25. YESU ANA KWENDA MBINGUNI “Huyu Yesu, aliyechukuliwa kwenu kwenda mbinguni, ataku tena jinsi iyo hiyo” Shabaha Ni kuonyesha jinsi Yesu alivyopaa kwenda mbinguni na akaahidi kuwa atarudi. Baada ya Yesu kufufuka katika wafu, aliendelekuwa wanafunzi wake kwa muda wa siku arobaini, kabla ya kuchukuliwa mbinguni kwenda mkono wa kulia Mungu.Wakati huu aliwafundisha mambo mengi sana alipokuwa akiwatayarisha kwa ajili ya kazi kubwa iliyokuwa mbele yao. Yohana21; Matendo ya Mitume 1:1-12 MWUJIZA WA SAMAKI: Yohana 2:11-13 Baada ya Yesu kufufuka, malaika pale kaburini waliwaambia wale wanawake kwenda kuwaambia wanafunzi wake kwamba Yesu atawatangulia Galilaya. Na pale angekutana nao mlimani (Mathayo 28:7,16). Kundi la mitume saba, wakiongozwa na Petro, wakatelemka hadi bahari ya Galilaya.Petro akasema, “Naenda kuvua samaki”, na wengine wakasema wakasemawatawenda pmoja naye. Lakini usiku huo ingawaje walifanya kazi kwa bidii, hawakupata samaki. Asubuhi, kulipokucha, mtu mmoja akawa amesimama ufuoni (hakika huyu alikuwa ni Yesu), akawauliza kama wamevua samaki yoyote. Wakamjibu, “La”. Akawashauri wajaribu upande mwingine. “Litupeni jarife upande wa kulia wa chombo, nanyi mtapata”. Wakazitupa nyavu zao upande wa kulia na mara moja wakapata samaki wengi sana hata wakashindwa kuzivuta nyavu, kwa sababu ya wingi wa samaki, lakini wavu haukukatika. Ghafla Yohana akamtambua mtu yule aliyesimama ufuoni ni nani. Akamwambia Petro, “Ndiye Bwana”. Wakakumbuka tena siku ile waliyovua samaki wengi sana mwa njia ya mwujiza wavu ukajaa samaki (Luka 5:4-7). Na Petro alipojua kuwa ni Bwana, akarukia baharini akaogelea mpaka ufuoni. Wanafunzi wengine wakamfuata katika mashua, wakilikokota lile jarife lililojaa samaki. Yesu pale alikuwa ana moto na alikuwa ameoka samaki pale.Kwa furaha wakakaa chini wakala samaki na mkate wakiwa pamoja na Bwana wao. Ulikuwa ni wakati huu ambapo Yesu alimgeukia Petro, Yesu akamwambia Petro, “Lisha kondoo zangu”. Kwa kuwa Yesu alikuwa Mchungaji Mwema, akautoa uhai wake kwa ajili ya kondoo, kwa hiyo mitume ni lazima wafaye kazi muhimu ya kulisha na kutunza kundi lake la kondoo. Petro alithibitisha kuwa mchungaji mwaminifu, akikumbuka kila wakati jambo ambalo Yesu alimtendea yeye. Akawahimiza na wengine “kulichunga kundi la Mungu”, mkijua kuwa, “wakati mchungaji mkuu atakapodhihirishwa mtaipokea taji ya utukufu, ile isiyokauka” (1 Petro 5:1-4) YESU ANAWAAGIZA WALE KUMINA MOJA: Matendo ya Mitume 1:1-5 Kwa muda siku arobaini kabla Yesu hajachukuliwa kwenda mbinguni, aliwatokea wanafunzi wake wengi. Akawaambia wale kumi na moja mambo yote yahusuyo ufalme wa Mungu.Bila shaka aliwaambia wakati wa utukufu ambapo Israeli atakuwa mkuu katika mataifa, naye ataketi katika kiti cha enzi cha Daudi katika Yerusalemu, akitawala dunia yote. Na sasa walipaswa kusubiri kule Yerusalemu, kwa maana Mungu angewapatia nguvu za roho mtakatifu ili ziwesaidie kuhubiri katika Jina lake.Baada ya hapo, walitakiwa kwenda kuhubiri ijili katika nchi zote, kwa watu wa mataifa yote. “Enendeni ulimwenguni mwote mkaihubiri injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka” (Marko 16:15-16). Neno “injili” maana yake “habari njema”. Ni habari njema kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo. MKUTANO WA MWISHO: Matendo ya Mitume 1:6-12 Kwa wakati huu, wanafunzi walikuwa na hamu sana ya kuyaona mambo yote ambayo Yesu aliwaambia yakitimia. Walipoondoka Yerusalemu na kwenda kwenye Mlima wa Mizeituni, walimwuliza, wakisema, “Je, Bwana, wakati huu ndipo utakapowarudishia Israeli ufalme?” (mstari 6). Lakini Yesu akawajibu, “Siyo kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe” (mstari7). Mungu mwenyewe kwa wakati