UFUNUO. MAELEZO YA MANENO YA MSTARI KWA MSTARI. Yanatoka Biblia ya Kiingereza (A.V.), maana ndiyo pekee iliyotangulia kutafsiriwa kabla ya tafsiri ya Kiswahili. Basi, kwa Kuwa Biblia yetu ni U.V., tafsiri hii ya KITABU CHA UFUNUO kwa lugha ya Kiswahili inatoka pande zote mbili. UFUNUO MLANGO WA KWANZA. MSTARI WA KWANZA. "Ufunuo wa Yesu Kristo". Hili ndilo Jina la kweli la kitabu, na neno Ufunuo - maana yake ni kwamba jambo fulani litafumbuliwa au kuonyeshwa kwa njia ya kudhihirishwa na ya kuwa maneno ni ya Kristo yanayoweza kuonekana kwa ukweli kuwa ufunuo ni wa Kristo. "Aliopewa na Mungu." Ni Wazi, kabla Yesu hajapewa Ufunuo na Mungu, Yesu hakuujua. Hii sio kweli kwa kile wanachoamini watu wanaoamini katika Utatu, ya kwamba Yesu yupo sawa na Baba. Ila hii ni kweli kwa maneno ya Yesu aliponena kuhusu kipindi atakachorudi duniani, aliposema "habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala mwana, ila Baba" (Marko 13:32). Yesu anayajua yale tu aliyoambiwa na Baba yake. "Awaonyeshe watumwa wake." Ujumbe huu haukutumwa kwa ajili ya ulimwengu wote. Kwa maana yake maalum ulitumwa huu ujumbe kwa watumishi wake/ yaani watumwa wa sharti (Kiyunani doulos). Kwa namna ya ugumu kueleweka ndivyo maelezo yalitumwa. Madhumuni ya kitabu yalikuwa kwa ajili ya watu, ambao, kwa kujua kwa kusudi la Mungu kama lilivyo funuliwa katika vitabu vilivyo baki vya Biblia vinashika ufunguo wa kufungulia haya yaliyo jificha na kutoa maelezo zaidi ya kuonyesha lengo la Mungu kwa jambo moja moja. Hakuna mtu yeyote anayeweza kukielewesha. Hii ndiyo moja ya sababu ya Kwanini hiki kitabu kimefahamika kidogo sana kwa walimwengu kwa mapana. Kama kingetumwa na Kristo kiende kwa wafuasi wa Kristo, ni wazi kila mmoja anayetamani kuhesabiwa kuwa na wafuasi wa Kristo ataona ipo haja ya kukifahamu / kukielewa hiki kitabu. "Mambo ambayo hayana budi kutukia karibuni." (1) Unabii wa kitabu hiki ulianza kutimia karibuni baada ya kutolewa na kupewa Mtume Yohana. Historia ya unabii inazunguka toka siku za Yohana hadi kuja kwa siku yake Kristo. Hii inamaana kwamba mambo mengi ya Kitabu kwa sasa ni historia iliyokwisha pita. Huu ni msaada mkubwa, kwa sababu tunaweza kuhakikisha kwamba ufahamu wetu wa mifano iliyotumiwa ndani ya, kitabu ni sahihi, kwa kuichunguza juu ya historia. "Nayo aliyaonyesha kwa kutumia ishara." Hakikutumwa kwa namna iliyowazi bali kwa namna ya fumbo au namna ya ishara. "Kuashiria" kitu ni kuonyesha kwa njia ya alama au mfano. Kutumia ishara na mifano ni desturi ya tabia ya Mungu kufanya mawasiliano na viumbe vyake. Mfumo wa Torati ya Musa ulikuwa ni moja ya kuelezea utaratibu wa mfano, kama tunavyojifunza katika Agano Jipya. (Ona hasa kitabu cha Waebrania). Sheria aliyopewa Israeli kwa njia ya Musa ilitumika kwa lugha ya maneno ya mifano ya sura nyingi za kuja kwa Kristo na sadaka yake. Ujumbe wa manabii mara nyingi upo katika maneno ya mifano, ingawa kwa muundo wao na mzunguko ni kwa maneno halisi. Kitabu cha Ufunuo sio cha kwanza kutumia lugha ya mifano ili kuonyesha matukio. Kitabu karibu chote cha Danieli kipo katika mifano. Maono ya sanamu na jiwe (Danieli 2), maono ya wanyama wanne (Danieli 7), ni mifano miwili. Hata katika manabii walioandika wazi wazi, ipo mifano, ya mafumbo halisi. Baba anasema kwa kweli hivi katika Hosea: "Nimenena na hao manabii, nami nimeongeza maono, na kwa utumishi wa manabii nimetumia mifano"(12:10). Ikiwa mifano ambayo alinena ilitumika pasipo alama yoyote kama kwa maana yake basi matumizi yake yasingekuwa yakuelimisha, lakini alama nyingi, karibu katika masuala yote zimetolewa, kama sio mara baada ya fungu la maneno yanayosemwa, basi, inakuwa ni katika sehemu nyingine ya Biblia inayolingana. Kwa kuwa wenye bidii katika kupekua tutafanikiwa kupata maana na kwa njia ya kulinganisha. MSTARI WA TATU. "Heri asomaye" Shauku ya haja ya kujifunza hekima ya Mungu ndiyo tabia ya waabudu wote wa kweli wa Mungu. Kuongeza maarifa ya kweli ya neno ni haja ya muhimu kwa wanadamu. Kama Paulo alivyowaambia wazee wa Efeso, "Basi, ndugu nawaweka katika mikono ya Mungu na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa" (Matendo 20:32). Tunajifunza kwamba ushawishi wa kutakaswa sio mwingine zaidi ya huu wa neno la Mungu kutoka kwenye maneno ya Yesu katika sala yake: "Uwatakase kwa ile kweli: neno lako ndiyo kweli" (Yohana 17:17). Mungu ameahidi kutusaidia ili tufikie maarifa kama tukimkaribia kwa njia inayokubalika mbele zake - "Kama mtu yeyote akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye watu wote kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa" (Yakobo 1:5). (2) Kuna neno la