_____________________
MASOMO YA BIBLIA KWA NJIA YA POSTA YA WAKRISTADELPHIAN 1-4
Correspondence Course Lessons 1-4
_____________________

Mtengenezaji: Jonathan Nkombe
MASOMO YA BIBLIA KWA NJIA YA POSTA YA
WAKRISTADELPHIAN SOMO LA 1.
JINSI YA KUTUMIA KOZI HII YA BIBLIA
Somo: Zaburi 19
Kozi ya Biblia kutoka kwa Wakristadelifia imekusudia ili ikusaidie kuielewa Biblia, ambayo ni Neno la Mungu. Wakati mwingine Biblia imeitwa “Maandiko”, ni kitabu tu ambacho ni cha kutegemewa kinacho tuambia kuhusu Mungu na kuhusu mipango yake kwa dunia na watu juu yake. Inaahidi baraka kwa kila mmoja akisomaye pamoja na nia njema ya kutaka kuielewa.
Unatakiwa uwe na Biblia yako
Ni haki ya mtu kuwa na nakala ya Neno la Mungu. Kwa kuifuata kozi hii unatakiwa uwe na nakala yako mwenyewe ya Biblia (sio Agano Jipya tu). Ikiwa huna unatakiwa kununua popote mahali panapo uzwa Biblia. Kila mahali katika kila nchi Biblia zinauzwa. Lakini kama haiwezekani wewe kupata moja, tafadhali mwambie mwalimu wako mara moja, atafanya utaratibu wa kukupatia moja.
Kozi hii ina karatasi 40 za mara moja kwa wiki. Kama mtu anayekutumia masomo anaishi mbali na wewe utakuwa unapokea masomo kadhaa pamoja na karatasi moja ya maswali yote kwa pamoja mara moja kwa mwezi. Mwalimu anayekutumia masomo ni:
Namba yako ya kumbukumbu ni _________________________
Tafadhali tuma namba hii juu ya majibu yako yote kwenye karatasi n.k.
Tafadhali tuma majibu yako yote (na swali lolote) kwa mwalimu wako. Itasaidia ikiwa tu utamwandikia mwalimu wako, hata kama utahitaji kusoma zaidi na ikiwa utaona anuani zingine kwenye vitabu vyetu vingine.
Vifungu vya maandiko ambavyo utavikuta katika kozi hii vimetolewa kutoka Biblia ya Kiingereza ya A.V. Vilevile kuna tafsiri zingine nzuri za kisasa kama R.S.V. na Tafsiri. Mpya ya Kimataifa (N.I.V.) lakini katika nchi zingine zaweza kutopatikana. (Utakuta kwamba tafsiri ambayo tunayo katika Afrika ya Masharika ni Muungano wa Tafsiri (U.V.) ambayo ni tofauti kidogo na nilizo zitaja hapo juu.) Lakina tafsiri yoyote utakayo tumia haitabadili usomaji wako wala maana haitatofautina sana.
(1)
Kozi hii ya Biblia ni bure. Gharama yako itakuwa ni kuisafirisha barua yako kwa Posta kwenda kwa mwalimu wako mara moja kwamwezi. Shabaha yetu ni kukusaidia wewe ufurahie usomaji wa Maadiko, na tunataka wewe utambue ujumbe wa ajabu wa wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Hatutoi vyeti baada ya kumaliza Kozi, bali mwisho wa masomo 40 tutapenda kukusaidia kuendelea na kujifunza Biblia.
Ushahidi wa Biblia
Wakati ushahidi unapo tolewa kutoka kwenye Biblia utakuwa umeandikwa kama hivi:
Mwanzo 1 – hii inamaana Kitabu cha Mwanzo, sura ya 1; au Mwanzo 1:1-7 – hii inamaana Kitabu cha Mwanzo, sura ya 1, mstari wa 1 hadi 7 na kuendelea.
Jinsi ya kujifunza masomo
Fanya mazoezi ya kujifunza somo moja kwa wiki. Tunashauri kwamba hakikisha kuwa unaelewa ukurasa wa kwanza kabla ya kuendelea na ukurasa unaofuata. Itakusaidia ikiwa utasoma kila somo mara tatu. Mara ya kwanza, ni kuelewo ni nini kinacho ongelewa; mara ya pili ni kufunua vifungu katika Biblia yako na kuandika neno au maneno kwenye karatasi kwa ajili ya maswali au jambo lolote gumu; na mara ya tatu ni kusoma somo lote tena pamoja na sura uliyo shauriwa kusoma ambayo unaikuta mwanzoni mwa kila somo. Kisha, mwisho wa kila somo utakuta mistari mingine ya kukusaidia kutafuta katika Biblia yako, na andiko mstari mmoja ambao umesisitizwa kwa nguvu ili wewe ujifunze kwa moyo. Utakuta kwamba mistari hii itabaki katika kumbukumbu yako na itakuwa ni msaada kwako maisha yako yote.
Pamoja na kuweka karatasi ndani kwa ajili yako pia tunaweka MPANGO WA KUSOMA BIBLIA. Huu unakupa njia ya kusoma sura moja ya Biblia kila siku. Ikiwa unapenda kufanya hivi kwa haraka utakuwa mzoefu wa sehemu mbalimbali za Biblia. (Ukipenda unaweza kuweka ndani ya Biblia yako huu mpango wa kusoma Biblia, kwa matumizi ya kila siku.) Kisha kuna msaada mwingine ambao tunatumaini utataka kuwa nao. Baada ya mwalimu wako kupokea karatasi majibu yako ya somo la 1, atakutumia nakala ya bure ya kitabu kidogo kinacho itwa KITABU CHA KUANGALIA KUSOMA BIBLIA. Hiki kina fafanuzi fupi juu ya masomo ya kila siku. Pia ni kitabu cha kumbukumbu ya maana inayohusu Biblia na kina ramani nyingi ndogo na mifano ya kukusaidia katika kujifunza.
Kujibu Maswali
(2)
Tunakuomba utume majibu yako kila mwezi kwa mwalimu wako. (Kwa njia ya Posta, tafadhali). Ujibu maswali katika maneno yako mwenyewe. Usinakili au kuigiza masomo yanavyo sema. Jaribu kusema kile ambacho wewe unaamini kuwa ni kweli. Ikiwa hukubaliani na chochote katika masomo, au una maswali yoyote, tafadhali sema. Hii ni muhimu sana. Kumbuka, tuna weza kukusaidia wewe zaidi mno kama tukijua unachofikiri. Iwapo kwa sababu yoyote huwezi kutuma majibu, basi tuma maelezo mafupi ya kusema bado unapenda na unataka kuendelea na kupokea makaratasi kwa ajili ya kujibu maswali.
Muda wako mzuri
Kwa kweli, kujifunza masomo haya yatakuchukulia muda wako mwingine – labda dakika 15 kwa kila siku kwa ajili ya kusoma Biblia na kiasi cha saa kwa wiki moja kwa ajili ya kusoma somo. Pia utahitaji muda wa kujibu karatasi ya maswali. Lakini utakuta kwamba Maandiko yanavutia sana hata utapenda kutumia muda zaidi na zaidi kwa kusoma.