wake anajua nyakati alizoziweka kwa Sayuni kutukuzwa. Wakati huo, watakapokuwa wamepokea nguvu za Roho Mtakatifu, kazi yao ilikuwa kuihubiri injili, kwa maana walitakiwa wawe mashahidi wake “katika Yerusalemu na katika Yudea na katika Samaria na mwisho wa nchi” (mstari 8). YESU ANA APAA MBINGUNI: Matendo ya Mitume1:9-12 Ikawa Yesu alipomaliza kusema, ghafla akachukuliwa kutoka katikati yao kwenda juu. Wakiwa wamesimama pale wakitazama juu kwa mshangao, wingu likampokea kutoka machoni pao. Wakaendelea kumkazia macho, wakiwa hawataki awaache. Ndipo wakaona watu wawili wakiwa wamesimama karibu nao wakiwa wamevaa nguo nyeupe. Walikuwa malaika, waliokuwa wametumwa kuja kuwapatia tumaini na kuwatia moyo. “Enyi watu wa Galilayambona mmesimama mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyechukuliwa kwenu kwenda juu mbinguni atakuja jisi iyo hiyo mlivyomwona akienda zake mbinguni”. Ni tumaini la ajabu jinsi gani ambalo limeelezwa katika katika maneno haya, maana malaika walieleza waziwazi kwamba Yesu atarudi tena duniani. Amekwenda mbinguni mkono wa kuume wa Baba yake, na atakuwa huko Mungu atakapomtuma kuja kuusimika ufalme. Wakitiwa moyo na malaika, mitume wakatambua kuwa hakuna sababu ya huzuni, kwa kuwa walijua kuwa yu hai milele naye atawalinda na kuwatia nguvu. Kwa furaha wakarudi Yerusalemu kusubiri wapewe Roho Mtakatifu, ambaye Mungu aliahidi kutuma kuwasaidia kuhubiri kwa jina lake. FUNDISHO KWETU “Haikuwa miaka mingi tangu Yesu alipo paa kwenda mbinguni, wengi waliokuwa wanasubiri kurudi kwake wakakata tamaa”. Wakasema, “Iko wapi ahadi ile ya kuja kwake?” (2 Petro 3:4). Petro akawaambia hao wenye mizaha uwa Mungu ataitimiza ahadi yake ya kumtuma Yesu aje. Kwa maana wale waliokataa tamaa au waliochoka kusubiri, Petro akasema, Siku ya Bwana itakuja kama vile mwizi anavyokuja usiku. Kwa hiyo akawaonya wafuasi wa Yesu kila wakati wawe wenye kukesha na kusubiri, maana Yesu atawashangaza tu wale wasiomtazia. Kama tumezama sana kafika mambo ya dunia, badala ya kufanya mapenzi ya Mungu, Bwana atakuja na atatukuta tukiwa kama wale wanawali wapumbavu. Tutakuwa na huzuni iliyoje ikiwa ni pamoja na aibu sana. Kwa hiyo tusiwajali kabisa watu wale wanaotucheka tunapowaambia kwamba Yesu anarudi upesi. N tuonyeshe kuwa tunayaamini maneno ya malaika kwamba “huyu Yesu” atakuja tena kutoka mbinguni. Na tukumbe maneno yake ya faraja, “Tazama, nakuja upesi a ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo” (Ufunuo 22:12). Na atukute tukifanya kazi kwa uvumilivu na tukmsubiri na tukiwatunajifunza Neno la Mungu, ili kwamba tuwe na furaha wakati wa kukutana naye. MAELEZO YA ZIADA Ingawaje watu wengi hawaamini kuwa Yesu atarudi tena, lakini Biblia inatupatia ishara zilizo wazi kabisa kuwa kurudi kwake ni hakika. Tunaishi katika siku za uovu na uovu mwingi sana wa dunia umetuzunguka, hata hivyo tujapaswa kumshukuru Mungu ka kutupatia sisi ishara hizo za ajabu, sawasawa na ishara mbaza Yesu aliwapatia wanafunzi wake zilizowasaidia wao kuamini. Na tufikirie baadhi ya hizi ishara zilizo wazi kabisa. Kurudi kwa Wayahudi katika nchi ya Israeli Kwa sababu ya kutokuaminikwao, Mungu aliwatawanya wana wa Israeli Katika mataifa yote ya dunia. Wayahudi walifukuzwa katika nchi yao wakati Yerusalemu ulipoharibiwa kabisa mwaka 70BK na wakabakia katika hali hiyo ya kutawanywa na kuteswa kwa zaidi ya miaka 1800. Na manabii waliotabiri kuhusu kutawanywa kwao pia walitabiri kuwa Mungu atawakusanya na kuwarudisha katika nchi yao (Yeremia 31:10, Ezekieli 37:21-22). Yesu pia alisema kwamba Yerusalemu “utakanyagwa na mataifa” mpaka majira ya mataifa yatakapotimia kabla ya kurudi kwake (21:24). Katika mwaka 1948 Wayahudi walitangaza