_____________________ WARAKA WA MTUME PAULO KWA WAGALATIA SURA NNE The Letter of Paul to the Galatians - Chapter Four _____________________ MAHALI PA TORATI PAMEELEZEWA NA MIFANO YA SHERIA YA MWANADAMU.(4: 1-7) Ingawa mlango wa 4 unaendeleza maneno ya kusadikisha ambayo kwayo Paulo aliwapata tena Wagalatia toka hatari yao ya kupotoka katika dini ya Kiyahudi, baada ya mlango, mgawanyiko unaelekea kuacha muunganiko itakuwa vema kujumlisha kwa ufupi katika maana hii yenye maneno ya kusadikisha ya mlango wa 3. Katika ziara yake Paulo aliwaelezea kwa uwazi ya kuwa Kristo ni Mwokozi aliyesulubiwa, na kwa kupokea kwao mahubiri haya wakapata karama za Roho zinazothibitisha. Muhubiri aliweka suala zima juu ya imani kama nguvu itendayo kazi katika maisha yake mwenyewe, na vile vile katika yao. Hii ilifanana na maelezo bora ya mfano katika Andiko- suala la Ibrahimu katika Mwanzo 15:6. Imani ilikuwa ndiyo sharti juu yao ambayo watu waliungana na Ibrahimu na ambayo kwayo kwa kweli walihesabiwa kama wanawe. Ushuhuda wa Andiko ulikuwa kwamba imani na sio matendo ya sheria ilikuwa moja ya mchango wa mwanadamu katika kuhesabiwa haki - kwa nafsi yake mwnyewe mtu hawezi kufanya lolote; inampasa akubali kile ambacho Mungu alitoa. Wakati baraka ilikuja kwa njia ya imani, Torati ilileta laana kwa sababu ya udhaifu wa mwanadamu na kutoweza kutunza matakwa ya Torati. Basi mambo ya Torati kabisa yalihitaji ukombozi toka humo, na hata huu ulipatiwa katika Kristo. Ndipo kitovu cha ahadi kilikuwa kwa Kristo; kwa njia yake zitatimilika, na kwa hiyo pia kwa yeye likapatikana jambo linalounganisha ambalo kwalo Mungu atawaleta watu katika "Umoja" na Yeye mwenyewe. Torati kilikuwa kipimo cha muda mfupi ikiwazuia watu katika ulinzi. Hii ilionyesha kama kuhusika na hatua ya awali ya maisha ya binadamu, katika kipindi cha utoto. Torati inahusika na utoto; imani katika utu uzima. Torati iliishia alipokuja Kristo, mwenye kuonyesha imani na kuhubiriwa kwa Injili kuliwaletea watu mwaliko kuwa wana wa Mungu, sio watumwa wa torati. Maadam hali ya kuwa wana imewekwa juu ya imani, na jambo la imani limekuwemo katika Andiko kwa asili limeunganika na Ibrahimu na ahadi zilizofanywa kwake, hali hii ya kuwa mwana pia ni ya urithi wa ahadi alizoahidiwa Ibrahimu. Kristo ni "mzao"; kwa imani wanakuwa watoto wa Mungu; wanafikia urithi. Watakatifu ni Warithi Neno Mrithi lililo katika 3: 29 linahusu kuungana na aya inayofuata 4:1, ambapo Paulo anataja maelezo ya mfano katika sheria ya mwanadamu ya utii wa kitambo kwa mrithi katika hali ya kuwa watumishi. Inabidi pawepo kufundishwa na kutiwa adabu ili mtu awaye yote afae kwa majukumu ambayo yanamwangukia katika maisha ya mtu mzima, na kuzoezwa katika urefu wake na ukali kunalingana wajibu wa kusadikika. Ilikuwa hata hivyo katika mapatano ya Mungu. Katika kipindi cha Torati ulikuwa muda wa kufundishwa na kuadilishwa yakiwa ni maandalizi ya kupewa jambo lingine. Kujilinda na kosa itakuwa vema kuweka mkazo wa kwamba Paulo anatoa maelezo ya mfano tu ambao kwa upana unafaa katika jambo. (1) Anatazama kwenye eneo refu la historia na kulinganisha yote na kubadilika desturi katika muda wa maisha ya mtu, na miaka yake ya utoto ikifuatiwa na utu uzima. Kipindi kirefu cha torati kililinganishwa na ulinzi na Mamlaka juu ya mtu- kipindi cha injili katika hatua ya imani iliyoendelea. Lakini hii haina maana kwamba hakuna watu mmoja mmoja wa enzi ya Musa aliyefikia imani inayookoa. Walikuwepo wachache chini ya torati, ambao wakiona sehemu ya mpaka wake kuwa kanuni ya kitaifa, walitazamia kuja kushiriki wakati ujao kwa imani. Torati ilikuwa ya kitaifa imani ni ya mtu mmoja; na Paulo anawazia maisha ya taifa, akiwa na raia wake katika mwendo wake unaofuatwa na sheria Kwa kukana toka maelezo ya mfano wa Paulo aidha kwamba wote walioishi chini ya sheria walitengwa na imani, au kuwa kinyume chake wote watakuwa katika imani na kusimama wakiwa warithi na uhuru unahusu imani, kungepunguza maelezo yake kuwa ya kuchekesha. Aya ya 1 na ya 2; inaonyesha ulinganifu wazi na mistari 3 na 4.Tunanukuu mstari wa 1 na 2 ukitumika mfano wa sarufi za italiki kwa ajili ya maneno ya kawaida ambayo usambamba utakutwa katika aya ya 3 na 4: "Lakini nasema ya kuwa mrithi, wakati wote awapo mtoto, hana tofauti na mtumwa, ingawa ni bwana wa yote; bali yu chini ya waalimu na watunzaji, hata wakati uliokwisha kuamriwa na baba". Mtoto,cheo chake chochote kinachokuja kitakavyoweza kuwa, ni kwa ajili ya makusudi ya kufaa kama mtumwa: yu chini ya uongozi wa watunzaji anayetunza mtu wake, na mawakili walio na amri ya utawala wa mali na mambo: Mashariti haya yanadumu kwa muda mrefu uliopangwa na baba. Aya ya 3 na ya 4 inasomwa: " Kadhalika na sisi, tulipokuwa watoto, tulikuwa tukitumikishwa na kawaida za kwanza za dunia: Hata ulipowadia utimilifu wa wakati, Mungu alimtuma Mwanawe ambaye amezaliwa na mwanamke, amezaliwa chini ya sheria." Angalia kutokea mara ya pili maneno "mtoto (aya ya 2 ), "watoto" (aya ya 3): "mtumwa au "mtumishi" ( aya ya 1 ) yanalingana na "kutumikishwa" (aya ya 3); "mawakili na watunzaji" wa aya ya 2 ndizo "kawaida za dunia"; huo "wakati ulipowadia" ulio katika aya ya 2 ni sawasawa na "utimilifu wa wakati" . (aya ya 4). Karibu mambo haya yote ya kuangaliwa yameamriwa kurudi katika "fumbo la maneno" ambayo kwayo Paulo anamalizia sehemu hii yenye maneno yake yenye kusadikisha katika 4:21-31. .. Paulo anaposema "sisi"-"tulipokuwa watoto" anamaanisha watu walio Wayahudi ambao naye alikuwa mshirika. Ni jinsi gani alikwisha vijua vizuizi vya sheria! Bali sasa ni kiasi gani zaidi alifahamu kusudi lake, na kufurahia uhuru wake uliokuwepo! Kawaida au maarifa ya dunia, vyanzo rahisi, kama herufi za alfabeti ni vyanzo vya kujifunza. Kanuni na matendo ya ibada ya sheria ya mwili yalikuwa ni kawaida za mafunzo lakini ndani yake yenyewe haukuwa ndiyo mwisho; ila kwa chini ya hayo ilikuwa lazima hadi mambo yaliyo ya kweli katika Kristo yaliyokuwa vivuli yalipokuja. Utimilifu wa wakati unadokeza kipimo kinachojaa taratibu kadiri miaka inapopita, kikipima mwendo kuelekea kipindi kilicho muhimu kabisa kilichokusudiwa na mmoja aliyetoa kipimo. Chembe ya mwisho iliingia chomboni- saa ya badiliko ikafika. (2) Hapo kabla tumetoa maelezo juu ya "historia ya elimu" ya Paulo kwa maneno yake katika 3:19: wazo lilo hilo linapatikana hapa katika maneno ya"utimilifu wa wakati". Tendo la "kuja mzao" (3:19 ) ilikuwa katika "utimilifu wa wakati". Ndipo " Mungu akamtuma Mwanawe". Kwa namna yake maalum mara mbili kabla Paulo alitaja Mwana wa Mungu. Ilimpendeza Mungu amdhihirishe Mwanawe kwa Paulo wakati ulio muhimu kabisa katika maisha ya Paulo ulipotokea akienda njiani kuelekea Dameski (1:16); na Paulo aliyeifia sheria na kumwishia Mungu "kwa imani ya Mwana wa Mungu ambaye", asema Paulo, "alinipenda na kujitoa nafsi yake kwa ajili yangu" (2:20). Vilevile ameonyesha kwamba jambo la imani kama dhamana ya watu wote wa ukoo mmoja miongoni mwao "mwenye heri" waliohesabiwa haki, inahusisha kufanywa wana katika jamaa ya Ibrahimu, kwa kuwa watoto wa imani wanakuwa watoto wa Ibrahimu, Mungu akiisha mfanya Ibrahimu kuwa "baba wa mataifa mengi". Ameenda zaidi, kwa kusema kwa nguvu ya kuwa wanaume na wanawake wenye imani iliyo kwa Kristo Yesu wanakuwa "watoto