_____________________ WARAKA WA MTUME PAULO KWA WAGALATIA SURA MOJA The Letter of Paul to the Galatians - Chapter One _____________________ UTANGULIZI Wa barua ya Wagalatia umesema ya kwamba; "Hakuna msemo wa kale au wa siku hizi wa kulingana na waraka huu . Nguvu zote za roho ya Paulo zinang'aa katika kurasa zake chache. Mtazamo wake mpana wenye kung'aa, uhodari wakutoa hoja ya kusadikisha, kufahamu sana mambo yaliyotokea kinyume cha kutazamiwa, kila jambo lenye nguvu nyingi kupita yote katika kushindana kwa maneno, ukali katika mambo yenye udhalimu, aliye na bidii sana pamoja na huruma ya upendo, hapa inapatikana, imeunganishwa na kutoka nje katika mkondo mmoja tu, na kutengeneza kazi ya nguvu isiyoweza kupingwa na mtu. Huu waraka kwa nguvu mno mara kwa mara umewavuta watu, na katikati ya watu umegeuza historia ya binadamu. Luther alihamishwa na waraka huu kwa nguvu, na kwa kufundisha kwake alishambulia makosa na vitendo viovu vya kanisa katika siku zake. Aliandika na kuandika tena jumla ya fafanuzi zake juu ya waraka huu, na ujumbe wa mtume ulibadili watu kuelekea uhuru toka kwenye utumwa wa kufuata kanuni za matendo ya dini ambayo yalikuwa maovu na yenye kuchafua. Neno la Mungu li "hai na lina nguvu." Ni nguvu inayowaweka huru, lakini tu kama wakilisoma na ujumbe wake wakiutumia vizuri; ndipo linawaingiza katika " uhuru wa wana wa Mungu." Kwa kuwa maandishi ya Agano Jipya sio tu ni asili ya historia ya Ukristo wa siku za kwanza, wala chimbuko la aya za Biblia zinazoathibitisha mafunzo. Kuwekea mpaka kusudi la kujifunza kwa mojawapo ya vizuizi hivi ni kukosa shabaha sana, na labda ni kukosa kuelewa maana. Kwa uhakika wa mafungu ya maneno inabidi lisomwe kwa maneno yake yenyewe, nayo historia inabidi itwae sababu ya mafunzo na uzima na zaidi ya yote, tendo la Mungu katika kuwatuma wahubiri Injili na ujumbe wa uzima katika Mwana wa Mungu, aliyesulubiwa na kufufuka na kupaa. Zaidi ya miaka mingi mwandishi amejifunza waraka kwa Wagalatia. Mwendo wa mara tatu hotuba zilitolewa, katika darasa la watu wajifunzao Biblia, kwa watu wazima wafundishwao, katika kundi la watu wanaojifunza, na kwa kila kusudi la kuanza tena kujifunza kumeleta ufahamu wa kina. Mambo ambayo ni lazima yakumbukwe tena kwa nia ya kuandika iwazi hivi ni kukuza uthibitisho wa kwamba katika neno la Mungu tuna "utajiri usiohesabika," lakini ni ambao yatupasa tutake kujua. Kama msaada unaowezekana kwa wengine ili kuelewa kwa kipimo kingine waraka huu wa " ndugu yetu mpendwa Paulo, " mjumbe wa Bwana kwetu sisi watu wa Mataifa," ukubwa huu mpana umechapishwa. Mwezi Aprili, 1949- na JOHN CARTER DIBAJI Kama ni heri kutambua mambo yote yanayonenwa katika waraka wa Paulo haihitajiki nia juu ya maswali yanayohusu hivi na kwa nani barua aliandikiwa - walakini kuna matukio yaliyotajwa kwa kuandikwa na watu wenyewe aliokutana nao, yanayotakiwa kuchunguza maswali haya kama tunataka kufahamu maneno yote ya Paulo. Lakini mara nyingine maneno yake yanaingiza maelezo tofauti na panaweza kuwa na mitazamo miwili, yote miwili yawezekana lakini yote miwili yawezekana lakini yote miwili si sahihi. Hata hivyo wingine wataona hali ya kuwa sawa ushuhuda kwa upande mmoja, ambapo wengine wanachukuwa mtazamo kinyume. Mijadala ambayo imetokea kwa wanafunzi wenye akili, na kanuni za mafundisho, na ambayo mitazamo ya kushindana imekwisha elezewa, sababu ya kutosha inabidi ifikiwe kwa kuliacha jambo linalonenwa peke yake. Galatia ni Jimbo Basi, shida ni nini, katika kupambanua ni akina nani waliokuwa wapokeaji barua kwa Wagalatia? Katika eneo la kwanza tunaona ya kwamba Galatia haukuwa mji, kama vile Korintho, Thesalonika, Filipi, Kolosai au Roma. Lilikuwa jina la jimbo la nchi, mipaka ambayo ilikuwa kwa sharti la badiliko mara nyingi. Hivyo jina laweza kutumika katika maana ya kuwekewa mpaka makazi ya watu na vilevile kwa utawala, na kuangalia kazi za nchi. Wakati wa robo ya kwanza ya karne ya tatu kabla ya Kristo, wimbi la wahamiaji wavamizi wa kivita waliingia Asia ndogo, na kwa nusu karne walitembea na kuteka nyara wapendavyo. Waliwekewa mpaka na mfalme wa Pergamo katika eneo la nchi ambayo ilipewa jina la Galatia, katika sehemu ya kaskazini mwa uwanda wa juu mkubwa wa katikati ya Asia Ndogo, na miji mitatu ya Ancyre, Tavium na Pessinus ilikuwa mikuu kabisa ya kabila tatu ambazo ndani yake Wagalatia waligawanyika. Mnamo mwaka 189 k.k. walipigwa na jeshi la Warumi, lakini wakati wa vita vya kienyeji vya Kirumi mtawala mwenyeji, Amntasi, alipata jimbo lililoenea mbali ambalo Agusto alimruhu kulishika. Alipokufa Amntasi mnamo mwaka 25 k.k. Galatia ikawa mikononi mwa Warumi. Yalifanyika mabadiliko mengine katika mipaka na jimbo la Warumi la Galatia likaundwa. Minne ya Antiokia Listra, Derbe na Ikonia yote iliingizwa katika jimbo hili nayo yote ikapata umuhimu katika utaratibu wa ulinzi ikaendelezwa na Rumi katika nusu ya kwanza ya karne ya kwanza. Miji hii ilitengwa na jangwa kubwa toka Galatia ya kale iliyokuwa mbali kwa upande wa kaskazini, lakini miji yote minne ilijengwa kando ya barabara za Rumi utaratibu ambao ulimrahisishia Paulo kuweza kusafiri kuliko ambavyo ingeweza kuwa wakati wowote awali, au baadaye sana. (2) Watu wa miji hii minne, asema Rakhamu, katika kitabu chake juu ya Matendo ya Mitume, " walikuwa na jambo la pamoja watu wote, wote walikuwa wa jimbo la nchi ya Galatia . Kwa sababu ya uwenyeji huu wao ukiwa ni wa Frigia au wa Likaonia , Uyahudi au Uyunani, kwa kuzaliwa walikuwa wote ni Wagalatia. Katika hali ya kufanana, Trofimo aliyekuwa wa Efeso, alikuwa ni mtu wa Asia, na Aristarko wa Thesalonike alikuwa Mmakedonia. Miji yote ya Filipi, Thesalonike, na Beroya ilikuwa katika jimbo la Makedonia, na Paulo anapotaja makanisa haya pamoja, anayaita makanisa ya Makedonia na washirika wao Wamakedonia. Katika mfano uliosawa, hapana shaka, alipotaka kusema makanisa ya Antiokia na Ikonia, Listra na Derbe, kama mwili mmoja (kundi moja), akayaita makanisa ya Galatia, na alipowaandikia kwa pamoja aliwahutubia wasomaji wake kuwa Wagalatia. Zaidi ya karne mbili baadaye jimbo lilivunjika, juhudi ya kuwaunganisha watu wa kabila tofauti kwa kusudi la umoja uliobuniwa wa kisiasa uliachwa. Kujua mipaka kamili ya jimbo la Rumi la Galatia ikapotea na tangu hapo kwa mara nyingine jina likawekea mpaka kwa upande wa Kaskazini, kwa urahisi wasomaji wa waraka wa Paulo wakaangukia katika mtazamo wa kwamba wenyeji wa kaskazini mwa Galatia walikuwa ni wale ambao Paulo aliwaandikia. Sura ya Kaskazini mwa Galatia Huo mtazamo wa barua ya Paulo kwa Wagalatia ulikuwa jimbo la kale, hasa eneo la wahamiaji lilikuwa na mvuto juu ya tafsiri ya Matendo anavyosema yanayostahili Luka, akiwa mwana historia. Matendo ya Mitume haitaji mahali popote kuzuru kwa Paulo katika miji mitatu iliyo Kaskazini mwa Galatia, na kwa lugha tupu ya kukaza safari inaweza kuwa huko Galatia ikiwamo katika historia ya Luka. Katika safari ya kwanza ya Paulo, baada ya kupita katikati ya Kipro alivuka pande za nchi hadi bara ya Asia Ndogo.Mara moja Marko alirejea Yerusalemu, Paulo na Barnaba walipanda hadi kwenye uwanda mpana, wakafika Antioki ya Pisidia. Wakiisha fukuzwa hadi Ikonia toka huko kwa sababu ya mafanikio ya mahubiri yao, wakaenda hadi Ikonia. Hapa hatari zaidi zikawafanya waende hadi kwenye miji ya Likaonia, Listra na Derbe (Mdo. 13:14,51; 14:6). Antiokia ulipewa jina la "Pisidia" kwa kuwa ulijengwa kwenye mtelemko wa mlima unaotazama kuelekea chini kwenye mji wa Pisidia. Ulikuwa mji wa Frigia, wakati ulipoingizwa katika mkoa wa Frigia ulio wa jimbo la nchi ya Rumi la Galatia. Mji wa Ikonia ulikuwa kwenye mpaka wa Likaonia, lakini kwa usahihi umepambanuliwa na Luka toka miji ya Likaonia ya Listra na Derbe. Miji yote minne, kama tulivyosema, ilitiwa katika Galatia ya Rumi. (3) Katika safari ya pili, baada ya baraza lililokuwa Yerusalemu, Paulo na Sila waliitembelea miji ambayo makanisa yalijengwa; halafu Luka anasema: "Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia." Fungu la maneno katika sentensi lina maana nchi zote mbili ya "Frigia" na "Galatia ," zinahusika, hii kwa usahihi, inaelezwa eneo la Frigia ambalo kiutawala lilikuwa la Galatia. Kwa maneno ya Kirsopp Lake (Nyaraka za awali za Paulo), " Kwa kweli ni vigumu kuona wilaya nyingine maana yake ." Luka anaonyesha ya kwamba baada ya kuzuru katika miji hii mwendo wa pande za nchi ulikuwa wa moja kwa moja hadi bandari ya Troa. Walizuiwa kugeuka kulia au kushoto. Lakini sura ya nchi ya Galatia Kaskazini imelazimisha kupoteza safari ndefu hadi Kaskazini mwa Galatia na kugeuza nguvu ya asili ya maneno ya Paulo. Sura ya Nchi Kusini mwa Galatia Katika safari ya tatu Luka anaandika ya kwamba Paulo "alipita katika nchi ya Galatia ili kuimarisha wanafunzi wote". Tokea hapo alifuata barabara hadi Efeso (Mdo 18:23; 19:1). Kuangalia mara moja ramani kunaonyesha barabara za kifalme na mgawanyo wa kiutawala katika siku za Paulo imekuwa wazi tena hata lugha katika maana asili yoyote hairuhusu kutembelea Galatia kaskazini. Kumnukuu tena Kirsopp Lake: "Hivi maana ya mafungu ya maneno mawili katika Matendo ambamo ushahidi wa Galatia katika Matendo 18:23, Ikonio na Antiokia waonyesha kwa makanisa ya Derbe na Listra kama hayo yaliyozungukwa na Frigia na nchi ya Galatia katika 16:6. Hakuna chochote katika Matendo kinachotaka kuonyesha kanisa lingine lolote la 'Galatia ,' na nadharia zinazomfanya Paulo asafiri kuingia katikati ya Ufalme wa kale hazisaidii kwa tafsiri ya nguvu ya matendo, na kwa kumfanya Paulo achukue safari ndefu yenye hatari katika nchi zilizo na watu wachache, badala ya kufuata, kama inavyoelekea kuthibitisha tena kuwa, katika barabara kubwa na miji mikuu ya jamii ya watu wanaozungumza Kiyunani." Nyongeza ni kwamba katika kuandika baadaye, katika kitabu cha V cha kuhusu Mwanzo wa Ukristo, Lake hasemi kwa uwazi sana kama katika madondoo haya. Katika wazo la Galatia Kaskazini muda unaoweza kuwa wa awali zaidi wa kuandika barua kwa Wagalatia ulikuwa kati ya safari ya pili na ya tatu. Kwa desturi imewekwa karibu katika safari ya tatu. Safari ya kwanza ya Paulo wakati ule ilikuja baada ya baraza la Yerusalemu mahali alipopokea maagizo naye akayapatia makanisa. Inakuwa shida sana, ingawa wanafunzi wengi walio na kipaji wameona iliwalazimu kuihakikisha kazi, katika kupatana