_________________________________ Matayarisho ya Ubatizo Preparing for Baptism _________________________________ _________________________________ Yaliyomo _________________________________ Kifungu Nambari Utangulizi 1 1 Biblia 2 2 Mungu 3 3 Mtu 4 4 Jehanam 6 5 Yesu Kristo - Mwokozi 7 6 Yesu Kristo - Ufufuo wake 8 7 Yesu Kristo - Kupaa kwake 9 8 Yesu Kristo - Kurudi kwake duniani 10 9 Yesu Kristo - Mfalme ajaye 11 10 Ufalme wa Mungu 12 11 Injili 13 12 Ufufuo, Hukumu na Uzima wa Milele 15 13 Roho Mtakatifu 17 14 Malaika 19 15 Dhambi Shetani na Ibilisi 21 16 Ibilisi na Pepo Wachafu 22 17 Njia ya uzima wa Milele 23 18 Ubatizo 23 19 Maisha ya Mkristo 25 _________________________________ Utangulizi _________________________________ Njia pekee ya kuwa Mkristo wa kweli ni kuamini na kubatizwa katika Kristo. (taz Wagalatia 3:27). Lakini kabla ya kuweza kubatizwa ni lazima tuelewe mafundisho ya Biblia na kuyaamini. (taz. Matendo 8:12). Kitabu kidogo hiki ni kukusaidia ufanye hivyo. Namna ya Kutumia Kijitabu Hiki (1) Usijaribu kwenda mbio na matayarisho yako ya ubatizo. Wengi wanatakiwa kujifunza Biblia angalau kwa mwaka mmoja au miwili kabla ya kuelewa vizuri zaidi na kubatizwa. Kama tayari umejifunza Biblia kwa muda mrefu, unaweza kupitia kijitabu hiki katika miezi michache. (2) Fanya bidii katika kujifunza Biblia. Ni jambo la maana kuongeza nguvu zaidi, sababu uzima wa milele ni tuzo kubwa. Uwe tayari kutumia angalau nusu saa kwa siku - kila siku - kusoma Biblia na ukikariri ulichosoma. (3) Soma swali moja kwa wakati mmoja. Soma swali na jibu. Halafu angalia vifungu vya Biblia vilivyo nukuliwa katika majibu. Kama unao uhakika kuwa unaelewa haya, na kwamba unakubaliana na jibu, ndipo unaweza kuangalia swali lingine. (4) Iwapo hutaelewa vifungu vinginevyo vya Biblia, au kutokubaliana na baadhi ya majibu yaliyotolewa. Kama ndivyo, tafadhali mwulize mwulize mwalimu, wako wa Biblia wa Christadelphian kuhusu hayo. Yuko tayari wakati wote kukusaidia. (5) Iwapo inawezekana jaribu kusoma Biblia katika kikundi na watu wengine. Utaweza kusaidiana na wengine, na ufanye maendeleo ya haraka kwa njia hiyo. (6) Kwa kadri unavyo soma kitabu hiki, ni wajibu usome sura ya Biblia moja au zaidi kila siku. Njia nzuri ya kufanya ni kufuata mpangilio wa kili siku wa vifungu vilivyo tolewa katika kitabu kingine kidogo, The Bible Companion. Unaweza kupata nakala yoyote kutoka kikundi cha Wakristadelphian au kutoka kwa wachapishaji wa kijitabu hiki. Onya Utastaajabu kama utapaswa kujifunza kwa kuyakariri kichwani maswali na majibu katika kujitabu hiki. Hii sio lazima. Jambo muhimu ni kukumbuka yale yaliyo fundishwa kitabuni, sio yale tuliyo eleza. Kama utaona inasaidia kujifunza maswali na majibu kwa moyo, basi fanya hivyo. Lakini hakikisha kwamba unaelewa hasa, na unaamini mambo uliyo jifunza. Mungu anataka wanaomuamini, wasiwe kama kasuku anayerudia mambo pasipo kuelewa. Kabla hujaweza kubatizwa kama Mkristadelphian unategemea kujibu baadhi ya maswali, kuonyesha kuwa unaamini na kutii mafundisho ya Biblia. Maswali haya HAYATAKUWA sawa na maswali katika kijitabu hiki. Hutaweza kuyajibu mpaka umeyaelewa sawasawa mafundisho ya kijitabu hiki. _________________________________ 1 Biblia _________________________________ 1.1 Biblia ni nini ? JIBU: Hakuna mfano wa kitabu kingine kama Biblia ulimwenguni, Sababu :- (a) Ni kitabu pekee kinachotuelezea ujumbe wa kweli kuhusu Mungu, Bwana Yesu Kristo na Wokovu. tazama Waebrania 1:1-2; Zaburi 138:2; 2 Timotheo 3:16; Zaburi 119:160. (b) Imeandikiwa na watu waliongozwa na Roho mtakatifu wa Mungu. taz. 2 Petro 1:21; 1 Petro 1:11; Waebrania 1: 1-2. (c) Inaahidi uzima kwa wote wamwaminio na kutii neno lake. taz. Yohana 17:3; Warumi 2:7; 2 Petro 1:11. 1.2 Tunawezaje kuelewa vizuri ujumbe wa Biblia ? JIBU: (a) Kuelewa na kuamini neno lake, tunatakiwa kusoma Biblia mara kwa mara pamoja na maombi ya baraka za Mungu. tazama 1 Timotheo 4:13; Zaburi 119: 103-105; Yeremia 15:16; Yeremia 9:24. (b) Biblia yenyewe ndiyo tafsiri nzuri. Baadhi ya vifungu vya Biblia hutusaidia kuelewa vifungu vingine. taz. Luka 24:25-27, 1 Wakorintho 2:13. _________________________________ 2 Mungu _________________________________ 2.1 Biblia inatufundisha nini kuhusu Mungu ? Jibu: (a) Mungu ni pekee wa kweli. taz. Isaya 44:8; Isaya 45:5; Kutoka 20:3; Waefeso 4:6. (b) Mungu ni Roho, taz. Yohana 4:24 (c) Mungu ni Muumbaji wa vitu vyote. taz. mwanzo 1:1, Isaya 45:18 (d) Mungu ni mweza wa vitu vyote, na huyatambua yote, na hata yaliyo akilini mwetu. Isaya 45:7; Zaburi 139:1-12. (e) Mungu ni mmoja, na si watatu. tazama kumbukumbu 6:4; 1 Wakorintho 8:6; Malaki 2:10; Marko 12:29. -3- (f) Mungu ni mtakatifu na wa kweli. taz. Kutoka 15:11; Isaya 6:3; Zaburi 10:9. (g) Mungu ni mwema na mwenye huruma. tazama Kutoka 34:6; Warumi 2:4; Zaburi 103:8-14. (h) Mungu ni mwenye haki na atawaadhibu wakosefu. taz. Kumbukumbu 32:4; Zaburi 145:20; Warumi 1:18. (i) Mungu ana mpango wa dunia nzima wa baadaye na Taifa zima. taz. Waebrania 14:21; Isaya 45:18; Ufunuo 21:1-4. (j) Mungu ni Baba wa Kristo Bwana Yesu. Mathayo 3:17; Luka 1:31-35; Waebrania 1:2-6; 1 Petro 1:3. tazama pia vifungu 5,6,7,8 na 9. _________________________________ 3 Mtu _________________________________ 3.1 Mtu aliumbwaje ? Jibu: Mtu aliumbwa "kwa mfano wake Mungu." Mtu wa kwanza aliumbwa tokana na vumbi la ardhi. Mungu alimpulizia pumzi yenye uhai na akawa hai, Mwanzo 1:27, Mwanzo 2:7. 