_____________________ WARAKA WA MTUME PAULO KWA WAGALATIA SURA TATU The Letter of Paul to the Galatians - Chapter Three SEHEMU YA TATU-KWELI YA INJILI YA PAULO: IMANI INAPITA TORATI. OMBI WAONE KWA KUJARIBU WENYEWE (3: 1-6) Ikiwa Kristo hakufa bure, km., kwa maneno mengine, kifo chake kilikuwa muhimu{2:21) katika wasomaji wa Paulo haukuna ambaye angepinga ya kuwa mauti yake ilikuwa kweli na ilikuwa kiini muhimu katika mpango wa Mungu kwa wokovu wao- basi kitu chochote kilichowaondoa toka kwa Kristo kiliwatoa toka kwa Mungu na ukombozi wake. Kuufuata mwendo wowote ambao ulikuwa na tokeo hilo ulikuwa upumbavu. Kwa hiyo yalikuwa ni maelezo ya kweli Paulo alipowaambia kuwa "Wagalatia wasio na akili". Matumizi ya neno la Kijiografia yaweza pia kudokeza ya kuwa hawakuwa wanaishi kulingana na ilivyotegemewa badala yake wao walijivuna.Kwa Wagalatia Paulo alikuwa na maana jimbo la Warumi la Galatia, na miji minne ya Galatia kwa karibu ilishughulika na utawala wa kifalme. Tabia ya miji ilishiriki fahari ya eneo hilo na utamaduni ambao kwa ujumla ulipatikana katika miji yenye mitindo ya Wayunani na Warumi- kujivunia maendeleo na elimu. Kwa watu wa jinsi hii, kuwa na kosa la upumbavu wa kugeuka toka katika neema ya Mungu imedokezwa ya kuwa jambo fulani liliwaloga. Ninani aliyewatupia "uchawi?" Paulo anauliza " Mbele ya macho yao Yesu Kristo aliwekwa wazi ya kuwa amesulubiwa." "Waziwazi mbele ya macho yenu"(B.H.N.) ni tafsiri ya kiarifa ambacho kinamaanisha "kuandika mapema", ambacho pia kina maana ya kujulikana mbele ya watu wote, kwa kutangaza kwa maandishi kwenye ubao wa matangazo au kwa kueleza na picha au tangazo la kubandika ukutani. Kuchukulia maana halisi ya neno, wengine wamedhania ushahidi ulikuwa barua ya kwanza ya Paulo kwao. Lakini kama tumeelewa usahihi hali ya mistari michache ya mwisho katika mlango wa 2, na kutambua ya kuwa Paulo yuko huko akikumbuka aliyoyasema alipomhuburi Kristo kwao, na ni wazi kwamba jambo la kutangaza habari linafaa fungu la maneno vizuri sana. Kwa maelezo dhahiri, ni kweli Paulo aliweka mbele yao habari za masihi aliyesulubiwa-ni jinsi gani kwa maelezo dhahiri sisi mwenyewe tunaweza kutambua leo tunaposoma maneno ya Paulo.Aliwafanya wamuone Kristo, aliwafanya waelewe ni jinsi gani kwa tendo la kumkubali Kristo iliwezekana kwa kujitambulisha wenyewe naye kwa tendo hilo la kuusuluhisha mwili wa nyama. Aliweka mbele yao kwa jitihada ya kwamba ilikuwa alama ya kweli ya majaribio ya kuona mwenyewe akiwa mtesaji na halafu akiwa ni mfuasi, na vilevile ni jinsi gani neema na rehema ya Mungu katika msamaha wa dhambi uliwekwa kati kwa Kristo na kupatikana kwa wote .Yesu alisulubiwa kati yao, kama Paulo alivyohesabia mara ya pili-hata kama walikuwepo na kushuhudia taarifa hasa nje ya mji wa Yerusalemu. Kibali cha Mungu Paulo anapita katika maelezo juu ya Kristo aliyesulubiwa hadi kuona wenyewe kufuatia ujumbe wake uliopokelewa nao. Huku kuona wenyewe ulikuwa ushahidi usio na makosa wa kibali cha Mungu, na ulikuwa ushuhuda katika kweli ya ujumbe wa mtume kwa wafuasi wa kazazi cha kwanza. (1) Tukigeukia katika Matendo ya Mitume, tunakuta kuwa mitume watapokea nguvu za Mungu, akiisha kuwajilia juu yao Roho Mtakatifu {1:8). Siku ya Pentekoste ahadi ilitimilika hapo uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi kukawatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto, Mitume walijazwa "Roho Mtakatifu" na matokeo ya mara moja kuweza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.(2:4). Kwa nguvu iyo hiyo ilimwezesha Petro na Yohana kumponya katika mlango wa Hakalu, na matokeo ya ushahidi kuhusu kazi ya Mungu katika Kristo Yesu (3:1-26).Uwezo huu ulionekana kwa namna nyingine, katika kugundua uongo wa Anania na Safira (5:1-11), katika kuponya wengi (5:15-16), kwa ushuhuda wa nguvu kwa Stefano (6:8). Katika tukio la Filipo katika Samaria linaonekana kwamba kuwa na uweza wa Roho haikuwezekana kupitisha uwezo huu na kuwapa wengine. Filipo aliweza kuponya (8:7); lakini Mitume walipotembelea Samaria ili kuiona kazi aliyokuwa akiitenda Filipo, waliwaombea waongofu wapya ili waweze kupokea Roho Mtakatifu. Ndipo Mitume wakaweka mikono juu yao wakapewa kipawa (8:15-17). Kwa muunganiko huu suala la Kornelio linafurahisha.Aliagizwa katika ndoto kutuma mtu akamwite Petro; naye mtume wakati uleule katika ndoto akiisha arifiwa kutembelewa na watumishi wa Kornelio. Petro akamtembelea Kornelio, akahubiri Injili,na "Roho Mtakatifu akawashukia wote waliosikia neno" (10:44). Kibali cha Mungu kwa alama ya jinsi hii hakikuruhusu shaka yoyote iwapo Kornelio mtu wa Mataifa abatizwe, na hivyo kwa nguvu kufunguliwa njia kwa Mataifa, ikaendelezwa kazi katika uwanja mpana zaidi, ambapo Paulo alitayarishwa katika mambo yaliyokuja tokea katika kuongoka kwake. Kuanzishwa kwa makanisa ya Paulo kulifuatiwa na uthibitisho wa kumwagiwa kipawa cha Roho. Katika mji wa Ikonio "wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu" (13:52). Paulo alianzisha iklezia mahali palipopokelewa kweli, "aliwachagulia wazee katika kila kanisa"(14:23). Ni vizuri kumalizia kwa kusema kwamba kwa kuwachagulia wazee Karama za Roho walipewa. Wazee miongoni mwao walikuwa na karama mbalimbali zilizotajwa moja moja na Paulo katika 1Kor.12 na 14- tunaweza kusoma sura hizo kama kielelezo cha kupewa iklezia za karne ya kwanza, kwa kutumia hizo, kwa kukosekana Agano Jipya, walijengeka kwa ajili ya kazi za huduma tofauti tofauti katika sura zake mbali mbali {tazama barua kwa Waefeso 4:11-13 kwa ajili ya fungu la maneno muhimu katika muunganiko huu uliowekwa wazi). Kwa hivi ulikuwepo ushahidi wa kudumu katika kila Iklezia nia ya Mungu na ushuhuda wa hakika ya kuwa Mungu alikuwa akitenda kazi pamoja nao. Njia ambayo iliwapatia Wagalatia Elimu Kwa mazingira haya tunaweza kufuatilia wazo la Paulo anapowavuta Wagalatia kutazama njia iliyowapatia elimu kipindi kile tangu alipowahubiria Injili. (2) Ujumbe wa Paulo aliwatolea kwa "kwa dalili za Roho na za nguvu" (1Kor.2:4), na "ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika" kwa Wakorintho hata hamkupungukiwa na karama yoyote (1Kor.1:6,7), kwa kuwa "mlitajirika katika yeye, katika maneno yote na maarifa yote". Lililotokea Korintho halikuwa tofauti na njia iliyowapatia elimu iklezia nyingine, na vivyo Wagalatia, kwa hiyo tazama ushuhuda wa ushahidi wa Mungu kwa Paulo na majaribio ya kuona miongoni mwao wenyewe katika karama za Roho zilizowapa ushahidi wake Mungu akitenda kazi pamoja nao. Paulo anawauliza ni kwa misingi gani karama hizi walipatiwa? Je! karama zinafuata kuhubiriwa kwa injili yake, au bidii ya Wayahudi iliwavuta kutii torati? "nataka kujifuza neno hili moja kwenu. Je! mlipokea Roho kwa matendo ya sheria,au kwa kusikia kunakotokana na imani?" Ni imani si matendo ya sheria, ilikuwa sharti lililosifu kibali cha Mungu. Kwa "kusikia" si "matendo ya sheria" kwa "imani" na sio kwa "sheria", je! walijifanya wenyewe wasifiwe na Mungu. Je! mmekuwa wajinga namna hii? aliendea Paulo, "baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?"(3:3). Hatua yao ya mwanzo ilikuwa bayana waziwazi-karama za Roho zilikuwa shahidi -lakini kwa kuigeukia torati walikuwa wakienda katika njia ambayo haikuwa inaenda na ushaidi wa kibali cha Mungu, kwa uhakika walikuwa wakiendelea kutafuta kukamilishwa kwa utaratibu ambao ulikuwa na alama za kushindwa. Kitu kinachotofatisha "Roho" na "mwili" hapa panashindaniwa neema na baraka ya uzima kwa injili, na njia ya amri za mwilini.Maneno yaeleza aina mbili ya chimbuko la maisha yao. Neno-Roho ya Mungu ilizaa ndani yao maisha mapya, ambapo walimwabudu Mungu katika roho na kweli (Yoh.4:23), wakimtumikia sio kwa andiko la Kale bali katika upya wa roho: huu uzima mpya alikuwa "Kristo ndani yao"au kama wazo lilo hilo lilivyoelezewa katika neno linaloanza katika fungu hilo la maneno, "Roho wa Kristo"na "Roho wa Mungu" katikati yao (Rum.8:9,10). Mwili ulikuwa uwanja wa ubinafsi wa kale na furaha yake katika amri kwa nje ya mwili na majivuno yake katika mafanikio yake. Kwa hiyo ilionekana mara nyingi kuwa sheria ilikuwa dhaifu katika mwili kuweza kuihukumu dhambi katika mwili, kama Paulo anavyothibitisha katika Warumi(8:1-14) na ilikuwa lazima Mungu amtume mwanae mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, ili humo (mwilini) aweze kuihukumu dhambi, na kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi kwa njia hiyo iliyotolewa. Kutaka kukamilishwa katika mwili ilikuwa ni kufuata uzuri wa njia ya mwanadamu, bali kutia nguvu maisha mapya kwa kushika moyoni imani ilikuwa njia ya Mungu, kwa wanadamu kumtumainia Mungu kwa utukufu wa neema ya Mungu. Kwa upuuzi wa tendo lao ilikuwa dhahiri kwa taarifa ya suala tupu. (3) Katika maneno kando yaliyo katikati Paulo anatazamisha mambo mengene ya kujaribu kuona-wakati huu ni mateso.Waliteseka katika mambo mengi kwa ajili yao kuambatana na injili. Luka anasema huo upinzani wa Kiyahudi kwao, na shambulio la pamoja watu wengi la Myahudi na mtu wa mataifa. Paulo alikwisha waambia ya kuwa ilikuwa ni kwa mateso mengi yawapasa kuingia katika ufalme wa Mungu (Mdo.14:2,5,22). Kuwa na imani katika injili ilisababisha mateso, dhiki-mateso yalikuwa yanaadilisha, na hivyo kufanya saburi, uthabiti na tumaini (Rum.5:3-4), na kwa sababu hiyo ilikuwa sehemu ya mpango wa Mungu akiwafundisha (Ebra. 12:6). Mambo haya yalihusu njia ya imani; kama walifuata njia ya sheria kutakuwa na maudhi ya Wayahudi, na kwa hiyo mateso yao yaliyopita hayakuhitajika; waliyastahimili bure.Lakini bado Paulo hakubali huo uwe mwisho, anamatumaini ya kuwapata tena kupotea kwao, anaongeza: "ikiwa ni bure kweli". Paulo anafungua wazo lake la kwanza kwa kueleza tena swali lake na halafu kwa kunukuu Andiko. "Basi, yeye (Mungu) awape Roho na kufanya miujiza kati yenu, je! Afanya hayo kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?" Mungu alifanya miujiza kwa mkono wa Paulo, na ujumbe wa Paulo ambao waliupokea na kwa huko kuitikia walipokea karama za roho wao wenyewe, lililkuwa tangazo la neema ya Mungu, ambayo waliisikia na katika hiyo waliweka imani. "Matendo ya sheria" yalikuwa "injili" ya maadui wa Paulo, ambao vilevile walikuwa ni maadui wa msalaba wa Kristo. Madondoo ya Andiko ni taarifa muhimu ya kitabu cha Mwanzo 15:6. Abrahamu alimwamini Mungu ikahesabika kwake kuwa haki. Hii taarifa ya Mungu katika Mwanzo imeandikwa kwa ajili