duniani kote kwamba Israeli limerudi kuwa taifa tena, wakaishi katika nchi yao. Katika mwaka 1967, Yerusalemu ukatwaliwa na kuwa chini ya udhibiti wa Wayahudi.Na sasa ni mji mkuu wa taifa la Israeli. Watu wakivunjika mioyo wakihofia kwa sababu uvumi na tetesi za vita Yesi alitabiri kwamba kabla ya kurudi kwake watu watakuwa na hofu kwa sababu ya ya tetesi za kila mahali (Luka 21:25-26). Unabii kuhusu vita ya Mashariki ya Kati (Yeremia 3:9-12). Urusi itakuwa ni nchi yenye nguvu zaidi duniani na itakuja na mataifa mengi katika nchi ya Israeli (Ezekieli 38:3-23;14-16). Mungu atayakusanya mataifa kufanya vita na Yerusalemu (Zekaria 14:2). Kitisho cha vita ya dunia ni ya kwelikwa kila mtu. Watu wanongea waziwazi kuhusu “Armagedoni”, ambayo ni kweli ni vita kubwa katika Mashariki ya Kati iliyonenwa na manabii (Ufunuo 16:18). Mataifa yanaendelea kukusanya na kurundika siraha nyingi. Na baadhi ya silaha hizo zinaweza kuangamiza maisha ya dunia yote. Jinsi tulivyo barikiwa kufahamu kuwa Mungu hataruhusu hilo litokee, ila atamtuma Mwana wake. Watu watakuwa wenye kupenda anasa kuliko kumpenda Mungu. Mtume Paulo anatuonya kuhusu uovu ambao utakuwepo duniani “siku za mwisho” kabla ya Kristo kurudi. “Watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kutamani, wenye kujisifu, wenye kujivuna, wanaokana nguvu za Mungu, wasio watii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu”(2 Timotheo 3:1-5). Ukweli wa maelezo ya dunia siku hizi, hasa katika nchi za Magharibi, mfano Australia, Marekani na Uingereza. Maduka yao yana kila kitu kinachotamanisha, ni rahisi sana sisi kuweza kutamani, mara nyingi tunahitaji vitu vipya, na hatuna shukrani kwa vile tulivyo navyo. Watoto ni wepesi kulikufuru jina la Kristo kama vile wanavyokufuru wakubwa wao. Walimu wana mamlaka kidogo sana kwa wanafunzi wao kwa sababu hao watoto hawawatii wazazi wao na wala hawawatii wenye mamlaka. Tunapaswa kuwa waangalifu muda wetu usiwe ni wa anasa za dunia, kwa kuwa hatutakuwa na muda wa kumpendeza Mungu Watakuwepo wenye mizaha, wakisema, “Iko wapi ile ahadi ya kuja kwake”. Mtume Petro alionyesha kuwa “katika siku za mwisho” watu hawataamini kuhusu kurudi kwa Kristo. Wataangalia mambo yanayowazunguka, watasema, “vituvyote vinakaa hali iyo hiyo, tangumwanzowakuumbwa” (2 Petro 3:3-4). Kwa hiyo watu siku hizi hawapendi kusikia kurudi kwa Yesu. Wanalicheka wazo hilo. Petro aliendelea kutoa onyo kwa wale wasiojali kurudi kwake: “Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwamnatazamia mambo hayo, fanyeni bidii ilimwonekane katika amani kuwa hamna mawaa wala aibu mbele yake” MASWALI Majibu ya Mafupi 1.Baada ya Yesu kufufuka katika wafu, kwaniniwanafunzi walikwenda? Galilaya 2. Ninani aliyekuwa wa kwanza kimtambua Yesu pale ufuoni? 3. Ni jambo gani liliwapa uhakika wanafunzi kuwa yule alikuwa Yesu? 4. Ni kazi gani maalumu ambayo alimwambia Petro aifanye? 5. Baada ya Yesu kufufuka aliishi duniani muda gain? 6. Malizia maneno ya Yesu: “Enendeni ulimwenguni mwote ...” 7. Ni swali gani wanafunzi walilomwuliza kuhusu ufalme 8. Ni katika Mlima upi ambapo Yesu alichukuliwa kupaa kwenda mbinguni? 9. Ni nani waliowaabia wanafunzi kuwa Yesu atarudi tena? 10. Ni kwa nini wakati huu wanafunzi hawakuhuzunika tena wakati Yesu Amewaacha? 11. Tunapaswa tufanye nini wakati huuambapo Yesu yuko mbinguni? Majibu ya Kina 12. Elezea tendo lililofanyika pale bahari ya Galilaya. Wakati wanafunzi wa Yesu walipokwenda baada ya kufufuka kwake? 13. Eleza palitokea nini katika Mlima wa Mizeituni. Yesu alipokuwa na wanafunzi wake Wakati wa mwisho? Majibu ya Nyongeza 14. Eleza kwa ufasaha ishara nne zinazotuthibitishia kuwa Bwana Yesu Kristo atarudi upesi duniani?