3.2 Je, Biblia inakubali mafundisho kuwa mtu alitokana na wanyama ? Jibu: Hapana. Biblia inalaani usemi huu kwa kutuonyesha kuwa Adamu alikuwa wa kwanza kuumbwa na Mungu, na mwanamke wa kwanza Eva, na kwamba wake kwa waume wote wametokana nao. Mwanzo 1:27; Mwanzo 3:20; Mathayo 19:4; Warumi 5:12. -4- 3.3 Ni jinsi gani Biblia inatueleza kuwa wote wanakufa? Jibu: Adamu alimuasi Mungu, Hivyo alistahili hukumu akahukumiwa kifo. Na adhabu ya kifo hiki imeingia kwetu sisi kutoka kwa Adamu, na sababu tuwazawa wa Adamu katika yeye hatuna budi kupata laana hiyo ya Mungu. Taz. Mwanzo 3:1-19; Warumi 3:9-10; Yeremia 17:9; Marko 7:21-23: Warumi 5:12. 3.4 Dhambi ni nini? Jibu: Kila siku twavunja moja ya amri zake Mungu, tunatenda dhambi. Hata kama hatutambui kuwa tunatenda, bado ni dhambi. taz. 1 Yohana 3:14; Walawi 4:27. 3.5 Kifo ni nini? Jibu: Kifo kililetwa kama adhabu ya dhambi taz. Mwanzo 2:17; Warumi 6:23, Ezekiel 18:4. 3.6 Kunatokea nini kwa watu wanapo kufa? Jibu: Watu wanapo kufa hawaishi tena, wafu hawawezi kufikiri, au kufanya lolote au kujisikia. Hawana fahamu (kujua lolote) mfano katika usingizi mzito usio na ndoto. taz. Zaburi 6:5; Zaburi 17:12, 14:20; Zaburi 146:3-4; Mhubiri 9:5-6; Yohana 11:1-14. 3.7 Je, Roho itaishi baada ya mwili kufa ? Jibu: Hapana. Biblia haitaji Roho za uzima "immortal soul" inatumia neno Roho "soul" kwa kitu chochote kilicho hai - mfano mtu, mnyama, ndege, samaki, mdudu. Biblia inatufundisha kuwa Roho inaweza kufa na itakufa taz. Hesabu 31:28; Ezekeili 18:4,20; Zaburi 8:48. -5- 3.8 Je, kuna matumaini yoyote kwetu sisi mbali ya maisha haya? Jibu: Ndiyo lakini tu katika Kristo Yesu. Ameshinda yote dhambi na mauti. Atakapo kuja tena duniani, wafu watafufuliwa na kuhukumiwa. Wale walio mwamini yeye watapata uzima wa milele katika ufalme wake. 2 Timotheo 1:10; 1 Wakorintho 15:21-23; Danieli 12:2-3; Yohana 5:28-29; Mathayo 25:31-34. (Utaona zaidi haya katika kifungu cha 12). _________________________________ 4 Jehanum _________________________________ 4.1 Nini maana ya Jehanum ? Jibu: Neno limeonekana katika vifungu vingi, kuwa Jehanum ni neno lingine la kaburi. Wakati Yesu alipozikwa, alilazwa katika kaburi "hell", na alipofufuliwa kutoka kwa wafu alitoka katika jehanum "hell" taz. Ezekieli 32:27-29; Matendo 2:25-31. 4.2 Je lakini Yesu hakusema Jehanum ni mahali pa hukumu ya moto ? Jibu: Ndiyo, kwa wakati mwingine alisema. Agano jipya liliandikwa kwanza na Wagiriki na neno ambalo hasa Bwana Yesu alilitumia alipokuwa akisema Jehanum ni sehemu ya moto neno lililotafsiriwa "Hell" katika vifungu kama Marko 9:43-48 na Mathayo 10:28 ni Gehenna. Hili ni jina halisi la hapa mahali pa duniani. Gehenna lilikuwa ni bonde nje ya mji wa Yerusalem, ambako takataka za mji Yerusalem, zilichomwa na moto, ambao haukupata kuzimika. Hivyo Bwana alimaanisha, Mungu atawaharibu kabisa watenda dhambi kama moto wa Gehenna unavyo haribu takataka za Jerusalem. Wakati Bwana Yesu alitumia kama vielelezo alivyotumia mara kwa mara. -6- _________________________________ 5 Yesu Kristo - Mwokozi _________________________________ 5.1 Yesu Kristo ni Nani? Jibu: (a) Yesu Kristo ni Mwana pekee wa Mungu. Hakuwa na Baba Mzazi, lakini alichukuliwa mimba kwa nguvu ya Mungu, iitwayo Roho Mtakatifu ambayo ilitenda miujiza kwa mamaye, ambaye alikuwa bikira, taz. Luka 1:32, 35; Mathayo 1:20-25, Mathayo 3:17; Yohana 1:49; Yohana 1:49; Yohana 10:36. (b) Hata hivyo alikuwa binadamu ambaye alijisikia njaa, kiu, alilia, alipata mateso na alikufa kama watu wengine, taz. Waebrania 2:17; Luka 2:52; Isaya 53:3; Yohana 1:35; Yohana 19:33. 5.2 Kazi ya Yesu Kristo Mwana wa Mungu ilikuwa ni Nini? Jibu: (a) Ilikuwa kuonyesha Baba yake, Mwenyezi Mungu kwa ulimwengu ili watu wapate kumjua. taz. Yohana 1:18; Yohana 12:45; Yohana 17:6, 26. (b) Kuonyesha watu ubora wa utukufu wa Baba yake na utakatifu, ukweli na upendo, taz. Yohana 1:14-17; Warumi 3:24-26. (c) Kuonyesha watu utiifu na maana ya kuwa mkristo taz. Luka 22:42; Yohana 5:30; 8:29. (d) Kuhubiri Injili taz. Luka 4:18; 9:6 na 20:1. (e) Kutufia sisi taz. Yohana 10:11, 15; Matendo 2:23. (f) Kutuleta kwa Mungu tazama Waefeso 2:16; Warumi 5:10; Yohana 14:6. -7- 5.3 Ni jinsi gani Bwana Yesu anaweza kutuleta kwa Mungu tena ? Jibu: Tumekuwa kama watoto waliopotea kwa baba yao. Tumetengwa na Mungu kwa ajili ya dhambi zetu. Bwana Yesu Kristo anaweza kutuleta kwa Mungu tena kutokana na kujitoa kwa kifo chake, na maisha yake safi. Sababu alizaliwa na Maria, Yesu alikuwa binadamu, lakini sababu pia alizaliwa na nguvu ya Roho Mtakatifu, ni mwana wa