ya vizazi vyote kama maelezo ya kanuni ya Mungu kwa baraka. Kwa nini ahadi alizoahidi Mungu ndiyo msingi wa Mungu katika kusamehe dhambi ambapo mtu anahesabiwa haki mbele za Mungu. Umuhimu mkubwa wa maneno umeonekana katika hoja ya kushindana maneno yaliyo katika Rum.4 mwishoni ambapo Paulo aeleza taarifa iliyo katika Mwanzo 15:6 haikuandikwa kwa ajili ya Abrahamu peke yake bali kwa ajili yetu, kama tutasadiki. Mungu ni mmoja, na sharti la fadhili ni moja, ikiwa mpokeaji ni Abrahamu, mtoto wa Abrahamu au Mmataifa. Taarifa kweli ya Mwenyezi yenye maneno ya mashauri ya kuwa Mungu aligeuza hali ilivyo kutokana na imani ya Abrahamu inakata swali. Ushahidi wa Abrahamu, katika imani yake na kule kuhesabiwa haki, walakini, sio tu kunatatua tukio kati ya "imani" na "matendo", bali kunatoa msingi ambao juu yake Paulo anaeleza vidokezo vya ahadi za Mungu zenye baraka ambazo Mungu alifanya kwa Abrahamu. IMANI NDIYO SHARTI LA BARAKA (3:7-9) Katika aya ya 6 Paulo aligeukia andiko ili kujibu swali ikiwa kwa majaribio ya kuona kwao matendo ya sheria au kwa imani ilikuwa ni ya lazima kabla ya jambo la fadhili ya Mungu kutokea. Ushahidi wa kuona ulionyesha ya kuwa karama za roho ya Mungu ulifuata imani na si matendo ya sheria; na kwamba injili ya neema iliyohubiriwa na Paulo, na sio sheria ya matendo iliyohubiriwa na watu wa tohara, ilipata baraka ya Mungu. (4) Lakini kwa majaribio ya kuona hata kwa karama za roho, ndani yake zenyewe haukuwa ushuhuda wa kutosha. Katika barua ya kwanza kwa Wakorintho Paulo anataja ujuzi wa kunena katika ibada ya kipagani, anaomba kwa nguvu ya kuwa maneno yote ya jinsi hii yaletwe katika kipimo cha kweli iliyofunuliwa (1Kor. 12:1-3). Katika barua hii Paulo anaona katika maandiko ushahidi wa kwmba kuhesabiwa haki ilikuwa ni kwa imani na huku kutiwa sahihi kwenye amri kuliongeza ushahidi wa kweli yake ambayo Wagalatia walikuwa katika kumiliki karama za roho. Aya iliyonukuliwa (Mwanzo 15:6) ilikuwa bora; ilijadiliwa katika shule ya Kiyahudi, nayo ilijulikana sana na wote ambao walilijua Agano la kale. Kwa suala la Abrahamu kukubalika na wote, lilikuwa kipimo; yeye alikuwa kichwa cha taifa, na aliitwa rafiki wa Mungu. Kuchaguliwa kwa taifa kulikuwa ni kwa sababu ya msimamo wa haki ya Abrahamu mbele za Mungu. Mara tatu katika maandishi yake Paulo anafanya kutaja Mwanzo15:6; mara mbili katika Warumi (4:3,22); na hapa kwa Wagalatia. Katika upendo wa Paulo hili fungu la maneno ni la kuthibitisha: Abrahamu akamwamini Mungu - ilikuwa imani ambayo kwake ilihesabiwa haki. Ushahidi wa (Mwanzo 15:6) kuhusu kuvutiwa Mungu katika imani ya Abrahamu, hayawezi kuwa ni maneno yanayotoa maelezo ya kumshuhudia Abrahamu pekee. Mungu anashughulika na watu kwa mambo ya kutumiwa na watu wote. Paulo mwamini mweye juhudi katika umoja wa Mungu aliona kwamba alikuwepo Mungu MMOJA tu, basi inabidi kuwa ni Mungu wa wote wawili Wayahudi na Mataifa, tena, hanabudi ana kanuni moja ya kuhesabia haki kwa kuwa watu wote wanashiriki mahitaji ya kawaida (taz. Rum.3:26-31). Lakini umoja wa Mungu ulihusisha mambo mengine vilivile: kuna kanuni moja inayokubalika, na tokeo moja la neema yenye baraka ile ile kwa watu wote mahali ambapo masharti yamefuatwa. Wazo la umoja wa Mungu linakwenda mbali zaidi: katika toleo la mwisho katika ukombozi wa Mungu wote hawana budi kuwa mmoja na Mungu, wote wakishiriki ummoja wa Mungu. Hili wazo lililo juu linakuja toka katika mistari inayofuata ya mlango wa tatu. Uzao wa Kweli wa Abrahamu Fahamuni basi, anasema Paulo akitazama toka matokeo ya utaratibu wa Mungu kwa Abrahamu, utaratibu ulioandikwa katika Mwanzo 15:6, "ya kuwa wake walio kwa imani, hao ndio wana wa Abrahamu". "Tunaye baba, ndiye Abrahamu", yalikuwa majivuno ya Wayahudi ambayo Yohana Mbatizaji aliyasukumia kando kwa jibu kali la kuwa Mungu aweza kumwinulia mawe kuwa watoto Abrahamu (Mathayo 3:9); mzao wa kimwili tupu haukutoa heshima kwa jina la tajiri la Abrahamu, maana ingekuwa hivyo, Waishimaili na Waedomi wangeweza wote wawili kudai. Kama zilikuwepo sababu za kukataa kwao - na huyu asiye Myahudi atakana - inakuwepo hali iliyosawa ya sababu za kukataliwa watoto wa Sara. Imani ilikuwa na umuhimu wote kwa Abrahamu; Haziwezi kuwako fadhili kwa Mungu hapo imani inapokosekana. Ni imani pekee wakati ule kwa upande wa watu wengine iliweka uhusiano na Abrahamu ukweli ambao uliwazuia Wayahudi wengi, ila ambao pia uliwaingiza watu wengi wa mataifa. (5) Paulo anaeleza ya kuwa "walio wa imani" ni "wana" wa Abrahamu, "hao ndio wana wa Abrahamu" kukosekana kwa mlango mmoja katika mapatano ya maneno kunatupa mkazo wote juu ya hali ya kuwa wana. Lakini kama hali ya kuwa wana msingi wake ni juu ya imani na inajitegemea kwa uhusiano wa kimwili, kwa kuwa (1) jamaa ya Abrahamu kwa kusudi la mwisho wa Mungu hauna budi kuwa roho na sio utaifa, na (2) kwa kuwa wengi walio wa "imani" ambao si watoto wa Abrahamu, hali yao ya kuwa "wana" katika suala lao halinabudi kuwa ni kuchaguliwa kuingia kuwa jamaa yake. Urithi unafuata katika hali ya kuwa wana. "Kama tu watoto, basi, tu warithi"(Rum.8:17), yaeleza mawili kama matokeo. Muunganiko wao usioepukika katika nia ya Paulo utatuongoza kutarajia ukweli wa kuwa na sehemu katika sababu za maneno ya kusadikisha. Basi hali hiyo ina "Uzao wa Abrahamu, na warithi" (Gal 3:29) inatia pamoja katika fungu moja la maneno mambo mawili. Jambo ambalo linadokezwa la "kuchaguliwa" katika kweli ya hali ya kuwa wana kwa hao wasio wana wa asilia, na wazo zaidi la urithi ambalo linachipuka toka wana, katika mlango huu linafuata baadaye. Lakini Paulo hana budi kwanza kuonyesha ya kuwa jamaa ya Abrahamu ina katika msingi wake imani iliyounganika, na si wa mwili. Anafanya hivi kwa kugeukia tena katika maneno ya Mungu kwa Abrahamu yalioandikwa katika Maandiko, "Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Abrahamu habari njema zamani, kusema, katika wewe Mataifa yote watabarikiwa".(3:8) Mtindo wa kutazama hivi Andiko unafundisha. Mtume na wasomaji wake wote waliangalia Maandiko kama ni yenye amri ya ufunuo wa Mungu. Maneno ya kusadikisha yapo juu ya maneno ya Andiko; katika aya inayofuata juu ya neno moja. Kwa mfano Paulo anahesabia maandishi ubora wa maarifa ambayo yanamhusu Mungu, ambayo yaweza kufanywa tu kama maandishi haya yakiwa yamebuniwa na Mungu. Maarifa ya kujua jambo kabla ndiyo kiini kabisa cha Injili: kwa maana Injili yahusu wakati ujao, ikiwa ni "habari njema" ya kusudi la Mungu litakalotimika. Mwenendo wa siku hizi unaovunja heshima ya kutabiri kama kazi ya nabii, utanyima yote yaliyo na Injili. Wokovu upo juu ya ahadi za Mungu zinazohusika na wakati ujao, na kwa sababu hiyo ni wa asili ya unabii. "Katika wewe jamaa (Mataifa) yote watawabariki" ilikuwa ahadi ya Mungu kwa Abrahamu kabla hajaondoka katika nchi yake ya Uru ili kwenda kwenye nchi ya ahadi (Mwanzo 12:3). Kusudi hili lilirudiwa kama sababu ya mazungumzo ya Mungu kuhusu kuangushwa kwa Sodoma. "Je! nimfiche Abrahamu jambo nilifanyalo; akiwa Abrahamu atakuwa Taifa kuu, hodari na katika yeye Mataifa yote ya dunia watabarikiwa?" (Mwa 18:17,18). Ni ahadi gani hapa iliyoaidiwa? Labda ya kwanza tunafikiria ya kuwa Baraka ya vitu tele katika Utawala wa Kristo, kipindi cha amani, kuwekwa haki, kuwepo chakula tele; nyumba kwa wote; usalama kwa kufuata sheria; kuondolewa usultani umwagaji wa damu, ukandamizwaji na mateso ya namna zote, kuleta hali ya kuelimishwa, na kupenda mambo ambayo ni mazuri wakati wote. (6) Ni kweli kwamba mambo haya yamekuwamo, kama picha zinakuwa nyeupe katika manabii walivyoeleza mambo ya habari za kipindi kinachokuja walivyoonyesha kwa wingi: lakini hayo si ya kwanza na yaliyo muhimu zaidi katika baraka. Paulo ananukuu maneno: "Katika wewe mataifa yote yatabarikiwa" kama ushahidi wa kuwa Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani. "Mataifa yote" wamekuwamo mataifa sawa sawa na Wayahudi- kwa udhahiri, kwa hiyo mbaraka kwa Abrahamu ni kwa ajili ya Mataifa. Uthibitisho wa kuwa Mungu atawahesabia haki umelala katika neno "kubarikiwa" - kwa maneno mengine, Mungu aliposema mataifa watabarikiwa ni ahadi kuhusu kuhesabiwa haki kwa mataifa. Kuhesabiwa Haki Kuhesabiwa haki ni nini? Jawabu limetolewa vema katika kitabu kidogo kisicho na jalada kiitwacho Kulipiwa: "Neno hili lina maana mbili ambazo zinapambanuliwa waziwazi: 1. tetea, dhihirisha kuwa na haki; na 2. Ondoleo la dhambi, kutokuwa na hatia, msamaha, upatanisho. "Katika maana ya kwanza ni Bwana wetu pekee aliyehesabiwa haki". Roho ya Kristo kwa Isaya inasema 'Bwana MUNGU atanisaidia' kwa sababu hiyo sikutahayari; kwa sababu hiyo nimeukaza uso wangu kama gumegume, na najuwa ya kuwa sitaona haya. Yeye anipatiaye haki yake yu karibu; ni nani atakeyeshindana nami? ( Isaya 50 7,8). Baadaye Yesu mwenyewe alisema hivi kwa Wayahudi: 'Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye ya kuwa nina dhambi?' (Yohana 8:46). Na ingawa kwa lile lilotokea walimwona kuwa na 'dhambi' (Yn. 9:24), pamoja na Warumi kumuua kwa jinsi hii, Mungu alimfufua katika wafu asife tena na hivyo 'alihesabiwa haki' katika maana ya kumtetea; kwa uwazi akathibitisha mbele ya watu wote kuwa ni 'Mwana wa Mungu wa pekee' ambaye Baba alipendezwa naye sana (Rum 1:4) "Katika maana ya pili ya "kuhesabiwa haki" watoto wa Mungu wa kuchaguliwa, wa kiume na kike wanaonekana mbele zake kutokuwa na lawama, hawana hatia, wamesamehewa, wamepatanishwa na nafsi yake katika neema yake kwa imani na toba, na (baada ya kubatizwa katika Kristo) kwa dhabihu ya Kristo, kubatizwa katika jina la Yesu Kristo, na kwa matendo mema tokea awali Mungu aliyatengeza ili tuenende nayo (Efe 2:10). Roho ya Kristo kwa Isaya vivyo hivyo ilinena msemo huu, 'kwa maarifa yake mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki; maana atayachukua maovu yao' (Isaya 53:11). Kuhesabiwa haki na Mungu ni kutamkwa kuwa mnyoofu Kwake, na kwa kila mwana wa Adamu isipokuwa Bwana Yesu, huu unahusisha msamaha wa dhambi. Hali ya kuwa sambasamba katika Isaya 53:11 umewekwa hivi: "Kwa maarifa yake mtumishi mwenye haki atawafanywa wengi kuwa wenye haki; naye atachukua maovu yao (7) Hali iliyosawa sawa inapatikana katika maandishi ya Paulo: Kufa na kufufuka kwa Yesu ni habari inayounganika barabara, "alitolewa kwa ajili ya makosa yetu" na "alifufuliwa kwa ajili ya kuhesabiwa haki kwetu" imeunganika sawa sawa - Kristo alikufa kwa ajili ya makosa yetu