1. NYAMA KWA ISRAELI "Nani atakaye tupatia Nyama tule?" Shabaha Kuonyesha kuwa Mungu atatupatia mahitaji yetu. Ana uwezo wa kufanya lolote na atawatunza wale wampendao. Muhtasari Mungu aliwaleta wateule wake wana wa Israeli kutoka Misri na kuwapa Torati na kiongozi shupavu. Wakawa Taifa, Taifa la Israeli, na BWANA akawa mfalme wao. Watu walianza kufanya kazi kwa kujenga maskani kulingana na maelekezo aliyopewa Musa ili kwamba Mungu wa Baba zao aweze kuishi nao. Ilikuwa wanamwabudu yeye tu. Walitakiwa wawe watakatifu au "Waliojitenga" na ilikuwa waishi kwa mujibu wa sheria yake (Torati) kuwaonyesha mataifa yaliyowazunguka kwamba walikuwa watu wa Yahwe (BWANA) wakiitwa kwa jina lake (Kumb28:9-10) Mungu aliahidi : "ikiwa mtaisikia sauti yangu kwelikweli na kulishika Agano langu basi mtakuwa hazina ya pekee kwangu mimi juu ya watu wote kwa kuwa nchi yote ni mali yangu" (Kutoka 19:5-8). Hesabu 9:15-23, 10, 11, na 12. KUSIMAMISHWA KWA MASKANI: Hes: 9:15-23. Baada ya miezi sita waliyotumika kutekeleza maagizo ya Mungu ya kutengeneza maskani na samani zake, kila kitu kilikuwa tayari. Katika siku ya kwanza mwezi wa kwanza katika mwaka wa pili baada ya kuondoka Misri, Maskani ilisimamishwa katika mlima wa Sinai (Kutoka 40:17-19). Mungu alijionyesha uwepo wake miongoni mwa watu wake katika wingu juu ya Maskani wakati wa mchana, na usiku ilionekana nguzo ya moto juu yake(Kut 13:21-27). Baada ya wingu kuondolewa juu ya Maskani, Wana wa Israeli waliendelea na safari yao,lakini kama wingu lisingeondolewa isingewezekana kuondoka mpaka siku ile mawingu yalipochukuliwa (Kut. 40:33-37) ISRAELI ANAONDOKA KUTOKA SINAI: Hes:10:1-13, 33-36. Musa aliambiwa na Mungu kutengeneza tarumbeta mbili za fedha ambazo viongozi wangezitumia kuwakusanya watu pamoja kwa sababu mbalimbali. Kwa mfano zilipulizwa kama ishara ya kuanza safari. Katika siku ya ishirini ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya kuondoka Misri; wingu lilitolewa kutoka juu ya Maskani. Hii ilikuwa ni ishara ya Waisraeli kwamba waondoke Sinai ambako walikuwa wamekaa kwa miezi kumi na moja (Kut. 19:1, Hes. 10:11) Sanduku kubwa na samani vilifunikwa kwa uangalifu na Haruni na wanawe. Hakuna mtu mwingine yeyote ambaye angevigusa au kuviangalia. Maskani iliteremshwa chini ya vipande vipande na vyote vilichukuliwa na Walawi (Hes.4:15,20) Watu waliposikia sauti ya tarumbeta ya fedha wangekuwa tayari kuondoka kuendelea na safari yao. Wingu lingewaongoza kuwaonyesha njia mara kwa mara Israeli alienenda kwa namna ya kipekee kama alivyoamuru Mungu, kila kundi la makabila chini ya bendera ya kiongozi wao. "Daima Yuda aliongoza njia na sanduku lililobebwa juu juu, na watu kila walipotembea walianza na kumaliza siku kwa sala aliyopewa Musa na Mungu" (Hes. 10:35- 36). ISRAEL ANALALAMIKA KUHUSU CHAKULA (MANA) NA AKATAMANI VITU VYA MISRI (Hes: 11-5,31-33). Ilikuwa ni safari ya siku kumi na moja tu kwa kupita mlima Sinai hadi mpakani mwa Kanaani (Kumb.1:2), lakini ilimchukuwa Israeli karibu miezi kumi kusafiri kutoka Sinai hadi Kadeshi upande wa kusini wa mpaka (linganisha Hes.10:11 na Kumb. 2:14). Njia ilikuwa kupita katika nchi kame, jangwa la kutisha hata kuwafanya watu kukata tamaa na kukinaishwa. Walisahau kuwa Mungu alikwisha kuwapa uhuru kutoka utumwani na kwamba alikwisha waondoa kutoka Misri; na kuacha kufikiria kuhusu Nchi ya Ahadi mbele yao; "nchi nzuri na nchi kubwa yenye kutiririka maziwa na asali". (Kumb. 3:8). Walianza kulalamika. Walilalamika kuhusu mana na kutamani aina mbalimbali za vyakula walivyokuwa wanapata wakiwa Misri. "Isipokuwa hiyo mana, hakuna chochote kilicho mbele yetu" walilalamika. "Nani atakayetupatia nyama tule?. (Hes. 11:4-6) Walikumbuka mambo ya nyuma walipokuwa Misri badala ya