Mungu. Kwa hiyo ni mpatanishi kati ya Mungu na sisi. Biblia ina mwita "Mpatanishi" (neno hili lina maana mtu wa kati) kati ya Mungu na watu. Kwa kuwa yeye ni mtu, Bwana wetu alijaribiwa katika sisi; lakini mbali na sisi mara kwa mara aliishinda dhambi. Ali tii Mapenzi ya Mungu katika kila jambo, na hasa katika kutufia msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Tutakapo amini kweli katika kazi hii ya Kristo, na kuonyesha hayo kwa ubatizo (taz. Kifungu 18), Mungu anatusamehe dhambi zetu na kutukubali kama watoto wake. taz. Waebrania 2:14; Waebrania 2:17-18; 1 Timotheo 2:5; Waebrania 4:15-16; 2 Wakorintho 5:21; Warumi 8:2-4. _________________________________ 6 Yesu Kristo - Ufufuo wake _________________________________ 6.1 Baada ya kufa Bwana Yesu, kulitokea nini kwake? Jibu: Alizikwa, lakini siku ya tatu Mungu alimfufua Mwili kutoka kwa wafu, kuishi milele. taz. Mathayo 27:57-60; Mathayo 28:1-7; Warumi 1:4; 1 Wakorintho 15:3, 4 na 20; Ufunuo 1:18. -8- 6.2 Kwa nini ilitokea hivi ? Jibu: (a) Sababu hakuwa na dhambi hakuonja mauti - "mshahara wa dhambi" kama Biblia inavyo sema. Hivyo Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. taz. Warumi 6:23; Matendo 2:24; Wafilipi 2: 8-11. (b) Kwa kumfufua Bwana Yesu kutoka kwa wafu, Mungu alionyesha pia jinsi atakavyo wazawadia wote wale ambao wanamfuata Yesu katika kweli. Kama tutajenga imani yetu katika Kristo na kama tutafanya bidii kutii na kumfuata, sisi, pia, tutafufuliwa kutoka kwa wafu siku ya mwisho (taz. Kifungu 12). taz, 1 Wakorintho 15:21-23; 2 Wakorintho 4:14. _________________________________ 7 Yesu Kristo - Kupaa Kwake _________________________________ 7.1 Kwa nini Bwana Yesu alikwenda Mbinguni? Jibu: (a) Siku arobaini baada ya ufufuo wake kutoka kwa wafu, Bwana Yesu alifufuliwa kwenda juu kwa Mungu Mbinguni. Mungu alimfanya kuwa Mkuu kuliko mtu yeyote. Mkuu zaidi ya Malaika. Ni Mkuu wa pili zaidi ya wote ulimwenguni. Baada ya Mungu mwenyewe taz. Waebrania 1:3-4; Wafilipi 2:9-10; Ufunuo 5:12-13). (b) Yesu Kristo sasa ni Mhubiri pekee wa kweli wa Mungu ambaye sala zake husikilizwa na Mungu. Pia anatuombea kwa Mungu taz. Warumi 8:34; Waebrania 4:14-15; Waebrania 7:24-27. -9- _________________________________ 8 Yesu Kristo - Kurudi kwake duniani _________________________________ 8.1 Tutajuaje kuwa Yesu Kristo atakuja tena duniani ? Jibu: (a) Sababu Mungu aliahidi katika Agano la kale taz. Zaburi 110:1-2; Danieli 2:13-14. (b) Sababu Bwana Yesu aliahidi wanafunzi wake kuwa atarudi taz. Mathayo 16:27; Ufunuo 22:12. (c) Sababu malaika wa Mungu walisema hivyo taz. Matendo 1:11. (d) Sababu mitume walifunisha. taz. Matendo 3:20-21; 1 Wathesalonike 4:16. 8.2 Ni lini atarudi? Jibu: Kwa wakati wake alioupanga si mbali sana. taz. Matendo 17:31; Warumi 2:6, 16. 8.3 Tunajuaje haya? Jibu: Soma Luka 21:24-27 na tazama jinsi ya dalili za kurudi kwake Yesu, zinatimilika wakati huu Wayahudi wameisha rudi katika nchi ya Israel, na Yerusalem haiko tena mikononi mwa mataifa (kifungu 14) kuna misukosuko hofu na uharibifu ulimwenguni kwa kiasi kikubwa. (Vifungu 25-26) hadi hapo aje Yesu upesi, wataangamizana wao wenyewe. taz. pia Mathayo 24:36-41; 2 Timotheo 3:1-4; Ezekiel 37:21-28. Zingatia: Miaka mia moja iliyopita, hapakuwepo na taifa la ki-Israel. Nchi ya Israel ilikuwa chini ya koloni la Waturuki. Waarabu -10- wengi waliishi pale, lakini Wayahudi wachache tu elfu moja. Leo Israel ni taifa lenye nguvu, karibu million tatu ya Wayahudi. Hivyo ni dalili ya wazi kuwa ufalme wa Mungu u karibu. taz. Yeremia 30:3, 21-22, 24; Ezekieli 36:24-28; Ezekieli 37:21-28. _________________________________ 9 Yesu Kristo - Mfalme wa baadaye _________________________________ 9.1 Je Yesu Kristo alizaliwa kuwa mfalme? Jibu: Ndiyo. Yesu alizaliwa "Mfalme wa Wayahudi". Mbele ya Pilato katika mashtaka alinena kuwa alikuwa mfalme, na alipo kufa anwani ya maneno juu ya kichwa chake msalabani yaliandikwa "Yesu Mnazareti, mfalme wa Wayahudi". Atakuwa mfalme wa Wafalme. taz. Mathayo 2:2; Yohana 18:37; Yohana 19:19; Zaburi 72:11; Ufunuo 19:16. 9.2 Ni lini Yesu Kristo ataanza ufalme wake juu ya Wayahudi? Jibu: Atakaporudi tena taz. Mathayo 19:28; Luka 19:11-12, 15. 9.3 Ni wapi Yesu Kristo atatawala ? Jibu: Atakaa penye kiti cha enzi cha Daud Yerusalem. taz. Luka 1:32; Isaya 9:6-7; Mathayo 5:35; Zekaria 6:12-13. 9.4 Je, Yesu Kristo atatawala tu juu Wayahudi? Jibu: Hapana. Israel itakuwa ni Taifa la kwanza atakalolitawala, lakini atatawala kila Taifa ulimwenguni. taz. Yeremia 23:5-6; Zaburi 72:8; Isaya 2:3-4; Zekaria 14:9. -11- _________________________________ 10 Ufalme wa Mungu _________________________________ 10.1 Je, Mungu amewahi kuwa na Ufalme kabla hapa duniani? Jibu: Ndiyo. Ufalme wa Israel uliitwa ufalme wa Bwana Yesu atakaporudi atasimamisha ufalme wa Ki-Israel tena, lakini ufalme ujao wa Mungu utakuwa bora zaidi ya ufalme wa Israel uliopita. taz. Mambo ya Nyakati 28:5; Mambo ya Nyakati 13:8; Ezekeili 21:25-27; Luka 1:32-33. 