9. YERIKO

"Ukuta ukaanguka chini kabisa"

Shabaha:

Kuonyesha kwamba Israeli walikuwa na sababu za kuuteka Yeriko kwa sababu waliyaamini yale Mungu aliyosema na walitii amri zake.


Muhtasari:

Watu wa Kaanani walisikia jinsi Mungu wa Israeli alivyotengeneza njia kavu kwa ajili yao kuvuka mto Yordani na "mioyo yao ikayeyuka wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena, kwa sababu ya wana wa Israeli". (Yoshua 5).


Ndivyo hata Rahabu alivyowaeleza wale wapelelezi "Wenyeji wote wa nchi wameyeyuka mbele yenu" - hivyo Waisraeli walisubiri tu maelezo ya Bwana; nao walitii kwa uaminifu amri zake kwa utaratibu ili kupata ushindi. Yoshua 5:12 - 15; 6

 

AMIRI MKUU WA JESHI LA BWANA ANAMWAGIZA YOSHUA:Yoshua 5:12-15;6:1-6

Baada ya majuma kadhaa wana wa Israeli walipiga kambi yao Gilgali si mbali na Yeriko." Nayo mana ikakoma ambayo Mungu aliituma kwao kula kila siku walipokuwa jangwani". Wakati huo walikuwa wanakula chakula kizuri kilichotokana na mazao ya nchi ya Kanaani (Yoshua 5:12).

 

Waliweza kuziona kuta imara za Mji zikiwa zimepanda juu kupita miti ya michikichi. Hapa kulikuwa na jaribio la imani na ujasiri, kwa sababu hawakuwa na siraha nzito kama vile mitambo ya kubomolea, kuweka tundu katika kuta ndefu; lakini Yoshua alikuwa na uhakika wa ushindi na alikuwa na kila tumaini kuwa Mungu yuko pamoja naye.


Hata hivyo,Yoshua aliamua kuharibu sana Yeriko, bila shaka kuuzunguka zunguka ilikuwa ndiyo njia ambayo Mungu angetoa mji na kuuweka katika mikono yake. Alipokuwa amekaribia alimuona mtu shujaa mwenye nguvu; akiwa na upanga mkononi mwake.Bila hofu yeyote, Yoshua alimkaribia na kumuuliza, "Je; wewe u upande wetu au upande wa wapinzani (yaani maadui)?". "Mimi ni amiri Jeshi wa BWANA" lilikuwa jibu lake.


Huyu hakuwa askari wa kawaida, bali malaika wa Mungu aliyetumwa kumtia nguvu. Mbele ya mjumbe wa Mungu (malaika), Yoshua akasujudia hadi nchi na akamwuuliza; Mungu anataka nifanye nini ?Yoshua aliambiwa avue viatu vyake - "mahali hapo usimamapo ni pa takatifu" (mst 15).


Malaika alianza ujumbe wake unaosisimua kwa maneno yafuatayo:-


"Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako na mfalme wake na mashujaa wake" (mst 2). Kisha aliendelea kumwambia Yoshua jinsi mji utakavyotwaliwa. Ulikuwa ni ushindi ambao ungepatikana kwa imani siyo kwa siraha za vita (mst 3-5).


Ndani ya mji, watu walisubiri kwa hofu kubwa mno maana walitarajia kuvamiwa na Israeli. Lango kuu lilifungwa mchana na usiku. Baada ya kufungwa usiku tu.


Hakuna aliyetoka wala kuingia. Hawakuweza kufanya lolote ila kusubiri na kutegemea ugumu wa kuta za Yeriko na urefu wa kuta hizo ndizo zizokuwa kuwa ulinzi wao.Walitazamia kwa hofu kila mwenendo kutoka kambi ya Israeli, na ni lazima kuwa walikuwa wamefadhaishwa sana kwa yale waliyoyaona.

 

Mara moja kila siku kwa muda wa siku sita waisraeli wote walitoka katika kambi yao na kuzunguka Yeriko. Kwanza walitangulia watu wenye siraha za vita, makuhani saba walikuwa wakizipiga tarumbeta saba za pembe za kondoo dume; walifuatia makuhani waliochukua sanduku la Agano na mwisho walifuatia watu wote wa vita. Na walipomaliza kuzunguka walirudi kambini.

 

Kama kawaida siku ya saba walizunguka lakini waliendelea hadi mji walipouzunguka mara saba.

 

UKUTA WA YELIKO UKAANGUKA KABISA- MJI UKATWALIWA Yoshua 6:1

Masharti ya Mungu yliyotolewa na malaika kwa Yoshua yalitimia kwa ukamilifu kabisa na kila siku walienda sawasawa na jinsi walivyoshauriwa. Kwa muda wa siku sita watu walizunguka hali wakiwa kimya isipokuwa tu sauti za tarumbeta zilipigwa na makuhani.


Waisraeli waliamriwa wasipige kelele ya aina yoyote hadi Yoshua atakapowaambia. Muda ungefika Yoshua angewapatia ishara nao makuhani wangezipiga tarumbeta kwa nguvu. Ndipo watu wote wangepiga kelele sana.Mafanikio ya kazi yote yalitegemea utii wao kabisa katika kuyatimiza maagizo ya Mungu.