pili ambalo pia limetafsiriwa kwa maana ile ile ya kuzimu ni JEHANAMU ambalo ni shimo la kutupia taka lililokuwepo Yerusalemu. Ilikuwa ni sehemu ya bonde la mwana wa Hinnom (kwa Kibrania "Gai Ben Hnnon" ) Haya maneno matatu yamepunguzwa na kuunganishwa ili kutoa neno ''Gehenna." "VIFUNGO VYA GIZA" ni neno limetokea mara moja, katika 2 Petro 2:4. Kwa Wayunani na Warumi palikuwa ni mahali pa kuwadhibia wapotovu, kwenye pango la chini kabisa ya dunia. Ayubu 41:32 = kilindi sehemu ya chini makao ya mamba. Wazo la kawaida ni kilindi na giza: maelezo yanayofaa kwa kile kilichotokea kwa Kora na mkutano wake "Walikwenda wazima shimoni na udongo wa juu ukawafunika" (Hesabu 16:33). MSTARI WA ISHIRINI. "Siri" Hii kwa usahihi zaidi liwe ni "fumbo". Katika kitabu cha Ufunuo, Kristo hunong'ona fumbo kwa marafiki zake ambapo ulimwengu haujui lolote. "Vinara saba vya dhahabu" Ma-eklezia yamefananishwa na vinara vya taa kwa kuwa yanatoa nuru ya injili katikati ya giza la kiroho. Neno ni nuru, na mahali ambapo likikutwa linatangazwa katika kweli, kinara cha taa kinakuwepo. Mfano umetwaliwa kutoka kwenye tawi lenye kinara cha taa katika hema ya kukutania. Mafuta kwa ajili ya kinara hiki (pasipo hayo mafuta nuru haiwezi kupatikana) yalitolewa na watu wa kawaida wa Israeli. Kuna mambo mawili ya muhimu yakuangaliwa kuhusu mafuta haya. Kwanza, Israeli wote iliwabidi watoe - haikuwa ni kazi ya wachache kufanya hivyo; pili, mafuta ya zeituni yalitakiwa yapondwe vema ili kuweza kupata mafuta safi. Huu ni mfano unaotufundisha kwamba ni wajibu wa wote kusoma neno na kutoa nuru, na ili kufanya hivyo yaonekane matokeo, kufanya kazi ngumu kwa makini ni lazima - mafuta ya zeituni inabidi yapondwe vema. "Nyota saba ... malaika" Neno dogo "malaika'' katika maandiko sio lazima kuwa linaashiria ni wa Mungu, bali pia linaweza kuwa kwa mtu wa kawaida anayekufa ambaye amewekwa kwenye nafasi ya mamlaka. Neno linaashiria "mjumbe" na katika nyakati za Mitume, walikuwepo watu (ambao kwa mfano wa alama iliyotumika waliitwa nyota kwa sababu kwa kielelezo walitoa nuru ya roho mmoja - yaani kwa vile vipawa) waliwekwa na Roho ili kutenda kazi wakiwa wajumbe wa Bwana kwa ma-eklezia. Walikuwa ni wazee wa ma-eklezia, na walikuwa ni wa pekee kwa kipindi kile, waliwekwa kwenye nafasi zao kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Kwa kweli, hakuna wazee wa namna hii katika makanisa ya leo. (15) "Funguo" Kuielewa injili mtu anapewa ufunguo, au uwezo, wa kufungua sehemu mbili kaburi na mauti. Yesu alitoa heshima hii kwa mtindo wa baadaye kwa Petro "mtume wa watu wa Tohara'', aliyekwenda na kuhubiri injili kwa Kabila Kumi na mbili za Israeli, akiwapelekea wale walioamini watoke kwenye gereza la milele la kaburi na mauti. Lakini kwakweli, ni Yesu ndiye hasa mwenye mamlaka, na maarifa, kufungua nguvu za mauti. Paulo aliwaandikia. Ndugu (1 Wakorintho 15:55-57) - "Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, mauti uchungu wako? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini Mungu ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo." "kuzimu" MAFUNZO YA BIBLIA YAHUSUYO KUZIMU. 1) Madhehebu ya watu wengi. - yanafundisha kwamba Kuzimu ni mahali ambapo "roho" za waovu huenda. Zinaongozwa na "Ibilisi" ambaye, pamoja na hao mapepo wanaadhibiwa kwa moto, n.k, kimsingi wazo hili mwanzo wake ni kutoka kwenye upagani. 2) Mafundisho ya Biblia. - "Kuzimu" katika Biblia maana yake ni "kaburi" tu, na sio vinginevyo. Waliofanya tafsiri ya Biblia hawakuwa katika kupatana kwa kupendelea kuwaelekea watu wa madhehebu ya othodoksi - yaani wanaojiita wana imani sahihi. Kwa hivi neno lili hili limetafsiriwa "kuzimu" au "kaburi" ili kufaa kwenye nia zao. 4) Mafundisho ya kanisa yahusuyo kuzimu yana upungufu; - Kwa sababu: a) Yanategemea juu ya elimu ya uongo ya kuhusu nafsi au roho haifi. b) Waovu hufa na kuoza kaburini. 4) Sifa njema ya Mungu imekataliwa. - Ikiwa Mungu ni mwenye fadhili na haki katika utaratibu wa kupatana na Maandiko, inawezekana vipi pamoja na maarifa ya kujua jambo kabla halijatokea na ni mwenye nguvu zote, aweze kuruhusu wanadamu wengi wawe hai pasipo kuwa na maisha mengine kuliko kuteswa? Utamfikiriaje mtu atesaye mbwa mshenzi kwa juma moja? 5) Kuzimu Kama neno lilivyo. Ni neno la Kiswahili kisichotumika sana kwa watu walio wengi - maana yake ni mahali pa uficho ambapo mara nyingi watu hufichwa mara wakifa. 6) Katika Agano la Kale tunasoma habari za neno hili "kuzimu" likiwa na maana 'kaburi' na ndivyo limeandikwa katika masuala yafuatayo . Zaburi 49:14,15 (mara 3) 141:7; Muhubiri 9:10; Isaya 14:15; Ezek. 32:27; Hosea 13:14. "KUZIMU'' pia imetafsiriwa "shimo" Hesabu 16:30-33 (mahali Kora na mkutano wake waliangamia); Ayubu 17:l6. Maana iliyowazi inapatikana katika Zaburi 55: 15; 86:13; Isaya 14:9; Yona 2:2. 