15.GIDION "Upanga wa BWANA na wa Gidion" Lengo: Kuonyesha kuwa Mungu wakati wote aliwatunza wana wa Israeli. Walipomgeukia Mungu aliwapatia viongozi kuwaongoza Muhtasari (Ufupisho) Kufuatia ushindi juu ya jeshi la Mfalme wa Kanaani,nchi ikastarehe miaka arobaini (Waamuzi 5:31). Lakini wakati huu wa amani, Israeli ilisahau upesi yote aliyowafanyia Mungu siku za nyuma na kugeukia tena kwenye ibada ya uongo na njia za uovu za Wakanaani. Kwa kuwaadhibu, Mungu aliwatia mikononi mwa Wamidiani waliowatesa kwa muda wa miaka saba. Waamuzi 6 na 7. WAMIDIANI: Wamidiani walikuwa watu wapendao vita ambao waliiteka nchi ya Israeli kama jeshi la nzige, waliangamiza mimea ya chakula na makundi ya wanyama wafugwao ambao wangekuwa chakula cha Waisrael hivyo kuleta hofu kati ya watu. Matokeo yake, Waisrael walikimbilia mafurikoni na mapangoni kwehye milima, ambakko walijaribu kujificha kutoka kwa adui zao. Katikati ya hofu na fadhaa yao walimkumbuka Mungu wao na kumlilia kwa msaada. Alimchagua mtu mwenye imani (Mwaminifu) katiyao kuwa mwamuzi wao, ambaye angewarejesha kwa Mungu wao na kuwasaidia kupata ushindi mkuu dhidi ya Wamidiani. KUITWA KWA GIDIONI: Waamuzi 6:11-12 Gidion aliishi Ofra na ingawaje baba yake Yoashi na watu wa mjini mwake walikuwa waabudu wa Baali, bado Gidioni alibakia mwaminifu kwa Yehova, Mungu wa Israel. Alikuwa amefanikiwa kuokoa kiasi cha ngano kutoka kwa Wamidiani,naye alikuwa akiipura au akiipepeta kila siri siku moja ikisema, Yehova yu pamoja nawe, ewe shujaa (mstari wa 12). Gidioni aliinuka kwa mshituko na kumwona mtu (ambaye kwa kweli alikuwa malaika) akikaa chini ya mwaloni uliokuwa karibu. Gidioni alisema kwake, Ee Bwana wangu, ikiwa Yehova yu pamoja nasi, mbona basi haya yote yametupata? (mstari 13). Kwa kweli Gidioni alikuwa akitumaini muujiza kutokea kuiokoa Israeli, kama alivyowahi kuwaokoa siku za nyuma. Alielewa vyema sana ni kwa nini matatizo yalikuwa yamekuja. Waisraeli walikuwa wakiteseka kwa sababu walikuwa wamemwacha Mungu na kuabudu sanamu hata nyumba ya baba yake mwenyewe ilikuwa kituo cha ibada ya Baali. Akimwangalia kwa makini Gidioni malaika alimweleza kuwa yeye ndiye ambaye mu ampatia Gidioni ishala ngu angemtumia kuwaokoa Waisraeli. Gidioni alishangaa na kuuliza "Nitawaokoaje Waisraeli?" naye akaambiwa, Hakika nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kama mtu mmoja" (mstari wa 16). Gidioni hakuamini kiurahisi kwamba (yeye) angeweza kuwakusanya Waisraeli na kuwaongoza kwenye ushindi mkuu kama huo. Gidioni aliomba ishara kwamba ujumbe huo ulitoka kwa Mungu naye akamwomba malaika kumngojea hadi atakapomtayarishia zawadi. Mara ilipokuwa tayari akamletea mwana mbuzi,mikate isiyotiwa chachu na mchuzi na kumwandalia malaika, ambaye alimwambia akiweke chakula kile juu ya jiwe (au mwamba) na kumwaga mchuzi hapo. Malaika aligusa zawadi hizo kwa ncha ya fimbo yake, na mara hiyo moto ulitokea mwambani na kukiteketeza chakula kile kasha malaika akapotea machoni pa Gidioni na ndipo Gidioni alipo tambua kwamba ni kweli malaika nduje aliye sema naye mungu alikuwa amemwonyesha Ishala ambayo alikuwa amemwona malaika wa mungu "Uso kwa uso" (mstali wa 22). Mungu akasema "Usiogope, hutakufa,"(mstaliwa 23).hapondipo Gidioni alipoanza kujitayarisha (au kujianda) kwa kazikubwa ya kuwaongoza watu wa mungu kwa (ajili ya) ushindi dhidi ya maadui zao. MUNGUAMPATIA GIDIONI ISHALA (WAAMUZI 6:34-40) Wamidiani