MAISHA YA MKRISTO SOMO LA 1 TUMAINI NI ZAWADI YA THAMANI SANA KATIKA MAISHA YAKO. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUANGALIA VIFUNGU VYOTE REJEA. Tumaini ni kati ya zawadi (Vipawa) vya thamani sana kutoka kwa Mungu. Mungu kwa upendo wake kwetu, alifahamu sana kwamba watu watahitaji alipokuwa akishughulikia utu wetu; yeye amefanya iwezekane kwetu kuitegemea hata kama mazingira yangekuwa ya hatari sana. Hebu fungua Biblia yako na usome Waraka wa pili wa Mtume Paulo kwa Wathesalonike sura ya 2 mistari ya 16 na 17. Mwanzo kabisa wa sura za kitabu cha Biblia; tunaweza kufahamu watu walioishi maisha ya matumaini kuna uhusiano sana kati ya Tumaini na Imani na tutaangalia Imani katika somo la 11. Katika Waraka kwa Waebrania sura ya 11 mstari wa 1 tunasoma kwamba Imani ni kuwa na uhakika na mambo yatarajiwayo. Tunapotarajia ufahamu wetu unakuwa na picha za mambo tunayoyatazamia katika akili zetu, mambo yale tunayoyapenda kuyafanya kwa sababu sisi ni Wanadamu, kwa mambo yale tunayopenda yawe yetu. Tumaini ni kati ya mambo matatu ambayo Mtume Paulo aliyaona kuwa ndiyo hasa tabia ya kweli ya mwanafunzi wa Kristo. Imani, Tumaini na Upendo. Kwa sababu hiyo hebu tuwaangalie baadhi ya watu katika Biblia waliokuwa na tumaini na wachache ambao hawakuwa na tumaini. Tutaanza kwa kumwangalia Yesu Kristo kwa kuangalia maneno ya Mtume Petro aliyekuwa wa kwanza kati ya wanafunzi wake. Maneno hayo yanapatikana katika Matendo ya Mitume sura ya 2 mstari wa 26. Petro alikuwa akisema kuhusu Yesu lakini akitumia maneno ya Mfalme Daudi kutoka Zaburi 16 mstari wa 9. Kama wewe mwenyewe ndiye ungechukua nafasi ya YESU wakati alipokubali kwa hiari yake kukamatwa, na kuteswa na hatimaye kufa msalabani, utakubali ni kwa jinsi gani Unabii uliotabiriwa na Daudi katika Zaburi hii ulivyokuwa wa muhimu kuhusu Yesu. Kisha tutaangalia maneno machache ya Nabii Yeremia aliyeteseka mara nyingi kwa kuogopa kunena ujumbe wa MUNGU kwa watu wa Yerusalem. Aliwaeleza wao pamoja na Wafalme wao kwamba ili waishi ni lazima wajisalimishe kwa jeshi la Baberi. Hapo Yeremia aliteswa kama msaliti hadi kutupwa katika shimo lenye kina kirefu sana cha Jiji la Yerusalem. Soma Yeremia sura ya 38, sura ya 6 na usome habari hii. Katika maombolezo Yeremia anaelezea huzuni yake na mateso yake. Angalia maombolezo sura ya 3 mstari wa 1 na 6. Somo hili ni muhimu sana kwetu kwa kuwa katika mateso na hatari bado Yeremia aliweza kuyaona mambo yakienda sawa sawa. Katika mstari wa 18, tunaweza kujaribiwa namna hiyo katika siku za shida katika maisha yetu lakini hasa soma mistari ya 19 na 21. Yeremia mara akakubali kuwa alikuwa angali hai na maneno ya ajabu kwetu ya kukumbuka yanapatikana mistari ya 24 hadi 26. Kwa sababu hiyo Tumaini ni kusubiri jambo, tunatakiwa kungoja Wokovu kutoka kwa Mungu. Habari nyingi zimeandikwa kuhusu kurudi Yesu Kristo hapa duniani kuwa Mfalme. Tungependa itokee leo hii, maana kuna matatizo mengi sana hapa duniani ambayo yangeisha kabisa. Wanadamu ingawaje wamejitahidi kwa bidii zao lakini hata hivyo wameshindwa. Maneno ya Nabii Yeremia ni muhimu kwetu leo kuyakumbuka. Tuendelee kusubiri kwa saburi saa MUNGU aliyoiweka. Na sasa tufikirie mfano wa Abrahamu aliyeacha nyumba yake na vyote alivyokuwa navyo akifuata maono ya wakati ujao. Wakati Mungu alipomuahidi mambo ambayo yangetokea wakati ujao mbali, ni dhahiri kwamba Abrahamu angehitaji mtoto wa kuendelea baada yake na yamkini wajukuu na vijukuu! Abrahamu alikuwa na miaka 75 alipohamia Hanani na alikuwa na miaka 100, Isaka alipozaliwa Miaka 25, muda mrefu sana kusubiri kwa imani. Inatisha sana kuishi maisha ya bila ya matumaini kwa muda kidogo tu, Ayubu alikuwa katika hali hii Ayubu sura ya 7 mstari wa 3 hadi 7. Unaposoma matatizo yote yaliyompata yeye na familia yake ni rahisi sana kuelewa ni kwa nini alifikiria hivyo. Hata hivyo baada ya kupingana na ushauri wa rafiki zake aliyatarajia maisha yaliyoboreshwa na katika sura ya 19 licha ya maisha yake kuwa mabaya sana ikiwa ni pamoja na ugonjwa uliomsumbua ghafla alibadilisha kilio chake (maombolezo) na akanena mambo tunayoamini siku hizi kuhusu KIFO na Ufufuo. Tunapaswa kushangazwa na maono yake yaliyo halisi kuhusu wakati ujao na tumaini lake thabiti la milele kuwa yalikuwa kiini cha pekee katika nafsi yake. Soma mistari ya 25 hadi 27. " Nina mjua Mkombozi wangu yu hai". Haya ni maneno mazuri ya kuzingatia hasa tunapokuwa katika mateso na hata kuwa na dhiki katika maisha. Kwa hiyo tumaini ni muhimu sana kuwa nayo, tumaini katika ahadi zote za Mungu Baba kuwa zitatimia hapa duniani. Kwa kuwa maisha ya watu yataweza kuboreshwa. Bado njia nzuri ya kuweza kulielewa neno hili tumaini. Mitume wa Yesu walilitaja kuwa ni TUMAINI PEKEE, ilikuwa njia ya kuelezea imani kuhusu YESU na ufalme wake ujao, maneno waliyoyatumia ni: "Tumaini la uzima wa milele" Tito sura ya 3 mstari wa 7 "Tumaini la wokovu" Waraka wa kwanza kwa Wathesalonike sura ya 5 mstari wa 8 . "Tumaini la Utukufu" Wakolosai sura ya 1 mstari wa 27. Mtume Paulo aliandika katika Waraka kwa Warumi sura ya 4 mstari wa 18 kuwa - tumeokolewa kwa njia ya Imani na katika waraka wa kwanza kwa Wakorinto Sura ya 15 mstari wa 19 anatuhimiza ili tunyamaze na kufikiri. 