“Jonathani alimpenda kama roho yake mwenyewe.”
Lengo:
Kuonyesha upendo wa kweli (usio na ubinafsi) wa Jonathani na maana ya urafiki wa kweli.
UFUPISHO:
Watu wote wa Israeli walimpenda Daudi na kuimba nyimbo za kumsifu kwa sababu ya ushindi wake mkuu juu ya Goliathi. Walipoona jinsi yeye mwenyewe alivyojisheheneza vyema (mbele ya wote) walianza kumpenda (Mstari wa 16)Jonathani, mwanae Sauli, aliyekuwa mtiifu kwa Mungu (au mcha Mungu ), mtu mwaminifu alimpenda sana Daudi; lakini Sauli alimwonea wivu Daudi na kuanza kumchukia Daudi (1 Sam. 18: 1 – 16; 20: 11 – 42; 24: 1 – 22 )
UPENDO MKUU / NA / WA / KUDUMU WA DAUDI NA JONATHANI: 1Sam: 18: 1 – 4.
Kwa sababu alikuwa mwana (kifungua mimba)wa kwanza wa Sauli, Jonathani alikuwa mrithi wa ufalme wa Israeli. Kila mmoja alitazamia atakuwa mfalme afuataye. Kuna hadithi nyingi katika kitabu cha kwanza cha Samweli juu ya imani na sifa na ujasiri wa Jonathani na Mungu angempenda kihalisi. Walakini Sauli alikuwa ameshakataliwa na Mungu kutokana na kutomtii (tazama somo la 20). Mungu alikuwa amemchagua mtu mwingine kuwa mfalme, “mtu aliyempendeza roho yake“ – Daudi mwana wa Yese, wa kabila la Yuda, kutokana na kabila lile masihi (yaani, Kristo)angetokea, kweli kabisa akaja kupitia jamaa (familia) ya ukoo wa Daudi. Habari kwamba Mungu alikuwa amemchagua Daudi pole pole zilienda kote nchini Israeli. Wakati Jonathani alibainisha kwamba Daudi angekuwa mfalme hakuchukia wala kuona wivu (1 Samweli 23: 17). Tokea wakati walipoonana kwa) mara ya kwanza, Daudi alipokuwa shujaa wa Israeli, Jonathani alianza kumhusudu (kumpenda)sana huyu mchungaji wa kondoo kijana, kwani Jonathani aliweza kuona alivyompenda mno Mungu. Ni wazi kuwa aliguswa sana na imani na ujasiri wa Daudi alipomkabili yule adui mkubwa wa Israeli, Goliathi, na bila woga kumwendea na kumuua. Kama alama ya heshima na upendo wake alivua joho lake la kifalme na mshipi na kumpa Daudi avae. Jonathani alikuwa askari shupavu, lakini alimpatia Daudi upanga na upinde pia kuonyesha jinsi alivyompenda mno. (Mstari wa 4)
CHUKI YA WIVU YA MFALME SAULI: 1 Samweli 18: 5 – 16.
Haikuwahi kumtokea Jonathani kwamba Babaye angemchukia kijana aliyependeza kama Daudi, lakini haikuchukua muda mrefu kabla matendo ya Sauli yalionyesha kwamba alikuwa na wivu na Daudi. Baada ya vita (pigano)moja na wafilisti, Sauli alisikia nyimbo na michezo ya wanawake wa Israeli kwa furaha yao kwamba Israeli ilikuwa imeshinda. Angepaswa kufurahi lakini alisikia wimbo wao – “ Sauli amechinja elfu zake na Daudi elfu kumi zake (Mstari wa 7 ). Hili lilimchukiza sana Sauli naye akaamua kumwua Daudi.
Siku iliyofuata Daudi alipomwimbia kwa kinubi kumtuliza, Sauli alimtupia mkuki akijaribu kumwua. Mara mbili, hili lilitokea na mara (zote)mbili Daudi alipona. Sauli alianza kumwogopa Daudi, kwani aliona kwamba Mungu alikuwa naye; lakini Mungu alimwacha Sauli kwa sababu ya roho yake ya uasi. Hivyo alifanya mipango, mara nyingi tu, kumwangamiza Daudi. Jinsi kila mpango ulivyoshindwa, Sauli alimchukia zaidi na zaidi. (Mstari wa 29 ), hadi hatimaye mfalme akamwamrisha Jonathani na watumishi wake wote kumsaidia kumwua Daudi “ Lakini Israeli yote na Yuda walimpenda Daudi. (Mstari wa 16).
