_____________________ WARAKA WA MTUME PAULO KWA WAGALATIA SURA MBILI The Letter of Paul to the Galatians - Chapter Two _____________________ SAFARI YA PILI KUTEMBELEA YERUSALEMU. Hao waandishi wanaojulisha safari ya kutembelea Yerusalemu iliyoelezewa katika mistari hii na Baraza lililo katika Mdo. 15 wamelazimika kusema yakuwa kwa maana ya sababu nyingine Paulo anaruka katika Wagalatia ushahidi wowote wa kuzuru kwa ajili ya kuchukua msaada uliosemwa katika Mdo. 11:30. Maana Paulo katika kufanikisha kuthibitisha kufuata mashauri ya Mitume wengine kwa ajili ya injili aliyohubiri, walakini ilionekana kuwa muhimu, kwamba ataje kila safari kabla ya kuzuru kwake kwanza katika Galatia. Kufanya vingine kungemtia wazi yeye mwenyewe katika kuagizwa kuwa ameacha ulinzi wake safari halisi mitume walipomuamrisha kuhubiri na kuagizwa katika ujumbe wake. Ushuhuda wake haukuwa umekamilika kwa kuruka hivi: kila kukutana na Mitume wengine basi ilibidi kutajwe. Huku kufikiri kunatoa hali inayoelekea kuthibitisha kuwa kweli, ikiwa sio hakika, katika uthibitisho wa Wagalatia 2:1-10 na Mdo. 11:30. Mwaka wa 14 inabidi basi uhesabiwe toka kuongoka Paulo, na si tokea safari ya kwanza katika Yerusalemu ya Wagalatia 1: 18. Ni muhimu kukumbuka kwamba katika habari ya mambo yenyewe vivi hivi kama utetezi huu, kama wazo la mambo ya maisha, yaliyokwisha pita, la shitaka, la shindano, yote ambayo hayajulikani kwa msomaji aliyepo lakini yalizoeleka kwa wasomaji wa kwanza. Maelezo ya maneno yasiyodhahiri kwetu yalikuwa wazi kwa Wagalatia; yaliyotajwa kwa kuandikwa ambayo tunaweza kukosa yalikuwa na maana kwao. Kwa kulinganisha Walaka na Matendo ya Mitume hatuna budi kukumbuka kuwa historia ya Luka iliandikwa kwa kusudi lingine kuliko ushuhuda wa Paulo dhidi ya shambulio la wasingiziaji wake Wayahudi; kwa hiyo kujaza kwingine kwa habari moja moja kulihusu kusudi mahususi kila moja lilikuwa na maandishi ya safari. Habari moja moja inatofautiana kwa kupatana na kusudi maalum katika simulizi. Kipangamizi kimoja cha nguvu kwa kawaida kukubalika uthibitisho wa Wagalatia 2: 1-10 na baraza katika Mdo. 15, ni kwamba katika Baraza Paulo alipokea amri ambazo zilikuwa zimetiwa pamoja mashauri ya maamuzi yake. (1) Lakini Paulo anaruka ushahidi wowote kwa jambo hilo katika Wagalatia 2: 1-10, na kuruka huku ilikuwa hatari kwa dai lake la uaminifu (1:20) ikiwa safari inayoeleza ilikuwa kwenye baraza. Lakini kama makanisa ya Galatia ni yale Paulo yaliyohubiriwa injili naye katika safari ya kwanza, basi baraza halikutokea kwa wakati na uthibitisho wa ujumbe Paulo aliowatolea ulikuwa umejitegemea. Kwa kweli, Paulo alichukua maagizo ya baraza hadi Galatia katika safari ya pili, na ushindi juu ya Wayahudi ulifikiwa kwa jitihada. Lakini kama tukitia tarehe barua ya Galatia mbele ya baraza ambayo inaelekea zaidi, ndipo tunaona kwamba Paulo anapigana vita katika waraka ambao vile vile ilikata shauri katika baraza. Katika matokeo yote mawili yaliamuliwa juu ya mafundisho ya kwamba sheria ya Musa ilikuwa haiwafungi Wakrito. SAFARI YA PILI YA PAULO Sasa tunaona matukio yaliyompata Paulo katika safari yake ya pili ya kutembelea Yerusalemu kwa maelezo zaidi. Alipanda kwenda huko na Barnaba, na Tito alikwenda pamoja nao. Hicho hicho kiarifa "Wakamchukua", kimetumika katika Mdo. 12:25 kwa Marko, kina maanisha kwamba Marko alikwenda akiwa msaidizi katika kazi. Vivyo naye Tito. Safari ikiwa ni ya kupeleka msaada ukawepo usafiri na utaratibu mzuri wa maana. Kwa kuwa hali ya njaa ilienea, Paulo na Barnaba iliwabidi wanunue chakula kila mahali na kupeleka hadi Yerusalemu. Tunakosea kama tukidhania walichukua pesa ambazo zaweza kutumiwa Yerusalemu. Kwa kazi hii ya kukusanya chakula mtu wa kusaidia alitakiwa, na uwezo wa Tito aliouonyesha baadaye ulidokeza ya kwamba uchaguzi wao ulikuwa ni wa busara. Katika Matendo ya Mitume tumeambiwa ya kwamba msaada ulipelekwa kwa "mikono ya Barnaba na