuizi hiki cha mwisho. Pamoja na mke wake na watoto , anasema mwandishi kwa Waebrania “ alikufa katika imani, wasijazipokea zile ahadi, bali waliziona tokea mbali na kuzishangilia” (Waebrania 11:13). (3) Sasa unaona ni kwa sababu gani Ibrahamu anaitwa “Baba ya wenye Imani”. Mungu alimleta katika nchi aliyoahidiwa. Mungu alimpa Mwana. Iwapo Mungu alimwambia atairithi nchi, aliamini kuwa hivyo, hata ingawa ilimpasa kufa. Karne nne baada ya Abrahamu kufa, jamaa yake ikaongeza na kuwa taifa. Mungu aliirudia ahadi ya kurithi na kwa mwanawe Isaka, na tena kwa mjukuu wake Yakobo, hivyo hiyo ahadi ilizunguka katika familia. Yakobo akawa na jina la pili, Israeli. Akazaa wana kumi na wawili, kila mmoja akawa kichwa cha kabila au ukoo ulio na maelfu ya wazao. Wakati wa kipindi cha njaa, jamaa ikahamia Misri na kuishi kule. Walipoongezeka, Wamisri wakawahofia uwezo wao, wakatiwa utumwani huku Wamisri wakiwa juu yao. Musa, mtoa sheria mkubwa alitumwa kuwakomboa. Baada ya misiba ya mfululizo iliyoiharibu Misri, Farao wa Misri alilazimika awaache huru waondoke, nao Israeli wakaanza safari kupitia jangwani kuelekea nyumbani kwao. La kushangaza tukio hili kabisa lilitabiriwa katika moja ya ahadi kwa Ibrahamu, kama ukiweza kuchunguza mwenyewe katika kitabu cha Mwanzo 15:13-16. Kiapo cha Mungu kwa Israeli… Katika Mlima Sinai, Malaika wa BWANA alifanya agano lingine wakati huu na mkutano wote wa Israeli. Lilitiwa muhuri kwa damu ya dhabihu, liliwapa ufunguo wa kuingia nchi ya Israel, maadamu wangetunza maagizo ya maneno ya Sheria ya Mungu. Miaka iliyofuata, walipokuwa wamesimama ukingoni mwa Nchi ya Ahadi, Musa aliwakumbusha ya kwamba Mungu, baada ya mamia ya miaka alikuwa anaelekea kutimiza neno lake. “Kwa sababu BWANA anawapenda ninyi, na kwa sababu alitaka kutimiza uwapo wake aliowaapia baba zenu, ndiyo sababu BWANA akawatoa kwa mkono wa nguvu…..Basi jueni ya kuwa BWANA , Mungu wenu, ndiye Mungu; Mungu mwaminifu, ashikaye agano lake na rehema zake kwao wampendao, na kushika amri zake, hata vizazi elfu”(Kumb.7:8,9). Hayo yalikuwa maelezo ya kushangaza. Mfano mmoja wa kizazi kupita katika jambo lingine kama robo karne. Vizazi elfu vilihitaji miaka elfu ishirini na tano ya kutunza agano. Hivyo neno la Mungu ni la kutegemewa kabisa.Kwa hakika idadi ya ahadi za Mungu bila kutikisika zikawa kweli, kama Waisraeli walipovuka mto Yordani kwa vilima na malisho ya nchi ya baba zao. Tunapita zaidi ya mia kadhaa kidogo miaka isiyo ya uaminifu katika wakati wa Wafalme wa Israeli. Mfalme Daudi aliyejulikana vema kwa utunzi wake wa Zaburi, alikuwa kama Ibrahamu, mtu imara kwa imani. Mambo yake mengine ya kumpenda Mungu na msisitizo wake katika kweli na haki yanatoka katika maandishi yake. Mara nyingi Ibrahamu ametajwa katika Maandiko kuwa ni “rafiki” wa Mungu. Daudi aliitwa na Mungu “mtu aliyeupendeza moyo wangu”. Sifa za hawa wawili zinaonyesha tabia ya kipekee kwa watu hawa. Kipindi cha safari jangwani na kuikalia kwao baadaye nchi, Israeli walimwabudu kwenye hema (maskani) iliyokuwa ikibebwa, ilikuwa mfano wa jengo. Sasa taifa likasimamishwa kwa uthabiti na mfalme, mji mkuu ukiwa Yerusalemu. Daudi aliona ni jambo zuri kumjengea BWANA jengo la kudumu zaidi lenye mawe. Alipodokeza jambo hili kwa nabii Nathani hakutegemea alipoambiwa ya kwamba huo ulikuwa mradi hauna budi kuahirishwa hata mwanawe aje aketi kwenye kiti cha enzi. Ingawa hivyo, alisema Nathani, BWANA alikuwa ameguswa na shauri la Daudi la kumheshimu, na katika kumjibu alimletea Daudi ahadi kubwa nzuri yeye na jamaa yake, inayofanana kabisa na ile iliyofanywa kwa Abrahamu. (4)Agano na Mfalme Daudi Kwa hakika ilikuwa ni ahadi nzito, imetajwa kuwa ni Agano na Daudi. Na kama ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu, ziliungana wazi , mashauri ya kufaa na maelezo yaliyo magumu kueleweka ambayo yalimtatiza Daudi kwa miaka. Hapa upo mfano uliochukuliwa kwa 2 Samueli 7: “Tena BWANA anakuambia” alisema Nathani, “ya kwamba BWANA atakujengea nyumba”(aya ya 11). Ilionekana ni habari isiyo ya kawaida, kwa kuwa alikuwa ni Daudi aliyetaka kumjengea BWANA nyumba. Lakini kama nabii alivyoendelea, ikawa bayana ya kwamba BWANA alikuwa na wazo tofauti kuhusu nyumba: “Nitainua mzao wako nyuma yako, atakayetoka viunoni mwako, nami nitaufanya imara ufalme wake. Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha Ufalme wake nitakifanya imara milele (aya 12,13). Mpaka hapo, ahadi ilifaa kwa uzuri kwa Sulemani, mwana wa Daudi aliyemrithi kiti cha enzi. Lakini Mungu aliendelea, “Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu” (aya 14). Hili lilikuwa fumbo. Ni jinsi gani mtu aliyetajwa kuwa mwana wa Daudi, kisha Mungu awe ni baba yake vile vile? Ilikuwa ni siri. Kilele cha ahadi kikafika mwisho: “Nyumba yako na Ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako; nacho kiti chako kitafanywa imara milele”(aya 16). Ni wazi nyumba ya Daudi ilikuwa jamaa yake au ukoo. Tunatumia neno lilo hilo tunaposema nyumba ya fulani- tunaelewa pande mbili, ukoo au familia. Lakini ni aina gani ya ahadi---kuwa na jamaa yako imepewa hakikisho la kuendelea kukalia kiti cha enzi, sio tu kwa miaka mamia, bali milele! Lilikuwa ni agano kwa Daudi alilofurahia katika maisha yake yaliyobakia: “Fadhili za BWANA nitaziimba milele”, ameandika katika Zaburi 89. “Mimi sitalihalifu agano langu”, Mungu alisisitiza, “Neno moja nimeliapa kwa Utakatifu wangu; hakika sitamwambia Daudi uongo. Wazao wake watadumu milele, na kiti chake cha enzi kitakuwa kama jua mbele yangu” (aya 1,34-36). Mara nyingine tena , Mungu alifanya ahadi ambayo, kwa Utakatifu wake, hawezi kuihalifu, naye Mfalme Daudi, kama Abrahamu, akiamini Mungu wa milele atatunza neno lake. Hatuna budi sasa kwa haraka kutia mkazo kupitia karne tano zaidi kufuatilia mfululizo wa mambo ambayo Mtume Petro anayaita katika Biblia ya UV. “Mungu ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani” (2Petro 1:4). Ni alama zilizoachwa na watu waliopita zenye mwisho wa kufurahisha. Kutimiza Ahadi… Sulemani, mwana wa Daudi alimjengea Mungu nyumba, Hekalu lenye fahari na lenye gharama pale Yerusalemu lililodumu kwa miaka mamia.Alipokufa, vita ya kiraia ikaigawa nchi ; na taifa likaja kutawaliwa na wafalme wawili walioshindana. Muda ulipopita, nguvu za kiroho kwa watu zikapungua na sheria za Mungu hazikutumika. Ukawepo ugomvi toka kipindi hadi kipindi, zaidi miongoni mwa makabila Yuda na Benyamini walioshika Hekalu na mji mkuu wa Yerusalemu. Lakini pole pole uadilifu ukashuka, na ustahimilivu wa Mungu ukaondolewa kabisa. Haki ya Israeli kuikalia nchi ilitegemea utii wao kwake, maneno yote mazuri ya upangaji wao ukavunjika. Hiki kilikuwa kipindi cha Manabii. Ukweli kwa jina lake BWANA akaonyesha huruma yake isiyo na kikomo, aliwainua wajumbe maalum waliovuviwa na Roho Mtakatifu ili kuwaonya watu kuwa mwenendo waliokuwa wakiufuata utawaletea balaa. (5) Hayo maonyo hayakuleta mabadiliko. Hatimaye kabila kumi wakavamiwa na Waashuru, wakawahamisha katika nchi, wakafuatiwa na kabila mbili baadaye karne na nusu, walitwaliwa kwenda Babeli. Kwa kweli huo ulionekana kuwa ni mwisho. Hekalu lilipochomwa moto na makao ya kifalme kuharibiwa, Sedekia, mfalme wa kumi na tisa kukalia kiti cha Daudi, alipofushwa macho akachukuliwa mateka, asirudi tena. Ni ahadi gani aliyoahidiwa Abrahamu ya kwamba uzao utamiliki nchi? Na ni jinsi gani agano lililofanywa kwa Daudi kwamba atakuwepo daima mtu wa kukikalia kiti chake ? Je! Mungu alisahau ahadi yake ? Au kibaya, Mungu hakuwa na nguvu kuliko Miungu wa Babeli ? Watu walihitaji sana mwongozo. Katika saa hiyo halisi, taa ya Israeli ilipokuwa inazimika, la kushangaza, zikaja kumiminika ahadi kubwa toka