7) Katika Agano Jipya pia hili neno limepatikana, na maana yake ipo wazi kufuatana na jinsi lilivyotumika. "Kuzimu". Matendo 2:27 (mara mbili); 31, Zaburi 16:10 imenukuliwa kuwa ni "kuzimu" = na kaburi la Kristo. Ufunuo 1:18; 6:8; 20:13,14 (na Biblia zenye kutoa maana shauri la pili ni 'Kaburi' angalia mafungu haya). Mathayo 11:23; Luka 10:15; Mathayo 16:18 na 16:23. (14) "Na wayasikiao" Katika kitabu chake 'Eureka' Daktari John Tomasi anaeleza kwamba, hili neno kwa Kiyunani linahusisha mtu ambaye 'anafahamu maarifa halisi ya jambo, au anayejua kwa usahihi au anayechunguza kwa bidii' na 'usomaji mtupu hautoshi kuitwa heri. Inahitajika kufahamu elimu bara bara. Huwezi kusoma Ufunuo na kisha ukafahamu maana yake, sio rahisi hivyo. Yatupasa kufanya kazi kwa uangalifu mkubwa ili kuhakiki maana ya KWELI ya kitabu hiki cha ajabu - ndipo uheri (baraka) itakuwa yetu. Kufanya hivi kunachukua muda na nguvu, lakini baraka hukaa juu yao wale wanaojishughulisha hivi kwa imani. SALAMU ZA YOHANA NA YESU KRISTO MISTARI 4-8. MSTARI WA NNE. "Makanisa" Neno la asili la Kiyunani lina maneno mawili: "EK", inamaanisha 'Kutoka kwa', na 'KLEISIS', limekuwa na maana "mwito au mwaliko". Kwa hivi neno eklezia ni mkusanyiko wa watu ambao wameutii mwaliko au mwito wa kutoka kati ya watu wa mataifa (yaani wasiomjua Mungu) - kama Yakobo alivyoeleza kwenye baraza lililofanyika mjini Yerusalemu, "Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake" (Matendo 15:14). "Aliyeko, na aliyekuwako, na atakayekuja." Mstari unamtaja Baba, mkuu ambaye hajaumbwa. Katika Ufunuo, Muumba Mkuu yupo mbele ya watumishi wake kwa vipindi kadhaa vya kujionyesha wazi alipojifunua na kujidhihirisha mwenyewe. Kujionyesha wazi huku kumetajwa katika Isaya 41:4 "Mimi , BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye ." Neno 'wa kwanza' katika huu mstari ni mmoja, na neno 'wa mwisho' ni uwingi. Yaani. "Wa kwanza" anatajwa Bwana Yesu ambaye ndiye anaonyesha wazi jinsi alivyo Baba; 'wa mwisho' linahusisha ndugu wa Kristo ambao watainuliwa na kufikia wawe na utukufu wake ataporudi. Mungu alijifunua katika Neno lake tangu mwanzo. Leo amejidhihirisha katika mwana. Vile vile atajidhihirisha katika jamii inayokaa pamoja ya waliokombolewa, ajapo tena mara ya pili. Jina analotoa Yeye mwenyewe (Kutoka 3:14, na 6:3) Yahweh (Yahu) linamaanisha 'Yeye atakaye kuwa' na linazungumzia lengo la Mwenyezi kujionyesha yeye mwenyewe katika wazawa wa Adamu. Yaani. Atajidhihirisha mwenyewe katikati yao. Wataonyesha nje tabia ya sifa zake n.k. "Roho Saba" Waandishi wengi tangu nyakati za mwanzo, wametaka kwa nguvu kuangalia umuhimu wa jambo linalozungumziwa la Tarakimu katika Maandiko. Yatupasa, kwa hiyo kuridhika na mambo makuu yaliyowekwa mbele, na kwa kutoa mifano michache kutoka kwenye Neno la Mungu linalo eleza kuhusu Tarakimu, kisha kuwaachia wengine matumizi mapana ya mambo hayo nao wajitafutie maelezo ya mifano yake wao wenyewe. (3) Inatubidi kwanza tuamue basi, juu ya maana ya tarakimu ya saba (yaani namba saba) katika maandiko ili kuona maana ya fungu hili la maneno. SABA. Sasa tunakuja kwenye tarakimu kubwa ya ukamilifu wa kiroho. Kwa sababu hii, ni namba ambayo inatenda kazi kwa sehemu pana katika matendo, na hasa Neno la Mungu ambalo limeletwa na Roho Mtakatifu. Yatupasa kwanza tupime maana ya neno. Kwa lugha ya Kiebrania, saba ni shevah. Asili yake ni kutoka neno Savah 'kujaa au kuridhika, kuwa na ya kutosha'. Kwa hiyo maana ya neno 'saba' limetawaliwa na asili. hii, maana, katika siku ya saba Mungu alipumzika kutoka kazi ya Uumbaji. Ilikuwa imejaa, yaani imetosha, na. Kamili, na njema na timilifu, hakuna chakuweza kuongeza au kupunguza toka hayo, bila kuharibu. Basi neno Shavath, kukoma, pumzika na Shabbath, Sabbath yaani Sabato au siku ya kustarehe ndiyo maana yake. Kwa sababu hii ni siku ya saba, inayotia chapa na ukamilifu pamoja na utimilifu ambao upo katika muungano wa jinsi saba ilivyotumika. Kwa wakati, inatuambia siku ya Sabato, na kuweka mipaka ya siku saba za wiki, ambazo kijuu-juu (haikuwa ni lengo lenyewe) kama zinavyoweza kuonekana jinsi siku zilivyo, zinatumika kwa watu wote tangu zamani za kale katika kuzikumbuka kati ya mataifa yote na kwa nyakati zote. Hizo siku zinatuambia kushika Sabato ile ya milele iliyobakia kwa watu wa Mungu katika ukamililifu wake wote ambao hautakuwa na mwisho. Kwa matendo ya kazi ya uumbaji wa Mungu, saba inakamilisha mkusanyiko wa rangi za