25. SIKUKUU TATU ZA WANA WA ISRAELI "Nawe utafurahi katika mambo mema BWANA, Mungu wako aliyokupa wewe" Shabaha Kuonyesha jinsi wana wa Israeli, walipokwisha kukaa katika nchi ya Ahadi, walipaswa kumwabudu Mungu kama Taifa kwa njia ya kutunza Sikukuu zilizokuwa zimepangwa katika Torati aliyopewa Musa. Mungu aliandika amri kumi kwenye mbao mbili za mawe, na pia alimpatia Musa sheria nyingine nyingi za kuwaongoza watu katika maisha yao ya kila siku. Jinsi walivyopaswa kuwatendea majirani, jinsi ya kupanda na kutunza mazao yao watakapokuwa wamefika Nchi ya Ahadi na sheria nyingine nyingi pia. Kama watu wangetii sheria ya Mungu, wangetarajia Baraka nyingi kuwafikia baadaye. Mungu angewabariki kwa wingi wa mavuno, afya njema na usalama kutoka kwa maadui zao (Kutoka 34:24). Kulikuwa pia na kanuni muhimu za kuabudu. Moja kati ya hizo ilikuwa ni lazima ila mtu ahudhurie mbele ya Mungu mara tatu kwa mwaka, mahali pale ambapo Mungu angechagua (Kumbukumbu la Torati 16:16). Nyakati zote hizo zilijulikana kuwa ni “Sikukuu za BWANA” .Na ingawa zilijulikana kuwa ni Sikukuu hazikuwa zinamaanisha kuwa watu watumie muda wao wote kwa kula na kufurahia kwa kunywa. Zilikuwa ni nyakati za kusanyiko makini, ambapo walikusanyika pamoja na kutafakari Neno la Mungu na kufurahi kwa pamoja kwa sababu ya tumaini moja ambalo wote walikuwenalo. Walikuwa wakitarajia wakati ambao ahadi kwa Ibrahimu, Isaka na Yakobo zitakapotimizwa na dunia yote kujawa na Utukufu wa Mungu (Hesabu 14:21). Mambo ya Walawi 23. SIKUKUU YA PASAKA:Mambo ya Walawi 23:4-8 Sikuu ya Pasaka ilisherehekewa siku ya kumi na nne ya kila mwezi wa kwanza kila mwaka, ilikuwa ni siku sawa na siku ambayo Pasaka ya mwanakondoo kwa mara ya kwanza alipochinjwa na kuliwa katika Misri. Ilikuwa ni ukumbusho au kukumbuka kwa wana wa Israeli. Usiku ambao Malaika wa Mungu alipita juu ya nyumba zao na kuwaacha hai Waebrania, ambapo wazaliwa wa kwanza wa watu na wanyama katika Wamisri waliangamizwa. Damu ya Mwanakondoo ili nyunyizwa kwenye miimo miwili na katika vizingiti vya nyumba za wana wa Israeli na wakawa wameokolewa kutoka hukumu ya Mungu ya kutisha. Na kila wakati kila mwaka, kila familia katika Israeli ilichinja mwanakondoo na kumwoka( kuchoma)motoni na kumla pamoja na mboga zenye uchungu na mkate usiotiwa chachu. Watoto walifundishwa jinsi Mungu alivyowachukua baba zao kuwatoa Misri kwa Ukombozi Mkuu. Ili kusherehekea siku kuu hii (na ikiwa ni pamoja na Sikukuu zingine) watu walipaswa wakusanyike “Sehemu moja ambapo nimeliweka Jina langu”. Hii ilikukwa ni kwa wengine kuwemo ndani ya Maskani na wengine wakiwa wameizunguka ,Hapoa wana wa Israeli walipokukwa wamekwisha kikaa katika Nchi ya Ahadi. SIKUKUU YA PENTEKOSTE (AU MAJUMA ) MAMBO YA WALAWI 23:9-22 Iliwapasa wana wa Israeli wahesabu majuma saba wakianzia siku ya kwanza baada ya Sikukuu ya Pasaka. Siku iliyofuata, na kufuatiwa na majuma saba (ikawa jumla ni siku hamsini) iliadhimishwa kama “Sikukuu ya Majuma” katika