MAISHA YA MKRISTO SOMO LA 6 Jinsi tunavyowafikiria watu wengine ni muhimu kwa Mungu TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUTAFUTA KUMBUKUMBU REJEA ZOTE. Siku moja Yesu alipoulizwa kwa kujaribiwa na Mwanasheria Myahudi kuhusu amri ipi iliyo kuu kuliko zote, alijibu kuwa mpende Bwana Mungu wako kwa Moyo wako wote na kwa nguvu zako zote na kwa mawazo yako yote na jirani yako kama nafsi yako. Ili kufafanua alikuwa na maana gani kuhusu jirani, alielezea mfano wa Msamaria mwema . Unaweza kuikuta hii katika Luka sura ya 10 mistari ya 25 hadi 37. Tutarejea tena sehemu hii ya mafunzo ya Yesu katika somo lijalo, lakini itabidi uwe ndiyo mwanzo wa somo hili halikadhalika kwa sababu tunapotumia upendo wa Wakristo katika uhusiano na watu wengine, hata wageni (kama msamaria mwema alivyofanya), maagizo aliyotoa Yesu kwetu sisi na Mitume yatakuwa rahisi kuyaelewa na kuyafuatilia. Ni rahisi kuwa wazuri kwa tajiri na kwa wenye madaraka, lakini tu kawaonea na kuwadharau wanyonge, maskini au wasiojiweza. Yakobo, ndugu yake Yesu anasema kwamba "kuwaheshimu watu"na aghalabu anatuasa kuhusu mawazo haya. Yakobo sura ya 2 mstari wa 1 hadi 9, kuna mengi yakufikiria kuhusu maneno haya na yana umuhimu wa kipekee katika nchi na jamii, yenye mchanganyiko wa mataifa, makabila au rangi za watu. Ukatili na ugomvi kutokana na ukorofi katika miaka ya hivi karibuni katika sehemu nyingi duniani ni matokeo yanayoelezea watu wengine kuwa ni duni, wasiowaaminifu au wasiostaarabika, vikionekana kama ni sehemu ya mawazo ya asili ya Mwanadamu. Aidha Biblia inasema kinyume chake kwamba mawazo na tabia kama hizo hazina nafasi katika mioyo ya wale watakaokuwa Wanafunzi wa Yesu. Paulo, mtume wa Yesu aliishi wakati utumwa ukikubalika kama sehemu ya Utawala wa Kirumi. Kuwa miongozo na maagizo mengi katika Waraka wa Paulo kuhusu mahusiano kati ya wale mabwana na watumwa ambao walikuwa Wanafunzi wa Yesu. Angalia waraka huu kwa Makanisa yaliyoko Galatia sura ya 3 mistari ya 26 hadi 29. Hapa Paulo anasema waziwazi kwamba Wanafunzi wote wa Yesu wako sawa mbele ya macho ya Mungu. Hakuna tofauti kati ya mwanaume na mwanamke kati ya rangi ya ngozi au jamii atokayo mtu. Tunapozungumza na watu tunaoishi nao au kufanya kazi pamoja, ni rahisi sana kutumia maneno yenye kuashiria vurumai na kutokuelewana ambayo yatawaumiza au kuwakatisha tamaa wengine, na Yakobo aliandika juu ya jambo hili pia angalia katika Waraka wake sura ya 3 mistari ya 5 hadi 11. Maneno magumu yazungumziwapo hayawezi kurejewa kama ilivyo tofauti kwetu sisi zote katika utu, mara nyingi wale wenye hasira za haraka wanapaswa kuwa waangalifu. Mungu kupitia Malaika wake anajua mambo tunayoyazungumza. Matumizi ya hukumu yanakuwa na umuhimu kwetu inapokuwa kati ya mema na mabaya, au iliyo kweli na isiyo kweli lakini tunapoitumia hukumu hiyo hiyo kwa watu wengine tunatakiwa kuwa waanglifu zaidi. Yesu anatupa ushauri wa maana kuhusu jambo hili na umeandikwa katika Mathayo sura ya 7 mistari ya 1 haadi 5. Kutokana na maneno haya pengine inawezekana ukaamua kutokumuhukumu mtu mwingine lakini siyo rahisi kushikilia msimamo huu. Yesu anaunganisha maagizo yake kwa mfano mdogo. Ufunuo wa kuyaelewa maneno yake ni kutokana na maelezo kuhusu, "Kuangalia kibanzi katika jicho la ndugu yetu"! Jambo hili linazua lawama mara moja kwa watu wengine, na huku tukipuuzia mapungufu yetu mbele za Mungu. Kuna wakati ambapo tunatakiwa kuwa waangalifu katika maamuzi yetu na Yesu anatoa mfano katika Mathayo sura ya 7 mistari ya 15 na 16. Ushauri huu bila shaka ulikuwa na maana katika miaka ya mwanzo ya Kanisa la Kikristo wakati ambapo kulikuwa na walimu wengi wa uongo ambao hata walidiriki kujiita Kristo. Halikadhalika ni muhimu leo ambapo kuna Makanisa mengi na walimu. Aidha kipimo muhimu ni " Mtawatambua kwa matunda yao" Wanayofanya wanaume na pengine hata wanawake katika maisha yao yanakuwa wazi kuliko yale wanayohubiri. Baada ya Yesu kuwachagua Wanafunzi wake alianza kuwafundisha jinsi ya kufanya mambo ambayo yangempendeza Mungu, na mengi ya mambo ya haya yamo katika Injili ya Mathayo sura ya 5,6,7. Sasa hebu na tuangalie kwa pamoja katika sura ya 5, tusome kuanzia mstari wa 21. Yesu ananukuu kutoka katika sheria za Kiyahudi za Musa ambazo zinaanzia miaka ya nyuma wakati Taifa la Israeli lilipo okolewa kutoka katika utumwa wa nchi ya Misri Hapa anaeleza kwamba wakati wa Sheria za zamani zilithibiti matendo ya Wayahudi, sheria zake mpya zitakuwa mbele zaidi kwa kuthibiti mawazo yao na hata hisia zao. Anazungumzia juu ya hasira, maneno ya matusi na mawazo ya tamaa mbaya. Anazungumzia juu ya uvunjifu wa ndoa unatokea mara nyingi kutokana na tamaa ya uzinzi na wengine nje ya ndoa. Katika mstari wa 33 Yesu ameonya juu ya kuapa kusikokuwa kwa ishara. Kwa kufanya hivyo wanatumia maneno ambayo wenzao watayakubali kuwa ni ya kweli na yakuaminika. Kwa bahati mbaya, wanachagua kutumia maneno ambayo ni Matakatifu kwa Mungu na ambayo amekataza kuyatumia. Hata kama tunafikiria tu katika mawazo yetu, ni muhimu kuwa daima