10.2 Je, nani atakayeishi katika ufalme wa Mungu? Jibu: Kama tunaamini ahadi za Mungu na kumtii yeye, ndipo tutaweza kurithi na Bwana Yesu ufalme wake. wengi binadamu wenye miili ya nyama na damu wataepukana na usumbufu wa dunia katika siku za mwisho na wataishi pia katika ufalme wa Mungu. Watawala watakaoishi milele watawafundisha njia za Mungu. taz. Mathayo 19:27-29; Luka 19:15-19; Ufunuo 5:10; Ufunuo 20:6; Isaya 65:20-22; Zekaria 14:16-18. 10.3 Maisha yatakuwaje katika ufalme wa Mungu? Jibu: Watu wenye miili ya nyama na damu watalima katika nchi na kazi yao itakuwa yenye furaha na utajiri wa mafanikio, watamsujudu Mungu wa kweli na kufuata amri zake. Mungu atawapa furaha na kuwaponya magonjwa. Vita na chuki vitakoma. Baada ya muda mrefu kutakuwa na ufufuo wa mwisho na hukumu. Waaminifu watapata uzima taz. Isaya 2:3-4; Isaya 11:1-9; Isaya 35; Zaburi 72:1; 1 Wakorintho 15:24, 28; Ufunuo 20:12-18; 21:4. -12- 10.4 Je, ufalme wa Mungu unaundwa sasa? Jibu: Ufalme wa ulimwengu huu hautakuwa ufalme wa Mungu hadi hapo Yesu atakapoarudi duniani. Danieli 2:44; Danieli 7:27; Ufunuo 11:15-18. Lakini bado Mungu anatawala juu ya watu na mambo yao na vitu vyote, Zaburi 104:1 na Danieli 4:17; hata hivyo, miaka yote amekuwa akiwaita wake kwa waume, wawe wake katika nyumba ya kifalme ya ufalme ujao. Matendo 15:4; 1 Petro 2:9; Ufunuo 1:6; watu kama hao ni lazima wakubali na kuamini na kutii Injili ya ufalme wa Mungu na kwa ubatizo kujitoa, kwake Mungu na kwake Kristo kama Bwana. Ndipo inapowalazimu kumtakasa Kristo Yesu kama Bwana mioyoni mwao (1 Petro 3:15 R.V.) kwa njia hii kiini cha ufalme wa Mungu tayari unaundwa kwa siku ile ya kurudi kwake, Yesu Kristo. _________________________________ 11 Injili _________________________________ 11.1 Injili ni Nini? Jibu: Injili (Gospel) ni neno la zamani la kiingereza lina maana habari njema (good news). Ni habari njema kuhusu ufalme wa Mungu na jinsi tutakavyopata wokovu katika ule ufalme - taz. Luka 8:1; Marko 1:14; Mathayo 4:17 na 23; Warumi 1:16. 11.2 Je, Yesu Kristo ni mtu wa kwanza kuihubiri Injili? Jibu: Hapana. Injili ilihubiriwa kwa Abraham ambaye aliishi karibu miaka 2,000 kabla ya Yesu Kristo. taz. Wagalatia 3:8. -13- 11.3 Mungu alimuahidi Abraham Nini? Jibu: (a) Alimpa habari njema ya Injili (Wagalatia 3:8). (b) Alimwahidi kuwa mataifa yote yatabarikiwa katika Abraham na mbegu yake. (c) Alisema Abraham atakuwa baba Mkuu wa Mataifa ya watu wengi na wafalme na atakuwa ni chanzo cha baraka kubwa Mwanzo 12:2; 13:16; 17:4,6. (d) Aliweka ahadi kwa Abraham na kwamba atarithi nchi ya Caanan milele baada ya ufufuo kutoka kwa wafu. Mwanzo 13:14-17; 15:7, 12, 17; 17:8; Matendo 7:5; Marko 12:26-27; Waebrania 11:8-9, 39-40. (e) Aliahidi kuwa mbegu ya Abraham (Kristo) atarithi nchi ya Caanan, na awe mfalme juu ya maadui zake Mwanzo 12:7, 22:17; Wagalatia 3:8, 16, 29. Ahadi zilitolewa tena kwa mtoto wa Abraham, Issac, na mjukuu wake, Yakobu tazama Mwanzo 26:2-4, 28:3-4, 13-14. 11.4 Mungu aliahidi nini kwa mfalme Daudi? Jibu: (a) Kwamba atapata mzao Mkuu ambaye Baba yake atakuwa Mungu. taz. Mambo ya Nyakati 17:11-12. (b) Kwamba ahadi ya Mungu na Daud itaimarishwa katika mzao huu; ambaye ni Kristo. (Matendo 2:30) atakayetawala katika kiti cha enzi cha Daud (Zaburi 89:28, 34-36; 132:11). (c) Kwamba Kristo pia atakuwa Mwokozi mwenye haki (2 Samweli 23:3-5). (d) Kwamba Nyumba ya Kifalme ya Daudi itakuwa ni nyumba ya Mungu na Kristo ataimarisha nyumba ya kuabudu katika Sayuni. (1 Mambo ya Nyakati 17:10, 12, 16; Zaburi 132:2-3. taz. pia Isaya 2:2-3). -14- _______________________________ 12 Ufufuo, Hukumu na Uzima wa Milele _________________________________ 12.1 Biblia ina maana gani kusema ufufuo? Jibu: Wafu kurudi kwenye uzima tena, kama Bwana Yesu alivyofanya alipofufuka katika wafu taz. 1:5; Wakolosai 1:18; Matendo 26:23; 1 Wakorintho 15:20. 12.2 Ni lini ufufuo utafanyika? Jibu: Ni wakati atakaporudi Bwana Yesu duniani taz. 1 Wathesalonike 15:23. 12.3 Je Wale watakaofufuka makaburini, wataishi milele? Jibu: Hapana. Kwanza ni lazima watokee katika (miili yao ya nyama na damu) mbele ya Kristo, Hakimu mkuu wa wote, ataamua wale ambao wanafaa kwa uzima wa milele na wale wasiofaa. taz. Warumi 14:10; 2 Wakorintho 5:10; 1 Petro 4:6; Danieli 12:2; Ufunuo 20:11-15. 12.4 Je, mtu yeyote ambaye amepata kuishi atafufuliwa na kuhukumiwa na Kristo? Jibu: Hapana. Ni wale tu ambao wamejifunza ukweli wa Injili na kujua kwamba inawapasa kumtii Kristo. taz. Yohana 12:48; Kumbukumbu 18:18-19; Mathayo 25:14-30; Warumi 2:12, 16. -15- 12.5 Je, ni nini kinachotokea kwa wale wasio fufuliwa kutoka kwa wafu? Jibu: Hawatafufuliwa kamwe kutoka makaburini mwao, watabaki wafu milele na milele. taz. Zaburi 49:20; Mithali 21:16; Isaya 26:14; Isaya 43:17. 12.6 Nini kitatokea kwa wale walio hai wakati atakaporudi Bwana? Jibu: Wale wanaopaswa hukumu watakusanywa na malaika kuonana na Kristo, sawa na wale walio fufuliwa kutoka kwa wafu. Halafu hukumu itafanyika. taz. 1 Wakorintho 15:51; 1 Wathesalonike 4:16-17; Mathayo 25:31-32. 