FRONT COVER THE COMMANDMENT OF CHRIST BY AUTHER EAST SEHEMU 1 - Amri za Yesu Kristo SEHEMU 2 - Mafundisho yanayokataliwa SEHEMU 3 - Sawa au Sisawa ??? AMRI ZA YESU KRISTO Mathayo 5:44 - Lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. Mathayo 5:39 - 40 - Msishindane na mtu mwovu, lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Warumi 12:18 - 19, 1 Wakorintho 6:7 - Msijilipize kisasi, lipisheni ghadhabu ya Mungu, maana si afadhali kunyang’anywa. Luka 6:29-30 - Na akunyang’aye vitu vyako, usitake akurudishie. Mathayo 5:25, 1 Cor 6:7 - Kubaliana na adui wako haraka, hata ukikubali makosa kwa sababu ya amani. 1 Tim. 6:8, Rom 12:13, Ebr. 13:16, Yak 1:27 - Usijisumbue kuwa tajiri, kuwa tayari kwa kila kazi njema, wapatie wanaoomba, wasaidie wanaoteseka. Mat 6:1-4 - Msifanye wema machoni pa watu, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wa kuume. War 12:17- Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Mat 5:44, War 12:4 - Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi. 1 Pet 3:9 - Watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu, bali wenye kubariki. Mat 5:44, Waombeeni wanaowaudhi. Yak 5:9, Mat7:1, Msinung’unikiane, msihukumu msilaumiane, msillani. Efe 4:31, 1 Peter 2:1 - Uchungu wote, na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya. Yak 5:16 - Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi. War 12:2, 1 Yoa 2:15 - Msiipende dunia wala mambo yaliyomo. Tit 2:12,Mat 5:30 - Kataa ubaya wote na tamaa za kidunia. Efe 6:5 - 8 - Watumwa watiini wao walio mabwana zenu, hata mabwana wabaya. War 12:16 - Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. War 13:17-18 - Msiwiwe na mtu chochote Mat 18:15, Wag 6:1 - Ikiwa ni dhambi (ijulikanayo au masengenyo) usieneze uvumi. Badala yake ongea na yule ndugu kuhusu jambo hilo, wewe na yeye, ukitumaini kumrejesha. Mat 22:37 - Mpende Mungu Bwana wako na moyo wako wote. Luka 18:1, Mat 6:7 - Omba kila wakati, maombi mafupi na rahisi, maombi ya kibinafsi yawe kwa siri. Efe 5:20, Met 3:6 - Kumshukuru Mungu Siku zote ukimkiri yeye. Mat 7:12 - Vile unataka watu wakutendee watendee vivyo hivyo. 1 Petro 2:21 - Chukua Yesu kama mfano Efe 3:17 - Wacheni Kristo akae ndani ya mioyo yenu kwa imani. Luka 14 - 26 - Mtambueni Kristo zaidi kuliko vitu vyote vya dunia katika maisha yenu. Luka 12:8 - Mkiri Kristo mbele ya watu wote. Luka 21:34 - 36, Mat 24;44 - basi jiangalieni masumbufu ya maisha haya na majaribu ya anasa yasije yakaupanguza upendo wako wa Kristo ndani ya moyo wako. Mat 22:39 - Mpende jirani yako kama unavyojipenda Mat 23:10 - 12 - Usijiweke mkuu juu ya yeyote. Waf 2:4, Wag 6:2 - Usijitaabishe tu na mahitaji yako bali pia saidia katika mahitaji ya wale wengine. Mat 5:16,Waf 2:16, Wag 6:10 - Mwangaza wako unga’e kwa watu wote, shikilia neno la Mungu - Bibilia, fanyeni mema kwa watu wote iwezekanavyo. Fil 2:15 - Mpate kuwa wana wa Mungu wasio na ila katika Kizazi chenye ukaidi. 