Agano Jipya sikuu hii inaitwa ‘PENTEKOSTE” ikiwa ni maana ya siku ya “Hamsini”. Sikukuu hii ilifanyika wakati wa kufurahi na kutoa shukurani. Sikukuu iliwapatia nafasi ya kukusanyika na kumtukuza Mungu kwa Baraka zake kubwa wakati wa mavuno. Ilikuwa ni kuwafundisha wana wa Israeli kuwa mema yote hutoka kwa Mungu na kuwa wao wanapaswa kumshukuru Mungu, wamtambua yeye ambaye Baraka zote hutoka kwake. Ngano ilikuwa inavunwa wakati wa sikukuu hii, lakini kabla watu hawajakula ngano hii waliyokuwa wamevuna, iliwapasa wamtolee Mungu kwanza sehemu ya mazao hayo ya ngano. Na baadhi ya mazao hayo yalisagwa na kuwa unga ambao walitengeneza mikate miwili au keki ambayo walimtolea Mungu. Hii ilikuwa ni kuwafundisha somo kwamba Mungu ni lazima awe ndiye wa kwanza kabla ya yote. Kama tutampatia Mungu vilivyo bora, atahakikisha kuwa wakati wote tuna vitu vya kutosha kwa ajili ya mahitaji yetu. SIKUKUU ZA VIBANDA: Mambo ya Walawi 23:24-44 Siku kubwa ya Upatanisho ilikuwa ni siku ya kumi ya mwezi wa saba na sikukuu ya Vibanda ilikuwa ni siku ya kumi na tano ya mwezi huo huo .Ilikuwa ni wakati wa mwisho wa mwaka wa kulima ambapo msimu wa kuvuna mazao ulikuwa umekwisha. zabibu, zeituni na tini zote zinakuwa zimekusanywa (zimevunwa) kabla ya mvua kuanza kunyesha. Neno ‘Kibanda ‘ au booth, kama inavyoitwa, maana yake ‘Kibanda kidogo’ mfano wa kimoja wapo kilicho pale Sukoth (maana yake booths). Soma somo la 18. Katika wakati wa siku hizo sadaka kubwa nyingi na dhabihu nyingi zilitolewa na kazi ya aina yoyote haikuruhusiwa kufanyika. Siku ya kwanza walipaswa kuchukua matawi ya miti mizuri, matawi ya mitende na mierezi ya vijitoni na kutengeneza vibanda kwa ajili familia zao. Walipaswa kuketi na kuzungumzia wakati Mungu alipowatoa wana wa Israeli kutoka Misri na kuisimulia habari hii yote tena, wakikumbuka kuwa baba zao (waliketi) waliishi kwanza katika vibanda au hata wakati Mungu alipowakomboa kutoka Misri. “Nanyi mtafurahi mbele za BWANA, Mungu wenu, muda wa siku saba” (mstari 40) FUNDISHO KWETU Kwa karne nyingi baada ya kuwapatia Torati ya Musa, Mungu alimtuma nabii wake Malaki kuwaambia wana wa Israeli jinsi ambavyo walishindwa kuishika torati ya Mungu. Bado walikuwa wakiendelea kwenda hekaluni kumtolea Mungu, lakini walikuwa hawampatii Mungu kilicho bora na wala hawakumtumikia kwa Upendo. Wakatoa sadaka za Wanyama walio wagonjwa na vilema badala ya wanyama wasio na doa na kasoro yoyote na Mungu akasema “Ninyi mna niibia mimi” (Malaki 3:8-10). Watu walifikiri kuwa ni vibaya kuteketeza mnyama aliye mzuri kwa ajili ya sadaka. Kwa hiyo wao wakajichukulia nafasi ya kwanza na wakampatia Mungu kitu kile ambacho wao hawakukitaka kwa namna yoyote. Lakini Mungu akasema, kama watu watatubu na kumletea Mungu kile kilicho bora katika vitu vyao walivyonavyo kwa upendo, Mungu angewapatia Baraka, ili kwamba katika maghala ya nyumba zao isiwepo nafasi ya kuweka mavuno ya nafaka zao. Tunapaswa kujifunza na sisi pia kuwa