katika midimo ya Manabii. Walisisitiza mabalaa yaliyokuja hayakuwa ajali, bali yalikuwa hukumu ya Mungu.Haikuwepo njia ya kuepuka adhabu. Lakini bado, katika kipindi kinachokuja, lipo tumaini. Taifa halitapotea kabisa. Utakuwepo ufalme wa kutawala katika kiti cha Daudi. Siku moja Mungu atamtuma kwao Masihi, mkombozi mwenye nguvu, atakayewaleta katika nchi waliyoondoka na kutawala juu yao kwa amani milele. Unabii wa Isaya kuhusu Masihi Hapa kuna madondoo matatu katika ahadi alizofanya Mungu ndani ya Kipindi hiki. Zimechukuliwa katika Manabii watatu tofauti. Isaya aliishi kabla ya kufikia mwisho, aliweza kuona maandishi ukutani. “Ole wake, taifa lenye dhambi,” analia katika mwanzo wa sura, “watu wanaochukuwa mzigo wa uovu----wamemwacha BWANA, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma….Kichwa chote ni kigonjwa moyo wote umezimia. Tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna uzima ndani yake” (1:4-6).Hata hivyo sura zote za kitabu chake zipo hai na sifa na shukurani katika ukombozi wa Mungu unaokuja. “Jikung’ute mavumbi, uondoke, pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja. Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa. Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, ameukomboa Yerusalemu”, anatukuza. Amewaona watu waliokanyagwa na Mataifa yenye kulipa kisasi Mungu anapotokea katika moto na tetemeko ili kuwakomboa: “Mtu hodari atakuwa kama makumbi….”Halafu anaendelea, “kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume; na uweza wa Kifalme utakuwa mabegani mwake. Naye ataitwa jina lake,Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo na enzi yake na amani hayatakuwa na mwisho kamwe, katika kiti cha Daudi na Ufalme wake; kuuthibitisha na kuutegemeza kwa hukumu na kwa haki, tangu sasa na hata milele”(9:5-7). Anatoa picha ya kuonyesha mwisho huyu mfalme atakayeketi katika kiti cha Daudi akitawala dola la ulimwengu mahali ambapo mataifa yote yakiishi kwa amani, na sheria za Bwana zitatoka Yerusalemu: “Na itakuwa katika siku ya mwisho”,anaanza, “…..maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA katika Yerusalemu.Naye atafanya hukumu katika mataifa mengi, atawakemea watu wa kabila nyingi….taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe” (2:2-4). Unabii huu ulionekana kutoweza kutimia kwa Myahudi aliyekuwa akiishi katika kipindi cha kuangushwa Yerusalemu. Lakini Mungu anayetunza neno lake kwa vizazi elfu alikuwa akiwaahidi. (6) Yeremia na Agano Jipya Nabii wetu wa pili aliishi hasa katika kipindi cha kuzingirwa Yerusalemu. Aliuona mji umetekwa na watu wake wametwaliwa uhamishoni. Hata hivyo Mungu akafanya unabii mwingine kwa Yeremia uliowazi zaidi katika Agano la Kale kuhusu wakati ujao kwa watu wake: “ Angalia, siku inakuja,asema BWANA, nitakapofanya agano upya na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, si kwa mfano wa agano lile nililofanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja.” Agano la Kale ni hilo lililofanywa na taifa pale Sinai, ambalo liliwapa Nchi ya ahadi, kwa masharti. Hili agano jipya limeingia mahali pa lile la Kale: “Agano hili ndilo nitafanya na nyumba ya Israeli, baada ya siku zile, asema BWANA; nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika; nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu”. Badala ya sheria zake kubakia katika mbao za mawe, zitachukuliwa ndani ya mioyo ya watu. Watu wote watamjuwa Bwana, aliendelea, naye Mungu atasamehe uovu wao, wala dhambi yao hataikumbuka tena (Yeremia 31:31-34). Ikiwa habari yote kwa kina haikuelekea kutokea kwa wasomaji wa Yeremia, wakaondoka kuelekea utumwani Babeli; aliweza kuwachangamsha na maneno haya: “Tazama, nitawakusanya, na kuwatoa katika nchi zote nilikowafukuza katika hasira yangu,…..nami nitawaleta tena hata mahali hapa, nami nitawakalisha salama salimini…Nami