12.7 Nini kitatokea kwa wale ambao Bwana atawakubali wakati wa hukumu? Jibu: Watapewa uzima wa milele, ambao watautumia duniani, katika ufalme wa Kristo. taz. Danieli 12:3; Mathayo 25:20, 21, 34; Danieli 7:27; Ufunuo 5:10; Mathayo 5:5. 12.8 Je, Biblia inaahidi huwa wakristo waaminifu watakwenda mbinguni? Jibu: Hapana. Kama tulivyoona, Biblia inaahidi kuwa wafuasi waaminifi wa Yesu wataishi milele duniani. Biblia pia inaeleza kuwa hakuna hata mmoja aliyepata kwenda mbinguni, isipokuwa Yesu taz. Zaburi 115:16; Matendo 2:34; Yohana 3:13. Angalia: Vifungu vichache vya Biblia mara nyingine vinadhaniwa kuwa vinafundisha kwamba wakristo wameahidiwa uzima wa milele mbinguni. Lakini yote yanaweza kuonyeshwa kukubaliana na mafundisho yote ya Biblia. Mfano (Nyumba ya Baba yangu), katika Yohana 14:2 haiko mbinguni. Nyumba ya Mungu imo hekaluni, kama vile Yohana 2:16 anavyotuonyesha. Hekalu kuu zaidi ya yote ni hekalu la kiroho, na waumini ni nguzo ya maisha katika nyumba kuu ambayo inaendelea kujengwa (taz. 1 Petro 2:5) kwa hiyo nyumba ya Mungu ipo -16- hapa duniani, na kwa jinsi hii Bwana Yesu anasema (katika kifungu kifuatacho - Yohana 14:3) "Nitakuja tena ni wakaribishe kwangu, ili nilipo mimi nanyi muwepo" 12.9 Ni jambo gani litakalowatokea wale ambao Bwana atawakataa? Jibu: Watajikuta wanahukumiwa na Kristo, wataona wenye haki wakiingia katika ufalme wake Kristo, wakati wenyewe wamefungiwa nje. Hatimaye na kupata kifo cha milele kifo cha mara ya pili Ufunuo 2:11 na Ufunuo 20:14, ambapo hakutakuwapo kuamka tena taz. Luka 13:28, Mathayo 22:13; Mathayo 25:46; Zaburi 145:20. 12.10 Kwa nini vifungu vingine vinasema kuwa wale ambao watakataliwa na Kristo watatupwa katika Ziwa la Moto? Jibu: Ufunuo 20:14 unatueleza kuwa ziwa la moto ni sawa na kifo cha mara ya pili. Watu wanatumia moto kuteketeza takataka. Katika Biblia, Mungu anazungumzia moto katika kielelezo, kuonyesha kwamba wale ambao hawafai watateketezwa kabisa. taz. Zaburi 37:20; Zaburi 68:2; Mathayo 3:11-12; 2 Wathesalonike 1:7-9. _________________________________ 13 Roho Mtakatifu _________________________________ 13.1 Roho mtakatifu ni nini? Jibu: Roho mtakatifu (mara nyingine huitwa kwa kiingireza "The Holy Ghost" na mara nyingine Nguvu ya Mungu "The Spirit of God"). Hii ni namna ya kuieleza Nguvu ya Mungu. Kwa Nguvu ya Mungu aliumba dunia. Kwa Nguvu yake Mungu ndiyo iliyo sababisha Yesu kuzaliwa. Kwa Nguvu yake Mungu iliwafanya Manabii na -17- Mitume kuandika maandiko matakatifu. Kwa Nguvu ya Mungu, Mungu yuko mahali popote na anayajua yote tunayotenda, na tunayowaza na kusema. Kwa Nguvu yake, Mungu atawafufua wafu kwenye uzima tena atakapo kuja Yesu. Nguvu hii ya Roho ya Mungu inaitwa takatifu "Holly" wakati inapotumika kwa kazi maalum yake Mungu kwa kutoa maandiko matakatifu na watu watakatifu. taz. Luka 1:35; Luka 24:49; Matendo 1:8; Mwanzo 1:2; Ayubu 33:4; Zaburi 139:1-14; Warumi 8:11; Matendo 7:51. 13.2 Vipawa vya Roho ni nini? Jibu: Vipawa vya Roho ni Nguvu ambayo Mungu aliwatolea baadhi ya watumishi wake na mara baadaye ya siku za mitume. Kwa njia ya nguvu hizi, wateule waliweza kusema na kuandika maneno ya Mungu, na kutenda miujiza. Vipawa vya Roho vilihusisha utume, unabii, uponyaji, na "kusema kwa lugha" (Ndiyo kusema, waliweza kusema lugha zinginezo bila kupata kujifunza). Vipawa hivi vilisaidia kanisa katika wakati wa matatizo ya aina yake. Kwa njia mbili vipawa vilirahisisha Injili kueneza mbali. Kwanza kabisa, Wahubiri wakristo waliweza kutangaza neno la Mungu kwa nguvu na ushujaa katika lugha nyingi mbalimbali pili waliweza kuimarisha ujumbe wao kwa miujiza mikubwa. Vipawa pia viliwezesha Agano Jipya kuandikwa na Kanisa la Ki-Kristo kuimarishwa kwa nguvu katika Agano la Kale. Nyakati za Musa Elia, Elisha na wengineo walikuwa na Nguvu zile zile. Paulo alifundisha kuwa wakati utakuja ambapo vipawa hivi vya Nguvu vitaondolewa. Hii ilitokea wakati wa Kanisa la Kristo lilipoanzishwa, na Agano Jipya lilitimia kuandikwa. Hii ndiyo maana hakuna mtu yeyote aliye na vipawa hivi leo. Wakati Bwana Yesu anarudi duniani watumishi wa Mungu kwa mara nyingine watapewa vipawa vya Roho. taz. Matendo 2:1-17; Joel 2:28-29; 1 Wakorintho 12:7-11; Warumi 15:18-19; Zaburi 105:26-27; 2 Wafalme 2:9-15; 1 Wakorintho 13:8-11; Waebrania 6:4-5. -18- 13.3 Tusemeje watu wanaodai kutenda miujiza na kusema "kwa Lugha" leo? Jibu: Ni walimu wadanganyifu ambao hawatendi kwa nguvu ya Mungu. Tena ni walaghai wa kuwaangalia, na mara nyingi hujidanganya wenyewe wamekuwa kama manabii wa uwongo na watenda mazingaombwe, wanaodai kutenda miujiza katika siku za Musa, Yesu na Mitume. taz. Kutoka 7:11, 12, 22; Luka 11:19; Matendo 8:9-11; Mathayo 24:24. 