wa Mungu"(3:26). Juu ya msingi ambao wanaweza kuwa watoto wa Mungu inabidi sasa kuuweka mbele. Kilele cha ufunuo wa Mungu kwa neema yake kinahusika na ukweli huu- wa kwamba watu wanaweza kuwa wana wa Mungu; lakini kikomo hicho cha mambo ilibidi kisubiri wakati ulio muhimu kabisa katika historia Mungu alipomtuma Mwanawe. Mwana wa Pekee Ni vyepesi kunena habari za kuzaliwa kwa Yesu, na ukweli wake kuwa ni Mwana wa Mungu ila si rahisi kufahamu ukubwa wake- kama kwa ajili ya malengo ya ukombozi wa binadamu Mungu akamzaa mwana wa ukoo wa mwanadamu. Ukiwa kama mshangao na hicho katika ukweli kwamba "Mungu alidhihirika katika mwili" kwa mtu ambaye alikuwa "Neno alifanyika Mwili" anazidi kwetu, hivyo tunathamini bila kosa kwa kupambanua sura za ufunuo wa Agano Jipya- ya kuwa tumefanywa wana wa Mungu kwa Yesu, Mwana mzaliwa wa pekee. Kupevuka kwa Daktari Thomasi kufahamu ufunuo wa Mungu kumeonyeshwa na ukweli kwamba alifahamu na hivyo kwa udhahiri alishika fundisho hili la udhihirisho wa Mungu katika kitabu chake Eureka, ambacho wasomaji waweza kuelekezwa vya kutosha hata maelezo yaliyo madogo (Vol. 1: kuanzia uk. 87-115). Paulo anaeleza mambo mawili ya hakika kulingana na kuja kwa Mwana wa Mungu, na kufanya picha mbili za matokeo yanayolingana. Lakini kwa kuwa anayeelezea kwa namna inayoitwa mambo ayaonayo mwenyewe na kutojishirikisha na wengine, mfano uliotumika mara nyingi kwa manabii na Bwana Yesu, tunashika mambo ya hakika na kuwa sawasawa. Mungu alimtuma Mwanawe "amezaliwa na Mwanamke amezaliwa chini ya sheria, awakomboe hao waliokuwa chini ya sheria, ili sisi tupate kupokea hali ya kuwa wana." (3) Kristo kwa kuzaliwa alipatwa na mambo mawili yaliyohusiana- katika ukoo aliokuwa mshirika wetu, na alikuwa Myahudi aliye chini ya Torati ya Musa. Mambo haya mawili yaliyohusiana yalimleta kukutana kwake na mahitaji makuu ya watu. Kwa sababu alikuwa chini ya Torati, aliweza kuwakomboa wale walio chini ya sheria; kwa kuwa alikuwa mwana wa Adamu (ingawa Yeye si mwana wa mtu) aweza kutukomboa toka dhambi na mauti na kuturejesha kirafiki kwa Mungu, na hivyo tunaletwa katika hali ya wana. Tayari tumeona cheo cha Kristo kulingana na Torati, tunapopima maneno ya Paulo katika 3:13. Kristo alitukomboa toka laana ya Torati kwa sababu yeye alifanywa laana kwa namna ya mauti yake. Tukitimiza jambo hili vizuri hanabudi kuwa chini yaTorati na kwa sababu hiyo inabidi azaliwe na mwanamke aliye wa ukoo wa Israeli. Maana halisi ya hakika kuwa alizaliwa chini ya Torati ilitambulika vema kwa Paulo kuliko sisi, kwa kuwa Paulo alijua kilichohusika kwa kujaribu kuishi chini ya Torati. Torati halikuwa jambo lingine lililojitenga - jambo tu lililo kwa ajili ya mjadala wa misingi ya dini na Mungu ya kuwa Torati ilikuwepo kwa kuitii na kwa uzito mtu wa bidii hapo. Kwa kuwa kuhamishwa Torati na kwa sheria yenyewe kuondolewa ulikuwa msaada usiosemeka; maana sio tu Torati ilieleza mapenzi ya Mungu, bali kwa ajili ya wote walio chini yake, ilileta hukumu ya Mungu. Katika kusema wakati huo kwamba Kristo alizaliwa chini ya Torati ilikuwa ni kusema ya kuwa alizaliwa katika uhusiano uliofanana katika mpangilio ulipo wa Mungu ili kongwa la Torati liweze kuchukuliwa naye, na kwamba laana imwangukie na lakini aweze kuokolewa toka mauti kwa Utukufu wa Baba, na hivi watu, waliolaaniwa na Torati kwa ajili ya makosa yao, wanaweza kukombolewa. "Kuzaliwa na mwanamke" kunanena wazi uhusiano ulio mpana kuliko "kuzaliwa chini ya sheria". Ya pili ina kikomo kwa Wayahudi, ya kwanza ni kwa watu wote. Ukombozi ulipangwa na Mungu kufaa haja za wote na mahitaji yao wote. Kuna jambo lingine katika maneno yaliyounganika "kutumwa Mwanawe" na "kuzaliwa na mwanamke" ambalo linamtenga Mwokozi akiwa Mwana wa Mungu. Asili yake kwa Mungu sio tu katika jambo la hakika kuwa Mungu "alimtuma", wala hata sasa tu katika taarifa iliyo wazi ya kuwa Kristo ameitwa Mwanawe, bali kana kwamba kufunga kamba ya nyuzi tatu Paulo anatumia neno "akawa" limetafsiriwa"zaliwa", ambalo sio neno limetafsiriwa hivyo kwa kawaida . Ni kwa sababu gani anatumia neno hili lingine hapa wakati baadaye katika sura, akimnena mwana wa Ibrahimu, amekuwa tayari kutumia neno la kawaida? Kuzaliwa na bikira ni maelezo tosha, na labda ni maelezo pekee ya kutosha, ya uchaguzi wa maneno ya Paulo anayotumia. Yesu akiwa ameonyeshwa hivi kuwa mwana wa Mungu, tunaweza kutambua maana ya maneno yanayoeleza matokeo ya kuja kwake. Alizaliwa chini ya sheria ili kuwakomboa walio chini ya sheria, lakini alizaliwa Mwana wa Mungu makusudi watu waweze kupata kufanywa wana wa Mungu. Uhusiano wake (Mwana) ulikuwa muhimu zaidi kuliko hali ile (chini ya sheria), na matokeo ni makubwa zaidi vilevile. Msemo unaweza kusemwa kuwa alizaliwa na mwanamke ili kutukomboa katika utumwa wa dhambi na mauti. Lakini Paulo anaeleza jambo hakika la kufaa lililokuwa na huo ukombozi, Yesu alikuwa Mwana wa Mungu, na kwa kuzaliwa kwale tuna mwanzo wa jamaa ya Mungu: lilikuwa lengo la Mungu kwamba yeye "awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi"(Rum. 8:29). (4) Kama tukisema, katika kipindi cha fundisho la mitume tuna kikomo cha mambo ya ufunuo wa Mungu, ambacho kilikuwa kwa taratibu kinaendelea mbele, kulingana na hali ya mambo yanayofanyika katika kila kusudi la sehemu iliyokuwa inafunuka. Mwishowe Mkombozi alipozaliwa, aliyeahidiwa siku nyingi na Mungu kwa "sehemu nyingi na kwa njia nyingi" kwa ufunuo wa Agano la Kale, ndipo ikatangazwa kwamba kwa njia ya Mwana wa Mungu watu wanaweza kuwa wana wa Mungu. "Wote waliompokea (waliomwamini) Jina lake - aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu"(Yohana 1:12 ). Kwa jinsi hii zinaweza kudokezwa ahadi za uzima wa milele katika Agano la Kale, ila maelezo yake dhahiri yalitiwa pamoja na udhihirisho wa Mwana wa Mungu. Kwa yeye watu hupokea "hali ya kuwa wana". Kupokea hali ya kuwa wana. Njia ya kukubali taarifa haina bila maneno mengine ya kuthibitisha kwa mfano katika "kutumwa" Mwana wa Mungu.Uzazi wa ki-Mungu umethibitishwa pande mbili: katika maana timilifu na iliyo kamili, hata kuwepo katika mwili wake, kwa suala la Yesu; bali kwa "utu upya" ukafanyika miongoni mwa wana wa watu, katika naman ya kuwaza na kwa uadilifu kufanywa upya kwa njia ya neno, kwa suala la kupokea hali ya kuwa wana. "Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi" ( Yakobo 1:18 ); au kwa maneno ya Paulo: "Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo tutende matendo mema" ( Efe. 2:10 ). Ni jambo la kuvutia kuona kwamba katika hotuba iliyotolewa kwa wasomaji Wagalatia hapo kwanza Paulo alipowatembelea huu ushuhuda maradufu hutokea. "Kwenu neno la wokovu limepelekwa"- Mungu alilipeleka neno - na huenda ikawa hapa ya kuwa (kama katika Ebra. 4:12). Neno lina maana mbili, ujumbe uliohubiriwa na yeye ambaye ujumbe ulitangaza habari zake - neno alifanyika mwili, ambaye kwake Paulo anatumia maneno yaliyo katika Zaburi 2:7: "Ndiwe Mwanangu, Mimi leo nimekuzaa" ( Mdo13: 26,33 ). "Kupokea hali ya kuwa wana" kunaleta familia kwa Mwana - hivyo anathibitisha ya kuwa "haoni haya kuwaita ndugu" (Ebr.2:11). Ila anaufurahia Undugu nao, si kwa sababu ya kuhusiana na badiliko lingine, bali kwa sababu ya "kuzaliwa mara ya pili", wana familia (jamaa) iliyofanana; na jambo la hakika kuwa