Sauli" (Mdo. 11:30). Safari ilifunuliwa. Kama tulitegemea katika waraka peke yake, kwa kiwango kinachokubalika tunaweza kufahamu sababu yake kwamba ufunuo aliopewa Paulo ndio uliopelekea afanye safari. Lakini Matendo ya Mitume inatuambia kwamba unabii wa Agabo kuhusu kuja njaa ulikuwa ufunuo. (2) Pengine huu huenda ulifahamika vema, lakini kwa vyovyote vile kitu cha muhimu katika suala la Paulo ni kwamba hakufanya hivyo kwa shauri lake mwenyewe bila kuamuriwa na mwingine kwenda kutaka ushauri au msaada kwa mitume waliokuwa Yerusalemu. Ingawa hivyo, wakati akiwa huko, aliweka mbele yao (kanisa) aina ya Injili aliyoihubiri, na ndipo akawa na mazungumzo binafsi na mitume watatu. Sababu yake kuwa na mahojiano haya binafsi anaeleza: hakutaka Injili ambayo tayari alikuwa anaihubiri isiwe na matunda. Hii ingekuwa ndiyo sababu kama pasingalikuwapo makubaliano juu ya kazi ya Paulo. Kwa kuunganika Myahudi na mtu wa Mataifa katika kanisa moja zilikuwepo sababu zote za ugomvi na matatizo. Kama lingekuwepo kanisa la Kikristo la Wayahudi na kanisa la Kikristo la watu wa Mataifa, ingekuwa sababu ya kufisha umoja huo wa wote waliokombolewa katika Kristo. Kwa hiyo Paulo aliwataka waijue kazi yake na shughuli za kazi, na matokeo ya mahubiri yake. Paulo anapowataja watatu kuwa "wale wenye sifa" na wale "walio kuwa vyovyote" (aya ya 2 na 6), inatubidi tusione msemo huu kuwa ni wa kuvunja heshima. Muundo kama huu ungekuwa ni mwenendo ulio nje na urafiki wa Paulo kwa wale waliokuwa mitume kabla yake, pia katika roho ya kirafiki ambayo katika mahojiano ni dhahiri ilienea. Ikiwa Wayahudi walitumia maneno yaliyowahusu mitume wakuu katika kuvunjiwa heshima na Paulo, tunayo sababu kwa ushahidi wa Paulo. Anasema kuwa alipokutana na wale wenye sifa kuwa wana cheo haikuwa afundishwe nao, bali kuingia katika kupatana kuhusiana na mgawanyiko wa kazi ya Injili baina ya pande mbili. Usaidizi wa Tito, yeye akiwa ni Myunani, kwa kawaida ulivuta macho ili kuangaliwa, ni wazi kuwa ilikuwa sababu ya mjadala mwingine. Paulo anasema kwamba ndugu za uongo walikuwa viongozi kwa huo mjadala. Lugha ya Paulo imefupishwa na kwa ujenzi wa elimu yake iliyovunjika: lakini mawazo mengine dhahiri yanatokea. Wayahudi hawakupenda Tito awepo, ndiyo waliofanya uchunguzi ufanywe na watu wengine. Huu ukafanyika chini ya kivuli cha kujifanya marafiki. Uchochezi ulianza kwa kusema Tito inabidi atahiriwe, bali Paulo aliposikia kwanza alipinga mpango huu. (3) Angekubaliana na mwendo huu uhuru ulio kwa Kristo ungeharibika na utumwa wa sheria ungaliwekwa juu ya Wakristo. Mitizamo hii inayotatiza iliyofanywa hivi dhahiri ikafanya Paulo atake kuonana na viongozi watatu- lakini mabishano hayakuwepo nao, hakuna kuhitilafiana katika wazo, ila upatano na makubaliano. Tafsiri inayofanya kazi kwamba neno lililoshurutishwa lilifaulu, kana kwamba Paulo alikubaliana kwa ajili ya amani kwamba Tito lazima atahiriwe, lakini kwa hiari na si kwa lazima, haistahili sababu ya maneno ya kubishana. Jambo hili lingetokea suala la Paulo kuhitaji kuelezwa kwa namna tofauti kabisa na kwa njia tofauti kabisa kwa hatua iliyochukuliwa. Paulo alishitushwa na watu waliojifanya wamoja naye wale walioazimia kwamba Tito lazima atahiriwe walijifanya marafiki huku wakiwa wameficha mawazo mengine. Mara ya pili Paulo hakukubali kwamba Tito awe chini ya kanuni ya sheria. Mambo ya makubaliano chini ya matendo ya jinsi hii yangekuwa ya kufisha. Kwa kweli - Paulo anarudia katika kukutana na watatu; mitume walio wakuu (aya ya 6) - Mahojiano hayakumwongezea lolote Paulo. Hao watatu hawakuwa na mamlaka katika suala la Paulo na hawakumpa fundisho wala habari.Tofauti kabisa, ilikuwa ni Paulo aliyeeleza suala la watu wa Mataifa kukubalika bila matendo ya sheria; na kwa kuwa mafundisho ya Paulo yalikuwa na kibali cha Mungu ilikuwa dhahiri, na kama tena huo utumishi wa Paulo ulikuwa na matokeo mazuri miongoni mwa watu wa Mataifa kama Petro