Usome Biblia yako kwa kumuomba Mungu
Anza kila kipindi cha kusoma Biblia au kujifunza kwa na kumuomba Mungu, ukiomba msaada ili Mungu akusaidie kuielewa Biblia. Hapo kuna sala kutoka kitabu cha Zaburi:
“Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zaburi 119:18)
Kama tukimuomba Yeye, Mungu atafumbua macho yetu na kutusaidia kukielewa Biblia kitabu chake.
Iwapo hatuta pokea ujumbe wowote kutoka kwako
Tunahakika kwamba utaelewa kuwa kuna watu wengi duniani ambao wanataka kupokea kozi hii ya Biblia. Iwapo hatutasikia toka kwako (kwa mfano wewe kutuma majibu yaliyo kamilika) tutasadiki kuwa hutaki tena kupokea kozi. Basi hatutaendelea kukufumia masomo.
Kama una matatizo yoyote katika kujibu au kutuma karatasi za majibu kamili, tafadhali wasiliana na mwalimu wako na utoe maelezo. Wakati huo tutapenda kuendelea kutuma kozi tunachotaka ni kujua iwapo masomo yanapokelewa na yanatumika kukusaidia katika kujifunza Neno la Mungu.
(3)
Masomo kamili ya koziya Biblia
Ifuatayo ni orodha ya majina ya masomo 40:
Jinsi ya kutumia Kozi hii ya Biblia
Wa-Christadelphian ni nani?
Biblia ni Kiongozi Wetu
Injili
Unapewa karatasi ya maswali ya somo la 1-4
Mungu na Uumbaji
Mungu aliupenda Ulimwengu
Kurudi kwa Yesu Duniani
Ishara za Kuja kwa Yesu
Unapewa karatasi ya maswali ya somo 5-8
Ufalme Wako Uje
Mtizamo wa Mungu kwa mambo yaliyopita
Ufalme wa Mungu – Amani Duniani
Unapewa karatasi ya maswali ya somo 9-11
Ahadi za Mungu kwa Abrahamu
Historia ya Wayahudi – sehemu ya 1
Historia ya Wayahudi – sehemu ya 2
Ahadi za Mungu kwa Daudi
Unapewa karatasi ya maswali ya somo la 12-15
Baba na Mwana
Maisha ya Yesu
Kifo cha Yesu
Kufufuka na Kupaa kwa Yesu Kristo
Unapewa karatasi ya maswali ya somo la 16-19
Roho Mtakatifu wa Mungu
Vipawa vya Roho Mtakatifu
Dhambi na Matokeo yake – sehemu ya 1
Dhambi na Matokeo yake – sehemu ya 2
Unapewa karatasi ya maswali ya somo la 20-23
Kwa Nee ma Mmeokolewa
Ufufuo wa Wafu
Hukumu
Uzima Usio na Mwisho
Unapewa karatasi ya maswali ya somo la 24-27
Malaika
Mashetani (mapepo) na Shetani
Ibilisi na Dhambi
Ubatizo
Unapewa karatasi ya maswali ya somo la 28-31
Ndoa ya Kikristo
Matatizo katika Ndoa
Jukumu letu kwa Serikali
Sala
Kuenenda katika Upya wa Uzima
Unapewa karatasi ya maswali ya somo 32-36
Kusoma Biblia kila Siku
Ushirika pamoja na wale wenye Imani Moja
Muhutasari wa Mafunzo ya Biblia
Hatua inayofuata
Unapewa karatasi ya mwisho ya maswali ya somo la 37-40
(4)
WA-CHRISTADELPHIA NI NANI? Soma la 2
Soma : Yohana 15
Nia ya kozi hii ya Biblia ni kukuongoza uangalie Maandiko. Ingawa, utaweza kustaajabu Wa-Christadelphia ni nani, basi tutakuambia kidogo kuhusu sisi wenyewe.
Wa-Christadelphia ni jamii ya wanaume na wanawake walio enea pote ulimwenguni ambao wanasoma Biblia yote na wanaiamini kuwa ni Neno La Mungu. Wanaziamini ahadi zilizo katika Angano la Kale na Jipya zinazo mhusu Bwana Yesu Kristo na ulimwengu ujao. Wanamsubiri Yesu arudi kutoka mbinguni aje kuusimamisha Ufalme wa Mungu duniani. Jina Christadelphian linatoka kwenye maneno mawili ya Kiyunani ambayo yanamaana Ndugu katika Kristo.
Wa-Christadelphian wanaishi wapi?
Kuna Wa-Christadelphia katika nchi zaidiya 50. Wanapatikana Uingereza na sehemu nyingi za Ulaya; katika nchi zaidi ya kumi na mbili za Afrika; katika mashariki ya mbali kutoka India hadi Indonesia; Australia na Pasifiki kwenye Visiwa; Amerika ya Kusini na Kaskazini kutoka Kanada kwenda chini hadi Ajentina, na Visiwa vya Karibeani. Hii jamii inamchanganyiko wa wanaume na wanawake wenye tofauti rangi na malezi tofauti. Wanaongea lugha tofauti.
Wana amini nini?
Imani yao Wa-Christadelphian imeweka juu ya mambo yaliyo aminiwa na yaliyo fundishwa na Yesu na wafuasi wake karibu miaka 2000 iliyo pita. Ujumbe wa kweli wa dini ya Kikristo haujabadilika. Kwa bahati mbaya, walakini, makanisa mengi ya “Kikristo”, yameiacha kweli na yamegeukia mafundisho ambayo asili yake ni kutoka katika imani za kipagani. Kwa upande mwingine, siku zote kumekuwepo na kundi la watu ambao wameishika imani ya kweli. Kwa mfano, Ulaya zaidi ya miaka 400 iliyo pita kulikuwepo na watu wengi walio jifunza injili ya kweli kwa kujisomea wao wenyewe Biblia wakat ilipo chapishwa katika lugha zao wenyewe, badala ya kusikiliza makasisi walio kuwa wanazungumza Lugha ya Kilatini, lugha ambayo walikuwa hawaifahamu. Hawa wanaume na wanawake walijiita wenyewe “Ndugu katika Kristo”. Jambo la kusikitisha wengi wao walitendewa jeuri ya ukatili au waliuawa kwa ajili ya imani yao. Wengi iliwabidi wahame makazi yao, lakini walichukua Injili Ulaya yote na kutoka upande mmoja wa bahari hadi upande wa pili. Haukupita muda mrefu, ukweli uka changanyika na mafundisho yaliyo potoka. (Hapa kuna somo — Kweli inafundishwa tu hapo watu wanapo jifunza Neno la Munga wao wenyewe.)
(5)
Jamii ya Wa-Christadelphian ilianza namna gani?
Katika mwaka 1832 daktari mmoja wa Kiingereza aliye itwa John Thomas, ambaye alikuwa mhubiri wa kanisa, alipanda meli kuelekea New York kwa sababu baba yake alitaka kuhamia Marekani. Meli ilipatwa na msukosuko wa mawimbi makubwa hata daktari Thomas aliwaza kuwa anaelekea kufa. Alitambua kwamba alijua kidogo mno kuhusu wakati ujao, ndipo alitoa nadhiri kwamba ikiwa atafika nchi kavu hatapumzika mpaka apate ukweli kuhusu uzima baada ya kifo. Vema, alifika New York, na akawa salama kama neno lake. Alitumia miaka 15 iliyofuata kwa kusoma Biblia kwa makini sana na kupima madai ya madhehebu mengi ya “Kikristo”. Alipo kuwa na uhakika ameelewa vya kutosha mambo yaliyo andikwa katika Agano la Kale na Jipya kuhusu Yesu Kristo na ujio wa Ufalme wa Mungu duniani alipanga kubatizwa, aliendelea kuhubiri hadharani Marekani na Uingereza naye alichapisha magazeti ya dini na vitabu.