wana- "kwa kuwa ninyi ni wana"- imeonekana, anasema Paulo, kwa kuwa "Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, Aba, yaani, Baba" (aya ya 6). Yatupasa kuona hali iliyosambamba: Mungu alimtuma Mwanawe ulimwenguni: Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu. Chanzo katika msuala yote mawili ni cha Mungu- njia ambayo kwayo nguvu ya Mungu inadhihirika yaweza kutofautiana. Kwa uwezo utendao kazi wa Roho Mtakatifu Mwana alitumwa; kwa uweza wa Roho- neno Roho wa Kristo anaumbika katika watu. Kwa sababu ni maisha ya Kristo yanayofunuliwa kwa aaminiye, ni maisha ya kumtegemea Mungu, ya ushirika na Mungu, ya kumtii Mungu, ya kumtumikia Mungu. Na kama Mwana alivyomwomba Baba siku zote, vivyo hufanya wana wa Mungu. Kwa kweli jambo hili la kuangaliwa la sala inayoelekezwa kwa Mungu na kutiwa wazo la kuwa njia ya kumkaribia ipo wazi, katika fikira za Paulo ni za nguvu hapa. Hizi zaweza kuonekana tunapotazama kwa makini katika injili na kuchunguza ni jinsi gani Yesu anatumia maneno "Baba", "Baba yangu", "Na sasa Baba mwenye haki". Kwa sababu ya uhusiano wake wa kipekee na Mungu anatumia mtu wa kwanza "Baba yangu". Lakini hakuna mwingine bali yeye aweza kunena hivyo. Wana wengine wote wa Mungu wanashiriki hali ya kuwa wana ambamo hakuna aliye wa kwanza; basi kwao Yesu aliwafundisha kusali "Baba yetu". (5) Katika kutumia sala hii, ikifahamika vema aaminiye hukumbuka ya kuwa haki yake ya kumkaribia si ya kumiliki peke yao, wala si haki ya mtu binafsi. Yeye ni mmoja wa jamaa, amekombolewa na Mwana wa Mungu, naye akiwa mmoja wa jamaa, akawa na haki kutumia ishara ya mtoto kwa Baba yake ambayo na wengine waishiriki, kwa maneno ya "Baba yetu". Maelezo yaliyo katika Gal. 4:6, kama yalivyo sawasawa katika Warumi 8:15, bila shaka ni ushahidi unaoitwa Sala ya Bwana . Ni Sala ya Bwana kwa kuwa ni yeye aliyeitoa, lakini ni sala ya wafuasi kwa ajili ya kuitumia. Kutumika neno lilo hilo maradufu "Aba, Baba", hapa na katika Warumi 8, lenyewe linatosha kudokeza kuwa jambo lilo hilo linaloandikwa linapatikana katika sehemu zote mbili. Warumi ni nyongeza ya habari ya Wagalatia juu ya jambo hili kama katika mambo mengine yaliyoshughulikiwa katika nyaraka mbili. Neno "roho" limezungukwa na mengi ya Mashindano ya maneno, wakati likiangaliwa katika maana na matumizi kungeruhusu mng'ao na uzuri wa nuru ya Mungu ing'ae toka kwake. Mfululizo uliotofautiana katika maneno unazunguka katika barua iliyoandikwa kwa Warumi toka mlango wa 7:7 hadi 8:17- wema na uovu, kiroho na kimwili, utu wa ndani na utu wa nje, sheria ya akili na sheria ya mwili, neno "nami au mimi" ambalo sasa ni moja na mara hiyo lingine, mwili na roho. Maneno matatu yamelinganishwa kwa Warumi 8:10 yanayofanya matumizi kuwa dhahiri: " Ikiwa roho wa Mungu anakaa ndani yenu", "Ikiwa mtu awaye yote asipokuwa na roho wa Kristo, "Na Kristo akiwa ndani yenu". Roho katika fungu hili la maneno mara moja ni roho wa Mungu, roho wa Kristo,na Kristo ndani yetu, Mahali alipo roho wa Mungu na roho wa Kristo, ndipo "ninyi hamuwi katika mwili bali katika roho" ingawa kama katika suala la Paulo kuna kulia kwa huzuni, "Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?" (Rum.7:25) Ukiwa ni ushahidi kutumwa roho wa Mungu, na lugha ya Sala ikiwa na ushahidi kabisa, ilithibitisha mara hiyo walikuwa wana. "Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu kwa njia ya Kristo. ( U.V. na R.V. ).Wasirudi "tena" kwenye utumwa - wapotoshaji walitoa ombi la uongo, kujionea hali ya kufanywa Mwana kulifanya sio wa kweli mwito wa kutoka utumwani: ila wana waovu walirudia katika utumwa. Lakini wana walio tayari na wazima katika hali ya kufanywa Mwana wanatambua kwamba hali ya kufanywa wana inaleta urithi, na wazo likipita katika maelezo yenye mifano ya watoto kuwa kama watumishi katika kukua kwa wana, huzunguka katika maana inayoanza ya urithi: "warithi sawasawa na ahadi" (3: 29 ); "warithi kwa Mungu kwa njia ya Kristo" (4:7). HATARI YA KURUDI NYUMA (4:8-11) Kutengwa kwa vituo katika Biblia (U.V) aya ya 8 na 9 kunaonyesha kwamba unganiko la neno la kwanza "LAKINI" lina "kurejea nyuma" aya ya 9. U.V. inasomwa kama ifuatavyo : "Lakini wakati ule, kwa kuwa hamkumjua Mungu, mliwatumikia wao ambao kwa asili si Miungu: bali sasa mkiisha kumjua Mungu, au zaidi kujulikana na Mungu, kwa nini kuyarejea tena mafundisho ya kwanza yaliyo manyonge, yenye upungufu, ambayo mnataka kuyatumikia tena?" Tofauti ya kuhuzunisha i dhahiri katika aya hizi na lugha inapokuwa na shauku kuhusu hali ya uwana wa aya za awali. (6) Kwa kutazama mambo ya hakika yenye Utukufu yaliyounganika na Injili ya neema ya Mungu, ni namna gani kuweza wao kurejea tena kwenye utumwa walikokombolewa? Walikuwa kama watu wa Mataifa wasio na Mungu, na walitumikishwa kwa desturi za kuabudu vitu ambavyo si Miungu. Hakuna ujinga uliowazi zaidi wa kuabudu sanamu kama ibada yake isivyofaa.. Miungu iliyoabudiwa haina sifa na nguvu walizowahesabia, wamewekewa dalili za tabia ambazo zimo tu moyoni mwake aabudie. Lolote lililokuwa na sanamu lilikuwa kwa ajili ya mtengeneza sanamu, lakini hakuna mstadi anayeweza kuhalalisha sanamu na sifa ya Mungu. Kwa kwenda mbio sana Hosea anaeleza: "Fundi ndiye aliyekifanya, nacho si Mungu kamwe; naam, ndama ya Samaria itavunjika vipande vipande"(8:6). Ujinga wa kuabudu sanamu uliingia mioyoni mwa Wagalatia mahali pa kumjua Mungu wa kweli. Hii ni hatua ya kwanza ya kuonekana isiyoepukika katika wokovu. Inabidi pawepo kumtambua Mwenyezi Mungu ya kuwa Yeye ni Muweza yote, na kwamba yupo juu na ni Mtakatifu, mwenye haki na wa kweli, Mwenye Upendo na Ustahimilivu. Hatuwezi kujua hivi isipokuwa Mungu akijifunua mwenyewe, na hata hivyo, kufahamu kwetu ufunuo sio nafasi ya kujitukuza. Maana kuna mwelekeo mwingi, wa muhimu zaidi, hata hivyo unawiana: maarifa aliyopata mwanadamu si ya uwezo wake, kwa kuwa sio tu neno lililofunuliwa latoka kwa Mungu, bali utendaji kazi wake kabisa juu ya wanadamu ni wa Mungu. Kwa hivi mwanadamu ametwezwa na kufaa kwa ajili ya wazo linalomfanya kuwa bora ya kuwa "amejulikana na Mungu". Ndani ya fungu hilo la maneno vile vile mna wazo la kina, sio tu kwamba Mungu anamjua mwanadamu, ila ni kwamba Mungu anamkubali mwanadamu. Kwa maana hii Paulo anasema: "Lakini mtu yoyote akimpenda Mungu, huyo amejulikana naye" (1Kor.8:3 ). Kwa kugeukia dini ya Kiyahudi, Wagalatia walikuwa wanarejelea kwa mtindo wa alfabeti mambo ya asili - ambayo Paulo ayaita "Manyonge, yenye upungufu" kuyatumikia tena. Mambo ya sheria pamoja na utoaji wake amri na kanuni zake za ibada, kwa upana yahusika na mwili wa utu wa nje, yanashughulika na msingi. Torati ilikuwa dhaifu kwa kuwa haina nguvu kuwapa watu uzima au ushirika na Mungu: sheria ilikuwa na upungufu katika unyonge wake inapolinganishwa na utajiri wa utukufu wa Mungu katika Kristo Yesu Mwana wake. Basi Paulo anaelezea kugeukia dini ya Kiyahudi ni kama kurejea nyuma, kurudi nyuma, ingawa ni dhahiri kwamba mwenendo wao wa kwanza katika maisha haukuwa na njia iliyounganika na sheria ya Musa. Ni kwa njia gani kuna hali ya jinsi moja sambamba kati ya mwenendo wao wa kipagani hapo kwanza kwa kugeukia utaratibu wa Torati kwao ilikuwa ni kukengeuka? Ni wazi, Paulo hawezi kuwa anafikiria hapakuwepo kuhitilafiana kati ya mambo makuu ya sheria