JUZUU NYINGINE KATIKA MFULULIZO "UKWELI KUHUSU", 1. UTATU 2. UFUNUO 3. UBATIZO 4. KUHILIKISHWA 5. MPINGA KRISTO 6. INJILI 7. WOKOVU 8. WAYAHUDI 9. DINI 10. MALAIKA WALIOTUPWA 11. MASHETANI 12. LUSIFA 13. IBILISI 14. ROHO MTAKATIFU 15. YESU KRISTO 16. NAFSI 17. ELOI 18. IBILISI / SHETANI 19. WAKATI WA TAABU YA YAKOBO 20. MTUME PAULO 21. ALAMA YA MNYAMA 22. "KUWAPO KABLA KWA" YESU KRISTO 23. UFALME WA MUNGU DUNIANI 24. KUJA KWA PILI YESU KRISTO KIELEZO: TUNAUTARATIBU MPANA WA KUGAWA JUZUU BURE NYINGINE KATIKA MASOMO MENGI YA BIBLIA. VILEVILE, TUNAWEZA KUTOA HUDUMA ZA BURE ZA USOMAJI WA BIBLIA KWA KUTUMIA CHATI ITAKAYO KUONGOZA KATIKA KUSOMA AGANO LA KALE MARA MOJA KWA MWAKA NA AGANO JIPYA MARA MBILI Kwa habari hizi zaidi kuhusu masomo ya bure wasialiana na: Kwa hisani ya : CBM Publications 32 Blenheim Rd, Far Cotton, Northampton, England NN4 8NW UKWELI KUHUSU .........MPINGA KRISTO......... JUZUU HII: INATUAMBIA KUHUSU MPINGA KRISTO NINI MAANA YA MPINGA KRISTO NA BIBLIA INAVYOFUNZA KUHUSU MPINGA KRISTO MPINGA KRISTO: Neno MPINGA KRISTO linaweza likapatikana mara 5 tu, kwenye Maandiko yote, ni kama nyaraka za mtume Yohana 1. Yohana 2:18 ..... KAMA VILE MLIVYOSIKIA YA KWAMBA MPINGA KRISTO YA UAJA...... 1. Yohana 2:18..... HATA SASA WAPINGA KRISTO WENGI WAMEKWISHA KUWAPO 1. Yohana 2:22 ..... YEYE AKANAYE YA KUWA YESU NI KRISTO HUYO NDIYE MPINGA KRISTO 1. Yohana 4:3 ..... NA HII NDIYO ROHO YA MPINGA KRISTO 2. Yohana 7 ........ WADANGANYIFU WENGI..... WASIOKIRI YA KUWA YESU KRISTO YU AJA KATIKA MWILI HUYO NDIYE YULE MDANGANYIFU NI MPINGA KRISTO UFUNDISHAJI WA KIDINI ULIMWENGUNI KOTE: Kwa kifupi ufundishaji huu ni kwamba "Mpinga Kristo ni mtu mwenye umaarufu mkubwa, atat oka Israel na kudai yeye ni Masihi. Katika SIKU ZA MWISHO atainuka haraka kwa nguvu na kutukuzwa na Wayahudi. Ata-jenga Hekalu kwenye eneo la msikiti uliopo Yelusalemu wa Omari, ambao siku hizi unazingatiwa sana na mataifa ya Waarabu kuwa ni hazina yao maalum kidini. Atafanya "Agano" na wayahudi kwa kuwa kiongozi wao kwa miaka mitatu na nusu, baadaye kidogo atapanua utawala wa nguvu juu ya ulimwengu mzima. Atavunja lile agano alilofanya na Wayahudi na kuwaleta kwenye janga kubwa na baadaye Masihi wa KWELI atatokea, na kumwangusha asiwepo tena. Ubishi wa wazo hili lipo kinyume na Neno la Mungu kuhusu kuja kwa Yesu 'kama mwivu" (uf.16:15) ikiwa wazo la mpiga Kristo lingekuwa ni la kweli kwa jinsi linavyofikiriwa na wengi, mataifa yangekuwa na maonyo mwengi ya kuhusu kurudi kwake Masihi. Sio hivyo tu, yapo magumu mengi ambayo hatuwezi kwa muda huu kutoa maelezo, kwani nafasi hii ni ya kutoa hoja kamili. UKWELI kamili ni kwamba .... Nguvu za Mpianga Kristo zipo hapa tayari duniani na zimekuwepo kwa mamia ya miaka mingi. ROHO YA MPINGA KRISTO: Tofauti na mafunzo ya siku hizi, hakuna kiunganishi cha moja kwa moja cha Maandiko kinachoweza kuwekwa kati ya MPINGA KRISTO na MWOVU ..... MTU WA KUASI ..... MWANAWA UHARIBIFU ..... YULE MNYAMA ..... ILE PEMBE NDOGO ..... AU YULE MWASI. Hakuna popote katika Biblia Neno la Mungu limewahi kudai katika matamshi rahisi ya kwamba yeyote Wa hawa ni MPINGA KRISTO. Walakini, kwa sababu ya maana kamili ya ma-neno