2 Tim 2:24, Tito 2:2, Fip 4:32- Kuweni wapole, wanyeyekevu, wenye huruma, wenye kusikitikia, wenye rehema, wanaosamehe. Fil 4:5, 1 Pet 1:13,5:8 - Wenye kiasi, walio jitolea, waaminifu na kiasi. Efe 4:25 - Ongeni ukweli mmoja kwa mwengine, wekeni mbali uongo wote Kol 3:23 - Lolote ufanyalo fanya kwa moyo wako wote kama unayemfanyia Mungu. 1 Cor 16:13, Waf 4:4, I Thes 5:6 - 10 Kuweni waangalifu, wenye macho, werevu, wenye furaha, wenye heshima ma shujaa. Wak. 3:12, war 12:12 - Mvikwe na unyenyekevu, Wavumilivu mbele ya watu wote Ebr 12:14 - Tafuteni amani na watu wote. War 12:15 - Furahini pamoja na hao wafurahio lieni pamoja nao waliao. Fip 4:8 - Tafakarini katika mambo yote yaliyo ya kweli, staha, haki, safi, kupendeza, Ukiwapo wema wowote, sifa nzuri. Efe 5:3,4 - Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe wala uchafu wowote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu, wala aibu, wala maneno ya upuzi wala ubishi, hayo hayapendezi, mbali afadhali kushukuru. 1 Kor 10:31,3:17, Chochote ufanyacho linganisha hayo na kuiaibisha jina la Mungu mbele ya watu. Fanya yote kwa sifa za Mungu. Rum 6:11, 2Kor 5:15 - Kumbuka ya kwamba umeifia dhambi ya kila namna kutoka sasa na kuendelea usiishi kwa ajili yako, lakini kwa yeye aliyekufia, na kufufuka tena. Tit 2:14, Gal 6:9, Tena tusichoke katika kutenda mema, maana tutavuna kwa wakati wema, tusipozimia roho. Tit 3:2 - Usimtukane mtu yeyote Kol 3:16 - Neno la kristo na likae ndani yenu katika hekima yote. Kol 3:8, 4:6 - Maneno yenu yawe na neema siku zote. Tit 3:1 - Uwakumbushe watu kunyenyekea kwa wenye uwezo kwa ajili ya Bwana. 1 Peter 1:15 - 16 - Iweni watakatifu katika mwenendo wenu. 1 Tim 5:14 - Usimpe mtu yeyote nafasi ya kulaumu neno la Mungu. (Amri za Kristo na Mitume zimekuwa wakati wowote msingi wa imani ya Kristadelfiano na yalinakiliwa mwaka 1886. Inatarajiwa yeyote ambaye anajiita na jina la Kristo, afuate maagizo yake.) MAFUNDISHO YANAYOKATALIWA KAMA MAKOSA Kwamba bibilia haikuandikwa kwa upuzi wa roho mtakatifu wa Mungu. Kwamba Mungu ni utatu Kwamba mwana wa Mungu amekuwapo pamoja na baba yake tangu enzi yote. Kwamba maumbile ya Yesu hayakuwa na dhambi. Kwamba Roho Mtakatifu ni kiumbe tofauti na Mungu. Kwamba mwanadamu huishi hata baada ya kufa. Kwamba waovu wanateseka katika jenahanamu. Kwamba wenye haki huenda mbinguni baada ya kifo. Kwamba ibilisi ni kiumbe cha ajabu ambacho kina ishi. Kwamba ufalme wa Mungu ni kanisa. Kwamba injili ni kifo kuzikwa na kufufuka kwa yesu kristo. Kwamba kristo haji mpaka ukamilisho wa ile miaka elfu. Kwamba kiti cha hukumu cha yesu kristo, wakati atakapokuja si kwa wale watakatifu, lakini ni kuwapa dhawabu kulingana na matendo yao. Kwamba ufufuo ni kwa wale wanyofu. Kwamba waliokufa watafufuliwa wakiwa katika hali ya kutokufa. Kwamba watu watakaotawalwa katika ufalme watakuwa katika hali ya kutokufa. Kwamba amri za Musa zingali zinatumika hata leo. Kwamba waamini lazima wakutane siku ya