_____________________ Bible Yaonyesha kuwa ni Uwezo wa Mungu Bible teaching about the Power of God _____________________ BIBLIA YAONYESHA KUWA NI UWEZO WA MUNGU Ninani au Roho Mtakatifu ni nini? Ni sehemu gani Roho Mtakatifu anashughulika katika kazi ya Mungu? Haya ni maswali ya maana na ya ndani. Yatupasa tutengeneze ulizo letu huku tukiwa wanyenyekevu kwa sababu hii tukijua tunachunguza mambo ya Mungu. Uchunguzi wetu wote utakuwa hauna maana ikiwa Mungu hakututia moyo kutafuta kwa kadri tuwezavyo kwa njia ya Biblia, ambayo ni Neno Lake lenye maarifa mengi. Hebu basi na tuvumbue kile alichotuambia kuhusu Roho Wake. Maelezo kadhaa yanapatikana ndani ya Biblia ambayo yanaonyesha Roho huyu Mtakatifu na yaliyowekwa ni: "Roho ya (wa) Mungu" (Mwanzo 1:2; Mathayo 3:16) "Roho ya Bwana" (Isaya 11:2; Matendo 8:39) "Roho yako mwema" (Nehemia 9:20) "Roho ya Bwana Mungu" (Isaya 61:1) "Roho yake Mtakatifu" (Isaya 63:10-11) "Roho ya Baba yenu" (Mathayo 10:20) "Roho" (Yohana 1:32) "Roho Mtakatifu wa Mungu" (Waefeso 4:40) "Uweza wa Bwana" (Luka 5:17) Ieleweke kuwa Agano la Kale neno "ya" limetumika mara nyingi kuliko katika Agano Jipya, ambapo neno "wa" ndilo linapatikana. Maneno Mungu Roho Mtakatifu hayapatikani katika Biblia. Walakini, kuna muunganiko mkubwa sana ulio dhahiri kati ya Mungu na Roho Mtakatifu. Kweli, Roho amesemwa ni wa Mungu, wa "BWANA", "wa "Bwana Mungu", na "Baba yenu". Kwa maelezo ya orodha iliyotolewa hapo juu ndivyo yanaonyesha kuwa Roho ni ya (wa) Mungu mwenyewe. Kama hii orodha ndiyo tutaifanya iwe ni mwanzo wa safari yetu ndani ya Maandiko, basi tutakuta maendeleo hayatakuwa na shida kwetu. Tazama kwenye maelezo yafuatayo yahusuyo uumbaji: "Hapo mwanzo Mungu aliziiumba mbingu na nchi … na Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji." (Mwanzo 1:1,2). "BWANA Mungu akamfanya mtu wa mavumbi ya ardhi, akampulizia pumzi ya uhai puani mwake; naye mtu akawa nafsi hai." (Mwanzo 2:7). (1) "Roho ya Mungu imeniumba, na pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai." (Ayubu. 33:4). "Ameiumba dunia kwa uweza wake … Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake … kwa ufahamu wake amezitandika mbingu." (Yeremia 10:12; 51:15). UWEZA WA MUNGU KATIKA UUBAJI Huu ni baadhi ya ushuhuda mwingi katika Biblia kuhusiana na kazi ya Mungu kwa uumbaji. Yeye peke yake kwa hekima Yake aliubuni mpango wa ajabu, nao ulitimizwa kwa uweza wake Mwenyezi, Roho yake. Mungu ni Roho (Yohana 4:24, U.V), na lolote afanyalo ni kwa Roho yake. Ni kwa jinsi gani uumbaji unadumu kwa kuwepo? Je dunia ni kama saa kubwa, iliyozungukwa na. Mwenyezi na kuiacha iende mbio za polepole kushuka? Au BWANA Mungu bado yuajishughulisha kuhusiana na kile alichokifanya? Biblia katika sehemu zote za maandishi inatuambia kuwa uumbaji unathibitishwa na Mungu naye yupo kila mahali popote na ndani ya yote aliyoyafanya. Pasipo Yeye hakuna kitu kitakachoweza kuishi au kuendelea kuishi: "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote .... anawapa wote uzima na pumzi ,... ndani yake yeye tuishi, tunakwenda, na kuwa na uhai wetu." (Matendo 17:24-28) "Kama akimwekea mtu moyo wake, akijikusanyia pumzi na roho yake; wenye mwili wote wataangamia pamoja, nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi." (Ayubu 34:14-15) "Mtafuteni yeye afanyaye nyota saba na Orioni, na kukigeuza kivuli cha mauti kuwa asubuhi, na kuufanya mchana kuwa giza kwa usiku; yeye ayaitaye maji ya bahari, na kumwaga juu ya uso wa nchi; BWANA ndilo jina lake" (Amosi 5:8). Mungu ameenea katika viumbe vyake. Vyote vinafanya kazi kwa sababu ya busara ya Roho ya kuvihifadhi, nguvu za Mungu zikitimiza kusudi lake lenye fadhili. * Hatutajishughulisha hapa na mafunzo yanayohusiana na Uungu. Jambo hili litafaa kutendewa vyema kwa kupatikana katika Kitabu kinachoitwa Yesu – ni Mungu Mwana au Mwana wa Mungu? (ona nyuma ya jarada la kitaba hiki kidogo). (2) Roho sio kwamba ni kitu “kilichojitenga" au kuwa ni mtu "mwingine. Ni nguvu za Mungu mwenyewe ambazo ni angavu, daima zinajaa kutoka kwake, kwa nguvu hizi, kwa kuwepo kwake "kila mahali" anatimiza atakalo. Roho ni yake mwenyewe kwa kuwa ni Mimgu mwenyewe: sio kitu kilicho pekee na kwa maana ya kusema ni mtu mwingine ndani ya Uungu. WAANDISHI WALIONGOZWA NA ROHO YA MUNGU Maandiko yatufundisha kwamba Mungu anakusudi la ukombozi kwa watu, na dunia ambamo wanaishi. Ukombozi utakuja si kwa kushangaza, maana tunajifunza kutoka ufunuo wa mapenzi yake ya kwamba yanatoka kwa Mungu mwenyewe kwa njia ya Roho yake mwenyewe: "Tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo mkiliangalia ...... Maana unabii hakuna katika Maandiko upatao kufasiriwa kama mtu fulani apendavyo, maana haukuletwa popote kwa mapenzi ya mwana-damu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu." (2 Petro 1:19-21, U.V.) Ujumbe ni rahisi kuuelewa. Mungu ameyafunua mapenzi yake yasiyo na kosa kwa njia ya Roho Mtakatifu kupitia kwa watu aliowachagua walioitwa manabii. Na ilikuwa ni kwa njia hii hata Maandiko yameweza kuwapo. Wale walioandika hao waliongozwa na Roho ya Mungu na kile walichokiweka juu ya karatasi kwenye kurasa ilikuwa ni uongozi wa Mungu. Kwa sababu hii, ingawa manabii wote