_____________________ Ufufuo Kwa Hukumu Raised To Judgement _____________________ Kufasiri: Simon Uswegi Kuumba: Carl Hinton Biblia inafundishaje ? MITUME wa Yesu Kristo walisafiri katika ulimwengu uliotawaliwa na Waroma kwa ujasiri na ujumbe unaoonyesha wanachokiamini na kuwataka watu waangalie. Yesu alikufa, lakini alifufuka katika wafu na kutukuzwa mkono wa kuume wa Mungu akawapa tumaini jipya wote wanaojaribu kufuata mfano wake wa kutii. Mbali na kudhihakiwa; kubezwa na kudhulumiwa nafsi zao; hawa mitume walitoa sauti ya mwito mkuu wa kusisimua; wao wenyewe wakiwa ni mashahidi wa kufufuka Kristo, waliamshwa kuonyesha matendo, wakitangaza mbele za watu wote tumaini la ufufuo wa wafuasi wote wa kweli wa Bwana Pengine haipo njia bora kwa ajili yetu kujifunza zaidi ya tumaini hili la mkristo la ajabu na kutia faraja na mafundisho yaliyojumuika kuhusu hukumu ya Mungu kwa mwanadamu, kuliko kuyapima katika mahubiri ya mmoja wa hawa mitume aliyeungana na kundi la mashahidi, kama “ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake” ( 1 Wakorintho 15:8 ). Naye pia aliumizwa na kufungwa kwa ajili ya mambo aliyohubiri, lakini wakati akiwa kifungoni hakunyamazishwa bali aliendelea kunena, hata kwa hao ambao walimfunga, juu ya tumaini lililojaa moyoni mwake mwenyewe. Akiwa mbele ya Feliki na Baraza la hukumu. Mtume Paulo alikuwa jela katika kundi dogo la askari wa Dola mbali na mji mzuri mkuu. Lakini hakuna shaka ya kwamba, ingawa jela hiyo inaweza kuwa haikuwa na hali nzuri, watawala wa majimbo makuu yaliyokuwa Kaisaria yalikuwa na hali iliyosawa na vyumba vya kutumika na watu wote vilivyojulikana kwa Feliki kutoka katika maisha yake ya awali kule Rumi. Akiwa na uwanja mpana wa mamlaka aliitisha baraza la hukumu na kutoa alichopendelea na isivyo sahihi kuita haki na bahati na ukali wa ukatili ililingana, na baadaye ulizidi, na mfalme Nero aliyekuja kuketi katika mamlaka. Kando ya Feliki alikuwa mke kijana Drusilla, kwa kueleza sababu kubwa nzuri na akiwa ni mjane kutokana na kufiwa na mfalme wa Siria Azizusi ambaye alimuoa, labda kwa maagizo ya baba yake Herodi Agripa wa kwanza, akiwa kijana mbichi wa miaka kumi na nne. Ikiwa upole wa tabia yake Drusilla ililingana na huo umri wake inaweza kuwepo hoja ya kabla ya wakati wake kwa kuungana na Feliki asiye na elimu zamani kabla ya kifo cha AZIZUSI hali ya mambo iliratibishwa. Ilionekana sehemu ya tabia ya familia ya Herodi kutojali usafi wa ndoa na kuidharau. Yohana Mbatizaji hakufungwa na baadaye alikatwa kichwa na Herodi Antipas kwa majivuno yake alipomlaumu kwa ajili ya kumchukua mke wa ndugu yake ? ( Mathayo 14: 1 - 11 ). (1) Ustaarabu wa watu ni mbovu. Sura ndogo ya utaratibu wa ustaarabu unasetiri uovu na matendo ya zinaa ipo sambamba na karne yetu ya sasa katika ulimwengu. Shutuma dhidi ya njia zake hazikufurahiwa wakati ule kama ilivyo sasa.Hata hivyo ilikuwa juu ya mambo ya maisha haya na mbele ya watu wawili mashuhuri sana waliomfunga Mtume Paulo “alitoa hoja zake katika habari ya haki, na kuwa na kiasi, na hukumu itakayokuja”. (Mathayo 24:25 ). Kwa hiyo inafaa kwamba sisi katika siku zetu tupime mambo yayo hayo ya awali, tukijijua ndani yetu wenyewe, vile vile katika ulimwengu ambao nasi ni sehemu yake, mahitaji ya hali ya juu ya mawazo na mwenendo. Hakuna faraja wala hakitumiki na watu wengi kukisema kipindi kijacho cha hukumu. Jambo linalozungumziwa linaonekana kwa karibu haliwezi kutengana na muungano wa mafundisho ya moto wa kuzimu, ambayo yamekuwa ni jambo la dhihaka na mzaha katika kumbi za muziki. Lakini wakati moto wa milele chini katika tumbo la nchi hakuna mahali palipofundishwa katika Maandiko, hukumu ni sehemu ya lazima kukamilisha orodha ya mambo yatakayoleta katika ulimwengu hatimaye kujaa utukufu wa Mungu Kiasi kama Feliki kale, ingawa kama tukijaribu kuisukuma mada kutoka katika fahamu zetu hatutafaulu. Hata Feliki alishikwa na