hii, na kujulisha Paulo utegemezi wake kwa mitume na maelezo ya ziara zake hadi Yerusalemu katika waraka. Hakuna shida inayozuka katika sura ya nchi Kusini mwa Galatia. Katika wazo la pili barua ya Galatia inaweza kuwa iliandikwa katika safari ya kwanza na ya pili. Kipeo katika Galatia wakati ule kinahusu mazingira yaleyale yaliyofanya baraza la Yerusalemu liitishwe. Ikiwa barua iliandikwa kipindi kile, Paulo anaweka ndani safari zake zote katika Yerusalemu kabla ya kuzuru Galatia; na hivi ni muhimu katika kusaidia kushindana maneno yake. (4) Tafsiri ya Wagalatia 1na 2 kwa uwazi unaofuata msingi wake ni juu ya mtazamo huu. Mazungumzo ya jambo mojamoja ya maana nyingi yamehusika katika mawazo ya ushindani yanaweza kutazamwa katika maisha ya uzee wa Paulo (Conybeare &Howson, Lewin n.k) na katika kazi nyingi ya uandishi wa Bwana Wm. Ramsay na wengine waliomfuata. Shauri lenye kushawishi la sura ya nchi Kusini mwa Galatia la Ramsay, linaonyesha kama linavyofanya la maandishi sahihi kabisa ya Luka katika maelezo yake yote ya mji na yanayohusu masharti ya wakaao mjini , sio tu yakawa jitihada ya wafuasi wengi, bali yameongeza katika kusoma marudio kwa uangalifu kwa kukadiria ambamo Luka amedumu kama mwana historia. Badala ya " hitilafu katika mashauri" katika historia yake, tunapata maelezo sahihi ya ushahidi wa kuona maeneo ya mipaka; tunamwona Paulo na wenziwe wakipita barabara kuu muhimu za karne ya kwanza na kusimamisha vinara vya taa katika miji mikuu muhimu toka ambako mishale ya nuru ilienea hadi maeneo ya mbali zaidi. Vilevile tunaona kuzuka upinzani wa kwanza toka kwa Wayahudi; na mapambano ya hasira, yaliyozuka kwa watu wa mataifa wakiisha pokelewa kama ndugu wafuasi na Wayahudi.Tunaona shitaka jepesi la kosa, na uthibitisho wa njia ya wokovu wa Mungu kwa Imani si kwa matendo ya sheria ; kwa neema ya Mungu na sio kwa vitendo vya mwanadamu kwa kuzuia majivuno ya mwanadamu ni kwa kuukuza utukufu wa rehema ya Mungu na Neema. BARUA KWA WAGALATIA - SEHEMU YA KWANZA DIBAJI MAAMKIZI (1:1-5) Maneno yanayoanza ya waraka huu yana maana kubwa sana, kwa muda kitambo kidogo ni ya salamu, tena moja kwa moja na kwa haraka yanaingiza jambo la kujadiliwa. Paulo alichukuwa Injili hadi kwa Wagalatia, yaani kama tunayoiamini, kwa wale waliounda makanisa ya Pisidia Antiokia, Listra, Derbe na Ikonia. Barnaba alikuwa mwenza wake, ni karibu hakika ya kwamba ugonjwa uliwapeleka katika nchi za juu na hivyo ikapelekea wamhubiri Kristo katika miji hiyo. Ujumbe wa Paulo na Barnaba ulipokelewa kwa furaha na wajumbe, walitazamwa kama wametumwa na Mungu. Katika kurudi hadi Siria Antiokia "huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kutimiza", walilikutanisha kanisa pamoja na kusimulia yote ambayo Mungu aliyofanya kwa mikono yao. "Mlango wa imani" ulifunguliwa kwa watu wa mataifa, nao ulikuwa wazi ya kuwa kazi iliyoanza huko ya kuhubiri kwa watu wa mataifa ilikuwa na uthibitisho wa Mungu. Kazi ya kutangaza habari njema lilipanuka polepole na kidogo kidogo: kwanza katika Yerusalemu na Uyahudi, kisha katika mji wa Samaria. (5) Maombi ya Kornelio, mtu wa mataifa mcha Mungu kwenye sinagogi, yalisikiwa na Mungu, naye Petro alitumia "funguo"aliyopewa na Yesu ili kufungua mlango wa maarifa ya kusudi la Mungu kwake. Lakini ikawa ni mji wa Antiokia mahali ambapo pakawa kituo cha kazi iliyoongezwa, kwanza kwa kuhubiri injili hapo, na ndipo katika mji ukawa ni nyumbani mwa shughuli kubwa ya kueneza ujumbe wa dini, na katika mji huu Roho ya Mungu liliwatenga Paulo na Barnaba kuwa wahubiri walioteuliwa. Maendeleo yote yalithibitisha mafanikio makubwa, yakawa sababu ya kufurahi na ukunjufu wa moyo. Lakini walikuwepo watu waliojiita wenyewe wafuasi wa Kristo walioona upanuzi wa kazi ya injili kwa kutoridhika nayo, si kwa sababu injili ilihubiriwa kwa watu wa mataifa, bali kwa kuwa katika mahubiri haya "msalaba wa Kristo" uliwekwa mbele kama msingi wa wokovu kwa kuondoa Torati ya Musa. Uliondolewa msingi kabisa wa Kiyahudi kwa kuwekwa kando, na pamoja mahali palipokuwa na haki ya Israeli. Hali hii ikawa haivumiliki na hatua zilichukuliwa kwa kuipinga kazi ya Paulo. Upinzani toka kwa Wayahudi Yaelekea kuwa wayahudi waliokuwa kwenye miji ya Galatia ambao Paulo aliwatembelea walileta habari hadi Yerusalemu za shughuli zake. Katika Antiokia ya Pisidia walichochea upinzani kwa wakuu, ambao walimtesa na kumfukuza Paulo; walifuata kwa karibu sana hatua zake hadi miji mingine ambako wahubiri injili walishambuliwa na kupigwa mawe. Katika kuzuru hadi Yerusalemu kwa ajili ya moja ya sikukuu watu hawa walitoa habari juu ya mahubiri haya mapya. Ni yakini yalikuwepo "madhehebu ya Mafarisayo" walioamini, nao watu hawa walisikia toka kwa mafarisayo wengine kazi ya Paulo, kwa uchokozi wao mkubwa na kujulisha hatari. Kwa hiyo walituma watu hadi Galatia ili kuwasisitiza waongofu wa mataifa ya kuwa hata ikiwa wamekuwa Wakristo inawapasa watairiwe. Wengine walitumwa katika ngome ya kazi mpya. Katika maneno ya Luka: "Wakashuka watu waliotoka Uyahudi (kwenda Antiokia) wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka (Mdo. 15:1). Tohara likiwa ni tokeo dogo, wapinzani wa Injili walitumia mbinu za ujanja. Walitoa kadhia ya kwamba kanuni moja haikuwa tu juu ya Torati ya Musa bali ilikuwa hata na msingi wa kale. Kwa kuwa Ibrahimu alipokea tohara nayo iliwekwa kuwa "Ishara" ya agano. Paulo aliona kwamba kuikubali maana moja ilikuwa nikukubali yote, kwa kuwa kama kutahiriwa ilikuwa muhimu. Mfumo mzima wa taratibu za ibada katika mambo ya mwili ulikuwa nao wa lazima vilevile, na wokovu ulikuwa ni kwa matendo ya mwili au sivyo kabisa. Alisema, "Kama mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia kitu." Katika Antiokia ya Siria Wayahudi walipingwa kwa nguvu. Paulo na Barnaba "walishindana na kuhojiana nao wongofu wa Paulo walidhoofishwa imani yao upesi. Ili kuiangusha kazi yake maadui wa Paulo iliwabidi wadhoofishe kidogo kidogo mamlaka yake. Walifanya hivi na matokeo yakawa yakuhuzunisha sana. (6) Hatujui taarifa zilimfikia vipi Paulo, lakini kama tumeonyesha kwa usahihi mpaka wa mahali na matukio yaliyoweka kwa uhusiano wa bila kosa, basi taarifa za ila katika Galatia zilimfikia wakati wa mashindano ya maneno katika Antiokia. Ilibidi hatua ichukuliwe mara moja, na barua ya kutumwa kwa Wagalatia ikaandikwa kwa kukabiliana na kazi au matendo ya waharibifu wa injili. Katika waraka Paulo amedhihirika katika mkazo wote wa mawazo yake, katika ujuzi wa maneno ya kushindana, katika wasiwasi wake kwa waongofu wake, na katika unyoofu wake mkuu na uaminifu kwa injili aliyokabidhiwa. Mamlaka ya Paulo Mamlaka yake kama mjumbe wa Kristo ilibidi isadikishwe, nayo kweli ya neno lake ya kuwa katika Kristo watu wamepatanishwa na Mungu na imani ilithibitishwa. Mambo haya mawili yamesemwa kwa nguvu katika maneno yanayoanza nayo ni ya maana katika waraka: "Paulo, mtume......wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu" (1:1,4). "Paulo, mtume (si mtume wa wanadamu, wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu;) na ndugu wote walio pamoja nami, kwa makanisa ya Galatia (1:1,2). Paulo, mtume - neno mtume maana yake mtu aliyetumwa, mjumbe, mpeleka maneno aliyeamriwa. Neno hili hasa limetumika kwa "mitume kumi na wawili wa Mwana kondoo" (Uf.21:14;Math.10:2), maana "Yesu aliwaita wanafunzi wake...ambao aliwaita mitume" (Luka 6:13). Lakini hili neno linatumika kwa upana. Ndugu walikochaguliwa na makanisa ya watu wa Mataifa kufuatana na Paulo na michango ya pesa kwa ajili ya Wayahudi walio Yerusalemu, wameitwa "mitume wa makanisa" (2Kor. 8:23), ingawa ukweli umebadilishwa kwa tafsiri "wajumbe". Walioteuliwa na makanisa. Kwa hiyo Epafrodito alikuwa "mpeleka habari" au "mtume kwa Wafilipi, akiwa ametumwa kumtembelea Paulo gerezani (Flp.2:25). Paulo na Barnaba wameitwa "mitume" katika Matendo 14:4,14, labda hasa kwa kuwa "walitumwa" na Roho Mtakatifu, "walitengwa" kwa ajili ya kazi kati ya watu wa mataifa. Agizo hili lililoamriwa na Mungu moja kwa moja lilimpa Paulo na Barnaba cheo kisichopingwa chenye mamlaka na uwajibikaji miongoni mwa makanisa ya wa mataifa . Lakini utume wa Paulo ulikuwa na msingi imara zaidi kuliko agizo walilopewa yeye na Barnaba kule Antiokia. Paulo alikuwa chombo kiteule: na kama alivyotambua baadaye ya kuwa "alitengwa tangu tumboni mwa mama yake", ingawa baadaye sana "aliitwa kwa neema ya Mungu" kuchukuwa neema hiyo kwa wengine hata sasa ametazamwa kama kuwa nje ya kazi yake maalum. Wakati mwanawe Mungu mwenyewe alikuwa akikua katika kijiji kule Galilaya akiongezeka katika kutambua kazi aliyotumwa na Mungu, kijana mwingine alikuwa anatayarishwa kuunganishwa na kazi hiyo, lakini bila kujua yote. (7) Kwa kweli matayarisho yalikamilika, kwa ukweli ulio kama uongo, ingawa katika juhudi yake kali ya kuiharibu imani ambayo ilikuwa kazi yake kuianzisha. Basi, huku akiwafuata "katika miji mingine" wafuasi wa Mnazareti, akakamatwa na Bwana wao ambaye alipatwa hivi, kama kadhia yao ilivyokuwa, kuwa ni kweli alifufuliwa katika wafu Bwana aliyethibitishwa na Mungu na si ulaghai Paulo alimdhania kuwa. Ushahidi wa Paulo katika ufufuo Tafsiri ya 2Kor. 5: 16 yaonekana kuwezekana kuwa Paulo alimjua Yesu katika kipindi cha utumishi wake. Mtu hawezi kumfikiria mtu kama Paulo, mwanafunzi aliyefundishwa na Gamalieli, mtu aliyekuwa na nafasi muhimu katika mabaraza ya taifa alipokuwa mwenye umri wa miaka thelathini, asijue uamsho na shauku ambayo nabii mpya aliileta. Hakuna budi aliwahi kutembelea Yerusalemu katika moja ya siku kuu kipindi cha miaka mitatu Yesu alipokuwa akihubiri. Ulikuwepo utambulisho wake mwenyewe wa kwamba mtu mwenye utukufu ambaye mwangaza wake ulimpofusha macho hakika alikuwa ni Yesu wa Nazareti. Huko kukutana na Yesu ilikuwa mamlaka ya mwisho ya utume wa Paulo, kwa maana wakati huu alichaguliwa kama chombo kiteule ili kuchukua jina la Kristo kwa watu wa mataifa. Wapinzani katika mji wa Korintho walipofanya mashaka juu ya msimamo kwake, aliongeza ili uwe ushahidi wa utume wake wa kukutana na Yesu: " Sikumwona Yesu Bwana wetu ? Ninyi si kazi yangu katika Bwana? " (1Kor.9: 1,2). Kwa sababu hii basi, Paulo hakuwa vilevile nyuma ya mtume mkuu, ingawa maadui wake walimwita kwa ufidhuli " mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake" (1Kor 