_____________________ WARAKA WA MTUME PAULO KWA WAGALATIA SURA TANO The Letter of Paul to the Galatians - Chapter Five _____________________ SEHEMU YA NNE - IMANI NA UZIMA SIMAMENI IMARA KATIKA UHURU WA INJILI (5:1-12) SIMAMENI IMARA KATIKA UHURU WA INJILI ( 5: 1-12 ) Ingawa umefumbwa kidogo na mgawanyiko wa sura aya ya kwanza ya mlango huu ni wazi ni muunganiko kati ya kile kilichowekwa katika mlango wa 3 na 4, na kile kilichofuata. Wakati wengine wataona ya kuwa aya ni kama inamalizia mlango wa 4, kwa kweli unakusanya na halafu kuchukua kwenda mbele maneno ya mwisho. Paulo anasema: "Katika uungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa." Onyo lenyewe "Simameni imara" vile vile ni mwanzo wa ushauri wa kufaa msingi wake ukiwa juu ya mafundisho yaliyokwisha wekwa. "Kristo ametuandika (ametufanya kuwa) huru" ni taarifa isiyotakiwa kuiwekea mpaka katika maana finyu.Uhuru unaowezekana kwa Kristo ni kuona uadilifu sambamba na kutolewa utumwani toka kuhusiana na kufanya sheria. Ulimwengu wa Roma ulitumikishwa katika uovu na tamaa mbaya; ulimwengu wa Kiyahudi ulikuwa mzuri kidogo, ila mafundisho ya Kikristo, yaliaminiwa kwa moyo na kwa uaminifu, yalianza kwa nguvu inayofungua. Ni kweli kwamba kulikuwepo kuwekwa huru toka huduma katika Torati ya Musa, lakini hii ni sehemu ya ukombozi. Kwa nyongeza, kuliweza kufunguliwa toka katika gereza ambalo kwalo dhambi ilikuwa na nguvu kwa wafungwa wake - toka mauti yenyewe. Huu kwa kweli ulikuwa ukombozi, namna kama unavyowahusu wana wa muungwana (4:23,26,31), wana wa ahadi (4:23), wana wa Mungu (4:29). Uhuru ukitumika vizuri, ni kitu kizuri kurithiwa. Mungu amempa mwanadamu kufanya mapenzi yake, lakini pia amempa sheria za kutii. Mwanadamu katika ushirika anakuta ni lazima kufanya sheria kwa ajili ya utaratibu wa kufanya shughuli ya maisha ya watu wote; bali kwa kazi ngumu amejaribu kwa akili ya maarifa yake yote na kuonyesha ya kuwa kuunga maisha ya utaratibu wa kukaa kwa makundi ni nje ya uwezo wake. Kwa wengi uhuru unaeneleza kutofikiria sheria, na amri ni kurejea kwa usultani. Kwa upande mwingine ushawishi unaoharibu wa uwezo juu ya ndugu ya mtu umeonekana katika hali isiyo na utaratibu kwa nchi nyingi zenye mfumo wa serikali wenye chama kimoja umeanzishwa. Uhuru wa chochote lakini usiopunguza kwenda kwa taabu umeondolewa kwa mamilioni ya wanaume na wanawake wasiohesabika. Hata katika nchi zinazosaidia maisha zaidi zimezungushia boma kwa masharti kama Taifa na si mtu mmoja anachukuwa nafasi ya majivuno. Uangalifu wa kuwa watu yawapasa kulipia uhuru wenyewe hauwezekani katika idara nyingi za maisha kama mikono ya Serikali imewaleta watu ndani na kuwakamata sana. Uhuru wa dini umepata hasara na mengi zaidi katika sehemu nyingi za ulimwengu- si kwa mara ya kwanza. Utumwa katika eneo hili la maisha umetoka mara nyingi katika hao wanaojitoa kwa dini, walioweka maagizo na kujipatia ushuru wa roho za wanadamu. Mara nyingine watu wanaweza kuwa watumwa kwa mwili lakini wana roho zilizo huru; bali hakuna utumwa uliombaya kuliko huo unaozuia fikira na ibada. Lilikuwepo dai linaloonekana zuri lakini sivyo la Wayahudi kuwa Torati ilitolewa na Mungu. Ilikuwa hivyo; pia iliondolewa na Mungu - Yeye peke yake akiwa na uwezo wa kufanya hivyo. Iliondolewa kama amri ya maisha kwa watu na tendo halisi la utii wa Yesu Kristo kwa kujitolea kwake mauti, kama pazia lililopasuka katika Hekalu lilivyoonyesha. (1) Namna hii ndivyo ilivyopangwa na Mungu thamani ya uhuru. Kwa dhabihu ya Kristo ikieleweka kwa uzuri katika uhusiano wake na torati, kusingekuwepo hoja juu ya wajibu wa kuudumisha uhuru. Ikiwa hiyo mauti ya Kristo tu yaweza kuweka huru, basi watu wasingetafuta kuweka tena sheria, na hao waliokombolewa wataepuka kujitia katika matata yoyote tena katika kongwa lenyewe lililokuwa utumwa. Tayari tumeona kifani kinachotokeza kati ya kanuni ya matendo ya ibada ya kibinadamu na matendo ya Ibada yaliyotumiwa vibaya aliyotoa Mungu. Hivyo hawa Wagalatia wanaweza kusemwa kuwa wamejitia matatani tena kama uhuru wao walijiweka chini ya dini ya Kiyahudi. "Simameni imara"- watu wametafuta kuweka kosa kwa ajili ya kweli kazi ngumu ya hali ya kuwa mwana, kujiingiza katika hali ya amri inayokuwa vigumu kujiepusha kwa tendo la kutumia jambo binafsi. Hivyo, ingawa yaliandikwa kwa ajili ya kundi la Asia Ndogo la waamini waliovutwa na namna ya mafundisho yanayohusu matendo ya utu wa nje katika shindano la maneno lililopita zamani, jambo ni zuri hadi watu watakapofikia uhuru wa Utukufu wa wana wa Mungu (Rum.8:21). Kuna mkazo katika kujipenyeza wenyewe katika aya ya 2: "Tazama mimi, Paulo nawaambia". Hii ni kwa sababu gani? Jawabu linapatikana katika upotoshaji wa mafundisho yake na wapinzani wake. "Anakata", walisema; tohara katika suala la Timotheo si tohara ya Tito: kwa hivi kuhubiri kutahiriwa ilipomfaa. Shambulio analitupa nyuma: "Mimi", ambaye nashambuliwa kuwa mhubiri wa kanuni ya ibada, nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno". Kushika siku, miezi na miaka, kosa kama Paulo alivyoonyesha, bado ilikuwa maana ndogo ikilinganishwa na kuipokea tohara. Kanuni ya kuabudu