tunakumbuka agizo lake katika Kutoka sura ya 20 msatri wa 7. Kama ulivyo utaratibu wa kawaida, Yesu anasema "Usiape kabisa - Mathayo sura ya 5 mstari wa 34. Ni afadhali kabisa kutokutumia viapo wakati wowote na hii inajumuisha Mahakama ya Sheria ikiwa tutajikuta katika mahali kama hapo. Aidha mara nyingi nafasi imewekwa kwa wafuasi wa Yesu kuthibitisha kabla ya kutoa ushahidi. Matumizi ya kuapishw kama njia ya kuelezea tufikirie nini juu ya wengine yamekwisha kushughulikiwa na Yesu katika maagizo yake kwamba tuwe waangalifu kwa yale tunayosema, mstari wa 22. Katika mstaari wa 44, agizo la kuwapenda jirani zetu, hatua nyingi zaidi zimechukuliwa. Sasa Yesu anatuambia tuwapende maadui zetu! Kuwabariki wale wanaotulaani na kuwatendea mema wale wanaotuchukia! Kuwaombea hata wale watu wanaotudhuru. Haitakuwa rahisi kuyazingatia maagizo haya kwa kuwa hisia zetu za asili ni kufanya yaliyo kinyume. Hata hivyo ni wazi kuwa yote hii ni mifano tu iliyotolewa na Yesu jinsi tunavyowafikiria wengine na jambo hili ni la muhimu kwa Mungu. Pengine msaada muhimu wa kutuongoza ni kuona jinsi Yesu alivyoonyesha kwa matendo kwa wale katili waliompiga na kumpigilia misumari katika msalaba. Maneno yake yaliandikwa na Luka katika sura ya 23 mistari ya 33 na 34. Ikiwa Yesu aliweza kusamehe akiwa katika maumivu na uchungu yumkini sisi tunaotaka kuwa Wanafunzi wake ni lazima tujifunze kufuata mfano wake ambao ni wa muhimu sana kwetu . Majivuno na kiburi havina nafasi mbele ya Mungu, katika matendo yetu lakini muhimu zaidi ni katika mioyo yetu na mawazo. Kwa kumalizia somo hili, hebu na tuangalie pamoja katika baadhi ya maneno ya Isaya sura ya 66 katika utabiri wake, mistari yaa 1 na 2. Inatupatia fununu ya mambo ambayo Mungu anataka kutoka kwetu na mwenendo wa utu wa kumpendeza Mungu. CBM Publishing, 32 Blenheim Rd, Far Cotton, Northampton NN4 8NW United Kingdom PO Box 2950, Mbeya, Tanzania (East Africa) ___________________________________ MAISHA YA MKRISTO. SOMO LA 7. Mpende Jirani yako. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUTAFUTA KUMBUKUMBU REJEA ZOTE. Katika somo hili tutatilia mkazo juu ya agizo la Yesu kwamba ikiwa kweli tunataka kuwa wanafunzi wake, tunapaswa kuonyesha katika maisha yetu upendo wa kupita kiasi kwa watu wengine. Mahali pa kuanzia katika somo hili ni mfano uliotajwa katika somo lililopita, msamaria Mwema. Tukiangalia kwa makini maneno ya Yesu katika Luka sura ya 10 mistari ya 30 hadi 37 tunaona mambo mengi muhimu. Kwanza, kwamba Yesu alimchagua Msamaria kumweka katika mfano huu kwa kuwa Wasamaria walichukiwa na Wayahudi, walidharauliwa kama watu duni. Pili, kwamba mtu aliyeshambuliwa na wezi hakusaidiwa na watu wawili ambao ndiyo wangalikuwa wa kwanza kumsaidia. Kwa kuwa Makuhani walitoka katika kabila la Lawi wakati wa Sheria za Musa waliopaswa kutoa huduma za afya na masaidiano mengine kuwaangalia watu wa Israeli kwa jumla. Alikuwa ni Msamaria aliyeonyesha upendo na huruma na alionyesha mambo haya ya msaada kwa vitendo. Alisafisha majeraha, alimchukua mtu aliyeumia juu ya punda wake na kumpeleka mahali pa usalama ili apumzike. Mwisho alikuwa ni yeye aliyewezesha mtu aliyeumia baadaye kupata mahitaji yote muhimu yaliyotakiwa. Tunaposoma katika Injili kuhusu matendo mengi ya kuponya yaliyofanywa na Yesu, mara nyingi mwandishi anamalizia kwa maneno "Na Yesu alikuwa na huruma" kwa mtu mgonjwa au katika kisa cha kijana aliyefariki, kwa mama yake aliyekuwa na majonzi. Angalia Luka sura ya 7 mistari ya 11 hadi 15. Mara baada ya Yesu kuchagua Wanafunzi wake kumi na wawili alianza kuwafundisha masomo ya upendo, msamaha na huruma. Sasa ukifungua katika Biblia yako katika Luka sura ya 6 mstari wa 17, tutaangalia pamoja mambo haya. Umati wa watu uliokuwa ukimsikiliza Yesu siku ile ulikuwa mkubwa sana na walikuwa wametoka mbali sana kuja kumuona. Wengi wao walikuja ama kuponywa au kuona vitendo vya Yesu akiponya. Aghalabu walikaa kusikiliza mafundisho yake juu ya Utume wa Mkristo na tutafanya vivyo hivyo tukitilia mkazo katika mistari ya 27 hadi 36. Hakuna mwingiliano kwamba yale tunayoyasoma katika Injili ya Luka karibu ni yale yale tuliyoyasoma katika Injili ya Mathayo katika somo letu lililopita. Habari hii ni muhimu sana katika Biblia. Linaloanza kama wazo katika fikira zetu mara nyingi linageuzwa kuwa kitendo, hivyo sheria za Yesu hazina budi kwanza kutawala mawazo yetu. Tunapoonyesha upendo na huruma kwa mtu mwingine, tunafanya hivyo kwa vitendo. Mara kabla ya Yesu kuondoka katika chumba cha juu alikokuwa akifurahia chakula cha mwisho na Wanafunzi wake kabla ya kifo chake, alirudia amri hii kuu kuhusu upendo. Tunaikuta katika Injili ya Yohana sura ya 13 mistari ya 34 hadi 35. Maneno yake yanahitaji mawazo makini kwani upendo wa Mkristo unaoonyeshwa na Wanafunzi wake hauna budi kuwa mkubwa kama ule ulioonyeshwa na Yesu kwa wanaume na wanawake wale katika nyakati zake na wote watakaomfuata kupitia historia. Alionyesha upendo wake kwa kukubali kufa katika msalaba ili wafuasi wake wote watakaoonyesha