_____________________ Mshitaki Wenu Ibilisi The Devil & Satan _____________________ BIBLIA NA DHAMBI "MSHITAKI WENU IBILISI" (1 Petro5:8) Neno dhambi halitumiwi na watu wengi, na hata wakati likitumika, linakuwa limepelekewa kwenye ubishi mara nyingi zaidi usio na akili kuliko kuwa dhambi imo moyoni. Ukweli wa dhambi hauepukiki ingawa hivyo. Huzuni na taabu zote za ulimwengu zinatokana na hiyo, kila mtu anajua kwamba ni mwenye hatia kwa sababu ya dhambi katika mambo makubwa zaidi au kwa kipimo kidogo. Kuvutwa kwa mabaya kamwe hakupo mbali na kukubaliana nayo ambapo hayapingiki mara kwa mara kwa karibu sana. Ni nani au ni yupi anahusika na kishawishi hiki? Jibu la kawaida kwa swali hili ni kutaja jina la kiumbe anaye dhaniwa kuwa anauwezo kuliko viumbe vingine anayejulikana kama "ibilisi" mtenda mabaya. Dhana hii mara nyingi imefanywa badala ya kufikiri kwa makini kama neno lenyewe ibilisi linamaana gani, na hivyo kufanya si chochote zaidi ya neno la kushika, Walakini Kwa hayo matokeo makubwa kama chanzo cha dhambi kwa wanadamu hakiwezi kuachiliwa mbali kwa urahisi, na imekusudiwa katika kurasa hizi kuchunguza jambo lenyewe na kutazama kabisa na kuelewa usahihi wake. Katika sehemu ya kwamza kwa lugha za wenzetu ufafanuzi wa kamusi unashauri kwamba neno "ibilisi" linakuja toka deoful, neno la kilatini ni hili linaloitwa diabolus. na kwa. Kiyunani (Kigriki) ni diabolos, jina lililoitwa mwishoni linapatikana toka diaballein. Neno hili lilipatikana kutoka dia, "katikati" na ballein, "kutupa", na maana yake ni kutupa katikati au singizia. Katika maana ya asili ya neno "ibilisi" kwa sababu hiyo, hakuna kidokezo cha mjaribu. UKWELI KUHUSU DHAMBI Kwa kadiri yoyote. ni katika Biblia ambako yatupasa kuangalia ili kutuwezesha kufahamu ukweli kuhusu dhambi. Hiki ni kitabu cha Muumba, Ambaye ni yeye aliyeumba ulimwengu ha wanadamu, na Ndiye anafanya shauri la hali ya uwepo wa wanadamu. Kwa sababu hiyo, tutegemee kupata ndani yake habari juu ya dhambi na kuvutwa ili kufanya mabaya. Mapenzi yetu kwa chimbuko hili la habari ni mara moja yaliongezeka hapo tulipokuta kwamba neno ibilisi mara nyingi limetumika katika Maandiko. Ukweli huu utatusaidia kuvumbua maana yake. (1) Zaidi ya neno moja katika lugha ambazo kwa mara ya kwanza Biblia iliandikwa limetafsiriwa "ibilisi". Moja ya haya ni neno la Kiyunani diabolos kutoka ambako kama lilivyoelezwa tayari, tunakopata hili neno, itakuwa vema kulitafakari kwanza. Linapatikana katika Agano Jipya tu, limetokea mara 38. Juu ya nafasi hizi 35 limetafsiriwa "ibilisi" na nafasi zilizobaki 3 limetafsiriwa "wachongeaji" na mara mbili "wasingiziaji", hasa katika Biblia za Kiswahili. Ni muhimu kujua ni nani wanaweza kuwa ni wasingiziaji au wachongeaji, waliotajwa kwenye maswala haya matatu. Katika jambo moja wazee wanawake wametakiwa wasiwe wasingiziaji katika kanisa (1). Katika jambo lingine wake wa mashemasi wameshauriwa wasiwe "wachongeaji au wasingiziaji" (2), wakati kwa jambo la tatu imetabiriwa kwamba katika siku za mwisho watu watakuwa wasingiziaji (3). Tafsiri hizi za diabolos, katika mambo ambako wazo la ibilisi kuwa ndiye anayeshawishi ili kutenda dhambi ni dhahiri litakuwa halina sehemu ya kufaa, fikiria kuwa itakuwa ni jambo lenye ushauri kutazama kwa kutaka kujua katika mafungu ya maneno ambamo neno diabolos limetafsiriwa ibilisi. Hapo haya yakipimwa, yanakutwa kwamba hakuna jambo litatiwa mahali pa jingine kwa. kuita msingiziaji au mchongeaji maana ibilisi linaharibu maana na katika mambo mengi utakuta kwamba litajidhihirisha. Haiwezekani kufafanusha mambo yote bali yanayo onyeshwa yanaweza kupimwa. Mengine, kama yanayohusu majaribu ya Yesu ambayo yanahitaji maelezo kwa kutaja moja moja zaidi, yatapimwa baadaye. "MMOJA WENU NI IBILISI" Yesu kwa muujiza alipowalisha umati wa watu mikate michache na samaki kwa njia ya kuzidisha, alitumia muujiza kama fungu dogo la maneno kuwa ni fundisho, akijionyesha yeye mwenyewe kuwa ni mkate wa uzima; kwa kudai kwamba wale ambao watakula mkate ambao atawapa wataishi milele. Huu ulikuwa ni ukweli wenye kutatiza kwa wasikilizaji wake walio wengi na wengi wao, ukijumuisha wengine ambao walikuwa ni wafuasi wake wa kawaida walijitenga naye. Kwa huzuni aliwageukia wanafunzi wake kumi na wawili na akawaambia "Nanyi mnataka kuondoka?" Kwa hili mtume Petro akajibu mara moja, "Bwana, twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tunaamini kuwa wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai". Hata maelezo haya yenye imani inayon'gaa hayakumfariji Yesu kwa jumla, kwa kuwa alisema "Je sikuwachagua ninyi kumi na mbili, na mmoja wenu ni ibilisi" (4). Habari inaeleza kuwa Yesu alikuwa anamfikiria Yuda Iskarioti, ambaye baadaye alimtoa kwa maadui zake. Kweli kabisa Yuda alikuwa ni diabolos, msingiziaji, mwongo, mchongeaji, maana alimsaliti Bwana wake kwa busu. Matumizi ya neno ibilisi yanapotosha, kwa kuwa Yuda alikuwa ni mwanadamu, sio kiumbe mashuhuri anayedhaniwa kuwa mwovu, na tafsiri sahihi ya diabolos inafanya neno hili kuwa wazi kabisa. Hapo wakati ulipofika kwa Yuda kuweka mpango wake katika kazi ili kuongoza maadui wa Yesu kwa Bwana; imeandikwa kwamba ibilisi alimtia moyo wa kumsaliti Bwana wake (5). Katika fungu hili la maneno neno ibilisi ni diabolos tena katika Kiyunani asilia. Hapa imeonyeshwa akili ya uovu ya msaliti ikitenda kazi ya uongo kama kunuia kumsaliti Bwana wake kwa vipande thelasini vya fedha. (2) Kama Yesu alivyokwisha sema tayari, Yuda mwenyewe alikuwa ni ibilisi mwenye kumchongea Yesu. Wakala wa uhaini alikuwa amezaliwa nao, na sio kuwa ni kiumbe aliye mwovu kuliko wengine, Tamaa ya mali aliyonayo mtu ilikuwa ni sababu tosha kwa tendo lake la kutisha. Kama mtunza fedha wa kwanza kwa watu waliofanya kazi pamoja na Yesu, alitumia vibaya fedha na sasa, labda alipoozwa kwa kukosa alichotegemea kuwa Yesu hakutumia uwezo wake wa miujiza kuwafukuza wavamizi wa Kirumi toka katika nchi yao, tamaa yake ilimwingia kwa uamuzi wa haraka ambao halafu ulimwangamiza. "MWANA WA IBILISO" Jambo Jingine ambalo neno diabolos limetafsiriwa ibilisi linataja ziara ya mitume Paulo na Bamaba kule Pafo katika kisiwa cha Kipro. Hapa liwali wa Kirumi Sergio. Paulus alivutiwa sana na mafunzo yao, naye akawasikiliza. Lakini palikuwa katika mji na mshirika wa liwali, mchawi aliyeitwa Elima au Bar - Yesu. Kwa uwazi alifikiri kwamba mahubiri ya mitume yataharibu ushawishi wake uliokuwa na bwana wake, na hivyo akajaribu kuzuia maneno yao, kwa kugeuza maana ya mitume, na "kumzuia liwali toka kwenye imani". Paulo aliposikia hili, akamkazia macho Elima, na kumwambia. "Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa ibilisi, adui wa haki yote huachi kukoma kuzipotosha njia zilizo nyooka za Bwana?" (6). Matokeo ya mtenda maovu yalikuwa makubwa mno maana alipigwa upofu kwa muda naye akawa mtu wa kumshika mkono kumuongoza. Elima, bila shaka hakuwa ni mtoto halisi wa kiumbe mwenye nguvu kuliko wengine. Alikuwa na hatia kwa kujaribu kuipotosha. Injili, hivyo alikuwa ni msingiziaji, kiasi kama tunavyomsema mtu mwovu kuwa "mwana wa uovu", kwa hiyo mchawi alikuwa ni mwana wa kusingizia. Vile vile, Wayahudi walipotaka kumuua Yesu, wakiisha fanya mashitaka ya uongo juu yake, aliwajibu "Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, na tamaa za baba yenu ndizo mnapenda kuzitenda" (7). Hapa tena Wayahudi hawakuwa ni watoto wa kiumbe anayedhaniwa kuwa na nguvu kuliko wengine. Ingawa hivyo, walikuwa ni watoto wa upinzani au wenye hali ya akili ya kushitaki uongo. Kitabu cha Ufunuo kina nyaraka saba za mwisho ambazo Yesu alizituma kwa walimwengu kwa. kupitia Mtume Yohana. Moja kati ya hizo barua ilipelekwa kwa kanisa lililokuwapo katika mji wa Smirna, mji