alivyokuwa kwa Wayahudi. Hao watatu wakampa mkono wa shirika. Mgawanyiko wa utendaji ulikubalika juu ya Paulo- kazi ikawa kwa Mataifa, wao miongoni mwa Wayahudi. Ila alishauriwa jambo moja la kwamba Paulo awakumbuke maskini. Hilo lilikuwa shauri la kufaa, kwa kuwa Paulo wakati huo alikuwa Yerusalemu kwa kusudi la jinsi hii. Kukutana na watu watano Yerusalemu, ambako kumetajwa katika waraka huu tu, na kwamba kama sehemu tu ya utetezi kwa utume wa Paulo, kwa kweli ulikuwa ni wa muhimu kuwahi kufanyika. Mapatano bayana yaliyoenea yanaonyesha roho nzuri ya unyoofu katika agizo la Mungu ambalo ilikuwa nguvu itembeayo kueneza Ukristo. Haukuwepo wivu mdogo; wala kundi la watu wenye mitazamo kama hii. (4) Hayakuwepo mafundisho ya Paulo yaliyopingana na ya mitume wakuu kama ilivyo leo watu wanavyodadisi walivyokubali kuwa ni kweli mawazo yenye matokeo yaliyo na uharibifu kuhusu historia ya kwanza ya Ukristo na uhalisi wa maandishi yaliyotolewa kwenye kizazi cha kwanza. Mapenzi ya Mungu yalitambuliwa na wote; neno lililosemwa kwa uaminifu lilifungua milango wazi kabisa na shughuli ya bure miongoni mwa watu wote. PAULO NA PETRO WAKIWA ANTIOKIA (2:11-21) Mkutano kati ya mitume wakuu wawili, ambao anaelezea Paulo,ulifanyika lini? Hauwezi kuyakinishwa na uhakika wa jambo lolote linalokaribia, na maneno yaliyodokeza yamevutwa kwa mtazamo ulioshikiliwa kuhusiana na wakati barua ya Wagalatia ilipoandikwa. Kama tukiiweka barua kabla ya safari ya pili ya kupeleka ujumbe kwa kawaida wazo linalofuata ni kwamba Petro alitembelea Antiokia wakati fulani wa kipindi kazi ilipoendelea kule ambayo Barnaba na Paulo waliishughulikia kama ilivyoandikwa katika Mdo. 14:27,28. Inaweza kuwa alipoachiliwa toka gerezani imeandikwa "mahali pengine" ambako Petro alikwenda (Mdo. 12:17) ilikuwa ni Antiokia. Juu ya wakati huo tunajua mambo yaliyokuwepo ambayo yametajwa katika Wagalatia 2. Paulo na Barnaba walikuwepo, na kipindi hicho watu toka Yersalemu walitembelea Antiokia. Katika Mdo.15:1 tunasoma "wakashuka watu waliotoka Uyahudi wakafundisha wale ndugu ya kwamba , Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamuwezi kuokoka", wakati Paulo alipowasema "watu kadha wa kadha waliotoka kwa Yakobo" ambao kwa ushawishi wao Petro na Barnaba wakafuata unafiki wao. Walakini inawezakuwa kwamba safari ya ndugu toka kwa Yakobo ilkuwa mapema zaidi kuliko Mdo.15:1. Uchochezi wa matukio ya wageni toka Uyahudi yalikuwa yamesumbua. Kabla ya wao kuja upatano kati ya Wayahudi na Mataifa waaminio ulitiwa mkazo zaidi kwa kuchanganyika bila sharti na watu wa Mataifa wakiongozwa na ndugu kama Petro na Barnaba. Walishiriki chakula kimoja na watu wa Mataifa, ukatambulika kwamba palikuwepo na uhuru kabisa toka kwenye torati ya Musa. Ndipo wageni wakafika na kueleza ulazima wa kutahiriwa ili kupata wokovu. Kwa kukosekana kushikilia kanuni, wageni wa Kiyahudi hawakukubali waongofu wa Mataifa kuwa Wakristo. (5) Kwa hiyo madai yalikuwa kwamba usikivu wa kale kwa Petro ukashinda uamuzi wake mzuri, akakoma kushiriki chakula cha kawaida na watu wa Mataifa. Kama Petro alipewa taarifa na wajumbe toka kwa Yakobo ya kuwa kifo cha Herodi kwa hukumu ya Mungu kiliondoa hatari aliyoikimbia, na kwamba alitakiwa Yerusalemu, tunaweza kumfikiria Petro kutokukubali ya kuwa hawezi kurudi Yerusalemu kama kwa ibada alikuwa amenajisika kutokana na kuwa pamoja na Mataifa. Kuiona kazi katika Yerusalemu itakuwa hatarini hivi, tunaweza kuwaza, aliacha kubishana na akakubaliana na walivyotaka.Tafsiri ya jinsi hii inaweza kuwa sahihi-ni nzuri zaidi, na labda ya haki zaidi, kwa Petro kuliko maelezo mengi. Lakini hata hivyo, tendo lake lilidhoofisha jambo la msingi wa Mungu anavyojishughulisha na watu. Wayahudi wengine wakafuata mfano wake, na hata Barnaba akachukuliwa na unafiki wao. Paulo akaona ya kwamba kazi nzima miongoni mwa Mataifa ilikuwa hatarini. Mazoea ya Petro kula kwa uhuru na watu wa Mataifa