walioandika wamelala makaburini, sisi tunalo Neno zima la kutegemewa ambalo Mungu aliongoza liandikwe, nalo limo mikononi mwetu. Mpaka sasa Mungu asema nasi ndani ya kitabu kama vile alivyosema zamani kwa njia ya vinywa vya wale manabii: "Maandiko matakatifu yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa njia ya imani iliyo kwa Kristo Yesu. Maandiko yote matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu .... ili mtu anayemtumikia Mungu awe mkamilifu, na tayari kabisa kufanya kila tendo jema." (2 Timotheo 3:15-17. Biblia Habari Njema) Neno la Mungu lililo tolewa kwa njia hii linatuletea nia ya Mungu na zote sifa zilizo kiini kilicho oanisha na jina lake Takatifu. Kuupinga ujumbe na amri ya Meno la Mungu ni kumpinga Mungu mwenyewe. Kweli, ni kumpinga Roho wa Mungu kwa kila maana ya neno hilo, ukijumuisha maana hiyo pana ambayo tunaidokeza tunapozungumza, kwa mfano, wa "roho" ya mapatano. Hivi ndivyo Biblia yauelezea upinzani wa wana wa Israeli kwa neno la Mungu ambalo lilipitishwa kwa manabii: (3) "Lakini miaka mingi ukachukuliana nao, nawe ukawashuhudia kwa roho yako kwa vinywa vya manabii wako; wao wasitake kusikiliza ...."(Nehemia 9:30) "Katika mateso yao yote yeye (Mungu) aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake aliwakomboa mwenyewe ... akawachukua siku zote za kale' Lakini wakaasi, wakamhuzanisha Roho yake Mtakatifu."(Isaya 63:9-10) "Enyi wenye shingo ngumu ... siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo."(Matendo 7:51) Kwa uwazi, haikuwa ni nguvu ta ya Mungu ilikuwa inaonekana ambayo waliiasi na kuipinga. Waliupinga upendo unaokomboa na wenye haki ya Mungu iwe kwa manabii Wake au kwa kipindi kilichofuata cha Kristo. Wao wenyewe walikataa kujinyenyekeza (kujishusha) na Kumtumikia. Hii ilikuwa ni roho mbaya ya mwanadamu ikishindana na Roho Mtakatifu wa Mungu. MIUJIZA NA AJABU Kulikuwa na nyakati, kwa kweli, asili ya uweza wenye nguvu ya Mungu katika Roho ulipoonekana dhahiri. Kutoka kipindi hadi kipindi Mungu aliingilia kati kwa uwazi na kufanya miujiza ya ajabu kati ya watu. Mwelekeo huu wa Roho iwe katika wema au kwa ukali hauna makosa: "Baba zetu katika Misri hawakufikiri matendo yako mengi ya ajabu; hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; wakaasi penye bahari, bahari ya Shamu. Lakini aliwaokoa kwa ajili ya jina lake, ili audhihirishe Uweza wake mkuu." (Zaburi 106:7-8) "Uweza wa Bwana ulikuwapo apate kuponya. Na tazama, wakaja watu wamemchukua kitandani mtu mwenye kupooza ... Akamwambia mwenye ugonjwa wa kupooza ... Inuka, jitwike kitanda chako, na aende nyumbani kwako. Mara hiyo akasimama ..." (Luka 5:17-25) "Kwa ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu wa Mungu hata ikawa tangu Yerusalemu... " (Warumi 15:19) (4) Miujiza ya Bwana Yesu Kristo kwa kutuliza dhoruba ya mawimbi ya Galilaya, muujiza wa kukamata samaki, kwa kulisha watu maelfu kwa mara moja, na kwa uponyaji wa kila aina, kwa nguvu ilikuwa ni kukumbusha matendo mbalimbali ya Mungu katika Agano la Kale. Ilikuwa kana kwamba matendo ya Roho wa Mungu yalielekezwa duniani, kama hayajawahi kuonekana, katika utu wa Bwana Yesu. Huu ulikuwa sawa kweli kwa maneno aliyosema. Maneno yake na miujiza kwa maajabu. yalioana pamoja. Ilikuwa ni kana kwamba Bwana Mungu alileta karibu kwa mwanadamu kila kitu kwa njia ya Mwana wake alichosema kwa huruma zaidi na kwa namna ya uweza. Roho alitimiza mapenzi ya Mungu zamani, wakati mwingine kwa ishara na maajabu, ya kuogofya na yenye neema; kwa maneno au kwa maono au kwa ndoto; bali sasa, katika Kristo, BWANA Mungu ametoa ufunuo wa ajabu usiosahaulika, Mwana amejaa mng’ao wote wa Neno la Mungu na katika nafsi yake mwenyewe alirudisha yote yale aliyosema, na alivyogawiwa uweza huu na mamlaka kama kuongeza neema ya Keno kwa matendo ya kuokoa ya wema zaidi usiopimika. Katika yote haya nia na mapenzi ya Mungu yalidhihirika kwa njia ya kuwakomboa wenye haja, na kuwapa tumaini wale walioinamishwa kwenda chini na dhambi, au walioonewa na mapokeo yaliyofanywa na mwanadamu na vizuizi vilivyofanya maisha kuwa magumu kwa mtu wa kawaida katika siku za Yesu. Maneno ya Kristo yalitoa faraja kwa wakiwa na wenye kukata tamaa. Matendo yake yalileta sifa isiyo lazimishwa kwenye midomo yao. Kifo chake alichojitolea msalabani kilileta msamaha wa kutoka dhambi zao. Mungu alikwisha sema kwa njia zote za maelekeo ya maisha ya Kristo. Kisha pale Kalvari na alivyo lazwa katika kaburi mle bustanini, wakati yote yalionekana kuwa yamepotea BWANA aliondoka tena kwa Roho yake: “Kwa uweza wake Mungu alimfufua Bwana kutoka wafu." (1 Wakorintho 6:14, N.I.V.) Hivyo uweza wa Mungu ulitenda kazi kwa upendo na haki, kwa kuliendea kaburi lililokuwa kimya na kumtoa Mwanae wa pekee ili kupata utukufu na uzima usio na mwisho: "Mungu ... akamfufua kutoka wafu, na akampa utukufu." (1 Petro 1:21) "Mwanawe Yesu Kristo Bwana wetu wa ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili, na kudhihirishwa kwa uweza kuwa Mwana wa Mungu, kwa jinsi ya roho ya utakatifu, na kwa ufufuo wa kutoka wafu." (Warumi 1:3-4) (5) "Kwa ukuu wa uweza wake, alioutenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume ... amevitia vitu vyote chini ya miguu yake." (Waefeso 1:19-22) "Kristo yuko mbinguni (alikokwenda), naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; malaika na enzi na nguvu zimewekwa chini yake." (1 Petro 3:22) UWEZA WA MUNGU KATIKA KUFUFUA WAFU Kuinuliwa na kuwa na cheo kilicho bora sana Kristo ndiyo chanzo cha furaha kubwa na kutukuzwa kwa wanaoamini. Kristo ni Mwokozi na Kristo ni Bwana. Tena, Mungu alimfufua Mwanawe toka wafu kwa uweza wa Roho yake na aliendeleza mapenzi yake na azimio katika yeye baada ya kufufuliwa: "Katika habari ya mambo yote aliyoanza Yesu kufanya na kufundisha, hata siku ile alipochakuliwa juu, alipokuwa amewaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua." (Matendo ya mitume 1:1,2) "Huyo Yesu, Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake. Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu ..." (Matendo 2:32-33) Kupandishwa kwa Kristo katika daraja lililo bora kumewezeshwa na kuidhinishwa na Roho ya Mungu. Maisha ambayo Yesu anaishi kwa sasa ni uzima wa Roho; kwa kuwa "amehuishwa na Roho" (1 Petro 3:18) na kwahiyo, sasa, katika maana ya alivyotajwa, yuaishi kwa njia ya Roho. Utu wake wa kufa umevalishwa kutokufa. Ulimezwa na uzima. Zaidi ya hayo, Bwana Yesu kwa sasa "ni roho yenye kuhuisha" (1 Wakorintho 15:45 U.V.): "Maana kama Baba awafufuavyo wafu na kuwahuisha, vivyo hivyo na Mwana awahuisha wale awatakao."(Yohana 5:21) Bwana Yesu Kristo kwa sasa yeye ndiye chanzo cha uzima wa milele kwa wale wote wanaomwamini katika ukweli. Yeye ni "mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi" (Warumi 8:29), ndiye atakayeleta "wana wengi waufikilie utukufu", naye amekuwa ndiye "chanzo cha wokovu wa milele kwa wale wote wanao mtii" (soma Waebrania 2:10 U.V. na Waebrania 5:9 B.H.N Kiswahili cha kisasa). (6) Ni vigumu kupima zaidi umaana wa msimamo wa sasa na kazi ya Bwana Yesu Kristo akiwa Mwana wa Mungu. Mungu amemfanya asife tena na amepewa nguvu ya kutoa uzima usiopatikana na mauti kwa wengine. Huu ni ujumbe wenye kutukuzwa wa Agano Jipya. Katika Kristo sio tu ipo ahadi ya uzima wa milele; ndiye hasa mtangulizi, amekwisha wasili, na yeye mwenyewe amekwisha fikia hali ya kutokufa. Hii ni ahadi ya uhakika isiyo tikisika kwa wote wanaomkaribia Mungu kwa njia yake. Kwa kweli Kristo ni mwokozi tuliyepewa na Mungu. Huyu Kristo ndiye kilele cha kazi ya BWANA Mungu kwa njia ya Roho wake Mtakatifu: manabii watakatifu walitabiri zamani na utimilifu ulikuja katika kuzaliwa, maisha aliyoishi, kwa kifo, ufufuo na kupanda katika daraja Yesu Kristo Bwana wetu. MITUME WALITIWA UWEZA KWA NJIA YA ROHO Kwa sababu hiyo, Injili sasa imehubiriwa "kwa jina lake", na ujumbe unaposonga mbele wenye wokovu duniani kwa sasa upo katika matunzo yake. Mitume walitumwa kuutangaza ujumbe ambao ni habari njema. Na moja kwa moja waliwezeshwa na Roho wa Mungu katika Kristo ili kwamba maneno waliyo nena na maajabu waliyo onyesha ilikuwa ni sehemu. ya lazima kuikamilisha ya ujumbe mmoja wa Mungu uliodhihirishwa katika Yesu: "Akiisha kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu, hiki mnachokiona sasa na kukisikia ... Na kila mtu akaingiwa na hofu: ajabu nyingi na ishara zilizofanywa na mitume." (Matendo 2:33,43) "Kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti ... wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote; kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo." (Matendo 4:10,12) Kuupinga ujumbe wa kazi ya Kristo na mitume ilikuwa ni kumpinga Kristo; na yeyote aliyezuia alikuwa anampinga Roho Mtakatifu kama walivyofanya walio wa mfano wao katika Agano la Kale (Isaya 63:10 na Matendo 7:51). Mamlaka za Kiyahudi zilizo zuia maendeleo ya Injili "zilikuwa kinyume na Bwana na pia kinyume na Kristo wake" (Matendo ya mitume 4:26). Sauli wa Tarso, ambaye baadaye akawa mtume Paulo mpendwa, kwa ukali aliwatesa waumini wa kwanza lakini, aliposimamishwa na kuulizwa na Yesu alipokuwa anakwenda Dameski, aliulizwa na kristo: "Kwa nini unanitesa?" (Matendo 9:4). (7) NENO NA ROHO Wale, ambao kwa upande mwingine, walioamini waliutii ujumbe wa Roho na kwa hivyo ni kwa Bwana Yesu Kristo na Baba yake. Neno la Roho lilithibitisha mioyo yao kuwa na makosa, na hivyo kuleta toba na tumaini la uzima wa milele. Hasa katika Agano Jipya, ujumbe huu, habari njema za "mambo yanayohusu. Ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo" (Matendo 8:12), ni wazi wazi linahusu Neno na Roho: "Lile Keno li karibu nawe; katika kinywa chako na moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tunalolihubiri ... Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo (Warumi 10:8,17) "Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu ... Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia ufalme wa Mungu." (Yohana 3:3,5) "Mmezaliwa mara ya pili si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele ... Na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu," (1 Petro 1:23-25) "Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu, maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima." (Yohana 6:63) "Pokeeni kwa upole neno lile lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu." (Yakobo 1:18-22) "Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamuwezi kufanya mnayoyataka ... Msidanganyike, Mungu hazihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele." (Wagalatia 5:16-17; 6:7-8) "Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu." (Wagalatia 5:22) (8) UJUMBE WA ROHO Kutoka Maandiko haya ni dhahiri kwamba njia ya wokovu Katika Kristo ni njia ya Roho. M njia ya Mungu. Wokovu watoka kwa Mungu. Kusudi lote na mpango wa huo wokovu na utimizo wake ni wa Mungu. Mwanadamu kwa pamoja alikuwa hana uwezo wa kufanya chochote na asiye na matunda ya kuzaa. Hana wema wowote ndani yake. Mungu amekuwa ni mwenye huruma na fadhili kwa kumtoa Kristo. Mapenzi ya Mungu yameletwa katika kazi kwa njia ya Roho yake. Hakuna lingine lililodhahiri kuliko Keno la Mungu ambalo ni ujumbe wa Roho: "Mwenye masikio ya kusikia, na asikie." (Mathayo 13:43) "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa." (Ufunuo 2:7) Ujumbe wa wokovu ni uweza wa Mungu (Warumi 1:16) ambao unawaleta wanadamu katika kupatana na nia ya Mungu, Roho ya Mungu. Kwa ukamili nguvu mpya inaingia katika maisha yake hapo kwa hiari anapopokea Neno la Mungu. Unyenyekevu katika kupokea Keno kunapelekea kuamini. Neno linatia nuru fikra na fahamu, na kuanza mfuatano wa kubadilika kunakoleta toba na kisha kuongoka. Neno la Mungu linapokuwa limeandikwa ndani ya moyo wa mtu kwa namna hii kwa kuamini ujumbe ulioandikwa katika Biblia kitendo hiki kimesemwa kawa: "imeandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama." (2 Wakorintho 3:3) Kutokea huku ni kwa kustaajabisha. Hakika ni kazi ya Roho ya Mungu imeletwa kukubalika kwa uaminifu habari njema za Injili. Mwanzoni mwa historia ya mwanadamu fikra za Eva zilichafuliwa kutokana na maneno ya nyoka. Yalikuwa ni maneno ambayo yalitokeza dhambi na mauti. Njia ya Mungu ipo kumfunza huyu mwanadamu namna mpya ya kuwaza. Akili inabidi ikombolewe toka ubinadamu tupu., fikra za mwili. Fikra za Mungu inabidi ziingie mahali pa zile za mwanadamu. "Msiige mitindo ya dunia hii, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikra zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu, kutambua jambo lililo Jema, linalompendeza na kamilifu." (Warumi 12:2 B.H.N) Neno la Injili limepangwa kwa ajili ya njia hii. Ni mzao ambao utazaa tunda la roho. Mtu ambaye analiingiza ndani ya moyo wake atachukuliwa juu katika maji yaliyo jaa ya upendo wa Mungu unaookoa katika kazi ya Bwana Yesu Kristo. (9) Sehemu ya tendo hili la Mungu anapoendelea kusafisha ni kutuhakikushia matunzo ya Mungu na ya Kristo kwa wale wanaoamini na wanatafuta kutii. Haya yote yanahusu Injili; imepangwa kutuleta kwa Mungu kwa njia ya Kristo: "Wamjiao Mungu kwa yeye (Yesu)." (Waebrania 7:19,25) "Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi." (Yakobo 4:8) Tumehakikishiwa matunzo ya Mungu na kivuli cha Kristo wakati wa maisha yetu ya kusafiri tunapoisubiri siku ya Ufalme wa Mungu. MATUNZO YA MUNGU KWA NJIA YA MALAIKA Moja ya njia ambayo Mungu awatunza watoto wake ni kwa njia ya malaika: "Je! hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?" (Waebrania 1:14) "Malaika wa BWANA hufanya kituo akiwazungukia wamchao na kuwaokoa." (Zaburi 34:7) Tunaweza kwa hiyo, hasa tunapokuwa wafuasi wa Kristo, kuthibitishiwa kuwa wale walioupande wetu ni wa maana sana kuliko chochote kilicholengwa dhidi yetu katika maisha haya. Labda baraka kubwa kuliko zote tuliyopewa na Injili katika maisha haya ni ushirika pamoja na Mungu kwa njia ya Bwana Yesu kwa sala, Huu ni mstari wa maisha. Mungu asikia sala. Kwa njia ya upatanishi wa Kristo kwa sasa alivyo mbinguni haja zetu na sifa vyote vinapelekwa kwa Mungu na kujibiwa kufuatana na kilicho chema zaidi kwa ajili yetu katika mapenzi ya Mungu: "Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea. Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?" (Warumi 8:34-35) "Tunaye mwombezi kwa Baba, Yesu Kristo mwenye haki." (1 Yohana 2:1-2 U.V.) "Kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai siku zote ili awaombee." (Waebrania 7:25) (10) Tuzo isiyopimika ya sala imetolewa kwetu kwa njia ya wema wa Mungu kwa Roho yake. Sauti yetu ndogo zaidi ya kunong’ona, au haja zetu tusizozitamka, zinamfikia kwa njia ya Yesu, tunapokuwa tunamhusu kwa kweli; Mungu hutega sikio lake zuri ili kusikia kilio chetu. Ni njia ya daima ya kuingia na kupata msaada katika vita vyetu vya kiroho. NGUVU YA SALA Je! ni hakika tunapata msaada kwa njia ya kuomba? Lakini, bila shaka. Mungu anaitikia kwa shida zetu, Ombi sio badala ya nguvu zivutwe kutoka kwenye Neno la Mungu. Sala inatenda kazi ikiwa pamoja na hilo Neno la imani. Sana, ni hapo tujuapo mapenzi na njia ya Mungu Kutoka Neno lake kama tukigundua ipo haja ya kuomba ili kwamba tusiingie majaribuni. Sala katika maisha yake ya kwenda juu inazuia kuvutwa kwenda chini kunakosababishwa na maumbo yetu yaliyo na dhambi. Tunahitaji kila chanzo cha msaada na wakati mwingine tunauhitaji mno huo msaada. Akiba ya kutosha ya Neno la Mungu inapokuwamo moyoni, nia ya Kristo ikikaa kwa wingi ndani yetu, siku zote litatoa ushauri na nguvu, kwa sababu limekusudiwa kwa shabaha hiyo. Hakuna kinachoweza kueleza jambo hili zaidi kwa uwazi kuliko namna ambayo Kristo alivyoyafukuza majaribu ya