uliokuwa karibu na pwani ya magharibi mwa Asia ndogo. Yesu aliwatahadharisha kuwa imani yao itawpatia dhiki nyingi, aliwaandikia "Wasiogope mambo yatakayo wapata; tazama ibilisi atawatupa baadhi yenu gerezani" (8). Kwakweli Wakristo walifungwa katika mji wa Smirna na sehemu zingine nyingi katika Dola la Kirumi, walakini sio kiumbe anayedhaniwa kuwa na nguvu zaidi ya wengine aliwatupa gerezani. Taabu zao zilitoka kwa mamlaka za kipagani za Rumi, ambazo ziliwasingizia kwa mwenendo wao dhidi ya Serikali. (3) 'MAJINI NA MASHETANI" Neno "ibilisi" katika umoja halionekani katika Agano la Kale, bali katika uwingi linapatikana mara nne. Maneno mawili ya asili yametumika, lakini wala hayana uhusiano wowote na neno la Kiyunani "diabolos". La kwanza, sairim, limetokea mara mbili na maana yake ni "wenye manyoya" au "watoto wa mbuzi" au mbuzi". Hawa walikuwa ni majini au mashetani wa kwenye mti, waliodhaniwa huishi katika pori. Waliabudiwa na Wamisri waabudu sanamu. Fungu la kwanza la maneno lina onyo kwa Waisraeli walipokuwa wanazunguka jangwani, kuwa wasiabudu majini au mashetani kama walivyofanya Wamisri (9). Fungu la pili la maneno linatuambia jinsi, wakati mfalme Yeroboamu alipoanzisha Ufalme wa Israeli, aliingiza utaratibu mpya wa dini ambao ulijumuisha na ibada ya sanamu kwa mfano wa "mashetani"(majini) na ndama alizozitengeneza" (10). Hapa tena ilikuwa m kurudia maovu ya kuamini mambo yasiyojulikana ya MISRI. Neno lingine lililotafsiriwa "mashetani" katika Agano la Kate ni Shedim ambalo linamaanisha "wanaoharibu" au "waangamizaji". Limetumika kutaja miungu ya uongo au sanamu, ibada ambayo iliharibu au kuchafua mioyo ya watu. Fungu la kwanza la maneno (11). linasimulia jinsi hao Waisraeli katika jangwa walivyo zitolea sadaka hizi sanamu na sio kwa Mungu, ambapo fungu la pili linataja kuwa walitoa hata watoto wao kwa hizo sanamu (12). Ni wazi kwamba mafunzo yetu mpaka hapa hajatoa sababu za kuamini kuwa maneno mawili ya Kiebrania yaliyotafsiriwa ibilisi katika Agano la Kale au neno "diabolos" katika Jipya yanataja kiumbe muovu kupita wengine. Ingawa hivyo, mafungu ya maneno mengine zaidi yanahitajika kuchunguzwa. SEHEMU ZA KUNUKUU 1. Tito2:3 2. 1 Timotheo 3:11 3. 2 Timotheo 3:3 4. Yohana 6 :66-71 5.Yohana13:2 6. Matendo 13:10 7.Yohana 8:44 8.Ufunuo 2:10 9. Walawi 17:7,8 10. 2 Mambo ya Nyakati 11:15 11. Kumbukumbu la Torati 32:17 12. Zaburi 106:37 (4) MSHITAKI WENU IBILISI - 2 MAPEPO NA ROHO WACHAFU Neno diabolos, au ibilisi, ambalo maana yake ni "msingiziaji" linatokea kama lilivyosemwa awali mara 38 katika Agano Jipya. Ingawa hivyo, kuna neno lingine, nalo pia limefasiriwa "ibilisi", limetumika katika sehemu hiyo ya Maandiko. Neno lenyewe ni daimon. ambalo pamoja na maneno linakopatikana, limetokea mara 77. Halina uhusiano wowote na diabolos kabisa. Maneno mbali ya daimon, ni daimonion na daimonzomai. Yote yametokana na daio. neno hili maana yake ni "kugawa". Kabla ya kutafakari namna yanavyotumika katika Biblia, inashauriwa kwamba. Tujaribu ilitupate kujua yanamaana gani kwa Wayunani (Wagiriki), ambao ni lugha yao, na ni lugha yao iliyotumika hapo awali kuandikiwa Agano Jipya. IMANI ZA WAYUNANI Kuna vitabu vingi vinavyoonyesha imani za Wayunani katika jambo tunalo lizungumzia. Kwa hivyo vitabu neno daimonia lilieleweka likiwa na maana ya "roho" za wanadamu, watu waliokwisha kufa nao wamefufuliwa na kufikia daraja la miungu. Daimonia hawakuwa ni miungu wakuu au wa-mbinguni. Kwa kweli hawa wa pili hawakuingilia mambo ya wanadamu, bali usimamizi wote waliweka zamani. Katika mambo haya haishangazi kuwa daimonia vilikuwa ni vitu vya kupata heshima kuu katika mioyo ya watu, pamoja na tumaini la dini, hofu, kutumainia, na kuabudu, yote yakiwa yamechanganyika. Vilifuatwa kwa kutoa faida, au vingine, kwa miungu wakubwa kwa wanadamu, kwa sababu hiyo ndiyo asili ya neno daio toka ambako majina yao yalipatikana. Wayunani walifuata zaidi kuwa roho hizi zilizotoka zaweza hata kuwamiliki wanadamu au kuzimiliki hata sanamu zisizosema. na kwamba kwa kuzifanyia uchawi zaweza kutolewa toka kwa wale waliopagawa nazo. Walatini walifuata mtizamo uleule kama Wayunani, na. hata miongoni mwa Wayahudi, siku zote walielekea kufuata mashauri ya dini za uongo wa mataifa yaliyowazunguka, kulikuwa na wengi walioamini katika daimonia. Imani hii kati ya wale walioishi katika wakati wa Yesu watasaidia kutujulisha kwa Maandiko matumizi ya neno hili. Inaweza kuonyeshwa kuwa neno daimon lilitumika kwa kuamini roho ya mwanadamu iliyotoka, wakati neno daimonion lilimaanisha mtu au sanamu iliyosemekana kuwa inamilikiwa na daimon. Neno daimonzomai lilikuwa ni neno liongezalo sifa nalo lilimaanisha "kupagawa na ibilisi (pepo)". BEELZEBULI Kwa nafasi nyingi Yesu aliwaponya watu walioonewa na ibilisi. Viongozi wa dini walipojaribu kumfedhehesha machoni pa watu, walisema, "Yuatoa pepo (daimonia) kwa Beelzebuli mkuu wa pepo", kwa kulinganisha Yesu aliwajibu "Ikiwa mimi natao kwa Beelzebuli hao pepo, na wana wenu watoa kwa nani? lakini, ikiwa mimi kwa kidole cha Mungu natoa pepo. basi hapana shaka Ufalme wa Mungu umewajilia" (5) (1). Beelzebuli alikuwa ni sanamu, mungu wa Wafilisiti, au yawezekana ni "Bwana wa makao". Mfalme wa Israeli, Ahazi, mara moja aliwahi kutuma wajumbe kwenye hekalu lake akiuliza ikiwa Mfalme atapona kutoka kwenye maradhi, ikionyesha kwamba hata siku zile za mwanzo Wayahudi tayari walikuwa wamepokea mapepo ya watu waliokuwa wamewazunguka. Upendeleo wa Ahazi kwa Beelzebuli kuliko kwa Mungu, Muumba, kulimpeleka hata asipone na mauti (2). Ni jambo linalostahili kuangaliwa, ingawa Beelzebuli ilikuwa nisanamu tu, isiyo na nguvu, Yesu hakuthibitisha ukweli huu, bali alitumia fikra za wapinzani wake. Kwa sababu hiyo hakukubali uwepo wa mungu aliye hai aitwaye Beelzebuli, wala hakuafiki mtizamo wa mapepo kwamba yaweza kumiliki wanadamu. KUTOKUWA NA AKILI TIMAMU Maandiko yanamaana gani basi yanapozungumzia mashetani au kukemea mashetani au mapepo? Katika moja ya hotuba zake mashuhuri Yesu anajisema yeye mwenyewe kuwa nj mchungaji mwema, na kusema kwamba atatoa uhai wake kwa ajili ya kondoo, akiongeza habari ya kustaajabisha kuwa sio tu alikuwa na uwezo wa kuutoa uhai wake bali pia alikuwa na uwezo wa kuutwaa tena. Hotuba hii iliwagawa Wayahudi. Kwani wengi walisema, "anapepo (daimonio) na ni mwehu". lakini wengine walisema, "haya sio maneno ya mtu mwenye pepo. je, mwenye pepo aweza kuwafumbua macho ya vipofu"? (3). Kwenye kipindi hapo Yesu aliposhughulika na kusema kweli kuwa alikuwa na uwezo wa kukemea mapepo kwa Beelzebuli, alizungukwa na umati wa watu hata kukawa hakuna wakati wala nafasi ya kupata chakula. Rafiki zake wakitaka asiumizwe, waliingia katikati ya umati na kumtoa, kwa maana walisema, "Amerukwa na akili" (4). Kwa lugha ya wakati ule wangeweza kusema "anapepo". Mafungu haya mawili ya maneno yanaonyesha kwamba, kile ambacho watu wa zama za Yesu walichoita kupagawa na pepo, tunaita kutokuwa na akili imamu. Mtizamo huu umesaidiwa na mfano halisi wa tiba ya Yesu. Hapo alipokwenda kwenye nchi ya Wagerasi, alikutana na mtu "aliyekuwa na mapepo". Hali ya mwili wa mtu huyo ilikuwa kwamba hakuvaa nguo. zozote wala hakuishi katika nyumba yoyote, bali aliishi makaburini. Majaribio yaliwahi kufanywa ili kumfunga na minyororo pamoja na pingu hayakufaa, kwa sababu ya nguvu za wazimu wake, alivivunja vifungo vyake na kukimbilia jangwani. Yesu "alimwamuru roho mchafu amtoke". Taarifa zilipoufikia mji kwa kile kilichotokea, wenyeji walikwenda wao wenyewe kujionea, nao walimkuta kichaa ameketi miguuni pa Yesu "amevaa nguo na yupo katika akili timamu" (5). Ni wazi kuwa hapo awali hawakumuona kuwa ni mwenye akili timamu. (6) KIFAFA Jambo ambalo kwa karibu