13.4 Je, Roho Mtakatifu wa Mungu anatenda kazi Leo? Jibu: Nguvu ya Mungu siku zote inatenda. Kila mara, kwa wokovu wa waume na wake. Inatenda katika neno lake, Biblia ambayo ni nguvu na ni maisha Yohana 6:63. Wakati neno la Mungu limechanganywa na imani katika moyo wa muumini inakuwa ni mbegu isiyoharibika, inayoleta zaidi, baraka kuu ya Mungu. Kuzaliwa upya kwa ubatizo (1 Petro 1:23-25, 1 Petro 2:1-3) kwa jinsi hii tunaingia ndani ya maisha ya Roho. Hivyo kupata kuwa wake Mungu na maombi kupitia katika Yesu Kristo na kupata nguvu kila siku ya maisha na kutii katika amri zake Mungu (Waebrania 2:18 na Waebrania 4:16 na Warumi 8:26-28) Mungu ameahidi kwamba kamwe hatathubutu kutuacha au kutukataa Waebrania 13:5-6. _________________________________ 14 Malaika _________________________________ 14.1 Malaika ni Nani? Jibu: Malaika ni watumishi wa Mungu wasiokufa. Malaika walimlinda Abraham, Isaac na Yakobo. Malaika walimpasha habari Loti kuhusu hukumu ya Mungu juu ya Sodom. Malaika walimpatia -19- Musa sheria za Mungu. Malaika walitoa habari za kuzaliwa kwake Bwana Yesu Kristo kwa wachungaji wa mifugo. Malaika wasioonekana wanalinda watumishi wa Mungu leo. Malaika watamsaidia Bwana Yesu Kristo atakapo kuja kuhukumu. taz. Luka 20:36, Zaburi 103:20; Mathayo 24:31; 2 Wathesalonike 1:6-10. _________________________________ 15 Dhambi, Shetani na Ibilisi _________________________________ 15.1 Dhambi ni Nini? Jibu: Tuna tenda dhambi wakati tunapovunja amri ya Mungu taz. 1 Yohana 3:4. 15.2 Je Ninani anaye tujaribu kutenda dhambi. Jibu: Majaribu ya dhambi yanatokana na mawazo yetu sisi na mwili, tunajaribiwa na asili yetu sisi wenyewe. Mtume Paul aliita sheria ya dhambi ndani ya mwili wake. Mara nyingine watu wengine hutushawishi kutenda dhambi tokana na asili yetu taz. Yakobo 1:14-15; Marko 7:21-23; Yeremia 17:9; Warumi 7:18-25; Warumi 5:12; Mithali 1:10. 15.3 Ibilisi ni Nini? Jibu: Ibilisi ni namna ya kielelezo cha dhambi ya asili. Kutobadilika kwa asili yetu hakumpendezi Mungu. Anaonyesha kwa kuita Ibilisi. Watenda dhambi mara nyingine pia huitwa Ibilisi. taz. Yohana 6:70; Yohana 8:44; 1 Yohana 3:8; Ufunuo 2:10. -20- 15.4 Kunatokea Nini kama tunatenda dhambi na kuishi katika maisha ya dhambi? Jibu: Tutakufa. Ndiyo maana Biblia husema kwamba Ibilisi (asili ya dhambi) ina nguvu ya kuleta kifo. taz. Warumi 6:23; Waebrania 2:14. 15.5 Yesu alifanya nini kwake Ibilisi? Jibu: Biblia inasema kwamba Bwana Yesu alimvunja Ibilisi. Hii inatuhakikishia kuwa Ibilisi hawezi kuwa jitu kubwa la ajabu aishiye leo. Bwana wetu alikuwa na mwili kama sisi, na alijaribiwa kama sisi. Hii ina maanisha kuwa Bwana Yesu alishindana na Ibilisi (mawazo yake mwenyewe) kama tunavyofanya. Lakini si kama sisi, Bwana alishinda kila jaribu, hata siku moja hakushindwa jaribu, na Ibilisi alishindwa. Tangu Yesu Kristo kupaa kutoka kwa wafu, alikuwa na mwili usio wa kufa na usio pata majaribu. Kwake eye, Ibilisi dhambi ya asili imevunjwa na imekufa. taz. Waebrania 2:14; Waebrania 4:15; Warumi 6:6-10; 1 Yohana 3:8. 15.6 Nini maana ya Shetani? Jibu: Ni neno la kiebrania likimaanisha adui Agano la Kale liliandikwa kwa kiebrania. Mara nyingine inatafsiriwa "adui" au "mpinzani", au katika kitabu cha Biblia King James imetafsiriwa mpinzani na mara nyingine linatumika kama jina. Petro alimpinga Bwana Yesu. Ndipo Yesu aliposema "Rudi nyuma yangu, Shetani". Dhambi yetu ni adui mkubwa wa Mungu (na pia kwetu), hivyo Agano Jipya ina taja "Shetani" katika sehemu nyingi. Watenda dhambi pia huitwa mashetani, katika vifungu, taz. Matendo 5:3-4; 1 Wathesalonike 2:18; Mathayo 16:23; 1 Timotheo 1:20. -21- Angalia: Kuna vifungu vichache vya Biblia vilivyoeleweka kufundisha kama Ibilisi mweza aishye, lakini kwa jinsi hii inatokana na usomaji mbaya wa Biblia. Mfano, "Lucifer" katika Isaya 14:12 si malaika mtenda dhambi. Ni mfalme wa Babeli, mtu mbaya, katili na mwenye majivuno. Soma kifungu chote ukianza kifungu 4. Kadhalika mzuri kama malaika aliyepakwa mafuta katika Ezekieli 28:14. Si malaika mtenda dhambi. Ni mfalme wa Tiro - kifungu 12 kinaonyesha hivyo. _________________________________ 16 Maibilisi na Mapepo _________________________________ 16.1 Ni nini maibilisi na Mapepo? Jibu: Katika Biblia, ugonjwa - na hasa wa akili unaitwa "maibilisi" au "mapepo" au "pepo wabaya" au "pepo wachafu". Watu walipo ponywa magonjwa pepo wachafu walisemekana walitolewa. Mara nyingine "pepo wachafu" ina maanisha watenda dhambi. taz. 1 Samweli 16:14; Mathayo 8:16-17; Mathayo 12:22. 16.2 Wapagani wanaamini kuwa "mapepo wabaya" ni viumbe wasioonekana. Je, Mkristo amini haya? Jibu: Hapana. Baadhi ya makanisa hufundisha imani hii ya kipagani, lakini si kweli. Biblia haifundishi hivyo. Biblia inasema Mungu ni Bwana wa ulimwengu wake. Hakuna mapepo hai isipokuwa Mungu, Bwana Yesu, na Malaika wa Mungu. Malaika hutenda kazi sawasawa kwa mapenzi yake Mungu. Hivyo hawawezi kutenda dhambi au kufa. Kama tulivyoona Ibilisi, Shetani na mapepo wabaya vinatumika kama ni kielelezo. Ni badala ya dhambi ya asili, na magonjwa, ambavyo ni matokeo ya hali ya dhambi zetu. taz. Isaya 45:5-7; Amos 3:6; Mathayo 6:10. -22- _________________________________ 17 Njia ya Uzima wa Milele _________________________________ 17.1 Ninataka kuishi milele katika ufalme wa Kristo. Nifanye nini? Jibu: Ni