Miongoni mwao walio amini mafunzo yaleyale na kujiunga na John Thomas katika kazi yake alikuwa ni mtu wa Scotland aliye itwa Robert Roberts. Alisaidia kupanga idadi iliyo kuwa inaongezeka ya wafuasi na kuwa eklesia. “Eklesia” ni neno la Biblia lililo na maana “kusanyiko la watu walio itwa”. Wa-Christadelpia wanapenda kulitumia neno hili, kuliko “kanisa — ambalo wakati mwingine linatana ya jengo kuliko kundi maalum la watu walioitwa na Mungu.
Kwa mara ya kwanza jina linaweza kuonekana ni geni kidogo
Jina Kristadelphia kwanza lilitumika katika mwaka 1864 wakati waumini walipo iomba Serikali ya Marekani kuachiliwa kwao toka shughuli za kijeshi wakati wa vita vya ndani ya Marekani. Wakihitaji jina la utambulisho. Waumini kama jamii iliyo ittenga, John Thomas alikumbuka “Ndugu katika Kristo” miaka 300 kabla, na hivyo alitumia jina hilo la namna ya Kiyunani. Jina “Christadelphian” maana yake “Ndugu katika Kristo”. Hawa Wa-Christadelphian wa karne ya 19 walikuwa wasafiri wakubrwa nao walihubiri sehemu nyingi za ulimwengu. Pia wafanya biashara wakichukua injili ya kweli pamoja nao kwenye safari zao, hivyo basi mwisho wa karne kukawa na vikundi vya waumini katika nchi nyingi.
Utaratibu wa Wa-Christadelphia ni wa namna gani?
Hatuna watumishi wanaolipwa na hakuna utaratibu wa uongozi kama makanisa yaliyopa. Mahitaji ya fedha yanakabiliwa na matoleo ya washiriki wanaotoa kwa hiari. Hatuna makasisi. Tuna ofisi kadha katika nchi sio nyingi kwa ajili ya kuchapisha magazeti na vitabu, na kuna halmashauri mbalimbali kwa ajili ya kupanga kazi ya kusafiri kuhubiri na kutunza wagonjwa, wazee na yatima. Lakini unaweza kuuliza: ikiwa hakuna mkusanyiko mkuu wa kuwaunga pamoja na
(6)
washirika wote, ni jinsi gani wanasaidiana hawa Wa-Christadelpia? Jibu ni kwamba imani yetu tuliyo nayo sote na nazoea yetu yote ni kiungo cha kanuni ambacho kinawashikamanisha washirika pamoja.
Kila sehemu moja ya kundi inakuwa na kila kitu na linachagua watu “wazee” wake, mara kwa mara kwa kuwapigia kura mara moja kwa mwaka. Wale ambao wamechaguliwa wanatumika katika eklesia kwa shiughuli mbalimbali kama ukatibu, kazi ya kutunza fedha, usimamizi au kama Mwenyekiti wa mikutano. Hawalipwi kwa ajili ya kazi zao. Wao sio “makuhani”, kwa maana tunaamini kuwa Yesu kwa sasa yupo mbinguni na ndiye Kuhani pekee — kwa yeye washirika wa Kanisa lake walio batizwa wanaweza kukiri dhambi zao katika sala. Wa-Christadelphian hawajengi majengo kwa kuyapamba mapambo makubwa. Kwa kweli, kuna sehemu zingine ambako maklesia yanauwezo wake yenyewe kuwa naukumbi au chumba kwa ajili ya kukutana na kukubiri. Lakini kila mahali wanakutana katika vyumba vya shule au katika kumbi za jamii zinazo kaa pamoja au kwenye nyumba zao.
Imani moja
Wa-Christadelphia, katika sehemu yoyote ya ulimwengu wanako ishi, wanasoma na kujifunza Biblia zao na wamekuwa na kanuni ya imani moja. Kwa zaidi ya miaka 100 tumekuwa na Maelezo ya Imani (muhutasari wa mufunzdisho ya Biblia) ambayo kila mshirika anakubali kuwa ni msingi wa ushirikiano pamoja na washirika wengine. Maelezo ya Imani pia yana orodha ya mafundisho potovu yaliyo anzishwa na Makanisa mengine ambayo tunayakataa kwa kuwa yapo tofauti na Maandiko. Kabla mtu yeyote hajabatizwa na kuwa Mchristadelphian mwanaume (au mwanamke) inabidi mwenyewe aridhike kwamba anaelewa mafunzdisho muhimu ya Biblia na kuwa anakubaliana na maandiko yote ya imani. Hivi ndivyo vinavyo wafungamanisha Wa-Christadelphia pamoja.
“Mwili mmoja... Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja” (Waefeso 4:4-5)
Hii inafanya iwezekane kwa Wa-Christadelphia, popote wanapo ishi, kushiriki furaha na ushirikiano wenye thawabu pamoja na kila mmoja.
Aina ya watu tunatakiwa kuwa
Sisi sote twahitaji msaada wa Mungu. Kwa hiyo tunaamini ni muhimu sana kuomba. Kitu kimoja tunacho jaribu kufanya kila siku ni kusoma Biblia. Hivyo ni muhimu sawa na kupata chakula kila siku. Mara moja kwa wiki tunakutana kula kipande kidogo cha mkate na kunywa divai kwa ukumbusho wa kifo cha Bwana Yesu Kristo. Utakuta kwamba Wa-Christadelphia ni watu wenye furaha sana kwa sababu wanau uhakika wa imani ya matendo.
(7)
Lakini hatufanyi mchezo na maisha tunayo ishi, kwa maana kurudi kwa Yesu kupo karibu sana hivyo twahitaji kuwa tayari kwa ajili ya ujio wake. Hiyo ina maana kuishi maisha mazuri na yaliyo nyooka. Ina maana kuwa na mke mmoja tu, na kutofanya tendo la ndoa kabla au nje ya maisha ya ndoa. Maana yake kuepuka ulevi, ulafi, kucheza kamari na tabia nyingine mbaya.
Wa-Christadelphia ni raia wanao shika sheria za nchi zao. Wanajaribu kufanya yote mema wanayo weza kufanya, walakini hawajishirikishi na siasa, wala hawafanyi ugonvi au kuwapeleka watu mahakamani. Baadaye katika Kozi hii utaona umuhimu wa mambo haya.
Kazi ya Biblia waliyotumwa Wa-Christadelphia
C B M kama tunavyo iita, ni tawi letu la kuhubiri Injili ya Ufalme wa Mungu ulimwenguni pote. C B M inatangaza kozi za kujifunza wasio lipwa, bali ni Wa-Christadelphia walio jitolea kufanya kazi hii, vilevile wanafanya kazi zao walizo ajiriwa. Shabaha yake ni kuwasaidia wanaume na wanawake kujifunza Injili, katika moyo, watubu na wabatizwe, na popote inapowezekana kuanzisha eklesia jipya la Christadelphia.