yalikuwa matokeo yenye akili ya imani iliyo kwa Kristo walishiiriki wote sawsawa, Wayahudi na Mataifa. Kurudia mtindo wa maisha ya kale ya Kiyahudi ilikuwa ni kukataa Injili ya kweli ya Kristo, nikudai tena ulazima kufuata sheria ya Musa kama sharti la wokovu. Tendo la Petro likawa na nguvu katika historia baadaye kwa nyongeza ya matokeo ya haraka ndani ya iklezia la Antiokia. Katika karne ya pili mfululizo wa mambo ulisababisha mabishano makali sana; na katika karne ya kumi na sita wazo la historia ya Kanisa la awali ambalo lilishawishi mno mitazamo inayoonyesha makosa iligeuza ukweli kwa kudhania ni kweli kuhitilafiana kati ya Paulo na Petro katika mitazamo iliyodumu. Namna ya utendaji wa Petro mbele ya Wayahudi ulivyoonekana ulipatana kabisa na Paulo: kupotoka kwake kulikuwa ni kwa muda mfupi tu, ulirejeshwa upatano pande zote mbili katika mafundisho na katika utu wake. Baadaye Petro anamtaja Paulo kuwa "ndugu mpendwa Paulo". Wote wawili Petro na Paulo walitambua ya kuwa kweli ya Injili ilikuwa yenye maana kubwa kuliko watu walioitangaza, na kosa kidogo katika kufanya lilikuwa jambo fulani la kujutia, na kuadibisha kwake ni sababu ya kushukuru sana. (6) Haja ya Kukaripia Wazo la Paulo linalopenya na lenye kutaka utii upasavyo kwa Injili likafanya kutoepuka kumpinga Petro. Hali ilivyo haikuruhusu kumshawishi asifanye hivyo kwa faragha: uhuru wa injili ulirukwa mbele za watu kwa mwenendo wa Petro na tendo la wazi wazi alilohitajika. "Walakini, nilipoona ya kuwa njia yao haiendi sawasawa na ile kweli ya injili, nalimwambia Kefa (Petro) mbele ya watu, Ikiwa wewe uliye Myahudi wafuata desturi za Mataifa, wala si za Wayahudi, kwanini unawashurutisha Mataifa kufuata desturi za Wayahudi?" (aya ya 14). Utetezi huu wa injili kwa Petro kama ulivyosimuliwa na Paulo unapita kwenye maana nyingine katika taarifa kwa Wagalatia. Bado unaendelea kueleza msimamo wa Paulo katika swali la tukio, lakini kwa namna ya simulizi katika barua ya wazo la Paulo, Petro ameachwa, yupo na Wagalatia akiwaeleza suala lake kwao. Mahali pasipo na kugeuka panaweza kusema: kuna mashauri ya kufanya mgawanyiko kwenye aya ya 15, aya ya16 na kati ya 18 na 19. Hakika ni kwamba kugeuka hutokea, na wakati jambo analoandika likiendelea na msemaji akiwa ni yule yule, wasikilizaji wamebadilika. Lakini ni ufunuo wa jinsi gani kwa taarifa hii ya mwanadamu Paulo! Hawezi kueleweka na awaye yote ambaye hajajaribu kufuata mkazo wake na maneno yanayo shauri kama anavyoeleza toka ndani kabisa ya fahamu za utu wake, uthibitisho wake kuhusu Kristo. Wala hapotezi uwezo wake wa fahamu kuwapa watu wazo lake, lakini limejazwa na hisia za kuona kwa kina. "Sisi", Paulo aliendelea kwa Petro - neno 'sisi' linamaanisha Petro na Paulo -"sisi tulio Wayahudi kwa asili wala si wakosaji (wenye dhambi) wa Mataifa..." (aya ya 15). Hapa ni Myahudi anayenena - Myahudi aliye na majivuno yote ya utaifa na juhudi ya dini ambayo ilionyesha wao kuwa bora - na sehemu zote mbili Myahudi anenaye ni Paulo mwanafunzi na rabi, na Petro aliyebutu kwa maneno lakini mwaminifu, wa kukumbushwa, bali mvuvi mwenye juhudi. Watu wa Mataifa walielimika kidogo zaidi pasipo sheria; walikuwa wakosaji. Wa mataifa hawakuwa na madai ya haki: pasipo Mungu na bila kuzuiwa na ushawishi wa sheria, maisha yao yote kwa usahihi tu yameelezewa mno katika barua ya Paulo kwa Warumi 1. Watu wa namna hii walipokuja kumfahamu Mtakatifu wa Israeli na haki ya sheria yake, ilikuwa dhahiri walikuwa ni wakosaji. (7) Lakini wote wawili Paulo na Petro walikuta kwamba nao vilevile walikuwa wakosaji mbele za Mungu; na hata kama waliepuka makosa makubwa zaidi ya watu wa Mataifa, walakini kwa elimu yao ya sheria waliupata mtazamo ulio wazi wa mwili ulivyo jaa dhambi na udhaifu wa binadamu mbele za Mungu. Ufahamu wao kwa dhambi haukuwa mdogo bali mkubwa zaidi ya watu wa mataifa. Ujuzi uliwafundisha ya kuwa mwanadamu haesabiwi haki kwa matendo ya