maelezo ya madawa kwa tiba iliyotolewa na Yesu imetajwa na Injili mwandishi Marko. Kuna mtu alimwendea Bwana na kusema "Mwalimu, nimemleta kwako mwanangu anapepo bubu, na kila apampagaapo humbwaga chini, naye hutoka povu na kusaga meno na kukonda; nikasema na wanafunzi wako wamtoe pepo, wasiweze". Yesu akataka aletewe kijana. "Mara alipomjia, papo hapo akamtia kifafa na kumbwaga chini, akagaa-gaa, akitokwa na povu". Bwana akamuuliza Baba yake, "Amepatwa na haya tangu lini?" Akasema tangu utoto. Na mara nyingi amemtupa katika moto, na katika maji amwangamize; lakini ukiweza neno lolote tuhurumie na kutusaidia. Yesu akajibu "Kama ukiamini, yote yawezekana kwake yeye aaminiye". Kwa haraka baba ya yule mtoto akatokwa na machozi kwa sauti akasema "Bwana naamini, nisaidie kutokuamini kwangu!" Watu wakaja mbio pamoja ili waone patatokea kitu gani, naye Yesu akamwambia "Ewe pepo bubu na kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke huyu na wala usimwingie tena". Kwa kuitikia, roho akalia, akamtia kifafa sana, akamtoka na akawa kama mtu aliyekufa; hata wengi wakasema, "Amekufa". Kwa njia ya kuwajibu akamshika mkono na kumwinua; naye akasimama (6). Ni wazi kuwa huyo mtu alikuwa na kifafa, na hapawezi kuwa maelezo mazuri ya matokeo ya kifafa katika kitabu chochote. Kwa habari iliyotolewa na Injili ya Mathayo kuhusu hilo tukio, mwenye kuugua ameelezewa kama ni mwenye wazimu vile vile akidhihirisha hali ya mwili kwa kifafa (7). Watu wa zamani wanashikilia kwamba kushikwa na kifafa kuliletwa na mwezi, kitendo hicho kimeitwa wazimu wa kifafa, au kupatwa na mwezi. UBUBU Yesu baada ya kumfufua binti wa mtawala toka wafu, na kuponya watu wawili vipofu. mtu mmoja bubu akaletwa kwake (8). Huyo mtu alisemekana kuwa amepagawa na pepo. Yesu alimtoa pepo na mtu bubu akaweza kusema. Hivyo basi, udhaifu huo, ambao sisi hatuwezi kuudhania umeunganika na kupagawa na mapepo leo, kwa nyakati za Agano Jipya watu waliona hivyo. UPOFU Katika nafasi nyingine, mtu aliyekuwa na yote mawili kipofu na bubu aliletwa kwa Yesu (9). Huyu mtu naye pia alifikiriwa kuwa anapepo. alipomponya yote mawili alinena na kuona. (7) UPONYAJI Njia ya kueleza neno iliyotumika kwa tendo la Yesu katika mfano wa mwisho tulio unukuu, "uponyaji" ni kutoka neno la Kiyunani etherapeusen, ambako neno letu uponyaji limewiana. na linaonyesha tiba na sio kufukuza. Ni neno lililo tumika mara nyingi kwa tendo la Yesu katika mambo haya, ili kutimiliza unabii wa Agano la Kale. "Yeye mwenye aliutwaa udhaifu wetu na kuchukua magonjwa yetu" (10). Yohana Mbatizaji alipokuwa ananyong'onyea gerezani, alianza kupoteza imani ya kazi iliyomleta Yesu na ikambidi atume wajumbe kwake akiomba aondolewe mashaka, Yesu alijibu kwa sehemu ya kwanza kwa kuponya wengi wenye udhaifu na wenye masumbufu, na wenye roho wachafu; na kwa wengi waliokuwa vipofu wakapata kuona. Ndipo alituma ujumbe kwa Yohana, "Mwambieni Yohana ... Jinsi vipofu wanavyo ona. waliolemaa wanatembea, walio na ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na kwa masikini Injili inahubiriwa". Hapa hajataja mambo ya "kukemea pepo", na ukweli huu unaonyesha kwamba wale waliokuwa "wamepagawa" walikuwa wanateswa na magonjwa ya akili na ya mwilini. Mtume Paulo alitoa neno la kukataa kama kuwa daimonia si chochote wala sio kitu halisi alipowaandikia Waraka wa kwanza kwa Wakorintho. Wakristo Wakorintho fulani walikuwa wanajiunga na sherehe za kuiheshimu miungu ya Kipagani, iliyo kuwa machoni pao waliokuwa wanaiabudu, daimonia au "roho za wanadamu waliotoka". Samahani kwa tendo lao, Wakristo hawa walisema. "Sanamu au daimonion sio chochote kabisa, kama tunavyojua vema, na dhamiri zetu hazifanyi kosa kwa kwenda kwenye sherehe kama hizi". Kwa jibu hilo mtume alijibu vikali, Ni semeje basi? kwamba sanamu ni kitu chochote, au wale wanaozitolea sadaka hizo sanamu (daimonia) NI CHOCHOTE? lakini nasema kwamba vitu wanavyovitoa sadaka watu wa mataifa. wanatoa kwa mashetani (mapepo) nami napenda msiwe na shirika na mashetani". Hapa mtume anakubali kuwa daimonia si chochote, wamo ndani ya watu wanaojitoa kwa hizo daimonia. Ni dhahiri, kwa sababu hiyo, kwamba mapepo na kwamba Yesu aliponena kuhusu kukemea mapepo. alikuwa anasema kwa maneno tu, ambayo kwa wale waliomsikia, walikuwa katika msemo wa kila siku, kama sisi siku hizi tunapo msema kichaakuwa amemilikiwa, bila kuamini kwamba "roho" za wanadamu za watu waliokufa zimemwingia. Kama tulivyoona kwa maneno, diabolos. sairim (wenye manyoya) na shedim (wanao haribu) neno daimon na maneno yanayo ungana nalo hayasemi uwepo wa kiumbe anayedhaniwa kuwa na nguvu kuliko wengine. SEHEMU ZA KUNUKUU 1.Luka 11:15-19 2.Wafalme1:24 3. Yohana 10:14-21 4. Marko 3:20,21 5. Luka 8:26-35 6. Marko 9:17-27 7. Mathayo 17:14-18 8. Mathayo 9:33 9. Mathayo 12:22 10. Isaya 53:4, Mathayo 3:17. 11. Luka 7:19-23 12. 1 Wakorintho 10:18-12 (8) MSHITAKI WENU IBILISI - 3 SHETANI Kwa kawaida imedhaniwa kuwa neno "Shetani" ni mzunguko wa jina "Ibilisi" na kwamba maneno mawili haya yanaeleza kitu kimoja. Kufuatia desturi yetu iliyotangulia. twaweza kupima mtizamo huu kwa maelezo ya maneno asili yaliyo tumika ndani ya Biblia. na pia kwa kujifunza fungu la maneno ambamo limetumika. Kabla ya yote, tunakuta kwamba neno "Shetani" limetokea sehemu zote mbili Agano la Kale na Jipya. mara 19 la kwanza na 36 la pili. Ni neno la Kiebrania Sathan, nalo limeletwa bila kuwa na tafsiri katika Biblia. Maana yake ni "adui, mshitaki au mpinzani" na lenyewe halitaji mjaribu kiumbe aliye na nguvu kupita wengine. Siku zote neno hili halijaachwa bila tafsiri katika Maandiko kama Shetani. Mara kumi na nne imetolewa maana ya tafsiri yake, "adui". Tafakari zingine kwa sehemu zilikotokea zitatoa nuru kubwa juu ya maana ya neno. MFALME DAUDI KAMA SHETANI Daudi alipolazimika kukimbia Hi kuokoa maisha yake toka wivu wa Mfalme. Sauli, alipata kimbilio kati ya Wafilisiti, ambaye mshindani wake Goliati, hapo awali alimuua. Wafilisiti wengine kwa kawaida hawakumwamini na vita ilipotokea, wakamlalamikia mkuu wake. aliyeitwa Akishi, "Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagizia, wala asiende nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani" (1). Hapa neno lililo tafsiriwa "adui" ni Sathan kwa Kiebrania. Hivyo mtu ambaye mahali pengine ameeleweka kuwa "mtu aupendezae moyo wa Mungu" (2) ameelezewa yamkini kuwa Shetani. MALAIKA MWAMINIFU KAMA SHETANI Tokeo la ajabu kwa neno Shetani katika lugha asili ya Kiebrania linatukia kwa muunganiko na fungu la maneno la safari ya Waisraeli toka Misri kupitia jangwani kuelekea Nchi ya Ahadi ya Kanaani. Mataifa yote yaliyokuwa karibu na Kanaani yalishikwa na hofu kadri Waisraeli walipokuwa wanasogea, na mfalme mmojawapo wa nchi hizo, Balaki Mmoabu, akatafuta mtu mmoja wa kuwalaani Waisraeli. Kwa kusudi hili akajitahidi kumkodi mtu wa kufanya uganga. ambaye ni Balaamu. (9) Mtu huyu kwa mara ya kwanza alikatazwa asiende kwa Balaki, lakini baadaye akaambiwa kwamba ikiwa wajumbe wa mfalme wakimwita aende nao. Sasa yeye kwa tamaa ya kupata zawadi iliyoahidiwa na Balaki, hakungoja kuitwa, yeye aliinuka mapema siku iliyofuata, akatandika punda wake na kuanza safari. Ingawa hivyo, sio muda mrefu, malaika wa Bwana, bila kuonekana kwa Balaamu, akasimama katika njia na upanga akiwa ameufuta na kuwa "adui (Shetani) juu yake". Punda aliweza kumuona malaika, na hivyo akakata kona kuingia shambani iii kumuepuka. Balaamu akampiga mnyama ili arudi kwenye njia. ambayo sasa inapita katikati ya shamba la mizabibu na ukuta ukiwa kila upande. Mara nyingine tena malaika akasimama katika njia, na mara moja tena punda akajaribu kumkwepa, kwa kufanya hivyo aliuchubua mguu wa Balaamu kwenye ukuta. Tena bwana wake akampiga