imani ya kweli wangekuwa na nafasi ya kuwa na maisha ya milele katika Ufalme wake katika dunia hii. Angalia katika Yohana sura ya 15 mistari ya 9 hadi 14 na ona jinsi amri hii ilivyorudiwa katika mstari wa 12 na mstari wa 17. Wakati Petro alipopinga kuwa asingethubutu kumkana Yesu, Yohana sura ya 13 mistari ya 36 hadi 38, Yesu alimwambia kwamba kabla ya alfajiri kabla ya jogoo kuwika utamkana Bwana wako mara tatu. Haya yalipotokea sawasawa kama Yesu alivyotabiri, Petro aliaibika, lakini alijifunza somo la kwamba chakula aina ya mkate na samaki kumpenda Bwana wake halikuwa jambo rahisi kulitelekeza unapokuwa katika shinikizo. Baada ya ufufuko wake, Yesu alikutana na Wanafunzi wake katika Galilaya ya Kaskazini ambako miongoni mwao saba waliamua kuchukua mtumbwi na kwenda kuvua samaki. Waliungana na Yesu katika Pwani ambako alikuwa ameandaa - Yohana sura ya 21 mstari wa 9. Ni muhimu kuelewa kuwa Yesu alionyesha huruma yake kwa umati wa watu elfu tano na baadae elfu nne kwa miujiza kuwalisha mikate na samaki. Baada ya chakula katika Pwani ya bahari ya Galilaya, Yesu alimalizia somo la Upendo kwa kumuuliza Petro mara tatu kuhusu upendo wake kwa Bwana wake. Yesu aliongeza maneno mpya katika maagizo yake ya awali - mistari y 15 hadi 17; aghalabu mara kwa mara Petro aliposema anampenda Yesu alipewa agizo na majukumu "lisha kondoo wangu" ,"lisha kondoo wangu". Katika miaka ya mwanzo ya Kanisa jipya, kulikuwa na kondoo wengi (wanafunzi wapya) waliotakiwa kuangaliwa. Kadri makanisa mapya yalivyoanzishwa katika sehemu nyingi za Israeli na nchi nyingine, vivyo hivyo majukumu yalibadirika na kwa hiyo ilikuwako haja ya kuyaangalia makundi yaliyokuwa yameanzishwa (Kondoo). Paulo alitumia lugha ile ile katika ujumbe wake wa kuagana na wazee wa kanisa la Waefeso - tazama Matendo ya Mitume sura ya 20 mistari ya 28 na 29. Mtume Yohana pia alijifunza somo hili la maana la Upendo kutoka kwa Yesu. Akiwa ametundikwa katika msalaba, Yesu alimwambia na kumkabidhi majukumu juu ya mama yake Maria. Utayakuta haya katika Injili ya Yohana sura ya 19 mistari ya 26 na 27. Takribani miaka 50 baadae, Yohana aliandika waraka ambao alitarajia kusomwa na makanisa yote. Katika waraka huo alielezea tu sheria ya Upendo wa Wakristo. Tafuta waraka wa kwanza wa Yohana na angalia katika sura ya 4 mistari ya 7 hadi 21. Soma haya kwa uangalifu kwani yana umuhimu wa pekee katika nchi ambako kuna chuki ya kutisha kati ya sehemu moja ya jamii na nyingine, kichaa cha mauaji ya halaiki cha kutaka kuteketezwa kati ya kabila na kabila. Vita kati ya sehemu moja na nyingine, mji na mji, kijiji na kijiji. Chuki na uchungu kati ya ukoo na ukoo. Maneno ya Yohana ni ya dhati na hayana mashaka katika mawazo ya watu. Haiwezekani kuwa Mwanafunzi wa Kristo kusema kwamba tunampenda Mungu wakati huo huo kuwachukia Wakristo wenzetu katika mioyo yetu. Kama mtu atasema anampenda Mungu na kumchukia ndugu yake ni mwongo. Haiwezekani kuyaepuka maneno haya, na kwa wale wanaotaka kubatizwa au wale waliobatizwa karibuni, hili ni somo muhimu. Kwetu sisi kuna mambo mengi muhimu ya kukumbukwa kutoka katika maneno haya ambayo ningependa kuyatumia kwa uangalifu kama kumbukumbu ya somo hili. 1. Mstari wa 7 "Upendo ni wa Mungu" hii ina maana kwamba wakati wa uumbaji, uwezo wa kutokujipenda ulijengwa kwa mapenzi ya Mungu. Anatutaka tuitikie wito wake wa Upendo na Upendo wa Yesu kwetu sisi. 2. Mstari wa 10 Mungu alimtuma Yesu kama dhabihu kwa ajili ya dhambi zetu. Hiki ni kipimo cha Upendo wake kwetu sisi. 3. Mstari wa 11 kwa sababu Mungu anatupenda, tunapaswa kuonyesha upendo kwa wengine. 4. Mstari wa 12 - Tunapoonyesha upendo huu tuliopewa na Mungu kwa wengine, kuna jambo ambalo ni la Mungu ndani yetu. 5. Mstari wa 17 - Tunapoweza kwa dhati kuhisi kwamba tunao uwezo wa kuonyesha upendo tuliopewa na Mungu kwa wengine, hatutakuwa na hofu ya hukumu wakati wa kurudi kwa Yesu. 6. Mstari wa 18 - "Upendo kamilifu unaondoa hofu". Kuna manufaa ya uhakika kwa wale wanaoweza kuonyesha upendo wa aina hii. 7. Mistari ya 20 na 21: Hivi ni vifungu tulivyoviangalia tayari lakini kwa sababu ya ongezeko la mauaji na uadui kati ya watu katika nchi nyingi duniani, nataka kutilia mkazo umuhimu wa ujumbe huu. Hatuwezi kumpenda Mungu na kumchukia ndugu yetu. Kwanza kabisa Yohana anazungumzia kuhusu Wanafunzi wa Yesu waliobatizwa, hakuna udhuru ya uadui kati yetu. Kama jirani ya mtu, katika mfano wa Yesu, alikuwa Msamaria, vivyo hivyo jirani yetu anaweza kuwa mtu yeyote anayehitaji msaada wetu. Katika maana pana zaidi ya majirani kuwa ni watu tunaokutana nao kila siku, tuna kazi kubwa mbele yetu. Kwa bahati nzuri hatuna haja ya kujiingiza katika mambo ya watu wanaotupita kila siku lakini tukifanya hivyo amri ya Yesu sharti ikumbukwe. "Mpende Mungu na jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe. CBM Publishing, 32 Blenheim Rd, Far Cotton, Northampton NN4 8NW United Kingdom PO Box 2950, Mbeya, Tanzania (East Africa) ___________________________________ MAISHA YA MKRISTO. SOMO LA 8. Mafundisho ya