jangwani. Habari za majaribu ya Kristo yanapatikana katika Mathayo 4 na Luka 4 ambapo mara tatu shambulio la kuwa Mwana limefanywa kwa mtindo wa maswali matatu, kila moja lilitoa ombi kwa mapenzi ya nafsi na yalikataa mapenzi ya Mungu yangekuwa na mafanikio. Bwana Yesu alipata majibu yake, na nguvu ya kuyatengeneza, kwa kufahamu kwake na utegemezi wa Neno lililoandikwa na Baba yake katika Agano la Kale. Kila jaribu lilikanushwa kwa maneno: "Imeandikwa", yakifuata maneno ya kufaa ya Maandiko. "Upanga wa Roho, ambao ni neno la Mungu" (Waefeso 6:17) ulilichoma kwenye kiini chake na ulisalimisha ushindi wa Kristo. Sawasawa na hivyo, nasi yatupasa tuvae kifuniko cha kukinga mwili wakati wa vita kwa kusali. Sala ilikuwa ndiyo kimbilio la Bwana na faraja. Ilikuwa chanzo cha baraka kuu kwa yeye. Ikiwa kwa uaminifu tukimuomba Mungu msaada wa kupigana vita yetu juu ya dhambi, daima utakuja: "Basi natukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa shida." (Waebrania 4:16) "Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; mwanadamu atanitenda nini." (Waebrania 13:6) (11) Mwamini anayepita na kuingia katika familia ya Mungu kwa imani na ubatizo anakuwa mwana wa kutunzwa kwa kila hali: aweze kurudiwa mara kwa mara, kuongozwa kwenye njia ya haki kwa ajili ya jina Lake, na abarikiwe kuwa na nguvu toka kwa Mungu katika maisha anayoishi kama akijiweka chini ya kongwa la Bwana Yesu Kristo. Toka asubuhi hadi jioni (usiku), kutoka siku hadi siku, maisha yote anayoishi yuasikia neno la Baba: "Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa." (Waebrania 13:5) VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU Muda mfupi kabla ya kupaa kwenda mbinguni Bwana Yesu Kristo aliwaahidi ahadi mitume wake: "Nanyi mtapokea uweza, baada ya huyo Roho Mtakatifu akiisha wajilia: nanyi mtakuwa mashahidi wangu." (Matendo 1:8) Ahadi hii ilitimizwa Yerusalemu siku ya Pentekosti. Roho Mtakatifu alimwagwa toka mbinguni na tangu hapo mitume walitoa ushuhuda kwa uwazi bila kujificha katika mji. Kusanyiko kubwa la Wayahudi toka Palestina, nchi za Meditraniani na Mashariki ya Kati walikusanyika ili wasikie, "kila mtu kwa lugha yake mwenyewe" (matendo 2:6), matendo makuu ya Mungu yalitangazwa haijawahi katokea. Kila mtu alishikwa na ushangao. Petro akaeleza ya kwamba yeye na ndugu, zake mitume walikuwa wanatangaza ujumbe waliopewa na nguvu za Roho Mtakatifu, na uwezo wao kufanya hivyo katika lugha zilizokuwa zinafahamika kwa wasikiaji ulitolewa na uweza wa Roho yule yule: "Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia." (Matendo 2:33) Petro aliyarudia maelezo yale yale wakati baadaye alipoandika waraka kwa waumini Kuhusu "mambo hayo, ambayo sasa yamehubiriwa kwenu na wale waliowahubiri ninyi injili kwa Roho Mtakatifu aliye tumwa kutoka mbinguni." (1 Petro 1:12) (12) Kwa sababu hii tumehakikishiwa kwamba ujumbe wa mitume uliitwa (mafunzo ya mitume), Matendo 2:42 ulikuwa unakubalika na ndiyo Baba na Mwana walitaka utangazwe basi. Zaidi, ujumbe wao ulishuhudiwa kwa kunena lugha mbali mbali, na kwa ishara nyingi na ajabu — miujiza ya kuponya na kufufua watu katika jina la Kristo (tazama Matendo 2:43; 3:4-7). Neno lililosemwa na ishara vilitoa msingi imara wa imani. Maelfu waliamini na, kwa sababu wageni waliotembelea Yerusalemu waliondoka na ujumbe pamoja nao, Injili ikaenea mpaka nchi za mbali. Makundi ya waumini katika sehemu kwa upana zimejitenga walihitaji msaada wa daima ili waitunze imani waliyoifuata, na "kukua katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo" (2 Petro 3:18). Ilikuwa ni vigumu kuwepo kwa mitume sehemu moja kwa muda mrefu akitumika, ingawa ni wazi wao walisafiri pasipokuchoka katika kumtumikia Kristo. Bado hapakuwa na Agano Jipya ambalo ujumbe wote wa mitume ungeweza kusomwa na kuhusisha na Agano la Kale ambalo tayari lilikuwa limesambazwa sana eneo kubwa. Uvuvio wa maelezo yaliyokwisha andikwa ya Injili, nyaraka maalum kwa kusanyiko moja moja na mtu mmoja mmoja zikawepo katika karne ya kwanza, maana sehemu kubwa kabla ya mwaka 70 B.K, na hizi au kopi zake — kwa haraka zilijulikana eneo pana zaidi. Tena maandishi haya yenyewe yalikuwa ni sehemu ya Maandiko yaliyotolewa na Roho Mtakatifu (2 Petro 3:15, 16). UWEZA MAALUM Lakini ni nafasi ya wakati gani kati ya ujumbe uliosemwa na mitume na maelezo yaliyotolewa na Mungu katika maandishi kuweza kuunganisha? Roho Mtakatifu alikuwa ni njia iliyotumiwa na Bwana Yesu Kristo. Nyongeza kwa mitume, watu fulani wengine walipewa uweza maalum ambao ulikusudiwa kutoa msaada kwa waamini katika mikusanyiko mbalimbali. Watu hawa walikuwa ni manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. (Waefeso 4:11), na vipawa vilivyokuwa vimeenea sehemu kubwa ni vile vilivyosemwa kama ifuatavyo: "Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule; ... na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja; na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha …" (1 Wakorintho 12:8-10) (13) Kwa njia hizi washirika wa kila jumuia au iklezia walifanywa imara kwa vipawa vya kuwasaidia kufanya kazi ya kufundisha, kuadibisha, kuonya na kundi la hao washuhudia waziwazi. Hakuna mtu aliyekuwa na vipawa vyote na washirika