WAKRISTADELFIANINI NANI? JE, NI WAPYA? Wakristadelfiani ni kundi la Kristo ambalo kwa kupima sana wamejaribu kurudi kwenye imani na sifa njema za kanisa la kvvanza la Kikristo. Tnmekuwapo kwa zaidi ya miaka 100. Jina hili "Kristadelfiani" maana yake ni "Ndugu katika Kristo.” WAKRISTADELFIANI WANAPATIKANA WAPI? Tumeenea ulimwenguni pote kama wakristo wa kwanza. Tunakutanika nyumbani, vyumba vya kukodi, na kumbi zetu wenyewe. (Matendo 1:3; 2:46; 18:7; 19:9; 28:30). WAKRISTADELFIANI WANAJIUNGAJE? Sisi m jamii ya watu waliofuata mfano wa Ukristo wa karne ya kwanza. Washirika wa kila kusanyiko wanaitana "ndugu" na "dada" nao wote wana majukumu yaliyo sawa kwa ustawi wa kanisa. Mshikamano wa nguvu katika imani unatuweka pamoja katika Undugu. (Math.23-,8,12; Warumi 12:4-6; 16:1, Wagalatia 3:28;Wakormtho 12:4-27). WANAAMINI NINI NA KUFUNZA? Tunaamini kuwa Biblia ndiyo ujumbe wa pekee uliofunuliwa kwa mwanadamu, umetolewa ili kuleta wajibu kwa kila mtu kutii kwa imani. Biblia tu ni yenye amri kwetu, nasi tunafundisha kwamba isomwe kwa kuomba na uangalifu kila nafasi inapopatikana. (Warumi 16:26; Yohana 17:17; Matendo 17:11). Ufumbuzi halisi wa mafunzo unaweza kuonekana zaidi. MUNGU MWENYEZI Yupo Mungu mmoja tu wa milele asiyepatikana na mauti. Yesu Kristo ni mwanawe wa pekee, na Roho Mtakatifu m uweza wake.(Isaya 45:5; 1Tim.1:17;Efeso 4:6; Luka 1:35, 24:29; Matendo 1:8). MWANADAMU Mwanadamu ni mfu na mwenye dhambi mbele za Mungu. Utu wake wote ni wenye tabia ya dhambi na adhabu kwa ajili ya dhambi ni mauti - mauti halisi, mwisho wa uhai wote.(Ayubu 4:17; Rumi 3:23; Yeremia 17:9; Marko 7:21-23; Rumi 6:23;Muhubiri 9:1-6; Zaburi 146:4) YESU Kwa upendo wake; Mungu alimtuma mwanadamu Yesu ulimwenguni ili kuwaokoa watu na dhambi zao. Wale wanaomwamini hawatapotea, bali watakuwa na uzima wa milele. (Mathayo 1:21; Yohana 3:16) DHABIHU YA KRISTO Yasu hakuwa na dhambi. Alikufa ili kuonyesha haki ya Mungu na kuwakomboa wanaoipokea dhabihu hii kwa imani. Mungu alimfufua toka wafu, akampa uzima wa milele, na kumjalia mamlaka yote ya mbinguni na dunia na amewekwa kuwa mpatanishi wa Mungu na mwanadamu (Matendo 2:23-36; Efeso 1:19-23; 1Tim. 2:5; Hebr. 4:14-16; Warumi 3:21-26). KURUDI KWA KRISTO Sio muda mrefu Yesu atarudi duniani. Wakati huo atawafufua wengi wa wafu, na kufanya hukumu ya pamoja na walio hai na kuwapa walio waaminifu ambao ni wafuasi wake uzima wa milele katika Ufalme wa Mungu. (Uf.22-.12; Luka 21:20-32; Yon. 5:28, 29; Dan.12:2; 2Tim.4:1; Math.25-.34). UFALME WA MUNGU Ufalme wa Mungu utawekwa duniani na Yesu akiwa Mfalme. Mji wake mkuu utakuwa Yerusalemu, utawala wake utakuwa m wa kuenea ulimwenguni pote, nayo mamlaka yake italeta haki na amani pasipo mwisho. (Dan.2:44,7:27; Matendo 3:21; Yeremia 3:17; Isaya 2:2-4; Zaburi 72; Dan. 7:14; Isaya 9:6-9; 11:1-9; 61:1-11). AHADI Injili haitenganishwi na ahadi zilizofanywa na Mungu kwa Ibrahimu na Daudi katika Agano la Kale. Ahadi hizi zinatimilika kwa Yesu Kristo. (Wagalatia 3:6-9,16,25-29; 1Petro 1:2-4; Mwanzo 13:14-17; 22:15-18; 1Samuel 7:12-16; Luka 1:31-33). NJIA YA WOKOVU Namna ya kuingia Ufalme wa Mungu m kwa imani. Hii inahusisha kuamini Neno Lake - Biblia na kutii yanayotakiwa, wanaume na wanawake wakiri dhambi zao, watubu na kubatizwa kisha kumfuata Yesu kwa uaminifu.(Waebrania 11:6; IWathesalomke 2:13; 2Tim.3-.15; Matendo 2:37;Marko 16:16; Yohana 3:3-5; Mathayo 16:24-27). TUMAINI Tumaini la Uzima tu baada ya kifo ni ufufuo wa wafu na kupata uzima wa milele katika Ufalme wa Mungu duniani. (1Wakointho 15:12-50, Zaburi 49:12-20; Yohana 11:25;Ufunuo 5:10,20:4). KWA HABARI ZAIDI WASILIANA NAJAMII YA WAKRISTADELFIANI WALIO KARIBU NAWEAU ANWANI HAPA CHINI:- CBM Publishing 32 Blenheim Road,Far CottonNorthampton, United Kingdom NN48NW www.Bedford-Ecclesia.org.uk CarlHinton@cmhdigital.co.uk