Biblia kuhusu Mateso TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUTAFUTA KUMBUKUMBU REJEA ZOTE. Ni muhimu kwamba tayari umekwisha kujifunza masomo yanayohusu Uwoga, tumaini, Imani na Sala kwa sababu mambo uliyojifunza yatakusaidia kulielewa somo hili. Mateso ni tatizo katika maisha linaloweza kumuathiri kila mtu. Mtoto anazaliwa kipofu au mlemavu na tunauliza "Imekuwaje"? mtoto hajafanya makosa yoyote. Wanaume na Wanawake, Vijana kwa Wazee, Matajiri na Masikini wanataabika kutokana na maumivu ya magonjwa ya kukatisha tamaa ambayo mwisho wake ni kifo. Kwa nini wapate mateso?. Adhabu kali na kifo vimepenyezwa kwa mamilioni ya watu wasio na msaada na mtu mwenye mabavu na uharibifu wa Jamii ya kisasa. Maisha yamepotea kutokana na vitendo vya ugaidi na makosa ya jinai. Mara nyingi zimekuwepo vurugu katika historia yote ya dunia, lakini, pamoja na idadi kubwa ya watu na ongezeko la uwezo wa kuharibu leo kiwango cha majanga (maafa) mara nyingi ni cha kutisha. Watu huuliza "Kwa nini Mungu anaruhusu mambo haya kutokea"?. Swali hili aghalabu linakubali kwamba Mungu yuko na inatarajiwa kwamba Mungu daima anatenda katika wema. Kinachoangaliwa kabisa ni sababu za mateso katika dunia. Sababu hii inaweza kujumuishwa kama ifuatavyo:- 1. Katika Edeni, Mwanadamu alichagua kwenda njia yake kuliko njia ya Mungu na kujiletea ahadi ya adhabu ya kifo. Hata hivyo hii ilikuwa ni sehemu tu ya adhabu tazama kitabu cha Mwanzo kifungu cha 3 mistari ya 16 haadi 19. Maisha ya Mwanaume na Mwanamke wa Kwanza yalianza kuwa magumu sana. 2. Kwa sehemu kubwa mateso ya wanaume na wanawake ni matokeo ya ukatili wa watu wengine. Tangu mauaji ya kwanza Kaini alipomuua ndugu yake Abeli, Biblia imeorodhesha Vita, hofu kuu, mauaji na udanganyifu. Kwa jambo lolote ambalo tumelieleza kwa kuwa kwa kila tendo la ukatili kuna jukumu la mabaya litafuata. Matokeo yake hayakwepeki. Hii ni sheria rahisi ya Tendo na matokeo. Nyongeza kwa hili ni matendo ya kizazi kimoja yanavyoleta maafa kwa kizazi kinachofuata. Vitu kama siraha za sumu, ambazo huiharibu ardhi, bahari hata yamkini kizazi cha watu kwa kuwasababishia ulemavu, kuharibu (macho) uwezo wa kuona, kusikia au uwezo wa kutembea, haya yanasababishwa na watu. Mateso tuliyojiletea sisi wenyewe hatuwezi kumhusisha Mungu. Mikataba yote ya nchi ya kuzuia kutengeneza mabomu na siraha za maangamizi zilizokuwa zimewekwa tayari na majeshi wakisubiri amri kutoka kwa Serikali ya Kibinadamu. 3. Mwanadamu anaishi katika Ulimwengu unaodhibitiwa na sheria za fizikia zinazoonekana za asili na zisizokuwa za asili. Kisababishi na matokeo yake ni ya kawaida kwa mazingira yetu na maafa makubwa ya asili kama Volkano, Matetemeko, Mawimbi ya baharini, Ukame na Mafuriko yanayoleta mateso yasiyoweza kusemekana kwa wanadamu bila ya uchaguzi. Iwapo tunafikiri kwamba Mungu ndiye anazielekeza nguvu hizi kubwa, je tunamtaka yeye kwa namna moja na nyingine atumie uwezo wake wakuchagua ambapo watu wabaya tu ndiyo watauawa na watu wazuri watanusurika?. Katika Injili ya Luka kuna maandiko kuhusu Yesu alipoulizwa juu ya uhusiano kati ya dhambi na mateso. Utayakuta haya katika sura ya 13 mistari ya 1 hadi 5. Fundisho la Yesu ni la wazi na la kueleweka hata leo kwetu sisi. Maafa hayawatafuti wale wenye dhambi na kuwapata wenyewe tu. Mambo haya sio matokeo ya dhambi. Utendaji kazi mbaya au pengine tetemeko la ardhi, katika kisa cha mnara wa Siloam na utawala wa ukatili na wa kutisha wa Kirumi katika matukio ya wale waliouawa katika Sinagogi. Yesu ni mwangalifu kutaja sawia kwamba wajibu wa mtu mbele ya Mungu siyo kujenga hisia za uchawi katika matukio kama hayo ,lakini badala yake yanakuonya na mtu afahamu kwamba maisha ya mwanadamu kuwa ni mafupi na toba na ubatizo usiahirishwe kwa siku nyingine kwa sababu inawezekana isiwepo siku nyingine kwetu sisi. Sasa nataka kugeukia suala lingine la mateso. Mithali sura ya 3 mistari ya 11 na 12 inatuambia kwamba yatakuwepo majaribu katika maisha kwa wale ambao ni waaminifu. Hii ni kwa sababu Mungu anawapenda na kwamba huwarudi kama ilivyo watoto katika familia aghalabu hurudiwa na baba au mama anavyowachunga na anataka wafundishwe vizuri kwa maisha ya baadaye. Kurudiwa ambako katika somo hili neno lingine ni mateso ambayo ni namna ya mafundisho ya Kiroho na yanapaswa kuonekana kama ushahidi wa Upendo wa Mungu kwetu sisi. Paulo alitumia nukuu hii kutoka katika Waraka wake kwa Waebrania sura ya 12 mistari ya 5 hadi 13. Hoja aliyoitoa katika Waraka ule imeelezwa vizuri zaidi katika Waraka wake wa pili kwa Wakorintho sura ya 12 mistari ya 7 hadi 10. Paulo, mtume aliyechaguliwa kwa Mataifa, mtu ambaye zaidi ya mara moja alipokea moja kwa moja ufunuo wa Yesu alimwelekeza na kumsaidia, alikuwa na ulemavu wa kudumu kiasi kwamba ulimsumbua na hivyo aliomba kwa Mungu mara tatu ili kuponywa. Paulo katika hoja yake aliweza kupata jibu kutoka kwa Mungu - mstati wa 9. "Neema yangu yakutosha, maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu". Ni wazi kwamba Paulo aliyakubali maneno haya