'Kama katika maisha haya tu tumemtumaini Kristo, sisi tu maskini kuliko watu wote". Kuwa na tumaini kwa Wanasiasa, mabalozi (wanadiplomasia), maaskari, hata mashirika yanayojitolea sana kwa misaada ya kiutu kama vile Medecin Sans frontiers, Save the children (Okoa watoto), Oxfam na msalaba mwekundu kuwa yanaweza kubadili dunia [ulimwengu] kuwa mahali / sehemu nzuri ya kudumu ni dhahiri kuwa tutavunjika mioyo. Paulo anasema inakuwa tofauti kabisa wakati unapo tumaini katika Yesu kwa sababu amefufuka kutoka kaburini, yu hai, na atarudi tena duniani. Wakati Yesu atakaporudi kusimamisha ufalme wake, wanafunzi wake wote wa nyakati zote za historia (watafufuka) wataamka toka makaburini na ikiwa walitunza imani yao, watapewa uzima udumuo milele katika dunia ya kupendeza na ya amani. Bwana Yesu Kristo atakuwa Mfalme wa watu wote na atatawala kwa nguvu za Mungu, Kwa haki pamoja na hekima na upendo. Ubatizo katika jina la Yesu ni njia inayofungulia mambo haya mazuri sana. Mtume Petro aliandika katika waraka wake wa kwanza sura ya 1 mstari wa 3. Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu". Ubatizo ni kuzaliwa mara ya pili kwa ajili ya uzima mpya kama mwanafunzi wa Yesu. Tunapaswa kushirikisha wengine tumaini hili la uzima ambalo ni jema na linalo tosheleza katika maisha yetu. * Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu. 1Petro 3:15 MAISHA YA MKRISTO. SOMO LA 2 UMUHIMU NA MATOKEO YA SALA (MAOMBI) NIA YA UWEZESHAJI WA SALA. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUANGALIA VIFUNGU VYOTE REJEA. Kwani wafuasi wote wa Yesu, Sala ni ya lazima kama ilivyo kwa mtu kupumua ili aweze kuishi. Hata hivyo katika waraka kwa Waebrania kuna maelezo kuhusu Mungu ambayo ni muhimu kuyatafakari kwanza kabla ya kuanza kufikiria umuhimu wa sala. Hebu tazama Waebrania kifungu 11 mstari wa 6 na soma kwa uangalifu. Kuna mambo muhimu ambayo hatuna budi kujifunza kutokana na kumbukumbu rejea hii. Kama uakumbuka somo kuhusu imani, utabaini umuhimu wa imani kwa Mungu waliyokuwa nayo Mitume wa Yesu. Hapa tunaambiwa kwamba bila ya imani, haiwezekani kumpendeza Mungu. Aghalabu kwa wale wanaotaka kuwa Mitume, ni sharti waamini kuwa Mungu yupo na kwamba huwapa thawabu ikiwa wanamtafuta. Je unafikiri ni nini maana ya kumtafuta Mungu ? Je ungefanyaje ili kumtafuta Mungu ? Napendekeza kwamba njia ambayo miongoni mwetu tunaweza kuizingatia ni mifano miwili iliyoonyeshwa katika Matendo ya Mitume. Kwanza chunguza Matendo ya Mitume kifungu 8 mstari wa 27 hadi 30. Kule kuongoka na kubatizwa kwa Muethiopia kulianza kutokana na kununua nakala ya utabiri wa Isaya na kusoma ili ajaribu kuuelewa. Kwa kuwa alidhamiria kumtafuta Mungu katika neno lake, Mungu alimpa msaada aliouhitaji. Sasa angalia sura ya 10 mstari wa 1 hadi 5. Katika mfano huu Koronelio alikuwa akisali ili apate msaada sala yake ilisikika na mungu ambaye alimwambia atume wahudumu japo kumwuliza mtu ambaye jina lake aliitwa Petro. Mipango ya Petro kusafiri hadi Kaisaria ilitayalishwa ili akamweleze Koronelio kwa undani juu ya habari njema matoke yake Koronelio na familia yake walibatizwa. Halikadhalika leo, wale wote wanaotaka kumfuata yesu na kutaka kuwa watume wake, unaposali mungu husikia sala zako na atakujibu kwa njia ambayo itakuwa na faida kwako au kwa wale uwapendao Majibu ya sala yako yanawea kuwa kinyume cha matarajio yako, Daima yatakuwa yale Mungu anayolikiri kuwa ni ya manufaa kwako. Nataka kukuonyesha mifano mingi ambayo sala zilikuwa na matokeo ya kushangaza Hebu tuangaalie kitabu cha kwanza cha Samwel kifungu cha 1 mistari ya 9 hadi 20 kwa vile alikuwa mgumba Hawai bila shaka katika sala yake mara kwa mara alitamka maneno ya kutaka apate mtoto. Hata hivyo, likiwa tukio la maana ya pekee Mungu aliweza kusikia maombi yake na kujibu sala yake. Chunguza maneno ya Hawai "Nimeiacha roho yangu mbele za Bwana"!!. Hebu angalia Waraka wa Yakobo kifungu cha 5 mstari wa 17 na 18. Hapa Yakobo anasimulia juu ya Sala mbili za Mtume Eliya. Sala ya kwanza inahusu jinsi Mungu atakavyosimamisha mvua na ya pili kwamba mvua ingenyesha tena baada ya kupita miaka mitatu. Unaweza kusoma maelezo kamili katika kitabu cha Wafalme vifungu 17 na 18. Sababu zilizomfanya Mungu akubali sala ya Eliya kwa nguvu zote ni kwa kuwa na watu wa Ufalme wa Kaskazini ya Israel walikuwa wakiabudu sanamu na kudharau maonyo ya Mungu kupitia Manabii