sabato. Kwamba ubatizo wa kunyunyizia watoto maji ni mafundisho ya maandiko. Kwamba watu ambao hawajasikia injili wataokolewa. Kwamba mtu anaweza kuokolewa bora tu awe anaishi maisha mema, hata kama hajui injili. Kwamba mtu aweza kuokolewa ikiwa hajui injili. Kwamba watu wanaweza kuhufikia wokovu bila masharti. Kwamba hakuna dhambi ndani ya mwili. Kwamba Yusufu ndiye baba wa Yesu halali. Kwamba dunia itaharibiwa. Kwamba watu wanaweza kubatizwa bila kujua injili. Kwamba kuna vyakula fulani vinaweza kukataliwa. Kwamba waamini wanaweza kutumika katika Jeshi, polisi, kuwa na nafasi katika siasa, kuuliza kulipwa madeni kupitia kwa koti. Kwamba mke asiyeamini anaweza kupewa talaka. Kwamba waamini wataenda mbinguni katika hali ya kunyakuliwa wawe na Yesu milele. Kwamba karama za Roho Mtakatifu hazikuondolewa wakati Bibilia ilikamilishwa. Kwamba kuna watu wana karama za Roho Mtakatifu ambao wanauwezo wa kufanya miujiza. Kwamba wadada hawana haja ya kuvaa vitambaa vichwani mwao. Kwamba waamini wanahitaji huduma ya kuhani kuliko yesu kristo. Kwamba Mkate na Divai ambao hutumiwa kwa meza ya Bwana, hugeuka kuwa Mwili na damu ya Yesu. Kwamba tunahitaji kula Mkate pekee katika meza ya Bwana. Kwamba tunahitaji watumishi wanaolipwa. Kwamba mazishi yawepo mahali ambapo pana makaburi yaliyotakaswa, na kaburi lilowekwa alama. (Orodha ya mafundisho ambayo yafaa kukataliwa yanahitaji kujumulishwa na amri za Yesu Kristo, kama mwongozo kwa waamini wa maandiko wakielewa na kufuata tangu 1886. Mafundisho yanayofaa kukataliwa yanaonyesha jinsi elimu ya madhehebu ya makanisa yalivyoenda kando ya injili ya kweli.) (Kumbuka haya ni mafundisho ambayo yafaa kukataliwa). KUWEKA KANUNI Watu wengi hulalamika kwamba uadilifu umeshuka chini. Hii ni kwa kila taifa katika dunia. Hata hivyo hawana kanuni fulani ya kuwaelekeza watu vile inawapasa kufanya. Sote tuna njia ya kuangalia. Vile ninavyosema kuhusu uadilifu fulani inawezekana sote tukawa tunakubaliana ingawa tunabishana. Kwa hivyo ni nani anapasa kutupa suluhisho kuhusu shida hii na ni wapi inatupasa kupata jawabu. Wakristadeifiano wanaamini katika Bibilia neno la Mungu, ndio tu mwanzo wa mafundisho ya uadilifu wa neno la Mungu ambayo inafaa tuendeleze katika taifa la wanadamu. Hii ni kwa sababu Mungu ndiye aliyetuumba na anajua ni kipi anafaa kutupa na ni njia ipi ambayo kwetu haifai. Bibilia inaweka hizo kanuni. Si kwamba ni rahisi, lakini tukiweka huo mpangilio katika maisha yetu, hatutakuwa na furaha tu bali pia tutakuwa na tumaini katika ufalme wake, wakati Yesu atakaporudi. 