kwa kukosa kumpita malaika. Punda akaanguka chini na mara hiyo alipigwa tena. Mnyama asiye weza kunena alipewa maneno, naye "alikaripia wazimu wa nabii": Mwishowe akamuona malaika yeye mwenyewe Balaamu, na baada ya kulaumiwa kwa kumtendea vibaya punda, aliambiwa mambo ambayo atafanya dhidi ya hao watu, na ndipo akaruhusiwa kuendelea na safari pamoja na Wamoabu. Lakini alipofika kwenye nchi yao, badala ya kuwalaani Waisraeli, kwa hofu ya Wamoabu, aliwabariki. (3). Katika jambo hili, malaika wa Bwana, kwa uaminifu akitimiza kazi ya Bwana, amesemwa kuwa ni Shetani au adui. MTUME PETRO KAMA SHETANI Yesu alipokuwa anaishi Palestina akitenda matendo magumu aliyoyafanya vizuri ya kustaajabisha ya uponyaji, palikuwa na fikra nyingi ya kuwa yeye alikuwa ni nani, ndipo siku moja aliwauliza wanafunzi wake kwamba watu wanasemaje kuhusu yeye. Walimwambia kuwa wengine wanasema ni Yohana Mbatizaji, na baadhi husema wewe ni nabii Eliya au nabii Yeremia, amefufuka tena. Basi Yesu aliwauliza wao walidhania ni nani. Kwa kulipuka likaja jibu la Mtume Petro. "Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai!" Yesu akamjibu Petro kwamba watu hawakumfunza ukweli huo, bali ukweli huo ulitoka kwa Mungu moja kwa moja. Yesu akaongeza kwamba Kanisa msingi wake utajengwa juu ya maelezo ya mtume na kwamba Petro atapokea funguo za Ufalme wa mbinguni. Zaidi ya hivyo uamuzi wake kutaka kufunga au kufungua kitu chochote duniani kitaheshimika mbinguni. Yesu alijua kwamba mbali ya kuwa ni Mwana wa Mungu aliye hai, ilimpasa kabla ya muda sio mrefu akumbane na msalaba. Akaanza kuwatayarisha wanafunzi wake kwa ajili ya mshituko watakao upata kwa kumpoteza. Aliwaambia kwamba imempasa kwenda Yerusalemu, na kutendewa vibaya na viongozi wa dini na kisha kuuawa. Pia akawaambia kuwa atafufuka tena toka wafu siku ya tatu. HH ni taarifa ambayo wanafunzi hawakuweza kuiamini. Ni kwa vipi mtu ambaye anaweza kuponya wengi na hata kuwafufua watu, aruhusu yeye mwenyewe kuuawa? (10) Kama jambo lililokuwa mara nyingi likinenwa, mtume Petro alitoa mawazo yao, "Hayo yakupishe mbali, Bwana, haya hayatakupata". Mara moja Bwana alimgeukia na kumwambia, "Rudi nyuma yangu Shetani: ukikwazo kwangu; maana huwazi yaliyo ya Mungu bali ya wanadamu" (4). "Mawazo yako ni ya kibinadamu, sio kama mawazo ya Mungu" - kama tafsiri zingine zinavyosema. Hapa lilikuwa ni badiliko la kushitusha kwa mtume. Awali aliambiwa kupewa funguo za Ufalme wa mbinguni na sasa akawa ameambiwa yeye ni Shetani. Ikiwa tunaelewa neno Shetani linataja mjaribu kiumbe mwenye nguvu zote, basi fungu la maneno haliwezi kufahamika vema. Lakini kama tukilipa maana yake ya asili ya "adui", kila kitu kinakuwa wazi. Kwa kweli Petro alikuwa ni adui kwa Yesu, kwa kuwa kama Bwana angemsikiliza angejaribu kuuepuka msalaba, na kusudi zima la kuwepo kwake kungekuwa kumeshindwa, maana pasipo kuutoa uhai wake pasinge weza kuwepo wokovu kwa wanadamu. MWIBA KATIKA MWILI Mbali ya kutumika kwa mmoja mmoja. neno Shetani pia limetumika kwa mwili au hati ya kiroho. Mfano unaofahamika sana ni ule wa mtume Paulo. Alilaumiwa sana na washirika wa Kanisa la Kikristo lililokuwa Korintho na kwa utetezi wake dhidi ya ubishi wao, aliwaambia ufunuo wa ajabu aliopewa na Mungu, "ambapo alisikia mambo yasiyotakiwa mtu kuyanena. ambayo yalikuwa sio halali kwa mtu kuyanena". Ingawa hivyo, hakuruhusiwa kujisifu kwa aliyoyapata na anasema kwamba ili asije kujivuna "alipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige" (5). Neno "wa" halipo katika lugha asili, na msemo "mjumbe wa shetani" maana yake mjumbe, au adui. Mwiba katika mwili ulikuwa ni aina fulani ya udaifu. Ambao ulikuwa sio dhahiri kabisa, na. udhaifu anaousema hapa ni astheneia kwa lugha ya Kiyunani na maana yake ni kudhurika na ugonjwa wa kupooza. Udhaifu huo ulidhuru hotuba ya mtume, maana uhusiano na udhaifu wake wadadisi waliokuwa Korintho walisema, "akiwepo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu" (6). Vyovyote mwiba ulivyokuwa mwilini mwake ni dhahiri kuwa ilikuwa ni kizuizi na ni adui kwake, akizuiliwa na kufanya kazi yake ya kuhubiri Injili iwe ngumu. Kwa sababu hii kwenye sehemu hii neno Shetani limetumika kwa kutaja ukosefu wa afya ya mwili. ANANIA NA SAFIRA Hapo imani ya Kikristo ilipoimarishwa Palestina. mara ya kwanza washirika wake walishirikiana katika mali walizokuwa nazo, na walikuwa na vitu sawa. Washirika wawili wa jumuia Anania na Safira walitaka kwa yote mawili kuyatengeza; nao wakiisha kuuza walivyo miliki, walileta sehemu tu ya faida, wakidai kuwa wanatoa vyote. Kwanza Anania alisemwa na Mtume Petro, ambaye alisema, "Kwa nini Shetani ameujaza moyo wako hata ukamdanganya Roho Mtakatifu, na kuficha sehemu ya thamani ya kiwanja? Kwa nini umeliweka jambo hili ndani ya moyo wako? Hujamdanganya mtu bali Mungu". Mara Anania akaanguka chini na akafa. (11) Punde mke wake Safira, bila kujua kilichotokea, akaingia ndani ya chumba naye akaanza kusimulia habari ambayo walikubaliana na mke wake na mume wake. Kwake Mtume alisema, "Ni jinsi gani mmepatana pamoja ili kumjaribu Roho wa Bwana? Tazama, nyayo za waliomchukua mumeo kwenda kumzika bado zipo mlangoni". Mara naye Safira akaanguka na kufa (7). Hapa ilikuwa ni tamaa na udanganyifu wa mioyo ya hao wawili ndiyo maana walipata mauti yao. Walikuwa ni maadui wa kweli, kwa sababu walitaka wafikiriwe kuwa wao ni wapaji, wakati huo huo wasipoteze kingi. KUMTOLEA SHETANI Mfano zaidi wa kufurahisha ni matumizi ya neno Shetani unaotokea kwa mtume Paulo juu ya uamuzi dhidi ya mshirika wa Kanisa la Korintho anayekuwa na hatia ya zinaa ya maharimu. Aliandika "Katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, mnapokutanika pamoja ... mtolee mtu huyu kwa Shetani ili mwili wake uangamizwe, na roho iweze kuokolewa katika siku ya Bwana Yesu" (8). Ikiwa kweli Shetani ni mjaribu asiyekufa, inaoneka hakuna maana ya kumkabidhi mtenda dhambi kwake ili amfunze adabu ambayo itampatia akili ya kuacha mabaya. SHETANI CHINI YA NYAYO Akiwaandikia ili kuwafariji waamini waliokuwa Rumi ambao muda kitambo walikabiliana na mateso makali na wapagani ndugu maadui wa taifa moja, Paulo alisema, "Sio muda mrefu Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya nyayo zenu" (9). Kwa njia ipi Shetani akanyagwe na nyayo za mwanadamu? Kuangamizwa kwa upagani katika Dola la Kirumi. ingawa hivyo, kwa majeshi yaliyodai kuwa ni ya Kikristo ulikuwa ni utimilifu wa maneno ya mtume Paulo. Basi kama neno "Shetani" litawekwa mahali pa neno adui kwa kila sehemu linapo tokea katika Biblia, kwa ukamilifu litafaa kwa maana ya neno lenyewe pasipokuwa na wazo lolote la ajenti yeyote wa uovu. SEHEMU ZA KUNUKUU 1. 1 Sam.29:4 2. 1 Sam.13:14 3. Hes. 22:20-33 4. Math. 16:13-23 5. 2Wakor.12:2-7 6. 1Wakor.2:3; 2 Wakor.10.-10 7. Matendo 5:1-11; Matendo 13:22 8. 1 Wakor. 