ambao walibahatika kuwa navyo, kila mmoja alimtegemea mwenzake kwa ajili ya kazi yote. Hakuna kipawa kilichotolewa kwa mshirika mmoja na huyo akatoa tena vipawa kwa washirika wengine. Ki mitume pekee ndiyo waliweza kufanya hivi (Matendo 8:14-18). Hatuna uhakika hasa na wakati wa kupewa na kufanya kazi kwa vile vipawa vilipokoma kutolewa, lakini iliweza kuwa wakati fulani baada ya kifo cha mtume ambaye alikuwa hai. Ya kuwa vipawa vitakoma yametolewa maneno kwa mtume Paulo akiongozwa na Roho: "Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu; hivyo vitatoweka siku moja, kama iii vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu (maarifa), nayo itapita." (soma Biblia Habari Njema - Kiswahili cha kisasa kifupi B.H.N katika 1 Wakorintho 13:8). Tena, kukoma kwa vipawa hivi kumetiwa pamoja na kuendelea kudumu kwa maadili makuu: "Basi, sasa inadumu imani, tumaini na upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo" (1 Wakorintho 13:13, U.V.), Imani na tumaini vitafuatana na ukweli na utimilifu utakuwa hapo Bwana Yesu Kristo akirudi. Mwishoni mwa karne ya kwanza Agano Jipya lilikamilika na likawa linapatikana kwa ajili ya wote wasome, kuenezwa na kulinganishwa kwa makini nakala za vitabu ishirini na saba kimoja kimoja kulifanyika kidogo kidogo. Kwa namna hii yote maiklezia vitabu vilipatikana kwao maelezo kamili ya maisha ya Kristo pamoja na utumishi na nyaraka za mitume. Inamaana kwamba Mungu hakuongoza tena uandishi wa Maandiko baada ya karne ya kwanza kufika mwisho. Kwa muda hao, kwa sababu hiyo, vipawa vilianza kutoweka. Kutoka vyanzo visivyo vya Biblia tunajifunza kwamba wakati wa karne ya pili watu waliinuka ambao walichochea kuwa na vipawa tu, ushahidi ndani yake unaonyesha kwamba vipawa vya kweli havikuendelea kuenea tena. VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU VIPO LEO? Toka kipindi hadi kipindi katikati ya karne zilizofuata kulikuwepo na makundi yanayodai kwamba mara nyingine tena vipawa vilikuwa vinapatikana kwa watu. Kwa nyakati za sasa Wapentekosti na makundi yanayosema ni ya kiroho yametoa madai haya. Kunena kwa lugha ndiyo kamezidi ya vipawa vyote vingine katika aina ya madai haya. Mara chache imedaiwa kuwa ni uwezo wa kusema lugha ngeni kama mitume (ona Matendo 2:4,6,11). Badala yake imesemwa kwamba wale wanaohusika wanakuwa wamepewa matamshi ya kusikia furaha moyoni ambayo wao wenyewe hawayafahamu, bali huwategemea watu wengine kawapa hiyo tafsiri ya wanayotamka. (14) Kwa sehemu zaidi kuonekana huku kunadhihirika katika mikutano wanayoiweka washirika wa makundi yanayohusika. Hayatumiki kama ni njia kuu kwa kufanyia mahubiri ya Injili kama waionavyo, sasa hii ni tofauti na mafunzo ya moja kwa moja na utendaji uliowekwa katika Maandiko (1 Wakorintho 14:22-25). Kweli, hakuna ushahidi wowote ambao uzushi wa siku hizi kwa vyovyote unahusika na kipawa cha lugha kama ilivyoelezewa katika Agano Jipya. Wala si namna ya pekee kwa makundi ya "Wakristo". Kutokea huku kunapatikana miongoni mwa makundi ya washiriki wa dini za dini za washariki na katika makundi ya Wamormoni. Tunaamini kwamba uzushi unainuka kutoka "uchochezi wa dini", hali ya maono yaliyo moyoni, na sio kutoka tendo lolote la Mungu. kwa njia ya Roho Mtakatifu. Fikra kama hizi zinatokea kwa kinachodhaniwa "kipawa cha uponyaji". Ule uponyaji uliofanywa na mitume haukufanyika kamwe kwenye "mikutano ya Kuponya". Hakukuwa na ibada ya kidini, wala maono ya bidii ya moyo inayoletwa na kuimba nyimbo za sifa na kuhabiri, lakini badala yake moja kwa moja na uponyaji wa uhakika mahali peupe, papo hapo, ili watu wote waone; au kwa faragha na mtume (ona Matendo 3:1-10 na 9:36-41). Miujiza hii ilifuata mfano mzuri wa uponyaji wa Bwana Yesu Kristo. Kwa sehemu zaidi, Bwana aliponya kwa kugusa an kwa kutamka neno na matokeo yalikuwa dhahiri. Utaratibu wa pande zote mbili na matokeo ya waponyaji wa siku hizi wapo tofauti sana kutoka kwa wale wa nyakati za Agano Jipya. Kuna makosa mengi na mara nyingi kukosa hali ya manufaa ya kudumu Kuweza kufaulu. Jambo hilo halikuwa na mitume. Katika siku hizo, mtu ambaye hakuwahi kutembea aliponywa papo hapo na kuweza kukimbia kwa furaha (Matendo ya Mitume 3:1-10). Mwanamke aliyekufa alirudi kwenye uhai kwa njia ya kusali kimya kwa mtume mmoja alipoitamkia neno maiti (Matendo 9:36-41). Waponyaji wa siku hizi hawapo kwa haki ya makundi ya Kikristo, ya Kiroho, na mengineyo kama wanaosema ni wa Kiroho. Roho Mtakatifu hawezi kuwatokea katika mgawanyiko. Inaonekana zaidi kuwa ni nguvu ya nia ya mponyaji juu ya nia na mapenzi ya mtu ambaye amekuja kuponywa. Kwenye maelezo yoyote yaweza kuthibitisha, kuuliza kwa msingi zaidi inapaswa kuendeshwe ndani ya madai ya wale wanakiri kuwa wanaongozwa na Roho. VIPAWA VYA ROHO MTAKATIFU NA KUJA MARA YA PILI Wakati mwingine imedaiwa kwamba tutegemee kufanywa upya kumwagwa kwa vipawa vya Roho kabla ya kuja mara ya pili Bwana Yesu Kristo. Imesemekana kwamba kama vipawa vilikuwa ishara Yesu alipokuja mara ya kwanza, basi itakuwa hivyo tena kabla ya kuja mara ya pili. Mistari katika Yoeli 2:28-32 imenukuliwa ili kutia nguvu dai hili. (15) Ikiwa tunasadiki kwa makusudi ya mahojiano kwamba sababu zinazotolewa ni