wake. Ukame huu mbaya na wa muda mrefu ilikuwa adhabu iliyotumwa kwao. Katika kitabu cha pili cha Wafalme sura ya 18 hadi 20 tunamkuta Mfalme aliyeitwa Hezekieli. Alikuwa mmoja wa wale wachache waliomwamini Mungu kweli kweli na kuzishika amri zake. Wafalme wa 2 sura ya 18 mstari wa 6 Wakati Yerusalemu ilipozingirwa na Waasari, Ezekia alisali kuomba msaada kwa Mungu; sura ya 19 mstari wa 15 hadi 19. Majibu ya Mungu yanapatikana katika mistari ya 32 hadi 35. Somo hili peke yake linadhihirisha matokeo Sala na tunaweza kujifunza mengi hata jinsi Ezekia alivyoendelea kumuomba msaada Mungu. Hebu angalia sura ya 20 mistari ya 1 hadi 6. Tunasoma jinsi Ezekia anavyoambiwa na Nabii Isaya kwamba angekufa kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua. Jibu la Ezekia ilikuwa ni kumuomba Mungu, mstari wa 3. Mungu anakubali tena mara moja. Isaya alikuwa hajaondoka Ikulu kabla ya Mungu kumuagiza arudi na kumwambia kwamba akamweleze Hezekia kuwa angepewa muda mwingine wa miaka kumi na tano ya kuishi. Pengine ungependa kusoma tena Sura ya 18,19, na 20 ili uweze kujua zaidi maisha ya Elia. Tumeangalia mifano kutoka katika Agano la Kale na Agano Jipya kuhusu nguvu na matokeo ya Sala; sasa inaatubidi tuangalie maagizo na mfano wa Yesu na Mitume wake. Sala fupi zilizo nyingi za Yesu kwa Mungu Baba yake tumeandikiwa katika vitabu vya Injili. Mahali pengine tumeambiwa tu kuwa alisali. Ningependa uangalie mfano mmoja wa sala iliyo muhimu ambayo utaipata katika Luka sura ya 6 mstari wa 12. Tunaa mbiwa na Luka kuwa Yesu alisali kwa Mungu usiku kucha kwa sababu siku ambayo ingefuata ingekuwa muhimu sana. Hana budi kuwachagua Mitume wake kumi na mbili amba watakuwa wafuasi wake wa karibu ili kuendeleza huduma yake. Hakudiriki kufanya kazi hii peke yake bali aliomba msaada. Funzo tunalolipata hapa ni kuwa tunapokabiliwa na maamuzi magumu, tunapaswa kuomba msaada kwa Mungu katika Sala. Akiwa anatokea chumba cha juu kuelekea Bustani ya Gertheman Yesu alifululiza kusali kwa Baba yake. Tunaweza kusma Sala hii katika Injili ya Yohana sura ya 17. Ningependa uangalie mistari miwili ya 9 na 20. Katika mstari wa 9 Yesu alionyesha kuwa sehemu hii ya Sala yake ilikuwa maalumu kwa Mitume wake na aliwabaini wao kama "Wao ambao nimepewa". Unapkuja katika mstari wa 20 utatambua kuwa Sala hii ilikuwa na mwelekeo wa mambo yajayo na ilijumuisha wale wote ambao watakuwa wanafunzi wa Yesu mpaka kufikia kipindi cha kurudi kwake duniani kama Mfalme. Angalia neno "wao pia niliopewa" inajumuisha wale ambao watakuwa wanafunzi baadaye. Kama unadhamiria kwa dhati kubatizwa kwa jina la Yesu, maneno haya yanakuhusu wewe pia. Kukuita utoke duniani na Mungu kukupa Yesu mwanae. Wazo hili ni la kushangaza na wewe pia unapaswa kuhamasika juu ya jambo hili. Katika Matayo kifungu cha 6 kutoka mistari ya 9 hadi 13 kuna mfano wa sala ambayo Yesu aliwapa Mitume watarajiwa wote hadi mwisho wa dunia. Inajumuisha mambo yote muhimu ambayo tunapaswa kuuliza na inaanza kwa kuuliza iwapo Ufalme utakuja na kwamba matakwa ya Mungu yatatimizwa duniani. Ukiangalia pia katika mistari ya 14 na 15 utaona kwamba Yesu alifikia mkazo haja ya kusamehe wengine. Tayari alikuwa amekwisha kutoa maagizo mahususi ikijumuisha sala ya mapema katika hotuba hiyo hiyo; sura ya 5 mstari wa 44. Agizo hili la mwisho linaonekana kuwa gumu kulitii lakini lina ujumbe uliotolewa na Yesu kwa moyo wake wa dhati. Unatambua watu wenye tabia maalumu ambao watakuwa watakatifu katika Ufalme ujao katika dunia hii. Iwapo tunaweza kuwaombea waliotukosea na ambao wanaotutesa basi tutakuwa tumeelewa tunachoambiwa na Injili. Katika orodha ya maagizo yaliyotolewa na Paulo kwa Wathesalonike katika Waraka wake wa kwanza sura ya 5 mstari wa 17, tunayakuta maneno "Sali bila ya ukomo". Mstari wa 18 unaendelea kuagiza, kushukuru kwa lolote. Anaposema kwa lolote, Paulo ana maana sio tu chakula na mavazi, mahali pa kujisetili na upendo kwa wengine lakini pia majukumu yetu ya kila siku ili kuyathibitisha kwa Mungu. Na kujithibitisha kwa Yesu kuwa tu wafuasi wake wa kweli na wa dhati. Tunapoangalia kwa makini sala aliyofanya Yesu kwa Baba yake katika Bustani ya Gethsemane tunaanza kuelewa hakika ushupavu wake wa kuelewa mpango wa Mungu kumkomboa mwanadamu kutoka katika kifo. Pia tumeanza kuelewa jinsi ushupavu na utiifu wa mapenzi ya Baba yake ulivyokuwa. Tazama Matayo sura ya 26 mistari ya 36 hadi 46. Hizi zilikuwa ni nyakati za huzuni kabla hajakamatwa kushitakiwa hatimaye kifo chake. Sala yake ya kwanza ilikuwa angehurumiwa vitisho na maumivu yaliyokuwa karibu kumpata. Iwapo Sala hiyo ingejibiwa hakika kusingekuwapo kwetu matumaini katika dunia hii. Hata hivyo Sala ya pili inakubali dhabihu ni lazima ifanyike mateso hayana budi kutokea, na maneno yenyewe ni " mapenzi yako yafanyike". Sala