5:1-5 9. Warumi 16:20 (12) MSHITAKI WENU IBILISI -4 UKWEU KUHUSU DHAMBI Mafunzo yetu ya kwanza ya Biblia juu ya jambo hili tunalo lineno yanaonyesha kwamba maneno "ibilisi". "shetani", na "pepo" kwa asili yake ya maana hayataji mjaribu asiyepatikana na mauti. Walakini kuna mafungu ya maneno ambamo haya maneno mawili ya kwanza yanataja watu moja mmoja mashuhuri, na imekusudiwa kuwaona hawa kwa njia ya haki. Kabla ya kufanya hivi, lakini, tunashauriwa kuvutwa kwa kuangalia kwenye mafundisho ya hakika ya Maandiko kuhusu dhambi; na kuhusu njia yake kuondoshwa na kuangamizwa. KILA MTU NA IBILISI WAKE MWENYEWE Biblia inaufafanuzi ulio rahisi juu ya dhambi. Inasema "Dhambi ni uasi wa sheria" (1). Sheria inayotajwa, pasipo shaka, ni sheria ya Mungu. Kwa neno hili watu wote wanahatia, kwakuwa. "hakuna hata mwenye haki mmoja" (2). Ni nini lakini kinachotusababisha tufanye dhambi? Basi tena Maandiko yanatupa jibu. Mtume Yakobo anaandika, "Mtu yeyote anapojaribiwa asiseme anajaribiwa na Mungu: kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa maovu, wala hamjaribu mtu yeyote. Bali kila mtu hujaribiwa na kuvutwa na tamaa zake mwenyewe. Basi tamaa ikiisha kuwaziwa, inaleta dhambi; na dhambi, nayo inapokamilika, inaleta mauti" (3). Kita mmoja wetu anajua kutoka na kuona kwa majaribio jinsi kwa usahihi maendeleo kwa upande wa dhambi ilivyoelezewa katika mistari hii. Isipo kuwa mara moja tukiondosha fikra zenye msukumo wa kutenda maovu, tunajikuta kwa haraka sisi wenyewe tena tunateleza na kuingia katika uasi. Maumbile yetu yanatoa kichocheo na, kwa maana hii, kila mtu ana ibilisi wake mwenyewe (msingiziaji, mwenye kumpaka matope Mungu) na adui (shetani) kwake mwenyewe. Umbo letu hili tumerithi toka kwa Adamu na Eva, ambao walikuwa watenda dhambi wa kwanza. Maandiko yaeleza hali kwa namna hii. "Basi kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na mauti kwa dhambi: kwa hiyo mauti imewapitia watu wote, maana wote wametenda dhambi...... kwa kosa la mtu mmoja watu wote walihukumiwa adhabu .... na kwa kuasi kwake mtu mmoja wengi waliingizwa katika hali ya kuwa wenye dhambi" (4). Kama Adamu, ingawa si katika njia ile ile, "wote wamefanya dhambl na kupungukiwa na utukufu wa Mungu" (5). Kwa maana hii ibilisi, anayeipaka haki ya Mungu matope na kukataa utii Kwake, ni maelekeo ya kutenda dhambi yaliyo ndani ya kila mwanadamu. Ukweli huu umeonyeshwa zaidi na mtume Paulo kwa kuwaandikia Wakristo walio ishi Efeso. Katika mstari mmoja, anaeleza mwenendo wao kabla ya kumwamini Kristo. naye anasema waliongozwa zamani na "roho atendaye kazi katika wana wa kuasi". Katika mstari unaofuata ameandika kwamba kabla ya kuamini walitawaliwa na "tamaa za mwili, wakitimiza mapenzi ya mwili na ya nia" (13) "NGUVU ZA MAUTI" Dhambi ilipoingia ulimwenguni, kifo kilikuja pamoja nayo, maana mshahara wa dhambi ni mauti, na dhambi na mauti vinatawala sasa (7). Hapa kwa, kwa kulinganisha mafungu mawili ya maneno katika Agano Jipya yataonyesha uhusiano wa kati ya ibilisi na dhambi. Kwa fungu la maneno ambalo tayari tumenukuu, mtume Yakobo amesema kwamba "dhambi ikiisha kamilika huleta mauti". Katika waraka kwa Waebrania tunasoma kwamba ibilisi ana nguvu za mauti (8). Hivyo basi dhambi ya mwanadamu na ibilisi ni kitu kimoja. "UZIMA WA MILELE" Dhambi inabidi, kwa haki iliyo ya Mungu, iadhibiwe kwa mauti. Wote ni wenye dhambi, kwa hivi wote wanaangamia na kufa. Bado haukuwa ndiyo mpango wa Mungu kuwa vizazi viende katika njia hii isiyo na matokeo katikati ya enzi zote. Uumbaji usingefanyika kama jambo lingekuwa ni hili. Mungu aliuumba ulimwengu kwa ajili ya utukufu wake, na aliamuru kwamba jamaa wengine wa taifa la mwanadamu wataukalia ulimwengu milele katika wakati ulio na furaha. Akiusema Mlima Sayuni katika Yerusalemu, Daudi mwandishi wa Zaburi alisema "ndiko BWANA alikoamuru baraka, naam uzima hata milele" (9). Ni jinsi gani shida itaondoshwa? Maelezo ya Biblia ya kumaliza kwa karibu yametiwa pamoja na jambo tunalo linena" la Ibilisi. "YESU MWOKOZI" Mtu aliyefanya iwezekane kwa wanadamu watenda dhambi kutubu na kuishi milele ni alikuwa Yesu wa Nazareti. Yote mawili alikuwa ni Mwana wa Mungu Mwana wa Adamu, Alikuwa wa kwanza sababu alizaliwa kwa uweza wa Roho wa Mungu Mtakatifu kwa bikira Mariamu. Alikuwa ni wa pili kwa kuwa Mariamu ni mama yake, na hii ilimaanisha kwamba Yesu alikuwa ni mshirika wa taifa la mwanadamu na aliweza kupata yale yote yanayo wasibu watu. Maandiko yanasema hivi dhahiri sana. Andiko lenye muungano uliopo kati ya Mungu na waaminio kwa njia ya Yesu, waraka kwa Waebrania unasema, "Hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu, bali alijaribiwa katika mambo yote sawa sawa na sisi bila kutenda dhambi" (10) Katika waraka ule ule imeandikwa kwamba, "katika siku za mwili wake", Yesu alimtolea Mungu "maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi" (11). Msalaba uliokuwa imempasa kuustahimili ilikuwa ni mateso ya kutisha kwake, ndiyo maana alisihi "Ee Baba yangu, kama ikiwezekana, niepushie kikombe hiki toka kwangu" (12). Haikuwezekana; Yesu ilimpasa akabiliane na mateso ya kuhofia na kupunguziwa heshima kwa kusulubiwa. (14) "UZIMA WA MILELE NA HATA MILELE" Ni nini kilicho malizwa na jaribio hili la njia ya kutisha na kwa nini ilikuwa ni lazima? Waraka kwa Waebrania unatoa majibu kwa swali tena. Humo tunasoma. "Basi kwa kuwa. kama watoto (washirika wa taifa la mwanadamu) wanashiriki mwili na damu, naye pia alishiriki yayo hayo; Hi kwa njia ya mauti aweze kumharibu yeye aliye na nguvu za mauti, yaani ibilisi, na kuwakomboa ambao kwa hofu ya mauti maisha yao yote walikuwa katika utumwa" (13). Ikiwa tunaamini kuwa ibilisi ni mjaribu asiyepatikana na mauti mstari huu utakuwa haufahamiki, kwa maana ni vipi kiumbe asiye kufa aharibiwe? Zaidi ya hivyo, iliwezekanaje kwa Yesu kumharibu kiumbe kama huyu kwa kufa kwake? Lakini hapo tukielewa kwamba ibilisi ni njia ya kuelezea mwili wenye dhambi wa mwanadamu, inakuwa hakuna shida kufahamu fungu la maneno. Ingawa Yesu alijaribiwa kama watu wote wengine, alikuwa na tofauti moja ya muhimu. Hakukubaliana na majaribu kamwe. Katika maisha yake yote aliyatunza maagizo ya Mungu, na msalaba ulipokuja, ikawa ndiyo mwisho wa maisha makamilifu. "Hakutenda dhambi yoyote",. na "alikuwa mtakatifu", asiye na waa wala uovu ametengeka toka wenye dhambi" (14). Kwa mara ya kwanza na ulikuwa ni muda pekee katika historia dhambi ililetewa vita kwa kufanikiwa, Ndani yake mwenyewe Yesu aliiharibu dhambi, au ibilisi, na maadam ilikuwa hivyo, nguvu za kufa juu yake nazo pia ziliharibiwa. Ingawa alikufa, alifufuliwa toka wafu, na akapewa uzima wa milele; na aliweza kusema, "Mimi nipo hai, nalikuwa nimekufa, tazama, mimi ni hai milele na hata milele" (15). DHAMBI IMESHINDWA Kifo na ufufuo wa Yesu, ulikuwa ni wenye maana ya mbali upande wa pili kuliko kumhusu yeye mwenyewe, ingawa ufufuo ulikuwa unahitajika. Maana kile alichofanya kwa ajili yake mwenyewe aweza sasa kufanya kwa ajili ya wengine. Kwa kuwa amemshinda ibilisi, au maelekeo yanayo kimbilia kutenda dhambi ya mwanadamu, njia ilifunguliwa na dhambi za watu zaweza kusamehewa kabisa kwa kupitia kwake. Kwa matokeo, watu wenye dhambi, mbali na dhambi zao, wanaweza sasa kuwa na tumaini la kuishi milele. Mungu anapenda kuipokea dhabihu isiyo na waa ya Bwana wetu kama njia ya kuwasamehe wale ambao wanachukua JINA lake juu yao wenyewe. Yesu aliitwa Yesu (Mwokozi) kwa sababu alikuja kuwaokoa watu wake kutoka kwenye matokeo ya dhambi zao. Kwa maneno zaidi ya waraka kwa Waebrania, "Aliiondoa dhambi kwa dhabihu ya nafsi yake" (16), na maelezo yaliyo sambamba na tuliyo nukuu tayari, ni "Kwa njia ya mauti alimharibu ibilisi". "Kwa makusudi haya Mwana wa Mungu alidhihirika, ili azivunje kazi za ibilisi" (15) (17). INJILI Kazi ya Yesu bado haijakamilika watu hata sasa ni wenye dhambi, "watoto wa kuasi" (18), au kama Andiko linavyosema "watoto wa ibilisi" (19). Wokovu toka hali hii isiyo na furaha hauji kwa njia yake wanaweza "kusimama na kupingana na hila za shetani" (20). Pia injili inaeleza kwamba Yesu atarudi tena kuja kusimamisha ufalme wa Mungu hapa duniani, ufalme utakao ondosha falme zote za mwanadamu, pamoja na upinzani wote wa ibilisi na shetani, maneno haya yanataja tabia yao ya kusingizia na chuki kwa upande wa mapenzi ya Muumba. Na kwa matokeo, "falme za ulimwengu huu zitakuwa ni falme za Bwana wetu na Kristo wake, naye atamiliki milele na milele" (21). Kwa kuiamini Injili; toba ya kweli; na kuikubali kazi ya ukombozi wa Yesu mwamini yampasa abatizwe kwa maji mengi kwa ajili ya ondoleo la dhambi zilizo pita. Toka ndani ya maji