ili kwamba tuweze kusamehewa dhambi zetu, au tuweze kuhesabiwa haki. Vile vile kwa ajili yetu, kwake ambaye (haki) atahesabiwa, kama tukimwamini yeye ndiye aliye mfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki(Rum. 4:24,25). Hali ilivyo kwa upande wetu - ni imani- imeelezewa kwa maneno machache "kama tukimwamini", na tena katika aya inayofuata kwa jina "imani". "Basi tukisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, tunayo amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo" (Rum 5:1). Juu ya hayo neno hili hili lenye maana na nyingine katika Lugha moja linapatikana katika maneno yaliyo katika kitabu cha Mwanzo 15:6, "naye akamhesabia jambo hili (imani) kuwa haki", jambo amblo ndilo limejadiliwa katika sura ya nne kwa Warumi hadi mwishoni anaposema Paulo kama yalivyonukuliwa hapo juu, ya kuwa mashauri yaliyo katika Kitabu cha Mwanzo hayakuandikwa kwa ajili ya Abrahamu pekee ila vile vile na kwa ajili yetu tunaoamini. Maana hii muhimu ya neno "kubarikiwa" kuwa sawa sawa na kuhesabiwa haki halina mpaka katika matumizi yake kwa ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu. "Lakini kwa mtu asiyefanya kazi, bali anamwamini yeye amhesabiaye haki asiyekuwa mtauwa, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki. Kama vile Daudi aunenavyo uheri (baraka) kwake mtu yule ambaye Mungu amemhesabia kuwa na haki pasipo matendo. Heri waliosamehewa makosa yao, Heri mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi" (Rum 4:5-8). "Uheri" (baraka) iliyotumiwa na Daudi ni ya muungano wa maneno tu na ahadi zilizofanywa kwa Abrahamu za "kubarikiwa" na katika tafsiri ya Paulo na maana inayofuatana na neno katika hizo ahadi zinazopatikana katika mashauri ya Daudi mwenyewe ya Daudi mwenyewe yenye nguvu juu ya makosa yaliyosemwa na kusitiriwa dhambi. Uheri wa Ahadi Tunaweza kuona bila shida ya kuwa tafsiri ya jinsi hii inahusu tu katika mafundisho ya maneno ya Paulo yaliyo karibu, lakini kwa kufikiria hivyo tutatoa dalili ya kuonyesha kushindwa kwetu kufahamu ujumbe wa mitume wengine. Petro alimtangulia Paulo katika kudokeza cha ahadi zenye Uheri. Kwa Wayahudi wa Yerusalemu, waliokusanyika katika moja wapo ya nyua za Hekalu, Petro alimalizia hotuba juu ya kazi ya Mungu kwa Kristo na maneno: "Ninyi ni watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zetu, akimwambia Abrahamu, katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa. Mungu akisha kumfufua mtumishi wale Yesu, alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumuepusha kila mmoja wenu na maovu yake". (Mdo 3:25,26). Kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa, bali Mungu alikuwa anapeleka baraka kwa Wayahudi kwanza na kuwapa uheri katika Mtu ambaye Mungu alimfufua kwanza katika ukoo wa Abrahamu, na akiisha kufufuliwa, "akimwepusha kila mmoja wenu na maovu yake". (8) Katika kupima fungu hili la maneno ya Petro - "kumwepusha katika maovu"- tunaona kabla ya yote namna linavyo hitilafiana kati yake na neno la Paulo "kuhesabiwa haki" ambalo Paulo analinganisha na maovu yaliyosamehewa na dhambi kusitiriwa, je! ipo tofauti kwa mtazamo? La pili tunaona ya kuwa Petro ananukuu katika Isaya. Katika Matendo Ya Mitume 3:13,26; 4:27,30 tunaona neno "mtumishi" limefasiriwa mahali pa "mwana" katika Biblia zetu U.V. Pasipo shaka hili ni sahihi - mara moja hili neno linatuleta katika unabii wa Isaya, hasa mlango wa 53. Katika hali ya kuwa maneno sawa na Isaya 53:11, neno ambalo tayari limenukuliwa, tunaweza kuongeza hayo ya aya ya 12: "Kwa sababu alimwaga nafsi yake hata kufa, akahesabiwa pamoja na hao wakosao: walakini alichukua dhambi za watu wengi, na kuwaombea wakosaji" Petro aliwataka "Watubu na kurejea, ili dhambi zenu zifutwe" (aya ya 19). Kugeuka toka katika maovu ni kuyaondoa ya kwanza kama jambo fulani lilosamehewa, na halafu kuyaacha kama mwendo wa maisha. Hasa kwa wasikilizaji wa Petro ilimaanisha kutomwangalia tena Yesu ya kuwa ni mtu ayari ambaye kusulubiwa kwake kulikuwa kumwacha tu kwa mtukanaji, ila kumtambua tu kuwa ni mtumishi wa Mungu ambaye kwa kumwaga nafsi yake na kisha kufufuliwa akawekwa kuwa ni masihi wao. Ilimaanisha kubadilika moyo na akili, na kukiri ya kuwa, ingawa wamefanya kwa kutokujua, bado walikuwa wamemuua Mkuu wa uzima. Na kuungama kwa upande wao, na kwa kuwaombea mtumishi, ingawa wakosaji kwa maovu yao watasamehewa na Mungu. Wazo la Petro limetengezwa kwa lugha ya kinabii kwa Isaya, ila Petro anaweka mkazo juu ya tukio kwa wasikilizaji wake kuhusiana na matendo ya Mungu katika Kristo. Maana ya tatu inayoshughulika na Isaya 53 iangaliwe. Petro alimponya mlemavu, aliyeingia hekaluni "akienda na kuruka-ruka, na kumsifu Mungu". Petro katika kufanya muujiza wa jinsi hii alikana kuwa ni uwezo wake. Yule mtu, "akatiwa nguvu" na akapewa uzima mkamilifu" kwa kuliamini jina la Yesu. Yesu, ambaye walimsulubisha akawa yu hai; naye alikuwa na uwezo mno wa kuponya. Ndivyo Isaya alitabiri: "Kwa kupigwa kwake sisi tumeponywa" (53:5); na Petro kwa kuonekana wakati uo huo katika hotuba yake anaacha huko kutumia, ili wasikilizaji wake wavutwe wenyewe, au ilizuiwa katika kuihutubia yeye mwenyewe kwa kukatiza kulikofunga hotuba (Mdo 4:1), katika waraka wake wa kwanza anamnena Kristo ya kuwa katika "mwili wake alizichukua dhambi zetu juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki, na kwa kupigwa kwake tumeponywa". "Kugeuka katika maovu", basi, ni kuwatambua wameonyesha uelekeo mwingine, kama jambo fulani ambalo mtu amekufa. Petro anakamilisha wazo "Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na mwangalizi wa roho zenu" (1 Petro 2:24,25). Na "kugeuka katika maovu" ni "kumgeukia" Mungu. Basi wote wawili Petro na Paulo wanaeleza agano lenye baraka na Abrahamu kuwa ni msamaha wa dhambi na ushirika na Mungu, Petro alisema na Paulo, "Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu (aliyekuwa amejaa imani) mwenye imani" (Gal 3:9). (9) MATENDO YA SHERIA YANALETA LAANA (3:10-12) Ikiwa imani, kama Paulo alivyonena ni sharti la kubarikiwa, kutumikia Sheria kulikuwa na nini? Mungu aliwapa sheria Israeli, Torati ilitumika na kitu gani? Matokeo ya juhudi ya watu yalikuwa na nini kwa kuitunza, na kwa uzima Torati ilikuwa na uhusiano gani? Haya na maswali mengine kwa kawaida yatazuka mioyoni mwao hao waliokuwa mawakili wa kuitunza Torati na hao ambao kwa ushawishi wao walikuwa katika shaka ikiwa Torati waitunze. Maswali haya yameshughulikiwa na Mtume kama hoja yake inayoendelea. Mataifa yanabarikiwa, Paulo ameweka, juu ya hali ya mambo ya imani; na sasa anaonyesha ya kuwa mpaka hapo katika Torati ndio njia ya kubarikiwa, taifa ambalo lilikuwa chini ya Torati na kujivunia katika hiyo waliojikuta wao wenyewe wapo chini ya laana. Hivi ilikuwa ni kupindua meza kwa Wayahudi. Walikuwa wanaidharau njia ya kubarikiwa na kuitetea njia ambayo ilileta laana. Kwa ujasiri Paulo amesema "Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana: maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye" (aya ya 10). B.H.N "yote yanayotakiwa na sheria" yanafanya mashauri ya mtume yazunguke sheria yoyote: ya Musa ilikuwa, bila shaka katika mtazamo, lakini ile iliyokuwa kweli kwa Musa ilikuwa kweli kwa sheria yoyote, na kwa hiyo Paulo ameeleza suala lake kwa upana. Kama anaweka neno la awali basi sheria yoyote inahusika: isitoshe lililo la muhimu ni kwamba atafikia kwenye katazo la msingi katika sheria kama sharti la kupata fadhili za Mungu na kupewa uzima. Watu wanapotafuta wokovu kwa matendo wanashughulika na nia ya kuweza kufaulu wakitafuta kujitosheleza kwa Mungu. Katika hali hii kujihesabia haki mwenyewe kunafanana na kosa la Adamu ambalo linachipuka katika haja ya kuwa kama Mungu, lilikuza mapenzi ya adamu mwenyewe na kutojali mapenzi ya Mungu. Mwanadamu kujihesabia haki, na kutukuza ubinafsi, kunadumisha kosa la Adamu. Mwanadamu aliyeanguka kwa kujishusha anafahamu neema ya Mungu; lakini badala ya kutembea kwa unyenyekevu, katika kutaka haki kwa juhudi yake mwenyewe anadhihirisha kiburi na majivuno. Juhudi yake inaanza na kuishia na kiburi; akiishapofuka na ubinafsi mwanadamu mwenye heshima kwa kuongezeka anakuwa ametosheka na juhudi yake mwenyewe, hafahamu kidogo upumbavu wake. Matokeo makubwa katika jambo hili kati ya Yesu na Mafarisayo yanaweza kupatikana hapa. "Akitaka kujihesabia haki mwenyewe" kunadhihirisha msingi kabisa wa juhudi za binadamu. "Mimi nafunga, mimi natoa zaka" - nafanya na ziada shughuli ziingine juu ya mwanadamu kwa kuweka kazi yake katikati haya yameelezwa kwa maneno machache na Yesu katika mfano wa Farisayo na Mtoza ushuru. Matendo ni kama matawi ya mti ambayo hayatoi matunda. "Ufanye mti kuwa mwema" ndiyo kanuni ya Mungu. Sheria ya matendo inamtenga mwanadamu. (10) Bila kuepukika anajilinganisha mwenyewe na wengine na kutaka kuzidi. Lakini Matendo ni mambo ya nje yanayojionyesha na kwa hiyo ni ya kutumika na mwili: na hukumu yote imekazwa katika tendo na si wazo - ni hukumu kwa tendo la kuonekana. Kwa hivi mtu wa jinsi hii anajiona mwenyewe yupo kando na ndungu zake; mafanikio yake yanamtofautisha nao. Kwa namna nyingine kabisa, njia ya Mungu inawaleta watu wote wajione kuwa hawafai. Ubora wa kazi ya binadamu imeonekana kuwa na waa fulani la dhambi. Popote Mungu amechagua watu kwa ajili ya kazi fulani kubwa na akawandaa kwa shughuli hiyo kwa maono (ndoto) ya Utakatifu wake, kutokufaa kwao kabisa kwa matumizi ya Mungu kumefahamika: "Mimi ni mtu mwenye midomo michafu", alisema Isaya aliposikia vifijo vitatu vya utakatifu wa Mungu. Hii haikuwa sababu eti alikuwa sehemu ya chini au mwovu; bali alikuwa "mtu mtakatifu wa Mungu" alichaguliwa kuwa njia ambayo kwayo habari iweze kupita yenye kuonekana dhahiri zaidi ya mafunuo ya Masihi. Na sio tu alitambua uchafu wa midomo yake mwenyewe, ila aliona vile vile ya kuwa taifa lake, watu wake vivyo hivyo walikuwa wachafu: "Nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu". Mtu anayeifahamu dhambi anajua umoja wake na ndugu zake kama washiriki wa ukoo mzima uliotekwa na dhambi. Hakuna mahali pa mapatano ya ukoo unaonekana wazi zaidi kuliko katika watu wote kuwa ni wenye dhambi. Nabii alichoona mbele za Mungu Petro alipata alipoona kuwa nguvu za Mungu zilikuwa juu ya Yesu: "Ondoka kwangu, Ee Bwana kwa kuwa mimi ni mwenye dhambi". Hali ya kujua haufai inatokana na kusadikishwa kweli ya Mungu, ila watu ambao wanashika matambara