kutoka kwa Mungu na kuendelea na kazi yake ya kusafiri na kuhubiri hadi siku alipokuwa mfungwa wa Warumi. Pia hatuna budi kujifunza somo lile kutoka katika maneno ya Mungu, udhaifu au mateso ni jambo ambalo tunapaswa kukubali katika maisha yetu. Tusikubali yatuharibie maisha yetu na tusiruhusu kuingilia kumwabudu kwetu Mungu na mwanae, Bwana wetu Yesu Kristo. Hata tunaweza kuelewa mateso kuwa njia ya kupunguza anasa na uharibifu wa dunia inayotuzunguka ili kwamba tukaribie uhusiano wa Mungu na Yesu. Hakika hii ilikuwa kweli kwa wengi wa Watumishi wa Mungu kutoka Nyakati za Agano la Kale kwa kuwa walijaribiwa sana katika maisha yao hata hivyo imani yao kwa Mungu yaliendelea kuwa na nguvu zaidi kutokana na majaribu hayo. Wengi wao wanaume na wanawake tayari tumekutana nao katika masomo haya na utakumbuka majina yao. Ayubu, Abrahamu, Josefu, Eliya, Danieli na Jeremia ni baadhi tu ya uchaguzi wangu kutoka katika wengi ambao ni mifano kwetu. Kwa hiyo tumeona kwa makini kuhusu mateso ya mwanadamu na sasa ninataka umfikirie sasa Mungu mwenyewe. Je aliweza kuteseka wakati Israeli watu wateule wake walipomuasi? Je anateseka leo hii kwa ajili ya watu wenye mioyo migumu na kwa ukatili wanaowafanyia wenzao wanaume kwa wanawake?. Fungua Biblia yako Injili ya Yohana sura y 3 mistari ya 14 hadi 17. Hakika haya ni mateso makubwa sana ambayo angeruhusu mwanaye wa pekee kupigwa na hatimaye kifo kwa kusulibiwa msalabani ili dhambi za binadamu zisamehewe ili wanaume na wanawake wenye imani waweze kuwa na tumaini la uhakika la ufufuo na uzima wa milele. Yesu alikuja katika asili ya binadamu, alishiriki asili yetu ya udhaifu na kustahimili majaribu yaliyompata na mateso yote yaliyo ya kawaida kwa wanadamu wote. Maisha haya ya kawaida, aliishi kwa ajili yetu, yamefafanuliwa katika Waebrania sura ya 2 mistari ya 10 hadi 18. Hapa tunapata fundisho muhimu. Yesu "alikamilishwa kupitia mateso" mstari wa 10, ili aweze kuwasaidia wote wanaojaribiwa, mstari wa 18. Katika Waraka kwa Waebrania sura ya 5 mstari wa 8 tunasoma kuwa Yesu alijifunza kutii kutokana na mateso yaliyompata. Kuteswa kwa ajili ya Mungu ikiwa, kwa kumtii Baba, Yesu alivumilia, matatizo yote ambayo ni maisha ya mwanadamu yanafanyika upya. Pasipo imani tunapoteswa kwa ajili ya Mungu ni kuendelea kuishi maisha ya dhambi. Kwa imani na kupitia mfano wa Yesu aliotuwekea, ni dhahiri kuwa njia ya mateso imani yetu husafishwa (hutakasika). Inawezekana Mungu akaleta mateso kwa mwanafunzi ili iwe njia ya mwanafunzi kunyenyekea. Bwana anapoturudi ieleweke kuwa ni njia ya Uungu katika kufundisha. Tunapoadhibiwa tushukuru na tumwabudu Mungu; kama tumeteseka katika maisha yetu na tukastahimili na kuzidi kumkaribia Mungu ieleweke kuwa hata yeye aliteseka na hupenda tupate nguvu kupitia uzoefu wetu. CBM Publishing, 32 Blenheim Rd, Far Cotton, Northampton NN4 8NW United Kingdom PO Box 2950, Mbeya, Tanzania (East Africa) ___________________________________ MAISHA YA MKRISTO SOMO LA 9 Kuishi Katika Hofu. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUTAFUTA KUMBUKUMBU REJEA ZOTE. Kwa wale wanaoishi katika nchi zenye Serikali nzuri ambako kuna amani na utawala wa Sheria ni rahisi kusema kwamba hofu ni jambo unaloweza kupambana nalo. Pambana na hofu ni kauli mbiu ya siku hizi. Katika miaka ya karibuni hata watu ambao wako katika nchi zenye amani wanakuwa wakijifunza inakuaje kuishi katika hofu mchana na usiku kwa sababu ya vita, mara nyingi vita vya mara kwa mara katika nchi zao. Kutokana na maafa ya asili kama matetemeko, volkano, mafuriko, maporomoko ya udongo wa milimani, pepo kali, vimbunga hutegemea wanaishi wapi katika dunia hii. Hofu hii inakuja kutokana na kutokujua nini kitakutokea baadaye, kutokna na mashambulizi ya ghafla juu ya mali yako au kutoweza kujisaidia wewe mwenyewe, familia yako au rafiki unapotishwa. Matukio ya ghafla na mstuko wa ghafla unaweza kumpata kila mtu, lakini kile kilichosababisha somo hili kuandikwa hasa ni kutuonyesha namna ya kuangalia na kuishinda hofu iliyoshindikana kuondoka. Hofu tuliyonayo mchana na usiku kwa siku nyingi, majuma au hata miaka. Kuna mifano ya wazi kabisa katika Biblia na sasa tunaweza kuisoma mifano hii pamoja ili kuona jinsi watu hawa walivyoathirika. Kwanza kabisa katika Kutoka sura ya 14 mstari wa 10 ambapo watu wa Israeli waliookolewa katika utumwa katika nchi ya Misri, wanagundua kwamba wanafuatiliwa na majeshi ya Wamisri yanayotaka kulipiza kisasi. Bahari iko mbele yao na Wamisri nyuma yao, kwa hali iwayo yoyote ile waliogopa. Mfano mwingine wakati huu ni kumbukumbu la Torati sura ya 28 mstari wa 63 hadi 67. Unaposoma maneno haya utaona kuwa yanaelezea hofu isiyoondoka. Mungu anawaambia watu wake kuwa hii itawatokea iwapo watamwacha na kuanza kuabudu Miungu iliyotengenezwa kwa mbao na mawe. Wayahudi walimwacha Mungu, na historia yao mpaka siku ya leo inajumuisha miaka mingi walioishi katika hofu kubwa. Katika Ujerumani, kati ya miaka ya 1939 na 1945, kati yao milioni 6 waliuawa kikatili kwa sababu tu walikuwa Wayahudi. Huu