nitawapanda katika nchi kweli kweli, kwa moyo wangu wote na kwa roho yangu yote” (32:37,41). Yeremia alirudia tena na tena ahadi ya kukusanyika tena. Na iwapo imani yao ilivunjikavunjika kwa kumwona mfalme wao akitwaliwa machoni pao, hata hivyo alikuwa na uthibitisho kuhusu kiti cha enzi: “Nitamchipushia Daudi chipukizi la haki; naye atafanya hukumu na haki katika nchi….Maana BWANA asema hivi, Daudi hatakosa kuwa na mtu wa kuketi katika kiti cha enzi cha nyumba ya Israel” (33:15-17) “Hukumu na haki”- maneno hayo ni taarifa inayojirudia tunayoipata katika Isaya miaka mia moja na hamsini ya awali. Manabii wote wawili wametoa picha ya jamaa inayoendelea kama mti, ambao tawi maarufu litazuka, mtu wa kipekee atakayeketi katika kiti cha enzi milele. Hakika na thabiti, vile vile, katika manabii wote wawili ni ahadi ya Abrahamu kurithi nchi. Walihakikishiwa watu mbali na kutawanyika kwao. Ezekiel aliona Maono ya Ufalme Hatimaye tunakuja kwa Ezekieli aliyeishi siku za baadaye. Ezekieli alitumia maisha yake yote akiwa ni mfungwa Babeli. Naye pia aliona maono ya kustajabisha sana ya amani na baraka kwa watu wa Abrahamu: “Maana nitawatwaa kati ya Mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe”, alitabiri; “ Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote.” Mungu anaenda kusamehe na kusahau matendo mabaya ya taifa (Ezekieli 36:24,25).Kama manabii wa kwanza waliomtangulia, Ezekieli anaimba ujio wa mfalme wa ahadi ya mababa wa Israeli: “Nao watakaa katika nchi niliyompa Yakobo, Mtumishi wangu, walimokaa baba zenu; nao watakaa humo, wao na watoto wao, na watoto wa watoto wao milele; Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele” (37:25). Udhahiri na juhudi havina makosa ya hakikisho la Mungu kwa watu wake. Ingawa wakati uliopo ni giza, walikuwa na jambo lingine la uhakika sana walitarajie kutokea mbele. (7)Waisraeli walikuwa watumwa Babeli kwa robo tatu ya karne. Mageuzi yalifuata, ambayo ndani yake dola la Babeli lilipinduliwa na Waajemi. Katika mwaka wa kwanza wa kutawala kwake mfalme mpya akatangaza msamaha wa kufunguliwa, ulioruhusu mtu awaye yote wa kabila ya Yuda aliyetaka arudi kwenye nchi yao wenyewe. Wengi walifanya hivyo, wakaanza kazi ya kuhuzunisha sana ya kujenga tena magofu yaliyoharibika. Labda walikuwa na shauku yenye matumaini iwapo Masihi angetokea na kufanya maisha yawe rahisi kwao. Ilikuwa kweli walipata, walirudi toka utumwamni, lakini maisha yalikuwa ni yale yale. Waliugua chini ya kodi ya mabwana wao wa kifalme, na miaka ilipopita walivamiwa na kupondwa na majeshi toka Kaskazini na Kusini. Idadi kubwa ya ndugu zao wakabakia katika utawanyiko, wakitangatanga mbali zaidi kati ya mataifa. Hakuna mfalme wa kuketi kwenye kiti cha enzi cha Daudi. Ujio wa Yesu Mwanamwali toka kabila ya Yuda, aliposwa ila hakuwa ameolewa, alikaa nyumbani mwake kule Nazareti. Alishangazwa na mtu aliyebisha mlango, akajikuta yeye mwenyewe anazungumza na mgeni aliyemtembelea aliyesema kuwa ni malaika wa Bwana: “Utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume”, alimwambia , “na jina lake utamwita Yesu”. Hadi hapo maneno haya yamezoeleka katika michezo ya maigizo wakati wa Christmas(Krismas). Lakini hebu tafakari ujumbe uliosalia: “Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye Juu,”alisema malaika, “na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, Baba yake, atamiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na Ufalme wake utakuwa hauna mwisho”(Luka 1:31-33). Hakuna kukosea, je! lipo kosa , katika muunganiko na ahadi hizo kwenye Agano la Kale? “Nguvu zake Aliye Juu zitakufunika”, aliendelea, “kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitakuwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”(aya 35). Katika tendo moja, siri ya karne nyingi ikaja kuwa dhahiri. Yesu mwana wa Mariamu