Jonathani alikuwa mwana mwaminifu sana, lakini alifahamu kwamba Mungu alikuwa amemchagua Daudi kuwa mfalme juu ya Israeli. Hivyo alimlinda Daudi hata wakati Sauli alikuwa anafanya mipango ya kumwua. Ilimfanya Jonathani kuhuzunika sana naye akamwonya Daudi, juu ya mipango ya uovu ya Baba yake kumbembeleza asilipe mabaya kwa Daudi kwa wema (ambao) Daudi aliokuwa ameutenda siku zote kwake. Maneno ya Jonathani yalikuwa ya upole na kweli hivi kwamba Sauli “ akaisikiliza sauti ya Jonathani; naye Sauli akaapa, kama aishivyo Yehova hatakufa (hatauawa ). (1 Samweli 19: 10, 18 ).
DAUDI AENDA MAFICHONI (1 Samweli 20: 11 – 42 ).
Jonathani aliamini kabisa kwamba Baba yake alikuwa amebadili mawazo yake. Daudi aliletwa tena katika Ikulu ya mfalme, lakini tena Sauli alichukua mkuki kumtupia Daudi. Hivyo mara hii Daudi alitoroka kwenda kwa nabii mzee Samweli na kukaa naye Rama (1 Samweli 19: 10, 18 ).
Basi (kasha) siku moja Daudi na Jonathani walikutana kwa siri. Kwa sababu kila mmoja wao alimpenda mno Mungu, upendo kati yao ulikuwa na kuimarika. Walifanya agano pamoja shambani, ahadi ya kubaki waaminifu na wa kweli mmoja kwa mwenzake. Jonathani alimfanya Daudi pia (naye)aahidi, kwamba atakapokuwa mfalme ataendelea kuonyesha wema kwa jamii (familia)ya Jonathani. Siku iliyofuata, wakati wa mwezi mpya (mwezi mwandamo), kulikuwa na sherehe, lakini Daudi alikuwa bado anajificha katika mashamba na hakuja kula mezani pa Sauli. Mwanzoni, Sauli alijidai kutokujali, lakini siku ya pili alimwuliza Jonathani kwa nini “mwana wa Yese“ hakuja kwenye sherehe? Jonathani alimwambia Baba yake kwamba alikuwa amemruhusu Daudi kujiunga na jamaa (familia) yake Bethlehemu kwa ajili ya dhabihu kule. Sauli aliweza kuona kwamba Jonathani alikuwa akimlinda Daudi, kwani alielewa kulikuwa na uhusiano wa nguvu wa urafiki kati yao. Sasa hasira za Sauli ziligeukia kwa Jonathani, mwanaye mwenyewe mwaminifu. “kwa kadiri mwana wa Yese anaishi (duniani)wewe hutapata maendeleo, wala ufalme wako. Kwa ajili hiyo sasa (hivi) mwite aje kwangu, kwani ni lazima afe.“ (Mstari wa 31).
Jonathani alipojaribu kumsemea Daudi, Sauli alikasirika mno kiasi cha kumfanya atupe mkuki kwake. Jonathani aliweza kuona kwamba maneno yalikuwa hayafai tena. Akiwa amepofushwa na wivu, Baba yake hangeweza kupumzika mpaka amwue Daudi. “ Hivyo Jonathani akasimama (akaondoka)mezani katika hasira kali – kwani alihuzunika kwa ajili ya Daudi. Kwa sababu Baba yake alikuwa amemwaibisha. (Mstari wa 34). Jonathani alikuwa amepanga kabla kukutana na Daudi mashambani na kumweleza iwapo hasira za Sauli zilikuwa zimemalizika au la.
Kwa masikitiko sasa wakaagana, kwani haikuwa salama kwa Daudi tena. Inambidi kukimbia kwa kuokoa uhai wake. “Nenda kwa amani,” alisema Jonathani kwa kijana rafiki yake,“ Yehova awe kati yangu na mimi, na kati ya uzao wangu na uzao wako milele. (Mstari 42).
DAUDI ARUDISHA WEMA KWA UOVU: (1 Samweli 24 ).