anainuka na kuwa kiumbe kipya, maisha yake msingi wake unakuwa juu ya Bwana. Wakati huo anakuwa ameitwa "ameuvua utu wa kale, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya" (22), au kwa maneno mengine ni kufanya vita juu ya dhambi ambayo kwa maumbile ya mwanadamu ni mwepesi kuelekea. Hii, kama tulivyo ona ni kupigana na ibilisi wa Biblia. Kwa jitihada hii hatakuwa ni mwenye kufaulu kwa ujumla, maana bado ni mwanadamu pamoja na maelekeo yote ya kutenda dhambi; lakini kama akipinga vishawishi hivi vya ibilisi vitamkimbia. Hata kama anashindwa na dhambi mara kwa mara kwa sababu ya udhaifu wa mwili, anaweza kumuomba Mungu ili amsamehe kwa njia ya Yesu ambaye alipata hali ya ubinadamu, anajua yote kuhusu udhaifu wake. Kwa maneno ya Yesu katika sala Mwokozi "atamuokoa toka uovu". KUMHARIBU IBIZISI Kilele kitafikia Yesu akirudi duniani, maana kwenye kiti cha hukumu wale watakao kubaliwa watawekwa huru milele kutoka dhambi nao watapewa uzima wa milele katika mwili wenye utukufu, kama ule wa Yesu (23). Kwa hao, vile vile ibilisi atakuwa ameharibiwa na Bwana. Wataingia pamoja naye katika ufalme wake; na kama utawala wake ukiwa unaenea mpaka kuijaza dunia yote, mamlaka yote ya mwanadamu yatafutiliwa mbali.Hatimae, ibilisi na shetani na upinzani wote kwa Mungu, iwe mmoja mmoja au wa taifa, wanao uwakilisha utaangamizwa na kuharibiwa kabisa. (16) SEHEMU ZA KUNUKUU 1. 1 Yohana 3:4 2. Warumi 3:10 3. Yakobo 1:13-15 4. Warumi 5:12,18& 19 5. Warumi 3: 23 6. Waefeso 2:2.3 7. Warumi 6:23; 5:21 8. Waebrania 2:14 9. Zaburi 133: 3 10. Waebrania 4:15 11. Waebrania 5:7 12. Mathayo 26:39 13. Waebrania 2:14.15 14. 1 Petro 2:22; Waebrania 7:26 15. Ufunuo 1:18 16. Waebrania 9: 26 17. 1 Yohana 3: 8 18. Waefeso 2: 2 19. 1 Yohana 3:10 20. Waefeso 6:11 21. Ufunuo 11:15 22. Waefeso 4:22 23. Wafilipi 3: 20, 21 MSHITAKI WENU IBILISI - 5 MWANADAMU NA MYAMA "MASHETANI" Katika nakala zilizopita kwa mfululizo huu mafungu ya maneno ya Maandiko yametajwa ambayo yanaonekana yanamwita ibilisi kana kwamba ni mtu. Sasa ni nafasi ya kupima mafungu haya. Itakuwa ni jambo la kufaa tukiyachukua kwa mpangilio yanamotokea katika Biblia. NYOKA NDANI YA EDENI Neno "ibilisi" halitokei ndani ya maelezo ya majaribu ya Adamu na Eva, bali watu wengi wanafikiria kwamba ibilisi alinena kwa kupitia nyoka aliye wajaribu wazazi wetu wa kwanza hata wakaanguka, kwa kuvutwa na tamaa zao na kula tunda lililokatazwa. Lakini fungu dogo la maneno ya Biblia katika Mwanzo sura ya 3, halimtaji mjaribu asiye kufa wala ukweli kwamba nyoka alinena haisaidii sababu yoyote katika mashindano ya maneno. Kwa kushughulika na maana ya neno "shetani" tulilo litaja awali kwa punda bubu, aliye pewa maneno kwa muda ili kumkemea Balaamu kwa haraka yake, kwa kwenda na wajumbe wa Mfalme wa Moabu ili kuleta laana kwa Waisraeli. Ikiwa punda aliweza kuwekewa maneno hivyo, basi hakuna sababu ya kufikiria kwamba nao uwezo kama huu haukuweza kuwekewa kwa nyoka. Ni dhahiri fungu hili la maneno halisaidii wazo la uwepo wa mtu asiye wa kawaida mwenye umbo lake la kutisha na mkuu wa maovu. Wazo inabidi lionyeshe maana yake kabla ya kuweza kufahamu humo. (17) SHETANI WA AYUBU Kitabu cha Ayubu ni habari ya mtu mwema aliye dumisha wema wake kwa uso wenye taabu kubwa. Imeandikwa kuwa wana wa Mungu walikuja kujihudhurisha mbele za Bwana. Tunawafahamu hawa kuwa ni waabudu wa kweli. Kati yao alikuwepo kiumbe aliyesemwa kuwa ni Shetani. Mungu alimuuliza ametoka wapi, naye alijibu kwamba amekuwa akizunguka zunguka duniani. Mazungumzo yaligeukia kwa kumfikiria Ayubu. Shetani alieleza sifa kwamba Ayubu anamtumikia Mungu kwa sababu ya afya yake, mali na ustawi wa vitu vyote tu; na kwamba kupata mateso kutabadili jinsi anavyo fikiri. Shetani aliruhusiwa kumjaribu Ayubu. Kwa mfululizo. mtu asiye na heri alinyang'anywa wanyama wake, watumishi na watoto wake. Mbali ya hivi hakulalamika. Kisha Shetani akatoa wazo kwamba kama afya ya Ayubu itaondolewa, atageuka na kumlaani Muumba wake. Na hoja hii pia ikakubaliwa. Ayubu akapigwa kwa majibu mwili wake wote. kwa sababu hiyo akaketi kati ya majivu ili ajaribu kupata nafuu kidogo kwa kujikuna kwa kutumia vigae vya vyungu vilivyo vunjika. Bado alikataa kumtukana Mungu. Matukio haya yamesimuliwa katika sura za kwanza mbili za kitabu, ambamo neno shetani limetokea mara kumi na nne. Sura zingine za Kitabu yametolewa mabishano kuhusu taabu ya kuteseka kati ya Ayubu na rafiki zake watatu walikuwa na wasiwasi Elifazi, Bildadi na Zofa, na aliyeingilia kati baadaye Elihu na mwishowe uwezo wa kushtusha Kabisa wenye kufafanusha wa Mwenyezi Mungu. Neno shetani katika Kitabu cha Ayubu ndilo moja ambalo. kama tulivyo ona mara nyingi, limefasiriwa "adui". Mara nyingine tena, hali ya mwenye kuhudhuria hayupo wa kumfikiria kuwa shetani alikuwa ni mjaribu asiye kufa. Kwa kuonekana hakuwa na tofauti kwa sura toka wale aliokuja nao kujihudhurisha mbele za Mungu. Huyu adui alikuwa hana uwezo wake mwenyewe wa kuleta misiba juu ya Ayubu. Uwezo ulitoka kwa Mungu, kwa maana Mungu amedhihirika akisema kwa shetani, "umenishurutisha juu yake (Ayubu) ili kumwangamiza bila kosa" (sura 2:3). Shetani alikuwa adui mwanadamu kwa Ayubu. Kilichotokea hasa hapa kimeelezewa vema, "Humu ndani ni maelezo yenye kuvutia ya desturi ambayo mtu anakuwa amefungiwa kwa dhehebu, kwa shughuli, inabidi apewe mtihani, masimulizi ya hali jinsi Hivyo ambayo chini ya mgawo wa amri ya Mungu, unatokea kwa mtu wa kawaida: na hali iliyo kinyume hapa imeonyeshwa kama kumtesa kwa kutolewa ruhusa juu ya mtu mwema ili ajaribiwe uaminifu wake, wema wake na hali ya akili inayopenyeza kidogo kidogo makusudi ya chini ndiyo sababu ya wema wa mtu. Imetolewa chini ya mfano sio wa Shetani bali wa adui, ambaye ni mwenye kumchongea mtu mwema". Mara nyingine tena shauri la mjaribu asiye wa kawaida na viumbe linapatikana katika Kitabu cha Ayubu tu ikiwa wazo la kuwaza kabla ya kuliweka humo. (18) MSHITAKI (Shetani) ASIMAME MKONO WA KUUME Fungu lililo dogo kama hili limetokea katika Zaburi. Kwa lugha ya Kiingereza mahali palipo andikwa shetani, kwa Biblia ya Kiswahili pame andikwa mshitaki. "Ee Mungu wa sifa zangu, usinyamaze: kwa maana wamenifumbulia kinywa cha mtu asiye haki, cha hila: Wamesema nami kwa ulimi wa uongo. Naam kwa maneno ya chuki wamenizunguka na kupigana nami bure. Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, ijapokuwa naliwaombea. Wamenichukuza mabaya badala ya mema, na chuki badala ya upendo wangu. Uweke mtu mbaya juu yake, shetani asimame mkono wake wa kuume. Atakapo hukumiwa ataonekana hana haki, na sala yake itadhaniwa kuwa dhambi" (Zaburi 109:1-7). Ijulikane katika fungu hila la maneno kwamba hapo kwanza lilapotokea neno la asili "shetani" limetafsiriwa washitaki (hunishitaki, kwa hiyo ni wengi); bali hilt neno linapotokea mara ya pili limeachwa pasipo tafsiri kama "Mshitaki". Hakuna sababu ya kweli kwa badiliko hili. Wale walio mpa mabaya badala ya mema walikuwa shetani au maadui kwa mwandishi wa Zaburi. Ilikuwa niihaki tupu, ambayo hapo itakapo badilika, adui analetwa kwenye hukumu, naye pia atakuwa na adui, kwa jambo hili adui mwenye haki kwa upande wake, ili kukumbusha matendo yake mabaya na kuyapatia adhabu katika njia aliyo waadhibu wengine. LUSIFA Ieleweke kuwa kwa Biblia tulizo nazo za Kiswahili jina hili halipatikani bali katika Biblia za Kiingereza baadhi, lakini pamoja na hayo nabii Isaya anatia fungu la maneno ambalo watu wengine wanafikiri linaonyesha kwamba ni kiumbe ibilisi aliye tupwa toka mbinguni naye anazunguka na kuwadhoofisha wanadamu. Maneno yake ni, "Jinsi ulivyo anguka toka mbinguni, Ee Lusifa, mwana wa asubuhi; jinsi ulivyo katwa kabisa mpaka chini ewe mwenye kuyadhoofisha mataifa. "Kwa kuwa ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za mbinguni. Nitaketi juu ya nyota za Mungu: Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano katika pande za mwisho za kaskazini. "Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye aliye juu. "Lakini utashushwa mpaka kuzimu. pande za mwisho za shimo. Wao wakuonao watakukazia macho kwa karibu wakikuangalia sana, wakisema, Je huyu ndiye aliye itetemesha dunia na kutikisa falme?" (Isaya 14:12-17). Kitu cha kwanza kujua kuhusu fungu hili la maneno ni kwamba hakuna kidokezo chochote cha anaye wajaribu watu. Ni swala la tamaa ya kutaka kuwa maarufu kwa upande wa aliye tajwa. Pili, kiumbe ameelezwa, sio mtu mwenye umbo lisilo la kawaida asiyepatikana na mauti, bali kama "mtu aliyeifanya dunia itetemeke". (19) Jambo linalo zungumziwa linatatuliwa upesi hapo maneno yenyewe ya sura nzima yakichukuliwa katika maelezo. Mstari wa 4 unasomeka, "Utatwaa mithali hii juu ya Mfalme wa Babeli, na useme. Jinsi alivyo koma mwenye kuonea, mji wenye dhahabu ulivyo koma! Bwana ameivunja fimbo ya waovu, na fimbo ya watawala. Yeye aliye wapiga mataifa kwa gadhabu, kwa mapigo yasiyo koma; Aliyewatawala mataifa kwa hasira, ameadhibiwa asizuie mtu". Lusifa, kwa sababu hiyo, hakuwa malaika aliye anguka bali Mfalme mwanadamu wa Babeli ambaye, kwa tamaa ya kutawala kama mungu, aliangushwa na adui zake na kuletwa chini mavumbini. Hii ni sehemu pekee katika Biblia ambapo neno "Lusifa" limeweza kutokea. Linatoka katika lugha ya Kiebrania hili neno na maana yake ni "Vuma" na Mfalme wa Babeli, akijisifu mwenyewe kuwa Mwana wa Asubuhi, au Nyota ya Asubuhi, aliweza vema kuvuma kwa kelele wakati wa maangamizo yake. KERUBI MWENYE KUTIWA MAFUTA Mfano mdogo kama huu uliotokea mwisho kati yake ni unabii wa Ezekieli. Mtu halisi mashuhuri amesemwa kama ifuatavyo, "Ulikuwa ndani ya Adeni. bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako; akiki, yakuti manjano na almasi, na zabarajadi. na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu ....... Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye: Nami nalikuweka ukawa hivyo: ulikuwa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto. Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako. Moyo wako uliinuka kwa sababu ya uzuri wako, umeiharibu hekima yako kwa sababu ya mwangaza wako; nimekutupa (Ezekieli 28:13-17). Maneno "ibilisi" na "shetani" hayajatajwa hapa, lakini watu wengine wamedhani kuwa maneno yanataja kiumbe kama huyu. Walakini wazo hili halishikiki hapo inapogundulika kutokana na maneno yenyewe kwamba mtu mashuhuri aliye elezwa ni mfalme mwenye kiburi wa Tiro, akijisifu kwa kuwa na mali na nguvu, ambaye ametajwa kuwa m "mwanadamu na sio mungu" (mstari wa 2). YOSHUA, KUHANI MKUU Fungu la maneno la mwisho katika Agano la Kale ambalo ni muhimu kulipima linatoka kwa unabii wa Zekaria. Yoshua, kuhani mkuu ametajwa kuwa amesimama mbele ya malaika wa Bwana, na Shetani amesimama mkono wake wa kuume ili kumpinga Shetani amekemewa na Bwana. Joshua, ambaye alikuwa amevaa nguo chafu sana, ameambiwa kwamba dhambi zake zimesamehewa Mavazi yake machafu yameondolewa na kuvikwa mavazi ya ukuhani, kilemba kizuri amevikwa kichwani pake (Zekaria 3:5). (20) Tukio lilikuwa dhahiri ni sehemu ya mfano wa maono na maelezo yake yanapatikana katika mfululizo wa matukio ya wakati. Yoshua huyu alikuwa ni kuhani mkuu wakati wa kipindi hekalu la Wayahudi lilipo jengwa baada ya kurudi toka Babeli utumwani hao Wayahudi. Mradi wa ujenzi ulikuwa na "upingamizi" na watawala wa sehemu maalum walio ongozwa na mtu aliye itwa Tatnai, na ilikuwa tu baada ya kuomba sana ruhusa ya kukamilisha kazi, nao walipata toka kwa Mfalme wa Uajemi, wakati ule alikuwa ni mtawala mkuu wa Palestina (Ezra 5:7). Maono yalitabiri mwendo wa matukio. Tatnai alikuwa ni shetani, au adui kwa Wayahudi, katika kuzuia kazi zao. Walakini alikemewa na Mungu na upinzani wake ulizimika. Hatimae Yoshua alipata hekalu lake, baraka iliyo ashiriwa kwa kubadilishwa mavazi, na kuvikwa kilemba kichwani pake. Hapa tena hakuna mstari unaomtaja shetani asiye kufa, bali adui wa mwanadamu. Mafungu ya maneno katika Agano Jipya yamebakia kupimwa yanayotaja Ibilisi na Shetani. MSHITAKI WENU IBILISI - 6 MAJARIBU YA YESU Tayari imeonyeshwa kwamba kuna mafungu ya maneno katika Agano Jipya, kama vile katika Agano la Kale, yanayo onekana yanamwita ibilisi kana kwamba ni mtu, na kwa nakala iliopo maneno haya ya kitabu yanapimwa. Majaribu ya Yesu yameandikwa na waandishi wa Injili Mathayo, Marko na Luka kwa maelezo ya nyongeza kwa kila mmoja. Kwa kifupi, ukweli ni huu. Mara baada ya ubatizo wake, Yesu aliona msukumo wa nguvu wa kutaka kuwa peke yake ili ajiandae kwa kazi yake. Kwa kupatana, alikwenda jangwani na alitumia siku arobaini akiwa amefunga. Mwisho wa kipindi hicho, ambacho alikuwa pamoja na wanyama pori na akiwa anatunzwa na malaika. akasikia njaa. Maneno yanayo fuata yanaeleza majaribu matatu yaliyo fuata. 1) "Ibilisi akamwambia, ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate....." 2) "Ibilisi akamchukua hadi kwenye mlima mrefu, na akamwonyesha falme zote za ulimwengu kwa dakika moja .... uwezo wote huu nitakupa na utukufu wake.... kwa hiyo kama utanisujudia mimi yote yatakuwa yako ..." 3) "Na ibilisi akamleta hadi Yerusalemu, na akampandisha kwenye kinara cha hekalu, akamwambia, Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe toka hapa kwenda chini, maana imeandikwa. Atakuagizia malaika wake wakulinde na kukutunza". Yesu aliyakataa mapendekezo yote haya na alibakia huru toka kutenda dhambi. Luka anayaita matokeo ya majaribu, "Ibilisi" ( diabolos). Marko ameyaita haya matokeo kuwa ni "Shetani". Tayari tumejua kwamba "diabolos" maana yake ni msingiziaji, ni kwamba "Shetani" maana yake ni adui. Zaidi sana, tumekuta kwamba majaribu yanatoka ndani ya mtu mwenyewe. Kutumia elimu hii kwa mtihani aliopewa Yesu, jambo linalo zungumzia linakuwa wazi. (21) Yesu alipokwenda jangwani, alikuwa amejaa na Roho Mtakatifu, na alikuwa na uwezo usio na mpaka. Kwa matokeo, palikuwa hapana haja kwa kiumbe anayedhaniwa kuwa mwovu, awe anakufa au hafi, wa kumjaribu. Njaa yake ilimdokezea kuwa anaweza kutengeneza mkate toka katika jiwe. Uwezo wake mkubwa ulimjaribu ili aongoze falme za ulimwengu, ambazo alikuwa tayari ameahidiwa (Zaburi 2:6-8). Kwa kujua kwake yeye kuwa ni Mwana wa Mungu ndiko kulimsisitiza atumie vibaya ulinzi wa Baba yake. Mawazo haya yote yalikataliwa, na wanyama pori wa majaribu, wakali zaidi kuliko wanyama halisi wa pori, walifukuziliwa mbali; vishawishi ambavyo vingemchongea kwa Mungu, na kuwa adui kwa azimio la Mungu alivishinda kabisa. Watu wengi wanaona shida kuamini kuwa Yesu alijaribiwa na mawazo yaliyotoka ndani yake mwenyewe. Wanadhani kuwa wazo hili ni kumvunjia heshima Bwana wetu. Lakini linakubaliana na kile ambacho Maandiko yanatuambia kuhusu Yesu - kuwa ingawa alikuwa Mwana wa Mungu, alishiriki umbo letu, na "alijaribiwa katika mambo yote kama sisi" (Waebrania 2:14, 4:15). Ukweli huo chini ya hali ya mambo haya alipinga kila jaribu na akawa "bila dhambi", ndicho kinafanya awe mfano wa kweli kwetu. Mbali toka kuwaza kuwa anavunjiwa heshima, unawekwa mlinganisho wa kweli kwa mafanikio yake ya ajabu na ushindi wake wenye utukufu juu ya mwili. KUANGUKA TOKA MBINGUNI Kwa nafasi moja Yesu aliwatuma rafiki zake 70 wakiwa na uwezo wa kufanya miujiza. Walirudi wakiwa na furaha, kwa sababu, "mapepo" yalitiishwa chini yao, na hivyo waliweza kuponya magonjwa kama magonjwa ya akili na kifafa. Kwa kujibu, Yesu akasema, "Nalimwona Shetani kama umeme akianguka toka mbinguni hadi chini" (Luka 10:18). Awali tuliona kwamba Shetani aliwekwa chini ya nyayo za Ukristo hapo upagani wa Mamlaka