ya tatu ikirudia maneno yale yale na kutilia mkazo dhamira ya Yesu kujikabidhi afe kuwa ufumbuzi wa kutisha wa dhambi ya mwanadamu. Katika Sala hii ya Yesu kwa Baba yake na katika mifano mingine ya sala tuliyoitafakari, tumeona jinsi inavyowezekana kuzungumza na Mungu. Hata hivyo, leo Yesu ni mpatanishi wetu na hii ina maana kwamba anatuombea kwa Mungu. Kwa hiyo, tunaposali hatuna budi kuelekeza sala zetu kupitia kwa Yesu, Injili ya Yohana sura ya 14 mstari wa 12 hadi 14. Mahusiano uliyonayo wewe Mungu na Yesu kupitia Biblia yak yanawezekana kuwa ndiyo jibu la sala zako. Yanawezekana tayari unajua jinsi ya kusali, lakini kama hujui basi tunataraji somo hili fupi litakusaidia. MAISHA YA MKRISTO. SOMO LA 3 Imani na kufanya Ukristo kufanya kazi. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUANGALIA VIFUNGU VYOTE REJEA. Mpaka sasa katika masomo yetu mara nyingi sana tumekuwa tukitumia neno "IMANI. Ni wakati muafaka sasa kuangalia na kutafakari nini waandishi wa Biblia walikusudia kutuelewesha juu ya neno hili. Linaweza kutumiwa katika lugha ya kawaida kwa njia mbalimbali. Utaratibu wa kuabudu unaweza kuitwa "Imani; Iwapo tungetembea katika njia nyembamba na kuvuka korongo au mto mdogo, tungehitaji imani ambayo ni madhubuti kuweza kuubeba uzito wetu. Paulo katika Waraka wake kwa Waebrania sura ya 11 mstari wa 1 anatupatia maelezo ya "imani". Maneno haya yanachukuliwa kutoka katika Biblia ya toleo mpya la Kimataifa The New International Version ya Biblia. "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya mambo yasiyoonekana, Maana kwa hayo watu walishuhudiwa". Sasa unaelewa kutokana na masomo uliyomaliza kwamba katika Agano la Kale Mungu alionekana kuwa karibu sana na Abrahamu na familia yake mpaka kufikia wakati wa Manabii. Watu walioishi siku zile hawakuwa mbali sana na nyakati za mojawapo ya maajabu. Labda ilikuwa rahisi kwao kuwa na imani kwa Mungu na ahadi zake. Mungu alitarajia watu hao kuwa na "imani" na kuwazawadia walipoitikia. Nyakati za Yesu miujiza yake ndiyo iliyowashawishi watu wa nchi ya Israeli kuwa alikuwa mwana wa Mungu ambaye ni Mesihi. Angalia Injili ya Yohana sura ya 11 mistari ya 44 na 45 kuwa mfano wa haya. Leo hatuna maajabu ya waziwazi kama kuachana kwa Bahari Nyekundu hata kuhusu Waisraeli kuyatoroka majeshi ya Misri; Angalia kutoka sura ya 14 hususani mstari wa 13. Hatuna Manabii wa Mungu wanaotembea katika nchi na hatuwezi kusimama na kuangalia miujiza kama ile iliyofanywa na Yesu. Wewe ulichonacho ni Biblia, aghalabu matukio yote, ahadi na maonyo yaliyoandikwa humo kwa nguvu za Mungu ili tuweze kusoma. Kwa kielelezo cha kudumu cha kukukumbusha mpango wa Mungu kwa dunia hii na ahadi yake kwako binafsi kuwa mshiriki wa wakati ujao. Kwa hiyo leo imani ni uthibitisho wa ndani unaokuwanao katika mawazo yako. Utakuwepo huo kwa sababu ya yale unayoyasoma katika Biblia yako na kwa sababu ya mambo yale ulivyojifunza kutoka kwa wengine amba pia wana imani katika Neno la Mungu. Ninachotaka sasa kufanya ni kukuonyesha kwamba Mungu pia anatutarajia tuiweke imani katika vitendo. Mtume Yakobo katika Waraka wake anatueleza haya. Tazama sura ya 2 mistari ya 14 hadi 18. Je unakubali kuwa uhusiano kati ya imani na vitendo ni wazi? Jambo lingine muhimu la kutafakari linapatikana katika Sala ambalo pia ni unabii, limo katika kitabu cha kwanza cha Samueli sura ya 2 mstari wa 3. Humo tunasoma kuwa Mungu anatuangalia na kufikiria juu ya matendo yetu yote. Kwa hiyo yale tutendayo kwa sababu ya kuwa na imani ni muhimu sana. Mungu anajua kwamba tunahitaji msaada ili kuyatenda haya na tumepewa mifano mingi jinsi imani inavyoweza kuwa katika vitendo. Kuna mifano miwili katika kifungu tunachosoma katika Waraka wa Yakobo ilikuwa katika sura ya 2 na sasa tuangalie mistari ya 21 hadi 24. Kama ukifungua kitabu cha Mwanzo 22 na kusoma mistari 1 hadi 18 humo unaweza kusoma matukio yote. Kuainisha kwa ukamilifu imani ya Ibrahimu huna budi kukumbuka kwamba Mungu alikuwa ametoa ahadi maalumu kwake alipotokeza katika nchi ya Ur. Tunaweza kusoma haya katika kitabu cha Mwanzo sura ya 12 mistari ya 1 hadi 3. Ahadi hii ilimtaka Ibrahimu kuwa na mtoto ili familia yake iweze kuwa Taifa kubwa. Hatimaye alipata mtoto, Isaka yeye na mkewe wakiwa wazee sana. Haya yanatusaidia sisi kuelewa jinsi imani ya Ibrahimu ilivyojaribiwa alipoambiwa kumtoa kafara Isaka. Paulo katika Waebrania sura ya 11 mistari ya 17 hadi 19 anatuambia Ibrahimu alikuwa na mawazo gani alipokuwa akielekea mlimani. Isaka alikuwa muhimu katika ahadi aliyoweka Mungu, bila yeye ahadi isingelitimizwa kama ilivyokuwa yeye afe; Mungu angemrejesha katika uhai. Wewe ukijifanya kuwa katika nafasi ya Ibrahimu, utabaini jinsi gani imani yake ilivyokuwa na nguvu. Jambo lingine muhimu katika tukio hili ni kwamba Mungu alifanya