15:8). Tangu kwanza ulifahamika kuwa kujidhihirisha kwa kazi ya utume katika maana ya mwanzo, ni kwamba mtu hana budi kushuhudia ufufuo (Luka 24:48 na Mdo. 1:8). Inabidi awe na maarifa yaliyonyooka ya ukweli wa msingi sana kwa mahubiri yao. Alama za kuonekana dhahiri kwa mtume ni zile za kumfahamu Kristo mfufuka; kumpokea kwa Roho, ya kweli iwe kwa mamlaka iliyotangazwa kwa wengine, kuwa na nguvu zenye miujiza na uwezo wa kugawa kwa wengine, na mamlaka kwa kulazimisha kuadibisha. Kwa hali zote Paulo alikuwa sawa na wale ambao pamoja wameitwa " Thenashara" (1Kor. 15:5). Tukio lilizuka miongoni mwa Wagalatia yakuwa Paulo hakuwa na udhihirisho wa kazi ya kuitwa mtume kama Petro na Yohana walivyokuwa; utume wake, jinsi moja kama alivyokuwa , ulikuwa wa pili nao aliupata. Huku kuvunjiwa heshima kumekabiliwa mara moja katika maneno yaliyo katika mabano katikati ya mstari wa 1. Hakuwa mtume aliyetumwa na mwanadamu, si hata wale Thenashara, wala na watu, kama Barnaba na Yakobo; wala binadamu hakuwa mshauri; na badiliko toka "mwanadamu" hadi "watu ," toka kundi la jamii hadi mtu mmoja, kunaongoza kwa mmoja toka ambako alipokea kazi ya mtume: "wala kutumwa na mwanadamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu." Ni kweli Yesu alikuwa ni mwanadamu, lakini alikuwa zaidi ya hivyo; alikuwa mwana wa Mungu ameonyeshwa hapa na Paulo akimwita Mungu " Baba"; naYesu Kristo, aliyemchagua Paulo, aliridhiwa na Mungu, kwa kuwa alifufuliwa kutoka kwa wafu. Maneno yana mkazo wenye nguvu wa kwamba alikuwa mtume kwa kuwekwa na Mungu mtakatifu. Ushahidi wake anasogeza mbele baadaye katika waraka anapokanusha visingizio vya uongo vilivyotungwa kuhusu Paulo. (8) Dibaji ya Haraka Ilikuwa desturi ya Paulo kuunganisha majina ya wengine na lake mwenyewe katika maelezo ya barua zake. Hapa amesimama akiitwa jina peke yake, kwa maana mkazo wa kadhia yake mwenyewe ya utume wake ulikuwa muhimu. Hata hivyo anaunga wengine ambao majina yao hayajatajwa na yeye mwenyewe katika hotuba "Ndugu wote walio pamoja nami". Ndani yake maneno yenyewe yanaeleweka pande mbili, ambayo yanaeleza sababu za maoni mengi yaliyofanywa kumhusu aliyekusudiwa nayo. Maelezo yamevutwa kwa mtazamo unaoweza kushikwa kuhusiana na mahali ambapo waraka uliandikiwa na ni akina nani watakuwa na Paulo muda huo. Ikiwa kidokezo ambacho kimekuwa tayari ya kwamba barua iliandikwa toka Antiokia wakati wa uchochezi uliosababishwa na Wayahudi wa Yerusalemu ni sahihi, basi maana ya awali ni kwamba fungu la maneno linataja kundi zima la kanisa la Antiokia. "na ndugu wote walio pamoja" na Paulo ni tofauti na waalimu waliokuwa wapinzani kule na Paulo na yeyote awezaye kufarijiana nao Ramsay anamnukuu na uthibitisho wa maneno ya Dr. Zockler, ambaye ameeleza maneno ya Paulo: "kundi zima la ndugu wa Kristo waliokuwa naye wakati ule (sio tu wasaidizi wake maarufu) wametajwa na Paulo kuwa ni wale wanaoungana naye katika kuwasalimia Wagalatia. Anafanya hivi ili kutoa mkazo kwa kile anachosema kwao. Ameandika kweli na mkono wake mwenyewe (6:11) lakini kwa jina la jumuiya kubwa nzima ya wakristo. Maonyo na maneno ya kuwafaa ambayo inabidi waandikiwe Wagalatia yanatoka kwenda katika kundi ambalo mamlaka yake haitaweza kutazamwa kwa wepesi. Kwa haraka sana Paulo anamalizia sentensi inayoanza: kwa makanisa yaliyo Galatia". Kutokuwepo kwa mafungu ya maneno yaliyofanana kama "kwa Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo" (1Thes. 1:1) AU "WALE WALIOTAKASWA KATIKA Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu" (1Kor. 1:2), yaangaliwe. Hakuna maelezo ya kusifu, hakuna kutoa shukurani, hakuna neno la sifa au upendo. Tunapokumbuka furaha ya jinsi gani mtume Paulo anaelezea shukurani zake za tumaini, imani na upendo wa waongofu wake ukali wa barua ya kwa Wagalatia inaonyesha kwa kina ni jinsi gani mtume Paulo aliona makosa na ila katika utaratibu wao, na ukubwa kiasi gani yalikuwa matokeo ya kubadilika imani yao. "Kutahiriwa" au "kutotahiriwa" kunaweza kuonekana vita inayoleta utata, lakini wanagusa mambo ya kina ambayo yana dhuru wokovu wa watu. Neema na iwe kwenu na Amani Walakini, mawazo ya Paulo kwa Wagalatia ni thabiti mno na hali ya juu. Daima akikumbuka utume wake - ya kwamba kwa njia yake injili ya Mungu iweze kuhubiriwa ulimwenguni kwa sababu hii haachi kuandika mbaraka ambao ni sehemu ya maamkizi katika siku za Paulo. (9) Lakini tengenezo lake lililofanywa na Paulo linatilia maana iliyojaa tele katika neno, kuliko kwa bahati na mara nyingi kwa kutoonyesha heshima inayostahili na kutoa salamu isiyoangalia wengine, ambalo kwa Kiyunani lilitolea salamu ya Kiyunani katika mitaa yoyote ya ulimwengu wa siku ya Paulo."Neema", kwa kutumia Paulo, anaelezea huruma na upendeleo wa Mungu, hasa upendeleo wa Mungu kwa watu wa mataifa. Siku zote Paulo alishika ajabu ambayo aliiona alipotambua ya kwamba kusudi la Mungu na neema yake ilijumuisha watu wa pande mbili watu wa Mataifa na Wayahudi, na zaidi alipojua ya kwamjba Mungu alimfanya yeye kuwa njia ya kupitishia rehema yake ijulikane kwa watu wa Mataifa. Neema inaweka baraka zote zilizofanywa kupatikana katika wema wa Mungu kwa kutoa wokovu kwa wanaume na wanawake wenye dhambi. Kigeugeu na kutokuwa na msimamo Wagalatia kuliwaonyesha wenyewe kwa muda; ujinga wao ulikuwa unakwenda kuwekwa wazi, lakini kwa sababu hiyo walihitaji "neema" yote zaidi. Katika neema imeongezwa "amani". Moja imepatikana katika Kiyunani, na nyingine katika desturi za Kiebrania. "Amani" (Shalom) ilikuwa salamu iliyotumiwa na Myahudi - labda mwangwi wa baraka ya ukuhani mkuu ulio katika Hesabu 6:23 - 26: "Bwana akubarikie .... Na kukupa amani". Ilitumiwa na Myahudi kwa namna ya mapatano kabisa siku kwa siku, kwa ujumla pasipo kufahamu uzuri na baraka yenye kupumzika. Yesu alipoinena amani yake ambayo atawaachia wafuasi wake, aliielezea haikuwa amani kama itolewayo na ulimwengu. Namna watu walivyosema "Amani" lilikuwa ombi halisi lililowazi ndani, yakiwa ni maneno tu yanayoanza na kufunga ambayo yatumika kwa mwanadamu alipomwamkia mwanadamu mwenziwe. Yesu alikuwa na amani ya kutoa, kwa upendo aliinunua kama tukifikiri maana yake yote ya neno. "Tukiisha hesabiwa haki itokayo katika imani, tuna amani na Mungu" (Rum. 5:1); kuwa na amani na Mungu kunaleta amani ndani ya moyo. Paulo anayakuza maneno haya ya salamu inayotumiwa na watu wote kwa usawa wao wa juu zaidi kwa kuwaongezea "zitokazo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo". Maneno yake ni maombi ya kwamba neema ya Mungu, ambayo ilifunuliwa katika mwana wake, iwe yao, na kuwa nayo waweze basi kujua amani. Kristo ni Dhabihu kwa ajili ya Dhambi Hii maana iliyokuzwa mara moja ipo dhahiri katika mwandamano, kwa kuwa Paulo ameeleza ya kwamba Bwana Yesu Kristo "alijitoa kwa ajili ya dhambi zetu, ili aweze kutuokoa toka katika ulimwengu huu mbaya wa sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu". Kwa kuongeza maneno haya katika salamu na kisha kuweka mpaka maana ya kusalimia katika hiyo ambayo ilitamkwa bila kujali na pasipo kuwaza, yalichukua thamani yote toka maneno yaliyoongezwa. (10) Walakini, maneno haya yana jambo la zaidi kuliko kuingiza au kutilia mbaraka wenye maana iliyojaa. Kwa unyoofu yanaonyesha juu ya matatizo katika makanisa ya Galatia. Neema ya Mungu lilikuwa jambo lililotolewa bure kwa kuwa halikuwa katika uwezo wa binadamu kulipata. Lakini wakati ikiwa ni ya bure, haikuchipuka toka tendo la upaji wa kuona wema mithili ya kuweza kusukuma watu katika mazoea ya ukarimu pasipo habari ya tabia nzuri au matokeo. Neema ya Mungu imewekwa katika namna inayopatana na tabia yake, na mambo ya uadilifu yaliyodumishwa, yameonyeshwa wazi katika kila hatua ya matendo ya Mungu, pamoja na kueleza kusudi la kuleta matokeo fulani yaliyotakiwa ndani na kwa watu. Bwana Yesu " alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu." Dhambi zetu ndio shida kubwa katika uhusiano wetu kwa Mungu. Hatuna uwezo wa kusema, " hebu zisahaulike ," kama watu wenye maono ya uzembe wanavyoweza kudhani itawezekana. Wala Mungu hawezi kusema, "basi tusiwaze tena kuhusu dhambi" - ila masharti fulani yakitekelezwa. Jaribio la watu wengi leo laweza kumtaka Mungu kwa maana "mjomba mkarimu" aliyejihusisha tu juu ya kutoa vitu hivyo ambavyo watu wanataka. Hii ni alama yenye fikra fupi zinazopita katika mafundisho ya dini za siku hizi. Hata mahali palipo na juhudi nyingine katika kueleza kazi ya Yesu kwa kujitoa kuwa dhabihu nafsi yake, idadi inayoongezeka ya waandishi wanaopunguza uzito wa mauti yake hadi aina ya mfia dinishujaa aliyewekwa mbele kwa kuamsha watu katika kujitenga kabisa na dhambi na kuwataka watu waifuate haki. Lakini inakuwa kazi ya bure, katika kujaribu kuelewa ni jinsi gani kazi ya Yesu imehusika kwa dhambi zetu na wokovu wetu, ila tukichukua maelezo ya maandiko, kwa kuwa ni kwa njia hiyo peke yake tunaweza kujua nia ya Mungu. Mawazo ya wanadamu hayatatupeleka popote; ufunuo wa Mungu utatuwezesha kufahamu tabia ya Mungu iliyofunuliwa katika dhabihu ya mwanae. Msalaba unaoondoa kuamini kuhesabiwa haki kwa matendo ya sheria Yesu "alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu". Kusema hivyo, Paulo analeta kutazama uhakika wa mambo yenye historia yaliyounganika na kifo cha Kristo kama kulivyohubiriwa kwao Wagalatia. Ingawa si shahidi wa kusulubiwa, Paulo kwa maelezo dhahiri alitambua ya kuwa msalabani Yesu alifanya tendo ambalo halikuwa na kikomo cha faida kwake Paulo mwenyewe. Kufahamu maana yake, aliuona ujinga wake mwenyewe na kujitahidi kwa ajili ya kupata haki yenye sifa njema kwa kuishika sheria, hakika kabisa ya Mungu kumtoa mwana hivyo kwa kufa, lilikuwa jambo lisilowathibitishia msimamo wa Wayahudi wa kujaribu kupata kupendelewa na Mungu kwa kuishika sheria. Kwa hiyo, Paulo akawa ameifia torati kwa kumwishia Mungu; alisulubiwa na Kristo ili aweze kuishi "kwa imani iliyo kwa mwana wa Mungu, aliyenipenda na kujitoa nafsi yake kwa ajili yangu" (Gal. 2:20). (11) Fungu la maneno " alijitoa nafsi yake" linaweza katika maana ya mstari mwingine kuwa linafahamika kuwili: mtu anaweza kutumia nguvu zake katika kumsaidia mwingine hivyo ni kujitoa nafsi yake: lakini katika matumizi ya Paulo, kama ilivyo bayana kwa maana ya maneno yaliyonukuliwa, yanakuwa na maana ya kwamba kwa hiari bila kulazimishwa Yesu aliutoa uhai