sheria. Paulo alitoa maelezo kwa ukweli wote alipoeleza ya kuwa sheria ilipokuja maishani mwake akajua msukumo tofauti ndani yake ulio tayari kujiinua wenyewe. Msukumo huu anauita dhambi; akafahamu nguvu yake wakati vizuizi vya sheria alipovielewa. Dhambi ilihuika - ilikuwepo pale bali ililala, ikisubiri tu dai la sheria ya haki kuamshwa kwa nguvu ya mwili ambayo haitapungua hadi uhai utoweke. Jaribio la jinsi hii kwa mtu kumjua Mungu kuwa ni mkweli, litamwongoza kutambua ya kuwa matokeo ya mauti hayaepukiki. Kwa kusema wazi, Paulo anasema, "nami nikafa" (Rum.7:9). Ikiwa sheria ilikuwa na matokeo ya kuamsha ushindani na mwili ni wazi kwamba kuhesabiwa haki hakuwezi kuwa kwa sheria - kwa maana kuhesabiwa haki ni hukumu ya kuwa na haki, ni kujulisha ya kuwa mwanadamu ni mwenye haki. Kile ambacho sheria haikuepuka kufanya ilikuwa ni kumthibitishia mwanadamu kuwa ni mkosaji. Katika maisha ya Petro, Paulo na Wayahudi wote waaminio waliifikia nuru ya wokovu. Ingawa nuru iliweka wazi zaidi bila shaka mwili uliojaa dhambi, lakini hata hivyo ilionyesha njia ya uzima kwa Kristo Yesu. Kwa kumwamini mwanadamu alihesabiwa haki, alihesabiwa kuwa ni mwenye haki; kwa kuitika kwa imani kwa kile kilicho timizwa na Yesu Kristo, Mungu alisamehe dhambi zake huyo mtu. Kile ambacho mwanadamu hakuweza kwa sheria sasa anaweza kwa imani, anaweza kusimama mbele za Mungu akiwa ni binadamu aliyesamehewa na hivyo kuhesabiwa kuwa ni mwenye haki. Kuondolewa Mzigo Furaha ya kuondolewa mzigo wa sheria na uhuru wa kufurahisha katika Kristo waliona kwa majaribio mitume wote wawili. Wote wawili walimwamini Kristo: walipata raha kwake kwa kuthibitishiwa ya kwamba kuhesabiwa haki hakuwezi kupatikana toka mahali pengine hata kidogo. (8) Maandiko yenyewe yamesema kwa nguvu ya kufundisha: "Kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili awezaye kuhesabiwa haki". Daudi aliomba, "Wala usimhukumu mtumishi wako; maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki" (Zaburi 143:2). Zaburi ilikuwa sehemu madhubuti katika wazo la Paulo, maana katika Warumi 3 anafunga mtazamo wake kwa haja ya ulimwengu mzima ni rehema za Mungu kwa neno la mwisho hadi umasikini mbaya kabisa wa haki ya Yesu: "Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu. Kwa sababu hakuna mwenye mwili atakaye hesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa kwa njia ya sheria" (Rum.3:19,20). Ulikuwepo ubishi wenye hila nyingi wa kukabiliana nao Wayahudi wapinzani. Injili haikuja ulimwenguni katika kipindi cha ubovu wa akili, ijapokuwa ulikuwa wakati wa ufukara wa maadili. Myahudi na Mmataifa walipinga fundisho la Kikristo kwa mawazo ya kibinadamu. Hakuna udanganyifu wa dhambi ulioonyeshwa kwa uwazi zaidi kuliko kwa " kujaribu kufahamu" ambapo dhambi imesamehewa na kuendelea kusadiki huhesabiwa haki. "Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi" ilikuwa sababu ya kuleta ubishi wa ujuaji wa kuishi katika dhambi ambayo ilitaka kupewa jawabu la nguvu. "Hasha". Hivyo ni kujaribu kumfanya Kristo ndiye sababu ya dhambi. Ilikuwa ni kusema kwa kupotoa kuwa ikiwa injili ya Kristo ilimfanya mtu ajue dhambi zaidi, hivyo kwamba yeye mwenyewe alijiona kuwa mkosaji sana, basi inabidi Kristo awe ni mfanyizaji wa dhambi. Sababu inayoleta ubishi wenyewe imehukumiwa na imekanushwa kwa ukali: "Hasha". Desturi ya dhambi ni ya peke yake kwa kuwa inampofusha mkosaji asifahamu ubaya halisi wa dhambi. Dhambi inadanganya, kwa asili yake inabidi dhambi iwe mbalimbali. Katika aya ya 18, Paulo anaeleza kwa utu wake mwenyewe nafasi ya wengine Petro, Barnaba, na Wagalatia waliotenda kwa jinsi iyo hiyo. Anaweka kwa kutafuta hakika kwake mwenyewe yale ambayo kwakweli walikuwa wanafanya wengine. Haya inabidi yatambulike kwa kufahamu maneno ya Paulo; na pamoja na kuelewa kwake tunapata kujua ya kuwa tunamwacha Petro na Antiokia, yapo mbele ya tendo la kufanya hivyo Wagalatia. "Kama nikijenga tena au