_____________________ WARAKA WA MTUME PAULO KWA WAGALATIA SURA SITA The Letter of Paul to the Galatians - Chapter Six _____________________ KUTENDA MEMA (6:6 - 10) Mgawanyiko wa waraka katika aya ya 5 unafuata mpangilio wa fungu la maneno ya U.V. ingawa mengine yanaunga aya ya 6 kwa karibu na aya ya 5. Aya ya sita inachukuwa wazo la aya ya 2 kuhusu kuchukuliana mizigo na neno linaloanza aya "lakini" (katika Biblia R.V.) linatujulisha kuwa namna nyingine kabisa; ikiwa namna nyingine kabisa ipo na aya ya 5, basi Paulo anasema ya kuwa wakati jukumu ni la kila mtu mmoja kwa tokeo la mwisho, kwa mahusiano yaliyopo hakuna tena umoja wa imani, lakini pia nafasi ya kutenda mema. Maneno yote ya kutiana moyo yanakuwa mbali mbali na onyo moja la mtu.. Tafsiri ya kawaida ya aya ni kwamba aliyeelimishwa katika injili wameamriwa kuwasaidia waalimu wao katika mambo ya dunia hii. Inadokeza ya kuwa walikuwepo watu wenye bidii sana au muda wao wote katika mafunzo ya mdomo kwa ndugu na dada - "mwanafunzi" ni neno la asili neno "catechumen". Paulo alitambua haki ya kupokea msaada wa vitu vya dunia hii kwa ajili ya kuhudumia mambo ya kiroho, ingawa yeye mwenyewe alikuwa na wivu wa kujitegemea, akipokea vipawa vya hiari toka kwa ambao ufadhili wao ulichipuka kutokana na upendo wenye shukrani, wakati uo huo akiwa makini asipokee toka kwa wengine. Mafungu yafuatayo ya maneno yanaonyesha uzito wake: 1 Kor.9:11; 2Kor.11:7; Flp.4:10; 1Thes.2:6,9; 1Tim.5:17,18. Msingi kabisa wa maisha ya Mkristo ni kufahamu kusudi la Mungu na mapenzi yake. Maandiko yaliyoandikwa kwa mkono yalipokuwa machache na mafundisho kwa upana yalitoka katika kumbukumbu, mafunzo kwa mdomo yalihusika kwa upana kuliko wakati kila mshirika alikuwa na nakala (kopi) ya Maandiko. Lakini mahitaji dhahiri katika siku za mwanzo kabisa ili kila Iklezia liwe na nakala za injili na nyaraka zilitaka kugawanya sehemu pana kuliko inavyofahamika mara nyingi, tunaamini, kwa suala la injili tatu za kwanza, kwa ajili ya taerhe za awali kwa kuchapishwa kuliko zilivyofungamana nazo kwa kawaida. Walakini sehemu iliyohusika kwa waalimu walioongozwa na roho katika ma-Iklezia ya miaka ya kwanza ya kazi za mitume hazina budi zilikuwa muhimu sana. (1) Hapana mfano wa mafunzo ulioshinda katika dini za kipagani. Tendo la sheria na si imani au mwenendo ilikuwa njia ya kupata kibali: na tendo la sheria liligeuza kazi ya makuhani ikawa ya kujipatia faida. Watu iliwabidi kulipia huduma zao kwa kumkaribia Mungu na kupata fadhila za Mungu. Katika Asia ndogo wakati mmoja vifuniko vya kichwani kwa makuhani vilifanyiwa mnada, ishara ya marejesho ya thamani kuchaguliwa namna hii ukuhani unatoa faida. Mtu anayeabudu alikuwa tayari kulipa, zaidi kama Katoliki wanavyolipa Misa, kwa sababu faida fulani zilidhaniwa hupatikana. Ikiwa mwalimu alitoa muda wa mafunzo kwa hasara ya muda wake wa kazi za kila siku basi alistahili kupata "vitu vya mwilini" vya huyo anayeelimika katika injili. Huyu mwanafunzi alisaidiwa kufikia faida