ni mfano wa kutisha wa kuishi katika hofu. Hofu ni mbaya zaidi ikiwa kitu chenyewe hakifahamiki. Inaweza kuathiri makundi mazima ya watu. Hofu kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine katika mazungumzo. Linapotokea kwako, jambo la kwanza unaloweza kufanya kama mtu binafsi ni kutambua kile kinachosababisha hofu. Nani au nini kiwajibike. Baada ya hapo inawezekana kuona jinsi gani unaweza kufanya juu ya kile kinachosababisha hofu. Kuikana nyumba yako, Kijiji chako, familia yako na marafiki zako, inaonekana kuwa ndiyo njia pekee ya busara unaweza kuichukua. Tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Kikristo, wafuasi wa Yesu wamekuwa wakiteswa kama ilivyo kwa watu wengine. Wakati mwingine ilikuwa hivyo kwa sababu ya kuwa Wakristo, hata hivyo haikuwakatisha tamaa kuwa wanafunzi, badala yake walizidi kuwa na nguvu zaidi katika imani yao na utiifu kwa Yesu. Kitabu cha Matendo ya Mitume kinatuambia kuhusu kazi ya kuhubiri iliyofanywa na Mitume katika nchi za Kaskazini ya bahari ya Mediteraniani inaonyesha kwamba kila walikoenda walitishwa na makundi ya Wayahudi walioishi katika maeneo hayo. Mitume walipigwa, walipigwa mawe hadi kufa na kutupwa katika magereza, lakini hatuoni kuwa waliogopa au kushindwa. Kinyume chake, mara nyingi Mungu aliwatuma Malaika wake kufungua milango ya magereza - Matendo sura ya 16 mistari ya 22 hadi 29. Hebu fikiria, Paulo na Sila kuumizwa kwao kulitokana na kupigwa hata wasiweze kulala, badala yake waliimba nyimbo za kumsifu Mungu (Labda kutoka katika Kitabu cha Zaburi). Kutoka katika siku za mwanzo za Kanisa la Yesu Wanafunzi walijua ilikuwaje kuishi katika hofu, hata hivyo hawakuruhusu itawale maisha yao. Badala yake Yesu alikuwa mtawala shupavu wa maisha yao na kwa sababu yake hawakukatishwa tamaa kwa kuogopa. Mfano wake mwenyewe, kutoka siku ile ya kutisha, akiwa anajua kuwa katika muda mfupi watu wakatili wangefika kumkamata na kumchukua kwenda kusulubiwa hata hivyo aliwatia moyo wafuasi wake wa wakati ule na atendelea kufanya vivyo hivyo kwetu sisi leo. Ni katika Injili ya Luka ambapo tunaweza kusoma hali ya wakati mgumu sana kwa Yesu sura ya 22 mstari wa 39. Sasa endelea kusoma mstari wa 44. Alijua kutokana na utabiri nini kingemtokea na kwa kuwa alikuwa mtu, aliogopa. Hata hivyo kwa kuwa alikuwa Mwana wa Mungu, alijua kwamba kifo hiki cha maumivu makali ilikuwa ndiyo thamani ambayo ni lazima kulipwa kwa sababu ya dhambi za wanadamu. Kwa ushupavu alisimama mahali alipolala kifudifudi akiwa katika kuomba Baba yake na kuondoka mahali pale penye usalama ili kukabiliana na wale waliokuwa washitaki wake wa uongo na hatimaye kifo chake. Yesu hakuwahi kuwa ahidi wafuasi wake maisha yasiyo na matatizo na hofu bali alionyesha kuwa maisha tunayoishi hivi sasa ni utangulizi katika Ufalme wake. Baadhi ya Wafuasi wake watafariki kwa sababu ya kuwa Wakristo lakini katika shabaha yake Mungu hawatapotea au kusahauliwa. Katika siku ya ufufuko, wataamka katika Dunia pamoja na wale wengine ambao wameishi na kufa kwa amani. Angalia katika maneno ya Yesu katika Luka sura ya 12 mistari ya 4 hadi 7. Katika maandiko haya kuzimu ni kaburi na wale ambao hawaukubali wito wa Mungu wa ukombozi watapumzishwa humo milele. Ikiwa tutajikabidhi mikononi mwa Mungu kuweka imani yetu kwa muumba mwenye nguvu Mungu aliyetuumba na kutuweka katika dunia hii kwa makusudi yake ya ajabu sana. Kutunyanyua juu ya athari za hofu tuna maneno ya kututia moyo kama yale yaliyo katika Waraka wa Paulo kwa Wakorintho sura ya 3 mstari wa 16. Msingi wa maisha yetu ni Yesu - mstari wa 11, kama tumebatizwa katika jina lake. Mistari ya 12 hadi 15 iko pale kutuonyesha wazi wazi kwamba ikiwa vitu vyetu vyote vimepotea lakini bado tuna imani, kwa hiyo bado tumeokoka katika makusudi ya Mungu. Sasa na turudi nyuma katika kitabu cha Kutoka sura ya 14 na tuone kilichowatokea wana wa Israeli. Kumbuka kuwa daima walikuwa katika hali ya mashaka, walijikuta kati kati ya bahari ya Shamu na Jeshi la Wamisri yakiwajongea karibu. Sasa angalia katika mstari wa 13 na endelea kusoma hadi mwisho wa kifungu hiki. Je uliona ushauri uliotolewa kwa watu wa Musa "Usiogope, simama tu na mkauone wokovu wa Bwana". Angalia katika Waraka wa kwanza wa Yohana sura ya 4 mistari ya 15 hadi 19. Mstari wa 15 unawataka wale wote ambao wamekuwa wakifikiria juu ya ubatizo lakini kwa hakika bado hawajaamua. Iwapo tumo "ndani ya Yesu" tumezungukwa na Upendo wake wa hakika na kwamba Upendo wa kweli unaondosha hofu. Kuna maneno mengine ya ajabu na ya kuliwaza katika Zaburi 34; jaribu kuisoma Zaburi hii. Haya yanaweza kubadilisha msimamo wetu juu y maisha; Angalia kwa makini mistari ya 4 hadi 8. Katika mstari wa 9 wa Zaburi hii, tunapewa mawazo mapya, ikiwa hofu itakuwepo katika maisha yetu basi iwe hofu ya tofauti, iliyo bora, hofu ambayo ni nzuri kwetu hofu ya Bwana Mungu. Ukisoma mstari wa 11 utakuta wito ulioandikwa na Daudi mtungaji wa Zaburi. Alikuwa ni mtu ambaye wakati wa ujana wake aliondoka kwenda kupigana na jitu la Filisti Goliati, kiwa