ya Kirumi yalipo angushwa na dini ya Yesu. Hii habari ya Bwana ni fungu la maneno linalo lingana. Watawala wa kipagani walianguka toka sehemu za mbingu, au nafasi za uwezo katika mamlaka ya Rumi. "MALAIKA" WALIO TENDA DHAMBI Katika kitabu cha mwisho lakini kimojawapo cha Biblia, Waraka wa Yuda, maneno yafuatayo yametokea, "Na malaika wasio ilinda, enzi yao wenyewe. bali wakayaacha makao yaliyo wahusu, amewaweka katika vifungo vya milele katika giza kwa hukumu ya siku ile kuu" (mstari wa 6). Maneno kama haya yanatokea katika barua ya Pili ya Petro (2 Petro 2:4). Mafungu mawili ya maneno yanafanana na ni habari ya adhabu alizo zileta Mungu, nyakati zilizopita juu ya wanadamu waliokosa imani. Miongoni mwa mifano iliyotolewa ni ya watu waovu waliogharikishwa wakati wa Nuhu; wenyeji wa miji ya Sodoma na Gomora; na Waisraeli wasiotii walioangamia jangwani katika safari ya kutoka Misri kwenda Palestina. (22) Katika ya mifano hii, jambo la -malaika walioanguka limetolewa. Inapaswa, kwa sababu hiyo, iaminike kwamba hawa malaika, au mawakala pia walikuwa ni wanadamu. Habari iliyotolewa haijaturuhusu kwa kanuni ya kuwatamabua, lakini inaonekana inaelekea sana kuwa walikuwa ni Kora, Dathani na Abiramu na mkutano wao, ambao japo walikuwa ni wakuu wa Israeli, walimuasi Musa na hivyo walijishushia hadhi yao. Nchi ilifunua mdomo na ikawameza ndani ya giza. Humo wanaweza kusemwa wametunzwa mpaka siku ya hukumu. Waraka huo huo wa Yuda unamtaja Mikaeli malaika mkuu akishindana na ibilisi kwa ajili ya mwili wa Musa, asilete mashitaka kwa Kumlaumu, akasema, "Bwana na akukemee" (mstari wa 9). Hapa tena mwandishi inabidi wanadamu walikuwa akilini mwake. Mikaeli ni mfano wa Musa, ambaye daima alishindana na adui, au mchongeaji (dhambi), kwa ajili ya kundi la watu ambapo yeye alikuwa kiongozi (wa watu wa Israeli), naye siku zote alikuwa tayari kujifanya kuwa si mtu astahiliye kufikiriwa na kuacha karipio tote kwa Mungu. Kwa mfano, Kora na mkutano wake walipoasi, alisema, "Kesho Bwana ataonyesha ni nani ni wake na wanao stahili". MIKAELI Fungu la maneno linalostahili kuangaliwa linapatikana katika Kitabu cha Ufunuo. Linasomeka, "Kulikuwa na vita mbinguni, Mikaeli na malaika zake wakipigana na joka; nalo joka lilipigana na malaika zake, nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana mbinguni .. Nalo joka kuu likatupwa, nyoka yule wa zamani aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa mpaka chini. na malaika zake walitupwa pamoja naye" (Ufunuo 12:7-9) Katika kusoma kwanza fungu hili la maneno linaonekana linadokeza kwamba ibilisi aliwahi kuishi katika mbingu za kweli, lakini wkati Kitabu cha Ufunuo ambacho kinajieleza kuwa ni cha kutumia ishara, kikisomwa chote, inaonekana tafsiri hii haiwezi kufaa. Ni dhahiri imesemwa katika mstari unaofungua Kitabu kwamba kinashughulika na mambo ambayo "yanatakiwa yatimie". Kitabi kiliandikwa mapema kabla ya mwaka 100 B.K., miaka mingine maelfu kupita baada ya Adamu na Eva waliopojaribiwa na kuanguka katika Edeni. Fungu la maneno halitaji kuingia kwa dhambi ulimwenguni. Kwa kweli habari yenyewe ni ukubwa wa maneno ya Yesu tuliyokwisha yaona, yatajayo kuanguka kwa upagani. Dini za Kipagani, pamoja na matendo yao maovu yaliyoudanganya ulimwengu wote kwa karne nyingi. Sasa upagani uliondoshwa kutoka katika nafasi ya mbingu na mamlaka ya ulimwengu kwa ushindi wa Ukristo, uliotajwa kwa mfano wa Mikaeli na malaika Zake. "NYOKA YULE WA ZAMAMI" Mawazo kama haya yametumika kuelekea mwisho wa Kitabu cha Ufunuo sura (20:1-3). "Kisha nikaona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu. na mnyororo mkubwa mkononi mwake. (23) Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani, ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu. Akamtupa katika kuzimu, akamfunga na akatia muhuri juu yake; asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile miaka elfu itimie". Ingawa upagani uliondolewa katika kiti Kostantini Mkuu alipousimamisha Ukristo kama dini ya Serikali ya Dola la Rumi, mafunzo yake yamedumu na kuendelea kuwepo katika ulimwengu, na sasa ulimwengu unaoitwa dini ya Kikristo kidogo umeachwa bali jina. Mwenendo wake unasingizia kwa Mungu na matendo yake yapo kinyume na mapenzi Yake. Hivyo inapaswa uondolewe, kiasi kama upagani wa Rumi ulivyoondolewa. Mstari unaofuata (Uf. 20:4) unatuambia kwamba wale ambao wamekuwa ni watumwa waaminifu wa Yesu wataishi na kutawala pamoja naye kwa miaka elfu. Yesu atarudi katika uwezo na utukufu mkuu; na kama uwezo wa kipagani wa Rumi ulivyoanguka toka mbingu za uwezo, basi na falme zote za sasa za dunia, zilivyo na upinzani na Mungu, zitapoteza uwezo wake na kutiishwa na Mpango Mpya utakao wekwa na Bwana. Maneno yenyewe "nyoka wa zamani", ibilisi na shetani" ni maelezoya ya dhambi zote za wanadamu na upinzani wake kwa Mungu. Matokeo ya kujifunza kwetu matumizi ya maneno Ibilisi, Mapepo na Shetani katika Maandiko ni kuonyesha wazi kwamba hakuna mafunzo yanayohusu mjaribu asiyekufa anayepatikana ndani yake. Kwa kweli wazo linahusu kwa vizazi hapo watu walipoongozwa na imani zisizo za kweli, na walitawaliwa na mawazo yao na woga, kuliko kufikiri kwa kufuata Nuru ya Neno la Mungu. Kwa utofauti Biblia yatuambia kwamba, kwa kufa msalabani, Yesu alimharibu ibilisi, aliyekuwa na nguvu za mauti (Hebrania 2:14, 15). Kwa muda ule, uharibifu huu ulimfaidisha tu Yesu mwenyewe, bali dhabihu yake ilionyesha njia ya uzima, ambapo wale wanaokuwa watumishi wa Mungu kama kwa matokeo ya utii wa Yesu kwa Baba yake, watawezeshwa kushinda vishawishi vya ibilisi na shetani vya mwili wenye dhambi vilivyo ndani yao wenyewe. Kwa kuiamini Injili; kwa ubatizo; na baada ya hivyo wakiyatengeneza maisha yao kwa kufuata mfano wa maisha ya Bwana, wanaweza kujitayarisha kwa ujio wake mara ya pili. Ndipo watakusanywa mbele ya kiti cha hukumu, wakiisha kufufuliwa toka wafu, ikiwa walikuwa wamekufa kabla ya kuja. Pale watapewa uzima usio na mwisho na mwokozi, atakaye fanya miili yao ifanane na mwili wake wenye utukufu (Wafilipi 3:21) Na kuwaweka huru mbali na dhambi na mauti. Hivyo Yesu kwa ajili yao, kama tayari alivyofanya kwa ajili yake, atamharibu ibilisi, na kuwaokoa kutokana na uwezekano wowote wa kupata dhambi. (24) Tena: 1 902059 00 - X Matayarisho ya Ubatizo 1 902059 01 - 8 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 1-4 1 902059 02 - 6 Ukimwi 1 902059 03 - 4 Mshitaki Wenu Ibilisi 1 902059 04 - 2 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 5-8 1 902059 05 - 0 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 9-11 1 902059 06 - 9 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 12-15 1 902059 07 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 16-19 1 902059 08 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 20-23 1 902059 09 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 24-27 1 902059 10 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 28-31 1 902059 11 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 32-36 1 902059 12 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 37-40 1 902059 13 - 1 Ufunuo mlango wa kwanza - Maelezo ya maneno ya mstari kwa mstari 1 902059 14 - X Ni Kweli Yesu Kristo Alishuka Kutoka Mbinguni? Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya Biblia kaitka somo hili muhimu. Lina itwa Kuishi katika Ukweli. Unaweza kupata nakala kutoka Kanisa la Christadelphian, au kutoka anuani iliyoandikwa katika kijitabu hiki. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW ISBN 1 902059 03 - 8 Registered Charity Number: 248979 / 1020558 Company Number: 2796412 Telephone +44 (0) 1604 463578 Facsimile +44 (0) 1604 765068 Email: CarlHinton@hotmail.com Web: http:\\www.Bedford-Ecclesia.org.uk