INJILI YA KWANZA The Original Gospel Tafakari ya mara ya pili ya mafunzo ya msingi ya Agano la Kale na Jipya _______________________ KAMA YALIVYOTOLEWA KATIKA ZABURI, NA MANABII NA BWANA YESU KRISTO, PAMOJA NA MITUME. _____________________________________________________________________________ Zaidi ya karne nyingi pamekuwepo na mabadiliko katika wazo la Kanisa, imani, desturi na jinsi mtu anavyofikiri. Lakini bado INJILI ni MOJA, MUNGU MMOJA, BWANA MMOJA YESU KRISTO, TUMAINI MOJA LA ISRAEL NA BIBLIA MOJA YA KWELI. Tunataka ufungue Neno la Mungu ili utazame na kulinganisha na imani za siku hizi.... Tokeo litakushangaza, lakini likuridhisha na kukuondolea mashaka, na litakupa Amani ipitayo ufahamu wote... Hata hivi, MAISHA, bila Mungu na Mwana wake, hayana faida na hayana maana. __________________________________________________________________________________________ NA ISHARA YA MKRISTO WA KWELI ni Yule anayejizoeza kila siku katika upendo, furaha, amini, uvumilivu, upole, utu wema, imani, fadhili, upole kiasi juu ya mambo hayo hakuna sheria. Wagalatia 5:22 NJIA KUU NI NJIA ZILIZO NJEMA "BWANA ASEMA HIVI, simamemi katika njia kuu, mkaulize mapito ya zamini njia njema mkaenende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha nafsini mwenu." Yeremia 6:16 ISHARA ILIYO KUBWA ZAIDI KWLETU LEO ni vurugu zilizopo duniani, hofu inayowakabili watu wote, matayarisho makubwa ya vita na iliyo ya pekee ni kurudi kwa Israel toka zaidi ya nchi 100 kama ilivyotabiriwa katika Biblia. Sasa ISHARA ILIYO YA AJABU ZAIDI YA ZOTE ni kitendo cha Israel kumiliki miji ya zamani ya Yerusalemu, ukanda wa magharibi wa mto Yordani, ukanda wa Gaza, mfereji wa Suezi (1967) mwezi wa sita waliweza kuchukua milima ya Golani na jangwa la Sinai. Mwisho umekaribia sana Mungu atalitakasa jina lake kuu kupitia kwa Israel mbele ya mataifa yote. (Ezekiel 39:27) _______________________________________ Kwa habiri zaidi waliana na: CBM Publishing, 32 Blenheim Road, Far Cotton, Northampton, England NN4 8NW Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanisa la Christadelphian Bible Mission limechapisha majira kuhusu mafunzo ya Biblia katika somo hili muhimu. Linaitwa masomo ya biblia kwa njia ya posta ya wakristadelphiano. Unaweza kupata nakala kutoka Kanisa la Christadelphiano au kutoka anuani iliyoandikwa katika kijitabu hiki. HIVI NDIVYO BIBLIA INAVYOFUNZA......... 1. YUPO MUNGU MMOJA, ambaye hana wa KUMLINGANISHA. Kum.6:4: 2Sam.7:22; Fal.8:23; 1Nya.17:20; Zab. 86:10; Isa. 44:8; 45:5;46:5; Mk. 12:29; Yn.17:3; 1Kor.8:6; Efe.4:6; 1 Tim.1:17; Sura 2:5. 2. YUPO BWANA MMOJA YESU KRISTO, Mwokozi na Mpatanishi, ambaye ni NJIA PEKEE ya wokovu, yupo karibu kurudi kutawala dunia. Isa.53:6; Mt. 20:28; Lk.2:11; Yn.17:3; Mdo.1:11; Mdo.4:12; Mdo 13:23; 1Tim.2:5; 1Yohana 4:14. 3. KUNA ROHO MTAKATIFU MMOJA TU, ambao ni UWEZA wa Mungu, anaotumia kutenda kazi. Mwa.1:2; Amu.14:6; Mt.1:18; Lk.1:35; Lk.12:12; Mdo.7:55; Rum.15:19; Ebr.2:4; 1Pet.1:21. 4. KUNA AGANO KUU MOJA TU, ambalo ni tumaini la ulimwengu, limetiwqa uhuri na damu ya Yesu Kalvari, Agano lililofanywa kwa Ibrahimu. Mwa.12:3; 18:18; 26:3; 28:14; Mik.7:20; Lk.1:72; Mdo.7:5; Mdo.3:25; 26:6, Rum.15:8; Gal.3:8; Ebr.6:13; Ebr.11:13. 5. KUNA CHANZO KIMOJA TU CHA HABARI ambacho ni Mpango wa Mungu na makusudi yake kwa dunia hii, NENO LA MUNGU. Isa.8:20; Lk.16:31; Yn.5:39; Mdo.28:23; Rum.15:4; 2 Tim.3:16; 2Pet.1:21. 