hofu kama alivyoona muungano wa nguvu kati ya menendo wake wa maisha na maisha yake ya mwisho. Hakupenda kurekebisha mwenendo wake na kujitahidi kufuata “Utakatifu pasipo huo hakuna mtu atakayemwona Bwana” ( Waebrania 12:14 ). Mambo yetu wenyewe yanayotupatia maarifa yanatufundisha ya kwamba, iwe tunapenda au la, upo muunganiko kati ya juhudi na thawabu; na kati ya uasi na adhabu. Ni kanuni ya mwongozo katika kuwaadibisha watoto na usimamizi wa taratibu nazo zimejumlishwa katika fungu la maneno ‘the carrot and the stick’ yaani kutumainia thawabu na kitisho cha adhabu vimetumika pamoja kama njia ya kumfanya mtu ajitahidi sana. Ona maneno yafuatayo, yaliandikwa na mtume yeye yule aliyesimama mbele ya Feliki na Drusilla: (2)“ Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa, nayo inatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, na Mungu mkuu na mwokozi wetu; ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu ili atukomboe na maasi yote na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema” ( Tito 2:11 - 14 ). Basi, kuna kuwajibika kunakowapasa hao wanaotaka kuwa wafuasi wa Bwana Yesu Kristo waishi maisha yanayopatana na huo wajibu, na kutoa nuru ambayo uadilifu na tabia aliyofundishwa. Ili kufanya hivi ni lazima “kukataa ubaya na tamaa za kidunia” hivi sasa kwa upana ambao tunajua uhakika wa kurudi Kristo. Ni jinsi gani maneno haya yanalingana na yaliyonenwa kwa Feliki ! Uadilifu wa Tabia - - Wakati ule na Sasa. Kufuata njia za Mungu (haki) inahusisha kwa kiwango cha juu kuwa na busara. Ni lazima kila mtu akubali ya kwamba akiachwa afuate shauri lake mwenyewe mwanadamu “ ni kama wanyama wapoteao” ( Zaburri 49: 20 ). Ni mara ngapi tunasikia kizuizi chenye kisingizio halisi ambacho kipo kati ya utaratibu na amani katika jamii na utawala wa watu ? Dola la Kirumi lililokuwa limestarabika na kupangiliwa vema, lilishushwa hadhi na watu kama Feliki na Nero, nalo halikuepuka kuwa mateka kwa Wavandali ( watu wa Ulaya ) asili na kabila zilizoitwa vibaya washenzi. Kwa mtindo wa jinsi hii, kama uadilifu wa tabia ya jamii yetu inavunjika vipande vipande na kuheshimu mamlaka inayeyuka, mitaa ya miji yetu inakuwa viwanja vya vita na ugomvi na hofu inaongezeka. Hakuna mahali bora panapodumisha busara au kuwa na kiasi. Badala yake “ kila mtu anafanya yale anayoona ni sawa machoni pake mwenyewe”( Waamuzi 21:25 ). Kiasi kama hiyo ilikuwa kweli hatua muhimu kabisa katika historia ya Israeli, vivyo ni kweli leo. Kwa kweli kama hakuna shughuli za uadilifu wa tabia, haiwezi kuwepo hukumu; au kwa kutumia maneno ya Maandiko, “maana pasipokuwepo sheria, hapana kosa” (Warumi 4:15). Jamii yetu inapodharau uadilifu wa tabia ya kuishi maisha yanayotakiwa na Mungu, kwa hiyo inabidi ikatae wazo la kuwepo hukumu. Fungu la maneno linalojulikana sana katika kipindi chetu, kama ilivyokuwa jinsi moja kutokujali, jamii iliharakisha uangamizi wake kwa gharika na kimbunga katika siku za Nuhu, ni: “Tule na tunywe, maana kesho tutakufa” (3) ( 1Wakorintho 15:32 ; Mathayo 24:28 ; Luka 17:27 ). Mungu ameeleza wazi katika taarifa yake kuwa uovu wa ulimwengu utasababisha hukumu zake ziangamize mno katika dunia: “kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu” (Warumi 1:18). Ingawa hivyo, Somo letu linahusu wajibu wetu mmoja mmoja kuitikia ujumbe wa Injili na kiti cha hukumu ya Kristo iliyo karibu sana. Maana Kesho Tutakufa… Kuwa na wajibu wa kufikiri hivi hakuna mtu kwa matendo yetu ameongezeka kukua. Lakini ya kuvutia zaidi, wakati Mtume Paulo anaelezea, analinganisha na kufikiri hivi na kutokuamini juu ya ufufuo: “Nina faida gani ? Wasipofufuliwa wafu, na tule, na tunywe, maana kesho tutakufa” ( 1 Wakorintho 15:32 ). Basi, ni wazi, ahadi ya ufufuo kutoka katika wafu igeuze mwenendo wa maisha ambayo tunaishi. Ni thawabu ya Mungu aliyowaahidia wanaojaribu katika maisha yao sasa kufuata katika njia zao na Amri kumpendeza