ipo kinyume hasa kwa njia ya wokovu ulio kwa Kristo. Ni ya kimwili, inadokeza kuutumainia mwili na kuonyesha kutumainia kanuni ya ibada na matendo ambayo yaiweka kando imani. Lakini imani ni njia ya Mungu - njia pekee inayowezekana - na imani haipatani na tohara. Hakuna njia ya kati, ambapo mtu aweza kupata haki kwa imani na wakati uo huo akaifikia kwa matendo yake mwenyewe. Basi, kama waliifuata tohara, Kristo na kazi yake haifaidii neno; kwa kutenda kwao wenyewe walimweka kando Kristo katika maisha yao. Kufuata kanuni ya kuabudu ilikuwa kukiri kwamba kwao imani haikutosha , na maadamu Kristo na kazi yake kwa imani ina kusudi lake, vile vile kwa kweli inakana njia ya Kristo kuwa inatosha. Hakuna kilichobaki ila tendo la kukubali kabisa la kale la kutakiwa kushika kwa sheria, lisilofaa na kutia utumwani.. Taarifa iliyo na nguvu ya aya ya 2 imekuzwa na kutiwa mkazo katika aya ya 3 na 4, kwa taarifa mbili. Kwanza sharti lililofuatia tohara halikuwa jambo dogo kuliko kuishika sheria yote: katika hiyo alikuwa mdeni, na toka adhabu zake hakukuwepo kuepuka. Pili, ilikuwa kujitenga na Kristo: tendo ambalo liliwakatilia mbali na Kristo. "Mnajitenga mbali na Kristo:" (B.H.N.)- ni neno zito, likiwa na maana kukosa nguvu iliyo hai. Ni wazi hivi ndivyo ilivyokuwa: kutafuta kuhesabiwa haki kwa sheria, walianguka mbali na neema; "walifukuzwa" kama Hajiri alivyokuwa kama Paulo anavyodokeza kwa kurudia neno lililo katika ml. 4:30. Walifuata njia isiyowezekana ya kutaka kuhesabiwa haki na hivyo walishindwa kufikia chanzo cha kweli cha msamaha na ukombozi.Torati na neema; kutahiriwa au Kristo; hayashirikiani na si yenye sifa kwa matendo. Kuchagua moja walikosa lingine. Tohara ilikuwa kwa nje; ilikuwa ya mwili. (2) Uzima wa utu wa ndani kwa hiyo haukubadilika. Kuhesabiwa haki kwa imani msingi wake ni utendaji kazi katika moyo, kuongoka na kubadilika. Mwisho wa uhai ulianza kwa kukata govi nao ni mwili basi ilikuwa kuukata uhai wenyewe. Mwisho wa imani ilikuwa haki. Mambo haya ya kweli yameelezewa katika aya ya 5: "Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani". "Kwa Roho" tunaweza kuongozwa vibaya. Hakuna nakala yenye maana dhahiri, na kama katika nafasi nyingine nyingi katika maandishi ya Paulo, yaliyojulikana sana Warumi 7 na 8, roho inakuwa na jina linaloashiria kile kilicho ndani ya moyo utu mpya, utu wa ndani, sheria ya moyo. Kwa roho, au katika roho na akili iliyotiwa nuru na mioyo iliyopatana na kweli ya Mungu inayookoa, walisubiri haki ambayo ingewajia kwa imani. Kwa mtazamo hapa Paulo zaidi alikuwa na kusudi. Haki ni taji wanayopewa hao wanaopenda kufunuliwa Kristo: sio taji ya haki, taji ambayo ni haki (2Tim.4:8). Katika maana "haki" sasa ni mali ya aaminiye: Kristo "aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi"(1Kor.1:30). "Watu wa mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani" (Rum.9:30). Haki hii imehesabika kwao na Mungu; na, inachipuka katika "imani" ambapo juu yake mtu anajizoeza imani yake inayokuja akimtafuta Mungu na haki. Kupo kuifuta haki: kuwa na njaa na kiu, kunako dhihirisha hao waliojizoeza hivyo kwa kuufuata mwili ambao ndani yake haki ni kama ya kawaida kama dhambi ilivyo hali ya sasa. Paulo anasonga mbele katika maelezo yake, na kumalizia akisema, "Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo". Tohara ya Ibrahimu iliyofuata kukubaliwa kwake Paulo aliitanguliza: lakini wala si kwa sababu yoyote tohara ilitoa mchango wowote katika imani. Kuondoa govi hakukuwa na kusudi la uzima, na watu "walio katika Kristo" walijua: kwa kuona walijua nguvu ya imani katika kuendeleza upendo na kujieleza katika upendo, pande zote mbili kwa Mungu na mwanadamu Hapa tunaweza kuona mkazo mbaya wa siku hizi wa kusahihishwa. Leo imani imepunguzwa thamani na upendo umetukuzwa. Njia ya Mungu inaifanya imani kuwa ni msingi - imani ambayo si ya kutendewa, bali ambayo inajieleza yenyewe katika upendo. Upendo ni chombo na wakati uo huo mwisho wa imani: "Mwisho wa agizo hilo ni upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki" (1Tim. 1:5) "Mlikuwa mkipiga mbio vizuri"- ni sauti ya mwalimu aliyetazama maendeleo yao na kufurahi, lakini ambaye sasa amesumbuka juu yao, na akitafuta kuwarudisha kwenye njia ya zamani. Anawasisitiza katika hii, ila kuna mtu mwingine alikuwa akiweka vikwazo katika njia yao na hivyo wakizuiwa, na inaweza kuwa maadamu Paulo anauliza "Ni nani?" ambaye Paulo anamfikiria ni mwalimu mmoja aongozaye, labda mwalimu pekee aliye na ushawishi wa ujanja aliwapotosha - mtu aliyesemwa "yeye anayewafadhaisha" Paulo anawauliza ni nani aliye na madaraka ya kumchunguza, katika mafundisho yake, shabaha yake, na tokeo la kazi yake. Paulo anaelezea ushawishi wake unazuia "msiitii kweli". Kukosekana nakala dhahiri inayounganisha inatupa mkazo juu ya ukweli wa kwamba waliokuwa wanaukataa ulikuwa kweli - na si orodha ya mafundisho yaliyotazamwa kwa kusudi kama "kweli", bali yale ambayo, maadamu yanahitilafiana na mfano, ulikuwa halisi, hakika. Si moja kwa moja yaonyesha ya kwamba ilikuwa kivuli ambacho wao walikuwa wakikifuata. Kwa kuwa Mungu ameiweka "kweli" katika