* Ujumbe kwa marafiki zangu
Ambao utaanzishwa juu ya dunia hii. Yesu Kristo atarudi kutawala kama Mfalme. Mji mkuu wake utakuwa ni Yerusalemu.
* Ninajua kuja kwake kukaribu, kwa sababu Biblia inasema itakuwa wakati wayahudi, watu wa Mungu watakuwa wakirudi katika nchi yao Israeli.
* Yesu mwenyewe alisema atarudi wakati kutakuwa dhiki kati ya mataifa na woga bila uwezekano wa mwanadamu kujipusha au kujiokoa
* Biblia pia inaniambia kuwa kutakuwa na vita na uharibifu duniani kote na kuwa ghadhabu ya Mungu itamwagwa juu ya binadamu.
* Ninaamini kuwa Yesu Kristo atawafufua waliokufa wakiwa wanajua ujumbe wa Mungu na kuwajalia uzima wa milele (kutokufa) wale waaminifu
* Watamsaidia Yesu kutawala ulimwengu hadi dhambi na mauti zimeondolewa kabisa na dunia itajawa na utukufu wa Mungu milele.
Matendo 1:11. Luka 21:24-28. Yoeli 3:1,2,16. 1 Wakorintho 15:22-26. Danieli 7:27. Habakuki 2:14.
“Maana katika Sayuni itatoke sheria na neno la Bwana katika Yerusalemu”. Isaya 2:3
* Jitayarishe kwa Ufalme wa Mungu ujao
Kama unataka kujua mengi juu ya mafunisho ya Biblia:- tafadhali rudisha Kuponi hii kwa anwani iliyochini hili upate Kitabu cha Mwongozo wa Kusomo Biblia pamoja na chengine cha Muhtasari Bila Malipo.
Tuma kwa:- Christadelphian Bible Mission (Tanzania)
Hivyo nina jaribu kumfuata Yesu Kristo Wakristadelfiano (Ndugu katika Kristo) wanaamini mafundisho yote ya Biblia ambayo ni pamoja na:-
1. Biblia ndio ujumbe pekee na wa kweli kutoka kwa Mungu na ilipeanwa kwa ujumia na Yeye.
2. Kuna Mungu mmoja pekee, Baba, aliyeumba dunia na anakusudi kubwa nayo.
3. Roho Mtakatifu ni uwezo (NGUVU) wa Mungu mwenyewe, ambayo uitumia kufanya mapenzi yake matakatifu.
4. Yesu ni mwana wa Mungu. Yeye pia ni mwana wa Adamu kupitia kuzaliwa kwake na Mariamu.
5. Yesu alishinda majaribu yote na akafa awaokoe wafuasi wake kutoka kwa dhambi na mauti.
6. Yesu alifufuliwa kutoka kwa wafu na Mungu. Baadaye alipaa mbinguni lakini atarudi.
7. Wakati ararudi atawafufua na kuwahukumu waumini waliokufa na kuwapa kutokufa (uzima wa milele) wale waaminiifu.
8. Atakuwa mfalme juu ya ufalme wa Mungu utakaoru-dishwa Israeli, na juu ya dunia nzima.
9. Wafuasi wake ambao watakuwa na miili hisiyoweza kufa watamsaidia kuleta haki ya milele na amani duniani kote.
10. Ibilisi sio kiumbe kisicho cha ulimwengu huu yaani si malaika lakini ni jina lengime la dhambi, iharibiwayo tu
katika Kristo.
11. Wokovu unausiana na kufunikwa kwa dhambi kupitia kwa Yesu na uhuru kutoka kwa dhambi na mauti wakati
atakaporudi.
12. Wakati mtu anapokufa ukoma kuishi. Tumaini pekee ya uhai ni ufufuo wakati Yesu atarudi.
13. Kuamini katika ahadi za Mungu juu ya ufalme wake na kazi za Yesu Kristo ni muhimu.
14. Toba na ubatizo katika Kristo kwa kuzikwa ndani ya maji na ufuasi wa kila siku wa Kristo ni muhimu kwa wakovu hatimaye.
Ninajua Mungu yuko – Ushuhuda wake unanizunguka. Kiumbe fulani kilifanya ulimwengu huu wa kiajabu – Na kiumbe fulani uufanya uendele!
Ninatakikana tu niangalie maua ama samaki ama nisikize sauti ya ndege au nitafakari maajabu ya jicho, sikio, au ubongo ...