alikuwa mtu wa pekee, ni yeye tu awezaye kutimiliza agano na Daudi. Alitoka katika ukoo wa Daudi, katika jamaa yake mwenyewe. Wakati uo huo alikuwa Mwana wa Mungu: “Nitakuwa Baba yake”, Mungu alimwambia Daudi, na uweza wa Mungu Roho Mtakatifu ulifanya Yesu azaliwe. Tena, Yeremia aliahidi, “Daudi hatakosa mtu wa kukaa katika kiti cha Daudi”, na malaika alisema Yesu atamiliki milele, juu ya kiti hicho halisi cha enzi. Mwishowe, kwa kuwa Daudi alikuwa uzao wa Abrahamu, Yesu alisimama katika mstari wa ahadi za Abrahamu kuhusu kubarikiwa mataifa yote vile vile: “Ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao,”Yalikuwa maelezo ya jina lake (Mathayo 1:21), ni baraka ya jinsi gani inayoweza kuwepo kuliko kuondoa mzigo wa kutisha wa mwanadamu-dhambi inayoleta huzuni, magonjwa na mauti kwa watu wote? Hivyo, kwa ukimya pasipo mfululizo wa matukio ya kushitusha, mtu ambaye Israeli na ulimwengu unategemea akazaliwa katika hori ya kulishia ng’ombe mjini mwa Baba yake Daudi. Kazi Ya Kristo Yesu alipoanza mahubiri yake pote kote akiwa na umri wa miaka thelathini, yalikuwepo matarajio makubwa katika Yuda. Wafuasi wake walimwita Masihi au Mtiwa Mafuta-Mwokozi ajaye. Jina Christos au Kristo katika Kiyunani cha Agano Jipya ni sawasawa hasa na Agano la Kale ‘Masihi’. Kila mmoja alitarajia atashindana na Waroma, kuwaweka Israeli huru toka maadui wake, kisha atwae kiti cha enzi. Miujiza yake ya ajabu ya kuponya iliongeza uthibitisho huu wa kwamba alitumwa toka kwa Mungu (8)Watu walikatishwa tamaa kwa kile wasichotarajia. Yesu alibakia kuwa mwalimu mwenye kuzungukazunguka na akadharauliwa na wale waliofungamana na utawala. Maadui wake viongozi wa Israeli, wakiwa wamejaa wivu kwa sababu ya umaarufu wake, kwa kufanikisha walipanga kifo chake. Baada ya miaka mitatu, ambayo ilibadilisha maisha ya maelfu kwa mfano wake na mafundisho yake ya utulivu, alisalitiwa na kuhukumiwa kuwa ni mhalifu. Wayahudi wakabakia katika kutawanyika, bila kukusanyika. Kiti cha enzi cha Daudi kimesalia kuwa tupu. Hata mwili wa Yesu ulitoweka. Ilionekana kana kwamba, mara nyingine tena,Mungu alifanya ahadi, yote ikaja kuwa haina kitu. Kwa majuma marefu sita, Yerusalemu ulilala. Siri Ikafunuliwa. Ghafla mji ukawa hai na habari ya kushangaza. Wanafunzi wa Yesu, wakiwa wamejaa na uwezo wa Roho Mtakatifu yeye yule aliyewavuvia manabii wa kale, wakawa wakitangaza ya kuwa Yesu alikuwa yu hai tena. Walikuwa wamemwona, walikula naye na kumwona akipaa kwenda mbinguni. La kushangaza zaidi, waliweza kuonyesha toka hayo Maandiko ya Agano la Kale ya kwamba kila moja waliyofikiri walijuwa vema, ya kwamba Masihi alikusudiwa kufa msalabani, na kisha kufufuka. Hakuna lililokuwa na kosa. Wote ulikuwa ni mpango wa Mungu. “Mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo”, alieleza Petro mvuvi. “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani, ambaye ilimpasa kupokelewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu” (Mdo. 3:18-21). Mambo yote yakawa wazi tena. Yesu amekuwa Mwokozi wa Israeli na mataifa ya ulimwengu, kama manabii walivyosema. Lakini imempasa kuja mara ya pili. Ilimpasa kuja mara ya kwanza kufa kama mtwaa dhambi, Mwokozi Mkuu katika adui mkubwa- dhambi na mauti ya milele. Imempasa kuja mara ya pili; kuwaokoa watu wake toka wadhalimu wao na kutawala juu ya ulimwengu mzima.Alipaa kwenda kwa Mungu kuketi mkono wa kuume, lakini si milele. Atakuwepo huko “HATA” wakati wa kuanzisha yote upya yaliyonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii. Kuwa na ufunguo huu, unabii wa Masihi unafunguka kama hazina katika sanduku.Mafungu ya maneno mahali ambapo Masihi anatawala kwa ushindi yaonekana yamefunikwa na maelezo ya mauti yake papo hapo yanakuwa dhahiri. Angalia kwa mfano, katika Isaya mlango wa 52 na 53. Mlango wa 52 unaelezea furaha ya Yerusalemu unapokombolewa