ya milele kwa hiyo ilikuwa ni jambo dogo kuwa alipie vitu vya dunia. Ingawa tafsiri iliyo juu ni maneno yote ya Paulo, inaweza kuwa na shaka ikiwa yaonyesha maana yake; neno la muhimu "kushirikisha " limetumika kuwa na maana kuwapa wengine. Lakini neno lina maana shirikiana au kuwa mwenza na mwingine katika shughuli fulani au mali. "Mambo yote mema ambayo ilibidi kushiriki yaweza kuwa matendo mema vile vile kama chakula kizuri. Basi amri ya kuifuata ni kwa wote, ikiwa ni mwalimu au wanafunzi, yawapasa kufanya kazi pamoja wakiwa ni washirika wenza katika kutenda mema, kwa kuchukuliana mizigo (aya ya 2), na kwa kumsaidia mkosa (aya ya 1). Shughuli ya kuheshimiana wao kwa wao katika matendo mema, iwe ni kusaidiana vitu vya mwilimi, katika kazi ya Iklezia, au katika faraja za kiroho, ni dawa ya maana kwa kutokuwa rafiki na kujitosheleza binafsi ambako kumetajwa katika aya ya 3. Mtazamo wowote wa aya ya 6 ukichukuliwa hakuna kukosea somo lote la aya ya 7 na 8. ":Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atachovuna. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele." Mtu mwenye cheo na anayepanda kwa unyimifu anavuna kwa kunyimwa, Mtu aonyeshaye imani kali katika dini ambayo inahusika na uchumi ni kujisingizia, na kumtolea Mungu matoleo ambayo ni ya uwongo, Mtoaji atajidanganya mwenyewe; hivyo onyo ni: Maana Mungu hadhihakiwi, na kanuni za sheria ya Mungu. "Mtu mkarimu anavumbua upaji wa vitu, na kwa upaji wa vitu atasimama:. Ni kanuni iliyorahisi kujifunza katika ulimwengu wa asili (2) Zabibu hazikusanywi katika miiba; na watu wapandao uovu wanavuna uo huo. Kupanda na kuvuna kwa asili kunahusika na wakati tulio nao sasa. Mvivu asiyelima kwa sababu kuna baridi, hana mavuno mwishoni mwa msimu. Mtu anayeacha magugu kwenye njia zao, hatavuna mazao mazuri. Lakini matendo ya watu sio tu yana ushawishi wakati uliopo, bali yanahusu wakati ujao Mungu atakapotoa thawabu zake. Kwa mtu ambaye alijua wajibu wake kwenye siku ya mavuno ya Mungu itadhihirika upandaji wake ulikuwa wa namna gani. Kuna aina mbili za upandaji - matendo yanayohusika na makonde mawili ya maisha: mwili na roho. Mtu hupanda katika mwili anapojitumikia mwenyewe, anapoishi maisha yake kwa kujifurahisha na matakwa ya kila siku. Mwili unahusika na wakati tulio nao sasa, katika utaratibu wa vitu vya dunia hii, vinavyopita. Hakuna tumaini la matokeo yoyote ya milele katika mwili; kama maji yasivyoweza kuinuka juu zaidi kuliko chanzo chake, wala mwili hauwezi kutoa chochote kilicho na ubora wa kudumu. Mambo yote ya mwili yatapita. Roho kama tulivyoona, imetumika katika mlango wa 5 ni maisha mapya katika Kristo, na maisha haya mapya yanachipuka katika mbegu isiyoharibika, neno la Mungu, lililo hai lidumulo milele (Pet. 1:23). Maisha mapya kama yakiendelezwa kwa bidii kwa kulelewa vizuri huzaa tabia kwa huruma ya Mungu yenye msingi mwingine wa kuishi maisha ya milele. Kwa rehema ya Mungu- maana hatuwezi kupata uzima, lakini tunaweza kuifuatia haki ili kwamba taji