ya Mungu, takatifu, ya haki na njema, na manyonge, mawazo mabaya na hali ya matendo ya ibada ya kuabudu. Usawa unatimilika juu yake aabuduye. Yote yanatumikia namna ya sheria; yote mawili yalishughulika na mambo ya msingi; yote kwa ushawishi wao yalikuwa dhaifu kwa mtu anayeabudu; kama kutimiza, hayakuwa na jambo lolote la kutoa ambalo lilistahili kudumu. Torati, kama desturi za kipagani, ilipeleka katika kujiamini binafsi, na mapenzi yakiwa katika matendo ya mwanadamu; hayakutoa kumwona Mungu kunakokuja kwa imani. (7) Ramsay ameelezea desturi za Kifrigia katika kitabu chake, miji na Uaskofu wa Frigia, kwa maneno yafuatayo: "Mfano wa dini uliotiwa madoido mno ulitawala katika nchi. Ibada ya kuamini mambo ya kichawi katika kanuni za mfumo ulio wa juu juu, na utii ulioonyeshwa kwa maelekezo ya makuhani, yalikuwa kwa wote miongoni mwa idadi kubwa ya wenyeji wasioelimika. Utaratibu wa kutenga madaraja kwa makuhani katika sehemu ambazo watu wengi hukutana pamoja kidini kwa ukubwa yalieleza wazi nia ya Mungu kwa wanaomwabudu. Kwa hivi serikali ilikuwa na utaratibu wa kuabudu mambo mawili yaani, Mungu na sanamu, na mfumo mzima na manabii wake, makuhani, sheria za dini, adhabu liliyowekwa na Mungu kwa ajili ya kuvunja sheria ya matendo ya ibada, maonyo na maneno ya kutia hofu, na orodha ndogo ya kuamini mambo yasiyoeleweka, kwa kuangalia yalionyesha usawa halisi katika mfano unaotumika nje kimwili katika matendo ya Kiyahudi ya kale kwenye ibada na kanuni ya dini. Hayapo hivyo, hadi haya yakifahamika vema kama Wagalatia 4:3-11 yanakuwa wazi na ya kawaida. Katika ujumbe huo Paulo anadokeza ya kuwa ushirika wa watu na kuenenda katika mtindo wa Kiyahudi kwa Wagalatia walio Wakristo ni kurejea katika mfumo wao wa kale wa mataifa. Baada ya kuwekwa huru toka utumwa wa vifungo vigumu vya matendo ya sheria ya ibada, mara nyingine tena walikuwa wanajiweka wenyewe katika vifungo vya sheria nyingine ya kuabudu, ambayo kwa kulingana ni ngumu. Kwa tendo lao walikuwa wanajionyesha wao wenyewe kutokuwa na akili ( Gal.3:1), bila akili iliyoelimika- ambayo yaweza kuona kweli hali ya mambo. Kuna mkazo wa kusudi katika hali iliyo karibu na 'kukosa akili` na 'Wagalatia` maana lilikuwa kundi la watu walioelimika zaidi, lilipopingana katika kuamini mambo yasiyo ya kweli ya wenyeji, ambali kwa shaauku lingekaribisha jina la jimbo. Huko kutamkwa 'Wagalatia wasio na akili`, tayari kunatazamia kukatazwa kwa urefu kutofanya hali hiyo (4: 3-11), 'Wagalatia wanaozama katika desturi waliyokuwa wameelimika hadi kwenye ujinga na kuamini mambo yasiyo ya kweli ya dini ya wenyeji`" Luther, ambaye alivutwa na waraka huu, na yeye ambaye mapinduzi katika ulimwengu wa dini kwa matokeo yaliyofanyika, aliona kidogo hali inayofanana. Tunanukuu toka tafsiri halisi ya Kiingerza ya Jumla ya Fafanuzi za Luther kwa Wagalatia iliyochapishwa katika 1944: "Lakini ni kwa nini anasema" Paulo ya kuwa Wagalatia walirejea tena Mafundisho Manyonge, yenye upungufu au matendo ya ibada, yaani ni kusema, kwenye torati, mahali ambapo hawakuwahi kuwa na sheria? Maana walikuwa ni Wamataifa (ijapokuwa aliandika mambo haya kwa Wayahudi vile vile, kama baadaye tutakavyoeleza) au ni kwa sababu gani anasema kidogo kwa jinsi hii? Zamani mlipokuwa hamumjui Mungu, mliwatumikia wale ambao kwa kawaida hawakuwa Miungu: bali sasa mkiona mnamjua Mungu, kwa nini ninyi kurejea nyuma tena, mkamuacha Mungu wa kweli na kuabudu Sanamu? Je! Paulo anachukulia kuwa ni mamoja, kutoka kwenye ahadi kuelekea katika torati, toka katika imani hadi kwenye matendo ya sheria, na kuwatumikia miungu ambayo kwa kawaida sio Miungu? Ninatoa jibu: Yeyote akianguka katika sharti la kuhesabiwa haki, hamjui Mungu, na ni mwabudu sanamu. Kwa hiyo ni mamoja ikiwa baadaye anarejea tena katika torati au katika kuabudu sanamu: yote ni mamoja, iwe anaitwa ni Monke, Mturuki, Myahudi, au ni Mbatisti. Maana sharti linapoondolewa, halibakii lolote lingine bali kosa, udanganyifu wa moyo, kutokutii na ibada ya sanamu, kiasi gani lolote linaonekana kwa utu wa nje kuwa kweli kabisa, kumtumikia Mungu wa kweli na Utakatifu wa kweli". (8) "Sababu ni, kwa kuwa Mungu anapenda au aweza kujulikana si kwa njia nyingine kuliko kwa Kristo, kulingana na msemo huo wa Yohana 1. Mwana wa Pekee aliye kifuani mwa Baba, yeye amemthibitisha. Yeye ni Mzao aliyeahidiwa Ibrahimu kwa yeye Mungu ameweka ahadi zake zote. Kwa sababu hii Kristo ndiye pekee anayeonyesha, kama ninyi mnavyoweza kusema, kwa kioo ambacho kwayo tunamwona Mungu, hivyo ni kusema, tunajua mapenzi yake. Maana katika Kristo tunaona kuwa Mungu si mkatili mwenye kulipiza kwa watenda maovu au hakimu, bali wa kupendwa zaidi, mwenye upendo na Baba mwenye rehema ambaye mwishoni atatubariki, hivyo ni kusema , ametuokoa katika torati, dhambi, mauti na mabaya yote na kuweza kupata neema, haki na uzima wa milele, asiyemwachilia Mwanawe, bali alimtoa kwa ajili yetu sote. Huku ndiko kumfahamu Mungu wa kweli, na ushawishi wa ki-Mungu, usiotuhadaa, bali unatupatia picha ya Mungu aliye hai. "Aliyekosa katika maarifa haya, inambidi ahitaji kuwaza dhana hii moyoni mwake: Nitaanzisha huduma ya Mungu jinsi hii . Nitaingia hivi katika utaratibu: Nitachagua kazi hii au ile, na ndivyo nitamtumikia Mungu, na sina shaka, bali Mungu ataikubali hii, na kunipa thawabu ya uzima wa milele kwa ajili ya yayo hayo. Maana yeye ni mwenye rehema na mwema, awapaye wote vitu vizuri hata wasiostahili na wasio na shukurani, zaidi mno atanipa nami neema na uzima wa milele kwa matendo yangu makuu na mengi mema na sifa njema. Hii ni hekima iliyo juu, haki na dini ambayo hoja yaweza kuamuliwa: iliyo ya kawaida kwa mataifa yote, kwa Waromani Katoliki, Wayahudi, Waturuki Wazushi n.k. Hawawezi kwenda juu zaidi kuliko alichofanya Farisayo, ambaye ametajwa katika Injili. Hawana maarifa ya haki ya Mkristo, au ya haki ya imani. Kwa kuwa mwanadamu wa tabia ya asili hawezi kuona siri za Mungu. Vile vile: Hakuna aliye na ufahamu, hakuna amtafutaye Mungu. Kwa sababu hii hawatofautiani kabisa kati ya Mkatoliki, Myahudi, Mturuki na Mzushi. Kwa kweli ipo tofauti ya watu, maeneo, kanuni za ibada, dini, matendo na namna ya kuendesha ibada: ijapokuwa yote ni mamoja na sababu ni ileile, moyo uleule, wazo na kufikiri sana katika hayo yote. Maana Mjaluo anafikiri jambo lilo hilo ambalo mkataba- mwanaume mtawa anafanya: analoita, kama nikifanya hivi au kazi ile, Mungu atanirehemu: Kama nisipotenda hivyo atakasirika. Hakuna lililo dogo kati ya matendo ya binadamu na maarifa ya Kristo. Kama maarifa haya yakiwa giza au yakiharibika uzuri, yote ni mamoja ukiwa wewe ni Mtumwa mwanaume, Msukuma, Myahudi." "Maana ninaona shaka kwa ajili yenu" alisema Paulo: sio tu kwa ajili yenu, ila kwenu: tendo lao la kugeukia kushika siku na siku kuu hofu ilimjaa ya kuwa kazi yake yote ingekuwa bure." OMBI LAKE LILIKUWA JUU YA MAPENZI YA KUONA WAO WENYEWE (4:12-20) Hangaiko la Paulo labda halipo mahali pengine wazi zaidi kuliko katika waraka huu. Kwa moyo, juhudi, mashaka, upinzani wa nguvu kwa hao waliokuwa wanaharibu kazi yake wote wanaonekana, na pamoja nayo yote tunamtafakari huyu mtu. Hofu ya kushindwa katika kazi yake miongoni mwao inapelekea upendo wa kina kwa kuwaomba, akikumbusha safari yake aliyowatembelea, matokeo yake na kuitikia