upinde wa mvua, na kutosheleza muhutasari wa mfululizo wa matengenezo ya kupimia. Kwa kila hizi nane ni kurudia namba ya kwanza. Kama tunaweza kupokea kuwa kweli, ya kwamba saba inadokeza ukamilifu au umoja basi tunaweza kukubaliana na jambo hili kuwa inataja wakati ujao na kuutumia msingi huu kwa kutaja wakati ujao. Waefeso 4:4 tunaambiwa kwamba yupo roho mmoja tu, lakini anaonekana wazi kwa namna mbalimbali, na katika (siku za mitume) kwa njia ya watu mmoja mmoja wengi. Hivyo kuelezea jambo la 'roho mmoja' katika kuonekana wazi kwa watu wengi ndipo neno "roho saba" limetumika. Namba saba inadokeza utimilifu au umoja. Tarakimu hii inaelezea wazi kabisa 'roho mmoja' katika ukamilifu wake, kuonekana wazi katika watu wengi. Mungu amejidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu kwa njia ya roho yake, maana roho yake ni uweza wake ambao anautumia kufanya mambo. Mungu atumia roho yake kama sisi tunavyotumia umeme. Hivyo umeme unakuwa ni mtumishi wetu kwa kutuwezesha kusema na watu wengine waliombali au kazi inaweza kufanyika kufuatana na mapenzi yetu. Neno la kuvutia kuangalia: Neno 'walioko' katika Biblia ya Kiingereza ya AV. ni neno 'alioko' katika Kiyunani, hii ni wazi haileti maana katika kanuni za sarufi kwa waliotafsiri, lakini kwa kile tulichokwisha sema kwa mwanga huu, tunaweza kuona jinsi inavyoweza kuwa hivyo. Watumishi wa Mungu aliye juu, mawakili wake kwa kufanya mapenzi yake, hutumainia kupeleka yaliyo bora. Labda mtu anaweza kusema kwamba hao walikuwa ni malaika saba, mmoja mmoja akiwa msimamizi wa kila moja ya ma-eklezia, akifanya kazi kama mmoja, kutimiza mapenzi ya Mungu. (4) "Uso wake kama jua". Ni vema ikitafsiriwa "sura" au mwelekeo - au matendo yote yanayoonekana ya kundi lote. Kutoka hili tunaweza kuona kwamba katika hali ya kutokufa, Yesu na watakatifu wote kwa maneno yenyewe "watang'aa" kama alivyo Baba, anayekaa kwenye nuru isiyokaribiwa. Maneno ya malaika katika Danieli 12:3 yanathibitisha wazo hili, maana tunasoma katika Biblia ya AV. namna hii "Na walio waalimu watang'aa kama mwangaza wa anga; na wanaowageuza wengi ili watende haki kama nyota milele milele," Kwa sababu hii, sura inayong'aa yaani mwelekeo wa Kundi hili la Kristo linalo onekana kwa mfano tunajulishwa kwamba watakatifu sio tu watang'aa katika viungo vya mwili, bali nuru yao inayong'aa itatokeza ili kumulika fikra za mioyo ya watu wakiwa "waalimu": kama mwanaishi wa kuimba Zaburi alivyoimba. "Neno lako ni taa ya miguu yangu, na nuru kwa njia yangu" (119:105). MSTARI WA 17. "Nalianguka miguuni pake kama mtu aliyekufa" Akiisha kuonyeshwa maono ya utukufu unaokuja, mara hiyo Yohana akafundishwa jinsi ya kufika mahali pa utukufu. Anatimiza kifo chake na ufufuo, kama alivyofanya huyo Danieli wakati fulani (Danieli 10:8-19). MSTARI WA 18. "Amina" (Ameni) Kwenye mstari wa 18 unapoishia pananeno la kumalizia nalo ni amina. Inasikitisha kuona kuwa waliotafsiri kwa Kiswahili hili neno hawakuliweka, lakini katika Biblia ya AV. hili neno lipo. Linatoka kwenye lugha ya Kiebrania Ahmain, "uaminifu" ... Sifa yote njema ya lazima ya kuangaliwa ya kundi hili ni uaminifu na ushahidi wa kweli, na waamini wa ahadi za Mungu, zilizo kwa Kristo, ni Ndiyo, na katika Yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi (2 Kor. 1:20). Mwana wa Adamu (Watakatifu wote wa kweli) waamini wa ahadi waliofanywa imara, hili kundi limesemwa ni la mtu mwaminifu, kwa sababu hiyo mchanganyiko wake wote ni Elohai Amina, (Wenye nguvu wa Mwaminifu), wote wakiwa na msingi wa kweli hiyo, imani ambayo ikikosekana, basi, "haiwezekani kumpendeza Mungu" (Ebr. 11:6) ... Katika kipindi cha miaka elfu ya utawala wa Kristo "ajibarikie mwenyewe duniani atajibariki kwa Eloi wa Amina; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Eloi wa Amina (Wenye nguvu wa Kweli - watakatifu) na nchi mpya (dunia) (watu waliokaa vizuri katika ufalme) , kwa kuwa mambo ya kale yanakuwa yamesahaulika, na kwa sababu yamefichwa machoni pangu. Maana, tazama, naumba mbingu mpya na nchi mpya. Mbingu Mpya (serikali mpya na ukuhani wa watakatifu), maana, tazama naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha (soma Isaya 65:13-18). Hawa Eloi (Wenye nguvu), wakati huo, wametiwa pamoja katika alama ya Mwanadamu, wao ni "Amina" (Wakweli) (13) Kielelezo kama hiki kimetumika katika Mika 4:13 - "Haya, simama upure, Ee binti Sayuni; kwa maana nitafanya pembe yako kuwa chuma, na kwato zako kuwa shaba; nawe utaponda- ponda mataifa mengi." Miguu ya shaba ikiwa ni alama ya Kundi la Kristo basi, ni hali ya kuonyesha kazi za korti ya watakatifu Kristo akirejea; Mungu atakapowapa