mambo manne: (a) Ni lazima uamini kwa moyo wako wote katika mafundisho ya Biblia. Hii inawezekana tu kama ni mpenda kusoma wa mara kwa mara Biblia. Soma kila siku. tazama 2 Timotheo 3:14-17. (b) Ni lazima "utubu". Hii ina maanisha kwamba ni lazima ukiri kweli kuwa umekosea na mwenye dhambi, ni lazima umtafute Mungu kupitia Yesu Kristo, aweze kusahau dhambi zako; na lazima umwahidi Mungu kuwa utajaribu kuishi maisha mazuri kwa wakati wote. taz. Matendo 3:19. (c) Ni lazima ubatizwe. taz. Matendo 2:38-42. (d) Ni lazima maisha yako yote uyatumie kutii amri zake Bwana Yesu Kristo. taz. Warumi 2:7. _________________________________ 18 Ubatizo _________________________________ 18.1 Ubatizo ni nini? Jibu: Ubatizo maana yake ni "kuzamisha". Unahusisha kuzamishwa kwa mtu kabisa ndani ya maji. taz. Mathayo 3:13-17; Marko 1:9-10; Yohana 3:23; Matendo 8:36-39. -23- 18.2 Nini maana ya Ubatizo? Jibu: Una maana mambo mengi. (a) Unatukumbusha kuwa Yesu, alizikwa na kufufuka tena, na hivyo ina onyesha kuwa tunaweza kuokolewa kupitia kifo chake na ufufuo. taz. Warumi 6:3-4. (b) Unatukumbusha kuwa sababu tuwatend adhambi, tunastahili kufa (kama tukizamishwa ndani ya maji ni lazima tufe). taz. Warumi 6:5-7. (c) Unatukumbusha kuwa sababu Mungu ni Mwenye huruma, anataka atukomboe tokana na dhambi kwa ufufuo. Ubatizo kwa hiyo ni namna ya "kifo" - kuzikwa ndani ya maji na namna ya "Ufufuo". Ni kitendo dhahiri. taz. Wakolosai 2:12-13. (d) Unatukumbusha kuwa kama vile maji yanavyosafisha uchafu, vivyo hivyo Mungu hutuondolea mbali dhambi kwa wale ambao humtii yeye. Tunapobatizwa Mungu husamehe wote sisi na dhambi zetu tulizofanya. Hivyo basi tuna kuwa wapya kama wanafunzi wa Yesu Kristo - taz. 1 Petro 3:21, Matendo 22:16. (e) Ni ishara ya kuwa wana wa Mungu na mwili wa mbegu ya Abraham ndani ya Yesu Kristo katika agano la milele. taz. Wagalatia 3:26-29. 18.3 Je lazima tubatizwe? Jibu: Ndiyo Bwana Yesu alibatizwa, waumili wa kwanza katika kanisa walibatizwa, kama ilivyo amriwa na Bwana Yesu. Ubatizo ni kitendo cha utiifu. Ni lazima tubatizwe sababu Mungu ameamuru sisi tubatizwe. taz. Mathayo 3:13-17; Matendo 2:37-41; Matendo 22:13-16; Wagalatia 3:27-29; 1 Petro 3:21. 18.4 Je tunaweza kubatizwa kabla hatujaelewa Injili? Jibu: Hapana. Ni lazima tuelewe kwanza Injili, ndipo tuiamini; halafu mara tubatizwe. tazama Marko 16:16; Matendo 8:12. -24- 18.5 Je Biblia inasema watoto wabatizwe ? Jibu: Hapana, watoto hawawezi kuamini, hivyo hawawezi kubatizwa sawasawa. taz. Matendo 8:12 na angalia maneno haya "walipo amini" na "wote waume na wanawake". 18.6 Je ni sawa kubatizwa kwa maji ya kunyunyiza au kumwagilia mtu maji? Jibu: Hapana. Bwana Yesu na wanafunzi wake walizamishwa ndani ya maji, hivyo nasi inatupasa kuwa. taz. Mathayo 3:16; Matendo 8:38-39. _________________________________ 19 Maisha ya Mkristo _________________________________ 19.1 Je, Wakristadelphian wanashiriki chakula cha Bwana? Jibu: Ndiyo wanakawaida ya kumega mkate Matendo 2:42. Bwana Yesu ametuamuru tumege mkate mara kwa mara tukiwa pamoja na kunywa divai kwa kumbukumbu ya kujitoa dhabihu hadi atakapo rudi tena. Mkate umekuwa badala ya mwili na mvinyo ni badala ya damu yake. taz. 1 Wakorintho 11:26; Yohana 6:53-56. 19.2 Kwa nini inatulazimu tumege mkate na kunywa divai? Jibu: (a) Tunapo kuwa tumebatizwa huku ni kuzaliwa upya. Mtoto mchanga anahitaji chakula kwa wakati wowote. Kumega mkate ni kielelezo cha chakula ambacho kina tupatia chakula cha roho. (b) Katika Ubatizo dhambi zetu zimesamehewa udhaifu wa asili hauwezi kuepuka dhambi. Kazi ya kumega mkate ina tuuganisha tena katika kujitolea kwa Kristo na kufanywa wapya na msamaha wa dhambi. -25- (c) Kwa kumega mkate tunakumbushwa unyenyekevu tulio fanya wakati wa ubatizo. Ni wakati wa kujitoa wakfu. Na inatukumbusha kuwa Yesu atarudi tena. (d) Pia ina tia nguvu ushirika wetu wa kiroho pamoja na wa waumini wenzetu. taz. 1 Wakorintho 11:23-29; Mathayo 26:26-28; 1 Wakorintho 10:16-17; Matendo 2:42,46. 19.3 Je, lazima tumege mkate na kunywa divai katika siku yoyote maalum. Jibu: Hapana. Kumega kwa mkate kulielezwa siku ya juma jioni. Yesu alisema, inatupasa kuiweka mara kwa mara, lakini hakusema mara ngapi au siku gani wanafunzi wa mwanzo waliweka siku hivyo katika siku ya kwanza ya Juma - Jumapili. Kwa maana wengi wao siku hii bado wameona ndiyo siku inayofaa. taz. Matendo 20:7; 1 Wakorintho 11:25-26 19.4 Ni kazi gani zingine za Kristadelphian (Ndugu katika Kristo) wanazo zifanya? Jibu: Mikutano ya mahubiri ya Injili ya kweli na mikutano ya kujifunza Biblia. Mikutano ya Kristadelphian kawaida inajumuisha nyimbo tatu au nne, sala mbili na kusoma Biblia sura moja au mbile. 