ya haki ikitolewa itakuwa ni kukaribishwa, ya kushukuru, na kipawa kinachofahamika. Mtu wa mwilini anayelima shamba la mwili wa nyama na damu, atajiona mgeni katika ulimwengu wa roho. Lakini maisha ya kiroho sasa yataonekana kuwa yalikuwa yanahitajika sana maandalio kwa uzima wa milele utakaotolewa siku hiyo Mungu atakapohukumu siri za wanadamu kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa kuwa mwili wa damu na nyamu daima unaendeleza matakwa yake, wa roho unaweza kulegea kama hautiwi nguvu. Mtume anaweka uhakika wa thawabu ya wakati ujao kama mvuto wa kuendelea kutenda mema. "Tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tisipozimia roho". Bwana akiwa moyoni (akilini) kama mvunaji, na hakikisho la matokeo katika upandaji mzuri, maonyo yanakamilika na maneno yanayofaa kwa wakati: "Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio. (3) SEHEMU YA TANO - MWISHO. MAANDIKO YA MKONO WAKE (6:11-18) " TAZAMENI NI KWA HERUFI GANI KUBWA NIMEWAANDIKIA KWA MKONO WANGU MIMI MWENYEWE". Na mwanzo wa maneno haya Paulo anaanza kuifunga sehemu yake ya mwisho: na eneo pana la kufikiria wamelipata hao waliojaribu kutoa tafsiri ya Paulo. Mashauri ya maelezo ya mambo ambayo Paulo aliumwa kutokana na udhaifu wa macho juu ya maono yake ya Bwana mfufuka ushahidi mmojawapo unapatikana hapa, unakisiwa ya kuwa aliandika waraka wote yeye mwenyewe kwa herufi zisizo nzuri sana. Deissman amepata ufafanuzi wa maneno ya kuchekesha, kama ya mwalimu mkuu na watoto ambao wamemuudhi, kidokezo ambacho kinaonyesha kupima barabara na Ramsay kuwa ni "dini safi ya kufurahisha yenye mwisho mzuri". Inaweza kugundulika kwanza kuwa ilikuwa mazoea ya Paulo kusoma wazi na mwingine akiandika kwa kuongeza kuandika herufi kwa mkono wake mwenyewe akitia mbaraka. "Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mimi mwenyewe, hii ndiyo alama katika kila waraka, ndio mwandiko wangu"(2Thes. 3:17). "Salamu zangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mimi mwenyewe. Kumbukueni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi" (Kol.4:18). Tazama pia 1 Kor.16:21. Hata usipokuwepo hivyo ushahidi wa uandishi wake mwenyewe Paulo, uliongozwa kwa taarifa ya kwamba ilikuwa desturi yake tunaweza kuona uhakika wa kwamba maneno yanayofunga ya nyaraka zingine ziliandikwa na Paulo mwenyewe. Ndipo Paulo , kwenye aya ya 11, akatwaa kalamu mkononi, na kwa herufi kubwa akaandika maneno ya kumalizia. Kama jinsi hii haikuwa kawaida ni wazi katika ukweli wa kwamba anataka itazamwe. Maneno haya ya mwisho yalibeba nini? Ramsay anaonyesha mifano katika Pisidia ya Antiokia na Pompeii ya desturi ya kusisitiza maana muhimu kwa kutumia herufi kubwa.Werevu wa kuchapa kwa njia hii unatumika leo kwa matangazo yanayoonekana. Kama jambo lipo hivyo, ni sentenso zinazokamilisha barua jinsi hii kama inavyoweza kusisitizwa hivyo? (4) Tunaona ni maelezo mafupi ya kile alichukuwa akisema katika waraka wote, na kwa kufaa kabisa yaweza kupewa mkazo wa jinsi hii. Lugha imenyooka