Yeye. Kwa hiyo ni muhimu tufahamu ni tumaini gani alilonalo mtu akifa. Sulemani katika kitabu cha Muhubiri, akiangalia tena matendo ya mwanadamu na kipeo cha thamani yao, alieleza ya kwamba: “ Mambo yote yawatukia wote sawasawa; kuna tukio moja kwake mwenye haki na kwake asiye haki - yaani mwovu” ( Muhubiri 9:2 ). Maelezo yake juu ya hali ya mauti ni ya kifupi na wazi sawia: “ Kwa sababu waliohai wanajua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui neno lolote, wala hawana ajira tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa” ( Muhubiri 9:5 ). Hili fungu la mwisho la maneno labda linaelezo mawazo mawili . Kwa upande mmoja muda unapopita wafu wanasahaulika, hata na marafiki wa karibu aliojuana nao; lakini vile vile kumbukumbu la mtu linakoma kifo kinapotokea. Ni kama mashine nyingi za mahesabu zinazowekwa mfukoni kumbukumbu yake inapofanya kazi, kwa muda nguvu zake zinapopatikana. (4)Mara hiyo nguvu ikizimwa, uwezo wa kuhesabu, kuamuru kurudi kumbukumbu, au kuonyesha kazi zingine zimekuwa zimeondoka. Hii ndiyo hali ilivyo wakati wa kufa mtu, kama maneno haya yanavyodhihirisha yalipotamkwa kwa Adamu baada ya uasi wake: “Utairudia ardhi; ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi” ( Mwanzo 3:19 ). Tamaa ya Kutokufa… Je! huu ni uhakika ambao wanaume na wanawake wanataka kukataa, wakitumainia kwa kweli si neno sahihi ? Hakuna kati yetu anayependa kudhani sisi ni viumbe visivyo maisha ya kudumu kwa kweli; kama kipepeo anayeishi kwa siku chache. Walakini juu ya karne nyingi za historia, hii ni kadhia. Mawimbi yetu mmoja mmoja katika dimbwi la maisha yanafaulu kidogo. Hata hao watu ambao ulimwengu unawahesabia ukuu hufanya marekebisho kidogo katika maendeleo ya mambo ya mtu. Lakini ndani ya kila mmoja wetu kuna tamaa ya kutokufa - kuacha jambo fulani nyuma yetu.Wazazi wanaona katika watoto wao maelekeo ya maisha yao wenyewe yakiendelea siku nyingi na pengine maisha ya mtoto yanaharibika na mzazi akitaka kuishi maisha yake tena kwa njia ya watoto wake. Labda ni tamaa hii iliyowafanya wanaume na wanawake kuamini ya kwamba kuna sehemu muhimu katika mwanadamu ambayo kamwe haifi. Huu ni uongo wa kwanza uliotamkwa katika jaribu kwenye bustani ya Edeni: “Hakika hamtakufa” ( Mwanzo 3:4 ).Huu ni uongo mkubwa, ulioambatana na wengi waliokata tamaa, kiasi kama waliookoka katika meli iliyovunjika wakijaribu kuelea katika bahari iliyochafuka juu ya kipande kidogo kilichopatikana cha ubao unaoelea. Si sahihi, na kama tunataka kuwa sahihi wenyewe ni kama tutoke katika uongo, tutake kuweka tumaini letu ndani ya hayo mambo thabiti na imara” kama nanga ya maisha yetu, nanga yenye salama yenye nguvu” ( Waebrania 6:19 U.V.; B.H.N. ). Imani ya Ayubu… Huku kutaka kuishi daima, kwa kuweza kupita toka upande mmoja hadi hatua nyingine kwa faida ya wengine masomo ya ujuzi wa maisha yamefundisha, si mara nyingi. Katika kitabu cha Ayubu, mateso ya huyo mtu mwenye haki yalipokuwa makali sana kwenye imani yake alipaza sauti na kusema: (5) “ Laiti maneno yangu yangeandikwa sasa! Laiti yangeandikwa kitabuni! Yakachorwa katika mwamba milele, kwa kalamu ya chuma na risasi” ( Ayubu 19:23,24 ). Kwa mtu kama Ayubu kufanya kilio cha jinsi hii,ujumbe uliombidi aufunue ni wa muhimu ni lazima. Alikumbwa na maradhi yaliyokuwa mabaya : mauti iliyohai. Kila kuamka asubuhi alitafakari mauti ni hali ya kuwa mwisho na maisha yosiyofaa. Hii iliweka dhahiri na wazi tumaini kuu, iliyokuwa ni hivi alitaka kuhifadhiwa kwa vizazi vijavyo, maana ulikuwa uthibitisho wa uthabiti wake mwenyewe katika msiba: “ Lakini mimi najua ya kuwa Mkombozi ( mteteaji ) yu hai, na ya kuwa hatimaye atasimama juu ya nchi: na baada ya ngozi ya mwili wangu kuharibiwa hivi na funza, hata hivyo katika mwili wangu nitamwona Mungu. Nami nitamwona mimi nafsi yangu, na macho yangu yatamtazama wala si mwingine; mtima wangu unazimia ndani yangu” ( Ayubu19:25-27 ). Kama hivi haikuwa dini ya kuvutwa au upendo uliomminya kutokana na uchungu wa ugonjwa wake ulioshuhudiwa na Mungu mwenyewe ambaye ufafanuzi kwa Ayubu umeandikwa baadaye katika kitabu chake. Anasema kwa marafiki wa Ayubu: “ Kuwa ninyi hamkunena yaliyo sawa katika habari zangu, kama alivyonena mtumishi wangu Ayubu” ( Ayubu 42:7 ). Mambo aliyonena Ayubu ambayo yapo sawa kumhusu Mungu ni ya muhimu kwetu. Alinena nguvu ya Mungu iliyo hai inayoweza kuwakomboa wanaume na wanawake waliojaa dhambi. Kwa muunganiko na huo ukombozi, alieleza tumaini la kwamba atakuwepo kuona na kusikia hukumu ya Mungu juu yake. Hata hivyo Ayubu alifahamu hali ya mauti kama Sulemani alivyoielezea. Alinena kuoza mwili wake, lakini aliamini ya kwamba mwili uo huo utasimama mbele ya Mungu. Jumla ya Fafanuzi za Isaya…. Ikiwa Ayubu alikuwa na sifa njema tu katika Agano la Kale kuweza kufanya kadhia hii tunaweza kuwa na udhuru kuwa shaka juu ya ushahidi wake.Lakini sivyo. Katika unabii wa Isaya mambo tuliyojifunza toka kwa Muhubiri na Ayubu yamerudiwa. Kwanza ona maelezo ya mauti hali yake katika mlango wa 26, aya ya 13 na 14: (6) …. “Mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki …. Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.” Maneno yaliyorudiwa kwa makini, juu ya watu hawa hakuna kuepuka- - ‘wamekufa’ na ‘wamefariki’, hao ‘hawataishi’ wala ‘kufufuka’. Kama Sulemani alivyosema:”Ukumbusho wao umepotea”. Lakini kwa hali iliyo tofauti, na hali ya kukosa tumaini, ni nafasi ya hao ambao ni watu wa Mungu: “ Wafu wako wataishi, pamoja na maiti yangu itafufuka; amkeni kaimbeni ninyi mnaokaa mavumbini: maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa” ( Isaya 26:19 ). Kwa hiyo tulichojifunza ni kwamba ingawa wengine ni kweli kuwa kifo ni hali ya mwisho, kwa wengine, ingawa mauti ni hali ile ile - kukosa fahamu kabisa, jambo “moja linawatukia wote” - lipo tumaini la kufufuka au kutoka katika ardhi. Unabii wa Danieli…. Kupanga madaraja jinsi hii kumechukuliwa hatua zaidi katika unabii wa Danieli mahali ambapo kundi la pili - watu wa Mungu - wanafufuka pasi na kujua hali yao ya mwisho. Njia iliyotumika kueleza ni ya wakati wa muhimu kabisa, kama tutakavyoona: “ Wengi (si wote) wa hao walalao katika mavumbi ya nchi wataamka, wengine wapate uzima wa milele, wengine aibu na kudharauliwa milele” ( Danieli 12:2 ). Tunajua vyema vya kutosha toka katika somo letu ya kuwa hii ni lugha ya Maandiko juu ya mada hii. ‘Mavumbi ya nchi’ ni sauti iliyorudi mara ya pili toka katika taarifa iliyo katika kitabu cha Mwanzo juu ya mkasa wa Adamu na Hawa na watoto wao. Ni bayana kutakuwa na kutenganisha kati ya hao ambao kutakuwa na aibu na kudharauliwa milele. (7) Usingizi wa Mauti…. Kwa pamoja na mafungu mengine ya Maandiko yanayotaja mauti ya hao ambao hatimaye watafufuka, Danieli anawasema kuwa ‘Wamelala Usingizi’. Katika nafasi moja, Yesu alipoitwa nyumbani kwa mkuu wa Sinagogi aliyefiwa na binti yake, “alichekwa na dharau” na waombolezaji waliokusanyika pale, alipoeleza wazi ya kwamba” kijana hajafa, bali amelala” ( Mathayo 9:24 ). Wangalikuwa na mazoea na maana halisi ya Maandiko yao wangefahamu kuwa lugha hii ilithibitisha lengo la Yesu kumfufua katika wafu. Kwa hiyo hii ndiyo njia ambayo ndani yake Mungu mwenyewe anawaona hao anaowakusudia kuwafufua. Kwa ajili yake wanangojea kuitwa kuamshwa tena wakati wa kupambazuka siku kuu ya haki. Maneno ya Danieli vile vile yanahusiana na msemo mwingine wa Bwana Yesu Kristo: “ Maana kama vile Baba alivyo na uzima nafsini mwake, vivyo hivyo alimpa na Mwana kuwa na uzima nafsini mwake. Naye akampa amri ya kufanya hukumu kwa sababu ni Mwana wa Adamu. Msistajabie maneno hayo kwa maana saa yaja, ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu” ( Yohana 5: 26-29 ). Kwa kawaida ufufuo si mada inayojadiliwa. Fikira za nini linatokea baada ya kufa zinafika katikati ya mawazo mbali