kama ni Petro au ni Barnaba au wewe ukijenga tena, mambo ambayo mimi au wewe tuliyoyabomoa, mimi nawewe tunaonyesha ya kuwa sisi wenyewe ni wakosaji" Walibomoa nini? (9) Walitupilia mbali wazo la kuwa uzima unaweza kupatikana kwa sheria - yaani, kwa matendo ya sheria waweza kuhesabiwa haki. Na sasa kurudi katika sheria ilikuwa ni kutaka kwao kuhesabiwa haki toka yale ambayo kuona kwao kote kulionyesha kuwa ni "huduma ya hukumu". Hii ilikuwa ni kuruka katika uso wa amri ya Mungu mwenyewe, na kusudi lake katika torati, na kwa sababu hiyo iliwafanya wao kuwa wavunja sheria. Kwa Majaribio Alivyoona Paulo Neno "maana" linaloanza katika aya ya 19 linaonyesha ya kuwa taarifa iliyoitangulia ni maelezo anayoonyesha kwa kuandika yale ambayo Paulo alimaanisha kwa maneno yake katika aya ya 18, "naonyesha yakuwa mimi mwenyewe ni mkosaji". Neno "maana linaingiza mashauri ya kipande cha maandiko ya maisha ya kiroho yaliyowahi kuandikwa mengi kupita yote: ndani yake mkazo wa juhudi ya mtume mwenyewe imefunuliwa, na kujiweka kwa ukamilifu kabisa chini ya Kristo kumeonyeshwa. Ni wachache waliomwelewa Kristo kama alivyofanya Paulo, kwa maana ya kina kabisa cha hali ya asili yake na uzuri akili yake vilikuwa sababu ya upinzani wake mkali na halafu msingi wa kujitoa kabisa kuwa mtumwa wa Kristo. Hakuna tena mfungwa maarufu aliyewahi kuonyesha maendeleo ya ushindi wa Mwana wa Mungu. Kufedheheshwa kwake kulikuwa kamili; kujiweka yeye kwa Kristo hakuwa na kiasi wala mipaka. Fikira yake halisi isiyokoma aliona ni kiasi gani alikosea kabisa jinsi alivyokuwa na kwa hiyo ilikuwa ni neema kubwa ya Mungu kwa Kristo iliyompa uzima na tumaini. "Maana mimi kwa njia ya sheria naliifia sheria ili nimwishie Mungu" (aya 19). Alivyoiona sheria kwa majaribio na bidii yake kamili na kujitoa kuifuata sheria akiwa ni Farisayo kulifanya ujuzi wake kuwa kamilifu- sheria ilionyesha ya kwamba haiwezi kutoa haki; na ya kuwa hiyo ilikuwa nje ya uwezo wake.Bali, sheria ilitoa hukumu ya kifo. Kuwa ndiyo chanzo cha kupata wokovu sheria haikufaa. Basi ikawa kwa sababu ilimhukumu kifo, au kwa kuwa kwa sheria hakuweza kupata uzima, Paulo aliifia sheria. Alipita toka hukumu yake juu yake- Paulo-alipoingia kumtumikia Kristo, akapata uhuru wa kufunguliwa toka katika milki yake ya matakwa yake. (10) Kama asemavyo katika barua yake kwa Warumi:"Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo.......Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao. Bali sasa tumefunguliwa katika torati,tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko"(7:4-6). Utumishi huo katika upya wa roho "unamwishia Mungu". Ushindani wa mauti na uzima waeleza uhusiano wake Paulo na torati na kwa Mungu. Alijitahidi kuishi chini ya torati nayo aliifia; alipita kwa mauti hiyo katika utumishi mpya ambao kwa kweli ulikuwa uzima mbele za Mungu. Mauti na uzima vimeelezwa baadaye kwa maneno yanayoleta mambo haya, na Paulo aliyeviona kwa kujaribu, katika uhusiano na Kristo. "Nimesulubiwa pamoja na Kristo: lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu(aya ya 20). Maneno yameelezwa katika mfano zaidi hivyo kwa watu wengi ambao maana ngumu ya mfano imepotea kwao. Kuna uzuri wa kudanganya kuhusu msalaba; maono, hisia yenye kuvuta kwa huruma ambayo imenyang'anya kusulubiwa ubaya wake na fedheha. Lakini Paulo alijua sana kusulubiwa maana yake nini kama namna ya kifo cha kutisha katika kueleza huruma juu yake. Vilevile alijua fedheha ambayo Myahudi alimuwazia mtu aliyetoa kadhia kuwa Masihi wake afikaye mwisho wa maisha yake jinsi hii. "Tendo la kuaibisha kwa msalaba" lilionewa uchungu uliokuwa umekaa ndani kwa wazo kabisa la kuwa mtu aliyepata mauti hivyo hawezi kudhaniwa hata kudogo kama Masihi wa Israeli; Msalaba ulikuwa ushahidi wa mwisho wa kuwa Yesu alikuwa laghai . Kwa karibu Paulo alikuwa pamoja na kundi la Israeli linaloongoza. Pengine alikuwa mwanachama wa baraza -Sanhedrini. Inafaa kudhania