ya kiburi na ya kujihesabia haki huzuia kuitii kweli ambayo inahusisha kusalimu amri katika mapenzi ya Mungu. Kwa hiyo kusudi la Mungu linazuia matendo kuwa ndiyo msingi wa kukubalika: kwa maneno ya Paulo, si "kwa matendo, mtu awaye yote asijivunie" au tena, "Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje: kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani" (Rum 3:27). Katika barua kwa Wagalatia Paulo anaacha kando hoja hizi zenye sababu kwa nini wokovu si kwa sheria na kwenda moja kwa moja katika matokeo ya sheria. Sheria inaleta laana: na pasipo kutengwa au kubadili inawalaani wote walio chini yake, maana laana haipangi cheo kulingana na kulingana na upana wa uasi. "Kudumu katika yote yaliyoandikwa" ndiyo njia pekee ya kuepuka laana. Yakobo kwa kueleza anaeleza hili jambo: "Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa katika yote" (Yakobo 2:10). "Laana" imeandikwa katika Kum 27:26. Inahusisha kutengwa na Mungu, kama ilivyo dhahiri Yesu alivyotumia neno kwa watakao kataliwa: "Ondokeni kwangu, mliolaaniwa" (Math 25:41). Kwa nyongeza ya kupinga ushahidi wa kuwa sheria haikutoa wokovu tangu wote walio chini yake walikuwa chini ya laana yake, Paulo anaweka mbele mfano wa ushahidi halisi wa kwamba ipo njia nyingine iliyotolewa ambayo ni mpya ya kufaa iliyotofauti na sheria- njia ya Imani. (11) "Ni dhahiri ya kwamba hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria; kwa sababu, Mwenye haki ataishi kwa imani" (aya ya 11). Kama Mungu ameeleza hivyo, ni uthibitisho wa nguvu kwamba njia ya Mungu ya uzima si kwa sheria. Aya iliyonukuliwa inapatikana katika Habakuki2, imetumiwa na Paulo mara tatu (Rum.1:17, Gal.3:11,Ebr.10:38). Kuweza kuwekwa kwake sana kunaweza kuonekana kwa kukaza katika kugeuza mambo matatu yaelezayo mambo yenyewe."Wenye haki"ni hao wathaminiwao hivyo na Mungu kwa sababu wamehesabiwa haki kwa neema yake.Wao "wanaishi"kwa imani, wakati sheria hufanya mauti.Ni mauti ndio mchango wa wenye kuhesabiwa haki-na imani hii kwa kutumaini kwake katika Mungu kuweka nje ubinafisi kuwa ndiyo msingi wa kadiri ya kutosha. Sheria na imani vipo mbalimbali.Kwa nguvu mambo ni sheria na neema- matendo na imani: ila Paulo anapata mkazo mkubwa zaidi kwa kusema kwamba "sheria (torati)haikuja kwa imani".Torati haihusu katika aina moja kama imani. Kwa maana Torati inahusika na kutenda, wakati imani inaeleza kuamini. Shida imepatikana namna Paulo alivyotaja; "Mtu atendaye hayo ataishi katika hayo". Kama inavyooneka husimama ikifundisha ya kwamba torati liahidi uzima kwa kuitii.Inawezekana kuweka orodha ya mafungu mawili ya maneno, orodha moja inayoonekana kusaidia wazo la kwamba torati iliahidi uzima kwa kuitii,na orodha nyingine ipo kinyume wazi na dhahiri.Walakini, maandiko, yenyewe hayapingani, na ni wazi kwamba kwa kuonekana kuhitilafiana inabidi kuzuke katika mtazamo ulioweka mpaka pia wa kueleza fungu moja la maneno(Tazama ufafanuzi wa barua ya Warumi, katika ml.10). KRISTO NA LAANA YA TORATI (3:13-14) Kwa sababu hakuna aliyeitunza kwa ukamilifu, Torati iliwalaani wote waliokuwa chini yake. Kwa hiyo katika upana wake mkubwa wa kuwapo, kama Wayahudi wengi walivyofikiria kuwa ni njia ambayo watu wanaweza kupata uzima,ilikutwa kuwa inatoa kizuizi chenye matokeo yaliyo kusudiwa kwa uzima-kwa hakika kama jambo lingine la laana yake huwatenga watu na uzima. Kwa hivi Torati iliweka wazi jinsi mtu asivyofaa na kwa sababu hii inahitajika tendo la Mungu ili watu waokolewe.Tayari Paulo ametaja tendo la Mungu katika Mwana wa Mungu"aliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu (1:4)," aliyejitoa nafsi yake kwa ajili yangu" akiisha kusulubiwa (2:20). (12) Maana shindano la maneno ya Paulo lilikuwa kamili, kuhusu Torati kukosa kutoa matokeo mazuri kama ndiyo njia ya kupata uzima haimpasi kuonyesha tu ya kuwa kazi ya Kristo ilikutana na mahitaji ya watu walio na mwenendo wa kukosa na kwa umbo ni wenye kukabiliwa na mauti, ila inambidi pia kuonyesha ya kwamba Kristo ameiondoa laana ya torati-torati ambayo sio tu haitoi uzima, bali ambayo inawahukumu watu kifo.Kwa kweli, ikiwa Kristo ni Mkombozi, inampasa kwa ulazima kuwakomboa hao walio chini ya laana ya torati watoke katika laana hiyo. Ni mbalimbali kabisa "Torati ililaani-Kristo alikomboa toka katika laana"Ni uthibitisho wa mwisho kabisa wa kuwa madai ya Wayahudi si ya kweli. Ni Kristo aliyefanya hivi : kwa kweli Kristo ni Yesu- lakini kwa kusema Kristo alifanya hivyo, Paulo anaeleza kuwa ni Masihi aliyeondoa laana. Atasema katika ishara inayofuata laana iliondolewa kwa kusulubiwa kwake- kwa kifo kile kabisa ambacho kilivunja heshima sana machoni pa Wayahudi. Na badala ya msalaba kuonyesha kama Myahudi alivyodhani, ya kwamba madai ya Yesu kuwa ni Masihi yalikuwa yanakufuru, msalaba ulithibitisha kuwa Yesu alikuwa Masihi. Paulo hapa anatetea mafundisho yake juu ya nafasi ya Kiyahudi akibisha kwa mbele, akithibitisha kuwa alihitajika Mfalme wa Israel aliyekuzwa na kutukuzwa ya kuwa atateseka na kufa kwa ajili ya makosa ya watu kama sharti na heshima na utukufu - "Si kutaka kujua lolote" asema Paulo, "ila Masihi Yesu aliyesulubiwa". Shindano hili la kwamba unabii wa Agano la kale ulitaka ya kwamba Masihi hana budi kujitoa nafsi yake kuwa dhabihu kwa dhambi, kiligeuzwa kipingamizi cha Wayahudi katika kuthibitisha ushahidi wa mapenzi yote kwa kupima ushahidi. Mitume hawakuwa wagumu kuutumia, kwa maelezo mengi Petro katika Mdo.2 na Paulo katika Waebrania 2:9,10, ni mifano inayoonekana kwa urahisi: lakini hapa wazo ni la bila kuuliza anaposema Paulo ya kwamba Kristo- Masihi- ametukomboa na laana ya Torati. LAANA ILIONDOLEWA Ni jinsi gani laana ya Torati "ilizuiwa kutenda kazi juu ya mtu?"-kwa maana hiyo ya neno lilotafsiriwa kukombolewa katika sehemu hii hasa, ndiyo maana yake. Paulo anajibu: kwa njia ya masihi "aliyefanywa laana kwa ajili yetu", kwa ajili yetu siyo badala yetu, ila kwa ajili yetu kwa kuwa amekuja chini ya Torati ili aweze kuiondoa katika nafsi yake mwenyewe na kwa ajili yetu, kwa ajili yetu, kwa kuwa sisi, na kujishirikisha wenyewe naye katika imani kwa utii wake hadi kushiriki laana naye katika matokeo, kwa tendo la kuondoa laana toka kwetu. Ni wazi kwamba Paulo anaposema Kristo ametukomboa katika laana ya Torati, anamaanisha ni hao waliokuwa chini ya Torati, "yetu" Wayahudi. Lakini jambo kuu ambalo laana hii ya torati imeliondoa ni hali moja na laana ya dhambi na mauti ambayo imeondolewa. Katika suala la pili jambo linapoeleweka, kwa namna ambayo laana ya Torati iliondolewa si vigumu kufahamu. Moja lilipimwa kama lilivyoonyeshwa katika 2:20 ambako shauri linaweza kufanywa. (13) Kwa uhodari jambo hili limewekwa katika vijitabu vidogo viitwavyo Damu ya Kristo na Mwana Kondoo. Hebu sasa tufuate wazo la Paulo kuhusu ni jinsi gani Kristo ameondoa laana ya torati. Kristo "alifanywa laana"; kila mahali anasema ya kwamba"alifanywa chini ya torati" na wakati kuna muunganiko wa karibu kati ya taarifa mbili, ipo maana iliyo kubwa zaidi katika fungu la maneno "alifanywa laana". Kama tukiiweka taarifa katika muundo imara badala ya kuwamo katika mawazo - ambayo yalipelekea Paulo kuyatumia kwa sababu aliyanena tu ya laana ya torati kwa uhusiano na wengine basi yaelezwa ya kuwa Yesu alilaaniwa! Kwa kweli taarifa hii inakuwa ni ya kushitusha, ila hatujabadili maana ya Paulo na mara moja kwa kulingana inadokeza yenyewe - alilaaniwa kwa ajili yetu na "alifanywa dhambi kwa ajili yetu" (2 Kor 5:21). Isitoshe, yakiwa hayawezekani kwa elimu ya matumizi ya maneno, yatupasa kuyatupia mbali kuwa hayafai kwa mwangaza huu uliolingana na kudokezwa "dhambi" Paulo katika sehemu hii anamaanisha "dhabihu ya dhambi". La. Paulo anakususia dhambi, ila hatuna budi kufahamu kwa hilo neno lilikusudiwa jambo gani. Kristo alifanywa dhambi kwa kuwa alishiriki mwili ambao ndani yake dhambi hutawala na ambao huzaa dhambi, na ambao kwa hiyo kutokana na hali yake umeitwa dhambi. Tunaweza kwenda zaidi na kusema kwamba alifanywa "dhambi" katika kustahimili matokeo ya dhambi - dhambi isiyo yake mwenyewe, maana hakutenda dhambi - bali dhambi ambayo imeacha matokeo yake juu ya ukoo mzima wa binadamu kwa kuwaletea wote kuwa chini ya mauti. Kama tukitambua ni jinsi gani dhambi ni ya kuchukiza machoni pa Mungu, ndipo tunaona ni kiasi gani matokeo yake yameletwa mahali pamoja kama ilivyokuwa kwa Mwanawe mtiifu. "Yeye asiyejua dhambi alifanywa kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye." Alifanywa kuwa - tunavyo kuwa; tofauti ikawa kwamba aliguswa na kustahimili katika utu wake mwenyewe matokeo ya dhambi, aliyapokea bila kulazimishwa matokeo hayo, lakini sisi tunasamehewa dhambi zetu na hivyo kuwa haki ya Mungu. Alifanywa "dhambi" bila kuwa mkosaji; vile vile "alifanywa laana" pasipo kuvunja Torati. Hali hii ilikuja vipi Paulo anaeleza. Alilaaniwa kwa namna ya mauti na hii haikuhusisha wajibu wake kwa upande wake. Amri ya Torati ilieleza: "Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti." Kristo alipigiliwa misumari katika mti na hivyo akawa chini ya laana. "Mti" Hebu basi tuone na kuangalia ya kuwa si sehemu hii pekee ambayo mkazo umewekwa kuhusu "mti" kwa kuunganika na Kristo. Ushahidi wote unaomtaja Bwana mwenyewe kukaribia kusulubiwa unatilia maana iliyoongezwa katika mwangaza wake. Shauri linarudia katika wazo la utume. Petro aliambiwa hivi mamlaka ya Kiyahudi kwamba Mungu "alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimua mkimtundika katika mti" (Mdo 5:30); alitumia fungu lilo hilo la maneno machache kwa wa Kornelio (10:39). (14) Kwa Wayahudi wa Pisidia Antiotikia Paulo alieleza ya kuwa "walipokwisha kumaliza yote aliyoandikiwa, wakamtelemsha katika ule mti, wakamweka kaburini" (13:29). Katika maneno yaliyo muhimu sana katika Waraka wake Petro wa kwanza anasema ya kuwa Yesu "alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti". Toka mashauri haya ni dhahiri kwamba jinsi Kristo alivyokufa yaliingizwa na kuonekana upesi katika fikira za waalimu wa kwanza wa Kikirsto walipokuwa wanaeleza kweli kwa Wayahudi au hao wa Kiyahudi walioonana nao. Kisha tunageuka ili tuone maneno katika Torati aliyonukuu Paulo. Fungu la maneno alilonukuu linaonekana limeingizwa katika maelezo ya ziada katika amri ya kuwa ikiwa mtu ametenda dhambi - kosa linalostahili kuuawa, auawe na kutundikwa katika mti, halafu mwili wake haupaswi kusalia juu ya mti