wake kusulubiwa. "Alijitoa nafsi yake." Paulo alifahamu kabisa kwa mawazo ya ndani yake sifa ya dhabihu ya Bwana kwa ajili ya dhambi. Wakati anasimulia dhabihu aliyojitoa Bwana kwa mapenzi ya Mungu, na kwa haki ya Mungu, kwa wakati anaelezea kwa maneno yasiyo na kina hasa, hata hivyo siku zote anafahamu ya kuwa kubeba msalaba ilikuwa ni kutoa uhai wa mtu kweli sababu zake kwa kweli ziliunganika na utakatifu wa Mungu, na kwa ajili ya "dhambi zetu" makosa yetu", "kuvunja sheria kwetu," na "maovu yetu". Lakini kwa kutoa sababu za utaratibu waMungu kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu , kamwe Pauloi hakupoteza kuona hili lilihusisha nini kwa Yesu mwenyewe, nakujitoa Yesu mwenyewe inaonyeshwa kazi kubwa aliyotwishwa. Aliye "nipenda mimi"; "Upendo wa Kristo unanibiidisha ;" "Kristo alikufa kwa ajili ya waovu";"Ni nani atayewahukumia adhabu?" Kristo Yesu ndiye aliyekufa?" "Ni nani atakayekutenga na upendo wa Kristo? Msemo huu unaelezea hisia zake na tendo lake, linaeleweka zaidi tunapokumbuka ya kuwa upendo wa Kristo nyuma yake yamefuata mateso; "Aliustahimili msalaba akaidharau aibu;" Yeye mwenyewe aliteseka ;" "alijifunza kutii kwa mateso yaliyompata". Haya lakini ni maelezo ya mifano ya msemo wa mtume inayoonyesha ufahamu wake imara kwa mwelekeo wake wa kazi ya Yesu: na ukiwa ni ushahidi kwao utatuzuia katika kutotazama maana ya utajiri na ya mawazo kwa maneno mepesi: " alijitoa nafsi yake." Msamaha na Mapatano "Bwana wetu Yesu Kristo ......alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu." Msamaha wa dhambi zetu unaopatikana kwa Kristo ulikuwa ni ujumbe ulio mstari wa mbele kwa mitume. "Naliwatolea ninyi hapo mwanzo," Paulo anasema kwa Wakorintho, "ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, yanenavyo maandiko" (1Kor. 15:3). Tunaona maana muhimu ambayo inashikana na taarifa ya Paulo ya kuwa ujumbe wake ulikuwa ni ule alipokea mwenyewe na moja kwa moja anaposema: "mambo yote yatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; yaani, alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu" (2 Kor.5:18-20). (12) Mungu alimkabidhi huduma hii Paulo kati ya watu wa mataifa na juu ya msingi wa matendo ya Mungu katika Kristo watu waliombwa wapatanishwe na Mungu. Mapatano yalithibitishwa kwa sababu dhambi hazikuhesabiwa; kwa Kristo dhambi zilisamehewa. Katika kuelezea msamaha huu na njia ambayo imewezeshwa, Paulo na mitume wengine wanatumia eneo pana kwa maneno ya hotuba mbalimbali. Maelezo haya tofauti yalikuwa mazuri kwa kazi iliyowekwa tayari ya sheria ya Mungu kama mpango wa kanuni ya kuwafunza Israeli. Sheria ya utaratibu wa kanuni hizo ulitumia maelezo mapana katika kuelezea matoleo mbalimbali yaliyoamriwa eneo pana kabisa la maneno katika maungano yaliyotakiwa. Matoleo yalikuwa kwa ajili ya dhambi na kukosa; katika siku ya upatanisho kuhani mkuu aliungama juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kisha alichukuliwa hadi jangwani, maovu, makosa na dhambi za watu. Basi Wayahudi waliyazoea maneno ambayo wanaweza kutoa maelezo ya matendo yaliyokuwa kinyume na sheria ya Mungu. Utaratibu wa kanuni, ukiwa ni mfano na sehemu ya maandalio ya kuja kwa Kristo, kwa ulazima ulitoa mfano wa maelezo ya maneno ambayo dhabihu ya Kristo ilielezewa. Kwa kutambua jambo hili yatupasa halitoi habari za ukweli halisi Yesu alipoutumia. Maneno "Damu" Kazi ya Yesu imeelezwa katika maneno ya sheria kwa sababu torati ilitolewa kuwafunza watu wa Mungu kuhusu mambo yanayoongoza uhusiano wa mwanadamu katika mambo ya Mungu ambayo hayana budi yaeleweke kama sharti kwa mwanadamu kurudia kupendwa na Mungu. Hii imeelezwa kwa mifano ya neno "damu". Damu ya wanyama ilionyesha mfano kwa njia nyingine katika cheo cha kazi za sheria; kwa kumweka wakfu kuhani mkuu, na katika siku ya upatanisho, ni kati ya mbili muhimu zaidi. Lakini sheria iliwaagiza Israeli ya kuwa damu isiliwe kwa kuwa "uhai wa nyama (mwili) umo katika damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu ,"(Law.17:11).Damu ilikuwa kijito cha uhai, na katika utaratibu wa matumizi ya kanuni ikiwa alama ya uhai uliotolewa. Wakati Yesu anenapo basi "damu yangu" na "damu ya Kristo" wanatumia utaratibu wa maneno ya sheria na maana ya kanuni zake kwa kueleza kutoa uhai wa Kristo. Ukweli wenyewe ni kwamba damu ya Kristo ilimwagwa katika hiyo mikono na miguu na ubavu ulipochomwa: lakini ukweli wa muhimu ni kwamba uhai ulitolewa hii ni bayana tunapoona kwamba damu yake halisi haikuchukuliwa katika patakatifu pa patakatifu damu iliponyunyizwa juu ya kiti cha rehema na kuhani mkuu katika siku ya upatanisho. Damu yake ikiwa maji mekundu, ilipata mikono yake ikadondoka juu ya udongo mahali aliposulubiwa. Haikuwa na muujiza wenye thamani, jinsi moja kama Wakatoliki wanavyo ifungamanisha nayo. Jambo lingine lililokuwa kweli kabisa, lakini lilifanyika kwa kifo cha Kristo, jambo la kuhani mkuu alipoingia patakatifu zaidi lilionyesha tukio lililokuja. Ingawa hivyo ukweli huo ulielezwa na Paulo kwa maneno yaliyochukuliwa katika mfano: "kwa damu yake mwenyewe aliingia mara moja tu katika patakatifu, akisha kupata ukombozi wa milele", na kwa maneno mengine yanayotangaza mfano anasema: "kwa sababu Kristo hakuingia katika patakatifu palipofanyika kwa mikono, ndio mfano wa patakatifu halisi, bali aliingia mbinguni hasa, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu" (Ebr. 9:12,24). Tunaweza kusema tena jambo hili: katika utaratibu ulio kivuli kuhani mkuu aliingia patakatifu pa patakatifu na damu ilimwagwa; (13) katika jambo halisi lilionyesha jambo lililokuja, Yesu alikwenda mbele za Mungu Baba kwa damu -yaani, kwa kifo chake cha hiari. Hata hivyo tumesema ukweli tu na kuacha bila kubainisha jambo la uadilifu ambalo juu yake jambo la hakika liliwekwa. Maneno yanayolingana Katika kurejea mambo ambayo lazima yakumbukwe kwanza ya kuwa ilikuwa ni "kwa ajili ya dhambi zetu" katika usemi wa Paulo ya kwambaYesu alijitoa nafsi yake, twaweza kujua maneno yafuatayo ambayo ni yenye thamani kwa kulinganisha "alitolewa kwa ajili ya makosa yetu" (Rum.4:25); "alitoa dhabihu moja kwa ajili ya dhambi" (Ebr. 10:12); "Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi" (1Pet. 3:18); "Kristo naye alitolewa sadaka mara moja azichukue dhambi za watu wengi" (Ebr.9:28); "Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti" (1Pet. 2:24); " Ndivyo ilivyoandikwa kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu: na kwamba mataifa yote yatahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu" (Lk. 24:46, 47); ".....kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi" (Mdo. 10:43); "Kwa hiyo mnahubiriwa msamaha wa dhambi" (Mdo.13:38); "katika yeye huyo, kwa damu yake tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake" (Efe. 1:6,7 tazama vilevile Kol 1:13,14); inafaa kuhesabia ya kwamba waliokombolewa watamke utukufu kwa mwana kondoo: "Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake na kutufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una yeye hata milele na milele" (Ufu. 1:5,6). Msamaha wa dhambi ni wa muhimu, au hakuna awezaye kuokolewa: lakini zaidi ya hivyo ni lazima, kwa kuwa msamaha unajieleza upande mmoja tu wa kazi ya ukombozi wa Yesu. Kwa hiyo Paulo anaongeza kusema kwamba "Alijitoa nafsi yake .... Ili atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu". Hapa "dunia " ni katika kipindi tunachoishi, cha mpito na uovu - dhambi ndiye mtawala. Kipindi kingine cha enzi kimenenwa - hicho kipindi cha ufufuo wa wafu ambacho watu wanaweza kufikia kama wakionekana wamestahili. Watu watengenezao maisha yao kufuata mifano na matendo ya watu wanaoishi wakati huu ambao hawaongozwi na sheria ya Mungu bali kwa nia zao wenyewe, hawastahili kufikia. Hatua ya kwanza katika kujinasua toka mpangilio uliopo sasa ni kuelewa ni mbovu: kwamba ulimwengu upo kwa yule mwovu. Kutambua huku huja kama sehemu ya kufahamu mwanadamu alivyo ni mwenye dhambi, kama anavyojiona mwenyewe, kufahamu kweli ya Mungu kunamleta mtu mahali palipokusudiwa. Yeye mwenyewe anajiona kuwa sehemu ya dunia inayotawaliwa na dhambi: mwenyewe anahisi kukamata kwake; lakini hana nguvu za kujiokoa mwenyewe. Ndipo anakuta kwamba mtu ambaye umo msamaha vile vile ndiye mwenye kumweka huru, aweza sasa "kumwokoa" mfungwa katika nguvu ambayo inamshikilia na kuwa mtumwa. Hajatolewa toka katika dunia - mazingira ya kimaumbile, bali walindwe katika uovu (Yn.17:15), na sala yake ya kila siku inakuwa "Tuokoe katika uovu". Ikiwa Paulo anawaza fungu la maneno yenye maana dhahiri katika sala ya Bwana yaonekana kwa kweli dhahiri anapobainisha kazi ya Kristo tena katika msamaha kama ukombozi toka "ulimwengu- dunia hii mbovu ya sasa". (14) Mapenzi ya Mungu Fungu moja zaidi la maneno katika aya zinazotangulia linahitajika kuangaliwa. Paulo anaeleza ya kwamba Yesu alijitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu ili atuokoe katika dunia hii mbovu ya sasa "kulingana na mapenzi ya Mungu na Baba yetu". Mapenzi ya Mungu ndiyo sababu ya kwanza ya ukombozi: kwa sababu ya mapenzi yake ilikuwa ni muhimu kwa Yesu kujitoa nafsi yake ili dhambi zetu ziweze kusamehewa na kukomboledwa toka matokeo ya uovu. Hakika ya kwamba yote ambayo yamefanywa kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu ni ya Mungu yameelezewa sshemu nyingi katika maandishi ya mitume: "Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na Ukombozi," (1WAKORINTHO 1:30). Katika Zaburi 40 Daudi alionyesha kwamba dhabihu za wanyama za kila aina hazikutosha kutimiza ukombozi. Akinena katika, roho wa Kristo aliyekuwa ndani yake" (1Pet. 1:11), na kwa hiyo akitumia maneno ambayo yaweza tu kutoka vema katika kinywa chake Kristo mwenyewe, alieleza ya kuwa Mungu "hakutaka" matoleo ya wanyama, Kristo akaja kutimiza mapenzi ya Mungu. "Ndipo niliposema, Tazama, nimekuja, katika gombo la chuo nimeandikiwa, kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu". Ni jinsi gani haiwezekani kwa Daudi kusema mwenyewe nafsi yake kuwa mtii kwa Mungu aliandikwa katika gombo la kitabu cha Mungu! Wakati alikuwa mtu aliyeupendeza moyo wa Mungu, kama Mungu yeye mwenye alivyoshuhudia, lakini yalikuwepo matendo katika maisha yake yaliyotia doa taarifa hii. Kwa maana ya maneno makubwa ya Zaburi, kuja kwa Daudi kusingeweza kusemwa ilikuwa ni "kufanya