mamlaka Ya "kufanya kisasi juu ya mataifa na adhabu juu ya kabila za watu; kuwafunga wafalme wao kwa minyororo, na wakuu wao kwa pingu za chuma", kuwafanyia hukumu iliyoandikwa: hii ndiyo heshima ya watakatifu wote waliowake (Zaburi 149: 7-9). "Kana kwamba imesafishwa katika tanuru" Watakatifu wataendelea kufanya au kuendesha hukumu juu ya mataifa yote hata asiwepo wa kupinga mamlaka sahihi ya Kristo, Mfalme wa Israeli. Hivyo shughuli za kiaskari za Kristo zitasambaa pande zote, hizo zimelinganishwa na tanuru. Yeremia 25:31-33 kimetajwa kipindi hiki - "Maana BWANA anamashindano na mataifa, atateta na watu wote wenye mwili; na waovu atawatoa wauawe kwa upanga, asema BWANA. Hivi asema BWANA wa majeshi, Tazama, uovu utatoka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho za dunia. Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata wa pili; "Sauti yake kama sauti ya maji mengi" Habakuki 2:14 tunaambiwa kwamba "dunia itajawa na maarifa ya utukufu wa Bwana kama maji yaifunikavyo bahari", maana ni sauti ya watu wengi (Linganisha kielelezo hiki na kile kilichotumika katika Ufunuo 17:15). Matumizi ya alama hii mahali hapa ni kuonyesha kwamba huyo "mtu aliye kama mfano wa mwanadamu'' Kweli ni jamii ya watu waliounganishwa pamoja na kuwa mtu mmoja. MSTARI WA 16. "Upanga mkali, wenye makali kuwili" Upanga unaotoka kinywani ni alama ya kuonyesha kwamba jamii ya watu wanaoelezwa wapo tayari kwa shughuli maalum ya kiaskari. BWANA asema Musa ni mtu wa vita; na huyo askari wa vita yupo mbele yetu katika mfano huu wa Mwana wa Mtu (Adamu). Kinywa cha mfano huu mmoja, na upanga unaothibitishwa kuwa watoka ndani yake, ni mfano wa amiri jeshi mkuu. Yusufu aliwapa magari, kulingana na kinywa cha Farao kilivyosema. Neno la amri linapotoka kinywani mwa jemedari, kinaamrisha majeshi yasonge mbele, kinawasababisha wawaharibu maadui wao kwa machinjo makubwa. Neno linalotoka kinywani mwake linasababisha damu imwagike; kama vile upanga ni zana ya kutumia kuchinjia ili damu imwagike, wazo lipo sawa sawa kwa mfano ulioonyeshwa wa kuweka upanga kwa upinzani ulio kinyume na kinywa, na kuthibitisha kwamba unatoka ... Hivyo, Isaya ananena kuhusu Kundi Moja likiwa katika Alfa na Omega kuonekana kwake asema "Shina la tawi la Yese litaipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya ... na dunia itajaa maarifa ya BWANA kama maji yaifunikavyo bahari" ( 11:4) . (12) MSTARI WA SITA. "Hata milele na milele" Hapa sio milele, kama mstari unavyoonekana kudokeza, maana utawala wa Kristo hatimae utaachwa mikononi mwa Mungu, kama Paulo anavyosema: "Hapo ndipo atakapompa Mungu Baba, ufalme wake, yaani huo ni mwisho wa ufalme wa Kristo .... ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote." (1 Wakorintho 15:24,28). Kwa hiyo utawala wa Kristo utadumu kwa miaka elfu moja kama, Ufunuo 20:6 inavyotuambia. "Milele na milele" kwa lugha ya Kiyunani maana yake ni vipindi kwa vipindi. Utawala wa Kristo wa miaka elfu moja utajumuisha vipindi vidogo vingi, kama vile kipindi cha Musa kilivyogawanyika katika muda wa Waamuzi, muda wa ufalme, na kadhalika. Vipindi kwa vipindi kwa hiyo vinaashiria muhula wa utawala wa Kristo, mwishowe dhambi na mauti vitakoma. Baada ya kipindi hiki kutakuwapo na Enzi ya Mambo Mapya yatakayofanywa na Uweza wa Milele, wakati miaka 7000 itakapokuwa imepita Ufunuo 21:5. Kudumu kwa kipindi hicho, kitabu cha Ufunuo hakisemi lolote. Kinaweza kuendelea mbele au la, lakini jambo hili hatuwezi kulisema. Vyovyote itakavyokuwa, kwa hili tunahakika, kwamba dhambi, laana, na mauti havitakuwa na nafasi tena duniani, au kwenye hali ya wakaazi wake. Mzunguko wake jamii hatakuwa na uharibifu bali itakuwa na uzima. MSTARI WA SABA. "Yuaja na mawingu" Katika Malaki 4:2 Kristo amelinganishwa na Jua: "Lakini ninyi mnaolicha jina langu jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake." Huyu ni Kristo anarudi Mathayo 24:30 "Mataifa yote ya ulimwengu yataomboleza, na kumwona Mwana wa Adamu akija katika wingu la mbinguni pamoja na uweza na utukufu mkuu." Lakini mawingu ni nini? Yeremia anatupatia jibu, anatamka maangamizi ya Yerusalemu hivi: "Wakati huo itasemwa kwa watu hawa na kwa Yerusalemu, upepo wa mahali pa juu jangwani kuelekea binti ya watu wangu ... Tazama, atakuja kama mawingu na kama magari yake yatakuwa kama upepo wa kisulisuli: farasi wake ni wepesi kuliko tai. Ole wetu! Maana tumeharibiwa." Hivyo mawingu yanamaanisha mkutano mkubwa wa watu. Katika mstari huu kwa Ufunuo ndugu zake waliokombolewa, watakatifu wamelinganishwa na mawingu, jeshi lake ukipenda, wakiwa na nguvu zote za Mungu. "Kuja" kulikotajwa sio