na inalenga tukio kwa maneno machache. Wayahudi kwanza wamelaumiwa kwa kuwa na mpaka katika mtazamo wa kimwili. "Wote watakao kuonekana ni wazuri kwa mambo ya mwili, ndio wanaowashurutisha kutahiriwa". Hapakuwepo kutambua mambo ya kiroho, waliwaza tu utu wa nje, wa kanuni ya dini na si maana yake. Ndipo Paulo anawapa azimio lao. Msimamo wao haukusimama kutoka katika upande wa Torati, lakini "makusudi wasiudhiwe kwa ajili ya msalaba wa Kristo, hilo tu." Ni wazi Wayahudi waliogopa mateso kwa ajili ya kumwamini Kristo aliyesulubiwa; haikuwa hatari ya kuiwazia, kama alivvyoona mwenyewe Paulo akionyesha. Lakini kwa kusisitiza kuifuata torati sambamba na kuiamini injili, sababu ya chuki ya Wayahudi iliondolewa. Hivi walijihusisha zaidi na kile ambacho watu walidhania kuliko jinsi gani Mungu aliwaangalia; Walitaka kujipatia mema ya wakati ujao ila sio mambo magumu ya wakati uliopo leo. Yote haya lakini ni kujionyesha kimwili. Dini ya Kiyahudi ilikuwa na sehemi nyingine zisizo patana. Kwa kuwa, kujaribu kuwashawishi wengine kufuata torati walikuwa wanaishi bila kuangalia sheria, ni wazi maisha yao kwa utu wa nje hayakunyooka. "Kwa maana hata wao wenyewe waliotahiriwa hawaishiki sheria; bali wanataka ninyi mtahiriwe, wapate kuona fahari katika miili yenu"(aya ya 13). Kwenye sehemu ya pili ya aya inaonyesha ya kuwa kwa kuwashururtisha kutahiriwa watajipendekeza wenyewe kwa ndugu zao Wayahudi. "Kwa kweli", walisema tunamwamini Yesu, lakini shabaha ni kuwaleta watu wa Mataifa katika asili ya Wayahudi. Tunajaribu kuwavuta katika dini na kuwafanya waongofu wa Kiyahhudi wafuasi wa Kristo". Lakini kumuungamia Kristo ilikuwa ni kukiri kuwa sheria haiwezi kuokoa, na kumhubiri Kristo na sheria wakati uo huo ilikuwa ishara ya kutokuwa wanyoofu katika maisha ya utu wa ndani. Paulo alitupilia mbali ujanja wa Wayahudi ili kudanganya kwa maneno na mkazo wa taarifa ya nafasi yake mwenyewe. "Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao ulimwengu ulisulubishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu" (aya ya 14). Kwa maneno haya Paulo anakana utukufu wake mwenyewe wote. (5) Amejifunza ni jinsi gani juhudi za mwanadamu hazina nguvu ndani yao wenyewe ili kupata kibali cha Mungu. Kumkaribia Mungu kwa msingi wa uzuri unaweza kuishia katika hukumu tu. Lakini katika msalaba wa Bwana Yesu Kristo (angalia jina kamili) mwili wa nyama na damu uliwekwa kando, Mungu akatukuzwa.Ulimwengu (ulikuwa ulimwengu wa Kiyahudi ambao ulitaka Yesu afe) ulifunua msingi wa uadui na Mungu, kama Yesu kwa maisha yake na mauti alidhihirisha mapenzi yake kukubali Mungu alivyomwamuru. Ulimwengu ukiisha funuliwa jinsi hasa ulivyo, hauna budi ufe; na kwa kadiri Paulo alivyohusika, maadamu mfano wa Yesu ulionyesha ya kwamba mwili wa nyama na damu inabidi usulubiwe, Paulo akaangalia ulimwengu wa mwili na damu kuwa umefanya kosa kubwa kwa kupata mwisho unaofaa msalabani. Nguvu ya ulimwengu juu yake hivi ikafikia mwisho; na kwa kuwa alisulubiwa na Kristo matakwa