tunaweza kumwibia Mungu ikiwa tutashindwa kumpatia kile kilicho bora kwetu. Yesu alifundisha kanuni ya namna hiyo hiyo; Utafuteni kwanza Ufalme wa Mungu na haki yake yote, na hayo yote mtazidishiwa (Mathayo 6:33). Mungu ataweza kuona kuwa mahitaji yetu ya kila siku anayatimizia ikiwa tunampatia nafasi ya kwanza katika mioyo yetu na mawazo yetu pia MAELEZO YA NYONGEZA Wakati wana wa Israeli walipofika Kanaani, walitakiwa kuishi katika nchi wakiwa wakulima.Mwaka wao wangeutumia kwa kuandaa udongo, wakipanda na hatimaye ni wangevuna.Bila shaka ilikuwa ni wakati wa kufurahia kwa maana kuvuna mavuno ni matokeo ya kazi ya mtu. Sikukuu zote za BWANA zilikuwa na eneo maalumu katika mwaka huo wa mavuno ya kilimo kwa sababu maalumu. Mungu ni kama mkulima anayepanda mbegu njema (Habari njema za ufalme wa Mungu na mambo yote kuhusu jina la Yesu Kristu). Aliwapeleka Watumishi wake kama vile Manabii na mitume ambao waliangalia kwa makini ukuaji wa mmea (hasa Neno la Mungu katika mioyo ya watu) hadi wakati wa mavuno (wakati Yesu Kristo atakaporudi tena duniani) (Mathayo 13:38-43). Mavuno haya yalikuwa ni ya watu, ambao katika maisha yao walimpenda Mungu na kumtii Yeye, na kwa wakati wote walimpatia kila kilichokuwa ni bora. Watu wa hawa watapewa sehemu katika ufalme wake wenye utukufu ambao utadumu kwa miaka elfu moja, na baada ya miaka hiyo, Mungu atakusanya tena atakusanya mavuno yake mengi ya mwisho. Watu wenye haki wa damu na nyama walioishi katika ufalme wake wakati wa miaka elfu moja. Na mwisho wote watakapokuwa wamekusanyika pamoja, kama mfano wa siku ile ya mwisho ya mavuno ya sikukuu ya Vibanda walipokusanyika ndani ya Vibanda, utakuwa ni wakati wa kufurahia ambao kamwe haukuwahi kuwapo wakati kama huo, kwa kuwa kusudi la Mungu la uumbaji litakuwa limetimia. “Hakika kama mimi, niishivyo” Mungu alisema “dunia yote itajazwa na utukufu wa BWANA” (Hesabu 14:21). MASWALI Majibu mafupi 1.Ni aina gani ya sheria ambayo Mungu alimpatia Musa pamoja na amri kumi? 2.Mungu aliwaahidi nini watu ikiwa watii sheria zake? 3.Wanaume walifika mara ngapi kuja kumwabudu? 4.Ni majina magapi ya sikukuu tatu zilizo muhimu sana. 5.Katika historia ni wakati gani muhimu wana wa Israeli walikumbuka sikukuu ya Pasaka? 6.Jina lingine la Sikukuu ya Majuma ni lipi? 7.Ni fundisho gani watu wa Israeli walilojifunza kutokana na Sikukuu ya majuma? 8.Sikukuu ya Vibanda iliwakumbusha wana wa Israeli kuhusu nini? 9.Wakati wa Sikukuu za Vibanda watu waliishi wapi? Majibu Ya Kina Sikukuu za BWANA ilikuwa ni kusanyiko la wana wa Israeli kwa ajili ya kumshukuru Mugu 1.Eleza yote unayoyajua kuhusu Sikukuu ya Pasaka. 2.Eleza yote unayoyajua kuhusu Sikukuu ya Vibanda. 3.Ni kwa nini Nabii Malaki alisema Waisraeli wamemwibia Mungu? Majibu ya Nyongeza 4.Ni aina gani ya mavuno ya dunia ambayo Mungu atavuna kwa ajili ya utukufu wake? 5.Ni wakati gani Mungu atavuna mavuno yake ya mwisho? 6.Ni kwa kusudi lipi wana wa Israeli walipewa Sikukuu za BWANA?