kushuka kutoka mbinguni, bali ni kuwa mbele ya wanadamu kwa ujumla. Kwanza atakuja kwa watakatifu wake, akiwa hafahamiki kwa ulimwengu; halafu, katika kundi la wateule ataonekana machoni pa mataifa yanayogombana wakati wa Har-Magedoni. (5) MSTARI WA NANE. "Mimi ni Alfa na Omega" Alfa na Omega ni herufi za kwanza na mwisho katika alfabeti kwa kiyunani. Waebrania 12:2 Yesu anaitwa ni "Mwanzilishi na mwenye kumaliza imani yetu". Kazi ya wokovu wa Mungu "ilianza" na Kristo ambaye alikuwa ni mtu wa kwanza aliyefanywa asife, na ni kwa njia ya sadaka ya Kristo kazi hiyo itakwisha, hapo wale walio waaminifu kwa kupitia karne zote watafufuliwa kutoka wafu na kutukuzwa pamoja na Kristo. DIBAJI YA YOHANA - MISTARI 9-11. MSTARI WA TISA. "Patmo " Patmo ni kisiwa kidogo asichoishi mtu kilicho pwani ya Magharibi mwa Asia ndogo. Kwa hali hiyo ya ukiwa wa sehemu hii alihamishiwa huko kwa sababu ya imani yake katika Kristo, na Mtawala wa Kirumi aliyeitwa Domotiani, ambaye imesemwa na wana histori wa kwanza alijaribu bila mafanikio kumwangamiza Yohana kwa kumtosa ndani ya mafuta yaliyokuwa yanachemka, Ni wazi kuwa kama ilikuwa hivyo, mipango yake haikufaulu! MSTARI WA KUMI "Katika Roho" Maana ya fungu hili la maneno ni wazi limeelezewa kwa mifano kidogo zaidi kwa mbele. Karibu na mfululizo wa mambo ya kwanza aliyoonyeshwa, Yohana akasikia sauti ikimweleza hivi: "Njoo huku, nami nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya haya" (Mlango wa 4:1). "Na" anasema, ''mara" nalikuwa katika roho, na tazama kiti cha enzi..." Kuwa "katika roho", basi, ni kushikwa, kufunikwa, au kukamatwa na roho (nguvu) wa Mungu kwa ajili ya kusafisha macho ili kuona maono au Ufunuo. Sasa kwa Yohana kuwa "katika Roho siku ya Bwana", ni kuwapo siku ile katika maono kwa nguvu za roho. Alikuwa akiangalia mambo haya yakitokea, kama vile alikuwapo. (6) mst. 16 "na mwaliko" -KELEUSMA - (toka neno KELEUO, kuweka katika mwendo kwa neno au amri), ni kuita, wito, au amri inayowakusanya, mwito au mwaliko wowote unaoita na kukusanya wote mara moja. (Katika vitabu vya Kiyunani mwaliko umetumika kulinganisha usawa wa makasia au mashua). Mithali 30:27 "Nzige... kwa neno la amri huenda kwa safu." Mwaliko sio lazima usikike masikioni mwa watu wote bali ni kwa wale tu waliokusudiwa; kwa suala hili wafu wanahusika. Hivyo maneno yapatikanayo kwa Yohana 5:28-29 yatatimia na wale "walio makaburini watasikia sauti yake." "Na sauti ya Malaika Mkuu" Malaika mkuu aliyetajwa katika maandiko ni Mikaeli, kwa Yuda 9. Jina linamaana "Aliye kama Mungu". Mikaeli anaonekana ndiye malaika aliyeamriwa kuongoza maisha ya taifa la Israeli. Kujua sababu yake inapatikana katika mstari kama wa Yuda 9, Danieli 10:21, 12:1. Inawezekana mno kwamba Mikaeli ndiye malaika wa mbele za BWANA (Isaya 63:9), jina linaonyesha malaika wa Kutoka 23:20-21 ambaye alifuatana na Israeli waliposafiri katika jangwa na alikutana na Yoshua nje ya ukuta wa Yeriko mwenyewe akajisema ni "mkuu wa jeshi la BWANA" Yoshua 5:14. Kristo ni mchukua jina la Mungu (Yohana 17:6,26) NAYE ameitwa "Mikaeli" katika Danieli 12:1. Kwa sasa amepewa nguvu zote na mamlaka mbinguni na duniani kujumuisha nguvu za uzima na mauti; mamlaka ya kusamehe na kuadhibu dhambi kazi aliyowahi kuifanya Mikaeli mara ikifanywa - Kutoka 23:21. Hivi huja sauti ya Malaika Mkuu. "Nao waliokwisha kufa katika Kristo watafufuliwa kwanza" Angalia mfululizo wa matukio yaliyotolewa na mtume katika kipengele hiki. 1) Watakatifu waliohai hawatawatangulia waliokufa. 2) Kristo atarudi pamoja na "mwaliko" au amri itakayowainua wafu. 3) Atakuja akiwa na mamlaka ya Malaika Mkuu ili kusamehe au kulaumu, kualika ili kushiriki au kufukuzwa. 4) Wafu wakiisha fufuliwa, atawakusanya waliohai wote kwa pamoja katika sehemu ya kufanyia hukumu. Jambo hili linakuwa limekwisha. Wale watakao onekana wanafaa kwa Kristo, sasa wanakuwa tayari kwenda kupigana na uovu uliosalia katika dunia. Ufunuo 1 mst. 15. "Miguu yake kama shaba" (11) MSTARI WA 14. "kichwa na nywele zake" Kama Paulo alivyowafundisha ndugu waliokuwepo Efeso, "Maana mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa: naye ni mwokozi wa mwili" (5 mst. 23). Yesu ni kichwa cha kundi la watakatifu, alikuwa hana dhambi, hivyo matumizi ya alama hizi ni kama zilivyotumika kwa Isaya 1:18 - "Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu" Nyekundu = dhambi / uovu. Nyeupe = uzuri, wema / haki. "Macho yake kama mwali wa moto." Jicho ni alama ya akili, ufahamu na maarifa. Wakati uliopita, malaika walitenda kazi wakiwa ni nacho ya Mwenyezi, wakiongoza maisha ya watu na mataifa kwa ajili ya faida ya mwisho