19.5 Je ni muhimu kuitukuza Siku ya Sabato? Jibu: Hapana. Amri ya kuwa na siku ya Sabato (Jumamosi) kama ni siku takatifu ilikuwa ya nne katika amri kumi, Amri, zingine tisa zote zimerudiwa kutajwa katika Agano Jipya, hivyo ni muhimu kwa Wakristo. Lakini Bwana Yesu na wanafunzi wake, hawajawahi fundisha kwamba Wakristo wanapaswa kuweka siku ya Sabato. Amri ya Musa ilifutwa baada ya kufa kwa Yesu Kristo. tazama Kutoka 20:10; Wagalatia 5:1-4; Warumi 14:5; 2 Wakorintho 3:3-11; Wakolosai 2:14. -26- 19.6 Ni mara ngapi Mkristo anapaswa asome Biblia yake? Jibu: Kila siku, ikiwezekana, wale wasioweza kusoma ina bidi waende kwa ndugu aliye jirani atakaye weza kusoma, ili waweze kusikiliza Biblia inavyosomwa. tazama Matendo. 17:11. 19.7 Ni maisha gani Mkristo anapaswa kuishi? Jibu: Mkristo awe mkweli, mnyenyekevu, mwenye busara, mtulivu, mpole, mwema, mwenye bidii na mwaminifu. Maisha yake yawe safi na takatifu. Wake na waume wawe wapole na wapole na wa kweli kati ya mtu na mtu, kama Yesu Kristo alivyo mkweli na mpole kwa kanisa lake. Watoto lazima walelewe katika nyumba ya furaha na upendo wa wazazi. Ambayo watawafundisha kumtii Mungu. taz. Warumi 12; Wagalatia 5:22-23; Waefeso 4:20-32; 5:1-5; 22-23; 6:1-9; Wakolosai 3:12-25. 19.8 Biblia ina maana gani kusema Imani? Jibu: Imani ni uaminifu katika ahadi ya Mungu. Mfano, Nuhu aliamini kuwa Mungu ataangamiza ulimwengu kwa gharika; alionyesha uaminifu (imani) kwa kujenga safina. Mtu asiye na imani ni mtu ambaye hana matumaini katika Mungu; haamini kuwa Mungu ataziheshimu ahadi zake. Ndani ya moyo wake, mtu kama huyo Mungu anamwita mdanganyifu ambaye huheshimu ahadi zake na asitimize. Imani ni sehemu ya lazima kwa maisha ya Mkristo. Tukiamini kuwa dhambi zetu zitasafishwa katika Kristo, hivyo tutakuwa tumeonyesha imani yetu kwa kubatizwa. Iwapo tukiamini kuwa Mungu atamtuma Bwana Yesu ku-utakasa ulimwengu na ku-ujaza utukufu, hapo tutakuwa tumeonyesha imani yetu kwa kujiweka safi mioyo yetu, kuja kwake mara ya pili na kuombea kila siku. Si rahisi kuwa Mkristo bila kuwa na imani. taz. Waebrania 11:6-7, Yakobo 2:21-26; Wagalatia 3:6-9; 1 Yohana 5:10; Waefeso 2:8. -27- 19.9 Je Yampasa Mkristo aombe kila siku? Jibu: Ndiyo. Mungu anataka sisi tumwombe mara kwa mara. Yesu alitoa kielelezo kufundisha kuwa watu, "Wanapaswa kila mara kuomba na bila kupungua" Mkristo asiye omba mara hupoteza mawasiliano na Mungu. Bwana Yesu mara nyingine alitumia usiku wote kuomba. Maombi yawe ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu pia. Yesu Kristo ni mhubiri Mkuu katika uwepo wa Mungu, na tuna mwomba Mungu katika Kristo. taz. Luka 18:1; Mathayo 6:5-13; Luka 6:12; Yakobo 5:16; Waebrania 10:19-22; Warumi 12:12; Matendo 2:42; Ufunuo 5:8. 19.10 Je, yampasa Mkristo agombane na watu wabaya? Jibu: Lahasha, kamwe asithubutu, Bwana Yesu alizungukwa na watu wabaya, ambao mwishowe walimwuua. Lakini hakumwuumiza hata mmoja, na sisi pia tusithubutu kumwuumiza yeyote hata kwa kujitetea. taz. Luka 9:54-56; Mathayo 26:51-52; Mathayo 10:16; Mathayo 5:38-48; Warumi 12:18-21; 2 Timotheo 2:24. 19.11 Je, Mkristo awe na ushauri gani juu ya sheria ya nchi anayoishi? Jibu: Iwapo sheria hizo haziendi kinyume na sheria ya Mungu, Mkristo anapaswa kuzitii mara kwa mara na kuheshimu sheria za Taifa. Mkristo anapaswa kuwa mzuri, raia mwema. Hata hivyo, kama serikali imetoa sheria inayokwenda kinyume na sheria za Mungu (mfano kama tumeamriwa kuomba miungu au kujiunga na jeshi) hapo ni lazima tutii Mungu kuliko watu. taz. Matendo 5:28; 3:1; Warumi 13:1-3; Luka 20:25. -28- 19.12 Je, Mkristo yampasa kujiingiza katika siasa ili kusaidia maendeleo ya nchi yake? Jibu: Hapana. Bwana Yesu hakuthubutu kusaidia kutawala nchi yake. Alishinda majaribu ya kumfanya yeye awe mtawala, na alikataa utawala juu ya wengine. Bwana alijua kwamba ufalme wake (haukuwa wa ulimwengu huu) na kwamba kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuihubiri Injili. Mkristo awe mwangalifu kutojiingiza katika mambo ya ulimwengu. Mara nyingine serikali inaweza ikafanya, mambo ambayo Mkristo hawezi kusaidia kwa mfano kwenda vitani, au kukuza kamali. Kwa jinsi hiyo mkristo, anapaswa ajiepushe na mambo ya watu, na atoe nguvu zake kuhubiri Injili na kufanya mazuri kwa wenye shida; huu ulikuwa mfano uliotolewa na Bwana Yesu. tazama Yohana 6:15; Luka 12:14; Yohana 18:36, 2 Timotheo 2:4. 19.13 Je, yampasa Mkristo kuwasaidia wale washindanao kupata madaraka katika siasa kwa kupiga kura? Jibu: Hapana. Kupiga kura kwa mtu kunaonyesha kuwa anapenda siasa, na Mkristo asipendelee siasa. Mkristo akubali viongozi wowote Mungu amewaruhusu kuchaguliwa, na kuomba kuwa Mungu atawasaidia wao kutawala kwa hekima taz. Danieli 4:25; Mithali 21:1; 1 Timotheo 2:1,2. 19.14 Je, kuna aina fulani ya kazi ambazo Mkristo anapaswa ajizuie. Jibu: Ndiyo. Mkristo anapaswa kuacha kazi yoyote ile ambayo anaweza kutumia nguvu juu ya mtu mwingine (kama vile jeshi au polisi) asijihusishe na sehemu yoyote ambamo muna kiapo cha utii: Mkristo hapaswi kutoa kiapo cha uaminifu kwa mtu yeyote, maana uaminifu wake ni kwa Kristo. Mkristo yampasa pia aepukane na mambo yasiyo ya Kristo, mfano kufanya kazi katika mashirika ya Kamali, au katika kiwanda cha silaha, au sehemu ambayo inywaji vikali vinauzwa au duka linalouza vitabu vibaya. taz. 1 Timotheo 5:22; 1 Wathesalonike 5:22. -29-