hadi jua kuzama, ili nchi isitiwe unajisi. Sababu iliyotolewa ni kwamba "aliyeangaika katika mti amelaaniwa na Mungu". Jitihada nyingine ilifanywa kwa kuwekea mpaka laana ya Torati ya adhabu ya kifo iliyowekwa kwa ajili ya kosa, katika sababu ya kuwa inaonekana hakuna haja kuongeza laana kwa ajili ya kufunua mwili tu - mtazamo ambao utakomesha laana kwa aliyekufa kwa sababu ya kuvunja sheria. Lakini taarifa inayoeleza sababu ya mwili uliongikwa hauna budi kuondolewa ni ya yo yote na haijawekea mpaka kwa mvunja sheria. Mvunja sheria anapotundikwa katika mti ipo hukumu iliyoongezwa inayomfanya auawe hivi ni laana inayofunuka. Mtu asiye kuwa na hatia ya kuvunja sheria ambayo kwayo alihukumiwa na ambayo alihukumiwa kifo kwa kuangikwa atakuwa chini ya laana. Jambo hili si kutafuta hakika, kwa kuwa ndivyo hasa ilivyotokea katika suala la Bwana, Paulo mwenyewe akiwa shahidi. Kristo akawa laana kwa sababu aliangikwa katika mti. Maelezo yaweza kupatikana kwa ukweli kwamba Torati ilishughulika hasa na tendo la kuvunja sheria na vile vile kunajisikia ambako kunaweza kumjia mtu asiye na dhambi. Kunajisikia katika matendo ya ibada kunaweza kuja kwa njia nyingi, lakini ya ajabu sana ni hayo yaliyokuja kwa kuitii Torati yenyewe. Kwa hivi Haruni ilimbidi aoge baada ya kutoa sadaka mahali patatifu zaidi katika Siku ya upatanisho.Mtu aliyechukua majivu ya hiyo sadaka nje ya kambi katika siku iyo hiyo vile vile alioga (Law 16). Kuhani aliyekuwa na zamu kumchoma mtamba mwekundi, majivu yaliyokuwa yaongezwe katika maji ya farakano kwa ajili ya kusafisha unajisi yalifupisha kwa kugusa kitu chochote kilichokufa, ilibidi aoge naye alikuwa najisi hata jioni. Na mtu aliyeondoa majivu alikuwa najisi hata jioni. Hata wahudumu wa tendo la ibada ya kusafisha unajisi huu walionekana kuwa najisi (Hes 19). Basi shughuli kamili iliyoamriwa na Mungu kwa ajili ya kutakasa ililetea unajisi matendo ya ibada. Torati ilikuwa na ugumu, kwa kuwa mtu aliyepuuza kanuni ya utakaso katika ibada alipopata kuwa najisi ilimbidi akatiliwe mbali. Kwa hiyo mtu aliweza kunajisika katika torati hata kwa kuitimiza ilivyotaka. Uchafu ulioletwa kwa kufanya sheria hizi za Torati ulikuwa hasa wa kufuata matendo ya dhambi. Lakini Torati haipambanui utendaji kazi wake kati ya uadilifu na dhambi ya matendo ya ibada. (15) Hatuwezi kutenga mpango wa kanuni za mema na mabaya toka matendo ya ibada katika torati ya Musa: Torati ni moja - hivi kwa upana wa kwamba mtu aliyejikwaa katika moja amekosa yote. Wakati ule Yesu, Paulo anatuambia, kwa namna alivyokufa, alikuwa chini ya laana ya Torati. Kwa taarifa hii yeye mwenyewe hakuwa na dhambi, na kwa kadhia yake kipindi wakati laana ilimfikia mambo yalipatana kwa kufahamu adhabu kamili ya laana ya Torati. Torati iliweka adhabu ya mauti. Yesu alilaaniwa kwa namna mauti yalivyokuja na madai yote ya Torati yalifaa kwa kifo chake, wakati maisha yake yasiyo na dhambi yalihakikisha ufufuo wake. Torati haiwezi kutaka lolote zaidi juu yake, akapita katika nguvu zake alipokufa, na hivi kwa mauti yake Torati iliyo mletea laana iliondolewa. "Kuifia Torati" Watu wote waliokuwa chini ya Torati walikuwa chini ya laana. Ni jinsi gani laana inaweza kuondolewa juu yao? Jawabu ni, kwa kujiunga na Yesu kushiriki mauti yake, na hivyo kushiriki matunda ya ushindi wake. Ni hivi tu ndipo laana ya Torati inaweza kuondolewa; na wote waliosuluibiwa na Kristo wanakuwa kwa maneno machache ya Paulo, "wameifia Torati". Torati haikuweza kuondoa dhambi; ilithibitisha hatia ya dhambi. Watu walio chini ya Torati hawana budi kuwa na Mkombozi. Ukombozi ulikuja kwa kufa Kristo; kwa maneno ya Paulo, yeye "ni mjumbe- mpatanishi wa agano jipya, ili kwa njia ya mauti, akomboe kwa makosa yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, na walioitwa waweze kupata ahadi ya urithi wa milele". Ufafanuzi mwingine mzuri sana kuhusiana na jambo hili linalozungumziwa unapatikana katika Torati ya Musa, mlango wa 18 na 28. Tunapoona hoja ya Paulo iliyo juu ya maneno kuhusu kuangikwa katika mti, inaonekana kuwa na maana kuishia kama kuingizwa kwake katika Torati Mungu aliweka tayari kwa ajili ya kutimiza kusudi lake. Chini ya utawala wa Waroma alikumbwa na mauti yake kwa kusulubiwa; katika muda wa awali au baadaye, kwa kawaida mtu hakuteswa na mauti ya jinsi hiyo. "Utimilifu wa wakati" ulileta pamoja mtu na matendo yaliyotimiza kusudi la Mungu. Matokeo ya Kristo kufanywa laana kwa ajili yetu (aya ya 13) ni mambo mawili, kila tokeo likiwa limeanza na "ili": "Ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie mataifa katika Yesu Kristo; ili (B.H.N) tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani" (aya ya 14). Katika mafungu mawili ya maneno "baraka ya Ibrahimu" na "ahadi ya Roho" tunayo maelezo ya mifano yenye maana zaidi ya moja ambayo yaweza kufungamana na matumizi ya jinsi ya kujijulisha - yaani, fungu la maneno linaloanza na kuonyesha uhusiano uliopo "ya". (16) Ni zile baraka za kwanza za Ibrahimu zinazoweza kutolewa, zile baraka zinazo mhusu Ibrahimu zinazoweza kugawanywa; au baraka zilizotajwa katika ahadi zilizofanywa kwake zitaletwa juu ya Mataifa yote? Je! "ahadi ya Roho", imetajwa awali katika aya ya 2; au Roho kwa maana ya utu mpya katika Kristo umezaliwa kutokana na neno kama lilivyotumiwa kwa Warumi 8; au Roho aliyoahidiwa katika kubadilika mwili kwenye ufufuo; au ni ahadi iliyofanywa na Roho kwa Paulo, wakili aliyetumiwa wa Roho; au ni neno lililotumika kwa kutiwa badala ya Mungu, anayetumia Roho kutimiza malengo yake? Jawabu linapatikana kwa kukumbuka maneno yanayoonyesha maana yake iliyokaribu sana na vile vile fundisho pana la Andiko. Katika aya ya 8 Paulo alieleza kwamba kuhesabiwa haki, masamaha ya dhambi, kilikuwa kiini cha baraka aliyoahidiwa Ibrahimu na uzao wake: hivyo alimaliza (aya ya 9) kwamba hao "walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani". Baraka ni kupatanishwa na Mungu kwa ustahimilivu wake wa kupishia mbali dhambi - makosa na hivyo kuingiza upendo wake. Hii ni baraka ambayo Mungu alimwonyesha Ibrahimu ya kuwa itawafikia mataifa yote. Kwa sababu gani, basi, Paulo anasema ya kuwa baraka hii sasa inaweza kuja kwa Mataifa kwa matokeo ya Kristo akiisha kuiondoa laana ya Torati? Jawabu ni kwamba kwa muda ambao torati ilitumika ilikuwa vigumu kwa Mataifa kumkaribia Mungu isipokuwa ni kwa njia ya kujiunga na taifa la Israeli na vivyo katika Torati. Taifa la Wayahudi lilikuwa ndio njia ya kupatiwa fadhili- na utaratibu wa kumwabudu Mungu ulitiwa katika Torati waliyopewa Israeli. Kuifuata Torati, mgeni hana budi kujishirikisha na taifa la Mungu. Ila Kristo alipoichukuwa laana ya Torati juu yake na vivyo akaitangua Torati, utaratibu mpya ukaanza kufanya kazi. Bwana mwenyewe alitaja badiliko hili kwa mwanamke yule wa Samaria: "Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika Roho na kweli, kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni Roho, na hao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli" (Yohana 4:23,24). Kwa hiyo baada ya ufufuo wake, Yesu akaagiza kwamba Injili ihubiriwe kwa Mataifa yote. Agano jipya (la Ibrahimu) likaidhinishwa na damu ya Kristo (Math 26:28), na tangu hapo na kuendelea mbele mitume, wakiwa ni "wahudumu wa agano jipya" (2 Kor 3:6) wakawavuta watu wote kuwa warithi wa ahadi za Ibrahimu. Matokeo ya pili- "ili tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani"- bila shida inaeleweka inapoweza kutambulika ya kuwa neno linalofanya kazi ni "ahadi". Mungu alifanya ahadi kwa Ibrahimu. Mara moja kwa namna yake maalum Paulo anaitaja katika aya ya 16: "Basi ahadi zilinenwa na Ibrahimu na mzao wake", na katika aya ya 29 "... ninyi (katika Kristo) ni warithi sawa sawa na ahadi". Hizi mbili zilizotajwa ni hakika zinafanywa kwa busara ya kuwa Paulo anapotumia neno "ahadi" katika aya ya 14, ana maana ya kwamba ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu. Kisha ni kwa nini imeitwa "ahadi ya Roho"? Kwa sababu Roho ilikuwa wakili aliyetumiwa na Mungu kwa kuzijulisha, na kwa Roho inamaana Mungu (wakili kwa mfano uliowekwa kwa ajili yake mwenyewe). (17) Kusoma kuwa "ahadi ya Mungu" maana inakuwa wazi. Lakini misemo iliyo katika mfano haitumiki kwa shauri lake wenyewe: kwa kuingiza kwao jambo lingine linaongezeka. Mungu anapoitwa "Kicho cha Isaka" ni neno linaashiria ya kwamba alikuwa Mungu wa Isaka na vile vile ni Yeye ambaye Isaka alimcha. Paulo alikuwa anasisitiza katika aya ya 2 kuwa kwa njia ya Injili walipokea Karama za Roho kuwa uthibitisho wa kweli yake. Kwa kuinena ahadi ya Roho, Paulo anaonyesha kwamba Mungu huyo huyo ndiye aliyefanya katikati yao uthibitisho huu wa Paulo na Injili yake, alikuwa ndiye kwa Roho yake alifunua nia yake na kusudi zamani, na sasa anathibitisha kuingizwa mataifa kwa uongozi wa Roho yeye yule katika mitume. Tunasisitiza kwamba Paulo hawazii kupewa karama za roho kuwa ni jambo lililoahidiwa. Wazo lake limekwenda kwa kina zaidi kuliko hivyo. Ahadi zilipokelewa "kwa njia ya imani" kwa kuwa imani ilikuwa sharti juu yake ambapo Ibrahimu alikubalika, na watu wakawa na warithi tu wa ahadi kwa imani. Uthibitisho ulionyeshwa katika aya ya 14 ulihimiza njia ya busara kwa nafasi ya Wagalatia. Ushawishi wao mbaya uliotoka kwa Wayahudi ulikuwa unawarudisha nyuma katika utaratibu uliofanya kazi kabla ya kifo cha Kristo, na kwa njia hii kama kuwaleta kuwa chini ya laana ya torati. Lakini kifo cha Kristo kilileta mwaliko wa kushiriki wokovu wa Mungu uliopelekwa kwa Mataifa. Wagalatia walikuwa wanapoteza mibaraka na fadhili zilizopo ambazo sasa zilipatikana bila kuchukua kongwa la Torati. Wanaweza kurudi nyuma, lakini Paulo si hivyo. Wala wasirudi nyuma kabisa kama atawapeleka mbele. Kwa ushawishi wa namna gani afanya hivi anapotumia neno "tupate"! Yeye mwenyewe Paulo anaungana nao kama mtu ambaye ahadi imekuja kwa imani. Si "ninyi" bali "sisi tupate" - Mimi, Paulo, niwaleteaye habari njema, waongofu wangu, mliopokea habari njema. AHADI HAIKUBADILISHWA KWA TORATI Historia (Gal 3:6; Mwa 15:6) na ahadi (Gal 3:8; Mwa 12:3) pande mbili huthibitisha ya kuwa ilikuwa ni kwa imani ndipo mtu atahesabiwa haki; tena Torati ilimletea mtu laana (Gal 3:10; Kum 27:26). Kwa kufahamu hivyo, Wayahudi wa Kikristo walijiuliza swali kwa nini Mungu alitoa Torati kwa wote kuwa njema, na moja lilihitaji jawabu. Basi kwa swali hili, Paulo anageuka sasa, kwanza akionyesha