ya wateule. Nebukadreza, akiisha kumuona malaika katika ndoto aliandika -"Nikaona katika njozi za kichwa changu kitandani mwangu, na tazama mlinzi, naye ni mtakatifu, alishuka kutoka mbinguni" (Danieli 4:13). Kwa enzi ijayo watakatifu hao watashika nafasi hii, kama Paulo anavyosema "Maana hakuuweka chini ya malaika ule ulimwengu ujao tunaounena" (Waebrania 2: 5). "Mwali wa moto" katika moto inazungumziwa hukumu itakayo tolewa na Kristo na watakatifu, jeshi hili kubwa, Kristo na hao watakatifu watatokea katika "mwali wa moto" na kuwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu; na wao wasio itii Injili ya Bwana wetu Yesu Kristo" (2 Wathesalonike 1:8). KUREJEA KWA KRISTO MFULULIZO WA MATUKIO Kazi ya kwanza ya Kristo itakuwa ni kuwafufua wafu wanaohusika na huo - ufufuo ndiyo utakuwa wa kwanza kufanywa kabla ya kuwakusanya wanaohusika waliohai - 1 Wathesalonike 4:14-17. 1 THES. 4: 14-17. mst. 15 "hatutawatangulia wao waliokwisha fariki dunia" - "kutangulia" kwa neno la Kiyunani ni PHTHANO - kuja au kufanya kabla, pata kufanya kwanza au kufanya au kufika kabla ya. Kwa sababu hiyo Biblia ya UV. inasema "hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti". Paulo anawafariji Wathesalonike kwa kufahamu kwamba waamini waliokufa ndio watakuwa wa kwanza kujua kwamba Bwana yupo duniani, kwa njia ya kufufuliwa kwao kupata uzima. (10) "Siku ya Bwana" Anatuambia kwamba kabla ya maono kuanza, alikuwa "katika roho siku ya Bwana". Watu wengine wanalichukulia jambo hili kwa maana ya kuwa alipokea maono siku ya Jumapili. Kwa hili kuna vipingamizi mbalimbali. Kwanza Jumapili haijaitwa kamwe siku ya Bwana katika Maandiko. Hata kwa Musa, Sabato ilikuwa ni "siku ya saba" (Jumamosi) - sio siku ya Bwana. Matumizi pekee tunayopata kuhusiana na "siku ya Bwana" ilivyowekwa ni kuelezea siku ya Bwana iliyopangwa ya kuja au kuonekana wazi kwa namna moja au nyingine, hasa siku iliyopangwa ya kuhukumu walimwengu kwa haki kwa njia ya Kristo. Hili fungu la maneno "siku ya Bwana" kwa kawaida limeelezewa hivi daima. Mfano mmojawapo uliotumika mara kwa mara maneno yapatikana kwa 1 Wathesalonike 5:2- "Maana ninyi wenyewe mnajua, kwa usahihi ya kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwivi usiku." "Nalisikia sauti kuu nyuma yangu." Sauti ilimfanya ageuke na kutazama nyuma yake, na kile alichokiona alipofanya hivyo yalikuwa yanatajwa matukio yanayoitangulia "siku ya Bwana." Aliiona historia ikijionyesha mbele yake. "Sauti kama ya baragumu (tarumbeta)" Katika Hesabu mlango wa kumi tunajifunza kwamba chini ya Torati ya Musa, baragumu ilitumika kwa ajili ya kuwakusanya watu pamoja. Hapa kwa Ufunuo inazungumziwa kuhusu kuwakusanya watu pamoja kwa hukumu kabla ya kudhihirika siku kuu ya Bwana hapo mataifa yatakapo tiishwa chini ya Mwana wa Mungu. Kuhusiana na hili Paulo aliandika, "Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu: nao waliokufa katika Kristo hao watafufuliwa kwanza" (1 Wathesalonike 4: 16). MSTARI WA KUMI NA MOJA Hapa ni vema kutambua kwamba ingawa ujumbe ulitumwa kwa ma-eklezia saba yalikuwapo wakati ule ule wa Yohana, ulikusudiwa matumizi yake yawe ni kwa ulimwengu wote kwa jinsi watakatifu wanavyohusika. Haukuwa kwa ajili yao tu: ulikuwa ni kwa ajili ya marafiki wote wa Kristo. Twajifunza kutoka ujumbe: "Yeye aliye na masikio ya kusikia na asikie." Pia tunajifunza kutoka huu kwamba Yesu anatuma ujumbe, kwa kutazama uwezekano wa wengine kutokuwa na masikio ya kusikia. Ni wazi upunguzwaji wa wasio wa muhimu mara nyingi unaweza kuwa ni wa matendo ya thamani. Tunaweza kukosa kwa kudhoofika na hata kubadilika kutoka fikra zilizo sahihi kwa utepetevu mkubwa yaani kutokuwa na moyo wa kupenda na haja ya kuvutia iliyoonyeshwa kuelekea mambo makubwa yaliyohusishwa ndani ya Ufunuo. Ujumbe ulitumwa kwa ma-eklezia saba kwa kuwa saba ni namba kamili. Ujumbe unaonyesha hali zote ambazo ma-eklezia yanajikuta yamo, sehemu yoyote, na. wakati wowote. (7) MAONO YA WATU WENGI KATIKA KRISTO - MISTARI 12 - 20. MSTARI WA KUMI NA TATU. Yohana alimwona mtu "mfano wa Mwanadamu." Huyu mwanadamu ni nani? Marko 13 mst. 32 tunapewa jibu. Yesu anasema mfano wake mwenyewe. ''Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walioko mbinguni... Maana mwanadamu (Yesu) ni kana kwamba mtu anasafiri", Kristo anajiita mwenyewe mwanadamu; kwa hivyo mwanadamu ni Kristo. Alikuwa ni mzawa wa Adamu kwa Mariamu mama yake. Jina Mwanadamu, linatukumbusha kwamba Yesu alijaribiwa kama sisi; ili kutenda dhambi. Maono hayakuwa ni ya Kristo mwenyewe, ingawa Kristo ni sehemu yake, bali mtu "kama" yeye, kile Yohana alichoona ilikuwa ni watu