yake mwenyewe kuwa na vitu vya ulimwengu yaliondolewa. Kwa watu wa ulimwengu ni maelezo ya kweli, wanaupa heshima na utumwa. Ni hakika , unapita, tena unawadanganya ambao wanauabudu. Lakini kifo cha Kristo kilifunua nguvu yake inayodhihaki; na mtu akisulubiwa na Kristo anapita toka nguvu yake na kuona utukufu wake kuwa kitu kinachong'aa na utumishi wake kuwa utumwa. Mungu ni wa kweli na kumtumikia ndio msingi pekee wa wema unaodumu. Paulo kwa utajiri wa mawazo yake anaifikiria misalaba mitatu. Kristo, ulimwengu na Paulo, wote wamesulubiwa. Lakini ni Kristo tu aliyesulubiwa, lakini kwa kumpokea Kristo, Paulo amesulubiwa naye, na mwili wa nyama na damu (ambao ndiyo msingi wa ulimwengu) umesulubiwa kwa Paulo. Msemo wa Paulo basi ni ufafanuzi wa yale yaliyompata. Sehemu pekee na ya kuonea fahari ni kwa Kristo aliyesulubiwa; kuona fahari katika kitu chochote kingine ni kuona utukufu katika ulumwengu ambao umehukumiwa kwa tendo hilo kabisa la ulimwengu kumsulubisha Yesu. Kuukata mwili wa nyama na damu ni nini dhidi ya tukio la jinsi hii? Kutahiriwa si kitu, wala kutotahiriwa. Kunahusika na utu wa nje unaopita: wala haumfanyi mtu awe kiumbe kipya; pande zote mbili humwacha mtu kwa uadilifu si mwema wala mbaya sana. Lakini katika Kristo msulubiwa ulimwengu wa kale unapotea ili upya uweze kuzaliwa; na kama Kristo alivyofufuka kwa uzima mpya, unakuwa "viumbe vipya" kwa neema ya Mungu. Hapa ni kukuza tena, lakini ni utendaji wa Mungu katika Kristo usiopatikana popote mahali pengine. Mbali ya hivi, na nje yake, watu wapo mbali na Mungu, wageni wa mibaraka ya agano, kwa kimwili wanawekwa kando. (6) Kuwait na Kristo, na kutembea kulingana na kanuni hii, ya kuwa mwili hausaidii kitu na ni ukuzaji tu wa Mungu kupitia Mwana wake wa pekee unaofaa, watu wanatambua kuna amani na huruma, maana wao ni Israeli wa Mungu - walio watiishaji na washindi wa kweli, warithi wa mibaraka na ahadi, wafalme na Mungu. Sauti ya aya ya kumi na saba ni kali; inabidi isomwe na moyo wote na maombi yenye maono ya sura mbili za mwisho za waraka akilini. Pasipo shaka ni kadhia ya nguvu ya mamlaka yake akiwa ni mtume, na kwamba kile alichoandika si jambo fulani karibu wanaloweza kuliingia katika mashindano ya maneno. "Tangu sasa mtu asinitaabishe". Kuna wakati mashindano inabidi yakome; hata watu wadogo zaidi kama Paulo, na bila mamlaka yake, wanaona ya kwamba kwa muda yote yaliyokwisha semwa yanaweza kuwa na faida. Wapo watu wajifunzao muda mrefu bado hawafikii maarifa ya kweli. Kuna matendo wakati wa kazi ya kujenga na kuwatia nguvu wanaume na wanawake waaminifu katika Kristo, haina budi kuchukua nafsi ya kwanza; basi maneno ya Paulo kwa Wakorintho, "Lakini mtu akiwa mjinga, na awe mjinga" (1Kor.14:38), yanachukuwa maana isiyoeleweka kabisa katika hali zingine. Inahusu mamlaka ya utume kusema, "Mtu awaye yote asiyempenda Bwana Yesu Kristo na awe Anathema (amelaaniwa), Bwana anakuja"; lakina maana yake imeeleweka vema matatizo yanapojadiliwa katika waraka uliokamilika