haya sio tu kumjaribu Abrahamu, bali Mungu alikuwa tayari anajua ushupavu wa imani yake na unaweza kuona hili katika kitabu cha Mwanzo sura ya 15 mistari ya 3 hadi 6. Amri ya kumtoa dhabihu Isaka ilikuwa kumfundisha Abrahamu jinsi Mungu alivyokusudia kumkomboa mwanadamu. Ilimfundisha Abrahamu kwamba siku moja katika nyakati zijazo Mungu kama Baba atamruhusu mwanae pekee kuwa shabaha kwa ajili ya dhambi za Ulimwengu. Kwamba angefanya uwezekano wa misamaha, ufufuko na uzima wa milele kwa wanaume na wanawake wenye imani katika Mungu na mwanae Yesu Kristo. Mfano mwingine uliotolewa na Yakobo ni ule wa Rahabu. Kwa mara ya kwanza bila ya matarajio mtu wa Mataifa ambaye wala hakuwa Myahudi kahaba aliyekuwa anaishi katika Jiji la Kanani huko Jeriko. Alikuwa ni mtu pekee aliyeamini katika Mungu wa Wayahudi. Hata hivyo, Rahabu alikuwa anaelewa kuwa watu wengi waliokuwa wamejenga makambi yao katika ufuko wa mto Jordani, walikuwa warejeshewa nchi yao ya kale, nchi ambayo Abrahamu alipewa na Mungu. Wewe mwenyewe unaweza kusoma ili upate kujua kitu gani kilitokea katika kitabu cha Joshua sura ya 2. Jinsi maajabu ya kuta za jiji zilivyoanguka na Rahabu na familia yake peke yake walivyookolewa kwa sababu ya kuhatarisha maisha yake ili kuwaokoa majasusi ya Kiisraeli. Tukio hili bila shaka halikuwa la kawaida na ndiyo maana Yakobo na Paulo walitumia kama mfano wa imani. Katika Waebrania sura ya 11 kuna mifano mingi ya imani katika vitendo na sasa nataka kuangalia mwingine mmoja zaidi. Noah aliishi katika nyakati zilizokuwa na machafuko mengi miongoni mwa watu wa ustaarabu wa Kale. Angalia mwenyewe kitabu cha Mwanzo vifungu vya 6, 7 na 8. Angalia hususani sura ya 6 mistari ya 5 hadi hadi 7, ona ni miaka mingapi ilimchukuwa Nuhu kujenga Safina hii kubwa; sura ya 5 mstari wa 32 na sura ya 7 mstari wa 6. Miaka mia moja ni muda mwingi sana kwetu sisi lakini kwa Nuhu aliyeishi miaka 950 haikuwa hivyo. Bilashaka hakuna mtu mwingine aliyewahi kuunda mtumbwi mkubwa kama huu kabla. Katika miaka yote hii, Nuhu alimbidi kate miti mikubwa, ajifunze namna ya kutengeneza misumeno, kukata na kuziweka katika umbo mbao ambazo aghalabu wakati wa utengenezaji atazisawazisha na kuziunganisha vizuri ili zisivuje maji. Mti huu wa mvinje ilikuwa lazima uwe mkubwa sana na uwe mahali pa usalama kwa watu na wanyama, ndege na wadudu kwaa muda mrefu wa mwaka mmoja. Katika kutumia nguvu nyingi wakati wa miaka ile ya kuunda Safina, Nuhu aliongozwa na imani katika Mungu. Paulo anajumuisha katika mfano huu wa muhimu sana kwetu sisi katika Waebrania Sura ya11 mstari wa 7. Mpaka sasa tumejifunza nini katika somo hili? - Kwamba imani ni kuamini kuwa Mungu yuko na kwamba wakati wowote atafanya kile alichoahidi. - Kwamba haitoshi kusema tu tunaamini, Mungu daima anajua kuwa ni kweli. - Kwamba imani peke yake haitoshi, inatubidi kuiweka katika vitendo katika maisha yetu. - Kwamba Mungu wakati mwingine anatutarajia sisi kuendelea kaatika kitendo hicho kwa miaka mingi. Kama unafikiria kuamua kamainkubidi ubatizwe au kama tayari umemkubali Yesu katika ubatizo, utatakiwa kuelewa ina maanisha ni siku hadi siku. Je umeiwekaje imani yako katika vitendo? Hapa kuna mapendekezo kutoka kwa Paulo katika waraka wake kwa Warumi sura ya 12 mistari ya 9 hadi 18. Soma kwa uangalifu na tafakari iwapo yanaweza kukuhusu katika maisha yako. Paulo anatuambia kuwa tuheshimu Serikali za nchi yetu hata kama imejaa rushwa. Hii ina maana ya kuwa tuheshimu nguvu za sheria na utengamano. Angalia sura ya 13 mistari ya 1 hadi 5. Hii pi inajumuisha ulipaji wa kodi kwa uaminifu, mistari ya 6 na 7. Maagizo yaliyo mengi na yenye nguvu yanatoka kwa Yesu katika Mathayo sura ya 25. Soma mistari ya 31 hadi 40. Hapa Yesu anatueleza jinsi tunavyopaswa kuyaweka mafundisho yake yafanye kazi katika maisha yetu. Ni muhimu kuyakumbuka maneno haya. Yesu anazungumzia juu ya siku ya hukumu kwa kuwa katika siku ile hatutajaribu kiasi gani tunaelewa, lakini kiasi gni tumejaribu kuyafanya mafundisho yake katika matendo. MAISHA YA MKRISTO. SOMO LA 4. Itikio kwa Biblia na haja ya ubatizo. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUANGALIA VIFUNGU VYOTE REJEA. Wakati mtengenezaji wa vifaa vya nyumbani anaweka tangazo katika gazeti, watu ndiyo husoma na kuitikia kwa kununua bidhaa hizo. Wakati Mungu katika uumbaji wake aliyapa maua harufu na rangi za kung'ara ilikusudiwa hivyo ili kuvutia wadudu ambao wangesambaza poleni kutoka ua hadi ua jingine na hivyo kuruhusu mmea kutengeneza mbegu. Kwa njia kama hii Mungu alipotoa neno lake ambalo leo tunaita Biblia, alifanya hivyo ili wanaume na wanawake waweze kusoma na kuongozwa kwa kutii wito uliomo. Katika kila hali, sababu zitolewazo kwa lolote linalofanywa ni "Uhai". Mwenye kiwanda anataka Kampuni yake idumu na iendelee kupata faida, vichaka na maua sharti vizae mbegu ili jinsia yake iendelee kuishi, na Mungu katika neno lake Biblia ameahidi maisha ya milele kwa wote wanaofikia ujumbe wake. Watu hununua bidhaa katika maduka huweza kufanya hivyo kwa sababu inaonekana kuwa ni vema kufanya hivyo katika wakati huo. Ndege na wadudu wanaonekana kutojali huduma wanayoitoa kwa mimea na maua ili mradi wao watapata maji maji ya maua (utomvu) wa maua. Hata hivyo ni jambo tofauti unaposoma Biblia na kuongozwa kutii yaliyomo. Je unatakiwa ufanye nini? Yesu alisimulia mfano wa mpanzi akipanda mbegu kuelezea swali hili hili na ukifungua Biblia yako katika Luka sura ya 8 mistari ya 4 hadi 8 unaweza kusoma mwenyewe. Iwapo utaona maneno ya Yesu ni magumu kuyaelewa usijali kwani hata wanafunzi wake Yesu hawakuweza vile vile kuelewa na katika mstari wa 9 tunaambiwa kwamba waliomba ufafanuzi. "Mbegu ni neno la Mungu" Yesu alisema inaonekana na kusikiwa na watu wa aina mbalimbali. Wako wale wasioafiki wako sawa na mbegu iangukayo kandokando ya njia wengine wanaonekana kujali kidogo na mara wanaisogeza pembeni Biblia na kuendelea kufanya mambo mengine wanayofikiria ni muhimu. Aidha kuna watu wanaoafiki kwa furaha na kukubari kwa dhati kuwa wafuasi wa yesu lakini tabu na usumbufu wa maisha yao yanawafanya wawe na muda mfupi wakusoma, hupata muda wa kusali, hatimaye kukata tamaa kabisa . Hawa ndio watu wanaokatisha mbegu inayoangukia katika miiba. Mbegu inayoangukia katika ardhi nzuri inakuwa na kuzaa matunda. Hakika watu hawa watakuwa wanafunzi. Kwao Biblia ni kitabu muhimu sana katika misha yao. Wanapokuwa katika matatizowazo lao la kwanza ni kusali, kwamba msaada wa mwongozo hata kama watakumbana na upinzani hawamwachi Yesu awe njia ya mwamba wao. Hii ndio maana ya kumfuta yesu kwa dhati. Haiji kwa kujifunza injili tu, ni uthibitisho wa ndani ambayo ni ya utu binafsi. Uhusiano unaendelea kati yako na muumini yesu na mungu baba yake. Sasa angali Injili ya Yohana sura ya 14 mstari wa 23 yesu alikuwa akisema kwa marafiki wake wa karibu mutume. Yuda Iskarioti. Mtu ambaaye alimsaliti kwa askari wa kuhani mkuu alikuwa ameondoka kutoka katika chumba. Hii ni ahadi maalumu ya pekee na inahusu waumini wa nyakati zote kuanzia wakati huo katika Yohana sura ya 15 mistari ya 1 hadi 9 tunaona Yesu akitumia neno lingine la picha ambayo safari hii alijisema yeye kuwa ni mzabibu, Matawi yalikuwa na yanaendelea kuwa wanafunzi wake na katika mstari wa 8 tunapelekwa kwenye wazo la kuzaa matunda. Zaidi ya hayo tunaambiwa wazi kuwa tunapofikili kikamilifu wito wa Yesu na kutoa maisha yetu kwa huduma yake Mungu anatukuzwa. Kwa mifano mingi katika Agano Jipya ya watu kukubali wito wa Injili ya Yesu; kuanzia kwa Zakaria akikwea mti ili kumwona Yesu, Luka sura ya 19 mistari ya 2 hadi 10, kwa mwanamke mzinzi ambaye alileta sanduku la manukato ya thamani kubwa ili kumpaka Yesu miguu yake, Luka sura ya 7 mistari ya 37 hadi 50. Katika kila kisa inaonyesha hamu ya kukubali wito wa ridhaa ya kutaka kujitolea bidhaa au fedha kuthibitisha hiyo ridhaa. Yesu hakuomba vitu kama hivyo lakini hii ilikuwa ni hatua ya kwanza ya mtu binafsi ufanyike kuwa mwanafunzi. Siyo watawala wote wa Mayahudi ambao hawakumtaka Yesu. Wakati wa kusulubiwa kwake, wawili kati yao Nikodemu na Josefu walimwendea Pilato kuomba idhini ya kupewa mwili ili uzikwe kwa heshima - Injili ya Yohana sura ya 19 mistari ya 38 hadi 42. Kwa kufanya hivyo waliobainika wamo na baadaye wanateseka sana kwa sababu ya kuwa wafuasi wa Yesu. Mara nyingi Wanafunzi vilevile waliokabiliwa na tatizo gumu la kuamua kuacha mali na maisha ya raha na kukubali shida ili waweze kuwa wafuasi wa Yesu. Yesu alitoa ahadi kwa wafuasi wake alipozungumza na Petro juu ya suala hili- tazama Mathayo sura ya 19 mistari ya 27 hadi 29. Kutokana na mifano hii ni wazi kwamba kuwa mwanafunzi wa Yesu ni jambo zito linalohitaji kufikiri sana. Sio jambo la kulikimbilia halafu baadae ukaanza kujuta. Huu utakuwa uamuzi utakaoweza kubadilisha maisha yako mpaka muda wa kufariki kwako au Yesu atakaporejea duniani kama Mfalme aghalabu kutegemea tukio litakalotangulia kwa hali iwayo yoyote ile uamuzi utakaowachukua utakufanya uendelee hatua ya mbele na hiyo itakuwa ubatizo. Katika masomo yaliyopita, tumeonyesha umuhimu wa ubatizo, jinsi ilivyokuwa ni amri ya Yesu kwamba wote wanataka kumfuata sharti wafanye hivyo kwa ubatizo wa maji. Injili inatuambia kwamba Yohana Mbatizaji alikuja mbele ya Yesu akibatiza ubatizo wa toba kutoka katika dhambi. Yesu mwenyewe alionyesha mfano kwa kumwendea Yohana na hapa ndiyo mwanzo wa wanafunzi wote watakaomfuata tangu siku ile na kuendelea. Tendo la ubatizo tangu awali ilikuwa kuzamishwa katika maji. Mara Yesu alipokuwa akitoka ndani ya maji, Mungu alionyesha kupendezwa na kitendo cha mwanae kwa kutuma