Yesu (Efe.4:21), kuigeukia torati hakuwezi kuwa ni kwa Mungu aliyewaita katika injili na kwa sababu hiyo mwalimu muongo hakuwa ametumwa na Mungu. (3) Ikiwa mafundisho yalikuwa ya upotoshaji usingelikuwepo mkutano na maadui wake: maana mafunzo ya uongo ni kama chachu, taratibu inaenea pote kwa ushawishi ukipenya kwa ujanja. Paulo anatumia kile kinachoonekana kuwa mithali "Chachu kidogo huchachua donge zima" - na mfano ni onyo juu ya kudharau mwanzo mdogo wa uovu. Fundisho lililotumika hapa, mithali inatokea tena katika 1 Wakorintho 5:6 mahali ambapo imetumika kwa dhambi mbaya sana. Katika sababu mbili onyo zito limetamkwa na kuondolewa kwa uovu ulioamriwa. Paulo anatazamia ya kwamba shauri lake litashinda. Hawaachii: "Nina matumaini kwenu katika Bwana, ya kwamba hamtakuwa na nia ya namna nyingine: Lakini anayewafadhaisha atachukuwa hukumu yake, awaye yote" (aya ya 10). Katika kutajwa hukumu ni wazo zito ambalo waalimu wote wanatakiwa wakumbuke. "Msiwe waalimu wengi" amesema Yakobo, mkijua ya kuwa mtapata hukumu kubwa zaidi". Watu wanaofundisha wanajiongezea wenyewe mema au mabaya kwa wanafunzi, na mtu anayesaidia kurejesha mwenziwe katika njia ya haki anategemeza wajibu wa kazi yake. Sasa hukumu imeonekana kwa kipimo, lakini hapana shaka ni kwenye siku ijayo ambayo wote wawili Paulo na Yakobo wanaitaja. Na mwalimu akiwa na wazo la wajibu akilini, Paulo anaongeza: "Nami, ndugu zangu ikiwa ninahubiri habari ya kutahiriwa, kwa nini ningali ninaudhiwa? Hapo kwazo la msalaba limebatilika." Ikiwa, kama Wayahudi wanavyodai, Paulo alisitasita na alihubiri tohara, ni kwa nini walimuudhi? Wao kumchukia kabisa Paulo, chuki yao ilionyesha tofauti kati yao katika mafundisho yaliyokuwa ya msingi. Shitaka lilikuwa la uongo, kwa hiyo na maadam shauri la msingi katika habari ni la uongo, dhana iliyotokea baada ya kufikiri juu ya kwazo la msalaba limebatilika ni la kichekesho. Tena kwa haki pia pamoja na fikira nzuri Paulo alijua kwamba kwazo lilisalia. Alifahamu msimamo wa maadui wake, maana aliwahi kushiriki maono yao. Lakini ushahidi wa kutamanisha ambao aliutumia vya kutosha ulidhihirika tu katika suala la waliomkataa Kristo jinsi mioyo yao ilikuwa na ukaidi. "Kwazo la msalaba" halikuwa kwamba Kristo alikufa mtini; lakini wala katika mauti yake Kristo alionyesha utiifu katika mabaya aliouweka mbele kuwa mfano mzuri kwa wengine; "kwazo" limo kwa ukweli wa kwamba Mungu aliamuru ya kwamba kwa mauti hiyo tu haki yake inaweza kudhihirika na watu kufikia katika haki yake kwa kuhesabiwa itokayo katika imani iliyo kwa Kristo aliyesulubiwa. B.H.N. aya ya 12 - "Laiti hao wanaowavurugeni wangejihasi wenyewe" - ni tafsiri inayokubaliwa na Wayunani wa kale waliotoa habari. Kwa nini wasifanye hivyo, anasema Paulo, maadam wanaimani ya jinsi hii katika kisu, desturi kamili ya kujikata iliyokuwa ya kawaida miongoni mwa watu waliojitoa kumwabudu Cybele? Kwa nyakati za sasa tafsiri hii imetupiliwa mbali kwa kuwa sio nzuri, lakini kama tunakumbuka ya kuwa kwa kugeukia kwenye dini ya Kiyahudi, Wagalatia kwa kweli walikuwa wanarudi nyuma isivyostahili katika jambo la tendo la dini ya kuabudu asili ya upagani wa siku hizo, na vile vile kukumbuka kuguswa na maneno ya mzaha katika yale yaliyotangulia, wakati huo ni hakika maneno ya Paulo yanamaana ya kwamba ikiwa dini ya Kiyahudi ilikuwa inawarejesha nyuma, basi hebu kwa uaminifu wa kulingana sawa sawa waende njia nzima, kwa kujikata binafsi kwa ishara ya kujiangamiza wenyewe katika maana kamili. Mwisho unaweza kujulikana ya kuwa Paulo anatumia neno la nguvu kuwaeleza wapinzani hawa. Walikuwa ni wazuiaji (aya ya 7); tena walikuwa wataabishaji neno lililotumika kwa shughuli za Paulo pale Thesalonike: waliupindua ulimwengu". (4) Huu ni uasi wa uchochezi, tendo la kuvuruga mfumo wa utawala wa kweli wa serikali iliyoratibishwa: nalo ni tendo ambalo linaelezea nafasi ya awaye yote atangazaye mafundisho ya uongo. UHURU SI KIBALI CHA KUFANYA YASIYOKUBALIKA (5:13-15) Siku zote watu hutaka kuelekea katika kutenda bila kutulia, wakipinga taarifa moja iliyo mbalimbali kwa kinyume chake; wengine huzunguka, kama mizani ya saa, katika mtazamo usioweza kuthibitisha wazo lisiloweza kuchukuliwa kwa hali iliyosawasawa. Mara nyingi kosa huzuka katika mkazo zaidi wa mwelekeo mmoja wa mafundisho wakati mwelekeo mwingine unaposahaulika. Kweli inafahamika, na kila sura ya mafundisho kwa uwiano ukilinganishwa baina ya kitu kimoja na kingine. Zote mbili katika mafunzo na kwa kutenda kwa hiyo kweli, inachunguzwa wakati kila sura ikiangaliwa, ikipewa mahali maalum na mkazo wake. Kwa mfano, Yesu hakuwa Mungu mwana au mtu tu; pande mbili alikuwa mwana wa Mungu na mwana wa Adamu (mtu). Tena, uhuru si nafasi ya kufanya mambo yasiyokubalika, wala kizuio sio utumwa. Uhuru wa kweli unajionyesha katika maisha yaliyorekebika yakiongozwa na utakatifu wa kweli. Katika utata wa fikira iliyogadhibisha kwenye karne ya kwanza, wakati mambo yakiwa katika hali isiyotulivu, mabishano mengi yalionekana yapo sawa wakati yakiwa ni ya uongo uliosogezwa mbele kuhesabia haki aina zote za ufisadi wa matendo ya uasherati. Vidokezo vya