sahihi, ni jinsi gani tutategemea vipawa kuja? Kwa makundi ya Kiroho kama haya ya leo? Ikiwa ni hivyo, kwa sababu gani? Kama sivyo, ni jinsi gani? Ingawa hii mistari ya kutoka Yoeli ilinukuliwa na mtume Petro katika kusaidia kuhusu kumiminwa kwa vipawa vya Roho katika siku zake, ijulikane kwamba mistari haikunukuliwa kabla ya kumiminwa kufanyika bali baadaye. Tena, kupewa vipawa vya Roho hakukutangulia kuja mara ya kwanza kwa Bwana Yesu Kristo; vilikuja baada ya kupaa yeye kwenda mbinguni, Ikiwa kumiminwa huku kulikuwa kutokee tena, basi tungetegemea mfano wake mzuri uwe wa aina moja wa ule uliowekwa ulipotokea ile mara ya kwanza. Kwa maneno mengine, kumiminwa kutafuata na sio kutaagulia Kabla ya kuja mara ya pili. Lakini, kwa njia hii hatuna haja ya kueleza kwa maneno tupu, Maandiko yanatupa ufahamu wa kazi ya Roho katika karne ya kwanza na kwa "ulimwengu ujao" (Maneno ya Kristo katika kueleza ujaji wa ufalme wa Mungu duniani, Luka 18:29-30). Wale waliokuwa na vipawa vya Roho wamesemwa kuwa "walionja ... na nguvu za ulimwengu ujao" (Waebrania 6:5). Vipawa vya Roho ilikuwa ni kuonja kwa sehemu (nusu) matendo yenye nguvu ya Roho wa Mungu Kristo atakaporudi katika uweza na utukufu mkuu. Ufufuo utafanywa wakati huo yaani waliokufa watafufuliwa (1 Wathesalonike 4:13-16); watakatifu watapokea kipawa cha uzima wa milele (Mathayo 25:31,46); Kristo atakuwa mtawala wa dunia yote tokea Yerusalemu naye atafuatana na watakatifu, ambao watakuwa ni makuhani na wafalme (Zekaria 14:9; Ufunuo 5:10; 20:4; Zaburi 2:6); wabaya kwa nguvu zote watakemewa (Zaburi 2:5,9; Isaya 11:3,4); na dunia itakuwa ni ya kupendeza na yenye kuzaa matunda mema (Isaya 35:1,2; Zaburi 72:16); walioathirika viungo vya mwili wataponywa (Isaya 35:5,6); na maajabu mengine yasiyohesabika yatafanywa na Roho Mtakatifu wa Mungu kwenye mikono ya Bwana Yesu Kristo na watakatifu wake watukufu. JARIBIO LA MAFUNDISHO YA BIBLIA Biblia inatupa jaribio la uhakika sana kwa kukata maneno ya uthabiti wa madai yao wale wanaosema wananena kwa lugha au wafanyao miujiza ya moja kwa moja toka ushawishi wa Roho Mtakatifu. Jaribio haliulizi tendo la kutaka kuthibitisha au unyofu wa wale wanaohusika, wala haliulizi mambo ya ujuzi ambayo mara nyingi yamesemwa walikuwa nayo. Jaribio linakwenda kwenye kiini cha jambo halisi: Ni mafundisho gani yaliyomo katika ujumbe wanaousema? Je! ujumbe unapatano na elimu ya mafunzo ya Biblia? Kwa maneno mengine, je! Injili inayohubiriwa na, wanaosema ni wa Kiroho, inalingana na mafundisho ya Kristo na mitume wake? Ni kwa sababu hii basi, tumeamriwa "tuzijaribu roho ikiwa zimetokana na Mungu: kwa kuwa manabii wengi wametokea ulimwenguni" (1 Yohana 4:1). (16) Kando ya kawaida hii, vikundi vya kiinjili vilivyoenea vinaonekana kuwa kwa huzuni vimekwenda tenge kutoka kwenye mafunzo ya Biblia. Hawasemi ukweli kuhusu uzima baada ya kifo, ibilisi, Uungu na Bwana Yesu Kristo, ubatizo na mambo mengi mengine. Ni jambo la ajabu kuona kwamba jumuia, kama kweli imebahatika kuwa na Roho, kisha namna hii hiyo jumuia ikaweza kuwa katika kosa, sio katika imani ya wachache kati yao, bali katika kikundi cha jumuia yote. Tunapopima kwa makini kile kinachofanyika, tunagundua kwamba wanaweka msisitizo zaidi katika kuongozwa na Roho kuliko kuongozwa katika kweli ya mafunzo ya Keno la Mungu. MWONGOZO KUTOKA KWA MUNGU. Mambo ambayo lazima yakumbukwe yaliyokwisha tajwa yanatuongoza tupime jambo lingine la kuliangalia la wale wanaosema kuwa wana Roho Mtakatifu, wanaita, umuhimu wa kuongozwa na Roho. Uwezo wa mtu kukata shauri umesemwa kuwa unaamuliwa na Roho. Majibu yamesemekana kuwa yanatolewa na Roho kwa njia moja au nyingine. Haidaiwi kuwa kila kitu kinawekwa kwa Bwana kwa njia ya maombi tu (mazoea ambayo hatutakiwi kufanya malalamiko) bali kwamba majibu yaliyodhahiri yanatolewa. Aina zote za mambo yanayotokea kwa pamoja ni "ushahidi" na yamewekwa kama mfano wa kuainisha namna hii ya kufanya maamuzi. Tutiaamini kwamba njia hii inafikiwa pale makosa ya kufahamu mafundisho ya Biblia yanapozuka. Sababu ya tatizo ipo katika kuona mamlaka ya Maandiko. Biblia ndiyo kitabu kilichojaa mwongozo. Maswali mengi ya maisha ya kila siku tayari yamejibiwa kiasi cha kutosha ndani ya kurasa za Biblia ambazo zinamaana ya kuwa ni "taa ya miguu yangu, na mwanga kwa njia yangu" (Zaburi 119:105). Kitabu cha Mithali kinaeleza kwamba: "Maana maagizo hayo ni taa; na sheria hiyo ni nuru; na maonyo ya kumwadilisha mtu ni njia ya uzima" (Mithali 6:23). Kuwa mtu wa maombi kunatuhakikishia kwamba miguu yetu inakuwa imeonyeshwa njia itupasayo kuenenda. Basi Biblia ni kitabu cha Roho Mtakatifu cha kutuongoza. Wakati mwingine imesemwa, na wale wanaodai kuwa Roho huwapa mwongozo, kwamba uongozi hutafuta mahali ambapo Maandiko hukaa kimya. Elimu ya ujuzi wa wadai kama hawa ni kwamba wanatafuta mwongozo katika maeneo ambayo Biblia ipo wazi kwa mafunzo yake kabisa, pia wanadai kuwa wanaongozwa hata kwa kile kilicho tofauti wanacho fanya kwa mafundisho ya moja kwa moja ya Neno la Mungu. Kwa maneno mengine, "Roho" alifanywa awe juu ya Neno la Mungu, na utata huu wa mamlaka umelala kwenye msingi wa kosa katika kufikia maamuzi ya kiroho. (17) Wafuasi walihakikishiwa