kwamba Torati ilitolewa baada ya ahadi haikutangua ahadi. Anaanza maneno yake ya kusadikisha kwa maelezo yaliyokubalika kibinadamu: "Ndugu zangu, nanena kwa jinsi ya kibinadamu; lijapokuwa ni agano la mwanadamu, hata hivyo likisha kuthibitika, hakuna mtu alibadilishaye, wala kuliongeza neno" (aya ya 15). Wino mwingi umetumika juu ya neno "agano". Kwa neno la Kiyunani agano ambalo limetumika katika Kiyunani cha Lugha iliyotumika zamani za kale katika gombo la maneno yaliyoandikwa, ni suntheke. Ila Paulo anatumia neno diatheke, ambalo kwa kawaida yake linamaana wosia, tabia, kisaidizi. (18) Tafsiri ya neno imevuta maneno ya majina ambayo leo tunayatumia kutenganisha maneno mawili ya Maandiko. Kwa upande mwingine, tafsiri ya Biblia ya Kiyunani (Septuagint) Agano la kale linatumia diatheke kutafsiri neno la Kiebrania birth, ambalo bila kuhoji maana yake agano. Kwa kweli kutumika hivi ni mfano mmoja, karibu tofauti tano tu zimejulikana katika mfuatano wa maneno ya Hatch & Redpath kwenye LXX. Zoezi hili la LXX katika kutumia diatheke kwa ajili ya agano linatosha kuweka matumizi yake miongoni mwa wasomaji wa Agano la Kale maneno ya Kiyunani. Lakini jambo linalozungumziwa laweza kufaa kupimwa . Yeremia 31:31 lipo agano jipya ambalo Mungu atafanya na Israeli. Agano la kale lilifanywa pale Sinai na likaimarishwa kwa kunyunyuziwa damu za wanyama. Tofauti ya Agano jipya na la Kale ni kule kutoa msamaha wa dhambi, na hili linahitaji kuthibitishwa na ":dhabihu zilizo bora" kuliko za agano la Kale (Ebra 10:16, 17; 8:6; 9:23). Hizo zilizo bora dhabihu zinazothibitisha ni kule kujitoa Yesu, hii dhabihu pasipo shaka 'ipo mahali pa maneno yake yeye mwenyewe: "Hii ni damu yangu ya gano jipya iliyomwagika kwa ajili ya ondolewa la dhambi za wengi (Math 26:28). Neno Diatheki limetumika hivi katika Wosia Mpya sawa sawa na Wosia wa kale "agano" na maana ya Agano la Kale ni moja, nayo haina budi kufuatana na neno lililo katika Agano Jipya lote ambamo neno limetokea. Kidokezo kwa nini LXX imetumiadiatheke kwa kuwa berith ni kwamba tangu desturi ya Kiyunani katika tabia ya wosia ilionyeshwa na neno ambalo halikueleweka miongoni mwa Waebrania, neno lilichaguliwa na lilitumika katika agano la Mungu na watu wake. "Haya yalikuwa ni matokeo ya Mungu mwenye enzi katika neema na upaji wake, na sio jambo la heshima ya mapatano ya wao kwa wao. (asema F.G. Rendall), "ilikuwa shida kueleza maneno ya Kiyunani kuwa agano; ilikuwa kwa upande mwingine ya kulingana katika madaraka ya mali na wosia na kwa patano lilionyeshwa na Neno diatheke". Karama za Mungu kwa Ibrahimu ni "maagano ya ahadi", haya ndiyo ayanena Paulo anawazia ya Kiyunani au desturi za Warumi za "kisaidizi". Agano la kale linatoa mambo ya hakika ambayo juu yake mtume anaweka maneno yake ya kusadikisha na kwa hiyo anayaweka maneno na maana yake iliyotumika Maneno ya Paulo ni ya kusadikika kwa mambo yote. Mtu anapofanya mipangilio au agano, nalo likithibitika, haliwi katika uwezo wa awaye yote mwingine kutangua au kuliongezea kitu. Je! Mungu ameongeza jambo lolote ambalo linageuza ahadi? Paulo anapenda kuonyesha ya kuwa wakati Torati ilikuja baadaye, haikubadilisha masharti na ahadi; Lakini kwanza anaweka maelezo sahihi ambayo atayathibitisha kwa mafunzo yake. Aya ya 16 imezoeleka sana kwa wote wanaotafuta kujibiwa na Maandiko kuhusu kusudi la Mungu lililofanywa katika Agano la Kale. Pasipo kupunguza thamani kwa njia yoyote ya matumizi ya kawaida ya hii aya, hebu tuone maana yake katika hali yake inayoonekana. Kama agano la Mungu kwa Ibrahimu (na tunaona kwamba Paulo analinganisha agano na ahadi kwa jambo analosema sasa): "Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. (19) Hasemi, kwa wazao, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, kwa mzao wako, yaani Kristo". Ahadi ndiyo iliyotangulia Ibrahimu aliahidiwa ahadi, na kwa hiyo iliitangulia Torati karibu miaka mia nne. Kwanza ahadi hii ni ya muhimu zaidi; pili, malengo ya Mungu yaliyonyeshwa kwa namna ya ahadi, na ahadi hazihusiani na makubaliano - pande mbili- huja kwa asili toka kwa mtoaji hadi kwa mpokeaji; tatu; ahadi si kwa wazao wengi, - ni kwa Ibrahimu na mzao wake, uzao mmoja, kama Paulo anavyoonyesha. Awali mtume amesema ya kuwa walio wa imani ndiyo watoto wa Ibrahimu (aya ya 7). Kuwa na ukoo mmoja na Ibrahimu katika mambo haya msingi wake haupo kutoka kwenye mwili wa nyama bali juu ya mapatano ya roho. Jamii ya kweli ya Ibrahimu ni wale wote wamoja katika kuwaza na kusudi. Zaidi ya yote, wao ni wa- moja na Mungu kwa sababu ya kujiuga na Ibrahimu na vile vile wao ni "watoto wa Mungu" (aya 26). Paulo amesema kwamba mzao ni mmoja. Na wakati kwanza tunadhaniwa huu ni ufafanuzi wa mahesabu tunakuta kwamba vile vile una uzazi mkubwa wenye umoja wa Kimungu. Neno "mmoja" linarudia tena katika aya ya 20 na 28 na muunganiko katika maneno ya Paulo yanayosadikisha. Uchaguzi wa "mzao" kihistoria umeelezewa katika shughuli za Mungu na wazao wa Ibrahimu. Kwa wana wawili Isaka na Ishimaeli (wazao wanaozumgumziwa kwa kuonyesha fumbo la maneneo katika mlango wa 4), Isaka alichaguliwa wakati Ishimaeli alitupwa nje. Wazao wa Isaka - watoto mapacha Esau akakataliwa na Yakobo akachaguliwa. "Kusudi la Mungu kulingana na uteuzi" ni hivi umeonyeshwa, ni "watoto wa ile ahadi" ndio wanahesabiwa kuwa "wazao" (Rum 9:7-13). Hawa wote "watoto" wanaunda pamoja "mwili mmoja" katika Kristo: wao ni kundi ambalo Kristo ni kichwa, nao wakiwa ni "mwili wake", wanakuwa, kwa maneno makubwa, "Ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote" (Efe 1:22,23). Hapo Waishimaeli na Waedomi walikuwa chini ya tendo la kufikiriwa, pasipo shida Myahudi alipunguza thamani ya ukoo wa kimwili. Paulo anasema kutoona muhimu kufanywe sawa sawa kwa wote wenye ukoo wa kimwili - Myahudi asiyemjali Mungu hakuwa na ubora kumpita Mwarabu asiyeamini. Hii haina maana kwamba utaifa wa Israeli umekatiliwa mbali toka haki yao ya uzaliwa wa kwanza wa mwana wa taifa la Mungu; karama na mwito wa Mungu hauelekei kubadili nia kama Paulo asemavyo. Lakini kutiwa wote "wazao" wa taifa hakutoi faida ya kiroho, kwa maana hiyo hutegemea juu ya sifa za kiroho kwa imani na utii. "Uzao mmoja" ni Kristo - Masihi - ye yote aweza kuthibitisha kuwa ni Kristo. (20) Nafsi yake ile ile ilikuwa kwa Paulo na wasomaji wake bila kukanushwa, na mabadiliko yanatoa sauti, si pasipo sababu, juu ya majina, "imani ya Yesu Kristo" (aya ya 22), " imani katika Kristo Yesu" (aya ya 26), "kubatizwa katika Kristo", "Kumvaa Kristo" (aya ya 27), "mmoja katika Kristo Yesu", (aya 28), yalimalizikia na: "Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu", "mzao mmoja" wa ahadi. Hatua zilizo katika uthibitisho wa maneno ya Paulo 3:15-18 ni: (a) Agano linapothibitika haliwezi kuondolewa au kubadilika, (b) Mungu kwa agano la ahadi aliagana na Abrahamu mbaraka halisi, (c ) vidokezo vya kulingana na torati. Kitu cha tatu kinashughulika na aya ya 17 na 18 ambazo tunasoma: "Ni semalo ni hili; agano lililothibishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini badaye haliitangui, hata kubadilisha ile ahadi. Kwa maana urithi ukiwa kwa sheria, hauwi tena kwa ahadi; lakini Mungu alimkirimia Ibrahimu kwa njia ya ahadi". Yaweza kutambulika kwamba U.V kwa ushahidi mzuri imeondoa maneno "katika Kristo" kwenye aya ya 17. Ni kweli kwamba ahadi zinapata masahihisho kamili katika Kristo, kwa kuwa haziwezi kutimilika mbali na kazi kama Mwokozi. Ibrahimu na watakatifu wote wa kale watapata uzima wa milele kwa njia ya kujitoa kuwa sadaka Bwana Yesu. Lakini kwa mfano mmoja ahadi zilithibitika kwa Ibrahimu, na huo uthibitisho unatoa sababu ya maneno ya Paulo yanavyosadikisha. Agano na Ibrahimu lilithibitishwa na Mungu kabla ya Torati - kwa maana ya kwamba ahadi zilitangulia Totati kwa miaka 430. Ahadi ilikuja kwanza, ikathibitika; basi Torati haiwezi kuitangua, au kufanya isiwe na maana. Torati haiwezi kuwa nyongeza au marekebisho kwa maana torati haipatani na ahadi. Torati inahusisha na matendo ya sheria, ahadi yahitaji imani; torati yahusu mapatano ya wao kwa wao, ahadi huja bila lazima na ni ya hiari; torati inaishia katika hukumu, ila ahadi ya Mungu inapelekea kuhesabiwa haki. Basi Torati na ahadi kwa ukubwa zimepingana. Tena kama jambo la hakika, urithi ni kwa ahadi. Ibrahimu alipouliza, "Nitapataje kujua kwamba nitarithi"? Mungu akamwagiza aandaye dhabihu; siku ilipokuwa inaisha usingizi mzito na giza kuu, maana yake mauti, vikamjia Ibrahimu, naye Mungu akasema: " Ujue hakika ya kwamba uzao wako utakuwa mgeni katika nchi isiyo yake; watawatumikia watu wale, nao watawatesa jumla ya miaka mia nne" ila kizazi cha nne kitarudi hapa. Ndipo tanuru ya moshi na mwenge unaowaka ulipita kati ya vile vipande vya nyama, baada ya zoezi la kuthibitisha agano, lililothibitika na agano la kuwa baba wa walioaminifu. Ahadi iliyothibitika kisha ikasemwa tena: "Uzao wako nimewapa nchi hii (Mwa 15:7-18). Neno laweza kuongezwa katika wakati wa vipindi. Kwa dondoo iliyotolewa katika Kitabu cha Mwanzo, Mungu alinena kwa miaka 400. Paulo anazungumzia wakati wa mambo mawili ya miaka 430 kati ya ahadi na torati. Taarifa zote mbili zipo sahihi. Wakati zote mbili zinaishia na kupewa Torati, 400 inaanza na kuzaliwa Isaka- ametajwa tena "uzao wako" ukiwa umuwekwa mbali mwanzo wa awali. Wakati huo Ibrahimu alikuwa mzee wa miaka 100. Ahadi ilitolewa miaka 30 mwanzoni alipokuwa mwenye miaka 70; na tangu alipoingia nchi ya ahadi alipofika miaka 75, ahadi ya kwanza haina budi ilitolewa miaka mitano kabla ya kuingia hiyo nchi. (21) NI KWA SABABU GANI MUNGU ALIWAPA ISRAELI TORATI (3:19-24) Ikiwa kama Torati haikugeuza kidogo ahadi, Mungu alikusudia nini kwa kuwapa? Jawabu limegusa kile kinachoweza kuitwa utaratibu wa historia kufikiri kwa kufuata elimu ya Biblia. Torati ilifanya kazi wakati wote wa historia ya taifa la Israel, na mamlaka yake iliisha mwishowe kwa kuangushwa taifa. Huko kuangushwa kuliletwa na sababu nyingi za wanadamu; kwa jamaa ya Israel kuinuka nguvu za Babeli na baadaye kuenea dola la Kirumi; katika roho ya ushupavu kidini kwa Israeli; katika mabishano yasiyoepukika ya kiburi cha watu wawili. Mmoja ambao ulionyeshwa wakati ule kama kiasi cha nguvu kubwa iliyoshindikana kwa ulimwengu kuwahi kujua. Lakini haya ni mambo ya nje ya kuangaliwa; mtazamo wa Mungu unatoa sababu za ndani za kina. Kabla ya kuangushwa Israeli