mapenzi ya Mungu". Tena, asingeweza kusemwa ya kwamba ndiye amesemwa katika unabii kwenye ufunuo wote wa Mungu na kusudi lake. Ni kwa Masihi pekee lugha ya jinsi hii yaweza kutimiwa. Lakini matumizi haya kwa Masihi, yanayotoka katika msemo wenyewe, kwa kuonyesha yamethibitishwa na Paulo anapotumia mistari iliyo katika Waebrania 10:5-9, ambapo Paulo anaongeza, "katika mapenzi hayo (ya Mungu) mpate utakaso, kwa kutolewa mwili wa Yesu Kristo mara moja tu kwa ajili ya wote" (mstari wa 10). Lakini mapenzi ya Mungu yanapanuka kupita kazi yake Yesu - kwani yanashika matokeo yote ya hiyo kazi juu ya watu waaminio. Paulo anawasema Waefeso ya kuwa "alitangulia kutuchagua ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawa sawa na uradhi wa mapenzi yake" (Efe. 1:5). "akiisha tujulisha siri ya mapenzi yake" (mstari wa 9), na kwa sababu hii Mungu " hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake.: nasi katika huyo tupate kuwa sifa ya utukufu wake, sisi ambao kwanza tumemtumainia Kristo" (mstari wa 11 na 12). Wakati hivi Paulo akiwa hapotezi kuona tendo la Mungu katika Kristo na mapenzi makuu ambayo yalihitaji dhabihu ya Yesu, ilikuwepo sababu mahususi ya kusema kwa nguvu katika hii mistari inayoanza ya barua ya Wagalatia, Yesu alijitoa nafsi yake kulingana na mapenzi ya Mungu. Wazo ni la muhimu katika uthibitisho wa injili ya Paulo katika upinzani wa mafundisho ya Wayahudi. (15) Mungu Baba yetu Kabla ya kukusanya mawazo ya mistari inayoanza inayotaka sababu ya kuthibitisha shauri la uwongo katika barua yote iliyowekwa wazi, yatupasa tujue kwamba Mungu ni "Baba yetu". Baadaye katika waraka Paulo anaonyesha ya kuwa kuiamini injili, aaminiye anaingizwa katika nafasi ya kuitwa mwana: mtu ambaye ni mtunza sheria ni mtumwa. Mungu, akiwa ni Mwenyezi atiaye sheria; lakini UBABA wake haujafunuliwa kwa sheria. Palikuwepo na sheria mbili za kuadhibisha katika huduma iliyopita. Ya kwanza ilikuwa katika Edeni mahali ilipoelezwa matokeo ya uasi itakuwa mauti. Hakuna mwanadamu mwingine aliyesimama kweli katika nafasi moja kama Adamu katika Edeni, kwa maana uasi wa Adamu sio tu ulimdhuru yeye mwenyewe bali uzao wake wote. Mauti yalimpata Adamu mwishoni mwa miaka 930; lakini baada ya kosa lile, kwa miaka yote hiyo alifanya kazi kwa jasho la uso ili kupata chakula chake, naye akajua huzuni na uchungu, udhaifu na hali ya kufa. Paulo anathibitisha ya kwamba "mauti yamewafikia watu wote" kwa dhambi ya Adamu (Rum. 5:12). Msemo una mkazo, kama ilivyo tena taarifa: "kwa mtu mmoja mauti ilikuja", na hii mauti ni dhahiri inamaliza uhai wa sasa, maana Paulo anaongeza kusema; "tena kwa mtu mmoja kiama ya wafu ilikuja". Kristo alifufuliwa katika wafu ni limbuko aliyefufuliwa katika mauti inayotawala katika dhambi ya Adamu. Nyingine yenye kutoa adhabu ilikuwa orodha ya kawaida ya maisha iliyokuwa ya Musa, iliyokuwa na sura moja fulani katika mapatano, ambapo kuvunja mapatano ilibidi kuadhibiwa na mauti. Kwa kuwa kanuni ya sheria ya Musa ulikuwa ni mwongozo wa maisha uliotolewa kama sehemu ya muhimu ya agano ambalo kila Mwisraeli alikubali kutii, kushindwa kutii sehemu iwayo yote laana ya sheria ililetwa juu ya mkosaji. Wagalatia walivutwa katika kukubali kuwekwa kwa kanuni hii ya sheria kama sharti la kupata wokovu; walikuwa wanapokea itakayotoa laana na si baraka; na kufanya hivi walikuwa wanaanguka toka hali ya kuwa "wana" hadi kuwa "watumwa". Katika aya hizi zinazoanza, wakati ule, Paulo amesema kwa nguvu kama juu ya wasingiziaji wake ya kwamba utume haukuwa wa wanadamu bali kwa Yesu aliyefufuka na Mungu Baba. Mamlaka yake ina kibali cha juu sana. injili aliyofundisha, ambayo Wagalatia waliipokea toka kwake, ilikuwa habari njema ya msamaha wa dhambi kwa njia ya dhabihu ya Kristo na ya kuepuka katika ulimwengu mbaya. Injili ilikuwa onyesho la njia ya wokovu wa Mungu, kwa neema ya Mungu na si kwa sifa njema ya mwanadamu. Ikiwa dhabihu ya Yesu ilikuwa katika mapenzi ya Mungu wakati ule, dhabihu hiyo ilikuwa ni ya muhimu kwa wokovu. Haja isiyo ya haki kwa Wayahudi ya masharti mengine ilidokeza ya kwamba utaratibu alioufanya Mungu katika kipawa cha mwana wake na kwa mwana huyo kujitoa mwenyewe, haikutosha kwa ajili ya ukombozi wao. Uhakika kabisa wa kwamba Mungu hakumwachilia mwanae mwenyewe ili watu waweze kuwa na uzima wenyewe ni mwisho mara moja kwa wote wazo la kwamba wazao wa Adamu wanaweza kupata uzima wa milele kwa kutunza Torati ya Musa au mpango mwingine wa kanuni unaotakiwa kwa sheria. Injili iliwaingiza watu katika uhusiano wa Mungu kwa njia ya mwanawe ambapo nao vivyo walitambulika kuwa wana wa Mungu, na kuweza kumwita Mungu kuwa ni Baba. (16) Wapinzani wa Paulo walimshambulia kwa maneno ya kwamba alikuwa ni mjumbe aliyetumwa na wale Thenashara, na kwa nyongeza injili aliyopewa ilikuwa imepotoshwa. Kwa wale Thenashara, walisema, walichaguliwa na Yesu lakini Paulo alikuwa amekuja karibuni; na mamlaka yake haikuwa ya kwanza bali alipata. Waliompinga walieleza ya kwamba waaminio inawalazimu kutahiriwa ili wawe washirika wa "jamii ya Israeli na kuwa watu wa nyumbani mwa Mungu". Paulo aliona ya kuwa kuikubali tohara kuwa ya muhimu na sharti la kupata wokovu kulihusisha kutunza sheria yote pia. Torati haikuleta neema wala amani, msamaha au kuitwa wana. Ilileta utumwa na si ukombozi. Mashauri yaliyoonyeshwa hivi katika aya zinazoanza yameelezewa katika barua. Ukweli wa historia una Paulo. Alimwona Kristo; alijua Yesu alifufuliwa katika wafu; yeye mwenyewe alijua neema na amani aliyoomba kwa ajili ya wasomaji wake; alijua kwamba ukweli wa historia ya Yesu ulikuwa unafunua mapenzi ya Mungu kwa ajili ya msamaha wa dhambi za watu; na kwa hiyo "utukufu una yeye milele na milele" (mstari wa 5) SEHEMU YA PILI UTETEZI WA PAULO KWA UTUME WAKE INJILI AMBAYO HAIWEZI KUVUMULIWA (1:6-9) Utaratibu wa kawaida wa kuandika barua katika karne ya kwanza ulianza na kuamkiana ukifuatia na kutoa shukrani. Toka idadi kubwa ya maelezo yaliyo katika picha yanayopatikana katika uvumbuzi wa maandishi yaliyo katika mafunzo nchini Misri, mifano mitatu au minne imetolewa katika uwazi wa barua kwa Waefeso. Kwa kawaida Paulo alifuata mapatano ya desturi, mara nyingi akiinua maelezo ya wakati uleule katika mapatano na matumizi yasiyoangalia wengine kuwa ni njia ya kueleza wazo la hali ya juu na tabia nzuri. Hata katika barua yake ya kwanza kwa Wakorintho inayoshughulika na shida nyingi na matatizo, yote yanampa Paulo sababu kubwa ya wasiwasi - Mtume anafuatilia kusalimia na maneno: "namshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu" (1Kor 1:4). Kukosekana huku kwa kutoa shukrani katika barua kwa Wagalatia kunaonyesha sio tu ni kwa kina kiasi gani mtume aliona badiliko kwa waumini wa Galatia, bali pia ni ukubwa kiasi gani kwenda kombo kwao toka injili. Mafundisho ya Kiyahudi, wakati akidai kukamilisha injili, kwa kweli yalipingana nayo. Ikiwa kadhia yao ilikuwa injili ya kweli haikuwa njia ya wokovu wa maana. Ni bayana aliona hivi waziwazi, na maneno yake makali ni mawazo ya mahali pa kufaa yenye maana katika Galatia. Badala ya wakati ule sentensi kuanza "namshukuru Mungu" tunakuta: "nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo na kugeukia injili ya namna nyingine." Kwenda kombo kulikuwa upesi, siyo tu toka muda mfupi wakati katikati ya mambo mawili tangu kipindi injili ilipohubiriwa kwao, bali pia katika kwenda kasi ambako walikubali matakwa ya waalimu wapya. Wale wanaodhani Wagalatia walihutubiwa katika barua walikuwa wakazi wa kaskazini mwa Galatia, wanaiona barua kuwa na maana kwa sababu ya urefu wa kipindi ambacho kilipita katikati ya kuhubiri kwao Paulo na kuandika waraka. (17) Lakini ikiwa makanisa yaliyo hutubiwa yalikuwa kusini mwa Galatia, maana iliyopita ni ya asili. Wagalatia hawakushika mwendo muda mrefu, na hii kwa mtazamo wa shauku ambao walipokea injili mtume alijawa na uchungu wa mashangao. Kutangua sheria "Yeye aliyewaita" ni Mungu ambaye mapenzi yake Paulo anayo katika aya inayotangulia inayohesabia kusudi lote la neema. Wayahudi bila shaka walifanya ukweli mwingi wa kwamba sheria ilikuwa ya Mungu na ya kwamba itunzwe na wote. Lakini Mungu aliyetoa sheria kwa Israeli aliwaita watu wa mataifa "katika neema ya Kristo". Sheria ilkuwa ya kitaifa; na kama nyakati zilizopita mtu wa mataifa kama Ruthu au Rahabu, walishika tumaini la Israeli, wakawa ni wenyeji wa Israeli. Kwa kukosekana kutangua sheria, Wayahudi waliomwamini Yesu waliendelea vilevile kushika sheria. Wakati wa kipindi cha historia hasa kilichozungukwa na Matendo ya Mitume, hili lilikuwa jambo; lakini barua kwa Waebrania, baada ya kusadikisha ya kwamba Mungu alinena katika mwana ambaye mambo yote yaliyoelezwa katika sheria yamepata utimilifu wake, wakatakiwa hata waumini Waebrania kujiunga na Kristo "nje ya lango" la Israeli. Kusudi hili kwa kipimo kipana kinaeleza uandishi wa barua kwa Waebrania usio wa kwaida kutokuwa na jina la mwandishi: na kwa kukosa jina la mwandishi wa barua ina idhini ya mamlaka ya Mungu bila kuwa na yeyote mtu wa kati. Badiliko hili la uhusiano wa muumini wa Kiyahudi katika sheria lilikuwa ni la polepole, kama lilivyofaa kwa kusudi kwa hali zilivyokuwa. Kutokana na kuhubiriwa injili na hitaji la kuiacha sheria, kungefunga masikio ya Wayahudi wote katika mwaliko wa Mungu. Kutenguliwa na Mungu katika barua kwa Waebrania kulifuatia muda mfupi tu wa maasi yaliyosababisha Warumi wateketeze mji na hekalu, ambapo ikawa vigumu kushika sheria kwa heshima nyingi. Basi, wakati ikiwa ya kipimo chenye kufaa, Wayahudi walinata katika njia za Kiyahudi kwa muda, haja ya kwamba watu wa mataifa wafuate mitindo yao ya ibada na mtendo yale ya ibada ilikuwa ni kuweka haja isiyo ya haki ya kitu cha mfano juu ya hali ya kweli iliyoonyeshwa katika mfano. Hii kuwa kweli ilifanya injili kutokuwa na maana iliyotakiwa pasipo sheria na wahubiri wa Kiyahudi tupu kwa sababu hii wakihubiri injili nyingine. Neno lingine katika mstari wa 6 na 7, linaonyesha maneno mawili kwa Kiyunani, na Biblia B.H.N. imejaribu kutunza hali ya kuwa si ya kawaida kwa kuelewesha katika mstari wa 6. Mengi yameandikwa juu ya maana ya utaratibu wa maneno mawili: ya kuwa ni yenye maana ileile na nyingine katika lugha moja lilipotumika kwa kutengwa imekubalika na wote, lakini waandishi wengine wanasisitiza ya kuwa