wengi katika Kristo. Utukufu aliouonyesha Kristo wakati wa utumishi wake alipokuwa hapa duniani, ulikuwamo kwa kuonyesha yale yaliyo "kiini cha tabia ya sifa ya uadilifu" uliowekwa kwa jina la BWANA Mungu - na katika kuonyesha kwa uweza wa Roho, kwa nguvu hiyo alifanya matendo makuu ya ajabu, miujiza ya neema yake. Nusu ya utukufu (sifa kuu) ilionekana kwa njia ya tabia alipokuwa mwenye kuteseka. Mateso yametajwa na nabii Isaya, mlango wa 53 - mahali ambapo "uvumilivu", saburi, kutokutoa malalamiko, na upole wa mwokozi umeonyeshwa kwa picha. Paulo aliwaombea wanao amini ya kuwa wawe "wamejaa na tunda la haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu" (Wafilipi 1:11). Na kwa bidii anawaagiza juu yao wavae utu mpya, ulioumbwa kwa mfano wa Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. (Waefeso 4:24). "Neno la Kristo nalikae kwa wingi kwa hekima yote" (Wakolosai 3:16). Kwa 1 Yohana 3:2 unasema "tunajua ya kuwa (Yesu) atakapodhihirika, tutafanana naye" WENYE haki watapokea kutokufa. Miili yao itabadilika kwa kitambo kidogo kwa uweza wa roho wa Mungu nao watapewa heshima ya kutawala katika ufalme. (Wafilipi 3: 20-21; Yohana waraka wa kwanza 3:2; Ufunuo 5:9,10). Basi maono ni ya uwingi wa watu wenye haki wakiwa kama Kristo; wana tabia yenye sifa alizokuwa nazo Kristo. Bwana Yesu Kristo ndiye kichwa cha kundi hili la watu, kama Paulo alivyotaja kwa waraka wa Wakolosai 1:18) - "Ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha eklezia, naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote." Kundi hili lenye utukufu la Kristo limekuzwa toka eklezia na hapa limeonyeshwa kuwa lipo ''katikati" ya makanisa (Kinara cha taa = makanisa ona mstari wa 20). Tunakumbushwa kwamba wote wanadai kuwa ni jumuia ya eklezia lakini sio lazima kuwa washirika wote wanakuwa ni mwili mmoja wa kweli wa Kristo. Sio Kila mtu anayekwenda kanisani, juma kwa juma yaani kila Jumapili, wawe ni watu wema, na kutii amri zote za Mungu. (8) "Amevaa vazi" Kuwa uchi ni mfano wa hali ya dhambi. Adamu na Eva walitenda dhambi. Dhambi yao ilifunikwa kwa kuvikwa ngozi za wanyama (Mw.3). Mtu alihitaji kuvikwa mara moja alipokosa. Nguo zinatukumbusha dhambi yetu. Uchi ni mfano wa dhambi, hivyo basi tunajifunza ya kwamba yatupasa kwa njia ya mfano kufunikwa na vazi lile lililonenwa na Isaya 61:10 "Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu". Uchi wa Adamu na Eva ulifunikwa kwa ngozi ya mnyama aliyechinjwa, akionyesha mbele kwa Kristo ambaye tunamvaa katika ubatizo. Israeli walifundishwa haja ya kufunikwa katika Siku ya Upatanisho, au kwa usahihi zaidi, Siku ya Kufunikwa, siku ambayo dhambi zao zilifichwa, au kufunikwa ili zisionekane kwa kuzisamehe. Tunapo "mvaa" Kristo, tunavaa vazi lake. Yatupasa tusiwe na doa, na kama tukifanya hivyo, tutaruhusiwa kuvaa nguo ya kitani kwenye Enzi ijayo - vazi la haki na kutokufa. Kwa kufuatana na nafasi za waliobahatika, wana wa Haruni walivaa nguo maalum - nguo ya kitani, mishipi, vilemba, kofia na suruali, zote za kitani (Kutoka 28:40-43; 39:27-29) - na vyote vilikuwa vya sehemu nyingi zaidi na mwanzo wake ukiwa na sherehe ya maana kupita kukusanyika kwa Walawi (Law.8). Hii ilikuwa hakika hata kwa baba yao Haruni. Alivaa mavazi maalum ya Ukuhani mkuu mbali ya koti, mshipi na suruali zilizovaliwa na wanawe; ambapo walivaa kofia lakini yeye alivaa kilemba; mafuta yalitumiwa kuwapaka vichwani wanawe lakini sio na mafuta mengine ya kutiwa kama kwa suala lake (Law. 10:7 na Law. 21:12; Zaburi 133). Tena matakwa ya utakatifu yalisadikisha mkazo wake katika suala lake; nyuzi za kitani kwenye kilema palikuwa na bamba, na taji takatifu (Kut.29:6), na yaliwekwa maneno ya kuchorwa, ''MTAKATIFU KWA BWANA" (Kut. 28: 36-37). Rangi nyeupe ni alama usafi, haki ya wema, na kitani ni nyeupe, na kitani haimfanyi mtu atoke jasho, kutoa jasho ni kuonyesha kuwa mtu ni mfu, chakula kimetumika, hivyo kitani inaweza pia kuonekana kama alama ya kutokufa. Imekuwa kwamba nguo ya kitani hapa ndiyo maana yake. "Kufungwa mshipi wa dhahabu" Dhahabu ni alama ya imani iliyojaribiwa, kwa mtazamo wa anachosema Petro katika 1 Petro 1:7, "Kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo inathamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu, na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.". Kwa Yohana 13:14, kabla Yesu hajaanza kuwaosha miguu wafuasi wake, tunasoma kwamba "akajifunga mwenyewe" kwa matayarisho ya kitendo. Mishipi wa dhahabu kuzunguka mwili wa watu wengi katika Kristo ni imani, iliyothibitishwa kwa matendo, na kujaribiwa katika moto wa machungu. Jeshi hili lipo tayari kwa vita. (9)