ya kuwa alikuwa Yerusalemu wakati wa kipindi fulani katika kipindi cha utumishi wa Kristo na alifahamu taarifa zilizotumwa ndani na wajumbe wa wakuu kuhusu Yesu. Hata kama hakuwa Yerusalemu hasa mwishoni mwa huduma hana budi alikuwa na mazoea na mwenendo wa mamlaka kwa Yesu. Alisikia kwa uthibitisho wa kuwa Yesu aliuawa. (11) Mtu ambaye baadaye aliangalia kuuawa kwa Stefano wakati mashahidi, katika kutojizuia mikono yao kutupa mawe, waliweka mavazi yao miguuni mwake, alisimama katika wazo akiangalia na idhini ya kufa kwa Yesu. Katika kuwaza naye, vilevile, alimfanyia mzaha, alimdhihaki, na kuona kwamba ulikuwa mwisho barabara. Yesu si Laghai Ndipo Paulo alijifunza, si kwa uzushi au kwa kuarifiwa, bali kwa kukutana hasa na Yesu ambaye hakuruhusu lifanyike kosa, ya kuwa mtu aliyemdhania alikuwa laghai alikuwa na hali ya kweli ni wa Mungu; mtu aliyewazia kuwa amekufa alikuwa hai. Nadharia yote ya maisha ya Paulo ambayo msingi wake ulikuwa juu ya wazo la kwamba Yesu alikufa, yenyewe ilifichika mavumbini alipokutana na Kristo aliyehai. Hakuwa amekufa; alikuwa hai. Hiyo ilimaanisha kuwa aunde mawazo yake kwa namna nyingine na maisha ya kuishi katika roho kwa kulingana na ukweli huo. Yesu hakuwa laghai: alikuwa mkweli: Paulo alikuwa amekosea katika nadharia yake kwa Yesu, basi tendo lake la kuwaudhi wafuasi wa Yesu ilikuwa ni kudumisha kosa ambalo lilifanywa na taifa katika kumkataa, na kumsulubisha Yesu. Paulo aliendeleza kusulubisha kwa kuwaua wafuasi wake, kwa maana Yesu aliyetukuzwa asingalimhukumu kwa kumuudhi yeye, "Kwa nini Waniudhi ?" Kwa huzuni Paulo alikosa, lakini alikuwa mwaminifu. Aliliona kosa, hakujaribu kulificha, ila alitumia mwenyewe kuiona kweli na kuishi ndani yake. Sasa hana budi kujua mapenzi ya Mungu yalivyokuwa katika kusulubiwa kwa Yesu, kwa maana hiyo mapenzi ya Mungu yalikuwa dhahiri, kwa kuwa Yesu alihesabiwa haki na Mungu kwa kumfufua katika wafu. Kama alivyosema kwa maneno yanayoanza katika barua hii ya Wagalatia: "Kristo alijitoa yeye mwenyewe kwa dhambi zetu... kulingana na mapenzi ya Mungu na Baba yetu." Paulo alipopita katika wazo lake kutoka kwa Petro hadi kwa Wagalatia, anafanya hivyo kwa kuwa vile alivyomwambia Petro alisema yaliyotangulia kwa Wagalatia. Anaeleza tena ujumbe aliowapa alipohubiri kwao mara ya kwanza. Hii walitambua mara moja: lakini ujumbe aliowapa haukuwa mwingine zaidi ya ujumbe aliousisitiza juu yao wakati Petro alistahili "kulaumiwa" na ujumbe ambao Petro alikiri kuwa kweli kwa kukubali karipio la Paulo. (12) Wakati ule, masimulizi ya kukutana hivi na Petro yanaonyesha mashindano ya maneno halisi juu ya utetezi wake Paulo. Hakupokea lolote toka kwa wengine: mitume walifahamu kutumwa na Mungu ya kuwa atahubiri kwa Mataifa: lakini alikuwa Petro aliyesita, na alikuwa Paulo aliyesimama imara katika kuilinda Injili ya kweli. Tunapo ona hivi, tunaweza kujaza maelezo ya ujumbe wa Paulo kwa Wagalatia "Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yao" (Gal.3:1), na sababu ya kifo chake ilielezwa. Barua ya kwa Warumi ni habari ya Paulo mwenyewe ya yale anayoeleza humo ndani kuwa "Injili yangu". Katika hiyo Injili inaonyesha kwa watu wote kufikia haki.Wote wametenda dhambi na kustahili mshahara wa dhambi, ambao ni mauti.Wote wanakufa kwa kuwa ni washirika wa ukoo ambao wao ni watoto wa "mtu mmoja" ambaye kwa njia yake dhambi iliingia ulimwenguni na mauti kwa dhambi, na mauti imewafikia watu wote, kwa kuwa wote wametenda dhambi.Paulo alionyesha kuwa Mungu amemweka Yesu kuthibitisha haki yake ya kwamba Mungu awe ni mwenye haki na mwenye kuwahesabia haki waaminio. Yesu aliithibitisha haki ya Mungu, kama mshiriki wa ukoo unaokumbwa na mauti, kwa hiari alipoutoa uhai wake. Katika mauti yake Yesu"alifia dhambi"kwa kuwa alikuwa chini ya mamlaka ya mauti kwa sababu dhambi iliweka taifa lote la wanadamu chini ya kifungo cha mauti. Kwa mapenzi ya kujitoa katika kusulubiwa Yesu alionyesha