na kombeo tu na mawe machache madogo hali akiwa na imani kuu kwa Mungu wake. Daudi anatupa ushauri mzuri, hofu ya Mungu ni safi na ni nzuri kwetu sisi. Hii ina maana kuwepo kwake. Daima tutamuheshimu Mungu na kutambua jinsi alivyokaribu nasi kupitia Malaika wake. Mambo tuyafanyayo katika maisha yetu yatakuwa ya uaminifu na mazuri na kama tunavyompenda Mungu ndivyo tutakavyoona rahisi kuwapenda jamaa zetu kama alivyofanya Yesu. Kumbuka hata wakati alipokuwa anasulubiwa msalabani akiwa katika maumivu makali mno, alimwomba Baba yake kusamehe. "Baba Uwasamehe kwani hawajui watendalo." Mtume Yohana anatueleza mengi juu ya Upendo katika maisha yetu lakini pia anatumbia juu ya hofu ya Mwanadamu na hii ndiyo sehemu nzuri ya kumalizia. CBM Publishing, 32 Blenheim Rd, Far Cotton, Northampton NN4 8NW United Kingdom PO Box 2950, Mbeya, Tanzania (East Africa) ___________________________________ MAISHA YA MKRISTO SOMO LA 10 Uaminifu mbele ya Mungu na Mwanae Yesu. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUTAFUTA KUMBUKUMBU REJEA ZOTE. Katika somo hili nataka kuangalia kwa makini katika mambo tuyafanyayo kila siku. Mengine yatakuwa kuhusu Mungu na kuhusu Yesu. Kama vile kuwahubiri wengine au kuwasaidia wagonjwa na wazee. Mengine yatahusu huduma na maongozi ya familia zetu au wale tulio na madaraka nao. Matendo mengine yote yatahusu watu ambao tunakutana nao kila siku, katika kazi, safarini au lolote linaloweza kujitokeza kila siku. Uaminifu unahusu kutii amri. Juu ya yote kutii amri za Jamii tunamoishi. Wakati mwingine, katika nyakati za Vita na maafa, sheria za Mwanadamu hudharauliwa, lakini mfuasi wa Yesu hakati tamaa kwa majaribu kama hayo kwani sheria zilizotolewa na Mungu na kuelezwa kwa uangalifu na Yesu na Wanafunzi wake, daima huwa mbele ya maisha yao. Katika somo la awali tayari tumeangalia katika mafundisho ya Zaburi 34 mstari wa 7. Haya ni maneno ya ajabu na ni kwazo kubwa katika wakati mgumu, lakini maneno yale yanatenda pande zote mbili. Iwapo Malaika wa Mungu wako karibu na watu wenye imani katika maisha yao ya kila siku, basi wako pale pia kusikiliza na kuangalia tunapokuwa wajanja na kutokuwa wa kweli, kusema uongo au kuchukua kisichokuwa chetu. Sasa fuatana nami katika maneno ya Paulo juu ya mada hii. Hebu natuangalie analotaka kusema. Kwanza halafu kwenye Waraka wake kwa Warumi sura ya 12 mstari wa 17. Paulo anasikitika jinsi wale wasio Wakristo wanavyomuona mtu anayemfuata Yesu. Kumbuka kuhubiri sio tu kusema yale tusemayo kwa wengine, ni pamoja na tuyafanyayo na jinsi tunavyoyafanya. Paulo anaendelea katika sura ya 13 mistari ya 12 hadi 14 kwa kutuambia juu ya matendo ya gizani; mambo ambayo watu huyatenda kwa udanganyifu wakifiri kuwa hawataonekana. Yesu alitumia wazo hili akizungumza na Nikodemu. Utayakuta haya katika Injili ya Yohana sura ya 3 mistari ya 19 hadi 21. Malengo ya mfuasi wa kweli wa Yesu ni kufanya mambo yote ambayo kwayo yataonekana katika nuru kamilifu na yawezekuoonekana kwa kila mtu, na Mungu na watu wengine. Je hii sio njia iliyo wazi kabisa ya kufundisha?. Katika Waraka wake kwa Wafilipi sura ya 4 mstari wa 8. Paulo anatushauri kufanya mambo mengine kama sheria katika maisha yetu. Mambo kama ukweli, uaminifu, haki, usafi, uadilifu, na mambo yenye kuashiria taarifa nzuri. Mambo haya yatajionyesha kwa wengine kwamba kwa hakika tunamfuata Yesu na wakati huo huo kuwa njia madhubuti ya mafunzo. Tunapokuwa tunazungumza kwa majirani zetu juu ya Yesu na Injili yake ya Ufalme, watakuwa tayari kuamini tunayoyasema. Inashangaza kusoma katika nyaraka za Paulo na Petro kuhusu inavyotupasa kuwa kwa wale wanao tutawala. Serikali zinatofautiana katika dunia hii, baadhi ni nzuri baadhi zimejaa rushwa, nyingine zina taratibu nzuri za utawala wa haki, nyingine ni za mabavu na ukatili na bado mitume walishauri kuonyesha uaminifu kwa wote wenye madaraka ya duniani. Hebu angalia katika Waraka wa kwanza wa Paulo kwa Timotheo sura ya 2 mistari ya 1 hadi 3. Maneno haya yaliandikwa wakati utawala wa Kirumi ukikazana kuwatesa Wakristo. Aghalabu yalikuwa mafundisho magumu kuyakubali na kuyaweka katika vitendo lakini pia yako pale kwa ajili yetu kuyafuata. Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kulipa kodi kwa Mtawala wa Warumi na katika maneno yake litupatia jambo moja la ziada la kukumbukwa. Hebu natuangalie maneno ya Yesu kama ilivyoandikwa na Mathayo katika sura ya 22 mistari ya 17 hadi 22. Maelekezo ni kutoa kwa jamii tunamoishi, malipo ya kodi na ushuru, lakini kwa Mungu tuonyeshe upendo wetu kwake na kutoa maisha yetu katika kumtumikia. Tulipoangalia ushauri wa Paulo alioutoa kwa Wakristo wa Wafilipi , je ulitambua maneno yoyote yenye sifa njema. Mambo ambayo kwa kawaida yalikubalika na wote kuwa ni mwafaka kwa wafuasi wa Yesu kuyafanya. Mambo ambayo haikuwa mtu mmoja aliyeamua bali uamuzi wa Wajumbe wa Kanisa wanaoaminika. Kuna mfano mwingine kama huo ambapo maoni ya Wanafunzi wenyeji wote yalitumika. Uko katika Matendo ya Mitume sura 6 mstari wa 3. Wengine, Kwa