nguvu zake katika umbo la njiwa kutua juu yake. Mathayo aliandika juu ya hili katika sura ya 3 mistari ya 13 hadi 17. Angalia jinsi Mungu alivyozungumzia kuhusu kupendezwa na kumkubali Yesu kuwa mwanae katika ubatizo huu. Marko aliandika mojawapo ya maagizo ya mwisho ya Yesu kwa wanafunzi wake kabla ya kupaa mbinguni. Angalia sura ya 16 mistari ya 15 na 16. "Enendeni ulimwenguni mwote na mkahubiri Injili. Yule anayeamini na kubatizwa ataokoka. Ukweli wa umuhimu wa ubatizo ulieleweka zaidi baada ya kifo cha Yesu. Waandishi kama Paulo na Petro, kwa nguvu za Roho Mtakatifu walianza kuonyesha kuwa ubatizo ni ishara ya kifo na ufufuko - Warumi sura ya 6 mistari ya 3 hadi 6. Kuna mambo mengi muhimu ya kujifunza kutoka maneno haya. Kitendo cha waumini kuzamishwa majini kwa muda kinawakilisha kifo cha Yesu. Kuinuliwa kwa waumini kutoka katika maji kunawakilisha ufufuko wa Yesu. Kama vile Yesu alivyobadilishwa baada ya ufufuko wake nasi pia tunabadilishwa, sio kwa kuonekana, sio kwa huzuni, kuwa huru wa majaribu ya dhambi, lakini kwa haiba, sasa tukitembea katika upya wa maisha, dhambi zetu zikiwa zimesamehewa kwa sababu ya kujitolea kwa Yesu. Paulo alitumia mfano wa utu wetu wa awali ukisulubiwa naa kuacha nyuma dhamira mpya ya kutupeleka mbele kumfuata Yesu, tukiwa na ongezeko la ushupavu na mafanikio. Kuna agizo moja muhimu ambalo liko katika mstari wa 6. Kwamba hivi sasa tusihudumie dhambi. Paulo anaendelea katika kifungu hiki kueleza alikuwa na maana gani katika usemi huu na kama unao muda, angalia mistari ya 14 hadi 23. Mabadiliko katika maisha yetu na jinsi tunavyokuwa sehemu ya kusudio la Mungu kuwa katika dunia hii ambayo imeonyeshwa katika Waraka kwa Wagalatia sura ya 3 mistari ya 26 hadi 29. Mfumo huu wa urithi wa Utukufu ambao utakuja juu ya nchi, ni matarajio yetu nyeti ambayo sasa wewe unayo nafasi ya kushiriki. MAISHA YA MKRISTO SOMO LA 5 Ushirika katika Njia ya kuelekea kwenye Ufalme. TAFADHALI BIBLIA YAKO IWE IMEFUNGULIWA NA UJARIBU KUTAFUTA KUMBUKUMBU REJEA ZOTE. Shabaha ya ajabu ya Mungu kwa wanaume na wanawake wa nyakati zote ni Ufalme wa Mungu katika dunia hii. Wakati wa maajabu na shughuli kubwa kama tutakavyoona katika somo la mada hii. Lile utakalofanya wakati huu kuwa ni la kipekee ni umbile la wale wote wanaofuata sheria ya Mungu kwa uaminifu ambapo hivi sasa tunayakuta katika mafundisho ya Yesu. Umbile letu hivi sasa ni halisi ikiwa na maana kuwa tunazeeka na kufa. Ahadi ya Mungu kupitia kwa Yesu ni kuwa katika Ufalme wake hatutakufa lakini tutakuwa na umbile la kiroho. Paulo Mtume wa Yesu alieleza haya katika Waraka wa kwanza kwa Wakorintho kifungu cha 15. Soma kutoka mstari wa 35 hadi mwisho wa kifungu hiki na utabaini kuwa Paulo alitumia mfano huu wa mbegu iliyopandwa katika udongo. Katika wakati muafaka mbegu inachipusha majani ya kijani juu ya uso wa ardhi na maisha mapya ya mmea huanza. Halikadhalika tumepewa ahadi hii ya ufufuko iliyotolewa kwetu na Mungu ikiwa ni malipo ya imani na utiifu wetu. Utakuta mfano ambao Paulo anatupa katika mistari ya 51 na 58 kuwa ni ya kututanabaisha. Iwapo utakuwa bado haujaamua kubatizwa, hili litakuwa ni jambo litakalo kusaidia kuamua. Mara nyingi katika Biblia tunakuta waandishi wakielezea maisha kama safari, na hii ni njia nzuri ya kutafakari juu ya hili. Angalia katika Injili ya Mathayo sura ya 7 mistari ya 13 na 14. Katika mfano huu Yesu alielezea safari ya kuelekea Ufalme wa Mungu kama njia nyembamba ambapo dunia nzima wanakimbilia kwenye njia pana ambayo ni nyepesi inayoongoza kwenye kifo cha milele,sisi kama wafuasi wa Yesu kwa uangalifu tunafuata njia nyembamba tukiwa tunajaribu kuvuka vikwazo tukijaribu kutokuondoka katika njia nyembamba ili tusipotee. Kama unaangalia sasa katika Injili ya Yohana sura ya 14 mstari wa 6 utakuta kwamba Yesu anajisemea kuwa yeye ni njia hivyo ushauri anaoutoa ni mzuri. Kama tutamtumaini katika maisha yetu, kufuata mfano wake na sheria zake, njia nyembamba itakuwa rahisi na muhimu kutuwezesha kupita kwa usalama. Kwa watu wengine kutembea katika njia hii kuelekea kwenye Ufalme sharti kufanyike bila ya kuwashirikisha binadamu. Hakuna mitume wengine waishio Umbali wa kusafiri au kuishi katika nchi iliyoathirika na vita ambapo itakulazimu kutembea kutoka sehemu moja hadi nyingine kuepuka matatizo. Kwa sisi tunaoishi katika sehemu zenye amani zaidi katika dunia hii, inawezekana kubatizwa na kuungana na ndugu katika Kristo (wakristadelfia) katika liletunaloita Ecclesia. Hii ina maana ya kwamba, kwa kutumia mfano wa Yesu, tunaweza kusafiri hadi kwenye Ufalme wa Mungu tukiungana na watu wengine wenye imani kama sisi. Unaposoma neno "Kanisa" katika Agano Jipya, neno la asili la Kigiriki lililotumiwa na Yesu na Mitume wakati wote ilikuwa "Ecclesia" na Wakristadelfia wamechagua kutumia