kuangalia mbele kuhusu Nchi ya Ahadi. Musa aliwakasirikilia kwa kumtaabisha aliposikia watu wakilia katika mahema yao. Mungu alichukizwa na malalamiko yao. Mungu angewapatia nyama wale iwapo shida yao ilikuwa ndiyo hiyo. "Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala siku kumi,wala siku ishirini; lakini mtakula kwa mwezi mzima hata hapo nyama hiyo itakapokutoka katika mianzi ya pua zako, nanyi mtaikinai". (V.V. 19- 20). Ndipo alipotuma upepo mkali ulio leta kware katika kambi lao. Kwa tamaa waliwakusanya na kuanza kula, lakini walikula kwa uchoyo, wakisahau kwamba Mungu ambaye aliwapa chakula alipaswa kushukuriwa kwa chakula alichowapa. Chakula kikiwa kikingali midomoni mwao, Mungu alionyesha hasira yake kwa kuwapelekea tauni miongoni mwao na wengi wao walifariki. Jina la mahali hapo likaitwa Kibroth - Hattaaval, ikiwa na maana ya "Kaburi la wenye tamaa". WIVU WA MIRIAM NA HARUNI: Hes. 12. Manung'uniko na malalamiko ya watu hata yalipelekea kuwaathiri viongozi wao. Hata Miriamu na Haruni walimpinga Musa. Walisema ,"Je! ni kweli BWANA amenena na Musa tu?. Hakunena na sisi pia?".(mst.2). Ilimbidi Mungu kuwaonyesha kuwa ilikuwa siyo sahihi kumwonea wivu Musa. Aliwaita Musa, Haruni na Miriamu kwenda hema ya kukutania kule alizungumza nao akiwa katika nguzo ya wingu. "Akiwapo nabii kati yenu, mimi BWANA, nitajifunua kwake katika maono na nitasema naye katika ndoto. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu Musa, yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote kwake nitanenanaye mdomo kwa mdomo, maana waziwazi wala si kwa mafumbo; na umbo la BWANA ataliona: Mbona basi hamkuongopa kumnenea mtumishi wangu ,huyo Musa?". (Mist.5-6) Kama ishara ya hasira ya Mungu, Miriamu alipigwa na ukoma. Haruni aliomba msamaha wa dhambi zao na Musa aliomba kwa Mungu akamsihi Mungu apate kumponya Miriamu. Mungu alikubali sala yake, lakini aliamuru Miriamu afungiwe njia ya kambi kwa muda wa siku saba, baada ya hapo arejeshwe tena katika kambi. Musa alionyesha upole wa kweli - alijua kwamba Mungu alimchagua yeye kuwa kiongozi wa Waisraeli, hata hivyo hakujivuna wala kujisifu hata kidogo.Alifanya tu yale aliyo agizwa na Mungu hakuwachukia au kuwakasirikia ndugu zake wakiume na wakike walipomuonea wivu bali alimtegemea Mungu kuyaweka mambo yote sawa. Haruni na Miriamu walipata funzo kwani hawakurudia tena kuhoji mamlaka ya Musa. FUNDISHO KWETU. Mungu anahitaji imani (Ikiwa na maana ya sisi tunaamini Mungu anayoyasema) na utiifu katika amri zake. Na tusiwe wasioamini na kulalamika kama vile Waisraeli walivyokuwa katika jangwa. Na tuwe kama Musa, mtumishi wa Mungu ambaye hakuwa na mashaka jinsi Mungu atavyowalinda Israeli. MASWALI Majibu Mafupi: 1. Ni nani aliyeteuliwa na Mungu kuwa kiongozi wa Israeli? 2. Je,watu walijuaje lini waanze safari yao ya jangwani? 3. Ni kabila lipi daima lililotangulia walipoanza safari?. 4. Ni nani aliyebeba sehemu zotu za madhabahu na samani zake?. 5. Ni namna gani Mungu alivyowaonyesha watu njia?. 6. Mungu aliwatumia nini watu kula baada ya wao kulalamikia mana?. 7. Kwa nini Mungu alituma tauni kwa watu ili hali walikuwa wanakusanya na kula kwale?. 8. Miriamu na Haruni walisema nini kumpinga Musa?. 9. Musa alikuwa ni mtu wa wasifu (tabia) gani?. MAJIBU YA KINA Watu wa Israeli walisafiri kutoka mlima Sinai kuelekea Nchi ya Ahadi. 1. (a) Je,watu walijuaje lini waanze kusafiri na lini wasimame ili kujenga kambi?. (b) Mungu aliwaonyeshaje njia? (c) Ni nani aliyebeba sehemu yote ya maskani na samani zake waliposafiri?. 2. Eleza unavyoelewa jinsi Waisraeli walivyonung'unika na kulalamika baada ya kuondoka Sinai. MAJIBU YA ZIADA: 3. Mariamu na Haruni walimwonea wivu Musa. Eleza nini kilitokea na Mungu alisema nini kuhusu Musa.