waka jikusanya katika jeshi kubwa (leye nguvu )na kuweka hewa yao kwenye bonde la yezredi.Gidionialikuwa amepeleka ujumbe kwa makabila ya manasse, Asheri, zebuluni- na Naftali ili(kwamba) wajiunge naye katika vita dhidi ya adui zao. Halafu (au kasha) ndpo alimgeukia mungu kwa sala na kuomba apewe ishala ili afuwe kuwa mungu ya pamoja naye katika juhudi. Ya kuiokoaishala. Tazama mtaweka ngoziya kondoo sakafuni, na iwapo Umande utakuwa kwenye ngozi tu, na iwapo ardhi izungukayo itakuwa kavu, hapondipo nitatambuwa kuwa utawaokoa Waisraeli mwono wangu kama ulivyosema. (mstari 37). Asubuhi Gidioni aliona kuwa hilo ndivyo lilivyokuwa, na usiku uliofuata ishara ikafanyika kinyume kipande cha ngozi kilikuwa kikavu ambapo sakafu ilijaa umande. Sasa Gidioni aliridhika kwamba angeweza kuongoza Waisraeli hadi ushindi na kuwaonyesha kuwa nguvu yao ilikuwa imetoka kwa Yehova, sio kwa Baali. UPANGA WA YEHOVA NA WA GIDIONI:Waamuzi 7: Kwa jumla watu 32,000 waliungana na Gidioni, wakiwa tayari kufanya vita juu ya Wamidiani, lakini Mungu alisema kwamba wa 32,000 walikuwa ni wengi mno. Wamidiani walikuwa na jeshi la watu 135,000 (Waamuzi 8:10)-jeshi kubwa! Walakini Mungu angewapa Waisraeli ushindi naye hakutaka waseme, ?Silaha yangu mwenyewe imeniokoa". (mstari wa 2). Hivyo akamwambia Gidioni kuwaeleza watu waliokuwa naye, ?Yeyote anayeogopa na kutetemeka na aondoke mapema," na watu 22,000 walirudi nyumbani, sasa walikuwepo watu 10,000 waliobaki kulikabili jeshi la Wamidiani 135,000. Hata orodha hii ilikuwa kubwa mno kwa kusudi la Mungu.(naye) ndipo alipomwambia Gidioni kuwapeleka mtoni ili wanywe maji, na Gidioni ilibidi awaangalie jinsi walivyokunywa. Watu kadhaa walichota maji kwa viganja vyao na kuyatupia ulimini kama anywavyo mbwa; wengine walipiga magoti na kunywa moja kwa moja kutoka mtoni. Wale waliokunywa kama mbwa waliwekwa upande mmoja nao wakafikia watu 300. walipokuwa wakinywa namna hiyo, waliweza kuangalia kuona yaliyokuwa yakitokea pande zote(kuwazunguka). Hakuna shaka hii ndiyo ilisababisha hawa wawekwe kando. Walikuwa watu waangalifu, ambao wasingeweza kuvamiwa na maadui ghafla(bila kujua). Mungu alisema kwa hawa watu 300 angewapa Waisrael ushindi juu ya Wamidiani. Watu wengine waliobaki makambini mwao.(mstari wa 7). Usiku ule Gidioni alitiwa moyo na mazungumzo aliyoyasikia ndani ya kambi ya Wamidiani(mistari 9-15), ambayo yalimfanya atambue kwamba Wamidiani walikuwa wakiwahofia kiasi Waisrael. (angalia maelezo ya ziada). Hivyo aliwagawa askari wake katika vikosi vitatu vya watu 100 na kumpa kila mmoja tarumbeta na.iliyofichwa ndani ya vyungu (au mitungi) isiyo na maji. Muda wa mashambulizi ungekuwa "mwanzo wa zamu ya kati" (kati ya saa 4 usiku hadi saa 7 usiku). Wakitumia giza Waisrael waliizunguka kambi ya Wamidiani. Kwa ishara ya Gidioni watu wake walipiga tarumbeta wakavunja mitungi, wakainua mienge na kupiga kelele kwa sauti kuu;? upanga wa Yehova na wa Gidioni"(mstari wa 20). Jeshi la Wamidiani likiwa limeamshwa na kelele yote hiyo,waliona nuru yote ya mienge ya wanaume wa Israel kuzunguka kambi yao. Wakifikiri wamezungirwa na jeshi kubwa, askari walitaharuki na kuanza kukimbia. Ilikuwa vigumu kutambua nani rafiki na nani adui ndani ya giza. Waliogopa kila mwendo nao wakaishia kupiga panga zao wao kwa wao. Hivyo Gidioni na kikosi chake cha askari walipata ushindi mkuu, kwa sababu walifuata amri za Mungu na kuweka imani