mbali mengi. Baadhi kwa kupenda wanawaza kuwepo wakiwa huru toka katika vifungo vyote vya maisha haya na nchi hii, lakini pengine bila kusudi. Labda tunaweza kuuliza ni raha gani maisha haya yanaweza kutoa au kumpa kiumbe au Muumbaji. Sawasawa na mtazamo huu ni hofu ya mateso ya milele, moto unaowaka sana na moshi wa kiberiti. Kwa kawaida yote mawili ni uhuru toka katika miili yetu ya sasa ya kufa.Vyovyote maisha yetu yaweza kuwa, yatahusisha ( hivyo imesemwa ) ya kuwa nusu ya utu wetu unaodhaniwa kutopatwa na mauti – utu muhimu au ‘nafsi’, kwa kutaja matumizi ya watu wote. Hadithi za Mwanadamu na Kweli ya Biblia…. Katika uchunguzi wetu wa fundisho la Biblia, tunajua mawazo haya hafifu hayana msingi. Badala yake, na kwa wepesi chini kwa maneno ya dunia, kuna ukweli wenye nguvu na wenye kushurutisha kuhusu hali ya kweli ya mwanadamu ya mpango wa Mungu kwa Ukombozi: (8) 1. Mtu anazaliwa ni mfu, kiumbe anayekufa amerithi mwili wake toka kwa mababu wake wote kurudi hadi kwa Adamu. 2. Mwanadamu ni mwenye dhambi. Watu wote wanajaribiwa na, ukimtenga Bwana Yesu Kristo, wanatenda dhambi kwa kuvunja sheria za Mungu. 3. Watu wote wanakufa, kwa sababu ya magonjwa, ajali, kuuawa au uzee. 4. Mauti ni kutokuwa na fahamu kabisa. Hatiwi nguvu tena na pumzi, mwili unaoza kuwa mavumbi ambako alitoka. 5. Mungu atawafufua katika wafu wote wanaomjua na sheria zake 6. Kwa njia ya Bwana Yesu Kristo, akirudi duniani, Mungu atawahukumu watakaofufuliwa. Baadhi watapewa kutokufa. Waliobaki watarudi makaburini mwao milele. 7. Waamini waliofanywa kutokufa, Watakatifu au walitakaswa wataishi na kutawala na Kristo katika Ufalme wa Mungu duniani. Kuwa hai wakati wa kuja Bwana….. Katika orodha hii ya mambo, mipangilio maalum imefanywa kwa ajili ya hao ambao watakuwa hai Kristo atakaporudi. Hili lilikuwa jambo kuu lililowahusu waumini waliofahamu fundisho juu ya ufufuo na hukumu, ila waliwaza ya kuwa itawalenga tu hao waliokwisha kufa. Mara nyingi katika Agano jipya waandishi walivuviwa kuweka wazi jambo hili. Tumekuwa na shukurani kwamba walifanya hivyo, maana ishara zinazoonyesha dhiki katika dunia zinaleta habari ya utabiri wa siku kuu aliyoipanga Mungu “atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu ( Mdo 17:31 ). Kwa hiyo tunaweza kuwa miongoni mwa kizazi ambacho “hawatalala (kufa), bali tutabadilishwa” kwa uwezo wa Bwana Yesu Kristo kuwa raia wasiokufa katika Ufalme wake wa Mungu. Vile vile wakati wa kuja Kristo watakuwepo wanaume na wanawake ( na hasa watoto ) ambao hawakufanya uamuzi wa kuitikia kwao itakuwaje katika Injili ya kweli. Wataendelea kuishi katika wakati hapo “katika Sayuni itatoka sheria na neno la Bwana litatoka Yerusalemu” (Mika 4:2 ) Kwa ajili ya Kristo kutawala kwa haki, hali ya ulimwengu itastawi na matumaini ya uhai yataongezeka pengine kuwa sawa na nyakati kabla ya gharika, Isaya alitabiri: “Hakutakuwa tena na vifo vya watoto wachanga, wazee nao hawatakufa kabla ya wakati wao; akifa mtu wa miaka mia amekufa akiwa kijana; na akifa kabla ya miaka mia ni balaa” ( Isaya 65:20, B.H.N. ). (9)Lakini kila mtoto, kijana na mwenye umri mkubwa, kwenye nyakati zao zilizopangwa watakufa. Mwishoni mwa utawala wa Kristo kutakuwa na siku ya pili ya ufufuo, hukumu ya pili na, kwa hao wasiopewa kutokufa ambao majina ’hayataonekana yameandikwa katika kitabu cha uzima”, mauti ya pili ya mwisho kabisa ( Ufunuo 20:12 - 15 ). Ufufuo uliosemwa katika Biblia ni wa mwili, sambamba na kipindi cha amani na haki kitaanzishwa na Yesu akirudi kinahusisha dunia hii tunayoishi. Hakuna wazo dhaifu la roho kuishi katika ulimwengu mwingine uliombali, kama kipimo cha ufufuo wa Yesu mwenyewe kinavyoonyesha.Kwanza, Mariam Magdalene hakumtambua, alidhani ni mtunza bustani, Yesu ikabidi amkemee asimshike: “Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba” ( Yohana 20:15,17 ). Baadaye wanafunzi walipokusanyika juu orofani wenyewe wakiwa na hofu ya kusulubiwa kwake, Yesu alitokea, wakadhania walikuwa wanaona roho. Jawabu la Yesu kwa hofu yao linaondoa mashaka yote: “ Mbona mnafadhaika ? na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu ? Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe: nishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama munionavyo mimi kuwa nayo” ( Luka 24: 38,39 ). Ufufuo wa Mwili…. Kwa hali ya kufanana, ufufuo wakati wa kurudi Kristo utakuwa ni wa mwili. Watu wote, “waliomo makaburini wataisikia sauti yake: nao watatoka” ( Yohana 5:28 ). Si vizuri kwetu kuuliza uwezo wa Mungu mfariji wa vyote kuifufua miili iliyooza, kwa kuwa hapo kwanza alimfanya mtu katika mavumbi ya ardhi, kwa hiyo anaweza tena kuwafanya wanaume na wanawake ambao tangu wakati ule walirudi katika mavumbi ambako walitoka, wakitumainia uwezo wake usio na kikomo. Katika hali iliyosawa ya wakati wa ufufuo na hukumu na yaliyompata Adamu mwenyewe ni dhahiri kabisa. Hakuumbwa asife. Ulikuwepo mbele yake uchaguzi wa kutii amri ya Mungu au kufuata haja zake, naye akachagua jambo lile lililofanya mfano ambao watu wote wamekuja kufuata baadaye.Kwa hiyo alihukumiwa na Mungu: “ Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako….. ardhi imelaaniwa….kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi” (Mwanzo 3: 17 -19 ). (10)Kwa hiyo, awali ya yote,ufufuo unadokeza vile neno lenyewe linavyodokeza - - ni kutoka kaburini na kusimama: si kubadilika mwili mara moja, bali ni kuurejesha mwili ulnaokufa kwenye uhai tayari kwa kutokea mbele ya hukumu. Wengine watakuwa waliendelea kufanya kosa “kwa mfano wa kukosa kwake Adamu” (Warumi 5:14 ); baadhi watakuwa wamejitahidi kuufuata mfano wa Mwana wa Mungu, kwa kutamba ushindi katika mauti na ufufuo wake aliofaulu. Ni akina nani watakaofufuliwa….? Kutakuwa watu wengi walioishi maisha yao bila kujua hata kidogo nia ya uwezo wa Mungu na kutofahamu ahadi ya kipawa cha uzima kilichowezeshwa kwa kazi ya Bwana Yesu Kristo. Watu wa jinsi hii tusitegemee kuwa watafufuliwa kwa kutokujua mambo ya awali yaliyohusika, ni jinsi gani watarajiwe kutoa jibu mbele ya hakimu wa dunia yote ? Kulingana na mwangaza wao wenyewe walioishi maisha, wanapokea sawia na wengine wote wakaazi wa dunia yake faida ambazo Mungu anamwaga juu yetu kila siku. Walakini, hao ambao wanajua kusudi lake wamewekwa katika nafasi ya kubeba dhamana na kila mmoja “atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu” ( Warumi 14:12 ). Huu mtengano ni “hukumu itakayokuja” ambayo ni hoja aliyotoa kwa Feliki naye Yesu mwenyewe atakuwa mwamuzi. Mwamuzi mwenye Haki….. Ni dhahiri kazi ya hukumu imetunzwa na Mungu kwa ajili ya Kristo. Ni jinsi gani ya kwamba anafaa kuwa mwamuzi! Alizaliwa kwa uwezo wa Mungu na mama wa kidunia na kwa hiyo alishiriki mwili wa binadamu. Anayajua majaribu yanayotufanya sisi tujikwae kwa kuwa yeye mwenyewe alijaribiwa kwa jinsi iyo hiyo. Kwa sababu alikusudia moyoni mwake “siku zote kufanya mapenzi ya Baba yake” alishinda kila jaribu. Akiwa mwanadamu katika mstari wa Adamu “jambo moja linalowajia wote” lilimfikia na kusulubiwa kutokana na sababu za utaratibu wa watu ambao hawakuweza kufahamu wema wake waliouonea shaka. Kwa sababu ya kuishi maisha ya utii “kaburi halikuweza kumshilkilia” na kwa nguvu iyo hiyo iliyofanya azaliwe kwa muujiza, Mungu alimfufua katika wafu na kwa sababu ya haki yake akapewa uzima wa milele. (11)Huko kuwekwa huru kunawezekana toka kwa adui wa awali wa mwanadamu, kama ilivyodhihirika kwa Ayubu, Isaya na Danieli kwa kusadikisha walithibitisha ufufuo wa Yesu Kristo. Kwa sababu ya ushindi wake juu ya mauti, wafuasi wake wamehakikishiwa kushiriki furaha yake kwa sababu ya kushinda. Wakijua ya kwamba mwanadamu hawezi kuishi kwa utii kamili kama Kristo. Mungu ameahidi ya kwamba waaminio wanaweza kuhusika na huo uzima na kufurahia faida ambazo kwa matokeo zinatiririka. Njia za kutimiza