Tunataka kushiriki imani sahihi, tumaini na furaha pamoja nawe
Wa-Christadelphia kwa ujumla wana amini kuwa imani yao inaonyesha Injili ya kweli kama inavyopatikana katika Biblia nzima. Tunatumaini kuwa nawe, pia, utafurahi kuivumbua Kweli.
Haitoshi tu kuwa inaridhisha kwa kuwa ni sahihi, bali pia inaleta tumaini, furaha na upendo kwa maisha yako. Mungu akubariki katika kuitafuta hii Kweli.
Mafundisho mengine muhimu yamechapishwa kwenye vijitabu vidogo vidogo.
Mistari ya kusoma : Zaburi 119:130; Mathayo 28:19-20; Yohana 17:3
Jifunze kwa moyo : Yohana 15:13-14
“Hakuna aliyena upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake, Ninyi mmekuwa rafiki zangu mkitea nda niwaa muruyo”
MAFUNZO MENGINE MUHIMU YA BIBLIA
Biblia ni ujumbe wa kweli tu kutoka kwa Mungu.
Kuna Mungu mmoja tu, Muumba, ambaye ndiye anayaongoza mambo ya ulimwengu.
(8)
Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, alizaliwa na Mariamu. Alikuwa ni mtu asiye na dhambi. Alikufa msalabani ili kuwakoa wanao mwamini. Alifufuliwa kutoka kaburini na sasa yuko mbinguni.
Yesu atarudi mapema kutoka mbinguni. Atausimamisha Ufalme wa Mungu duniani. AtakuwaMfalme na makao yake makuu yatakuwa Yerusalemu katika nchi ya Israeli.
Wayahudi ni mashahidi wa Mungu katika makusudi yake, hata ingawa wengi wao hawatambui. Mungu aifanya ahadi kwa Abrahamu na Daudi ahadi ambazo zitatimizwa wakati Yesu ataporudi.
Mauti ni adhabu kwa ajili ya dhambi na watu wote ni wenye dhambi. Tumaini la pekee la uhai baada ya kifo ni ufufuo wa mwili kutoka kaburini hapo Yesu atakapo rudi.
Kutakuwa na hukumu. Wale ambao ni wafuasi waaminifu wa Yesu watapewa uzima wa milele nao watamsaidia Yesu kutatua matatizo ya ulimwengu na kuleta amani na baraka kwa mataifa yote.
Yatupasa kuiamini Injili, kutubu dhambi zetu na kubatizwa. Kama tukijaribu na kuendelea kujaribu kwa bidii kutii maagizo ya Mungu, na kuomba msamaha tunapo shindwa, ndipo tutaokolewa.
Unabii wa Biblia kuhusu mambo yaliyopita na matukio yaliyopo ya ulimwengu yote yamekuwa kweli. Ishara zinaonyesha kwamba kurudi kwa Yesu Kristo duniani kumekaribia sana. Ndiyo maana unatakiwa kushughulika na Biblia yako sasa.
(9)
MASOMO YA BIBLIA KWA NJIA YA POSTA YA WAKRISTADELPHIA Somo la 3.
Kusudi La Uzima wa Milele Ni Nini?
Mamilioni ya watu watakosa uzima wa milele na wao wenyewe hawajui kusudi la vumbaji na maana yake au mwisho dunia hii. Mungu, Muumbaji mkuu wa vitu vyote, ametuambia yote tunayo hitaji kuju katika kitabu, Biblia.
Tunapo fikiri maajabu ya ulimwengu unao tuzunguka, na njia ya kushangaza namna miili yetu ilivyo umbwa, tunaona pasipo shaka kuwa Muumba mkuu alikuwa katika kazi. Lakini tunawezaje kumjua zaidi, na kutafuta anatutaka tufanye kitu gani? Kama tukitaka kumpendeza, yatupasa tuichukue Biblia na tuisome kwa bidii, na tuitafakari siku kwa siku.
Biblia inayo madai makubwa. Inanena kwa mamlaka, na kudai kuwa ni Neno la Mungu. Mara nyingi manabii wa Agano la Kale wana anza ujumbe wao kwa maneno: "Bwana asema hivi". Mtume Paulo anatuambia kwamba "kila andiko lina pumza ya Mungu" (2 Timotheo 3:16). Neno "pumzi" maana yake ni kwamba Mungu yeye ndiye kwa ujumla aliongoza kila kitu kilicho andikwa ndani ya Biblia. Aliwaambia watu kipi cha kuandika. Ni Neno lake hasa. lkiwa madai haya yangekuwa siyo ya kweli na Biblia isingekuwa ya kweli wala isingekuwa ni Neno Lake, tunge achana nalo. Hatakama mafundisho yake ni mazuri kiasi gani, yangekuwa hayana matokeo yoyote kwetu.
Lakini Biblia ni ya kweli. Tusithubutu kuidharau - isipokuwa tukitaka kumdharau Mungu, na kujizuia wenyewe kwenye uzima wa milele aliotupatia sisi.
Je, kuna ufunuo mwingine ulio andikwa kutoka kwa Mungu?
Jibu kwa swali hili ni "Hapana". Kuna dini nyingi ulimwenguni, zote zina "vitabu vitakatifu". Waislamu, kwa mfano, wana Korani, ambayo wanaiona kuwa ni Neno la Mungu. Wamormoni wana "Kitabu cha Mormoni" ambacho wanasema kilitumwa kwao na Mungu. Vitabu hivi vina baadhi ya vifungu vya Biblia, vingine vinatoa ushauri wa maana ulio na busara, lakini sehemu nyingi ya vitabu hivi hazikubaliani na ujumbe wa Biblia na ha baadhi ya vifungu vya Biblia wamenakili tofauti kabisa.
Sasa ni wazi kabisa kuwa Mungu hawezi kusema kitu kimoja katika kitabu kimoja, na kitu kingine tofauti katika kitabu kingine. Kimoja tu kinaweza kuwa ni uongozi wa Neno la Mungu. Biblia ndiyo Neno la Mungu).
Ni kwa jinsi gani tunajua kuwa Biblia ni ya kweli ?
Tunalo neno la Bwana Yesu Kristo. Yesu alipokufa Mungu alimfufua siku ya tatu. Huu ni muujiza wa kushangaza. Kamwe katika historia
(10)
ya ulimwengu hakuna yeyote aliye mfufua mtu aliyekufa na kumpatia uzima wa milele.
Yesu alikuwa kaburini, alikufa na hakuwana uhai, kwa siku tatu, Baada ya siku tatu, alifufuka, akaiwa nauzima wa milele. Huu ni uhakika wa kweli kuwa alikuwa ni Mwana wa Mungu, nasi tuliamini kila neno alilo lisema.
Katika siku alizo ishi Yesu duniani, Agano la Kale pekee ndilo lilikuwa limeandikwa, naye aliamini kila neno Iililokuwa limeandikwa. Chochote alicho ulizwa popote juu ya jambo alilofanya au kusema, alisaidia maneno yake na matendo kwa kutaja maandiko katika Agano la Kale.