Mpinga Kristo au Wapinga Kristo, yeyote wa hao, na kwa kweli yeyote kati yetu aweza kuwa MPINGA KRISTO. Mtume Yohana hakufundisha kwamba Mpinga Kristo alikuwa ni mtu mmoja maalum kabisa aliyejulikana, bali ni kwamba alikuwepo, na ipo ROHO YA MPINGA KRISTO, badiliko la wazo linatokana ya kwamba Kristo alikuja katika mwili. Wengi wanaodai kuwa ni Wakristo watanyanyua mikono yao juu kwa sikitiko la kidokezo cha kwamba watakuwa ni wapinga Kristo, lakini jambo hili linatokea siku hizi, kama tutakavyotoa nnaelezo. UPINZANI ULIOJITOKEZA BAADA YA BADILIKO LA WAZO: Ukweli na ushahidi ulio wazi wa wazo hili ni dhahiri limeandikwa kuwa ...... "KILA ROHO (MTU) ISIYOKIRI KWAMBA YESU KRISTO AMEKUJA KATIKA MWILI, HAITOKANI NA MUNGU; NA Hll NDIYO ROHO YA MPINGA KRISTO, AMBAYO MMEISIKIA KWAMBA YAJA; SASA IMEKWISHAKUAKO DUNIANI. :Je! Unaona urahisi wa haya maelezo? Mtume Yohana ameweka wazi upokeaji wa imani isiyo sahihi toka Biblia, ipo kwa watu wengi, hasa kwa siku hizi, kwa kulinganisha pamoja na upinzani wa badiliko la Wazo la akili hii anaita ni ROHO YA MPINGA KRISTO. Hii nj kinyume na ROHO WA KWELI ambaye Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa tayari anakaa ndani yao (Yn 14:17). Hii ROHO YA MPINGA KRISTO. Upinzani wa badiliko la wazo ametaja kinaga - naga ili kwamba pasiwepo mtafaruku. llikuwa ni ukiukaji wa mafunzo ya Biblia wazi ya kwamba YESU ALIKUJA KATIKA MWILI. JE YESU ALIKUWA "MUNGU" KATIKA UTATU? Huo "ukiukaji" wa kufur.disha mambo yaliyo wazi toka ndani ya Biblia unastaajabisha kwa kuwa unaonekana wazi kwenye makanisa mengi leo. Kwa kuwa wanaenenda na uzalishaji wa sera za kirumi ya kwamba Yesu kwa kweli alikuwa Mungu, kiumbe wa roho, aliyejibadilisha kwa kuvaa mwili, nafsi ya kiroho aliyekuwa "Mungu Mwana" nafsi ya pili" (inayodhaniwa) na utatu, sera hata Kanisa la Roma linahusishwa katika mojawapo ya mafundisho ya utaratibu wake, kamwe haukutambuliwa na watu wa Mungu. Kwenye Kitabu cha 2 cha mafundisho ya utaratibu wa Katoliki (Catholic Catechisms for schools) ya mashule toleo la tarehe mosi, September 1963 .... MUNGU HAKUWAAMBIA WATU WAKE ...... (wayahudi) na (mtu wa mataifa)?? SIRI ILIYOBARIKIWA YA UTATU WALA HAKUSEMA KWAMBA MASIHI MWENYEWE ANGALIKUWA MUNGU MWENYEWE MALENGO YA UFUNUO WA IMANII Katika uthibitisho wa wazi kwa udanganyifu unaofundishwa kwa mamilioni kitabu kiitwcho ENCYCLOPAEDIA BRITANNICA hapo kinasema ...... "Sera ya utatu pamoja haukutolewa moja kwa moja toka kwenye Agano jipya na sera hii haikuweza kuelezwa kwa maneno yaliyo katika Agano jipya ..... Yalikuwa ni matokeo ya hoja,MAWAZO juu ya ufunuo wa imani ....... Uliundwa tu kupitia kame za jitihada, yaliundwa kipekee kwa usaidizi wa mawazo yaliyotungwa na kukubalika katika utaratibu wa falsafa za Wayunaai & Warumi....." "MPINGA KRISTO" SIO FUNDISHO LA BIBLIA Kwa maneno mengine, utatu unapomkana Yesu Kristo kuja katika mwili, ni kuonyesha kwamba sio fundisho la Biblia. Ni mawazo yaliyoungwa na ndiyo msingi wa ROHO YA MPIPNGA KRISTO. Kwa kuwa mafundisho ya Utatu hayamo katika Biblia, sio FUNDISHO LA MUHIMU KWA WOKOVU". Kama Makanisa mengine yanavyodai yanapowashurutisha waumini wao wakubali kuwa ni "kweli Utatu upo"