kupotoka huku vyaweza kupatikana katika nyaraka. Katika Kristo neema ya Mungu imedhihirika kwa kusamehewa dhambi. Kosa moja la Adamu limewahusisha watoto wake wote kwa matokeo ya tendo moja; lakini neema ya Mungu inazidi kwa hayo makosa mengi yanavyosamehewa kwa ajili ya utii wa Kristo. Hili ni fundisho la mitume; halafu huja kidokezo cha udanganyifu wa mwili: kama tukizidisha makosa ndipo neema ya Mungu itakuwa na nafasi ya kuzidi zaidi! Paulo anapouliza swali katika Warumi 6:1 : "Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi?" hakuwa anazusha mambo mengi ya mbali yanayozungumziwa na maana, bali akijishughulisha na tukio la maana lililoletwa na waalimu kwa makosa haya. Hadi hapo watu hawa wasio wa rohoni wanakwenda ambako Yuda anasema "wabadilio neema ya Mungu kuwa ufisadi". Uelekeo mwingine wa kosa lilo hilo kwa mtazamo wa kwamba mwili umerithi uovu na kwa sababu hiyo vitendo vyo vyote vya mwili vimemwacha mtu wa rohoni bila kuguswa, na uovu wo wote uliotendwa umemwacha mbali na dhambi. Kama Yohana asemavyo, ye yote anayepinga hivi wanajidanganya wenyewe. Wengine katika Korintho waliharakisha kutumia vibaya kadhia ya Paulo ya kuwa "vitu vyote vilikuwa halali" na kwa kutimiza mfululizo wa sababu za kuthibitisha maneno ya mifano yaliyoishia katika kuhesabia haki maisha ya zinaa (1 Kor. 6:12-18). Paulo anatumia neno uhuru mara nyingi zaidi katika Wagalatia kuliko katika waraka wo wote mwingine. Amewataka Wagalatia kusimama imara katika uhuru unaowahusu wana wa Mungu. Wapinzani wa Paulo waliweka shitaka la kwamba mafundisho yake hasa humfanya mtu kuwa huru mbali na sheria. Huu ulikuwa ni uongo, lakini alieleza hatari ya kweli kwa kuwa fundisho lake laweza kupotoshwa hivyo. Mbali na elimu ya kibinadamu, iwe njema au mbaya, uhuru unaweza kuwa na hatari. Uhuru wa kufanya apendavyo mtu bila kutazamiwa hutoa kwa hao wasio na elimu katika kutumika kwake, huweza kuleta msiba. (5) Uhuru na majukumu yake na majaribu yake, sio kwa watoto ambao hawajajifunza kujiweza binafsi katika uhuru unaoleta adabu, wala kwa watu wazima ambao kwa kasoro ya akili hawawezi kuutumia kwa usahihi. Kwa upande mmoja Wagalatia waliambiwa haki yao ni kwa Kristo: walikuwa warithi wa ahadi, wana wa Mungu wa kuchaguliwa. Mungu aliwaita, nao walijifunza ya kwamba "Bwana ajua walio wake": hata kwa hiyo wanaweza kumwita "Aba, Baba" (4:9,6). Iliwapasa pia kujifunza ya kwamba "kila mtu anayelitaja jina la Bwana" hana budi "aondoke katika uovu" (2 Tim. 2:19). Basi, kwa sura mbili zilizotambulika, kama Paulo asemavyo kila mahali, "Msingi wa Mungu umesimama imara". Pande hizi mbili za jambo zimeletwa pamoja hivi na Paulo katika 2 Timotheo 2, zilielezewa katika jambo mojwapo la uasi wa kora na mkutano wake. Walitaka uhuru wa kushika nafasi ya Musa na Haruni, waliolaumiwa kwa kujikweza wao wenyewe mno. Taifa lote lilikombolewa katika utumwa, lakini uhuru huo haukuwafanya kuamua watakavyo kwa kutafuta kila kitu juu yao ambacho roho zao zilitaka. Mungu aliwakomboa ili kwamba wamtumikie, na kumtumikia katika njia aliyoiweka. Musa, akiwa ameduwaa kwa ufidhuli, alieleza kwamba Mungu ataonyesha kesho "ni nani walio wake", na hii ilifanyika kwa njia ya kimungu iliyotakiwa kwa ardhi kuwameza waasi. Lakini kabla hii hukumu haija waangukia mwito ukafanywa kwa hao waliopata usalama, "Ondokeni penye hema za hawa watu waovu". Hapa basi, katika Hesabu 16:5 na 26, ndiyo msingi wa misemo miwili inayoweka baraka na uwajibikaji wa binadamu katika maneno ya Paulo kwa Timotheo. Kora na mkutano wake bado walikuwa ni watumwa na kwa sababu hii hawafai kwa uhuru wa kweli. "Atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi", Yesu alisema. Na dhambi ya nafsi ambayo haipati sura katika tendo la nje inatia mtu utumwani kama ile iliyodhahiri kwa wote. Dhambi hudanganya sambamba na kumtia mtu utumwani: na hapo shauku ya kwanza kuishi maisha katika Kristo inakuwa imetumika kidogo yenyewe na maisha ya kale yanaanza kujikuza yenyewe tena ni mvuto wa kujipendekeza wa kwamba kuna msamaha, dhambi inaweza kutendwa. Kwa hiyo halikuwa shauri lisilofaa Paulo alipowafundisha wasomaji wake kuwa uhuru wao haukuruhusu kujifurahisha nafsi katika dhambi. "Uhuru wenu usiwe wa kuufuata mwili", na tukumbuke "mwili na nyama" unamaanisha utu wote wa asili, ambao matendo yake yameorodheshwa katika mstari wa 19-21 kuzunguka shughuli za binadamu. Lakini kutangua shauri ni kidogo kuliko nusu shauri lililohitjika, na ni mwendo wa Paulo kutoa ushauri wa muhimu halisi zaidi ambao kwao kosa linatiishwa au kuondolewa. Hivyo anaongeza: "tumikianeni kwa upendo". Kwa kweli hii iliyo kama uwongo ya kutumika kwa upendo watapata uhuru wa kweli. Kuhalalisha kunahusiana na shughuli ya akili; na mhalalishaji ni mwenye kuambatana na sheria ambayo kwayo hakuna mwenye mwili ahesabiwaye haki. Kwa kweli, kama tulivyopata awali (ona3:10-11), njia yake kabisa ya kukaribia inakuza majivuno na hivyo dhambi. Mwenye kutakiwa na sheria kama akiwa mwaminifi anakuwa Farisayo; kama si mnyofu mnafiki; na kwa kadhia mojawapo hakubaliwi na Mungu au hawi baraka kwa watu. Ila upendo unaingiza sababu nyingine kwa