1 Petro 3:12 “Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya”. KITU KWA BURE Luka 16:10. Aliyemwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Efe 4:28 “Mwiibaji asibe tena, bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji. UFAFANUZI: Hii ina maanisha tuwe waaminifu katika vitu vidigo na vikubwa pia - kuwa waaminifu kwa kazi zetu na biashara zetu uaminifu katika kanisa. Uaminifu katika familia. Uaminifu tunapokabiliana na Polisi au watoza ushuru. MCHEZO WA KAMARI 1 Tim 6:10 “Kupenda fedha ndio chanzo cha uovu wote” Luka 12:15 “Aangalieni, jilindeni na choyo” Mith 16 : 8 “Afadhali mali kidogo pamoja na haki: Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu” UFAFANUZI: Mchezo wa kamari unaweza geuka ukawa uzoefu. Kupitia huo, mke na watoto wanaachwa wateseke. Hata ingawa si vibaya kuwa na pesa, ni vibaya kuzipenda kiasi ya kuzipata kwa njia isiyofaa. Kupata fedha kwa njia ya kamari inaweza kugeuka ikawa ni sawa na dini, pesa hapa ikawa ndio Mungu. NIKO SAWA WAKATI WOTE Matt. 7:12 - Basi yoyote mtakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo. 1 The 4:11 -12 - Kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi na mikono yenu. 1 Peter 4:15 - Basi mtu wa kwenu asiteswe ……… ajishughulishaye na mambo ya watu wengine. Yak 3:1 Ndugu zangu msiwe waalimu wengi UFAFANUZI Tunaweza kufikiria ni rahisi kujua yale mema kwa watu wengine kuliko wao wenyewe. Lazima tukumbuke ya kwamba Bwana wetu ni mmoja - Bwana Yesu. Yeye tu ndiye anayejua hali ya kila mtu, kwa sababu hatujui, kila mtu aji shughulishe na mambo yake mwenyewe. POMBE Rum 13:13 - Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu, si kwa ulafi na ulevi. Efe 5:18 - “Tena msilewe kwa mvinyo” 1 Kor 6:10 - “Wala wevi, wala watamanio ………… hawatauriithi ufalme wa Mungu. Luke 21:34 - “ Basi jiangalieni ……. Na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya, siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo.” UFAFANUZI Sababa inayofanya watu walewe sana ni kujiepusha na matatizo ya maisha haya. Jamii zinapuuzwa. Tabia ya mtu inamshinda na anaanza kufanya mambo ambapo baadaye anayajutia. Kama yesu alivyoelekeza, Bwana atakaporudi wakati huo, hatutakuwa katika hali nzuri ya kusimama mbele yake. Tunaweza kukataliwa. Kinywaji kimoja si kibaya, lakini kina weza kutufanya tuwe waovu na kujiingiza katika ulevi, kwa hivyo ni vyema kujiepusha. UASHERATI 1 Kor 6:18 - “Ikimbieni zinaa” Efe 5:5 - “Hakuna mwasherati wala mchafu ……… aliye na urithi katika ufalme wa kristo na Mungu”. Efe 5:33 - “Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose, kumstahi mumewe. UFAFANUZI Tamaa zetu za gono lazima zitawaliwe, sisi si kama wanyama ambao hufanya gono na mmoja na kuelekea mwengine. Lazima tusubiri hadi tutakapo olewa ndipo tufurahie pamoja na Bwana au Mke. Magonjwa yasiyotibika yanatokana na Uasherati. KWA NINI NDUGU SI SHUGHULI YANGU?. Yak 2:8 - “Lakini mkiitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa, mpende jirani yako kama nafsi yako”. Luka 10:30-37 - “Ni nani alikuwa jirani wa huyo aliyevamiwa na wezi”. Mat 25:35 - 40 - “Nilikuwa na njaa na hamkunipa chakula ……… kadiri mlivyomtendea mmoja wapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. UFAFANUZI Hii ni kazi ya kila mwamini, kujali maslahi ya ndugu yake na dada yake. Kabla hujaambia mtu mwengine kusaidia jiulize “mimi nina weza kusaidia vipi hata kama sinavyo vingi vyakujitosheleza katika hali hii?”