6. KUNA ADUAI MMOJA MKUBWA WA MWANADAMU, Dhambi iliyoingia Adeni, imeitwa IBILISI, Wakristo kwa muda wa maisha yao yote wamekuwa na mashindano naye. Mwa.3:15; 1Fal.8:46; Isa.53:6; Mt.15:18-20; 16:23; Mdo.10:38; Rum.3:12; 5:12; 7:23; Ebr.2:14; Yak.1:14; 1Pet.5:8. 7. HAKUNA UKWELI MKUBWA, kuliko kwamba mauti yalikuja kwa sababau ya dhambi na kwamba mautini hakuna ufahamu wowote. Ayu.3:17,18; 14:2; Mhu. 9:5-6; Zab.6:5; 17:15; 39:13; 115:17; 146:4; Isa.38:18; Dan.12:2; Rum.5:12; 6:23; 1Kor.15:21. 8. NI UHAKIKA KWAMBA, Kuzimu ni kaburi, amboko watu wote huenda. Mwa. 15:15; Zab. 6:5; 31:17; 89:48; 115:17; Mhu. 3:20; 6:6; Isa. 38:18; Mt. 11:23; Mdo. 22:27-31; Kor. 15:54- 55. 9. KUNA UKWELI ULIO WAZl, kwamba neno NAFSI maana ya asili ni UHAI, na viumbe WOTE wanao huo uhai na imeonyeshwa kuwa wapo chini ya mauti. Ayu.7:15; Zab. 22:29; 33:19: 78:50; Eze. 18:4; Mt.26:38; Yak. 5:20; Ufu. 16:3. Nafsi inaende kaburini (kuzimu). Ayu.33:22; Zab. 89:48; Mit.23:14; Isa. 38:17; Mdo.2:31; Nafsi inaweza kuangamizwa Law. 23:30. 10. HAKUNA LILILO LA AJABU ZAIDI, kuliko ufufuo utakaofanyika Yesu akirudi. Dan.12:2; Mt.22:30; Lk.14:14; Yn.5:29; 6:40; 11:24,25; Mdo.23:6; Rum.6:5; 1 Kor.15:12; 1The.4:16. 11. KUNA SIKU YA HUKUMU, kwa wanaopaswa, ambayo watapaswa wakabiliane nayo - Yesu akirudi. Zab.98:9; Mt.8:12; Yn.5:22-17; 11:24; Mdo.17:31; 24:15; Rum.14:10; 2 Kor.5:10; 2Kor.5:10; 2Tim.4:1; 1Pet.4:17; Ufu:20:12. 12. KUNA THAWABU YA UZIMA WA MILELE, watakayopewa waaminifu, waliokufa au walio hai Kristo ajapo. Isa.40:10,11; Dan.12:2; Mt.8:11; 16:27; 24:31; Lk.13:28; Yn.5:29; 6:40; 1Kor.15:23; 2Tim.4:8; The.4:16; Uf.22:12. 13. KUNA MAUTI YA MILELE, kwa wasio waaminifu watalia na kusaga meno Yesu atakapowakataa akirudi. 1Sam.2:9; Ezek.18:4; Mt.7:21-23; 8:12; 13:41; 25:46; Lk.13:28; Yn.5:29; Mdo.24:15; 2Kor.5:10; 2Thes.1:8,9. 14. KUNA UTHIBITISHO WA MUNGU, kuwa watakaokubaliwa watatawala na Yesu kwa miaka elfu dunia. Kipindi cha Amani duniani. Zab.72: Dan.2:44; Dan. 7:27; Zek.9:10; Lk.1:30-33; Uf.5:10; Uf.20:6. 15. KUNA UHAKIKA, kwamba Yesu atarudi katika MWILI WA KUONEKANA, na kuketi kwenye kiti halisi. KITI CHA ENZXICHA DAUDI YERUSALEMU. 2Sam.7:12-16; Zab.89:19-37; Isa.9:6-7; Ezek.21:26; Isa.33:17; Zek.12:10; Sef.2:11; Mt.16:28; 25:31-32; Mk.13:26; 14:62; Lk.13:35; 21:27; Uf.1:7; 2:27. Kwa sasa kiti cha Daudi hakipo Zab.89:39-44; Ezek.21:26,27; Amo.9:11; Mdo.1:6,15:15,16; 17:31; Rum.15:12; Uf.15:4. 16. MUNGU AMEHAKIKISHA, kwamba Yerusalemu utakuwa ni mji mkuu wa ulimwengu wakati wa utawala wa Yesu. Zab.48:2; lsa.2:1-4; 24:23; 33:20; 60:14; 3:17; Yoe.3:16; Mik.4:2-8; Zek.1:17; 8:22; 14:16; Mt.5:34-35; Lk.19:42. 17. KUNA ISHARA KUBWA INAYOONEKANA YA SIKU HIZI, ishara ya Mungu, Waisraeli walitawanywa pote ulimwenguni na Yeye lakini kwa sehemu sasa wamekusanyika katika nchi ya ahadi, kama ilivyotulewa, na sasa wanaumiliki mji wa Yerusalemu tayari kurudi kwa Bwana. Isa.11:11-12; Yer.32:37; 31:10-28; Ezek.11:17; Ezek.36:24; 37:3-14; Mt.23:39; Rum.11:12, 15, 26. 18. KUNA AGIZO LA YESU NA MITUME, kuwa Imani, Toba na Ubatizo (wa maji mengi) katika Kristo ni muhimu kwa wokovu. Mt.28:19; Mk. 16:16; Yn.3:23; Mdo.2:38; 10:47; 16:31-32; 22:16; Rum.6:3,4; Gal.3:27-29; Kol.2:12; Efe.4:5; 1Pet.3:21. 19. KUNA MATAKWA YA LAZIMA, ya kuwa utakatifu, maisha mema, na haja ya kumpendeza Mungu katika maisha ya kila siku YAPASWA yatekelezwe. Zek.14:20; Rum.6:19; 2Kor.7:1; Fil.4:8; 1Thes.3:13; 1Thes.4:7; 1Tim.2:15;Tito 2:12. 20. NI UHAKIKA, kwamba wokovu hauwezi kupatikana isipokuwa ni kwa njia ya Yesu Kristo. Mathayo 1:21; Matendo 4:12; Yohana 11:25; 15:4.