kwao. "Ndugu zangu, nawasihi iweni kama mimi, maana mimi ni kama ninyi." Yeye na Barnaba walipokuwa nao kuhusiana na maadhimisho ya desturi hawakutenda, hawakushika sikukuu. Walikuwa wajumbe walioleta neema ya Mungu kwao. Walijua Torati na kuwa walikuwa wanatumikishwa nayo, ila walipofika Galatia wakiwa na injili, walikuwa huru katika Torati kama Wagalatia wenyewe. (9) "Iweni kama mimi" unganeni nami kwa kusimama katika imani ndani ya Kristo aliyesulubiwa na kufufuka. Sehemu hii ya waraka katika usemi ni ya namna yake kabisa, na ukweli huu unatusidia kutambua misemo iliyotajwa ambayo inaweza pengine kutoangaliwa. Hapo kwanza tumeona ya kuwa Paulo anataja mawasiliano toka kwao hadi kwake mwenyewe, na vile vile tunaweza kuona maneno yaliyotajwa waliyotumia kwake. "Hamkunitendea ubaya wowote"- B.H.N. Yaelekea kupatia neno lilitumiwa kwa Wagalatia. Yanaweza kusemwa hivyo kwa namna ya kuelezea ni kwa nini walibadili mwenendo wao. "Hamkunidhulumu", Paulo anaendelea, "ila sasa mnafanya. Wakati ule hamkufanya hivyo, bali kila kitu vingine. Hebu tukumbuka ni jinsi gani mlinipokea", na anawakumbusha udhaifu wa mwili uliomsumbua alipokuwa kati yao- udhaifu wa aina ambayo kwa kawaida ungeangaliwa kana kwamba ni malipo ya Mungu yaliyostahilika; lakini badala ya kumdharau walimpokea kana kwamba ni malaika wa Mungu. Kwa furaha yao wangalimpa macho yao, hivyo kwa utayari walitoa vitu vyao wavipendavyo. Ulikuwa ni ugonjwa gani ambao ulimsumbua Paulo alipokuwa Galatia? Ni wazi ushahidi kamili kwa nadharia yoyote Haiwezekani, na maelezo mengi yalikwishaletwa. Kwa asili kuunganisha na ushahidi huu wa ugonjwa wake na mwingine ushahidi uliotajwa kwa 2 Kor. 12:7 mahali anaposema mwiba katika mwili, tunapata sehemu zote mbili limetajwa kwa kuandikwa tatitzo lilelile. Kwa ushahidi uliotaja macho mtazamo ulioshikwa kwa upana umetambulisha maradhi yake na maumivu makali ya shida ya jicho, yaelekea baada ta tokeo la upofu uliosababishwa na kukutana na Bwana aliyetukuzwa akiwa njiani kwenda Dameski. Lakini katika uandishi wake Paulo ameweka suala hili labda kama mwandishi awaye yote. Ramsay ametoa shauri lingine lenye maelezo ambayo yanasifu sana. Katika Paulo wake, Traveta anatoa sababu ya kuwa iliompeleka Paulo na Barnaba hadi Antiokia. Ramsay anasema: "Katika kupita toka Perga hadi Pisidia Antiokia, wasafiri walipita katika jimbo la Rumi Pamfilia hadi jimbo la Rumi Galatia, na safari yao iliyobaki imetiwa ndani ya Galatia hata waliporudi Perga. Basi tunayo barua aliyoiandika Paulo kwa Makanisa yaliyoko Galatia, ambayo kwayo anasema, 'Mwajua ya kuwa naliwahubiri Injili mara ya kwanza kwa sababu ya udhaifu wa mwili - kati ya safari zangu mbili; na jaribu lililowapata katika mwili wangu hamkulidharau wala kulikataa, bali mlinipokea kama mjumbe wa Mungu'. Tunajifunza hapo kwa Paulo mwenyewe ya kuwa ugonjwa (kwa ujasiri tunaweza kusema ogonjwa mkubwa) ulikuwa wakati wa kwanza alipohubiria makanisa ya Galatia. Maneno hayadokezi ya kwamba ugonjwa ulimuanza akiwa Galatia; sana yalikuwa na tafsiri ya kwamba ugonjwa ulikuwa ndiyo sababu iliyomfanya aje hadi Galatia na kuwa na nafasi ya kuhubiri pale; pia yanadokeza ya kwamba udhaifu wa mwili ulidumu kwa muda fulani mrefu, nao ulikuwa wa kuonekana kwa wageni, wakati akiwa Galatia. "Hapa tuna sababu iliyodokezwa na Paulo mwenyewe, kikamilifu inayoeleza jambo lote geni la fungu dogo la maneno yaliyo katika Matendo ya Mitume. Paulo alikuwa na ugonjwa mkubwa alipokuwa Pamfilia na kwa sababu hiyo aliondoka Perga na kwenda hadi Antiokia. Sio lazima kurudia maneno ya kusadikisha ya kwamba hii kwa utimilifu inapatana na maelezo yaliyotolewa. (10) Udhaifu wowote ulielekea kuletwa kwa kutumbukia ghafla katika hali inayodhoofisha ya Pamfilia baada ya safari ngumu na ya kuchokesha ya kutembea kwa miguu kupitia Kipro, akifuatana na kichocheo thabiti chenye kazi ya kueneza ujumbe wa injili, jitihada ikifikia upeo katika hali ya fahamu za kujitahidi sana kwa bidii kubwa pale Pafo. Tiba ya asili na kutumiwa na watu wote kwa ugonjwa wa jinsi hii ni kwenda nchi za nyanda za juu bara; na hali ya Antiokia (kadiri ya futi 3,600 juu ya bahari, imetiwa vivuli vya milima ya upande wa kaskazini mashariki, inatazamana na uwanda mpana upande wa kusini na kusini - magharibi), wakiwepo idadi kubwa ya Wayahudi, na muunganiko wa shughuli za kibiashara na miji ya pwani ya Pamfilia ikafanya iwe ni sehemu inayofaa kwa kusudi la Paulo". Ramsay vilevile anadokeza ya kuwa malaria ya vipindi ilikuwa "mwiba katika mwili". Ansema: "Sifa ya nchi ya Pamfilia sio tu kwa hali yake eneo nusu lililolimwa, bali nyakati zote, haina budi ilikuwa inachokesha na ilifikiriwa huleta desturi isiyoonekana kwa udhaifu uliopo. Basi yaelekea kwa kawaida mtazamo uliokubalika wa kuwa 'udhaifu wa mwili' uliomfanya kwa nini Paulo akawa na nafasi ya kuhubiri kwa Wagalatia, yalikuwa maradhi yale yale yaliyomsumbua mara nyingi kwa vipindi. Nimedokeza ya kwamba ugonjwa huu ulikuwa aina ya homa ya maralia sugu; na, katika mtazamo au maono ya kutoridhika na hali, ni muhimu kukaa katika maana hii; kwa kuwa nimepata kulaumiwa kwa kuzidi kushambuliwa kwa muda usiodumu. Hoja imewekwa ikiwa ugonjwa wa jinsi hii 'kwa kweli uliweza kuonyesha dharau yao na kuchukia sana'. "Udhaifu wa mwili" unaorudi kila mara katika hali fulani ambayo mtu anatakiwa mara kwa mara afanye kazi, unaleta uchungu na tokeo geni katika mwili wetu wanadamu.... "Kwa hiyo katika hali nyingine ya mwili homa ya maralia inakuja na maumivu makali sana na kushambulia ghafla, na viungo vya mwili kuwa dhaifu, wakati wo wote nguvu za mtu zikitaabishwa kwa kazi kubwa. Shambilo la namna hii ni kwa kuondoa nguvu kabisa: mgonjwa anaweza kulala tu na kujiona mwenyewe akitetetmeka, akiwa hoi wakati alikuwa hana budi kufanya kazi. Anajiona kudharau na kuichukia nafsi, na kuamini kwamba wengine wanaona sawasawa na kuchukia mno". Yaonekana kwamba ushahidi mwingine katika maneno yaliyoandikwa ya kuwa maralia iliangaliwa katika nyakati za zamani kuwa ni adhabu iliyoletwa na Mungu. Kuja kwa kushambulia ghafla ilionekana moja kwa moja ni tendo la Mungu. Ikiwa wazo la jinsii hii lilishikiliwa na Wagalatia, linatoa maana ya nguvu katika taarifa ya Paulo ya kuwa "hawakudharau wala kukataa-jaribu-udhaifu wangu wa mwili, bali mlinipokea kama malaika wa Mungu". Kwa kuelekea walifanya katika kile kilichoweza kutarajiwa, lakini kufanya hivyo waliamua kwa usahihi. Nyongeza kwa hii, maralia ya kuumwa na kichwa ilielezwa na mgonjwa kana kwamba "chuma cha moto kimesukumizwa kwa nguvu kupitia katika kipaji cha uso. Juhudi imefanywa ili kueleza ugonjwa wa Paulo kuwa ni kifafa, hali iliyo sawasawa iliwahi kudokezwa na viongozi mashuhuri waliojulikana kuwa na kifafa - Juliasi Kaisari, Napoleoni, Cromwell. Mashaka yamewekwa katika tendo moja kwa maelezo haya kama "maono" kwa huku kunung'unika ni jambo la kuangaliwa, na maono ya Paulo yameangaliwa hivi kama tokeo la ugonjwa. (11) Tofauti moja na hawa wengine, ingawa hivyo, ni ya kufisha katika kulinganisha. Paulo alihesabia nafasi yake, agizo lake ni kwa kukutana na Kristo aliyefufuka. Kifafa hakipatikani katika udhaifu wake kuwa namna ya welekevu wa jambo lake moja. Kwa nyongeza, maumivu sio kuangalia kifafa, na vyo vyote maradhi ya Paulo yanavyoweza kuwa