na Masihi toka kwa watekaji wake. Mlango wa 53 unatoa maelezo yenye kutabiri maumivu na kuaibishwa kwake msalabani. Kuonekana kuja mara mbili, sehemu zote mbili za sura zinafanya wakati mkamilifu. Au Zaburi ya 2; ikitazamwa na aina moja fungu hili la maneno linatuelezea maadui wa Masihi wakiungana kumuua. Ukibadilisha urefu wa kuangalia jambo, unaye Masihi mara nyingine tena amezungukwa na maadui, ila mara hii akiwa mshindi, kama Baba yake alivyoamuru: “Nami nimemweka mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu” (aya 6). Tunaweza kuendelea, lakini utapata furaha katika kufafanua siri wewe mwenyewe. Hivyo ndivyo hasa Mitume walivyoliita Agano Jipya habari njema---siri imedhihirika, ambayo sasa walikuwa na ufunguo. (9)Haja ya Kuja Kristo Mara ya Pili Vile vile ilikuwepo siri nyingine ambayo Mitume waliweza kuitatua. Tayari utakuwa unauliza swali lililo wazi- Ni kwa sababu gani Mungu alipanga kuja mara mbili ? Ni kwa sababu gani Yesu alifufuka katika wafu mwenye uweza wa kutokufa tena, kutawala mara moja juu ya kiti cha enzi cha Daudi ? Kwa nini pamekuwapo kipindi kirefu karibu miaka elfu mbili ? Jawabu kwa swali hilo ni la muhimu hasa kwako na kwangu, nalo linashughulika sana na Agano Jipya. Hebu tusome maneno ya Mtume Paulo katika Waefeso 3. “Siri hiyo” anasema, “kwa kujulishwa nalifunuliwa. Hawakujulishwa,” aliendelea,”wanadamu katika vizazi vingine kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho, ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili” (aya 3,5,6). Haya ni maneno ya kustaajabisha. Mataifa ni watu wasio Wayahudi. Kwa karne nyingi, maneno ya Mungu na ahadi zake yalihusika na watu wa Mungu. Sasa, anasema Mtume, jarife la Injili limeenea sehemu pana kujumuisha watu katika mataifa mengine. Hizo ahadi kuu za Ufalme Masihi atakapo tawala zaweza kuwa ni zetu pia. “Kwa ajili ya hizo”, ameandika, “kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili…. mlikuwa hamna Kristo, mmetengwa na jamii ya Israeli, wageni wasio na maagano ya ahadi. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo” (Waefeso 2:11-13). Je! umegundua ni jinsi gani fungu hili la maneno linavyopamba neno letu tunaloandika, Tumaini la Israeli ? “Kutokana na tumaini” ndivyo waumini Waefeso walikuwa hivyo.Ndivyo walivyo mamilioni leo, kwa muda huu unaweza kujisikiaje. Lakini walijifunza kuhusu “maagano ya ahadi” ambayo tumekuwa tukisoma. Walishika tumaini lililotunzwa katika hizo ahadi. Kwa njia ya damu ya Kristo, waliletwa karibu. Agano lililotiwa Muhuri na Damu Maagano bora ya ahadi aliyofanya Mungu bado ni ya wakati ujao.Hatujui kikamilifu ni lini ahadi zitatimia. Idadi kubwa ya watu walioamini na kutumainia ahadi za Mungu tayari wamo makaburini, na bado ipo nafasi nasi tutakufa vilevile, kabla Yesu hajarudi. Lakini ukweli wenye utukufu ni kwamba hata kama tukifa, bado tunaweza kuonja furaha ya Ufalme wa Mungu. Kama mtume Paulo alivyoandika akiwa jela yake ya mauti, tunaweza kurudishwa tena katika uhai, kupokea “taji ya haki ambayo Bwana”, alisema , “atanipa katika siku hiyo, sio mimi tu, bali pia na wote waliopenda kufunuliwa kwake. Masihi atakaporudi atawafufua wote katika wafu waliokufa katika imani, na kuwapa mwili usiokufa wenye nguvu kama wa kwake. Ni yakini Abrahamu atakuwepo, na hivyo Daudi, na Paulo. Nasi tunaweza kuwapo vile vile. Yote yawezekana katika damu ya Kristo, iliyotuleta karibu kwa Mungu. Kwa maana tukiwa Wayahudi au Mataifa, ni wenye dhambi. Tunavunja sheria za Mungu, hatustahili lolote bali mauti. Kifo cha Yesu kuitoa nafsi yake isiyo na dhambi kuwa dhabihu, kilivunja nguvu za kaburi kwa wote wanaojiunga naye.Basi kuja mara mbili muunganiko wake hautengani. Msalaba huitangulia taji, mtumishi mwenye kuteseka anakuwa mfalme wa wafalme. Na nchi ile ile ambayo Abrahamu alingojea katika hema lake na Yesu alitembea