. MASENGENYO NA LUGHA MBOVU Kut 20:7 - Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu 1 Kor 6:10 - wala ……. Watukariaji (Lugha mbovu) hawatauridhi ufalme wa Mungu. Efe 4:29 - Neno lolote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu. 1 Peter 3:10 - Kwa maana atakaye kupenda maisha, na kuona siku njema, auzuie ulimi wake, usinene mabaya na midomo yake isiseme hila. UFAFANUZI Ingawa watu wengi wanakataa kukubali imani yeyote kuhusu Mungu, wana kufuru jina lake kila siku. Udaku ni wakati tuko na uoga wa kuzungumza na mtu aliyefanya makosa. Hali hizo zote ziko na makosa sawa na haziwezi kukubaliwa kwa mkristo wa sawa. Je tunaweza kumdhania Yesu kutokuwa na huruma? Udaku unadunisha umoja wa kanisa na kuzuia washiriki kutokuwa mashahidi wa kweli wa yesu kristo. JE INAPASA MWAMINI AWE TOFAUTI 1Yoa 2:15 - 17 - Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. UFAFANUZI Si rahisi wakati wote kujua zile anasa za dunia ambazo inatupasa kufurahia. Kwa mfano, tukiangalia shughuli fulani, tunaweza kusema kwa uaminifu kwamba tutafurahia tukimchukua Yesu nasi, kwa hivyo inaonekana ni uamuzi mzuri, bora tusiwe tunajidanganya wenyewe. NATAKA NICHUKUE SEHEMU KATIKA SIASA Zab 24:1 - “Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake”. 1 Dan 4:17 - “Walio hai wapate kujua aliye juu anatawala katika ufalme wa wanadamu, tena humtawaza juu yake aliye mnyonge”. Rum 13:1-2 - “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu, na ile iliyopo imeamriwa na Mungu. UFAFANUZI Misitari hii inaonyesha, Mungu ndiye anaongoza mambo ya ulimwengu, hata katika siasa. Ikiwa tungepiga vita, tunaweza kuwa tunapigia kura mtu ambaye Mungu hakumchagua na kwa hivyo tunakuwa tunampinga Mungu? Vivyo hivyo na siasa za vyama. NATAKA LILILO NYOFU LIWE NA UGOMVI Yak 3:17 - 18 - Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani. Kut 20;13 - Usiuwe 2 Tim 2:24 - Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi NATAKA KUSOMA CHOCHOTE NITAKACHO Yak 1:21 - “Kwa hivyo wekeni mbali nanyi ubaya wote ………….pokeeni kwa unyenyekevu neno lililopandwa, ambayo inaweza kuokoa nafsi zenu”. Mat 5:28 - “Yeyote amwangaliaye mwanamke na kumtamani amezini naye katika moyo wake. UFAFANUZI Dunia inapoendelea kuwa na uovu zaidi, majaribu kupitia kwa vitabu na runinga zinaleta uzito zaidi. Aidha tunatia nguvu njia zetu za mawazo kwa kuangalia vitu ambavyo vinatia nia mbaya katika mawazo, au tujaze mawazo yetu na neno la Mungu. (Katika sehemu hii ndogo tumeangalia jinsi Mungu anavyochukulia mawazo yetu ya maumbile na jinsi yanavyo fanya kazi. Tumeona vile Mungu anataka sisi tuwe, kama vile bibilia inavyosema. Tafadhali soma habari hii na ndugu, dada na wanafunzi. Lazima tuhakikishe ya kwamba hatuamini mafundisho peke yake bali pia mwenendo uwe ni wa Kiungu. Arthur East Translated into Kiswahili by: Sammy Mutunga (Kenya)