tofauti iliyokusudiwa wakati maneno yanapotumika katika muunganiko wa karibu. Tofauti halisi - neno gani linaweka mpaka wa kuachana tarakimu tu (nyingine ya daraja lilelile) na tofauti ambayo ya muhimu (daraja lingine moja) ni maana iliyopingwa; maelezo yake yaliyosimuliwa ambayo ni lazima yakumbukwe kwanza hayatakuwa na faida ya juu juu tu. (18) INJILI iliyo "tofauti" Kupambanua kunaweza kuwa kama ifuatavyo: Wayahudi walikuwa wanahubiri injili tofauti: kwa Paulo ilikuwa kanuni tofauti tupu hata anakana usahihi wake wa kuiita injili: ni injili ya namna nyingine kwa kuwa haiwezekani pawepo injili mbili; injili yake na injili ya wapinzani wake kwa heshima ya wao kwa wao zilikuwa hazishirikiani. Kwa hakika inaweza kuitwa ni injili nyingine tu katika maana ya kwamba Wayahudi walikuwa wanawageuza nia zao na kuitupilia mbali injili ya kweli. Ni kazi gani kuelezea kuwa injili! Wakati ule tafsiri hii iliweza vile vile kueleweka kuwa ni kukutana na madai yaliyofanywa na Wayahudi, waliosema kwa kweli injili ya Paulo ilikuwa ni geuzo kidogo la Injili ya kwanza aliyoipokea kwa wale kumi na mbili. Paulo anarudisha maneno ya kwamba anahubiri injili ya kweli - hii nyingine, ambayo sasa Wagalatia walikuwa wanaisikiliza, si injili kabisa; na kabla ya kushughulika na hoja muhimu ya chanzo cha hii injili, anaeleza ya kwamba ni yenye mamlaka injili aliyohubiri na kwamba yeyote anayetangaza injili nyingine yoyote alikuwa amelaaniwa. Ni lugha ya nguvu, yenye mkazo uliorudiwa: "kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe". Wengine walisema ya kwamba Paulo alipamba matendo fulani, na katika sehemu ya mafundisho yake; ikiwa hivyo, alijumuisha katika kulaumu mambo fulani kuwa maovu; lakini katika kuwa na fikira zile zile daima za mwendo wake atalinda. Lakini tangu Wayahudi walikuwa na dai tofauti katika fundisho lao na la Paulo, wao walikuwa na laana. Itakuwa vyepesi kueleza ukali wa maneno haya kama yanatokea tu katika uwezo wa mawazo ya Paulo; lakini tunapopima ni mabadiliko gani yalikuwa kama Paulo hakushinda hii vita ya Galatia, tunaweza kuona kwao wote uzito ambao unaohusu kuthamini kwao wote alioukusudia Paulo. Injili ni kwa ajili ya wokovu wa watu, na ni ufunuo wa nia ya Mungu. Kupotoka kwa injili kunaonyesha vibaya nia ya Mungu na kunaondoa maarifa ya wokovu. Mwenye kuigeuza injili ni yule anayeangamiza tumaini la kweli- ndiye anayetupilia mbali ufunguo wa kupata elimu na anaufunga mlango ambao kwa huo watu waweza kuingia katika Ufalme wa Mungu. Ukweli wa Injili ya Paulo Paulo alikuwa na hgakika ya ukweli wa injili yake. Ujasiri wake ulikuwa na maana inayoanza katika kuona kwake na kukutana na Kristo; lakini uthibitisho uliotolewa wakati ule uliongeza nguvu kwa mambo mawili. Wa kwanza ulikuwa na ushahidi ulioletwa na maandishi ya Agano la Kale ya kwamba Kristo hana bidi kuteswa na kisha kufufuka tena. Ushahidi ulikuwa mwingi na ulikuwa wazi, pande zote mbili kwa ufafanuzi wake mpana wa kazi ya Mtumishi wa Mungu ambaye uhai wake ulikuwa dhabihu kwa dhambi, na vilevile katika kiasi cha maelezo moja mojaa yaliyodhihirika kuhusu matendo yalivyo upande wa nje yaliyounganika na mauti ya Masihi. (19) Pia ilkuwepo ushahidi wa ushuhuda unaoendelea wa Roho mtakatifu, pande mbili katika nguvu aliyopatiwa Paulo na vilevile katika kujitokeza wazi kwa karama za roho miongoni mwao walioamini. Matumaini ya Paulo, yameandikwa kwa kifupi kwa maneno yake, "kwa maana namjua yeye niliyemwamini na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile" (Tim.1:12), kimehesabiwa haki. Ingawa hivyo, itakuwa ni kosa, kuhesabia sifa kwa hilo tumaini katika kweli ya injili yake kinachoweza kuitwa kutovumilia kutoelezwa katika maneno, "Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe". Mashauri ya taarifa hii yote pamoja yapo nje ya kutunza roho za watu wote siku hizi katika mambo ya dini. Mtu anaweza kuwa na ruhusa kujishughulisha sana katika wazo la siasa, lakini ujasiri na kusema kwa nguvu kwa kuweka mbele fundisho lake Kikristo linachukiwa. Mtu anayefundisha ya kwamba vitu havikuumbwa bali vimegeuka na kuendelea toka vitu vya asili aweza kujifurahisha kwa maneno katika fundisho lenye kanuni za kanisa na kupata idhini; fundisho hili la kanisa juu ya mafunzo yalifunuliwa limeangaliwa kama alama ya ufinyu wa kufikiri. Lakini ikiwa injili ni kweli kutovumilia hakuwezekani. Ikiwa Mungu amenena, neno lake halina budi kutopingana. Ikiwa Mungu atamwondokesha miongoni mwa watu nabii na "kutia maneno yake kinywani mwake" naye "atanena yote ambayo Mungu amemwamuru", kimsingi ni haki kwamba Mungu aweke adhabu juu ya mvunja sheria. "Hata itakuwa mtu asiyeskiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu nitalitaka kwake"(Kumb.18:19). Mungu alisema kwa Israeli. "usiwe na miungu mingine ila mimi" (Kut. 20:3). Mtakatifu wa Israeli, Mungu aliye hai, hawezi kushiriki heshima na kuabudiwa na watu wa miugu ya uongo ambayo watu wamevumbua wenyewe na sanamu za miti na mawe. Lililo la kweli kwa Mungu mwenyewe ni kweli vilevile kwa kazi ya ukombozi wa watu. Ikiwa Mungu atafunua habari njema ya wema kwa watu, chochote kinachogeuza injili hiyo humfanya Mungu kuwa mwongo, na kuingiza upuuzi wa binadamu mahali pa hekima ya Mungu. Katika utendaji wa kusudi hilo Mungu anapojidhihirisha mwenyewe kwa mwanadamu ambaye pande mbili ni mwana wa Adamu na ni mwana wa Mungu, na kisha kulingana na nia ya Mungu iliyofunuliwa ya kwamba mwana anateseka na kufa na ya kuwa Mungu kwa huruma yake aweza kusamehe dhambi za watu, kutia mahali pa njia nyingine yoyote iliyoendekezwa na kudharau tendo la upendo wa Mungu. Kuikana injili ikiwa ni papo hapo au bila kuuliza, na kuwa badala ya mafundisho yanayodhoofisha, kunaweza kuleta kuitwa kwa ajili ya hukumu ya Mungu na upingamizi wa watu ambao ni waaminifu katika neno la Mungu. Mtu anayeiharibu injili ni adui wa Mungu na wa ndugu zake mwenyewe. Anakuwa adui wa kusudi la Mungu na kuwanyima watu njia ya wokovu. Ikiwa Mungu ni mmoja, kaama kadhia ya Paulo katika Warumi 3:30. "Injili yoyote nyingine isiyo ya kweli, na wanaoanzisha inabidi walaaniwe. (20) Njia ya Mungu haishirikiani na nyingine Mkazo wa kutoshirikiana kwa njia ya Mungu uliofunuliwa katika Biblia haupendezi katika mioyo ya watu wa siku hizi, lakini mwenendo wote wa watu katika neno la Mungu hauna budi kukaripiwa na Mungu. Umedhihirika ya kuwa Mungu ni Mungu mwenye wivu. Kama hakudai ukuu wake ingekuwa sawa na kujiuzulu katika cheo chake, kitu ambacho kingekuwa hakiwezekani maana ni kama kujikana mwenyewe. Vilevile kutoshirikiana na wengine kunatokea katika maneno yasiyo na idadi. "utukufu wangu sitampa mwingine" nitatakaswa kwao wanikaribiao". Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote" "Hapana jina jingine chini ya mbingu litupasalo kuokolewa kwalo". Aliye na mwana anao uzima:asiye na mwana wa Mungu hana uzima". "Hakuna amjuaye mwana bali baba:wala hakuna amjuaye baba, ila mwana, na yeyote ambaye mwana ampenda kumfunulia"(Mat.11:27). "Kama tukisema hatukutenda dhambi twamfanya yeye kuwa mwongo, wala neno lake halimo mwetu."lakini hii ni baadhi ya mifano; karibu kila ukurasa wa Biblia unatoa mingine. Mtu anayekana elimu ya hesabu ya taarifa zilizowazi, anaonyesha upumbavu wa akili. Lakini ikiwa mtu akikana kweli za kawaida kwa wokovu zinapojulikana katika ufunuo uliothibitishwa kuwa kweli kwa ushahidi mwingi, kosa lake lapita toka kwenye akili hadi uso uliosawa sawa katika mema na mabaya. Kama ni kosa la adili kwa kukana njia ya Mungu, inakuwa haja ya wema katika kuitegemeza. Hifadhi yake na kudumisha si kitu kidogo zaidi kuliko kuwa upande wa Mungu, na kukataa kufanya hivyo ni kuungana na maadui wa Mungu. Maelezo ya laana kwa Paulo, wakati ule, sio tokea la ushupavu wa dini kwa nguvu, bali yanahusu haja katika ukweli wa kwamba injili yake ni habari njema ya Mungu. Paulo aliona dhahiri ya kuwa wapinzani wake, kwa kugeuza injili yake, walikuwa waondoa maarifa ya Mungu yanayookoa toka waongofu wake, na kuweka pafaapo ile ambayo si injili kabisa. Pamoja na hivi, kuiba mfuko wa mtu hakukuweza kulinganishwa. Ubishi toka mtazamo wa maana unapatikana katika taarifa ya Paulo. Kama Paulo anatamka laana kwa mpotoshaji injili yake yaonyesha kubwa kiasi gani, ni muhimu kiasi gani na jinsi gani kweli, ni ujumbe wake. Mtu duni na mzembe akikana haweki matokeo ya kutisha jinsi hii. Matamshi ya laana, basi ni kielezo kimewekwa kwa kusudi maalum, katika kukabili kuipotoa hao wapinzani wake Wayahudi ya kuwa injili yake ilikuwa ya kweli. Injili ya Paulo ilifunuliwa na Kristo (1:10-12) Maamuzi ya Paulo yaliyofanywa kwa haraka, ambayo bado kamwe hayakomi kuwa yenye akili na yenye maana, wakati mwingine yaonekana kutotii mchanganuo ulikoagizwa. Tumetia aya ya 10 kwa sehemu hii, lakini ingekuwa imelingana vyema kuwekwa katika sehemu iliyotangulia. Wengine wanagawa fungu dogo la maneno ya Biblia kwenye mstari wa 9; ambapo Bibilia ya Kiingereza R.V. fungu la maneno linaishia katika fungu la 10 maneno, lakini vyovyote tukifanya mgawanyiko wazo la Paulo linasonga mbele. (21) Kwa maana hii, katika barua yake Paulo anaanza kujitetea mwenyewe, kwa unyoofu wake, na ukweli wa ujumbe wake katika mgawanyiko wa sehemu hii ya barua unafika hadi mwisho wa mlango wa 2. Yameangaliwa vyema ya kuwa katika nyaraka za Paulo tunazo nakili za maneno ya wapinzani wake. Wakati mwingine amechukua maneno machache ya ubishi wao, ila tukiona ushahidi huu mwingi kwetu sisi kufahamu jibu lake tutakubali. Yeyote mwenye udadisi katika kupima jambo asome nyaraka zake kwa wakorintho kama tulivyotafsiriwa na Conybeare na Howson, na kuchunguza alama zilizoonyesha namna hii (' ` au " ") aangalie ni kiasi gani limeendelea katika nguvu na udhahiri. Yawezekana kuonyesha kuzidi kwa juhudi katika alama hizi za maneno machache kwa wapinzani wa Paulo, lakini hiyo haituhitaji sisi kutojua maelezo bayana ya hakika yalioonyeshwa. Ramsay anamnukuu Prof. W. Locke kwa matokeo kuwa "ili kufahamu mafungu mengi ya maneno katika nyaraka ya Paulo yatupasa tuelewe ya kwamba maneno fulani machache yaeleza kitu, kama si maneno hasa ya mashutumu ya kumsuta katika kusema juu yake na wapinzani wake Wayahudi Wakristo." Gal.1;10 unatoa maelezo yenye kutiwa picha ya mifano kwa ajili ya jambo hili. Maadui wa injili ya Paulo walimlaumu mtume kwa kulazimisha