mwishowe, lakini matukio yalipokua yanasogea mbele kuelekea kwenye baa kuu, mzao wa ahadi ulitokea na ukakataliwa. Kifo cha mzao, kwa upande wa Mungu kilikuwa na matokeo ya kuitangua Torati. Torati ilitumikia kusudi lake, na mwisho wa kusudi hilo lilipatana, likawa katika maana halisi iliyounganika na mwisho, kwa muda uliokuwepo, wa taifa la watu walio na utaratibu. Paulo anasema ya kuwa Torati, iliongezwa kwa sababu ya makosa, hata aje huyo mzao aliyepewa ile ahadi (kwa jinsi ya maana hasa ya maneno) kwa sababu ya kuvunja sheria, yaani, kuihalifu (3:19). Kazi ya torati ilikuwa na matokeo ya kufunua upinzani wa ndani ya mioyo ya watu na nia ya Mungu: ilileta upande wa nje ukaidi na utundu uliopo lakini hauonekani. Mambo yaliyo sambamba na Waraka kwa Warumi ni ya muhimu hasa yakiwa msaada kwa Paulo kufasiri maana ya Paulo katika sehemu hii. "Sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana" (5:20). Katika mlango wa 7 anaielezea sheria aliyoiona yeye mwenyewe, na katika hii alishuhudia matokeo yake. Alikuwa hai bila sheria mara moja akiwa kijana mdogo wa Kiyahudi. Akiwa na elimu ya sheria, dhambi, anasema Paulo kwa mfano dhahiri, ikahuika, na dhambi hai ilifanya mauti ndani ya Paulo (aya ya 9). Hakuitambua dhambi ila kwa sheria (aya ya 7) na dhambi, ilionekana kuwa dhambi hasa (aya ya 13). Vile vile anathibitisha kwamba nguvu ya dhambi ni torati (1 Kor 15:56). Matokeo ya torati yalifunua uwingi wa dhambi katika mwili wa mwanadamu, na kuwa thibitishia wale waliokuwa chini yake kuwemo sheria ya dhambi katika viuongo vyao: pia sheria ilionyesha kwamba dhambi ilikuwa inapingana na mapenzi ya Mungu, na ya kuwa binadamu kwa hiyo kwa sheria hawezi kupata kwa yeye mwenyewe, kwa uzuri wake mwenyewe kukubaliwa na Mungu. Basi kazi ya Torati iliwafahamisha katika dhamiri za watu utakatifu wa Mungu na tofauti kubwa iliyowatenga watu wa Mungu. Majivuno ya Israeli yaliwapeleka katika upana mkubwa, kukosa somo wao wenyewe; lakini hii pekee iliwafanyia mafundisho zaidi ya mwili wa mwanadamu usivyo na upendo unapojitegemea wenyewe katika matakwa yake. Lakini mtu anapotambua mambo ya hakika ambayo torati kwa kazi yake hufunua nuruni, anakuwa tayari kugeukia rehema ya Mungu aliyo azimu, ikafunuliwa katika Kristo. Wakati uo huo, kukataa kabisa Israeli kukubali maandiko ya Mungu katika ujumbe wa mitume juu ya neema ya Mungu ikaonyesha haja kwamba Mungu kuwaletea adhabu kwa kuvunja agano. Hivyo Mzao uliotokea katika kilele cha historia. (22) Mzao katika Unabii Mzao wa kwanza ni wazao wa Ibrahimu, lakini kuna mfuatano wa kinabii unaothibitisha Mzao ulioandikwa. Ahadi ya kwanza kuhusu uzao wa mwanamke (Mwa. 3:15); mbaraka wa Yuda ambo hauelezi moja kwa moja umetaja kuhusu uzao (Mwa. 49:10); mrithi wa kiti cha enzi cha Israeli ni uzao wa Daudi (2 Sam. 7:12); Mungu alikuwa anatafuta "mzao unaomcha Mungu" (Mal. 2:15). Katika "mzao" uliokwisha kuja, vivuli vyote hivi vimetimilika, ila, kwa kuingiza, fungu la maneno lililotajwa katika Wagalatia ni mzao wa Ibrahimu. Torati "iliamriwa kwa utmishi wa malaika kwa mkono wa mjumbe" (3:19). Kwa hiyo, kulikuwa na viungo viwili, kati ya Mungu mtoa sheria, na watu wake waliopokea sheria. Ni mara moja tu Mungu alinena moja kwa moja, watu hawakuweza kuvumilia kusikiliza waliyoyaona, wakataka yasirudiwe (Kut. 20:19; Kumb. 18). Mungu akakubali ombi lao, ila sio nia iliyowasukuma hata wakaomba hivyo. Bali kutokana na kutotaka kwao kusikiliza sauti ya Mungu ukaja utaratibu wa kwamba manabii ndio wapokee ujumbe toka kwa Mungu na kisha kuuwasilisha kwa watu. Kwenye kichwa cha mfululizo huu wa manabii alikuwa Musa. Lakini alikuwepo mtu mwingine alikuwepo kati. "Malaika aliyesimama mbele za Mungu" (Isa 63:9) alimwakilisha Mungu kwa Israeli. "Jina langu limo ndani yake", alisema Mungu (Kut. 23:21). Malaika aliyemtokea Musa katika kijiti (Kut. 3:2), naye malaika "alinena na Musa katika mlima Sina", "katika Iklezia nyikani" kama Stephano alivyowakumbusha washitaki wake, akawatajia "Iklezia" lingine ambalo ndani yake masihi atatoa sifa (Zab. 22:25). Mtu aweza kustaajabu huenda neno la kusadikisha alilotoa Stefano lilikuwamo moyoni mwa Paulo alivyotoa hoja ya mjumbe wa Torati na kutofautisha mibaraka ya juu iliyounganika na mzao wa ahadi. Katika Waebrania 2:2-4 ipo tofauti na jinsi hii kati ya Torati na wokovu mkuu; lakini hapa suala zaidi lililotaja kuhusu malaika limekusudia kuonyesha umuhimu wa Torati, lakini tu kwa kufahimisha umuhimu wa neno "lililonenwa kwa Bwana" Yesu. Torati ilikuja kwa kupitia watumishi wa Mungu; Injili imewekwa karibu, ndani ya Mwana wa Mungu. Musa alikuwa mjumbe wa agano, amabapo malaika walikuwa matarishi ambao kupitia kwao Mungu aliwasilikisha nia yake. Musa alijitia kati ya agano la kale alipotamka maneno ya agano na kukaribisha watu wakubali ndipo "alitwaa damu ya ndama na mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu, na hisopo, akakinyunyuzia kitabu chenyewe, na watu wote, akisema, Hii ni damu ya agano mlipoamriwa na Mungu" (Ebra 9:19,20). Mjumbe Kwa mambo ya mjumbe yameelekea kufafanuliwa na Paulo nayo yamewatatiza mno wachambuzi kama maelezo ya 430 yaliyokwisha tolewa na kama yalivyosemwa. Kama taarifa ilivyo, "Basi aliye mjunbe si mjumbe wa mmoja", vivi hivi ni shauri lililo dhahiri na ukweli ndani yake na tena moja isiyo na maana ni fungu hili la maneno - kama taarifa ilivyo bayana ipo yenye kina iliyofungamana na neno "mmoja" kuliko "kundi moja" tu. Ni jambo muhimu kama tukikumbuka kwamba katika fungu hili la maneno "mjumbe" Paulo anamwazia Musa ambaye anamtaja kwa neno hili katika aya ya 19. (23) "Mmoja" ni yupi wa ambaye Musa si mjumbe? Basi anaweka, jawabu mara moja lipo wazi- mzao "mmoja" uliotajwa katika aya ya 16. Ikifuatia kama habari iliyo muhimu ya kufanya ukumbusho wa kupewa torati - malaika na Musa- walakini taarifa yaeleza kutotosha kazi ya Musa. Mwanzo wa Israeli kuwa watu wa Mungu kumetofautiana na "umoja" mkamilifu ambao ni alama ya "mzao" mmoja aiyeahidiwa. Musa na malaika walikuwa wa kwanza kuwa wawakilishi, ila hawakuweza kuweka wa pili. Umoja wa kimungu umeletwa na tendo la moja kwa moja zaidi la kimungu. Jambo hili limethibitishwa na maneno yaliyofuata, "Bali Mungu ni Mmoja", ambayo sasa hatuna budi kuyaangalia. Si kusema kwa nguvu tu ya kwamba yupo Mungu mmoja kama Paulo anavyofanya: ni nini kilicho muhimu kilikuwamo katika fungu hili la maneno? Hata hivyo fundisho la hakika kwa Mungu ni Mmoja linaweka msingi kwa wazo la Paulo. Kwa mtume "Mungu ni mmoja" jambo hili limeelezewa wazi katika Agano la Kale (Kum. 6:4), na vivyo kwa wazo la Wayahudi alivyo Mungu, ilihusisha elimu ya wokovu. Kwa muda Mungu akiwa mwenyewe ni mmoja, katika ulimwengu wake hakuna upatano, pande zote mbili ndani yake wenyewe na vile vile katika mahusiano yake na Muumba wake. Kutopatana namna hii ni changamoto kwa asili ya Mungu, na kwa kuwa ni mkuu, kutopatana inabidi kutoe sehemu ya amani na upatano; kama Mungu alivyo mmoja, wote waishio yawapasa kuwa wamoja ndani yake, kumkiri na kumpa heshima na utukufu yawapasa kuwa mmoja ndani yake, kumkiri na kumpa heshikma na utukufu inavyostahili. Si hivyo tu, bali kwa kuwa Mungu ni mmoja, hawezi kuwa na mpaka wa kuwa "Mungu wa taifa moja". Ikiwa kama miungu walikuwa wengi kungeweza kuwa na mgawanyiko wa miungu kadhaa katika mataifa mbalimbali, Yahweh (Yahu) akiwa ni Mungu wa Israeli. Lakini Yahweh hakuwa sawa katika cheo daraja au kwa uweza na awaye yote. "Bwana Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja". Yahu mwenyewe amesema kwa nguvu kuwa hapana Mungu zaidi yake. Kama tukigeukia katika barua waliyoandikiwa Warumi, tunakuta Paulo akitumia ukweli huu wa Mungu ni "mmoja" kwa kuweka njia zinazofuatana ambazo ndani yake Mungu anashughulika na watu, na haya maelezo yaliyotolewa yametajwa katika Wagalatia. Paulo amesema kwa nguvu "mwanadamu anahesabiwa haki kwa imani bila matendo ya sheria"(Rum.3,28). Kanuni hii ni kwa watu wote; kwa maana mwanadamu ni mtu yoyote, akiwa ni Myahudi au mtu wa Mataifa, ingawa njia mahsusi ambayo kwayo habari imetumika kwa utendaji wa imani yaweza kupishana. Utaratibu wa Mungu ni mmoja kwa wote: pengine, kama pakiwapo utaratibu ulio tofauti kwa Myahudi na kwa mtu wa Mataifa Mungu hawezi kuwa ni Mungu mmoja kwa wote. "Au je! Yeye ni Mungu wa Wayahudi tu?" Paulo anahoji; akimaanisha kwamba ikiwa wokovu ulikuwa kwa matendo ya kuishika torati, kwa kuwa Mungu aliwapa torati Israeli pekee, ndipo Mungu inabidi awe ni Mungu wa Israeli pekee. "Je! yeye si Mungu wa Mataifa pia?" Naam, Paulo anatoa jawabu, na kupata ushahidi wake katika kilichokubalika kwa neno na wote wenye akili hao Wayahudi - kuwa Mungu alikuwa Mmoja: "Kwa maana kama ikiwa hivyo Mungu ni mmoja" basi ni Yeye Mungu wa wote, Myahudi na Mataifa, na utaratibu wake unaokubalika haunabudi kuwa mmoja kwa wote. (24) Mungu atamhesabia haki Myahudi "bila" imani na mtu wa Mataifa "kwa" Imani. Israeli alikuwa na ufunuo wa Mungu, - "pasipo imani" katika lengo humo ndani lililofunuliwa Myahudi alihesabiwa haki: kwa Mataifa Injili ilihubiriwa, na madondoo ya habari ya mafundisho wakajulishwa kwa imani yote pamoja yakasimamisha "imani" ambayo kwayo Mataifa walikubaliwa. Wakati ule imani ilikuwa kwa kutumiwa na watu wote kigawanyo kwa pande mbili nyakati za agano la kale na jipya, namna moja ya kukaribia kwa Myahudi na kwa mtu wa Mataifa. Imani iliwaunga watu kwa Mungu ikawafanya mmoja ndani yake na mtu aliye pamoja Naye. Sambamba na habari hii inayofundisha kwa Warumi tunaweza kufasiri maneno ya Wagalatia "bali Mungu ni Mmoja". Kusudi likiwa moja lawapasa kuwaleta watu kuwa mmoja Naye. Maadamu torati iliweka mkazo wa asili ya kutopatana mwili wa binadamu na Mungu, basi Musa mjumbe wa torati hakuweza kujitia kati ya agano la "Mmoja" lakini la pili lilikuwa timizo lisilo na shaka na ndipo inabidi litimizwe vizuri kwa njia nyingine. Njia hizi Paulo ameonyesha kuwa ni kwa ahadi, ambazo kitovu ni katika Mzao Mmoja (aya ya 16), ambazo zinatenda kazi kwa imani, ambapo wote wanakuwa "watoto wa Mungu" na wote ni "wamoja" katika Kristo Yesu. Sala ya Mzao ambao damu yake ilikuwa inakaribia kumwagwa ili kuthibitisha maagano ya ahadi, yahusu umoja huu:"Ninawaombea....wote wawe umoja......ndani yetu" (Yohana 17:20,21). Mungu ni Mmoja Ukubwa zaidi unatoka katika Umoja wa Mungu. Ulitambulika kuwa Mungu kwa pande mbili torati na ahadi ndiye mwenye