Wakati Masadukayo walipo mjia, wakishindana naye kwa maneno kuwa hakuna kitu kama ufufuo wa wafu, aliwaambia:
"Mwapotea, kwa kuwa hamyajui Maandiko wala uweza wa Mungu" (Mathayo 22:29).
Kisha aliendelea kuwathibitishia kutoka Agano la Kale, kwamba ufufuo wa wafu ulikuwa ni sehemu ya ufunuo wa Mungu.
Yesu aliamini...
... Katika Adamu na Eva (ona Mathayo 19:4,5)
... Katika Abrahamu, Isaka na Yakobo (ona Mathayo 8:11)
... Katika Daudi na Sulemani (ona Mathayo 12:3,42)
... Katika Yona na samaki mkubwa (ona Mathayo 12:40)
Hakuna hata mmoja aliye thibitsha kuwa Biblia ni potovu
Maadui wengi wa Biblia, ukijumuisha na watu wengine wajanja, wamejaribu sana, lakini wote wameshindwa. Tukisita kufikiri hivi, basi yatupasa kukubali kuwa ni ya ajabu
Biblia yatabiri wakati ujao
Watu hawawezi kunena kwa uhakika kuhusu wakati ujao. Pia hatuwezi kuthibitisha kipi kitatokea keshoau wiki ijayo - au mwaka ujao. Na kama kwa miaka mia moja au zaidi haiwezekani kabisa kwa yeyote kutabiri kile kitakacho tokea. Bali BIBLIA inasema, toka wakati hadi wakati, matukio ambayo yatakuja tokea miaka mingi baadaye.
Hapa ni baadhi ya mifano:
1. Kuzaliwa kwa Yesu
Katika Mathayo 2 tunasoma kuwa wenye elimu ya nyota walifika kwa Herodi na kumuuliza "Yuko wapi aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi?" Sasa ilibidi Herodi awaulize wakuu wa makuhani swali hili, nao mara moja walijibu, "Katika –
(11)
Bethlehemu ya Uyahudi". Walijuaje? Kwa sababu miaka elfu moja kabla, katika moja ya vitabu vyo Agano la Kale ilikuwu wa imekwisha tabiriwa - Mika 5:2.
Soma Zaburi 22 kisha soma kwa makini. Katika Zaburi hii kuna maelezo ya kusulubiwa kwa Yesu. Tazama mwisho wa mstari wa 16- "walinichoma mikono na miguu yangu". Angalia tena mstari wa 18-"wamegawana mavazi yangu kwa kuyapigia kura."
Sasa ukisoma Yohana 19:23-24, utaona kwa kweli kile ambacho maaskari walifanya baada ya kuwa wamemsulubisha Yesu. Kwa jinsi gani mwandishi angetabiri kifo cha Yesu muda mrefu sana kabla hakijatokea, asipokuwa ameongozwa na Mungu?
Hii ni ajabu, kwa sababu katika siku za mwandishi wa Zaburi, Wayahudi hawakujua chochote kuhusu kusulubisha - wakosaji waliuawa kwa kupigwa mawe
3. Matukio makubwa yalitabiriwa
Soma Isaya 13:19-20.Kwenye kipindi ambacho nabii Isaya alipo andika maneno haya kuhusu Babeli, lilitokuwa ni taifa kubwa ulimwenguni; lenye utukufu na nguvu, sasa mahali lilipokuwapo taifa la Babeli, kuna magofu katika eneo nusu jangwa. Miaka mia nyingi baada ya kutolewa, unabii wa Isaya ulikuja kutimia sawasawa kama alivyo tabiri. Ni Mungu pekee aliweza kuona mabadiliko kama hayo makubwa yaki timia, na ndiye anayetenda aliyoyakusudia.
Kuna mifano mingi kama hii. Ni Mungu mwenyewe tu ndiye anaweza kuona yajayo. Manabii walikuwa sahihi walipo andika: "Bwana asema hivi... "
Ajabu ya unabii wao ni ushahidi mwingine kwamba kweli Biblia ni Neno la Mungu.
Kitabu gani kisicho cha kawaida. llichukua miaka 2000 kukiandika, nacho kiliandikwa na wachunga wanyama, wafalme, daktari, mtengeneza hema, wavuvi na wengineo. Kwa kweli siyo kitabu kimoja, bali ni mkusanyiko wa vitabu. Jumla kuna vitabu 66, 39 ni katika Agano la Kale, na 27 ni katika Agano Jipya.
Waandishi wote wameunganika kutupatia habari moja nzima - habari ya nia ya Mungu na wanadamu, tangu kutoka ilivyo andikwa katika Mwanzo, hadi kwenye kipindi ambacho "Ufalme wa dunia huu umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu, na wa Kristo wake; naye atamiliki hata milele na milele" (Ufunuo 11:15).
Vitabu vya Agano la Kale
Vitabu vya kwanza vitano viliandikwa na Musa katika Agano la Kale. Kitabu cha kwanza kinaitwa Mwanzo, maana yake kuanza uumbaji wa kila kitu. Kinatuambia shughuli ya Mungu na wanadamu wa kwanza walio ishi duniani humu.
Kisha kitabu kinachofuata ni Kutoka, Walawi, Hesabu na Torati. Hivi vinne vinatuambia jinsi Mungu alivyo watwaa Wayahudi, ambao aliwachagua kuwa watu Wake, kutoka Misri
(12)
na aliwapa nchi ya Kanaani (Israeli). Vitabu vinavyo fuata vinaeleza habari ya hao Wayahudu, na Mungu akishughulika pamoja nao.
Tunapokuja katika Zaburi, tunakuta shairi zuri sana ambalo halikuwahi kuandikwa. Labda utasema mashairi hayapo kwa ajili yako? Mashairi ya kwenye Biblia ni tofauti. Yanazungumzia mawazo tuliyo nayo wakati mwingine, bado hayawezi kuwekwa katika maneno. Kwa mfano, chukua mistari hii ya Zaburi 8:3-4:
"Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani, hata umkumbuke, na mwana damu hata umwangalie?"
Haujawahi kuona namna hiyo wakati ukitazama juu kwenye nyota usiku?
Baada ya Zaburi kunakuja vitabu vitatu zaidi vya mashairi: Mithali, Mhubiri na Wimbo wa Sulemani. Kisha kuna vitabu vya manabii - kazi ya unabii mrefu wa Isaya, Yeremia na Ezekieli, vikifuatiwa na vitabu vingi vyenye unabii mfupi.
Manabii walinena kwa watu wa siku zao. Hapo Wayahudi walipo acha sheria ya Mungu na kwenda njia zao wenyewe, manabii walijaribu kuwarudisha watu wamrudie Mungu wao. Tayari tumeona jinsi walivyo zungumzia kuja kwa Bwana Yesu. Pia, walinena kuhusu matukio mengi muhimu ambayo yametokea katika historia ya ulimwengu. Matukio mengine bado hayajatimia.
Katika masomo yatakayo fuata utasikia unabii kuhusu Makusudi ya Mungu yalivyo timia katika mambo yaliyo pita, na kuhusu kusimamisha Ufalme wa Mungu.