wakati ule ilikuwa muhimu kuwachagua watu wazuri zaidi walipokutana. Hawa wangekuwa mashemasi,viongozi na waongozaji wa wengine. Pengine ulikuwa ni uchaguzi mzuri uliofanywa kwa sababu tunazo habari za wawili tu kati ya watu hawa ambao walionekana kuwa watumishi wazuri wa kanisa watawala wenye uwezo wa kuongoza na wahubiri hodari. Somo la kutoka agano jipya limerudiwa mara kwa mara ? Fuata mafundisho ya Yesu na maelekezo na maelezo makini ya wanafunzi" Ingawaje kuna ushauri huu wa kibiblia, kama kawaida tunawategemea marafiki na wale tuliozoeana nao kwa ushauri wa kibinadamu. Je umewahi kufikilia ni nini kinachosababisha hata ushauriwe na mtu mwingine ili ukubali ushauri wao? Pengine ni wazee wenye uzoefu mkubwa katika maisha, wenye busara au waaminifu.Natuangalie mifano miwili ya watu waliotoa ushauri. Mfano wa kwanza tunaukuta katika kitabu cha hesabu sura ya 13 katika mpaka wa nchi ya ahadi Musa alikuwa amewatanguliza mbele ya taifa zima la israeli wapelelezi kumi na mbili ukisoma mistari ya 26 hadi 33 utaona taarifa ya wapelelezi inayofuatana. Kumi walirejea wakijawa na hofu na mashaka, na wawili tu ndiyo walikuwa na imani na uhakika kwamba mbele ya Mungu hakuna lisilowezekana. Sasa soma katika kifungu cha 14 na kwa uangalifu angalia maneno ya Kalebu na Joshua katika mistari ya 6 hadi 9. Ni nani unadhani watu hawa walimwamini? Ni bahati mbaya kwa wale kumi ambao hawakumwamini. Hasira ya Mungu kuambatana na uchaguzi wao inatuonyesha ni nani kati ya hao kumi na wawili walikuwa waaminifu, wakutegemewa na wenye imani. Walikuwa ni Kalebu na Joshua mshahara wao ulikuwa ni kuvuka hadi katika nchi ya Ahadi na familia yao ambapo wale wote waliokosa imani walifariki Jangwani. Mfano mwingine wa marafiki waliotoa ushauri unapatikana katika Kitabu cha Ayubu 42 mistari ya 7 hadi 10. Ilikuwa sawa kwa Ayubu kudharau ushauri wa Mwanadamu na badala yake kuzingatia imani katika Mungu. La muhimu kubaini ni kwamba watu wale watatu walijaribu kumsaidia Ayubu na walitumia muda mwingi wakijaribu kumliwaza katika huzuni aliyokuwa nayo, sura ya 2 mstari wa 13. Tatizo lao ni kuwa katika ushauri wao hawakutumia njia na maadili ya Mungu. Badala yake walitumia ubinadamu na hekima za mwanadamu. Hii ni tofauti ambayo hatuna budi kuangalia tunapopewa ushauri kutoka kwa marafiki. Mambo mengine yanayohusu uaminifu yanaonekana kuwa hayana maana, lakini kwa Mungu hata yale madogo tunayoyafanya ni muhimu kwake. Sasa anglia Unabii wa Mika sura ya 6 mstari wa 8. Baadhi ya mifano inapatikana katika mistari ya 10 na 11. Hebu fikiria mizani ya Wafanyabishara iliyorekebishwa kwa makusudi ili kupima kiasi kidogo cha bidhaa kisicholingana na kiasi kinacholipwa na mteja. Mfanyabishara atajifikiria kuwa ni mjanja na mwelevu lakini Mungu anamchukia Mfanyabishara huyu aliyejificha. Aidha yawezekana usiwe Mfanyabiashara, lakini je maneno haya yatakuhusu vipi? Katika maisha yetu tunawafanyia mambo wengine, aghalabu tuna ajira; katika mambo yote haya tunaweza kutumia nguvu zetu kwa bidii au kidogo tu. Tunaweza kulipwa au kutokulipwa mshahara wetu. Hali kadhalika tunapomtendea Mungu, tunaweza kumtolea zaidi au kidogo tu katika wakati na nguvu zetu. Udanganyifu unatokea tunapojifanya kwa Wakristo wenzetu kuwa tunajitolea vyote tulivyonavyo. Tunapokuwa tumepewa madaraka juu ya wengine au madaraka ya fedha, tunapaswa kukumbuka sana somo hili. Hata kama tutapata majaribu ya kutumia vibaya madaraka yetu, Mungu atajua tunachofikiria na tunatarajia kufanya nini kwa siri. Inawezekana kuficha matendo yetu kwa watu wengine lakini haiwezekani kuyaficha kwa Mungu. Somo hili linafafanuliwa barabara katika Matendo ya Mitume sura ya 5 mistari ya 1 hadi 11. Hapa mtu na mkewe walijaribu kumdanganya Mungu na Mitume. Mshahara wao wa udanganyifu ulikuwa mchungu na mkubwa. Unaweza kuona kwamba hii ni sawa kabisa na Utukufu wa kuwa na mizani au vipimo vya udanganyifu mahali pa soko na tunasoma katika Mika kwamba Mungu analichukia hili. Matukio ya Anania na Safira bila shaka yalikuwa mabaya kiasi cha kupelekea hatua za haraka kuhitajika kwani ni tukio la kipekee katika Agano jipya ambapo nguvu za Roho Mtakatifu zilitumika katika kutoa uhai. Katika hali nyingine zote ilitumika kuponya na hata kuwafufua wale waliokuwa wamefariki. Wakati Yesu aliporuhusu achukuliwe na askari, kupigwa na halafu kusulibiwa, alijitolea kila kitu kwetu. Aliyafanya haya ili watu waume kwa wanawake wawezeshwe kuwa na njia iliyofunguliwa na hatimaye kuokolewa kutoka katika uharibifu wa kifo. Hakukuwa na udanganyifu katika Yesu, daima alikuwa mwaminifu kamili na muwazi kwa wote waliomwendea. Katika mafundisho yake kuhusu misha ya Mkristo , alitupatia vipimo maalumu vya malengo yetu katika kumfuata. Angalia Injili ya Luka sura ya 6 na soma mistari ya 35 hadi 38. Maneno ya mwisho katika mstari wa 38 yanatukumbusha haja ya kujitolea kwa uaminifu iwapo tunataka kuupokea urithi wa Ufalme. CBM Publishing, 32 Blenheim Rd, Far Cotton, Northampton NN4 8NW United Kingdom PO Box 2950, Mbeya, Tanzania (East Africa)