ni wazi kwamba maumivu lilikuwa ni jambo linalosumbua ambalo kwalo Paulo angependa kuwa huru Bwana wake angetaka. Mara nyingine kifafa kimeungana na akili kutokuwa thabiti ambako kunaonyesha watu wengine walio na uelekevu, na watu waliokuwa wanamkosoa Paulo hawakukosa kumhesabia kuwa mwenda wazimu. Lakini maneno ya Ramsay katika masomo yaliyo ya Pauline ni sahihi na ya haki: "Kuangalia kwamba jambo lililompata Paulo akiwa safarini kelekea Dameski ilikuwa kwa sababu nyingine ya namna ya wazimu kwa upana ulisemwa kwa miaka ya karibuni. Hili shauri kwa kudhihirika bila kusemwa lilishikiliwa na wengi wanao jitenga na uwazi wakielekeza akili yao wenyewe. Kwa uwazi na uthabiti lilielezwa na wasomi wengi ambao ni wanyoofu. Wachunguzi wa kisayansi wamejadidili na kutoa jina kwa namna halisi ya wazimu ambao kwa maono ya uongo yaliyoletwa na wazimu wa Paulo yalipaswa kutajwa." "Mara hiyo waliwahi kuwepo wengi wenye wazimu katika nyakati zote lakini shida ambayo wengi wanaiona katika kumtofautisha Paulo miongoni mwao inazuka toka ukweli kwamba sio tu alimshawishi kila mtu aliyemsikiliza kuwa hakuwa ni mwenye wazimu bali aliinena iliyo kweli, tena kwamba aliubadilisha ulimwengu,aligeuza mwendo mzima wa historia, na kutufanya hivi tulivyo. Je! ulimwengu ulibadilika kwa neno la mwenye wazimu? Kufanya hivyo itakuwa kuacha imani yote iliyo katika utaratibu na umoja katika ulimwengu na katika historia; na kwa hiyo tunasukumwa katika dhana ya kwamba aliloonyeshwa Paulo ni moja ya mambo ambayo yahusu ushahidi unaopaswa kuchunguzwa na kupimwa bila dhana yo yote iliyokuja baada ya kufikiri sana iliyokwisha tajwa mwisho na akili ya mtu..." "Kwa hiyo inabidi iwe kweli ya kwamba Mungu hujifunua mwenyewe kwa mwanadamu katika njia moja au nyingine. Paulo ansema kwa nguvu kwamba alipokea ufunuo huu; haitupasi kutenga dai lake kuwa si la busara na kwa kweli si la muhimu. Madai mengi ya jinsi hii yanaweza kuwekwa kando upesi; lakini historia ni dhahiri kwamba suala lake ni moja ambalo lastahili uchunguzi, kupimwa, kwa jaribio lisilobadilika." Fungu la maneno katika aya ya 15; "Ku wapi, basi, kule kujiita heri?" katika UV halifahamiki vema. Lakini B.H.N. "Mlikuwa wenye furaha; sasa kumetokea nini?" hili fungu linatuweka katika mwendo wa kufahamu. Waliipokea ile kweli kwa furaha, wakijiona wenyewe ni wenye heri kwa upendeleo ambao sasa ni wao. Huku kupokea ujumbe wa injili kwenyewe kulidhihirisha kumshukuru Paulo kwa kuwa hakuna dhabihu iliyokuwa kubwa mno hata macho, mali iliyo na thamani sana kwa ajili ya Paulo wangeweza kumpa. "Hii "furaha" ni wazi ilipita na mafundisho mapya, pamoja nayo vile vile ilikwenda na kumpenda Paulo. Waliona hakuwa rafiki wa kweli - inaweza kuwa kwamba Paulo anawashika akiwazuia wapinzani wake, maelezo yake anapotumia neno "adui". "Je! Nimekuwa adui wenu kwa sababu nawaambia yaliyo ya kweli?" Ilisemwa ya kwamba wakati injili ilipoletwa kwao, alileta ujumbe usio kamili na upuuzi - ambayo kwa kweli ilikuwa kazi ya adui; ndivyo walivyodokeza wenye dini ya Kiyahudi. (12) Walakini, je! shida aliyoichukuwa, ni hiyo ya "adui?" Anauliza. Je! "kweli kushughulika" na watu ni "tendo la adui?" Wayahudi walijipendekeza kwao; hawakunena iliyo kweli, walijifanya ni wenye mapenzi ya furaha kwa Wagalatia, walakini hawakufanya vyema. Waliwaweka mbali - au "walitaka kuwafungia nje"; walifundisha kwamba walizuiwa katika wokovu wasipoishika Torati. Walifanya hivi ili Wagalatia "wawahangaikie (BHN) wao". Paulo yeye binafsi hakupendezwa kuwaangalia wao: alitaka mtu mwingine awe nao siku zote, na siku zote "awaonee shauku wao", kuwagawia ilikuwa kwa wema. Hakupenda tegemezi lao liwe juu ya Paulo; haijalishi ni nani aliwahudumia maadam huduma ilikuwa nyoofu na kwa ajili yao wapate mema wakajengwe. Lakini hapo umedokezwa ukweli kwamba waalimu waliokuwa wakifanya kazi kwa kuleta madhara kati yao hawakuwa wanawatendea mema, na mawazo ya Paulo yanapata maelezo kwa mfano ulio wazi wa kuona utungu - alifanya kazi ya kuwaleta wazaliwe katika Kristo, na sasa aliona uchungu kwa ajili yao kama anavyoteseka kuwarudisha kwenye uhuru wa wana wa Mungu. Alitamani kukaa nao, ili asiwaonye tena na kuwasadikishia ukweli, bali kwa sauti iliyobadilika inayopatana na habari njema ya Mungu. "Laiti .... Maana naona shaka kwa ajili yenu"; au kama maneno yayo hayo katika B.H.N. yanavyotokea kuwa na maana, "Nina wasi wasi sana nanyi". FUMBO LA MANENO (4:21-31) Baada ya ombi linaloshawishi kuwa mwaminifu kwenye injili ya Paulo aliyowahubiria Wagalatia, mtume anarudia swali juu ya Torati na huduma ya utumwa iliyowekwa juu yao hao waliojaribu kuitunza. Mlinganisho ulio mbele yake ulifanywa kwa cheo wakati wa utoto kwa mrithi na huo wa mtumwa, unadokeza historia ya wana wawili wenye hali tofauti katika nyakati za mababa. Maisha ya Ishimaeli na Isaka yameonyeshwa kuwa na kitu kinachoonyeshwa kwa fumbo la maneno katika kusudi la Mungu ndani ya Torati na katika Injili. "Niambieni, ninyi mnaotaka kuwa chini ya sheria", anaanza, "Je! Hamuisikii sheria? Kwanza tunaangalia namna ya matumizi ya Andiko. Sheria aliyopenda waisikie sio nyingine ya kufuatana na kufanya sheria ya Walawi, bali maandiko katika kitabu cha Mwanzo. Kati ya vitabu vitano, katika hiki cha kwanza ambacho pamoja vikiitwa Torati katika mgawanyiko mara tatu wa Agano la Kale kilichotendeka wakati ule, kitabu icho hicho ndilo "andiko" la aya ya 30, na kunena toka hiki kumetangulizwa na maneno "Imeandikwa". Mtindo wa kunena kwa jinsi hii unadokeza imani isiyohojiwa katika historia ili kutumiwa kwa namna ya kusadikisha maneno. Ibrahimu alikuwa na wana wawili toka kwa mama wawili, Mwanamke mmoja alikuwa Mjakazi aliyepewa mume akiwa mke-mtumwa kwa sababu mke wa kweli alikuwa hazai, ambaye alikuwa mke wa mfalme. Baadaye kwa muujiza wa Mungu mtoto akazaliwa kwa mke. Kwa kufuatana na tokeo la kukua kwa ukaidi wa kukosa adabu mtoto wa mjakazi ulipodhihirika, kukapelekea kufukuzwa wote wawili mama na mtoto. Paulo anakuza fumbo la maneno kwa maneno moja moja mengine ambayo yaweza kuwa kwanza kuonekana katika namna ya picha ya mfano. Wanawake wawili waliwakilisha maagano mawili, milima miwili, miji miwili na kuna wana wawili; hali ya hawa mama na wanao imeonyeshwa kuwa na maana, yote pamoja ikifanya kuwa na somo moja. (13) Masimulizi yote kama yalivyoandikwa katika Mwanzo yapo katika kuendelezwa desturi za nyakati za mababa kama ilivyoonekana katika sheria ya Khammurabi (aliyedhaniwa kuwa ni Amrafeli wa Mwa. 14:1, lakini kwa kubadilikabadilika mawazo ya watafiti wa mambo ya kale wamekuwa na mashaka na baadhi). Sheria ya mtawala huyu wa Babeli ilikuwa ikitenda kazi kwenye mipaka ya bahari ya magharibiya Mashariki ya Kati; na kati ya amri nyingine ilizuia kutorithi mwana wa Suria badala ya wa pili- mwana aliyezaliwa kwa mke wa kweli. Abram alipomwomba Mungu ya kuwa Ishimaeli aweze kuwa mrithi alikuwa akithibitisha sheria hii kwa kutambua urithi wa Ishimaeli. Lakini sheria ya Mungu ilivuka amri ya mwanadamu, na Ishimaeli hakuingiza kuwa mzao. Sababu ifanyayo kazi katika kuzaliwa wana wawili inahusisha kanuni ya Mungu. Mwili ulitosha kwa kumzaa Ishimaeli, katika jambo la kuwa kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, mienendo ya kimwili kwa uwazi kabisa ilidhihirika yenyewe