Agano Jipya
Hili linaanza na maelezo manne tofauti juu ya maisha ya Kristo, yalivyo andikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohana - kila mmoja anasimulia habari katika namna yake. Kisha inafuata habari ya kile kilicho tokea baada ya Yesu Kristo kufufuka toka wafu. Hapa tunasoma kuhusu makanisa ya kwanza, au maklesia ambayo yaliundwa, katika kitabu kinachoitwa "Matendo ya Mitume".
Yamekuwa ni mfano wa kuigwa na makanisa yote ya leo, na tuyachukue kama mfano wa kuufuata. Kila mshirika wa kanisa siku hizo alibatizwa wakati alipokuja kuwa Mkristo. (Ubatizo huo ulikuwa wa maji mengi.) Na leo iwe vile vile.
Baada ya kitabu cha Matendo, kuna nyaraka zilizo andikwa na mitume mbalimbali ill kuyasaidia makanisa haya machanga na mwishowe kuna kitabu cha Ufunuo. lwapo unataka idadi kamili utakuta imeandikwa ndani ya Biblia yako ukifungua ukurasa wa kwanza ndipo utapata idadi kamili ya vitabu.
Mungu amepanga kutimiza makusudi yake na hii dunia kwa njia ya taifa moja - Israeli. Ni kwa njia yao, Biblia imetufikia na sisi : waandishi wa Biblia wote karibu walikuwa Wayahudi.
(13)
Mungu aliwachagua Wayahudi kuwa watu wake maalum, na kuwa mashahidi wake kwa mataifa yote (Isaya 43: 10). Mara nyingi walishindwa, na waliziasi sheria zake zenye busara. Waliadhibiwa sana kwa jambo hili.
Lakini Mungu alisema:
"Ingawa nitayakomesha mataifa yote huko niliko kutawanya, bali wewe sitakukomesha kabisa, nitakurudi kwa hukumu, nawe sitakuacha bila adhabu". (Yeremia 30:11).
Mtu aliyekuwa mkuu zaidi wakari wote alikuwa Myahudi - Bwana Yesu Kristo. Mungu alipomtuma Mwanawe, Wayahudi walimuua. Wakatawanywa ulimwenguni pote kama adhabu. Sasa, katika siku zetu, Mungu anawakusanya tena; siyo muda mrefu atamtuma tena ili awe Mfalme wao. Ndipo watakuwa kichwa cha mataifa yote.
Mambo yote haya yalitabiriwa katika Angano la Kale. Historia ya taifa la Wayahudi ilitabiriwa zamani sana, inashuhudia ukweli wa Neno la Mungu.
Ni wazo kubwa kuwa Mungu yuko mbinguni ametupatia kitabu ili kwamba tupate kumjua, na tuishi kama anavyo taka. Kwa kweli amewaambia wanaume na wanawake katika kitabu hiki kwa nini aliumba ulimwengu, na vile historia itakavyo kuwa, mpaka hapo Injili itakapo timia, na Mungu atakuwa yote kwa wote.
Biblia ni kiongozi, Mungu ametupatia, akituonyesha njia ya uzima wa milele katika Ufalme wake. Hakuna kitabu kingine kama hiki. Siyo kitabu kilicho kufa bali ni neno lililo hai. Kama tukisoma kila siku, kwa makini na sala, kitatubadilisha maisha yetu, na kuyafanya yampendeze Mungu.
Muhutasari
Biblia ni ya pekee. Inadai kuwa ni Neno la Mungu kwa wanaume na
wanawake.
2. Kinampatia mwanaume na mwanamke tumaini la uzima wa milele.
3. Yesu aliiamini Biblia.
Kuna ushahidi mwingi kuwa ni kweli: historia yake imethibitishwa na wavumbuzi wa siku hizi, kuna unabii ulio kwisha timilika.
Kinasimulia habari ya Mungu akishughulika na watu, toka kuumbwa kwa
mtu wa kwanza hadi wakati dunia itajawa na utukufu wa Mungu.
Ni zawadi ya Mungu kwetu, akituonyesha njia ya uzima wa milele Hebu na tuisome kila siku.
Mistari ya kusoma : Zaburi 1;Zaburi 22; 2 Timotheo 3.
Jifunze kwa moyo: 2 Timotheo 3:16-17.
(14)
MASOMO YA BIBLIA KWA NJIA YA POSTA YA WAKRISTADELPHIANO.
Soma la 4
Soma: Wagalatia 3:6-16
Habari Njema
Kila mmoja hufurahi kusikia habari njema. Na ndivyo injili ilivyo. Neno "Injili" maana yake "habari njema"
Habari njema ya injili ni kuhusu Bwana Yesu Kristo, na Ufalme wa Mungu unaokuja. Ni habari njema kwako na kwangu, kwa sababu inatuambia jinsi tunavyo weza kushiriki katika Ufalme huo.
Habari za maisha ya Bwana Yesu zimeandikwa katika vitabu vinne vya kwanza katika Agano Jipya: Mathayo, Marko, Luka na Yohana. Habari hizi za maisha ya Yesu Kristo zimesemwa kuwa ni 'injili'.
Hapo mwanzo
Injili ilisimuliwa kwanza maelfu ya miaka kabla ya kuzaliwa kwa Yesu • nyuma kabisa kwenye Bustani ya Edeni.
Hapo Mungu alipoumba ulimwengu, malaika waliingiwa na uzuri wake hata wakaimba kwa furaha (Ayubu 38:7). Mungu aliwaumba mwanaume na mwanamke pia, Adamu na Eva, ili kuishi humo ulimwenguni na kufurahia uzuri wake. Jambo la kusikitisha, siku moja walimuasi Mungu, nao walijitetea hukumu wao wenyewe. Na muda kadri ulivyo kwenda walizeeka na hatimaye kufa. Watu wote, tangu wakati ule wanakufa, na kipindi cha maisha wanahuzuni nyingi.
Kama mambo yangeishia hapo, ingekuwa ni habari ya kusikitisha namna gani. Bali haiukuwa ndiyo mwisho! Kwa sababu Mungu ni mwenye upendo na mwenye kuujali ulimwengu Wake, na wanaume na wanawake aliowaumba, tayari akawa na mpango wa kuwaokoa. Kule katika Bustani ya Edeni Mungu alinena mpango wake wa kuondoa uovu ulio letwa na uongo wa nyoka na dhambi ya Adamu na Eva. Mpango huu umewekwa kwa Bwana Yesu Kristo, kama itakavyo jadiliwa katika kozi ifuatayo (tazama Mwanzo 3:15).
Injili ilianza!
Injili ilihubiriwa kwa Abrahamu
Hapa, inashangaza kidogo, lakini utakuta kwamba imeandikwa katika Agano Jipya, kwa Wagalatia 3:8, kama ulivyo soma. Katika kipindi ambacho karibu watu wote walipo abudu miungu, na kutojali kuhusu Mungu, Abrahamu alikuwa mmoja wao. Akamwamini Mungu na kusadiki. Mungu akafanya ahadi kubwa kwa Abrahamu.
Injili au habari njema ambazo Mungu alimpa ilikuwa ni kitu gani? Kwanza, ilikuwa kuwa baba wa taifa kubwa - taifa la Israeli ambalo miaka ijayo litaishi katika nchi ya Israeli. Baadaye utajifunza zaidi katika kozi. Abrahamu mwenyewe aliambiwa kuwa atapatiwa nchi hiyo na kuishi ndani yake milele!