injili yake kwa wasikilizaji wake ili aweze kuwashawishi waongofu. Kwa kuona maneno yao yamepotoka na yametumika vibaya ni jaribio la wote ambao wanahutubu injili, na kwa kufanya hivyo wanafunua uzushi. Kwa njia hii Paulo aliteseka sana. yeye mwenyewe amesema ya kwamba amekuwa mambo yote kwa watu wote. Matendo ya nje aliyosifu yaweza kuonekana kuachana lakini kweli yanaugumu katika usawa ambao haukueleweka na wapinzani wake. Alimtahiri Timotheo, lakini alikataa kumtahiri Tito. Alikataa matakwa ya kwamba watu wa mataifa wawe chini ya sheria, yeye mwenyewe lakini hakusita kufuata ibada za hekalu na taratibu za kuabudu Wayahudi. Maneno na matendo kama ya jinsi hii yalitoa sababu za mashitaka ya kutopatana yaliyofanya ugumu wa kazi yake kusemwa ina thamani ndogo. Paulo alieleza kutoshirikiana na wengine na kutovumilika kwa injili ya Mungu kwa maneno ambayo hayawezi kufanywa kuwa na nguvu (msitari 8,9). Katika aya ya kumi anauliza, "maana, sasa je! `Ninawashawishi wanadamu`. Au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo. Katika maneno hapakuwa na lolote ambalo aliandika kusaidia shitaka la kwamba "alikuwa mtu mwenye kupendeza wanadamu" tu na kupamba akishurutisha ujumbe wa injili. Kuruka katika sentensi maneno yaliyotakiwa ili kukamisha maana kumetatanisha katika swali la kwanza, wazo lililotolewa kwa njia nyingine laweza kuwa jinsi hii, "Je! Nimejihusisha juu ya Mungu?" aliweza kuwapendeza watu na kuwaridhisha wasingiziaji wa Kiyahudi kwa kufundisha haja ya kufuata sheria na kukubali kanuni ya tohara. Kwa hakika, chuki aliyoistahimili kwa Wayahudi jambo la kushitakiwa lilikuwa la uongo dhidi yake: lakini, anasema Paulo (R.V.). "kama bado ningekuwa nawapendeza wanadamu" - kama alikuwa anakubali matakwa ya Wayahudi - wakati ule hangelikuwa mtumishi wa Kristo au mtumwa. Kwa hakika angekiri kushindwa na kuwa mtumwa wa mwadamu. (22) Lakini alichukua chapa zilizomthibitishia kuwa mtumwa wa Kristo. Matokeo ya mateso yaliyoshuhudiwa na Wagalatia wa Listra na Derbe yalikuwa ni alama nyingi katika mwili wake zilizoonyesha alikuwa wa Kristo. Wagalatia hawakutakiwa kuwa na shaka juu ya jambo hilo. Asili ya injili ya Mungu Ikiwa basi unyoofu wa Paulo ulikuwa hauna shaka, walakini alidhaniwa amekosea? Msingi wa mafundisho yake ulikuwaje? Mamlaka yake ni nini? Kwa hili anageuka kwa maneno yafuatayo: "kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubili, nawajulisha ya kuwa sio ya namna ya kibinadamu. Kwa maana sikuipokea kwa mwanadamu wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo" (mstari wa 11,12). "Sio ya namna ya kibinadamu" inaonyesha ya kuwa haikuvumbuliwa na mwanadamu; haikuwa tokeo la mawazo ya watu na kutunga. Katika sifa na utaratibu wake ujumbe wake ulichukua alama asili ya kutoka juu na ulikuwa na mamlaka ambayo chanzo chake ni kwa Mungu. Paulo anakuza zaidi maana yake: hakupokea toka kwa mwanadamu, wala hakufundishwa na watu. Hivyo ni kusema, wala ujumbe haukuja toka kwa mtu awaye yote, au mwanadamu yoyote alieleza maana yake kwa Paulo. Kwa kila namna njia ambayo kwayo mwanadamu hupata habari imewekwa mbali. Basi alipokea "kwa ufunuo wa Yesu Kristo". Kwa fungu hili la maneno machache hatuna budi kuelewa ya kuwa Yesu ndiye aliyefanya ufunuo, na-si kwamba Yesu ndiye aliyenenwa katika ufufuo, uliofanya kwa Paulo. Kwa maneno mengine, elimu yake ya injili, ujumbe wake aliotangaza, ulikuwa na mamlaka ya Yesu mwenyewa. Ni lini na jinsi gani injili alipewa hivi kwa utimilifu Paulo hatutaweza kuyakinisha na uhakika. Tunajua ya kuwa lililompata lilikuwa la kipekee akiwa njiani kuelekea Dameski. Manabii walipokea neno la Bwana kwa ndoto, kwa usia, kwa mawasiliano na Malaika. Hata Yohana, mwanafunzi aliyependwa hakuwa na ufunuo wa Yesu Kristo moja kwa moja toka kwa Bwana wake, bali kwa kupitia malaika ambaye Yesu Kristo alimtuma kwa lugha ya ishara. Lakini Paulo alikutana na Yesu, na "alimuona yule mwenye haki, akasikia sauti toka kinywa chake". Lini huu mwazo wa ufunuo wa Yesu Kristo ulipoongezwa hatutaweza kujua. Paulo anataja maono na mafunuo ya Bwana aliyopata miaka kumi na nne kabla ya kuandika nyaraka kwa Wakorintho. Hii haina budi inataja wakati mwingine miaka mitano baada ya kuongoka kwake. Lakini vyovyote tena mawasiliano aliyokuwa nayo Paulo, uhakika ni kwamba Yesu alikutana naye, alinena naye na kumpa agizo lake, ilitosha ndani yake yenyewe kumtenga na kuwa na nafasi isiyo ya kawaida. Maarifa yetu ni njia ambayo mawazo ya Mungu yaweza kutiwa ndani ya moyo wa mwanadamu na hivyo kuwa yake na lakini si yake, ni kidogo sana. Katika maneno ya manabii yalikuwepo mambo mengine wao wenyewe ilibidi kupima ili kujua maana ya maneno yao wenyewe. Walakini, kwa suala la Paulo, ujumbe uliohubiriwa haukuwa tangazo tu la neema ya Mungu bali ushahidi wa kutumia akili ukiunganisha ushuhuda wa ufunuo wa awali katika Agano la Kale. Ujumbe wa Paulo inabidi siyo tu uliwasilishwa kwake kwa namna nyingine, bali hauna budi pia ulijengwa katika fahamu zake mwenyewe hivyo kwamba ukawa namna yake mwenyewe ya kuwaza. Katika suala lake mwenyewe hii ilihususha mambo asiyojifunza ya maana yalifundishwa kwake na mwalimu wa Kiyahudi, na katika mafuatano hayo alikuta kwamba muda mmoja vikwazo kwa imani vikawa hatua ambazo alipanda kwenda juu katika maono yaliyodhahiri na imani iliyo kubwa. (23) INJILI YA PAULO HAKUIPATA KATIKA MAISHA YAKE YA KWANZA (1:13,14) Tangazo la kuwa maisha ya Paulo ya kwanza hayakutoa machango katika maarifa yake yaliyopo yanatia faraja kubwa ukweli wa kuwa kufahamu kwake mpango wa Mungu ilikuwa kwa ufunuo. Kwa kweli kukosekana mtazamo wake wa awali ulikuwa na mbegu zozote za maendeleo ambayo yalikua katika imani ya Kikristo. Pengine mbali. Wagalatia walijua masimulizi yake - mwendo wake wa maisha akiwa adui mkali na mtesaji wa Wakristo, na bidii yake kuiharibu imani yao katika dunia. Hiyo ilikuwa matokeo ya imani yake ya kwanza; na mkazo wa upinzani wake kwa Yesu na wafuasi wake ulikuwa wa kulinganisha kujitokeza juhudi ya Kiyahudi. Alilelewa katika nyumba ya Kiyahudi ya peke yake, akiwa kama alivyodai Mwebrania wa Waebrania; alisomeshwa katika chuo kinachoongoza cha Taifa lao, aliketi miguuni pa mwalimu wao mkubwa. Alikuwa mwanafunzi mwepesi wa kujifunza, aling'ara kuwazidi ndugu zake wanafunzi katika bidii yake na moyo wa kutumia somo la sheria. "Naliendelea", anasema, "katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu" (aya ya 14). Mapokeo ya mafunzo ya Wayahudi yalikuwa ni maisha sana: yalimwongoza kupinga ujumbe wa Wakristo. Kwa hiyo ilikuwa dhahiri ya kuwa imani yake iliyopo na ujumbe havikuweza kuchipuka toka maisha yake ya awali kwa yale aliyoamini. INJILI YA PAULO TOKA KWA WAALIMU WENGINE (1:15-17) Katika aya 12 Paulo alitoa kadhia ya kwamba ujumbe wake hakuupokea kwa wanadamu, au kufundishwa na wanadamu. Alionyesha kwa ushahidi katika mwenendo wake wa kwanza kuwa ujumbe wa Kikristo haukuweza kuchipuka katika imani yake ya zamani. Ilimpasa kukamilisha ushahidi wa asili yake toka kwa Mungu kwa kuonyesha vilevile ya kwamba hakufundishwa na wanadamu. Kwa kufanya hivi ilikuwa lazima kuhesabu mara ya pili wale ambao alionana nao kwa mtazamo wa maadui wa Paulo waliowahi kuwa waalimu wake,. Kwa hiyo akawa hanabudi kuanza na kuongoka kwake. Hilo lilipotokea, anasema, ingawa aliamriwa wakati ule kuhubiri, hakutaka mahojiano na, mitume waliokuwa kabla yake bali aliishi maisha ya kujitenga. Itakuwa vema kunukuu maneno yake: "lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake, alipoona vema kumdhihirisha mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili wa damu; wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski" (mistari 15-17). Paulo alikuwa Farisayo "aliyetengeka" kama jina linavyoelekeza. Wakati ule alidhani kuwa alipata jambo lisilo na kombo na kujua kusudi la maisha; alifikia upeo wa kiroho katika mwenendo wa kuwa Farisayo. Sasa akakuta kuna "kutengeka" kwingine kunaendelea kusikojulikana kwake, ambako Ufarisayo wake wa kibinadamu haukutoa mchango ila soni na kutahayarika. (hilo kwa hakika lilikuwa jambo lingine, katika maana hii: tokeo la Ufarisayo lilionekana na Paulo kutokuwa sawa katika njia ya Mungu na ya kuwa njia mpya (24) iliyo hai katika Kristo ilionekana kwa tofauti kubwa; na nguvu za Paulo zenye bidii ya kale zikamfanya atambue basi, unaweza kuwa mkubwa upumbavu wa mwanadamu kiasi gani na kiasi gani anahitaji rehema ya Mungu). Paulo alipotazama nyuma katika maisha yake aliweza kufuatia na kuangalia mkono wa Mungu katika mazingira yaliyoenda katika kutengeneza maisha yake, tangu siku za mwanzo kabisa. "Tangu tumboni mwa mama yangu" inaelekeza ya kuwa hata kabla ya kuzaliwa kwake alijulikana kabla na kuteuliwa kwa ajili ya kazi iliyombidi afanye. Kuungana kwa ushawishi wa ajabu uliofanya kuhubiri injili uwepo uwezekano katika karne ya kwanza, kama kabla hapakuwa na kipindi kingine au tangu yote yalipohusika katika maendeleo yake mwenyewe Paulo na majaribio ya kazi ambayo jukumu la Mungu alikuwa nalo kwa ajili ya kufanya. Warumi, Wayunani na Wayahudi wote walikuwa na mchango kwake. Uraia wake, uwezo wake, wa kunena na dini yake - vigawanyo vyenye nguvu vinavyofanywa na mtu - vilikuwa vigawanyo vilivyojitokeza dhahiri vilivyopatikana katika maisha ya karne ya kwanza. Hivi vilikuwa vishawishi vilivyo nje vilivyotenda katikati, vilimfanya Paulo mtesaji, na ambavyo - kipindi jambo lingine muhimu zaidi kuliko yoyote matatu lilipoongezwa - likamfanya Paulo mtume. Hilo jambo lingine Paulo analielezea anaposema "aliitwa kwa neema yake". "Kuitwa"kwa Paulo kulikuwa kwa nguvu zaidi ya ushawishi wote mwingine tangu kipindi cha kuongoka kwake ulisaidia "utu mpya", ukiisha tumika na huo "utu mpya"kuwa njia ya kusaidia kusudi kubwa alilokuwa nalo toka kipindi hicho na kuendelea mbele katika kutimiliza. Hilo kusudi la Mungu alilomwandaa Sauli limeelezwa wazi kabisa ya kuwa Mungu aliona vema "kumdhihirisha mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri mataifa habari zake".Katika aya ya 12 alinena ya kuwa ni kwa "ufunuo wa Yesu Kristo" - ufunuo uliokuja toka kwa Yesu Kristo. Matokeo ya ufunuo huo ikawa ni kufanyizwa kwa Paulo afanane na mwana wa Mungu, amejieleza wazi kabisa mwenye kuwa "Kristo ndani yangu". Kwa hivi akafaa kumhubiri Kristo na kumdhihirisha Kristo kwa wengine. Mtu na ujumbe walikuwa katika mapatano. Kwa sababu hii aliweza kuwaandikia Wathesalonike: "kama vile mnavyojua jinsi zilivyokuwa tabia zetu kwenu, kwa ajili yenu.nanyi mkawa wafuasi wetu na wa Bwana (1Thes.1:5,6): na kwa Timotheo, "Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake; ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani. Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana pamoja na amani na pendo lililo katika Kristo Yesu. Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubaliwa kabisa ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristo au dhihirishe uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakao mwamini badaye, wapate uzima wa milele." (1Tim 12-16). (25) Mungu alipoingilia kati katika maisha ya Paulo kwa mtindo wa moja kwa moja ambao ni Paulo tu miongoni mwa mitume alipata (ila yalikuwepo mengine katika maisha ya Petro yaliyolingana ambayo Yesu aliyataja anaposema , "mwili na damu havijakufunulia, ila Baba yangu aliye mbinguni"), mara akaenda Arabuni. Hapakuwepo mashauriano na wengine wala kukutana na mitume mengine Yerusalemu. Hakuna kinachoweza kusema na uhakika kuhusu ni mahali gani anapopataja Arabuni. Katika mlango wa 4:25 anataja Sinai Uarabuni, na kwa sababu hii ni vigumu kuweka mbali eneo la nchi iliyozungukwa na bahari ya Sinai toka neno Arabuni kama anavyolitumia katika 1: 17. Yaonekana liliwekwa jina hilo likijumuisha nchi zilizo karibu sana na Dameski, na hata kwa kipindi mji huo wenyewe. Lakini haikuwa kawaida Paulo alipokuwa huko mara moja baada ya kuongoka kwake kusema kwenda Arabuni ikiwa Dameski ilikuwa sehemu yake. Walakini, aliweza kusema alikwenda Arabuni lakini hakusafiri mbali katika mji wa Dameski. Lakini popote alipotembelea msemo wake ulidokeza ya kuwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya kwenda Yerusalemu hakikutumika aidha kuhubiri au kujadili injili yake na viongozi wengine. Kilitumika kwa kuzoeza akili yake katika ufahamu wa Mungu na njia zake, akiongozwa na ufunuo toka kwa Bwana. SAFARI YA KWANZA YA PAULO KUTEMBELEA YERUSALEMU (1:18-20) Wote ambao wamesoma maisha ya mtume Paulo wanajua kwamba pamewahi kuwapo mashindano mengi ya maneno kuhusiana na kuthibitisha safari za Paulo kutembelea Yerusalemu kama zilivyoandikwa katika Matendo ya Mitume na Wagalatia. Sababu nyingi hazina budi kuchukuliwa katika maelezo. Kuanzishwa tena wazo la kuwa Wagalatia ambao waliandikiwa waraka ni makanisa ya miji minne ambako Paulo alihubiri katika safari yake ya kwanza, kumeongoza kutazama kuwa Wagalatia waliandikiwa mapema zaidi kuliko ilivyoaminika kwa muda mrefu. Utetezi wenye nguvu wa Bw. W. Ramsay na wanafunzi wawili au watatu umesimamia tendo la kukubali wazo la Kusini mwa Galatia, pamoja na kulirekebisha tena kumehusisha sio tu kwa tarehe ya barua ilipoandikwa, bali pia kwa ushahidi ulio katika sehemu nyingine ya vitabu katika Matendo ya Mitume na waraka. Hatukusudii kujaribu majadiliano yoyote ya sababu zilizowekwa kwa mbele katika upande mmojawapo wa mashindano ya maneno. Tutafuatilia waraka na kutoa muunganiko na matendo ambayo tunaamini kuwa na msingi bora zaidi na ambayo yanabainisha wazi sababu za mitume kusaidia mashauri vilevile mwendo wa historia katika nyakati za kwanza za mitume. Paulo alieleza ya kuwa kwa kukabili mashitaka yaliyofanywa na wapinzani wake, aliyohubiri injili hakuipokea kwa wanadamu, wala hakufundishwa na wanadamu. Kuweka uhakika wa kwamba hakuna mtu aliyemfundisha injili, ilibidi atoe uhakika wa kweli kuhusu aliokutana nao mitume wa kale kuliko yeye. Kwa hakika Wayahudi walibuni mazingira zaidi yoyote ambayo yataelekea kumuumbua Paulo. Jambo lingine lililohitaji kusahihishwa ilibidi lililokwisha semwa juu ya safari yake ya kwanza ya Yerusalemu na sababu dhidi ya kutembelea. (26) Hii pekee yaweza kutoa maelezo ya maneno ya mambo yenyewe kwa uzito mno uliofanywa kwa kiapo cha kwamba alilosimulia lilikuwa kweli. "Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo" (1:20). Paulo anataja safari mbili kutembelea Yerusalemu katikati ya vipindi viwili alivyotumia katika Siria na Kilikia. Vilevile anaelezea kukutana na mtume mara ya tatu kuliko- fanyika Antiokia. Safari ya kwanza imetaja miaka mitatu baada ya kuongoka kwake - kipindi cha wakati ambacho hakiwezi kuwa zaidi ya miaka miwili. Sehemu ya kipindi hiki alikitumia Arabia. "Alipanda", Paulo alieleza, "ili aonane na Kefa ", ambaye alikaa kwake siku kumi na tano. Hakuonana na mitume wengine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana, ambaye, ingawa si mtume katika maana ya kuwekewa mpaka, alikuwa na nafasi muhimu katika mabaraza ya kanisa Yerusalemu. Alikwenda kuonana na Kefa: au kama R.V. "kumtembelea". Neno analotumia Paulo linatoa habari ya kuzuru kama hivi hapo watu wakienda "kutazama" mahali, kuona majengo yake n.k. Paulo alikuwa mtu wa kwanza aliyejulikana vema kati ya mitume, na lilikuwa ni jambo la kawaida kabisa kwamba Paulo atataka "kuzoeana"naye (ufafanuzi wa Biblia R.V.). lakini maana hii kabisa ya neno inaweka mbali - pembeni wazo la ushauri wowote wa kutaka mafunzo na habari. Kuingilia kati kwa Barnaba. Taarifa katika Matendo ya Mitume yaonyesha kwamba mpaka hapo toka Paulo akaribishwe kama mwanafunzi wa kupendeza, kwa mara ya kwanza aliepukwa. Taarifa ya Luka inasomeka: "Na Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi, nao walikuwa wakimwogopa wote, wasisadiki ya kuwa yeye ni mwanafunzi. Lakini Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwmaba alisema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ushujaa katika Dameski kwa jina la Yesu. Naye akawa pamoja nao katika Yeusalemu akiingia na kutoka. Akahubiri kwa jina la Bwana kwa ushujaa, akinenea na kuhojiana na Wayahudi wa Kiyunani. Nao wakajaribu kumuua. Lakini ndugu walipopata habari wakamchukua mpaka Kaisaria, wakampeleka aende Tarso"(Mdo. 9:26-30). Habari hii inatupatia mambo ya nje yanayostahili kuangaliwa na kuzuru. Ulihitajika wema na faraja, ukarimu wa udhamini wa Barnaba ili kufanya Paulo akubalike katika kanisa. Barnaba akamtwaa Paulo, "akampeleka kwa mitume". Hii haihitilafiani na Wagalatia kwa kuwa neno lenyewe haliwaweki wazi watu mmoja mmoja bali washika uongozi katika mitume, na kwa kutambulishwa kwa Yakobo, kwa hivi akajulikana kwa wawakilishi wa mitume. Mitume wengine yawezekana walikuwa katika safari za kuhubiri. Tumeachiwa kuunganisha mambo ya matukio ni kwa sababu gani kazi za Paulo kiasi chake kilikuwa kwa Wayunani. Alizuru masinagogi ya Wayahudi waliotawanyika, mahali ambako Wayahudi wanaozungumza Kiyunani na mataifa wanaongofu wanapokusanyikia Akafanya kile alichofanya Stefano kabla na kukabiliana na upinzani uleule ambao ulimpata Stefano. (27) Tuna taarifa nyingine ya kuzuru huku katika maelezo ya Paulo mwenyewe ya uongofu wake katika Mdo. 22. Hapo anasimulia kuzuru hekalu, ambapo, wakati anasali, akapokea mawasiliano toka kwa Bwana: "Hima, utoke Yerusalemu upesi, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako katika habari zangu". Paulo aliwaza kwamba hakika kabisa alikuwa mtesaji wa watu waliofuata njia hii, ila sasa alikuwa mhubiri wa kile alichotafuta kukiharibu, ataweka katika kutunza ujumbe wake. Hivyo akabisha alipoambiwa atoke katika mji; lakini agizo lilirudiwa tena kwa maneno ya amri zaidi: "Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa mataifa." Ikiwa uvumi wa hila ya kumuua Paulo ulifika masikioni mwake ujumbe huu ulionyesha ni tendo gani halina budi kufuata. Kwa hiari akapelekwa na ndugu hadi Kaisaria na toka huko hadi Tarso. Habari ya mambo yenyewe anayofanya Paulo kwa Wagalatia yaonekana rahisi tena dhahiri kwa kitambo kidogo. Hata hivyo kwa uzito Paulo anathibitisha kweli yake, na kwa sababu hii ilipasa kuwa na thamani kubwa katika utetezi wake. Umuhimu wake usio na shaka umetiwa katika kutoa makosa ya habari ya mambo yenyewe mengine ya upotoshaji yaliyoenezwa na maadui wake kwa habari ya kuzuru, mkazo wa habari yenyewe usio gawanyika wa kwamba ilikuwa ili kujuana na Kefa ulitosha kuthibitisha habari zilizosemwa kuwa sio za kweli. Maadui zake walichosema linaweza kuwa jambo la kukisia tu. KATIKA SIRIA NA KILIKIA (1:21-24) Kwa vipindi viwili kati ya safari ya kwanza na ya pili kutembelea mji mtakatifu, habari tuliyonayo ni katika mistari hii tu. Mkazo "baadaye"unaotujulisha taarifa ya mambo yenyewe unaonyesha kuwa ni sehemu ya idadi ya mambo yote kuhusiana na kukosekana na mamlaka ya kibinadamu kuweka utume wa Paulo. "Baadaye", anasema, "nalikwenda pande za Shamu - ndio Siria - na Kilikia; lakini sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo; ila wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani. Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu".Kupatana kwa habari na Matendo ya Mitume kunapatikana kwa ukweli kwamba mwishoni mwa miaka tisa iliyotumika hivi, Barnaba akimhitaji Paulo kwa kazi iliyokuwa inaongezeka katika Antiokia ya Shamu, akatoka aende Tarso "kumtafuta Sauli" (Mdo. 11:25). Ilibidi amtafute: mahali alipokuwapo hasa hapakujulikana maana alitumia muda wake katika kuhubiri. Shughuli zake kwa kweli zilikuwa zimejulikana. Makanisa ya Uyahudi yalisikia kwamba aliyewaudhi zamani alikuwa na shughuli ya kuhubiri ile imani aliyokuwa anaiharibu. Paulo anazungumzia hakujulikana uso kwa makanisa ya Uyahudi. Hii imedhaniwa kuwa na utata na taarifa iliyo katika Matendo ya Mitume, lakini utata huu unakuwepo tu hapo tofauti isipogudulika katikati ya kanisa lililo Yerusalemu na makanisa yaliyo Uyahudi. Katika kuzuru, Paulo alikutana tu na ndugu walio katika mji mkuu; hakujulikana kwa wengine wowote katika jimbo lote. (28) Ukweli wa kwamba kipindi hiki kilitumika kwa kuhubili kwa mafanikio mno hata sifa ikafika Uyahudi, kinahusiana na suala la Paulo. Agizo lake kuhubiri halikuanza na kutengana mwenyewe na Barnaba kwenda kuhubiri. Huko ilikuwa kwa ajili ya kazi mpya, yakifanywa maendeleo mengine ya kazi. Agizo lilikuja na matamshi wakati wa kuongoka kwake alikuwa ni "chombo kiteule", akiwa pamoja na hili mahubiri yake yakaanza. Likaja kuthibitishwa alipopata maono katika hekalu katika safari yake ya kwanza kwa kuamriwa aondoke Yerusalemu na kwenda kwa watu wa Mataifa. Vivi hivi kwa upana kazi yake ilisifiwa hata habari yake ikasababisha makanisa ya Uyahudi kumtukuza Mungu katika Paulo. (29)