 

Mapema alfajiri siku ya saba walianza safari yao ya kuzunguka mpaka walipokuwa wamezunguka mji mara saba siku hiyo. Ndipo makuhani walipiga tarumbeta kwa nguvu na Yoshua akawaambia "Pigeni kelele kwa maana BWANA amewapeni mjii huu" (Mst6)


Watu walipiga kelele sana, na Mungu akasababisha kuta za Yeriko kutikisika sana na kuanguka na kuacha nafasi kwa maaskari kwenda moja kwa moja kuchukua mji na kutekeleza hukumu ya Mungu kwa watu waovu (Kumb 7:24:2-5)

 

RAHABU ANAOKOKA YOSHUA 6:21 – 27

Mungu alikuwa amemwambia Yoshua kwamba kila kitu katika mji kiangamizwe isipokuwa Rahabu na wote watakokuwa ndani ya nyumba yake wataokolewa kwa sababu yeye aliwaficha wapelelezi na alionyesha Imani katika Mungu wa Israeli.Rahabu alikuwa amekwisha kusanya familia yake yote ndani ya nyumba yake na kufunga kamba ya uzi mwekundu katika dirisha.


Kwa hiyo yeye na wote aliokuwa nao wakaokolewa kama wapelelezi walivyomwahidi. Watu wote waliobakia pamoja na wanyama waliangamizwa kwa upanga.

 

Waisraeli walikuwa wameshaonywa wasichukue kitu chochote kuwa chao kwao. Maana wangesababisha laana katika kambi ya Israeli. Mji ulikuwa umewekwa wakfu kwa BWANA aliyewapatia ushindi na kwa sababu hiyo vyote vilivyokuwemo vilikuwa ni mali ya BWANA.


Hii inamaana kwamba fedha, Dhahabu, Shaba na Chuma vitawekwa katika hazina ya BWANA na vitu vingine vitateketezwa kwa moto.


Yeriko ndio ulikuwa mji wa kwanza katika kulaaniwa na kuchukuliwa; na ushindi ulikuwa ni wa BWANA. Kwa hiyo waisraeli walipaswa kujifunza kwamba hawakupaswa kujitwalia kile ambacho ni mali ya Mungu.

 

FUNDISHO KWETU.

Fundisho kwetu kuhusu kuharibiwa kwa Yeriko matokeo ya Imani na utiifu. Waisraeli walipaswa kuamini neno la Mungu na nguvu zake zilizowawezezesha kupata ushindi na kufanya kwa usahihi yale waliyokuwa wameambiwa na Mungu.

 

UKUMBUSHO WA NYONGEZA.

Katika waebrania 11:6 tunasoma "Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu". Habari hii inatufundisha kuhusu somo hili waziwazi. Yoshua na wote walipaswa kuwa na imani ili Mungu aweze kuharibu Yeriko. Kwa imani kuta za Yeriko zikaanguka zilipozungukwa mara saba (‘Waebrania 11:30) Ilikuwa ni kazi ya Mungu. Mungu alisababisha kuta kuanguka chii. Lakini waisraeli walipaswa kuamini na kutiii kwanza.

 

"Kwa imani Rahabu hakuangamia pamoja na hao waasi". Waebr 11:31 ni Mungu alimwokoa Rahabu wakati kuta zingine zilipoanguka kabisa hadi chini.

 

Lakini tunaweza kuwa na imani kubwa namna hiyo? Paulo anatueleza kuwa imani chanzo chake ni kusikia neno la Mungu ( Rumi 10:17) kwa njia ya kusoma Neno lake ni jambo tunalopaswa kufanya ili tumpendeze Mungu. Hii inamaana tunapaswa kujifunza kumpendeza Mungu.


Rahabu alikuwa amejifunza jinsi ya kumpenda Mungu na tunafahamu jinsi alivyofanyika mwisraeli kuwa mmoja wa mzazi wa zamani wa mfalme Daudi ( Mst 1:5). Na sisi tukiwa na imani kama Rahabu tunaweza kuingizwa katika tumaini la Israeli kwa njia ya ubatizo katika Kristo yesu Bwana.


Ni kwa njia hii tunafanywa kuwa wana wa Ibrahimu na warithi sawa sawa na ahadi iliyoahidiwa na Mungu (Wag 3:29)

 

MASWALI

MAJIBU MAFUPI 

1 . Je waisraeli waliweka kambi yao wapi baada ya kuacha Yorodani? 

2. Ni maneno gani Yoshua alimwambia yule shujaa aliyekutana naya? 

3. Yule shujaa alisema kuwa yeye alikuwa ni nani? 

4. Ni mara ngapi waisraeli walizunguka mji kila siku kwa muda wa siku sita?

5. Ni mara ngapi wana wa Israeli walizunguka mji siiku ya saba? 

6. Je ilitokea nini kwenye kuta za Yeriko

7. Je wana waisraeli walipaswa kufanya nini katika mji wa Yeriko?

8. Je kuma watu waliookoka mji wa Yeriko ulipotwaliwa

9. Je hazina za Yeriko zilikuwa ni mali ya nani? 

10.Hazina ya Yeriko zilipaswa zifanyweje?

 

MAJIBU YA KINA

1.Eleza habari jinsi mji wa Yeriko ulivyoharibiwa (eleza kwa kuamzia Israeli walifanya nini kila siku. 

2. Ni fundisho lipi muhimu tunalojifunza kutokana na kuharibiwa  kwa Yeriko?

 

 MASWALI NYONGEZA

3.Eleza kuhusu Joshua kuonana na malaika karibu na Yeriko. 

4.  a) Ni jinsi gani tunavyoweza kuwa na imani kama Rahabu   na Joshua?

  b) Ni jinsi gani tunavyoweza kuingia katika tumaini la waisraeli.