usawa mwingine wa kiumbe. Upendo wa Biblia si tu ni kuwa huruma kama wengi wanavyodhani, bali unagusa moyo na maono. Upendo wa Kibiblia sio kuona bali ni jambo fulani linalosukumwa na nia au mapenzi, unapeleka moyo uelekeo unaotakiwa. Upendo unahusisha uaminifu na ni alama ya uhusiano wake mwenyewe. (6) Ni jinsi gani Mafarisayo walikosa kufahamu vema mtazamo wa sheria aliyoikazia Yesu aliposema ya kwamba torati nzima ilikuwa na amri mbili - kummpenda Mungu kwa roho na akili na moyo na nguvu yako yote na jirani kama nafsi yako. Torati ilitunzwa kama Mungu alivyotaka ufuatwe msimamo huu kwake mwenyewe na kwa watu waliposhughulika na bidii na kutunza amri. Basi hizi zinaeleza wazi kabisa njia ambazo habari na upendo utatiririka kupitia hizo. Kudokeza kwamba mtu anaweza kutenda dhambi ili neema ipate kuwa nyingi ni kukataa uhusiano mkuu wa peke yake uliowekwa kwa neema. Kuunganika na Kristo aliyekufa na kufufuka tena ni kuungana na mtu ambaye hakutenda dhambi. Na neema iliyoelezwa katika yeye sio udhuru kwa dhambi bali ni sababu kwa ajili ya dhambi kuwa imeepukwa. "Mtumikiane kwa upendo" - kufanya hivyo na haja ya kutaka kuwa chini ya sheria itakuwa imetoshelezwa kabisa; kwa kuwa sheria "imetilika katika neno moja, nalo ni hili: "Umpende jirani yako kama nafsi yako" (aya ya 14). Amri hii inapatikana katika Walawi 19 kati ya "sheria mbalimbali", kuzunguka eneo pana la utiifu, na katika maneno haya sababu ni kwa nini wasiwe na chuki mioyoni mwao, au unyimivu, au kulipa kisasi, ilikuwa kwa kuwa mtu alitakiwa ampende jirani yake kama anavyojipenda. Kwa kuweza kuweka sana umuhimu huu, amri imeminywa katikati ya maelezo mengi kwa kuwa sheria ya Mungu ni moja, basi kueleza maneno yote ni njia ya kueleza neno la awali. Utiifu hauna kupanga madaraja, baadhi ni muhimu, mengine makubwa kidogo, kwa sababu kushindwa kwa yo yote ni kushindwa kupenda. Kama upendo unaleta amani, hivyo kuonyesha kuiheshimu sheria sana hupelekea ugomvi. Matokeo ya mafundisho ya uongo yalileta mabishano juu ya mambo yasiyo na muhimu yenye mashindano, yakifanya uhai wa iklezia kuwa kama kichaka mahali ambapo wanyama wana njaa na kurarua. Kwa hiyo Paulo alikuwa tayari tu kueleza hali na matokeo ya hawa ambao wakinaswa: "Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana". Kujiangamiza binafsi hufuatia ugomvi wa ndani; waumaji wanahitaji kufungwa midomo; waangamizaji wanahitaji minyororo. Ni uhuru gani uliokosewa ambao ulihitaji kuzuiwa jinsi hii! Kanuni ya sheria ambayo walitaka kuikalisha kwenye kiti cha enzi machafuko ya kuishi maisha ya porini. Injili ya neema ya Mungu ilitoa uhuru wa ki-Mungu wa kujizuia binafsi. MAMBO YA ROHO NA YA MWILI (5:16-24) Ni kwa njia zipi watu waweza kuepuka uharibifu wa kuheshimiana wao kwa wao ulioonyeshwa katika mstari wa 15? Jawabu limetolewa kwa uchunguzi wa kifupi wa uadui wa nguvu ukifanya kazi ndani ya Mkristo, na mwongozo kwa njia ya kuhakikisha kwamba mambo ya roho yatashinda. Mivutano hii inayopingana imefafanuliwa kwa maneno "roho na mwili", lakini kutumia na kutotumia vema herufi kubwa katika neno la kwanza kwa kiasi fulani limetoa kutofahamu vema maana ya Paulo. "Roho" ni neno kuu na maana mbali mbali zinazotokeza miunganiko kuwa zifuatiliwe, lakini zote hazitakiwi kufuata hapa. " Mungu ni Roho" alisema Yesu; uweza wa Mungu umeitwa roho, na nguvu hizo kwa udhihirisho mahususi imeitwa Roho Mtakatifu. " Maneno yangu ni roho na ni uzima" Yesu alieleza. Roho haionekani lakini ni yenye nguvu nyingi, na inaonyeshwa katika idadi ya mafungu ya maneno hayo ambayo halisi na siku zote yapo mbalimbali kwa upande wa nje na namna yanvyopita. (7) Kwa kanuni ya kutahiriwa Myahudi kwa nje alidhihirika kwa jinsi hii, lakini pia kulikwa na Myahudi mwingine - mwana wa Ibrahimu kwa imani- ambaye tohara yake ilikuwa ya moyoni, ambaye tena aliitwa Myahudi kwa ndani. Ishara ya nje ilikuwa alama ya kuzikata tamaa za kimwili, lakini ishara ilichukuliwa na wengi ambao hawakufanya juhudi yoyote kuibadili ishara katika kitendo. Kwa upande mwingine mtu wa Mataifa aliyeitimiza maana muhimu ya kanuni, ingawa pasipo alama ya tohara ya nje. Alikuwa Myahudi wa kweli kuliko mwingine. Ndivyo anayotoa hoja kwa Warumi 2:25-29. Katika maneno ya kuyapima tunayo hali iliyo sawasawa mara moja zaidi na waraka maneno kwa Warumi, mlango wa 7 na 8. Hapo Paulo ananena "ile dhambi ikaayo ndani yangu", "ndani yangu (yaani ndani ya mwili wangu) halikai neno jema"; "Sheria - ninalolichukia ndilo nilitendalo"; katika viungo vyangu", neno moja lina maana ile ile kwa msemo mwingie "mwili wa nyama". Katika utofauti kwa maelezo haya ya nguvu za upinzani kwa mapenzi ya Mungu, tena neno "Mimi" ambalo halikubali, "nia" ambayo ipo, "utu wa ndani", "akili zangu" pamoja na hili, anasema Paulo, "Naifurahia sheria ya Mungu". Tunapopita kuelekea mlango wa nane maneno yaliyotumika kinyume ni "mwili" na "roho" la pili linachukuwa mahali pa "akili zangu". "Mwili" unaeleza mtu mmoja mmoja akifanya vitu kwa mvuto unaotoka katika mwili na ambao unaupendeleo ulio mbali na Mungu, umeinama kinyume na mapenzi ya Mungu. Huu ndio mwili waliorithi wana wote wa "Adamu". Ni nje ya uwezo wa mwili kujiinua wenyewe katika usawa wa juu, na nguvu yoyote inayosogea kuelekea mambo ya ki-Mungu kwa sababu hii hainabudi kuja toka upande wa nje. Ikiwa uhuru wa mtu unabakia bila kuharibika nguvu mpya inabidi itwae mfano wa mawazo ambayo kwayo mtu anafundishwa na anatakiwa apeleke maisha yanayolingana na mapenzi ya Mungu. Kuwaza kwa jinsi hii kupatikana tu katika neno la Mungu, na hili likipokelewa kwa imani na unyenyekevu linaweza kumbadilisha mtu kwa kufanywa upya nia yake. Katika Elpis Israel (tumaini la Israeli), Daktari Thomas anakusanya pamoja katika neno la Mungu baadhi ya maelezo ya njia hii iliyotengenezwa ya kuwaza ulinganifu na ufunuo wa Mungu. "Hii namna mpya ya kuwaza na kuona, ikiumbwa katika Muumini wa kweli kwa sheria ya ki-Mungu na ushahidi, kwa wingi kumeonyeshwa katika mandiko." Ni namna ya kusema "moyo safi na njema; 'roho mpya` na "moyo wa mwili", "utu mpya; kiumbe kipya" "utu mpya ulioumbwa katika haki na utakatifu wa kweli"; na "uliofanywa upya katika maarifa kwa mfano wake yeye aliyeumba"; 'utu wa moyo uliojificha` na kadhalika. Huu utu uliojificha unadhihirika katika maisha ambayo ni mema kama inavyopata kuwa injili. Sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, na ananena kila siku shuhuda zake. Huyu mtu anakataa mabaya yote na tamaa za ulimwengu, anatembea kwa busara, kwa unyoofu na kwa utauwa katika ulimwengu. Tumaini lake ni lenye kudhihirisha utukufu wa Yesu Kristo, na taji ya haki, utukufu usiobadilika, na kutokufa, kumeahidiwa kwa wote wanaomtazamia, na wanaopenda kufunuliwa kwake, na wanaotaka ufalme wake". Ongeza neno "roho" kama muhimu sana ya hayo yaliyozunguka kwa neno "na kadhalika" katika dondoo la juu, msomaji ana mambo ya hakika kwa ajili ya tafsiri sahihi ya sehemu hii ya waraka kwa Wagalatia. "Enendeni kwa roho" asema Paulo, "wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili". (8) Hii ni njia ambayo kwayo njia za kimwili zinaweza kuepukwa. Ikiwa mtu hawezi kupita barabara mbili zinazoelekea njia tofauti kwa wakati mmoja, vivyo hawezi kuenenda katika roho na katika mwili wakati uo huo. Shauri la kutembea kama tendo la kuipita njia, tendo ambalo Paulo analifurahia kulitumia sana, ni mfano uliochukuliwa katika Agano la Kale, mfano ulioelezwa kwa maelezo mengi katika Zaburi na Mithali. "Roho" ni mazingira, hali ya maisha iliyoelezewa hivyo; ni maisha ya kiroho. Ni bora mwili ukomeshwe, sio hivyo sana kwa juhudi ya moja kwa moja yenye nia ya kuutiisha, bali kwa kuuangalia na kuuongoza kinyume. "Mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake" (Rum. 13:14). Kitu ambacho hakilishwi hufa kwa njaa na kutofanya kazi. Ni wazi hii ni kweli, lakini hivyo habari ni yenye maana dhahiri inayoweza kuwa ni kuelezea jambo kwa kulirahisisha zaidi. Kwa kweli, "mwili" na "roho" vyote viwili vipo pamoja ndani ya mtu wa Mungu; "roho " inahitaji kuipalilia, hiyo haina uenyeji; mwili wenyewe upo kazini. Kwa hiyo roho haina ushindi kamili katika pigano na wakati mwingine huonekana karibu kushindwa. Walakini Paulo anaujasiri wa kwamba ushindi upo upande wa roho kama kuenenda kwa roho kutafuatwa. Maneno yake katika aya ya 17 kwa kweli ni wazo la "kutotimiza tamaa za mwili" ya aya ya 16; sana akikiri ya kuwa "maadui" walikuwa wameishika sana, lakini akieleza "roho" ni mshindi. "Maana mwili" asema Paulo "hutamani ukishindana na Roho, na Roho hushindana na mwili: kwa maana hizi zimepingana; hata hamwezi kufanya mnayotaka". Fungu la mwisho kwa maneno, "kufanya mnayotaka", limepewa tafsiri mbili tofauti; ya kwanza ni kwamba mwili unatutiisha na kushindwa kufanya tunayotaka, lakini ya pili, kwamba kwa kuwa roho ni yenye nguvu sana inafanikiwa, na hatujitii katika mambo ambayo mwili unatutaka tufanye. Ya pili ni kuendeleza sifa ya kujiamini katika maneno, na tena linafaa fungu la maneno pande mbili kabla na baadaye; kwa kuwa Paulo anaendelea kana kwamba roho ilikuwa imeshinda: "Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria". Tofauti ya kweli hapa ingekuwa, kama waliongozwa na roho wasingalikuwa chini ya mwili: lakini wakati Paulo alimaanisha ya kuwa, pia kwa kubadili maneno anasema tena sana, uadui wa kimwili unaletwa na Torati, kama mtume anavyoonyesha: uwezo wa mwili hufungamana na sheria: na kwa hivi sheria haiwezi kuwaletea watu wokovu. Basi kuongozwa na roho sio ni ushindi tu juu ya mwili, bali kufuata desturi ya njia ya wokovu wa Mungu kwa injili ya neema na si kwa sheria. Kwa kuifuata roho hawakutafuta kuufikia wokovu kwa Torati: na kwa hiyo wakiwa wafuasi wa njia ya kweli ya uzima hawakuwa chini ya sheria. Chini ya uongozi wa roho kanuni zote za kimwili kufaulu kulipunguzwa nguvu, hawakuja chini ya Torati kuwa ndio chanzo cha agizo au cha hukumu. Katika mistari ya 19-20 Paulo anafunua tabia za mwili na "matendo" yake; na aya ya 22 "tunda" la roho. Matendo ni shughuli, na kwa kuwa zimekatazwa na sheria, ila zimefunuliwa na sheria, matumizi ya neno "matendo" hapa yameweza kudokezwa kwa "sheria" katika aya ya 18; kana kwamba Paulo alisema, "Mnataka kuwa bora kwa matendo ya sheria; haya ni matendo ambayo sheria inayaonyesha