vizuri huu uhusiano ni kwa ubatizo baada ya kutubu mienendo ya dhambi na kuikiri kweli ya ujumbe wa Injili: “ Hamfahamu ya kuwa” alisema mtume Paulo kwa waumini waliokuwa Rumi, “ sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. Kwa maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake” ( Warumi 6:3 - 5 ). Thawabu Nzuri kwa Wafuasi Waaminifu… Haiwezekani kusoma mafundisho ya Injili ya Bwana Yesu Kristo na bila kujua haja ya hukumu. Ikiwa ni kwa wazi kwa wanafunzi wake au kwa mfano wa mithali kwa makutano waliomkusanyikia kumsikiliza, Yesu alifundisha kwa kuisema wazi siku ya hesabu kwa watumishi wake Mungu. Katika safari moja alinena mtu mmoja kabaila alikwenda nchi ya mbali kumpokea mfalme.( Sambamba na kupaa kwake mwenyewe na alivyoahidi kurudi kusimamisha ufalme wa Mungu duniani hakuwezi kuepukwa ). Wakati wa kurudi kwake, watumishi waliokabidhiwa mali yake waliitwa kutoa hesabu ya jinsi walivyotumika wakati hayupo. Watumishi waaminifu walio na bidii walipewa thawabu, wakati wasio waaminifu wakaadhibiwa kwa kunyang’anywa sehemu ya mtu kabaila aliyopewa aitumie. Katika habari nzima, upo mkazo wa kuwa “mwaminifu”.Ni imani ya mwamini katika ahadi za Mungu ndiyo itakayofanyiwa hukumu. Hakuna mtu aliyeishi maisha ambayo yenyewe yana ujasiri wa kuhesabia haki ya kwamba thawabu imepatikana. (12)Yesu mwenyewe alisema:- “Mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, sisi tu watumwa wasio na faida: tumefanya tu yaliyotupasa kufanya” ( Luka 17:10 ). Kwa kupatana na neno hili, ahadi ya uzima wa milele haijaelezwa katika Maandiko kuwa jambo fulani linaloweza kupatikana. Badala yake ni “karama ya Mungu” ( Warumi 6:23 ). Haiwastahili wapokeaji wake, karama imewezekana kwa kazi ya ukombozi wa Bwana Yesu Kristo. Msingi wa Hukumu…. Abrahamu, mtu mmoja mkuu wa Agano la Kale, ni mfano mzuri wa jambo hili.Alitakiwa afanye mambo ambayo yalikuwa makubwa kuliko wajibu wake aliotakiwa kufanya. Mojawapo ilikuwa kumtoa mwanawe kuwa sadaka (Mwanzo 22 ). Ulikuwa ni uwezo wake kwa yote haya kujua daima uhakika wa ufunuo ujao ( Waebrania 11:17-19 ) ndiyo uliomwonyesha kuwa mtu wa imani kubwa.Habari zake zimeandikwa ya kwamba kwa matokeo ya uaminifu wake Mungu amemuhesabu kuwa ni mtu mwenye haki ( Warumi 4:3 ). Basi huu ni msingi wa imani. Labda, tunapounganika na neno la sheria za korti (mahakama),tumejaribu kukabili jambo fulani la aina ya mjadala, na maneno ya kusadikisha kuhusiana na sifa za matukio mbalimbali katika maisha ya mtu. Tunaweza kidogo wakati kama nafasi ya kupewa msamaha utamkwe na mmoja aliye na mamlaka kufanya hukumu na ambaye ana sifa za pekee kufanya hivyo.Kupewa msamaha hayatakuwa ni matokeo ya kufaulu, maana ilikuwa ni mmoja atakayesema kwa ujasiri. “Bwana, Bwana kwa jina lako hatukufanya miujiza mingi ?” Kwake huyo Bwana atatoa jibu la kutisha, “Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu” ( Mathayo 7:22 - 23 ). Kama Isaya alivyotabiri zamani, Mungu anawataka watumishi wanyenyekevu na wepesi kusikia na kuona: Mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu”. ( Isaya 66:2 ). Sana, msamaha utakuwa juu ya kujitoa, maarifa ya kujua ya kwamba kila mtu anategemea kabisa fadhila za Mungu kwa mambo yote; katika maisha haya na pia kwa mibaraka ambayo kwayo dunia itamwagiwa katika kipindi cha ufalme. (13)Kutoka katika Mauti hadi Uzima…. Ingawa hivyo, hukumu ni sehemu pekee ya maendeleo yanayoongoza wanaume na wanawake waaminifu toka katika mauti hadi kwenye uzima. Lengo la Mungu tangu mwanzo lilikuwa kwamba wanadamu wawe katika mfano wake. Mwanawe ndivyo alivyo na kwa hiyo aliweza kusema na wafuasi wake: “Aliyeniona Mimi amemwona Baba” ( Yohana 14:9 ) Yesu alionyesha ajabu ya tabia ya Mungu kwa utimilifu zaidi; alikuwa “amejaa neema na kweli” ( Yohana 1:14 ) Wengi waliomsikia “walistajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake” ( Luka 4:22 ); ndiyo maana aliweza