kwake. Fundisho kwetu: Gidioni aliendelea kumwabudu Mungu wakati wengi wa Waisrael na hata familia nyumba ya baba yake, walimwabudu Baali. Malaika aliposema naye bayana( au wazi) kwamba alikuwa akifikiri mambo ambayo Mungu alikuwa amewatendea Waisraeli katika enzi zilizopita (huku) akiomba ili Mungu aonyeshe nguvu zake kuwaokoa kwa mara nyingine tena. Inatupasa kuwa hivyo pia. Tunaweza kuona pia jinsi Mungu alivyo mwema kwetu siku zilizopita, katika kutuonyesha kweli iliyo ndani ya Biblia na kutubariki na mibaraka ya kila siku. Kutoka kwenye Biblia tunajifunza kwamba Mungu hivi karibuni ataonyesha. Nguvu zake duniani kwa mara nyingine tena. Atatuokoa pia,tukimtii,kutokana na uovu wa dunia inayotuzunguka. Hili ndilo tumaini kuu tulilowekewa. Inatupasa kujifunza juu yake na kulitazamia kila siku. Ndipo, Kristo ajapo,(lo)jinsi gani tutafurahi! MAELEZO YA ZIADA. Siku ile ambayo Mungu alimwonyesha (alimwelekeza) Gidioni jinsi ya kuwachagua wanaume ambao wangekwenda naye, Mungu alisema naye usiku akisema, "Amka, nenda ndani ya kambi ya Wamidiani; kwani nimewatia mikononi mwako" (mstari wa 9). Mungu aliuelewa ujasiri mkuu uliotakiwa kwa watu 300 kwenda kinyume na jeshi lile kubwa na kuwa na uhakika wa ushindi. Hivyo alimwambia Gidioni kuwa, kama alikuwa na hofu alipaswa kwenda na mtumishi wake,Fura na kufanya upelelezi ndani ya kambi ya Wamidiani. Huko angesikia kitu Fulani kingelichompa nguvu ya kwenda na kuwashinda Wamidiani. Walinyemelea (kwa kutambaa) katika giza la usiku, nao hakika kabisa walimsikia askari mmoja akimwambia mwingine juu ya ndoto ya kutisha aliyokuwa ameota. "Tazama mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika hata hema moja, ukaipiga hadi ikaanguka nao ukaipindua, hata ikalala chini. (mstari wa 13). Jibu la mwenzake lilimshangaza Gidioni kwa kuwa mkononi mwake Mungu umewatia Wamidiani na jeshi lote.(mstari wa 14). Akiwa ametiwa moyo sana na maneno haya ya kushangaza, Gidioni aliharakisha kurudi kwa watu wake 300 na kusema, Inukeni:kwa kuwa Yehova amewatia mikononi mwenu jeshi la Wamidiani.(mstari wa 15). Sasa Gidioni alihisi uhakika wa ushindi na kumtukuza Mungu kwa kumsaidia kwa njia hii. MASWALI: Majibu mafupi: 1. nani alichaguliwa kuwaokowa waisraeli kutokana na wamidiani? 2. kwa nini tunaambiwa kwamba wamidianiwalikuwa kama"mzigo? 3. Gidioni akifanya nini siku mojawakati ghafla malaika alipo sema naye? 4. Maneno gani ya malaika yalikuwa ya kwaza kwa Gidioni wakati mungu alipo mwita kuwaokowa waisraeli kutokana na adui zao? 5. Ni ishala mbili gani (ambayo) mungu alimpatiya Gidioni wakati malaika alipo sema naye? 6. Ni ishala mbili zipi Gidioni alimuomba mungu kuonyeshwa kwa ngozi ya kondoo? 7. Ni watu wangapi mungu aliwa chaguwa mwishoni kwenda na Gidioni? 8. Jinsi gani Gidionina watuwake wali wavamiya ghafla maaduizao? Majibu ya kina: 1.Gidioni hakuamini kikamilifu (au kwa dhati)kwamba mungu alimtaka yeye kuwaongoza waisraeli dhidi ya wamidiani. (a) eleza jinsi malaika alisema naye na kuwapatiya ishara (b) Ni ishala nyingine mbili zipi alizoomba Gidioni? 2. Mungu alimwambiya Gidioni kwamba watu 32,000walikuwa wengi mno kupigana na midiam. (a) Kwa nini? (b) jeshi la Gidioni lilichaguliwaje ? 3. Upanga wa Yahava na wa Gidioni" Eleza habali za vita ambapo kelele hii kubwa ili tekelezwa . Majibu ya ziada: 4.Eleza jinsi mungu alivyomtiamoyo Gidioni kwa mazungumzo aliyoyasikiya kwenye kambi ya wamidiani.