kuwa ni zao la mwili". "Tunda" linakuzwa kwa kushughulika na uvumilivu, kwa ukulima wa busara, linakuja kwa kulipanda na kusubiri kupevuka kwake. Kuna maovu mengi makubwa katika maisha ya mwanadamu ambayo mara kwa mara hayaonekani kwa kutazamwa, matendo ya mwili na ya giza kwa kila maana. (9) Lakini mwili kwa hali iliyosawa unatenda kazi katika mazoezi mengi mengine kuliko maovu ya mwili; katika hasira, ugomvi, uasi, ulevi ambao zaidi unaonekana kwa uwazi. Lakini kuna tamaa za ndani za jinsi hii kama ibada ya sanamu, majivuno, husuda ambavyo vyote hivi vinachipuka katika mwili. Hakuna kipindi chenye uwezo kuongoza mambo yote haya yaliyotajwa, na wala hakuna kipindi kisichokuwa na kila uovu uliotajwa. Tunda - maana kuna tunda moja - lina "upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, wema, imani, upole, saburi". Hakuna sheria juu ya mambo haya. Sheria iliyokuwa na nguvu za kuuamsha mwili haina nguvu za kuzuia kukuza mambo ya roho. Wakati sheria shabaha yake ni kuweka kizuizi kwa utendaji kazi wake wa kawaida, katika mambo ya kiroho hakuna kinachohitaji kuzuia. Ni bayana kwamba Paulo analenga jambo lingine lenye maana zaidi katika matokeo kuliko kuikubali tu sheria. Watu walioiwekea mpaka sheria kuwa ndio upeo wa maisha iliwafunga na upeo wao unakuwa kama gereza. Kilichokuwa kinahitajika ni nguvu mpya ya kuifikia haki. Paulo mwenyewe aliiona nguvu hii katika Kristo Yesu: "Nayaweza mambo yote kwa njia ya Kristo anitiaye nguvu." Aliuona mwili jinsi ulivyo; akapata kufahamu namna Yesu alivyoukataa kwa tendo la kujitoa kusulubiwa. Aligundua umuhimu wa kujihusisha mwenyewe na mauti yake: "Nimesulubiwa na Kristo". Kwa kushiriki hivi hicho kifo vivyo akashiriki ufufuo wa Kristo kwa kuwa katika Kristo akafufuka kwa upya wa uzima, yaani kuishi maisha mapya. "Maana kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; tukijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena" (Rum. 6:5,6). Nguvu kuu mpya imeanzishwa na huku kumtii Kristo, na hata kama desturi za kale zinaendelea na kudhoofisha nguvu, na ingawa kuna kurudia kukosea kufikia uadilifu unaotakiwa, lakini mazoea ya kale makuu yamevunjika, kwa kuyatiisha pole pole. Kumkubali Kristo kuwa mwokozi ni mamoja na kukana madai ya dhambi kuwa bwana juu yetu. Kristo anakubalika kuwa ni Bwana kwa namna ya kujitoa mwenyewe kama mawazo yatendayo kazi kwa utakatifu yakichukuwa nafasi kuu ambayo awali ilishikwa na matakwa ya kimwili. Hao walio wa Kristo "wameusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa" (aya ya 24). KUWAANGALIA WENGINE (5:25-6:5) Kuishi maisha mapya katika Kristo humbadili mtu ajitenge na jamii; maana sio tu kwamba amejihusisha na Kristo bali pia anajihusisha na hao walio katika Kristo. Roho mpya huongoza matendo ya mtu na hutawala mahusiano yake na wengine. Waumini wote hufungamana pamoja ili uhusiano wao kwa Kristo na kila mmoja na mwenziwe umeelezewa kwa mifano ya mzabibu, na mwili wa binadamu. Kristo ni mzabibu, wao ni matawi; Kristo ni kichwa, wao ni viungo vya mwili wake. Katika aya 16 Paulo alikwisha sema "enendeni kwa roho", ushahidi ukiwa katika mwendo wa maisha mtu mmoja mmoja kufanya hivyo. Katika aya ya 25 anatumia neno lingine lakini kwa maana ile ile likionyesha kutembea na kusimulia wengine. "Tuenende kwa roho" hii inahusisha kutembea kwa pamoja kama katika jeshi - yaani gwaride." Kama tukiishi kwa roho" ikiwa maisha mapya ni mazingira yetu, basi na tuenende kwa Roho"; basi matendo yetu yaliyounganika yahuishwe kwa tabia nzuri iyo hiyo. (10) Maungano ya ulinganifu yanayoonyeshwa katika aya ya 25 kwa kawaida hupelekea katika shauri la kutopanda mbegu mbali mbali. "Tusijisifu bure, huku tukichokozana na kuhusudiana". Ubora wa jeshi hutegemea sana juu ya roho inayowaamsha maafisa na askari wasio maafisa . Kila juhudi inafanywa kwa niaba yao ili kwamba wasiachwe kwa adui. Labda pengine wazo la jinsi hii ni pete inayoungana na shauri lililo katika 6:1 kuhusiana na mkosaji; "Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lolote, ninyi mlio na roho mrejesheni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe. Wajibu wa mshirika anayekosa umewekwa katika amri hii kufuatana na fundisho la Bwana. Ikiwa mtu amemkosea mwenziwe, Bwana ameweka jukumu la kutafuta kutengeneza hatia ya mkosaji juu ya upande uliokwazika. Kwa sababu nyingi, kwa mfano wa kwanza, ni yeye peke yake anayejua kosa; na badala ya kuudhika na kutaka kurekebisha, Bwana anamtaka achukue hatua ya kuondoa kosa la mwingine kwa kuzungumza naye yeye mwenyewe kwanza, na kama ikishindikana basi chukua msaada wa wengine. Mathayo 18:15-20 haujafafanuliwa wazi kama ni kibali cha kuadhibu au hata kurekebisha mkosaji; ni habari nzito na ya maana sana ya wajibu wa kumwelekea mkoseshaji na ukiwapo mtazamo wa kupona katika dhambi yake. Yesu anaweka nuru ya kutisha kwa tendo linalomsababisha mtu mwingine kukosa: "Bora kutoswa katika kilindi cha maji kuliko kuwa na kosa hilo", anasema Yesu. Ikiwa wafuasi wanagundua ya kuwa kuweka kikwazo katika njia ya mwingine ni kosa zito, basi amri "ya kukemea"na "kusamehe" inafuata ikiwa ni wajibu wa maana (Luka 