Kujua kuwa kuna kiumbe kiliazimia haya yote Mbingu juu yangu na vilivyomo lazima vina utukufu wao na kila kitu kina la kusema juu ya yule anayeziunganisha pamoja kwa mkono wake wazi wenye nguvu. Chini hapa katika sayari dunia ambayo imeharibiwa na mwanadamu, maajabu ya Mungu ni mengi. Ujaza mashamba mapya na maziwa madogo na aina mbalimbali za uhai. Yake ni mifugo katika milima elfu, na yake ni uhai (Nafsi) wa kila mwanadamu Nimemwona Mungu akifanya kazi. Ufanya kazi maishani mwangu pia-Akiongoza matukio yote, na kupitia Neno lake Takatifu Uniongozakuwa na imani katika Mwana wake mpendwa.
* Omba Mungu msaada wake ...
Kuna Biblia moja ya kweli. Ni kitabu cha kale zaidi duniani. Udai kuwa kinatoka kwa Mungu na, wakati nikikisoma ufanya kweli. Vitabu vyake 66, vilivyoandikwa kwa mda wa miaka 1500, ushikamana kikamilifu pamoja, na ujumbe wake unakubaliana. Agano la kale na agano jipya zinasema injili moja kuu. Vile Biblia inavyosema na matukio ya kale yanaambatana. Hakuna mwana historia au mtu wa sayansi alivyeonyesha kuwa inasema kivyengine. Na hakuna siku atafanya hivyo. Kwa hakika kile wachunguzi wa mambo ya kale na uchunguzi wa kweli unafumbua, ni kuwekea mkazo ukweli wa maandiko matakatifu. Mungu uongea na watu wanyenyekevu kupitia kurasa za kitabu hiki. Ndani yake kuna ahadi Zake na masharti ambao anapeana uhuru, haki na uzima wa milele. Ni hapa tu ninaweza kujifundisha mpango wake mkuu juu ya dunia kupitia kwa mwana wake, Yesu Kristo – na hapa ninaweza kupata sehemu pia. Mungu amehifadhi neno lake kutoka karne hadi karne, ingawaje mwanadamu mara nyingi amejaribu kuiharibu. Kwa hivyo ninaweza kuisoma kwa lugha yangu na hivyo kuanza kufanya yale Mungu ananiambia nifanye ndani yake. Gambo la chuo liloiovumbuliwa katika Bahari Mfu (Dead Sea) mwaka 1947 ni thibitisho kuwa Agana la kale juu ya siku ya Yesu haijabadilika kwa karibu miaka sasa 2,000.
* Soma Biblia kila siku …
Ninaamini Yesu alizaliwa Bethlehemu karibu miaka 2,000 iliyopita. Mungu alikuwa Baba yake kupitia kwa Roho mtakatifu juu ya Mariamu, mwanamwali wa kiyahudi, kwa hivyo Yesu aukuwa mwana wa Mungu, na pia mwana wa Adamu. Akikuzwa huko Nazareti, alikua na neema na hekima katika neno la Mungu. Akiwa na miaka 30 alikuwa tayari kutangaza Injili baada ya kubatizwa katika mto Yordani. Kwa maneno ya ajabu na miujiza mingi. Yesu alihubiri habari njema ya Ufalme wa Mungu. Mwishowe alikufa juu ya msalaba, hili awe Mwokozi kwa wote waaminio. Siku ya tatu Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na kumpatia Uzima wa milele. (kutokufa) Sasa yuko mbinguni kama Bwana aliyefufuka mpatanishi pekee kati ya Mungu na Mwanadamu. Kwa sababu ninaamini katika Injili na ushindi wa Kristo juu ya dhambi namauti ninatafuta kumfuata yeye sasa na kujitayarisha kwa kurudi kwake kuwa Mfalme juu ya Nchi. Hii ndio sababu nimebatizwa katika Kristo na hivyo kupokelewa kama mmoja wa Jamii ya Mungu katika Kristo. Katika jina lake ninamuomba Mungu: ninamkumbuka Yesu kila juma katika kumega mkate na kunywa Divai.
Luka 1:35, 2:52. 4:43 1 Wakorintho 15:3-4, 11:23-26 Warumi 6:3-4
Jifudishe juu ya Mwokozi Yesu Kristo.