na habari njema za Ufalme, wanapewa wote wawili na jamaa yao pande zote, kufurahia milele. (10)Petro aliposimama Yerusalemu siku ya Pentekoste na kuanza kueleza siri ya kuja mara mbili, alikuwa na ujumbe muhimu kwa watu wabadilike. Tutazame tena maneno yake: “Tubuni basi,” alipaza sauti, “mrejee tena” (Mdo3:19). Alikuwa akiwaasa wasikilizaji wake wajiandae kwa ajili ya ujio wa Yesu kwa kubadili maisha yao, wageuke na waelekee njia tofauti na awali. Awali siku ile umati wa watu walipomuuliza wafanyeje aliwaambia: “Tubuni, Mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Yesu Kristo kwa ajili ya ondoleo la dhambi” (2:38). Warithi wa Ahadi Mara ukianza kufahamu tumaini aliloweka Mungu mbele yetu katika neno lake, unataka kujua namna ya kulishika. Unaelewa kadiri unaposoma zaidi, ya kwamba umeweka uwiano sawa kwa watu kufuata ambao hujaanza kuufikia. Kama kweli unataka kumpendeza Mungu, unaona ipo haja, kama wale watu kule Yerusalemu, kuwa na dhamiri safi. Njia ambayo Mungu ametuamuru ni kubatizwa katika Bwana Yesu, kwa mfano kuosha katika maji mwenendo wetu wa maisha ya kale, na kuanza tena maisha mapya kama mtoto aliyezaliwa, washirika wa watu watakatifu wa Mungu. Halafu, Agano Jipya linasema kwa nguvu, tutakuwa warithi wa hizo ahadi za Ufalme wa Mungu: “Kwa kuwa katika Kristo Yesu”, ameandika Paulo, “mnakuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani” (Wagalatia 3:26). Fikiri hilo! Ni bahati gani kuitwa wana na binti wa Mungu! “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo Yesu mmemvaa Kristo. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi” (aya 27-29). Yote ambayo Yesu anarithi---nchi, kiti cha enzi, baraka-yote yatakuwa yetu. Ni ya kusisimua na kugusa moyo kiasi gani, kuwaza anayotupatia Mungu. Ni kama kwamba tayari tumeingizwa katika agano jipya ambalo Mungu atafanya na watu wake. Sheria za Mungu zimeandikwa katika mioyo yetu, dhambi zetu zimeoshwa, tumeorodheshwa kuwa na sehemu kipindi hicho hapo vita na njaa, dhambi na huzuni vitaondolewa milele katika dunia. Paulo anatumia mfano mwingine katika Warumi 11. Anasema sisi wa Mataifa tumefananishwa kama machipuko ya mti wa mzeituni mwitu ambao umechukuliwa na Mungu mwenye bustani na kupandikizwa katika kikonyo cha mti wa mzeituni wa Israeli. Tunashiriki unono unaotunza uhai wa mti, nasi tutakuwepo pale katika kipindi cha mavuno. "Kwa maana ndugu zangu, sipendi msiijue siri hii”,anasema, anapoendelea kueleza nafasi ndefu kati ya kuja kwa pili: “ni kwa sehemu ugumu umewapata Israeli”. Ana maana ya kwamba ni idadi ndogo tu ya watu wa Kiyahudi walioipokea habari njema aliyoileta Yesu na mitume; mioyo ya waliobaki ilikuwa migumu mno kwa mbegu njema ya Ufalme kuweza kuota. Lakini ugumu wa moyo wa Israeli si wa kudumu. “Mpaka utimilifu wa Mataifa uwasili”, anaendelea, “hivyo Israeli wote wataokoka kama ilivyoandikwa”---ananukuu toka fungu la maneno ya Masihi katika Isaya ---“Mwokozi atakuja kutoka Sayuni, atamtenga Yakobo na maasi yake. Na hili litakuwa agano langu nao”, anaongeza, akirudia fungu la maneno tunayosoma katika Yeremia 33, “nitakapowaondolea dhambi zao” (Warumi 11:24-27). (11) Angalia muda wa kipindi- hapo idadi kamili ya wa Mataifa iwasili, yaani iingie.Bado haijawasili. Hata sasa Mungu anatuita kuja katika jamaa yake. Lakini siku moja, mapema, labda mapema sana, mlango utafungwa. Bwana Yesu atakuwa hapa akiwa na uwezo wa kutawala Mataifa, na kuwaleta watu hukumuni kwa kudharau sheria za Mungu. Ishara zinazoonyesha kwamba Mungu Hajasahau Tunajuaje kuhusu kuja kwa Yesu kumekaribia sana? Lipo jibu moja rahisi. Tazama Waisraeli! Kwa karne nyingi walitawanywa katika Mataifa, kamwe hawajaangamia, kama wasivyoweza, iwapo Mungu anatunza neno lake.Katika kizazi chetu wenyewe, walianza kwenda katika nchi yao. Katika mwaka l967 waliutwaa mji wa Yerusalemu, au