na hayo maneno, yakifahamika (1Kor.16:22). Ikiwa mtu awaye yote katika Galatia alitaka ugomvi basi haukuwa na Paulo ambaye wangeshindana naye. Aliwapa jawabu lenye mamlaka: na muhutasari ambao ulianza na waraka umesikika tena wakati wa kuufunga. Walakini anawakumbusha; kwa nini ananena hivyo; "kwa maana ninachukuwa mwilini mwangu chapa zake Yesu". Kule Antiokia alipata "mateso" ambayo yalipelekea afukuzwe katika mji. Tendo hili la mamlaka ya serikali karibu ni hakika lilifuatiwa na mapigo toka kwa maadui waliohudhuria mahakama. Pale Listra alipigwa mawe. Alama ya makovu na mateso mengine aliyostahimili kwa ajili ya Kristo, Paulo analinganisha na chapa walizochukuwa watumwa. Alama za makovu ya jinsi hii, yalivyosababishwa na kupigilia misumari mwili wa Kristo kwa jina la Bwana zilikuwa bayana, au kwamba mtumwa alifungamanishwa na ibada nyingine ya hekalu ambayo kwa mabadiliko ilimpatia ulinzi fulani. (7) Paulo alikuwa mfungwa, mtumwa wa Kristo, kwa huo, maneno ya Paulo ni wazi yanashuhudia maana yoyote kamili ambayo Paulo alikuwa nayo alikini. Anaziita alama hizi chapa zake Yesu. Hizi za pili zinaleta picha katika wazo la kwamba Paulo anafikiria uwiano kati alama zake na alama za majeraha katika mikono na miguu ya Yesu. Katika uwiano uliotegemezwa kwa 2 Kor.4 anazungumzia "kuchukuwa katika mwili kuuawa kwake Yesu, ili uzima wa Yesu nao udhihirishwe katika mwili wake" (aya ya 10); na kwa Wakolosai 1:24 anazungumzia "mateso ya Kristo" aliyoyatimiliza katika mateso yake. Ikiwa mawazo haya yalikuwapo katika akili yake hapa, basi kwa kutaja "chapa" anapatia wazo alilokuwa nalo zaidi ya mara moja aliloeleza la kusulubiwa na Kristo. Mawazo yote mawili yalikuwa kumbukumbu yenye nguvu kwa Wagalatia namna walivyompokea kama mjumbe wa Mungu. Mbaraka ni kifupi lakini kwa kushangaza umewekwa upande wa kazi muhimu. "Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu ndugu" (R.V.) "Neema", majina kamili ya Yesu, kutumia "roho" pamoja "nanyi" hukumbusha matumizi ya neno hapo awali katika waraka na mwisho, neno "ndugu", hukusanyika kwa neno la kuaga ujumbe wa waraka. Hivyo jitihada kuu ya kwanza inaisha kwa ajili ya "kweli iliyo kwa Yesu" katika kipindi cha Ukristo. Maana tunaweza kuwa na hakika ilikomesha ugomvi katika Galatia, kiasi kama mashindano ya maneno yote katika sheria ya Kiyahudi ya kuwatwisha Wakristo yalifikia ukomo. Namna ya uzushi hubadilika, lakini mambo makuu muhimu ya asili ya kweli hayabadiliki. Waraka kwa Wagalatia, kwa sababu hii, ingawa unafundisha mno na maono yaliyoletwa na matatizo, bado ipo hai na kunena kwake maneno wazi ya maneno ya Mungu ya asili kwa ajili ya vizazi vilivyohamia mbali kwa muda na nafasi katika Asia Ndogo jimbo la Galatia. Waraka umekuwa kama "moto ulio hai" mara kwa mara ukiwahuisha watu kwa kufikiri mambo muhimu wakati ushawishi wa kanuni ya ibada ulikuwa unaua maisha ya kiroho. Waraka unahifadhi uzima katika roho kwa wote kila nchi na muda kwa kila asomaye pamoja na moyo wa kuelewa. Mwisho (8)