neno lile la Kigiriki kama kikundi chao cha ndugu wanaume na Wanawake. Wakati Mwanafunzi wa Yesu aliyebatizwa hana uchaguzi bali kuwa pekeyake, ni muhimu kumtegemea Mungu halikadhalika na Yesu kupitia Sala za kila siku na kusoma Biblia. Hali hii ikijitokeza, ndugu sharti aulize maswali, "Kwa nini niko pekee yangu? Je ni kwa sababu sitaki kuwa pamoja na wengine? Kwa nguvu kidogo au kwenda katika mji tofauti je inawezekana kuungana na Wakristadelfia wengine katika kuumega mkate?. Katika hali nyingine, jambo hili bado halitawezekana na kwa bahati nzuri kuna njia nyingine. Daima ni jukumu la Mwanafunzi kuhusika katika uelewa/ufahamu ambao ni nyeti atakapokuwa amepata na kuwaambia wengine juu ya jambo hilo. Waambie wengine juu ya imani na matumaini yako makubwa katika Yesu. Kwa njia hii unaweza kukusanya kikundi kipya cha waumini katika mji wako au kijiji. Yesu alitarajia Wanafunzi wake kukusanyika pamoja katika vikundi ili waweze kuabudu pamoja. Wangeweza kumkumbuka Yesu pamoja katika Mkate na Divai na kusaidiana katika njia hii kuelekea katika Ufalme. Sio vizuri kusafiri pekee yako, mara kwa mara ni rahisi na ni salama kuwa na wenzako. Mwanzoni mwa huduma yake Yesu hakutembea pekee yake, aliwachagua Mitume kumi na wawili na siku hadi siku alitembea na wanaume na wanawake wengi. Paulo aliposafiri katika nchi nyingi kuhubiri Injili, hakuwaacha nyuma ndugu, wanaume kwa wanawake wakiwa wamejitenga, aghalabu alianzisha Makanisa mapya mahali ambapo wanafunzi wangeweza kusaidiana. Angalia katika waraka wa pili wa Paulo kwa Wathesalonike sura ya 1 mistari ya 3 hadi 5. Hususani katika nyakati ngumu, ni nzuri kusaidia kubeba mizigo ya wengine. Inakupasa kuelewa kwamba kama umebatizwa utakuwa kaka au dada katika Kristo na sehemu ya kukaribishwa kwako kuwa kiungo cha Ecclesia iliyokaribu nawe na mjumbe wa familia kubwa ya Wakristadelfia duniani. Kama kuna ecclesia nyingi karibu na wewe, unaweza kuchagua uwe wapi. Ecclesia zote zinajiendesha zenyewe na kuna kikundi cha wazee ambao ni ndugu wenye uzoefu watakao kuwa na madaraka ya kuendesha shughuli za kila siku. Aidha, wakati muda muafaka, ecclesia nzima itakutana kujadili juu ya mambo mazito zaidi yanayokihusu kikundi na mara moja kwa mwaka ili kuchagua wazee watakao hudumu katika mwaka ujao. Uchaguzi katika makundi makubwa unaweza kuwa kwa kura ya siri. Pia Katibu na Mweka Hazina huchaguliwa. Wakati mwingine Katibu huitwa ndugu mwandishi kwa sababu ni wajibu wake wa kuweka kumbukumbu zote za mikutano. Kwa njia hii ecclesia ina demokrasia kamili na waumini wote wanahusika katika maamuzi. Wote wako sawa mbele ya Mungu na hakuna wachungaji, Mapasta au wainjilisti miongoni mwetu. Elimu yetu ya Biblia inapatikana kutokana na kila mmoja wetu kujisomea. Kuhusu ndugu, kuna haja ya kuandaa uimarishaji na mafunzo maalumu ya madarasa ya Biblia na Makundi ya kujifunza. Halikadhalika, wanawake pia wanatakiwa kuandaa masomo ikiwa wanafundisha katika madarasa ya Jumapili ( Sunday school) au madarasa ya wanawake. Hakuna anayevaa nguo maalumu, hakuna majoho au kola ya shingoni kwa ndugu na vyeo maalumu mbali ya vile vilivyoelezwa. Wote wanafanya kazi pamoja katika njia rahisi mbele ya Mungu. Jumuiya ya Wakristadelfia ambayo hivi sasa inazungukwa na ndugu yaani wanaume na wanawake katika nchi nyingi wanaungana katika imani yao kwa maelezo ya kawaida ya imani. Ecclesia nyingine zimejengeka katika misingi ya maoni ya mila nzito na hizi husawazishwa na nyingine ambazo zina maoni ya kisasa zaidi. Nyingi za ecclesia zina maoni nusu kati ya tofauti hizi na mafunzo yote ya Biblia kati yetu ni suala la majadiliano ya mara kwa mara. Hii inasaidia udugu duniani pote kuwa na imani ya aina moja na kuabudu ambako kungeeleweka kama nguvu kubwa moja. Kama Mkristadelfia aliyebatizwa, unaweza baadaye kusafiri katika sehemu nyingine za dunia ambako unaweza kuabudu na ndugu zako katika njia utakazo kuwa umezizoea kabisa. Taarifa hii kuhusu muundo wa ecclesia za Wakristadelfia imejumuishwa katika somo hili kwa sababu ni muhimu kwamba unaelewa thamani kubwa ya kuwa katika ecclesia wewe mwenyewe kuweza kumwabudu Mungu pamoja na wengine walio na imani kama yako. Unaweza kuongeza nguvu zako katika kuunganisha kazi ya uhubiri na kuwahudumia wengine ambayo ni sehemu muhimu ya maagizo ya Yesu kwetu sisi. Mara nyingi ni kweli kwamba ndugu anapokuwa hayupo katika ecclessia kwa majuma kadhaa, na hivyo kutokujiunga katika huduma ya chakula cha Bwana (Mkate na Divai) katika kumkumbuka Yesu. Imani yao binafsi inaweza kuanza kuteteleka. Inakuwa vigumu kwao kuishi katika njia ile nyembamba iendayo katika Ufalme. Imani ni mwaka wa moto unayohitaji kulishwa chakula cha kiroho mara kwa mara. Matunzo na kulishwa tayari vinapatikana katika ecclesia; ni vigumu sana kuvipata ukiwa pekee yako.