Sayuni mji wao wa zamani. Na sasa adui zao wanajikusanya tena juu yao. Tukio limepangwa Mwokozi kuja katika kiti chake cha Enzi, kwa ajili ya Mungu kumweka Mfalme wake juu ya Sayuni mlima wake Mtakatifu. Ishara zote zipo kutia nguvu imani yetu. Mungu anayetunza maagano yake kwa vizazi elfu mkono wake sio mtupu tena. Hebu tumalize na maneno yenye kupendeza, yanayojumlisha Tumaini hili kuu la Israeli tumekuwa tukifikiria kwa muda mrefu. Tumesema linaweza kutupatia faraja, mwongozo, na ujasiri katika kukabili mawimbi yote ya maisha. Hivi ndivyo Mtume anaeleza katika barua waliyoandikiwa Waebrania: “Mungu alipofanya ahadi kwa Ibrahimu……aliapa kwa nafsi yake akisema, ‘Hakika nitakubariki na kukuzidisha’ ”. Nanga yenye Salama “Katika neno hilo” anaendelea, “Mungu akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati, ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo,-----sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yamewekwa mbele yetu” (Waebrania 6:13-18) Vitu viwili visivyobadilika: tunalo neno la Mungu, ambalo peke yake linatosha. Kwa kufaya hakika maradufu ametupatia kiapo vile vile. Ina maana hatutakiwi kuwa na shaka kuhusu ahadi ni hakika itatimia na kuwa kweli. “Tuliyo nayo” anamalizia, “kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu” ( aya 19). Wanaume na wanawake wanaoamini ahadi za Mungu wapo salama kama merikebu, inayoyumbishwa usiku katika bahari iliyo na hasira, imelindwa katika hatari zote kwa nanga imara iliyotumbukia katika kina kirefu kwenye mwamba chini. Kwa nini usifanye tumaini hili kuwa lako ? DAVID M. PEARCE. (12) Tena: 1 902059 00 - X Matayarisho ya Ubatizo 1 902059 01 - 8 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 1-4 1 902059 02 - 6 Ukimwi 1 902059 03 - 4 Mshitaki Wenu Ibilisi 1 902059 04 - 2 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 5-8 1 902059 05 - 0 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 9-11 1 902059 06 - 9 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 12-15 1 902059 07 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 16-19 1 902059 08 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 20-23 1 902059 09 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 24-27 1 902059 10 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 28-31 1 902059 11 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 32-36 1 902059 12 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 37-40 1 902059 13 - 1 Ufunuo Mlango wa Kwanza 1 902059 14 - X Ni kweli Yesu Kristo alishuka kutoka mbinguni? 1 902059 15 – 8 Nyimbo za ndugu wa Kristo 1 902059 16 – 6 Ufunuo Mlango wa Pili 1 902059 17 – 4 Katiba ya Makanisa 1 902059 18 – 2 kitabu-mwalimu wa kristadelfiani 1 902059 19 – 0 Kuanzisha Kristadelfiano (CBM) Eklesia 1 902059 20 – 4 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura moja 1 902059 21 – 2 Ni kwa sababu gani Mungu anaruhusu mateso? 1 902059 22 – 0 Ufufu Kwa Hukumu 1 902059 23 – 9 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura mbili 1 902059 24 – 7 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura tatu 1 902059 25 – 5 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura nne 1 902059 26 – 3 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura tano 1 902059 27 – 1 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura sita 1 902059 28 – X Fungu Lako Katika Ahadi za Mungu Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya Biblia kaitka somo hili muhimu. Lina itwa Kuishi katika Ukweli. Unaweza kupata nakala kutoka Kanisa la Christadelphian, au kutoka anuani iliyoandikwa katika kijitabu hiki. ? CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW ISBN 1 902059 28 -X Registered Charity Number: 248979 / 1020558 Company Number: 2796412 Telephone +44 (0) 1604 765068 Email: CarlHinton@hotmail.com Web: http:\\www.cbm-tz.org