(15)
Lakini Abrahamu alizeeka na akafa, pasipo kumiliki nchi aliyo ahidiwa. Bado tunajua kwamba Mungu siku zote hutunza ahadi zake. Hivyo, kuishi katika nchi alivyo ahidiwa inabidi Abrahamu aletwe tena kutoka wafu, au 'afufuliwe'.
Pili, ilikuwa awe na uzao (umeitwa katika Biblia 'mzao') utakao leta baraka kuu kwa dunia yote. Hizo zilikuwa ni habari njema! Uzao wake katika huu bila shaka alikuwa ni Bwana Yesu Kristo:
"Uzao wako utamiliki miango wa adui (yaani, utawashinda adui zake); na kwa mzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia" (Mwanzo 22:17,18).
Ahadi alizo ahidiwa Abrahamu, Mungu alizirudia kwa mwanawe Isaka, na kwa mjukuu wake Yakobo.
Ahadi nyingine kuu
Daudi, mfalme mkuu wa Israeli, ameitwa katika Biblia, "mtu aupendezaye moyo wa Mungu". Naye pia, aliahidiwa uzao wa muhimu sana, utakao tawala kwenye kiti cha enzi huko Yerusalemu milele. Sio hivyo tu, bali uzao huu ulikuwa ni Mwana wake Mungu - hata kuwa mwingine zaidi ya Bwana Yesu Kristo. Mungu alimwambia 'Daudi:
"Nitainua uzao wako nyuma yako atakaye kuwa wa wama wako, nami nitaufanya imana ufalme wake ... nitakuwa baba yake ... nitamstalehesha katika nyumba yangu na katika ufalme wangu milele; na kiti chake cha enzi nitakifanya imara milele" 1 Mambo ya Nyakati 17:11-14).
Ujio wa mwokozi aliye ahidiwa
Hapo Yesu atakapo rudi, atatawala ulimwengu toka Yerusalemu.
“Naama kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto wa mwanamume ... maongeo ya enzi yake na amani, hayatakuwa na mwishi kamwe, katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake, kuuthibitisha, na kuutegemeza kwa hukumu na haki tangu sasa na hata milele" (Isaya 9:6-7).
Nabii Isaya aliandika maneno, haya wakati fulani baada ya kifo cha Daudi.
Wayahudi
walisubiri kwa hamu ujio wa wa mwokozi aliye ahidiwa na mfalme.
Ndipo, siku moja Malaika anayeitwa Gabrieli alikuja kutoka kwa Mungu
na kufika kwa mwanamwali aliyekuwa ana ishi katika nchi ya Israeli.
Jina lake bikira huyu aliitwa Mariamu. Malaika alimwambia:
Hii ilkuwa ni "habari njema za furaha kuu". Yesu alipo zaliwa, habari njema waliambiwa wachungaji mifugo waliokuwa kondeni usiku, wakilinda kondoo zao. Na ndipo - kama walivyo imba kwa furaha kwanzo hapo Mungu alipoumba ulimwengu, walikuja malaika na kuimba tena kwa furaha. (Unaweza kusoma Luka 2:8-18.)
Yesu anahubiri habari njema
Yesu, mwokozi aliye ahidiwa hatimaye alifika. Yesu akahubiri lnjili. Alikwenda "na kuzunguka Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuhubiri injili ya ufalme" (Mathayo 4:23). Kwa muda wa miaka mitatu na nusu alikwenda katika sehemu za juu za chini
(16)
akifundisha watu kuhusa Ufalme wa Mungu ujao, na akiwaambia watu jinsi gani Mungu anataka waishi. Mwisho wa kipindi hicho, kwa hiari alijitoa maisha yake makamilifu kuwa dhabihu, na kufa msalabani, Ili kwamba wote wanao mwamini wawe na tumaini la uzima wa milele. Akawa "mwana kondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu" (Ufunuo 13:8). Basi ahadi ya Mungu ilitimia kama alivyo sema kwa Eva kuwa atamtuma mwokozi.
Mungu akamfufua Yesu kutoka kwa wafu.
Bwana alitumia siku arobaini pamoja na wafuasi wake baada ya kufufuka kutoka kwa wafu. Halafu akapaa kwenda mbinguni, kuwa na Baba yake.
Yesu atarudi tena duniani
Wafuasi wake walipokuwa wanamtazama akienda zake, malaika wawili wakawatokea na kusema:
"Huyu Yesu aliyetwaliwa kutoka kwenu kwenda mbinguni atarudi namna hiyo hiyo kama mlivyo mwona zake mbinguni" (Matendo ya Mitume 1:11).
Atarudi tena. Hii yote ni sehemu ya habari njema.
Atarudi lini?
Hatujui siku ya kuja Yesu mara ya pili kwa Yesu. Bali tunajua kutokana na mambo yanayo tokea ulimwenguni leo kuwa haitakuwa muda mrefu kabla hajarudi tena. Kwa karibu miaka 2000 Wayahudi walikuwa hawana nchi yao wenyewe. Sasa hivi wamerudi katika nchi yao ya zamani, na mnamo 1948 Taifa la Israeli lilianzishwa. Hicho kilikuwa ni kitu kingine ambacho ilibidi kitokee kabla ya kurudi Bwana.
Ulimwengu leo umejaa na vurugu na matendo ya kuvunja sheria, na watu wanafanya wanayo yapenda kufanya, bila kizuizi. Kuna njaa, vita na magonjwa ya kutisha ulimwenguni pote. Watu wamekuwa na hofu ya mambo ya nayo kuja kutokea, kama Yesu alivyo sema kuwa itakuwa:
"Watu wakivunjika mioyo kwa hofu, na kwa kutazamia mambo yatakayo upata ulimwengu" (Luka 21:26).
Aliendelea kusema kwamba wakati mambo yote haya yakitokea, kurudi kutakuwa karibu sana. Utajifunza zaidi jambo hili katika masomo yatakayo fuata.
Yesu atarudi kuwa Mfalme wa ulimwengu
Yesu alimwambia Pontio Pilato kwamba alizaliwa kuwa Mfalme. Juu ya msalaba paliandikwa : "Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi". Lakini hatakuwa mfalme wa Wayahudi peke yao. Atakuwa Mfalme wa ulimwengu wote. Mungu alisema jambo hili miaka mingi iliyo pita. Alisema: "Atatawala toka bahari hata bahari, na toka mto hadi miisho ya dunia" (Zaburi 72:8).
Patatokea nini Yesu Kristo atakapo rudi katika dunia hit?
Atawafufua wafu na kuwahukumu. Wale wenye haki na Mungu atawapatia uzima wa milele na sehemu katika Ufalme ujao duniani. Kisha watamsaidia Yesu katika kutawala ulimwengu.
(17)
Wakati huo, Yerusalemu patakuwa makao makuu ya ulimwengu, naye Yesu Kristo atatawala dunia yote. Itakuwa furaha kuu wakati huo. Yesu aliwaambia wanafunzi wake waombe kwa ajili ya wakati huo. Aliwaambia, mnapo sali, semeni:
"Ufalme wako uje. Mapenzi yako yafanyike duniani kama yanavyo fanyika mbinguni... Maana ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu hata milele" (Mathayo 6:10-13).