kusema ya kuwa yeye ni njia, na kweli na uzima” ( Yohana 14:6 ). Ni tofauti jinsi gani kutokana na udhaifu wetu kujaribu kukamilisha tabia yetu! Kwa njia tofauti kila mmoja wetu anakosa uwezo wa kujitawala mwenyewe. Mmoja itakuwa ulimi wa kunena kwa haraka, kwa mwingine hasa huzaa tamaa, bado hata hivyo wengine dhambi ya kiburi. Tunapoanza mafuatano ya kujihoji kwa wakati ulio muhimu kabisa, orodha haina mwisho. Hata sasa Mungu amewaahidi wao wanaojitahidi kumtumikia kwa uaminifu kushiriki tabia ya Mungu. Akitumia ufasaha wa maneno, Danieli anaeleza matokeo haya ya ufufuo na kukubaliwa kwenye kiti cha hukumu: “ Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele” ( Danieli 12:3 ). Elewa ya kwamba watang’aa “kama mwangaza wa anga” na “kama nyota”. Hii ni lugha ya mfano wa kuelezea kwa mashairi badiliko toka utu wa kufa hadi kutokufa. “ Mungu ni nuru”, mtume Yohana aliandika, “ndani yake hamna giza lolote” ( 1Yohana 1:5 ).Danieli alikuwa anatabiri ya kwamba hao watakaofufuliwa na kukubaliwa kwenye kiti cha hukumu ndipo watabadilika kuwa watu wasiokufa, wakiishi na kutawala na Kristo na kuonyesha, kama anavyofanya, tabia ya sifa ya Baba wa mbinguni. Hili ni tumaini la juu lililo katika ujumbe wa Injili, “haki” itakayodhihirika kwa “hukumu ijayo” iliyomfadhaisha Feliki, na ambayo itatimilika tu wakati wa mavuno ya ufufuo yakikusanywa. Kristo, ambaye ni limbuko la haya mavuno ( 1 Wakorintho 15:23 ), ni hakikisho la kwamba yote tuliyoona kulingana na mada hii ni hakika yatatimilika. (14)Siku ya Nafasi…. Feliki alimwambia Paulo kwa maneno “Enenda zako sasa”, nami nikipata nafasi nitakuita ( Matendo 24:25 ). Tunaweza kama tukitaka, kufanya yayo hayo na kugeuza migongo yetu toka habari za Ufalme wa Mungu. Tunaweza kujisadikisha wenyewe ya kwamba utakuwepo “wakati wa kufaa” baadaye, lakini tutakuwa tumekosea. Kama mtume Paulo aliposema, akiwaandikia waumini wa kule Korintho: “Wakati uliokubalika ni sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa” (2 Kor.6:2) Haya ni mambo ya uzima na mauti, ni ya muhimu mno, si vema kuyapangia siku nyingine. Michael Ashton (15) Tena: 1 902059 00 - X Matayarisho ya Ubatizo 1 902059 01 - 8 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 1-4 1 902059 02 - 6 Ukimwi 1 902059 03 - 4 Mshitaki Wenu Ibilisi 1 902059 04 - 2 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 5-8 1 902059 05 - 0 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 9-11 1 902059 06 - 9 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 12-15 1 902059 07 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 16-19 1 902059 08 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 20-23 1 902059 09 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 24-27 1 902059 10 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 28-31 1 902059 11 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 32-36 1 902059 12 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 37-40 1 902059 13 - 1 Ufunuo Mlango wa Kwanza 1 902059 14 - X Ni kweli Yesu Kristo alishuka kutoka mbinguni? 1 902059 15 – 8 Nyimbo za ndugu wa Kristo 1 902059 16 – 6 Ufunuo Mlango wa Pili 1 902059 17 – 4 Katiba ya Makanisa 1 902059 18 – 2 kitabu-mwalimu wa kristadelfiani 1 902059 19 – 0 Kuanzisha Kristadelfiano (CBM) Eklesia 1 902059 20 – 4 Waraka wa mtume Paulo kwa Wagalatia sura moja 1 902059 21 – 2 Ni kwa sababu gani Mungu Anaruhusu Mateso? 1 902059 22 – 0 Ufufu Kwa Hukumu Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya Biblia kaitka somo hili muhimu. Lina itwa Kuishi katika Ukweli. Unaweza kupata nakala kutoka Kanisa la Christadelphian, au kutoka anuani iliyoandikwa katika kijitabu hiki. ? CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW ISBN 1 902059 22 -0 Registered Charity Number: 248979 / 1020558 Company Number: 2796412 Telephone +44 (0) 1604 765068 Email: CarlHinton@hotmail.com Web: http:\\www.cbm-tz.org