katika maisha ya Ishimaeli. Wokovu hauna budi uwe wa kuongozwa, maadamu mwanadamu hana uwezo wa kujikomboa yeye mwenyewe, njia ya kuongozwa inabidi ije toka kwa Mungu. Hii inaonekana katika kila hatua ya kazi. Tunaiona kwa kuzaliwa Mwokozi aliyekuwa Neno akafanyika mwili; tunaiona katika ufunuo wake kwa utukufu wa Baba lililokuja kuwa neno la uzima; kwa kweli, mwendo mzima umeelezewa katika mafungu ya maneno ya mitume Mungu alikuwa ndani ya Kristo akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake. Kuna ulinganifu katika kazi hii ya roho kwa mzaliwa wa kwanza kwa namna"wana wengi" wanaletwa katika utukufu. Neno la Mungu ni wakili aliye wa muhimu na ushawishi wa maendeleo chini ya kutumia vizuri busara ya Mungu:"Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake" (Yakobo 1:18).Neno linaendelea kuongoza na kuwa chombo kinacho umba katika maisha yote ya uchunguzi katika kipindi. Katikati ya mwendo mzima ni nguvu ya Mungu inayoumba. (14) "Mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani; na kwamba si kwa nafsi zenu: ni kwa kipawa cha Mungu: si cha Matendo, mtu awaye yote asijivune. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu tutende matendo mema..., ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo". (Efe.2:8-10). Paulo hasiti kueleza sawasawa sababu mbili za lazima kwa wokovu wa mwanadamu ambao kwa fikira za kibinadamu yaweza kuonekana kutofanya kazi yakuridhisha: "Basi...utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka; kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kutimiza kusudi lake jema" (Flp. 2:12,13). Na ili isiwe huu utendaji kazi wa Mungu ukapelekea kuamini kwamba mambo yote ni amri ya Mungu anaongeza kusema, "Yatendeni mambo yote pasipo manung'uniko wala mashindano." Kwa upande wake mwanadamu akifanya kwa kupokea neema ya Mungu na kuziepuka dhambi badiliko la mwisho la kufanana na mwili wa utukufu wa Kristo litafanyika kwa "utendaji kazi wa hiyo nguvu ambapo anaweza kuyatiisha mambo yote kwake mwenyewe". Katika fumbo la maneno tendo la kuongozwa na Mungu likaonekana kwa kuzaliwa Mzao aliyeahidiwa Ibrahimu. "Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake" (Ebra. 11:11). Wala muujiza haukuuwekewa mpaka kwa Sara, maana Paulo ansema, "Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia, na hali ya kufa ya tumbo lake Sara: lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi" (Rum. 4:19-21). Kwa hiyo Paulo anaweza kusema ya kuwa "mtoto wa ahadi" - ambaye kwa sababu hii alionekana na Mungu kabla na akaingizwa katika kusudi lake "alizaliwa kwa roho." Mwili na roho, na mwanadamu na Mungu, mambo haya mawili ni mwanzo wa watoto wawili wa Ibrahimu. Kwa jambo hili, kama katika sehemu zote za shughuli za Mungu na wanadamu, basi huanza wa asili na baadaye wa roho. Wa kwanza Ishimaeli, kisha akasubiri muda mrefu wa miaka kumi na minne wakati ambao tumaini lote lilipungua nguvu, na mwishowe lilipokuwa wazi ya kuwa ni nguvu za Mungu pekee zaweza kufikisha kusudi lake, ndipo Isaka akazaliwa. Wakati taifa la Kiyahudi linawiwa hivi asili yao ni kwa kuzaliwa katika muujiza, huu haukulifanya taifa liwe "uzao", maana wao wote ni wana waliozaliwa kwa mwili toka kwa Isaka na Yakobo, nalo likiwa taifa likamkataa aliye mfano wa Isaka. Maisha ya Isaka, kwa kuzaliwa, na kutolewa awe dhabihu, kwa kurejeshwa tena, ni fundisho la mfano wa "Mzao" ambao kwa huo ahadi zitatimilika. Maagano mawili yamelezewa kama ya Ibrahimu na lingine la Musa, ingawa majina yamefungamanishwa hivi si mamoja katika masuala mawili. Yeye mwenyewe Ibrahimu alipokea agano la Mungu; Musa alikuwa mjumbe wa agano la Mungu kwa Israeli. Moja lilikuwa la mtu mmoja kwa matumizi yake; lingine la taifa. Lamtu mmoja lilihusu urithi wa nchi usiokoma, na kwa hiyo kupewa uzima wa milele: la taifa lilihusu kukalia nchi, taifa likiendelea kutii. La Ibrahimu, kwa kupatana na kanuni "baadaye huo ulio wa kiroho", ni la mwisho kutenda kazi, na bado linasubiri siku ijayo kwa ajili ya kutimilika kwake. La Musa, likiwa la kwanza kufanya kazi, na likiisha timiza kusudi lake katika nyakati za mitume, limeitwa "agano la Kale" ambapo la Ibrahimu linaitwa "agano jipya". (15) AGANO JIPYA Kwa ukubwa wa "upya" maadamu linatoa jina kwa uzima wa milele, ni msamaha wa dhambi. "Agano la Kale" na marudio yake dhabihu halikuwakamilisha wale wamkaribiao Mungu.Dhabihu inayoweza kufanya hivi ni sadaka ya Yesu Kristo: "Tumepata utakaso kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu" (Ebra. 10:10). Hivyo Yesu alikisema kikombe cha kumbukumbu: "Hii ndiyo damu yangu ya agano jipya, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi" (Math. 26:28). Hii habari ya Yesu kwa maneno imeungana na unabii ulio mara dufu muhimu katika Agano la Kale. Yeremia, akiwa wakati ule ule wa kuangushwa Ufalme, anatabiri kukusanyika tena na kujengeka tena uhai wa taifa lao. Agano la Kale lilivunjwa na Israeli, lakini Mungu atawaanzisha wakisha kusanywa na kuingia agano jipya litakalo hitilafiana na la kale kwa mambo kadhaa mahususi. Sheria aliyopewa Musa iliandikwa juu ya mbao za mawe, mfano mzuri wa mioyo ya jiwe ya Israeli, isioitikia mapenzi ya Mungu kijiwe,.Chini ya agano hili jipya Mungu "atausamehe uovu wao, wala dhambi yao hataikumbuka tena". Ukweli huu sana unahusika kwamba masharti yaliyo kwa ajili ya msamaha inabidi yawekwe, na kwa sababu hiyo kutambulisha pasipo shaka agano jipya la unabii wa Yeremia na ule uliothibitishwa katika damu ya Bwana iliyomwagika. Israeli wakikusanywa tena kila mmoja peke yake watakubaliwa na Mungu - uasi utakuwa umetakaswa, na wote watakao iingia nchi "wataliitia jina la Bwana", wakitambua ya kwamba katika Mlima Sayuni kuna ukombozi: Mkombozi atakuwa amekuja Sayuni na kumtenga Yakobo na maasi yake, ambao kwa upande wao watamgeukia Bwana, utaji unaofunika mioyo yao wakati wa sasa utakuwa umeondolewa. "Imwagikayo kwa ajili ya wengi", Yesu alikisema kikombe kilichokuwa mfano wa damu ya agano jipya. Ni neno moja tu, lakini mwandiko umetambulika na wasomi waangalifu kuwa umetaja unabii wa Mtumishi wa BWANA, atakayefanya nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, ambaye Mungu alimsema: "Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki" (Isaya 53:11).Umuhimu na ubora wa agano jipya umeshughulikiwa katika Waebrania, mlango wa 8 hadi wa 10, unabii wa Yeremia mlango wa 31 ukiwa na kipengere kinachoanza na vilevile msingi unaoweka wazi zaidi sura. YERUSALEMU: WAKATI ULIOPITA NA ULE UJAO Milima miwili ni Sinai na Sayuni, lakini Sayuni kuna mawazo yanayotatiza. Kwa kuwa Yerusalemu upo mbele yetu kwa vipindi viwili, wakati uliopita na ujao: na katika wakati uliopita, hapo Torati ya Musa ikiwa na nguvu ndani ya nchi, Yerusalemu ulikuwa katika fumbo la maneno kwa Paulo pamoja na Sinai: "Maana Hajiri ni kama mlima Sinai ulioko Arabuni, umelingana na Yerusalemu wa sasa; kwa kuwa anatumika na watoto." Yerusalemu chini ya agano la Musa uliwakilishwa na Sinai; sehemu zote mbili ziliungana na Torati na kuwiwa umuhimu wao kwa sheria. Sinai palikuwa pa kupewa agano la kale - na chini ya agano hilo Yerusalemu ulikuwa mji ambao matoleo yaliyotakiwa na kufanywa kwa sheria. Torati ilipotanguliwa mji ulishiriki hukumu juu ya watu. Miji ya Palestina ilifanywa ukiwa watu walipopelekwa