Baada ya miaka elfu moja, hakuta kuwa na dhambi tena wala vifo. Mungu atakuwa yote katika wote - kama alivyokuwa amepanga tangu mwanzo:
"Kwa maana dunia itajazwa na maarifa ya utukufu wa BWANA, kama maji yaifunikavyo bahari" (Habakuki 2:14)
Ajabu ya ujumbe wa Injili ni kwamba tunaweza kuwa sehemu ya huu Ufalme
Kwa jinsi gani tunaweza kupewa sehemu katika Ufalme wa Mungu duniani?
Tunatakiwa kutambua jinsi tulivyo wenye dhambi, na tufanye kitu kingine kuhusu hili jambo la dhambi. Mtume Paulo alipokuwa Antheni alisema:
(18)
"Mungu ... anawaagiza watu wote wa kila mahali watubu, kwa maana ameweka siku atakayo wahukumu walimwengu kwa haki kwa mtu yule aliyemchagua; naye amewapa watu wote uthabiti wa mambo haya kwa kumfufua katika wafu"
(Matendo 17:30).
Mungu anawaagiza watu wote watubu. Kutubu maana yake ni kuacha kujipenda mwenyewe na kujaribu kumpendeza Mungu. Sisi sote ni wenye dhambi, hivyo yatupasa kutubu na kubatizwa katika maji. Inatubidi kuishi kama Yesu alivyosema. Kwa wale wafanyao hivi, Yesu atawapa uzima wa milele atakapo rudi.
(Nadhani umegundua kuwa Injili haipo kuhusu kwenda mbinguni - hayo siyo mafundisho ya Biblia. Injili inahusu uzima usio na mwisho katika Ufalme wa Mungu duniani.)
Maelezo mafupi
Injili ni jambo linalo semwa
katika Biblia nzima; ni Habari Njema.
Injili inamuweka Bwana Yesu
Kristo, Mwana wa Mungu, kubiri Neno la Mungu pande zote za dunia.
Injili ilifahamika na watu wote
wa zama zote waliokuwa waaminifu, katika Agano la Kale na Jipya
tangu wakati huo.
Injili ni jibu kwa dhambi na
mauti.
Injili inahusu mpango wa Mungu
kwa mahitaji ya watu. Mungu alimtoa mwokozi, Bwana Yesu Kristo.
Kuwaokoa watu Yesu aliishi
maisha makamilifu na alikufa kifo cha hiari.
Mungu alimfufua kutoka kura wafu
Bwana Yesu – na baadaye kidogo alipaa kwenda mbinguni.
Yesu atarudi kutawala ulimwengu
na kuweka Ufalme wa Mungu duniani.
Atawafufua wafuasi wake kutoka
kaburini kwa ajili ya hukumu; na wale watakao kubaliwa na yeye
watapewa uzima wa milele katika Ufalme wake.
Yatupasa tuiamini Injili na
kukubali shindano na tujaribu kuishi maisha yanayo mpendeza Mungu.
Kuiamini Injili maana yake ni
kukubali kuwa sisi ni wenye dhambi na tunahitaji kuokolewa;
hatuwezi kujiokoa; Yesu atatuokoa kama tukitubu, tukibatizwa na
kufanya kwa bidii kumfuata.
(19)
Mistari ya kusoma: Mwanzo 3:14-15; 9:11: Zekaria 9:9:
Mathayo 25:31-34; 1 Wakorintho 15:28
Jifunze kwa moyo: Mwanzo 12:1-3
"BWANA akamwambia Abramu, toka wewe katika nchi yako, na jamaa yako, na nyumba ya baba yako, uende katika nchi nitakayo kuonyesha: nitaku fanya kuwa taifa kubwa na kukubariki na kulifanya jina lako liwe kubwa; nawe utakuwa baraka: nitawabariki wakubarikio: na kuwalaani wakulaanio: katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa."
(20)
Masomo ya biblia kwa njia ya posta ya wakristadelphia.
Karatasi Ya Maswali
Jaribu na ujibu maswali katika maneno yako mwenyewe. Panaposemwa 'kazi ya ziada' unaweza kujibu swali ikiwa unataka kufanya hivyo, au kuacha ikiwa utaona ni gumu sana. Tafadhali jaribu kujibu maswali mengine yote. Usisahau kuweka jina lako kwenye karatasi ya majibu yako. Maswali yajibiwe kwenye karatasi ulizopewa.
MASOM0 1 - 4
A Andika mambo matatu 3 unayoyajua (au
uliyojifunza) kuhusu:
(a) Abrahamu
(b) Yesu Kristo
(c) Ufalme wa Mungu
B Daudi aliahidiwa nini?
C Neno 'Injili' Maana yake nini?
D Tunawezaje kuwa rafiki zake Yesu? (Yohana 15)
E Kwa nini tuna hitaji kutubu?
F 'Kwa pumzi ya Mungu' maana yake nini ?
G Kwa nini Biblia ni tofauti na vitabu vingine vyote?
H Kazi ya ziada
Zaburi 1 inatuambia nini sisi kuhusu waovu na wenye haki?
I Kazi ya ziada
2 Timotheo 3 inasemaje kuhusu 'siku za mwisho' (nyakati tunazo ishi sasa?)
(21)
Tuma majibu yako kwa:
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Jina lako ni:
![]()
Christadelphian Bible Mission
32 Blenheim Road, Far Cotton, Northampton NN4 8NW, England
(22)
Masomo ya Nyongeza:
1 902059 00 - X Matayarisho ya Ubatizo
1 902059 01 - 8 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 1-4
1 902059 02 - 6 Ukimwi
1 902059 03 - 4 Mshitaki Wenu Ibilisi
1 902059 04 - 2 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 5-8
1 902059 05 - 0 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 9-11
1 902059 06 - 9 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 12-15
1 902059 07 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 16-19
1 902059 08 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 20-23
1 902059 09 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 24-27
1 902059 10 - 7 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 28-31
1 902059 11 - 5 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 32-36
1 902059 12 - 3 Masomo ya Biblia kwa njia ya posta ya Wakristadelphian 37-40
1 902059 13 - 1 Ufunuo mlango wa kwanza - Maelezo ya maneno ya mstari kwa mstari
1 902059 14 – X Ni Kweli Yesu Kristo Alishuka Kutoka Mbinguni?
1 902059 15 – 8 Biblia Yaonyesha kuwa ni uwezo wa Mungu
Kama unataka kujifunza zaidi njia
ya Mkristo wa kweli anavyopaswa kuishi, basi ni lazima ujifunze
Biblia. Ili kukusaidia; Ecclesia la Christadelphian Bible Mission
limechapisha kijitabu kuhusu mafunzo ya Biblia katika somo hili
muhimu.
Kina
itwa Kuishi katika Kweli. Unaweza kupata nakala kutoka
Ecclesia la Christadelphian, au kutoka anuani iliyoandikwa katika
kijitabu hiki.
CBM Publishing
32 Blenheim Road, Far Cotton
Northampton, England. NN4 8NW

ISBN 1 902059 01 - 8
Registered Charity Number: 248979 / 1020558
Company Number: 2796412
Telephone +44 (0) 1604 765068
SMS: +44 (0) 772 407 2906
Email: cbmtanzania@yahoo.co.uk
Web: http:\\www.cbm-tz.org
VERSION 2