2. WAPELELEZI KUMI NA MBILI KATIKA NCHI. "Waliwasilisha taarifa ya maovu ya Nchi." Shabaha Kuonyesha kwamba hatuna budi kuamini ahadi ya Mungu kwa sababu atatusaidia ikiwa tutamwamini na kumtumainia yeye. Muhtasari Israeli alisafiri kuelekea Kaskazini katika nyika za Pwani, na baada ya kutua katika sehemu kadhaa walifika Kadesh- Barnea, mpakani mwa Nchi ya Ahadi. Musa alimwambia kuigia na kuimiliki nchi ambayo Mungu aliwaahidi kuwapatia, akisema, "usiogope wala usifadhaike". (Kumb. 1:20-21) Lakini walikosa imani. Walisahau ahadi ya Mungu ya Sinai. "Tazama namtuma malaika aende mbele yako" na "nitawafanya adui zako wote wakuonyeshe maungo yao". (Kut. 23:20-27). Yaelekea hawakuamini kuwa Mungu angeweza kuwafanyia yote haya. Watu walienda kwa Musa kumuomba apeleke watu watakao ipeleleza nchi na Mungu aliruhusu ingawa ilionyesha kuwa walikosa Imani katika Neno lake. (Hes. 13 na 14). NCHI WALIYOIPELELEZA: Hesabu 13:17-25. Musa alituma watu kumi na wawili - mtawala (au mkuu) kutoka katika kila kabila - kuipeleleza nchi. Kwa siku arobaini walisafari katika nchi ya Kanaani na baadaye walirejea na taarifa ya safari yao. Walileta baadhi ya matunda - tini, makomamanga na kishada kikubwa cha zabibu kutoka Eshikoli (maana ya jina "ni kishada hicho cha zabibu"). TAARIFA YA WAPELELEZI: Hesabu 13:26-33 Taarifa ya wale watu, walisema kwamba ile nchi ilikuwa ni nchi nzuri ama Mungu alivyo kuwa amewaambia "hakika ni nchi imiminikaayo maziwa na asali". Wote walikubali lakini wapelelezi kumi kati yao walivunja mioyo ya watu. Walisema kwamba miji ni mikubwa yenye maboma marefu na watu hodari waliishi pale. Isipokuwa watu wawili kati ya wale wapelelezi , Kalebu na Yoshua, walikuwa na Imani ya kutosha kuamini ya kwamba Mungu ataitunza ahadi yake kuiangusha miji hii na watu wale hodari hata kuwapatia Waisraeli nchi, Kalebu alisema "na tupande mara tukaitamalaki maana twaweza kushinda bila shaka. Lakini wale wapelelezi kumi walisema, " hatuwezi kupanda kupigana na watu hawa, kwa kuwa wana nguvu kuliko sisi". "Huko tuliwaona wamefili wana wa Anaki... tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona". Wao walifikiria jinsi ya kuyashinda matatizo - ya miji mikubwa na watu hodari waliowaona . Wasahau kwamba Mungu ndiye angewapigania. MUNGU ANAWAZUNGUSHA WAISRAELI JANGWA Hesabu: 14 Mioyo ya watu ilijaa hofu waliposikia taarifa ya wale wapelelezi kumi. Hawakuamini ahadi ya Mungu ya kuwa nchi ile yote itakuwa yao. Wakamnung'unukia Musa na Haruni na walitaka kumchukua mtu mmoja awe akida kuwaongoza Misri. Kalebu na Joshua walijaribu kuyabadilisha mawazo yao kwa kusema , "Ikawa BWANA anatufurahia, atatuingiza katika nchi hii, atupe iwe yetu... lakini msimwasi BWANA (mist. 7-9). Lakini watu wote wakawageukia na wakataka kuwapiga mawe, ghafla Utukufu wa BWANA ukaonekana. Waisraeli wote waliisikia sauti yake kuu, akiongea kupitia malaika. "Je watu hawa watanidharau hata lini?." "Nitawapiga kwa tauni nami nitakufanya wewe (Musa) kuwa Taifa kubwa, lenye nguvu." Musa akamsihi MUNGU awasamehe watu wake kwa ajili ya Jina lake kuu. Musa alikuwa mpole sana hakutaka kitu chochote kwa nafsi yake. Yeye alifikiria ahadi ya Mungu kwa Israeli tu, na yale ambayo mataifa wasiomwamini Mungu wangeyanena kama ahadi zisingetimizwa. Mungu alimsikiliza Musa, akasema; "Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa; LAKINI HAKIKA YANGU KAMA NIISHIVYO,NAKAM DUNIA YOTE ITAKAVYOJAWA NA UTUKUFU WA BWANA." Mungu hakuangamiza taifa lote mara moja, lakini alimwambia jinsi atakavyowaadhibu wasiotii na wasioamini. Wasioamini kuanzia wale wa miaka ishirini au kuzidi wangekufa jangwani. "Hawataingia katika Nchi ya Ahadi. Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini kila siku itahesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu ndiyo miaka arobaini". Tayari walikuwa wametimiza miaka miwili walikizungukazunguka jangwani, tangu watoke Misri. Na hivyo wangeendelea kuzunguka miaka thelathini na nane zaidi (kumb. 12:14), hadi hapo watu wote waliokataa ahadi ya Mungu watakapokuwa wamekufa. Wapelelezi kumi waliowashusha mioyo watu walikufa kwa tauni iliyotoka kwa BWANA, MUNGU (Hes. 14:37). Watu Waisraeli waliposikia maneno haya yakutisha, walibadilisha nia zao, badala ya kukubali maneno ya MUNGU, waliamua kwenda ili kuimiliki nchi. Musa aliwaonya wasiende kwa kuwa BWANA hakuwa pamoja nao, lakini wengi kati yao wakakwea kuingia Kanaani na wakashambuliwa na kurudi nyuma jangwani. Kwa hiyo wakawa wamelazimishwa kuzunguka jangwani kama BWANA alivyokuwa amesema kuwa watafanya. Wapelelezi wawili waaminifu peke yao, Joshua na Kalebu, walipewa ahadi ya kuwa wangeishi hata watakapoingia nchi ya Ahadi, pamoja na watoto wa wale walioasi na kufariki. FUNDISHO KWETU. Ingawaje Waisraeli wote walikosa Imani katika ahadi ya MUNGU, Kalebu na Joshua walisimama imara katika imani yao ya kuwa MUNGU atafanya yale anayo yaahidi. Huu ni mfano kwetu wa kufuata katika siku hizi ambazo watu wengi sana wanakataa neno la BWANA. Inatia moyo mtu mmoja anapoitetea imani yake huku akiwa amezungukwa na watu wasioamini, lakini MUNGU anafurahia sana tunapoweza kuilinda Imani. MAELEZO YA ZIADA: KUSUDI LA MUNGU KUHUSU DUNIA Tumeona jinsi MUNGU alivyochagua Israeli ,alivyowaongoza na kuwaleta Sinai. Pale, aliwaambia kwamba lilikuwa kusudi lake kuwafanya Waisraeli "Taifa Takatifu",mliotengwa kwa ajili ya BWANA. Wangeitwa kwa Jina la BWANA na wangetunza amri zake, wakionyesha Utukufu wa Mungu kwa yale Mataifa yaliyowazunguka. Hata hivyo ingawaje maajabu yalitendeka katikati yao (Mfano mana kutoka Mbinguni, kwale, na maji kutoka katika mwamba) hawakuamini neno la Mungu. Na kwa sababu ya Waisraeli kukosa imani, Mungu naye akawakataa na hawakuingia katika nchi ya Ahadi. Lakini bado Mungu alimueleza Musa:Kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na Utukufu wa BWANA" (Hes. 14:2) . Hili bado ni kusudi la Mungu kwa dunia, miaka elfu nyingi imepita tangu Mungu alpoimwambia Musa maneno haya muhimu na bado hatujaona dunia kujawa na Utukufu wa BWANA. Kwa sababu Waisraeli wachache walidumu katika uaminifu toka nyakati za nyuma, Yeye kwa neema yake anawaita wanaume na wanawake kutoka mataifa mengine iliwamwamini na" kumtii BWANA, ili waweze kushiriki utukufu wa Mungu ujao na wa "Mbegu ya Abrahamu". Leo anaendelea kuita watu kutoka katika mataifa kwa Injili ya Jina lake (Math:15:14) Wale waaminio neno lake na kuzitii amri zake wanaweza kwa njia ya ubatizo katika Yesu Kristo Bwana , "kufanyika kuwa uzao wa Abrahamu na warithi sawasawa na ahadi" (Wagalatia 3:26-29). Wakati Bwana Yesu Kristo atakaporudi (Mdo. 1:11) ,kuuweka ufalme wake (Dan:2:44) tumaini la muhimu la MUNGU BABA WA MBINGUNI alilowaahidia Waisraeli litatimizwa. MASWALI: Majibu Mafupi: (1) Ni Waisraeli wangapi walitumwa kuona jinsi ilivyo? (2) Kumi kati ya waliotumwa walisema nini waliporudi? (3) Majina ya wapelelezi wawili waaminifu ni? (4) Je, Kalebu na Joshua walisema Waisraeli wanapaswa kufanya nini? (5) Je, ni kwa nini Mungu aliwakasirikia watu wakati wale wapelelezi 12 waliporudi. (6) Je, ni jinsi gani watu walivyoadhibiwa walipokataa kwenda katika nchi ya Kaanani?. Majibu ya Kina: 2. Eleza habari ya Wapelelezi walioingia katika nchi ya Kaanani na matokeo ya safari yao. 3. Ni jinsi gani BWANA alivyowaadhibu Taifa la Israeli kutokana na uovu wao walipokuwa penye mpaka wa Kaanani? 4. Ni kwa namna gani tunaweza kufuata mfano wa Kalebu na Joshua?. Majibu ya nyongeza: 5. "Lakini kama niishivyo mimi, dunia yote itajawa na utukufu wangu." Kwa msingi wa maneno haya, unaweza kufafanua?. (a) Nini lilikuwa kusudi la Mungu na watu wake Israeli waliokusanyika mbele ya Mungu pale sinai?. (b) Ni jinsi gani walishindwa? (c) Ni kusudi lipi leo alilonalo Mungu na watu toka mataifa wanaoamini na kutii Neno lake?.