kwamba "mambo yote hufanya kazi pamoja na wale wampendao Mungu" (Warumi 8:28). Maisha ya waaamini wa kweli yapo mikononi mwa Bwana, nasi yatupasa kumtafuta siku zote kwa njia ya sala ili atubariki katika safari yetu katika maisha. Hajaahidi kujifunua wazi kwetu ili tufanye kitu gani. Tumepewa mwongozo ili tufuate mafundisho ya Neno la Mungu na kwa maombi tutafute baraka za Bwana na msaada wa kutusaidia kutimiza maagizo yake, tanajua kwamba matunzo ya Mungu yatatuhakikishia kwamba katika safari ya maisha itatuleta kufikia hatua za mwalimu, na kutufikisha salama, kama tukiendelea katika imani, kwenye uzima wa milele Kristo akirudi. YATUPASA TUCHAGUE! Uchaguzi ni moja ya ufunguo wa kazi ya maisha ya kila mfuasi. Yampasa akate shauri kati ya mageuzi yanayowaweka katika maisha ya kila siku. Maamuzi yake yanatakiwa msingi wake uwe kwenye Neno la Biblia. Njia ambayo haikubaliki katika Maandiko ni kujitenga toka kufanya uchaguzi wa kiroho wa kuweka kila jambo kwa Bwana au kumuomba Mungu akupatie jibu. Ufunuo wa namna hii haujaahidiwa ndani ya Biblia. Tunategemewa kujizoeza nia zetu juu ya matatizo ya maisha kwa kutumia mwangaza wa mafunzo ya Biblia na katika maombi ya kujinyenyekeza kwa Mungu. Biblia inamafundisho yaliyowazi yanayo mtaka mwamini afanye uchaguzi uliosahihi ambao msingi wake upo juu ya mambo makuu yaliyowekwa katika Maandiko. Kwa mfano: "Nimekuwekea mbele zako uzima na mauti, baraka na laana: Basi chagua uzima." (Kumbukumbu la Torati 30:19) “Chagueni hii leo ni nani mtakaye mtumikia" (Yoshua 24:15) "BWANA yu mwema, mwenye adili, kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia. Wenye upole atawaongoza katika hukumu: na wenye upole atawafundisha njia yake. Njia zote za BWAKA ni fadhili na kweli kwa walishikao agano lake na shuhuda zake ... Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua.” (Zaburi 25:8-10,12) "Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya, watu makosa yao, na kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema." (2 Timotheo 3:16-17). (18) BIBLIA MWALIMU WA MUNGU Neno la Mungu ni mwalimu atokaye kwa Mungu mwenye akili naye anatupatia sisi uongozi mkubwa juu ya mambo ya maisha ya kila siku. Ndani yake yamewekwa mafundisho yaliyo wazi juu ya uchaguzi wa kuufanya karibu kila mwelekeo wa maisha ya Kikristo. Kuliacha ni hasara yetu. Zaidi Neno la Mungu, ni chakula kwa ajili ya moyo nalo linatutia nguvu katika kufanya uchaguzi wa kuwa ka-ma Kristo. Kwa maneno mengine, Neno 3 Mungu linatuambia tuchague kitu gani. Ikiwa kwa unyenyekevu tunalipokea Neno lenye mafundisho la Mungu na kunuia kweli kulifuata, tunaweza kwa haki kuomba baraka za Mungu kwa njia ya sala, Ameahidi kuwa hawezi kutuacha. Uchaguzi wetu unapokuwa na shida kuunuia hata ikiwa tunayo Biblia mkononi na moyoni, njia yetu ni kuikabidhi kwa Bwana katika sala na, pasipo kawa ne ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwake, ila ni kuendelea kufanya kwa imani yale mambo tunayoyaamini kawa yana busara mbele yake. Maongozi haya yaliyo rahisi yanatosha kwa mahitaji ya maisha. Paulo aliwapa maelezo moja moja ya mafundisho wafuasi wa siku zake, wengi ambao walikuwa na vipawa vya Roho, na akamalizia kwa kusema: "Basi, sasa nawaweka katika mikono ya Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliotakaswa." (Matendo 20:32) HARRY TENNANT Kimebadilishwa na kuwa katika lugha ya Kiswahili na ndugu wa CBM Mwanza. Shukrani nyingi kwa ndugu yetu ambaye ndiye mwanzilishi wa kitabu hiki. (19) Tena: 1 902059 00 - X Matayarisho ya Ubatizo 1 902059 01 - 8 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 1-4 1 902059 02 - 6 Ukimwi 1 902059 03 - 4 Mshitaki Wenu Ibilisi 1 902059 04 - 2 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 5-8 1 902059 05 - 0 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 9-11 1 902059 06 - 9 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 12-15 1 902059 07 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 16-19 1 902059 08 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 20-23 1 902059 09 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 24-27 1 902059 10 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 28-31 1 902059 11 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 32-36 1 902059 12 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 37-40 1 902059 13 - 1 Ufunuo mlango wa kwanza - Maelezo ya maneno ya mstari kwa mstari 1 902059 14 – X Ni Kweli Yesu Kristo Alishuka Kutoka Mbinguni? 1 902059 15 – 8 Biblia Yaonyesha kuwa ni uwezo wa Mungu Kama unataka kujifunza zaidi njia ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze Biblia. Ili kukusaidia; Kanise la Christadelphian Bible Mission limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya Biblia kaitka somo hili muhimu. Lina itwa Kuishi katika Ukweli. Unaweza kupata nakala kutoka Kanisa la Christadelphian, au kutoka anuani iliyoandikwa katika kijitabu hiki. CBM Publishing 32 Blenheim Road, Far Cotton Northampton, England. NN4 8NW ISBN 1 902059 15 – 8 Registered Charity Number: 248979 / 1020558 Company Number: 2796412 Telephone +44 (0) 1604 463578 Facsimile +44 (0) 1604 765068 Email: CarlHinton@hotmail.com Web: http:\\cbm-tz.org