ya kuwa hali ya mwili ambamo dhambi imerithiwa, lakini mwili ambao kamwe hakuruhusu umshinde, haukufaa kuishi, aliutia barabara chini ya hukumu ya Mungu. Mkuu wa ulimwengu huu (dhambi) aliamuriwa na akahukumiwa katika mwili wa nyama ya dhambi ili kwamba awe dhabihu kwa dhambi, matoleo kwa dhambi. Yote yalifanyika ili Mungu aweze kutoa msingi sawasawa ambao juu yake anaweza kusamehe dhambi. Sadaka ya Dhambi Mahali ambapo sheria ilifanya hasira kwa kuwa ilimleta mtu chini ya adhabu ya kuvunja sheria, kusulubiwa kwa Kristo ilikuwa kuonyesha upendo wa Mungu kwa kutoa njia iliyo kwa ajili ya kutumia rehema yake."Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi"(Rum.5:8). (13) Vilevile ni kuonyesha upendo wa Kristo: kama Paulo asemavyo "Upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao" (2 Kor. 5:14,15).Lakini muunganiko kati ya mkosaji na Kristo-sadaka ya dhambi unapatikana kwa hiari bila kulazimishwa mwenye dhambi akijiunga na Mwokozi.Katika ubatizo mtu anazikwa na Kristo na kufufuka naye.Kwa tendo hilo utu wetu wa kale unasubiliwa na Kristo.Tendo hili la kuthibitisha limeonwa na Paulo kwa maelezo yote dhahiri ya kujiunga na Yesu msalabani. Badala ya kusimama na jamii ya watu wenye kutazama wakidhihaki, Paulo anavuka kwa msulubiwa .Anaweka tendo la kusulubiwa kwa kuwapo hapo, kwa kutoa uhai wake na kwa kuutia chini kwa njia hiyo. Anaungana na Kristo msalabani, na kufa naye. Kwa njia hii Paulo anaweka mambo makuu ya Mungu yaliyoonyeshwa katika kifo hicho cha Yesu. Ingawa hivyo,Yesu msulubiwa na aliyezikwa, alikuwa ni Yesu aliyefufuliwa katika maisha yasiyo na mwisho. Kama Paulo anavyoshiriki mauti yake, anashiriki maisha mapya kumwelekea Mungu aliyewezesha kwa Kristo. Hivyo anasema, "Ni hai": lakini mara moja, ili asije kuonekana kudai ubora wake wowote mwenyewe Paulo,anaongea lakini si mimi, bali Kristo yu hai ndani yangu. Hivyo haina maana kuwa Paulo utu wake alikoma kuwa hivyo, hiyo ana maana kuwa Paulo katika kuishi amewezeshwa kuishi maisha ambayo Kristo ameonekana kuishi katika maisha ya Paulo. Maana dhabihu ya Kristo sio tu ya kutolewa, sio njia pekee ya fadhili za Mungu kusamehe dhambi bali dhabihu ya Kristo ni nguvu ya kuendesha katika utakaso; kwa maneno ya Paulo: "Maisha ninayoishi sasa katika mwili naishi kwa imani ya Mwana wa Mungu, aliyenipenda akajitoa mwenyewe kwa ajili yangu." Paulo mwepesi kuona kwa akili anafahamu mno dhambi; Paulo mwenye kuwatesa wafuasi wa Kristo, aliona katika mauti ya Kristo ufunuo wa upendo wa Kristo kwa Paulo uyo huyo. Kusulubiwa hakukuwa mapatano tu ya elimu ya dini na sifa ya Mungu bali kiini halisi katika maisha ya Paulo mbele za Mungu. Aliona ndani yake neema yote ya Mungu. Kufuata njia nyingine ya kuishi ni bila kuridhika na njia hiyo ya Mungu, ni kutoridhika na neema ya Mungu. Hivyo njia aliyoichagua Mungu ni njia pekee inayoweza; maana ikiwa haki ilikuwa kwa njia nyingine, kwa torati, basi Kristo alikufa bure. (14) Chini ya utaratibu wa torati mauti haikuwa muhimu-na kama watu waligeukia sheria walitenda kana kwamba huo ulikuwa ukweli. Tunapo jaribu kufuata mfano wa maelezo dhahiri kwa kujithibitisha na Kristo aliyesulubiwa na kidokezo chake, tunaweza kufahamu kitisho cha ila ya Paulo kwa Kristo. Kitisho hicho kimeelezwa katika mano wa kurudi nyuma. Kama mtu aliyekwisha ijua kweli akageuka mbali, anaikana hiyo kweli na kwa matendo anamthibitisha Yesu kuwa laghai Myahudi aliyedhaniwa kuwa. Wakati huo matendo yake yanaweka tendo la Wayahudi kumsulubisha Yesu. Paulo anasema kwamba ikiwa mtu alikuwa shahidi bayana wa kweli halafu anaikataa,"wamsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao"(Ebra. 6:6).Kama kushiriki kusulubiwa Kristo ni kushiriki wokovu wake, kumsulubisha kunastahili maangamizi yajayo kwa wale waliomsulubisha na wote ambao wanasukumia mbali upendo wa Mungu na upendo wa Kristo; Kristo aliyeidharau aibu ya msalaba ili watu waweze kuwa hai. (15)