utumwani, na kidini Yerusalemu ukakoma kuwa na umuhimu wake wa kwanza, kitaifa na kimataifa. Ushindani ukakua katika vilima saba na Tiberi, na kwa karne watu wamegeukia Roma kwa ajili ya uongozi na kufundishwa. Ni ishara ya kuja badiliko la kwamba tayari umuhimu wa madaraka ya Palestina umerudi. (16) Wakati wa kipindi cha dola la ulimwengu, Rumi ukawa mji wake mkuu, lilipozunguka Mediterania, Palestina ilikuwa ndogo sana; lakini siku hizi, hapo ulimwengu mzima ukifanyika "makazi" umuhimu wa Palestina unarudishwa. Wakati hali iliyopita ya Yerusalemu imeunganika na Sinai, wakati wake ujao utakuwa katika msingi mwingine. Mungu ameuchagua Sayuni alikalishe jina lake, kwa Andiko kuingiza kabisa fungu la maneno. Hapo Mungu ameamuru baraka, hata uzima wa milele. Makuhani wake watavikwa haki, Watakatifu watashangilia kwa furaha; na hali iliyo sawasawa kwa hii ni aya inayofuata: "Na Makuhani wake nitawavika wokovu: na watauwa (watakatifu) wake watashangilia"(Zab. 132:9,16: 133:3) wakati huo Sayuni itakuwa na kuhani "aliyefanywa kwa kufuata uwezo wa uzima usiokoma", aliye mfano wa Melkizedeki; na Mungu atainyosha toka Sayuni fimbo ya nguvu zake (Zab. 110:2,4). Hapo chipukizi la Bwana likifunuliwa "kwa uzuri na lenye utukufu"(ona hapa lugha ya ukuhani mkuu akivikwa, Kutoka 28:2,40), ndipo "itakuwa ya kwamba yeye aliyebaki katika Sayuni, na yeye aliyeachwa ndani ya Yerusalemu, ataitwa Mtakatifu; yaani, kila mmoja aliyeandikwa kwa uzima (tafsiri ya Biblia nyingine) ndani ya Yerusalemu" (Isa.4:2,3)."Nitakufanya" asema Mungu, "utukufu wa milele, furaha ya vizazi vingi", maana watu watauita "mji wa Bwana , Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli" (Isa.60:1,14). Manabii watainuka kwa usemaji kuwa wakubwa kwa kusifu sana utukufu huu unaokuja wa mji wa Mfalme Mkuu. Basi tuna Yerusalemu katika vipindi viwili vya historia yake; kwanza ulipokuwa mji mkuu wa Ufalme wa Mungu uliosimamishwa juu ya msingi wa agano la Sinai na Isaraeli, wakati mkataba wake ulipounganika bila kutenganishwa na Sinai mlima wa Arabuni; na pili - na hiki ni bado ni kipindi kijacho wakati utakuwa kiti cha enzi cha Bwana ufalme ukisimamishwa tena na Mwana wa Mungu na watakatifu wake katika shughuli, na jina la heshima lililotolewa kwa agano la Mungu na Ibrahimu agano la uzima wa milele. Wana wawili wamesimuliwa kwa mama wawili na wameunganika na hali yao ya kama mama. Watoto wa Yerusalemu wa wakati uliopita walikuwa jinsi hii chini ya agano- sheria, na kama Ishimaeli walikuwa watoto wa mjakazi."Sheria inaainisha utumwa"" na Wayahudi walitumikishwa na torati. Sheria ya Mungu iliyotolewa kupitia Musa ilithibitishia hatia ya dhambi, na kwa kufanya hivyo ilifunua utumwa wao kwa dhambi. Wote walihitaji ukombozi, na huu torati haikutoa. Mtumwa hana jina la heshima ya kudumu nyumbani, nao Wayahudi wakiitumikia torati (au kutoijua siku hizi bado ni watumwa wa dhambi) "watafukuzwa". Kwanza Sara alinena maneno ya kukataa. Isaka alipoacha kunyonya (kwa umri alikuwa mkubwa kuliko umri wa mtoto aachishwaye kunyonya leo, na Ishimaeli aweza kuwa alikuwa na miaka kumi na saba). Sara alimwona mwana wa Hajiri akimdhihaki Isaka. Hali hii ikamhuzunisha, akataka ya kuwa "afukuzwe". Ibrahimu akawa hakuridhika kabisa kukubali, ila akaambiwa kwamba hivi yalikuwa ni mapenzi ya Mungu: "Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako; kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa." (Mwanzo 21:10-12). Ishimaeli akafukuzwa, naye Isaka akatajwa na Mungu kuwa mrithi. Uthibitisho huu wa Mungu kwa matakwa yake Sara unampa maneno ya maandiko kuwa na mamlaka, naye Paulo anayanukuu yakitanguliwa na "Andiko lasemaje?" (17) Paulo anaona katika dhihaka ya Ishimaeli maelezo ya upinzani usioepukika kwa mwili na roho. Chuki iyo hiyo ilionekana katika maudhi kwa Wakristo na Wayahudi. Hata vitendo vinavyokengeusha vilivyokuwa vinawapotosha Wagalatia vilikuwa ni udhihirisho wa Ishimaeli, sheria iliitumikisha roho, na kuwaonyesha hao Wayahudi wapo nje na kama waliokataliwa na sio warithi. Kwa namna nyingine kabisa anawatia moyo wasomaji wake katika kufashamu haki zao za hali ya juu. "Yerusalemu wa juu ni muungwana, naye ndiye mama yetu sisi." Kwa kutaja neno 'wa juu' halionyeshi eneo la mji wa kimbingu ambao huo wao walikuwa watoto. Si "Yerusalemu wa dhahabu" wa siku hizi katika mafundisho ya Ufalme wa Kikristo mafundisho ya nafsi isiyokufa yalipolazimisha makao kwa ajili ya walioondoka. Yerusalemu wa kipindi kijacho ni mji wa mbinguni, ukiwa na sheria ya kimbingu. Katika ishara iliyo katika Apokalpusi serikali yake, baraza lake la mji, vimeelezewa kuwa ni pande nne za mraba mji unaoshuka toka kwa Mungu. "Bwana toka mbinguni" Adamu wa mwisho, ni Mfalme wake. Ni wa juu, kama kiroho ulivyo juu kuliko wa mwilini, kama kutokufa kupo juu kuliko kufa, kama watu wa Mungu waliotiwa nuru wapo juu kuliko wakaidi, waasi waongozwao na mwili. "Mama yetu sisi" ni mfano mzuri, uliokuwa ombi la nguvu kwa Paulo. Ni jinsi gani kwa kufaa anamtaja Rufo, na "mamaye, aliye mama yangu pia" (Rum.16:13). Msafiri aliyechoka alipata kupumzika nyumbani na mama - faraja katika nyumba ya Rufo. Hivyo Mungu kwa upole wa nabii anasema; nanyi mtafarijiwa katika Yerusalemu" (Isa. 66:13); na fungu lenyewe la maneno linasimulia "taifa limezaliwa mara moja" kwa uchungu wa kuzaa Sayuni, taifa ambalo dunia imefanywa kuletwa kwa siku moja, kwa ufunuo (aya ya 7,8). Zaburi yaeleza kwamba Bwana ayapenda malango ya Sayuni kuliko maskani zote za Yakobo. Umetajwa kwa mambo matukufu, Ee mji wa Mungu" (87:2,3); na wageni toka nchi za Mataifa yenye kiburi, zikiisha jifunza malengo ya Mungu ambayo "ameyatamka" kuhusu mji, wanaonekana kama wameorodheshwa kuwa wenyeji wa Sayuni. "Huyu alizaliwa humo. Naam, mintarafu Sayuni itasemwa. Huyu na mtu huyo alizaliwa humo, na yeye Aliye juu ataufanya imara. Bwana atahesabu atakapowaandika watu kwamba mtu huyu alizaliwa humo". Kwa hiyo Sayuni ni mama yao: na tafsiri ya Biblia LXX, ambayo Paulo aliizoea, inasomwa: "Kila mmoja atauita Sayuni, Mama! Naam, kila mtu mmoja alizaliwa humo". Kwa nguvu inayopata kulazimisha kwake katika uzazi wa ki-Mungu kwa neno la Mungu, watu wa imani wanavutwa hadi Yerusalemu kuwa "mji wao mama"; kwa ushawishi Paulo anawavuta Wagalatia kwa huu kama anapofunga fumbo lake la maneno: "Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye muungwana." Ni jambo la kuvutia kujua kwamba barua waliyoandikiwa Waebrania ombi lipo juu kwa kuwekwa pamoja Sinai na Sayuni. Kuongozwa na jambo linalo andikiwa ni tofauti, kwa kuwa wasomaji hawakuwa sawasawa kabisa. Lakini, kuamini kama tunavyofanya kwamba Paulo aliandika barua zote mbili Wagalatia na Waebrania, tunaweza kuona uhodari ulioonekana kwa namna ile ile ya mazingira yaliyotumika kwa ajili ya maonyo. Tofauti kubwa ipo kwa kipengere kinachoanza - Wagalatia inaanza na habari za Ibrahimu nyumbani na kutimiza fumbo la maneno kwa usambamba wa milima miwili na wanawake wawili. Katika Waebrania vitisho vya Sinai pakiwa mahali ilipotolewa torati chini ya masharti yasiyochukulika kwa wale waliopo, ipo tofauti na furaha ya kushirikiana na malaika na watu katika kukusanyika kwenye mkusanyiko wa siku kuu katika Sayuni kwa waliohesabiwa haki katika Kristo, kwa upatanishi wake wa agano jipya. (18)