17:1-5). Ugumu wa kukubali, kama mitume walivyotambua mara moja, wakisema, "Bwana, atuongozee imani." Ikiwa mtu akigundulika na kosa juhudi inabidi ifanywe kumponyesha, "mrejezeni upya mtu kama huyo". Tunatumia neno "kurejea" tunapomsema mtu amerudia hali yake ya kwanza baada ya kuugua; kukosa ni kama ugonjwa inatakiwa bidii ifanywe kumrejeza upya mkosaji katika hali ya kiafya kiroho. Neno lililotafsiriwa "kurejeza" linaweza kuwa ketengeneza nyavu vizuri zaidi (Math.4:21), kwa "kuweka tayari" mwili wa Masihi (Ebra. 10:5), "kuwa wakamilifu" (Ebra.13:21 - mahali ambapo hatuoni basi kurudiwa neno hili katika 10:5, lakini tena linatokea mara ya pili na "mapenzi"; 1Petro 5:10), na vyombo "vilivyofanywa tayari", kwa uharibifu (Rum. 9:22) na kwa ukamilifu kuungana pamoja katika nia moja na shauri moja, jambo ambalo linapelekea kunena mamoja na hivyo wanaepuka "faraka" (1Kor. 1:10). Neno laelezea kupatana tena wafitini wanaoshindana; kukirudisha mahali pake kiungo kilichoteguka; au kushona tena nguo iliyotatuka. Kwa kila sababu kuna kubadilika hali na kuwa ile ya kwanza, ili kitu kije kifae kwa matumizi ya mwisho ambayo mtumiaji anatazama. Nini kifanyike "kumrejezea upya" mtu mgonjwa kiroho? Hatua gani zaweza kuchukuliwa ili kuleta ahueni? Ipo tofauti kati ya asili na ya kiroho. Kwa desturi ya mwili wakati wa sehemu kubwa ya maisha kuna nguvu zisizoonekana tayari kufanya kazi ya kuleta uahueni au kuponyesha majeraha au viungo vilivyovunjika au viungo vyenye ugonjwa. Lakini ya kiroho kwa mtu hutegemea juu ya kukubali mashauri yaliyo nje ya nafsi yake. Mtu aliye tayari kusikia anatambua afya ya maradhi ya mwili wake kuliko ugonjwa wa nafsi yake, maana dhambi hudanganya na siku zote inatafuta kujificha na kugeuza sura kwa kubadili uso wake halisi. Lakini kupona husubiri kutambua kosa, kukiri kwake, kutafuta kwake msamaha, pande zote mbili kwa mwanadamu na kwa Mungu. (11) Hii ni kazi ya watu wenye busara, na hivi ndivyo Paulo anaelewa. Anawataka "ninyi mlio wa roho" kujiingiza katika kazi. Mtu wa asili hawezi kuchunguza na kuyakinisha mambo ya roho, wala haoni "matibabu"yanayohitajika. Bali mtu wa rohoni, anafahamu ya kuwa wokovu wa nafsi unahusisha kuona jinsi asivyofaa. Majivuno au kiburi hukwamisha kazi: "roho ya upole" matabibu waangalie wakati kila mchangiaji wa kazi akumbuke kila mmoja huelekea kuanguka ajaribiwapo. "Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo" ni agizo linalochipuka katika wajibu uliowekwa wazi katika aya ya 1. Linaeleza wajibu ambao mstari wa kwanza ni haja mahususi. "Mpende jirani yako kama unavyojipenda nafsi yako" ilikuwa kiini kabisa cha sheria kwa pande mbili , kwa Musa na kwa Kristo: lakini vile vile Yesu alieleza kwa namna nyingine: "Kama mnavyopenda watu wawatendee, nanyi watendeeni vivyo". Lakini Yesu aliitia pamoja kanuni katika maisha yake mwenyewe, na kwa sababu ya utiifu kamili katika mambo yote akafufuliwa kupata uhai. Hii kazi ilikuwa kazi ya Masihi kama ilivyotakiwa na manabii wa Agano la Kale, na inastahili kuangaliwa kuwa Paulo haisemi sheria aliyoinena Yesu bali "kuitimiza sheria ya Kristo", sheria ya Masihi. Sheria hiyo ni sheria ya maisha yake, na kutimiza sheria ya Masihi ni kuhifadhi uhusiano wake mwenyewe kwake unaomfanya mtu awatumikie wengine. Amri iliyo katika Warumi 15:1-3 inamfunga muumini kwa Kristo katika huduma moja ya kutaka mema kwa ajili ya jirani, na wazo la mstari huu ionekane kuwa inapanuka ya Wagalatia 6:2; Inasomeka hivi: "Sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, haitupasi kujipendeza wenyewe. Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate mema, akajengwe. Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa , Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi" (Rum.15:1-3). Ikiwa mtu hapendi kutumika amepofushwa na kiburi na kujidanganya mwenyewe. Kwa kujidhania mwenyewe kuwa kitu, anaonyesha naye si kitu (aya ya 3). Basi shauri ni kwamba mtu "aithibitishe" kazi yake: inambidi apime matendo yake mwenyewe; maana kwa matokeo ya kupendeza katika kipimo cha jinsi hii na si kwa kulinganisha na mwingine ipo sababu ya kuifurahia kazi yake. .Hakutaweza kuwapo kuhamisha jukumu lake mwenyewe; mtu hawezi kujiona mwenyewe amesifiwa kwa kuwa yeye, kama Farisayo, anadhania yeye mwenyewe ni tofauti na watu wengine. Mwishowe kila mtu atatoa hesabu ya uwakili wake mwenyewe. Hili jukumu limeelezewa kwa mfano wa kusimuliwa vizuri , uliofumba katika tafsiri kwa kurudia tena maneno kuchukuliana mizigo yanayoingiza kuchanganya kati ya mistari ya 2 na tano. Kwa tafsiri ya kwanza, mizigo ni masumbufu ya maisha ambayo tunaweza kushirikiana: ya pili ni mzigo wake mwenyewe askari kwa ule anaowajibika, au shehena ya meli. Maisha ni kama biashara mpya inayoingia, na meli zote zinapoingia bandarini ni shehena inayochukuliwa na kupimwa kwa kwa kuihakikisha. Kila mmoja hana budi kutoa hesabu kwa matendo yake mwenyewe.Wakati huo kila nahodha atahangaika kidogo karibu na safu ya shehena ya mwingine, kuliko iliyomo mikononi mwake mwenyewe. Kuhamisha matokeo ya biashara hakutawezekana; kila mtu inampasa kutoa taarifa yake mwenyewe. (12)