kuanzisha; lakini kwa Myahudi hapo ulionekana uadui usiopatanishwa katikati ya mbili. Huu kwa kuzunguka ulidokeza vitu viwili kwa Mungu, kwa mawazo haya mawili ya nia yake yalionekana kuhitilafiana. Lakini je! ulikuwepo huu uadui? "Je! torati haipatani na ahadi za Mungu?" Upinzani ulikuwepo tu katika moyo wa Myahudi kwa sababu ya kutofahamu kwake kusudi la Torati. Mungu akiwa ni Mmoja, hapakutakiwa pawepo chuki kati ya utaratibu wake mbalimbali. Ukweli wa kutofahamu ulikuwa kwamba hata siku moja Torati haikukusudiwa kuleta ushindani katika mfumo na ahadi. Ya pili inahusu urithi wa milele na kwa hiyo uzima wa milele kwa hao waliopokea ahadi. Torati haikukusudia kutoa uzima - utaratibu wa jinsi hii haukuwezekana; Mungu angeutumia, lakini kwa kuwa mtu hakuweza kufikia katika uzima kwa kuishika Torati, Mungu akajifunua mwenyewe akiwa ni mwokozi. Basi Paulo anaongeza ikiwa ni sababu yake ya kukataa kwa nguvu maneno yaliyodokezwa ya ushindani katikati ya mambo mawili. "Kama ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, yakini haki ingalipatikana kwa sheria" (aya ya 21). Kutolewa sheria wakati ule haikukanusha karama ya ahadi: bali Torati ilionyesha mwanadamu asivyofaa kitu, na kwa sababu hiyo yu katika hali isiyo na matumaini mbali na neema ya Mungu na kipawa cha uzima. Kwa mtazamo huu Ushahidi wa Andiko unakubaliana. "Andiko (kwa mfano, moja lililonukuliwa katika aya ya 10) limeyafunga yote chini ya nguvu ya dhambi, makusudi hao waaminio wapewe ile ahadi kwa imani ya Yesu Kristo" (aya ya 22). (25) Maneno haya yamefupishwa sana. Mungu "ameyafunga" (R.V.) yote. Kuna kifungo kinacho mzunguka binadamu na matendo yake vivi hivi sana hata hawezi kutimiliza kuokoka. Katika Warumi 11:32 Paulo anasema kwamba "Mungu amewafunga watu wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote": lakini maneno yaliyoandikwa katika Wagalatia ni ya kuweza kueleweka zaidi. Andiko(huyo ni Mungu, mwenye kulianzisha)"ameyafunga mambo yote chini ya nguvu ya dhambi" Dhambi ndiye mlinzi mkuu; wa "mambo yote" nayo yote yapo chini ya nguvu zake, kwa juhudi zote nzuri za Mwanadamu, malengo ya hali ya juu, bado yanakuwa na dosari ya dhambi. "Ahadi" kando ya jambo lingine lililiokuja baadaye hubakia kuwa neno lililoahidiwa -baraka, ambayo kwa mzunguko ni kuhesabiwa haki, kama tulivyoona katika aya ya 8. Juhudi yote ya mwanadamu ikiwa imeharibiwa hivi na dhambi, kuhesabiwa haki tu ni kwa imani iliyo kwa Yesu, aliyekuja kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi makusudi dhambi zisamehewe, kunaweza kufungua njia toka jela ya mwanadamu. Torati iliingizwa hata aje huyo mzao (aya ya 19). Hadi kuja kwa Kristo, na matokeo ya kuihubiri imani iliyo katika jina lake, (au, kama kwa kifupi imewekwa katika aya ya 23, "kabla ya kuja ile imani"), "tulikuwa tumewekwa chini ya sheria", iliyotenda kazi kama mlinzi. Ilikuwa mlinzi aliyelipiza kwa nguvu kama dhambi ilivyokuwa na nguvu sana, kwa zote mbili dhambi na sheria Paulo anatumia neno"kufungwa" (aya ya 22 na 23). Ingawa hivyo, huyu mlinzi alitazama maendeleo ya "imani ambayo baadaye itafunuliwa". Wakati ule sheria haikuwa ndiyo mwisho wake yenyewe, bali wakati wote ilikuwa inaendeleza shabaha. Ilikuwa kivuli cha mambo mema yaliyokuwa yanakuja; utendaji kazi wake ulikuwa mtumwa-Mkufunzi, au paedagogus. Kazi yake, zaidi kwa vitu vya nyumbani, ilikuwa kulea vijana wa nyumbani wenye umri kati ya miaka saba na kumi na saba, katika uadilifu, kwa tabia njema na huduma ya elimu. Hili lilikuwa ndiyo kusudi la torati, ilikuwa mtumishi wa kuongoza, kufundisha na kuzoeza lakini wale waliokuwa chini ya mamlaka yake walikuwa na cheo kidogo, ambao kwa kufikia utu mzima,wanakuwa wamepita toka mamlaka ya mtumwa- mkufunzi. Utimilifu wa kimo cha utu mzima ulikuwa katika Kristo: huduma ya torati ilidumu kwa wakati hadi Kristo alipofika, na utendaji wake wa kufundisha kuhusu yeye ulikoma alipokuja. Kristo akiisha kuja, njia ya kuhesabiwa haki kihistoria ilionyeshwa kwa dhabihu ya mauti yake, ufufuo wake na tangazo la msamaha wa dhambi katika jina lake. Kazi ya mtumwa mkufunzi ilifanyika, kwa vile ilivyowaelekeza wale walio chini ya mamlaka yake alipokuja; watu waliweza kuhesabiwa haki kwa imani. HALI YA KUWA MWANA KATIKA KRISTO (3:25-29) "Imani" (aya ya 25 U.V.) katika fikira ya Paulo ni utaratibu wa ile kweli iliyotangazwa ili watu wasadiki. Kazi yake na ujumbe wake ilikuwa"kuwageuza watu waiache giza na waielekee nuru, makusudi waweze kupata msamaha na ondoleo la dhambi na kupata urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwa Kristo. Mpaka kifo cha Kristo hili "ondoleo la dhambi kwa jina lake" halikutangazwa. (26) Tumeona kwamba kudhihirika Mwana wa Mungu kwa wakati kulingana na mwisho wa sheria, pande mbili, katika kusudi la Mungu na kwa matokeo ya mabadiliko ya kihistoria yaliyoletwa kwa utawanyiko wa Wayahudi. Kwa fundisho la Yesu na lile la Mitume tunafikia utimilifu wa ufunuo wa kusudi la Mungu. Ufunuo huu ulikuwa ushindi wa polepole haukuwa na sharti, ingawaje - kama mitazamo ya wakati wa sasa iliyo muhimu kabisa na inavyodokeza- kwa maendeleo ya uvumbuzi wa mwanadamu njia za Mungu, bali kwa mabadiliko yaliyo katika mazingira.Ahadi iliyokuwa rahisi kufanywa katika Edeni ilikuwa ni njia tu ya taarifa ya kusudi la Mungu lililofanywa wakati ule. Kugawanyika kwa jamii ya binadamu katika mataifa na mashindano kama matokeo ya jambo la kumiliki mema na kwa maarifa ya nchi muhimu yalitoa hali ya mambo kihistoria kwa ajili ahadi iliyofanywa kwa Ibrahimu kuhusu kumiliki nchi milele. Jambo lililojitokeza sana la kufuatana na kiti cha enzi na kanuni mpya iliyowekwa kwa wafalme wa Israeli lilipelekea agano la kiti cha enzi na Daudi. Uzima wa milele, kumiliki nchi milele, kutawala mataifa na Masihi, haya ni Mambo yaliyo ya Msingi wa imani. Ufunuo wa Agano la Kale ulikuwa na kila moja ya hizi ahadi tatu za "Mzao" habari ya kuwa kwa mmoja ambaye zitatimilika atakuwa Mwana wa Mungu. Huyo Mwana alipotoa ujumbe wa Mungu kwa kizazi chake ukweli wa kuwa Mwana ulikuwa na sehemu iliyojitokeza. Lakini hali hiyo ya kuwa Mwana haikuwa ni yake mwenyewe tu, bali hali ya kuwa mwana na kwa hao wa mwaminio iliwekwa mbele. "Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu; ndio wale waliaminio jina lake" (Yohana 1:12). Ufunuo huu kuhusu daraja la watoto ni wa maendeleo muhimu katika kudhihirika kusudi la neema ya Mungu kwa watu. "Sasa tu wana wa Mungu" Yohana aliandika. "Ikiwa mnamwita Mungu ni Baba", ndipo Petro akasema, "Iweni watoto wa kutii" (Petro1:14). Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana Mungu.... Mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia , Aba yaani Baba" (Rum. 8:14,15). Hakuna uhusiano wa juu na Mungu kuliko huo unaowezesha kuwa wana: na kuja kwa Mwana wa Mungu tunayo kila maana utimilifu wa ufunuo wa Mungu tu utakaozidi sana, ila matokeo yatafikiwa kwa huo uhusiano, kwa kupewa mwili usioharibika hao watoto. Torati, ikihusu katika tukio la amri ya Mungu kabla ya kuonekana Mwana wa Mungu, ilikuwa ni sehemu ya ufunuo ulioandaliwa. Kuadibisha kwake na utaratibu wa kanuni ya mafunzo ulikuwa na ulinzi wa mamlaka juu ya mtu, kwa hiyo kuna wepesi katika matumizi ya Paulo katika mfano wa mwalimu-mtumwa, mfano ambao ameulinganisha na Torati. Mfano huu unatumika hivi tena: kadiri muda unavyopita unaleta kupevuka kwa maagizo yake, huduma ya Mkufunzi-Mtumwa ikafikia mwisho. Wale waliokuwa chini ya uangalizi wake wamefikia daraja la kufanywa wana. Hali hii ya kufanywa wana ni kanuni ya"imani" iliyohubiriwa sasa; na kwa sababu hii watu hawawi tena chini ya kuamrishwa na Torati. Kwa hoja hii Paulo anaongoza katika Wagalatia kuona kwamba maendeleo ya mpangilio wa Mungu umeiacha nyuma Torati. (27) "Lakini, iwapo imani imekuja, hatupo tena chini ya kiongozi." Badiliko toka "hatupo" hadi "ninyi"kwenye aya inayofuata ni jambo linalobainisha kuwakumbusha wasomaji wa waraka ya kuwa wameiacha nyuma Torati. "Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mun gu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu" (aya ya 26). Ni jinsi gani waangaliwe kuwa ni watoto ambapo kwa kweli hawakuwa hivyo kwa kuzaliwa? Njia pekee ni kufanywa Mwana. Namna ya kufanywa wana ni kwa kuunganika na Kristo, ambaye alikuwa Mwana wa Mungu kwa kuzaliwa. Kwa yeye wanashiriki hali yake mwana. Kuunganika naye hutimilika kwa kufuata kanuni ya kujishirikisha na mauti yake na kufufuka kwa kubatizwa katika Kristo. Huko kuunganika na Kristo ni "kumvaa Kristo". Paulo anazungumzia mara nyingi "kuvaa" katika mfano wa vazi hauna budi kutoa maana kamili, ila maana kamili inabidi iamuliwe na fungu la maneno. Katika fungu hili la maneno yenyewe Paulo anawazia juu ya kupita toka utoto hadi utu uzima, na linaweza kuwa hivyo kwamaba limo akilini mwake tendo la kuvaa nguo ya kujifunika mtu mzima ambayo kwayo kijana katika ulimwengu wa Wayunani na Warumi ilionyesha badiliko la maisha ya kila siku. Aaminie "humvaa" Kristo, anapokea majukumu na haki ya kufanywa Mwana; anakuwa ni ndugu mwenyeji na Watakatifu wa Mungu: na yote yaliyo ya Kristo yanakuwa yake. Katika msimamo huu mpya tofauti za kibinadamu hazipo. Sala ya Kiyahudi siku ya baadaye walakini ambayo inaweza kuwa asili yake ni nyakati za zamani, ilisemwa: "Mungu wangu nakushukuru kwa kuwa sikuzaliwa Mmataifa, bali Myahudi, si Mtumwa ila mtu huru; sio mwanamke bali mwanamume". Binadamu ni mpumbavu kiasi gani kujivunia tofauti za kibinadamu! Mambo haya ya kuainisha hayana thamani yoyote katika Kristo-hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala aliye huru, mtu mume au mke. Aina zote za watu, ikiwa ni taifa lenye cheo cha jamii ya watu, au ya jinsia, wanasadikika kutokuwa na maana ndani ya kusudi la Mungu. Wote wanakuwa "wamoja" katika Kristo Yesu: kwa wanaume wote na wanawake vyo vyote wakitofautiana kwa utaifa au cheo, wanainuliwa juu katika hali ya kushiriki Umoja wa ki-Mungu ambao ndio kusudio lake na mwanadamu. Tumetazama katika "hali ya kuwa mmoja" kwa kuangalia aya ya 16 na 20. Sasa tunaona ni kujumuishwa katika jamaa ya wana wa Mungu waliokombolewa: kuwa mmoja na Yeye kwa njia ya Mkombozi aliyetukuzwa, Mwana wa Mungu. Jambo lililoandikiwa maneno katika kipindi hiki yamemalizwa na kusimuliwa katika neno lililozungumziwa ambalo limenenwa katika mlango wote wa 3 kwa kuishia na maneno: "Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi". (28)