Sauli sasa amwinda Daudi mithili ya mnyama. Akiwa na kundi dogo la wafuasi, Daudi alijificha katika majangwa na milima. Wakati Sauli alimfuata, Mungu alimlinda (alimtegemeza), wakati mwingine alimwonya jinsi ya kutoroka kutoka kwa Sauli (1 Sam. 23: 9 – 12). Siku moja Sauli alikuja kupumzika ndani ya pango ambamo Daudi na watu wake walikuwa wakijificha. Askari wote 3000 wa Sauli walikuwa nje na Sauli alikuwa peke yake. Watu wa Daudi walimnong’oneza kwamba sasa ilikuwa fursa (nafasi) yake kumwua mfalme, lakini Daudi hakufanya hivyo kwani Sauli alikuwa mpakwa mafuta wa Mungu. Lakini alimnyemelea (kwa kutambaa)karibu na Sauli aliyekuwa amelala usingizi, na kukata kipande cha upindo wa nguo yake, mara alipotambaa tena kurejea kwa watu wake akiwa na kipande cha nguo ya Sauli mkononi mwake, Daudi alisikitika hata kwa kufanya hivyo. Sauli alipoamka kutoka usingizini na kuondoka kutoka kwenye pango, Daudi akamfuata nje na kumpigia kelele kumwita, “ Bwana wangu, mfalme (Mstari wa 8 ), na kuinama mbele yake kumsujudu.
Alimwambia Sauli jinsi alivyotiwa moyo na watu wake amwue pangoni, lakini alimwachia uhai wake. Kuthibitisha jinsi alivyokuwa karibu akamwonyesha Sauli kipande cha vazi lake. Daudi akasema (kwa dhati)na Sauli ili amwamini na kuona kwamba hakumfanyia dhambi yoyote; basi je, ni kwa nini mfalme amwinde ili achukue uhai wake? Mfalme Sauli alisukumwa na wema na uaminifu wa Daudi na kuona aibu kwa uovu wake. “cha haki kuliko mimi “ alisema Sauli kwa Daudi, “kwa kuwa umenilipa wema, ambapo nimekulipa maovu”. Na sasa tazama najua wazi kwamba utakuwa mfalme na kwamba ufalme wa Israeli utastawi mikononi mwako. (Mstari wa 7 – 20). Akamwomba Daudi kamwe asimdhuru yeyote katika ukoo wake kama yeye alivyotaka kumdhuru Daudi. Daudi aliahidi kwa furaha kama alivyoomba Sauli na hivyo wakaacha Sauli akienda nyumbani lakini Daudi na watu wake wakirudi mapangoni na vilimani mwa Israeli.
Majuto ya Sauli, kama siku zote, hayakudumu kwa muda mrefu. Upesi alikuwa nje tena kumwua Daudi, mpaka Daudi alilazimika kukimbilia katika nchi ya wafilisti. Alikaa kule mpaka Daudi alipokufa nao watu wa Yuda kwa haraka wakamwita arudi ili wamfanye mfalme.
FUNDISHO KWETU:
Kwa sababu ya pupa na chuki, Sauli alijaribu kumzuia Daudi kufanyika mfalme. Chuki yake ilimpeleka kwenye hasira na uongo na hata kujaribu kumwua Daudi. Mungu hangemsaidia mtu wa aina hii. Sauli, kwa hiyo ni mwongo kwetu sisi dhidi ya pupa (wivu)au chuki kwa wengine. Wivu haraka hugeukia kwenye chuki, na hiyo ni mbaya kama uuaji machoni pa Mungu (1 Yohana 3: 15 ). Daudi alihisi huruma tu kwa Sauli. Alirudisha wema kwa maovu na upendo kwa chuki. Bwana Yesu Kristo hutukumbusha sisi juu ya funzo hili muhimu: “Mimi ninawambia wapendeni adui zenu, wabariki wanaowalaani wafanyie wema wanaowachukia, na waombee wanaowaonea au wanaowaudhi, na wanaowawinda. (Mathayo 5; 44).
Daudi na Jonathani wote walikuwa waaminifu na watii kwa Sauli – Daudi, kwa sababu Sauli alikuwa mfalme wake, naye Jonathani kwa kuwa Sauli alikuwa Baba yake. Mungu atapendezwa nasi pia ikiwa tutatenda kama walivyotenda. Jonathani alikuwa rafiki wa kweli. Daudi naye alikuwa hivyo.
Upendo wao ulikuwa wa ukarimu na kamwe haukupungua. Wote ni mifano bora sana kwetu juu ya upendo usio na ubinafsi na hilo ndilo hasa Mungu anataka kutuonyesha – Upendo kwa Mungu na upendo kwa ndugu na dada wa Kristo na watoto wao; bila kujifikiria wenyewe, bali wengine. Waulize wazazi wako au Mwalimu kukusaidia kufahamu maneno yanayopendeza ya Paulo kuhusu upendo katika (1 Wakorintho 13: 4 – 8 ). Ni Bwana Yesu Kristo peke yake aliyetupenda namna hiyo. Yatupasa kujaribu kila siku kuonyesha upendo wa jinsi hiyo kwa wengine.
MAELEZO YA NYONGEZA:
SAULI NA JONATHANI WANAKUFA VITANI. 1 Samweli 31
Pigano la mwisho la maisha ya Sauli lilipiganiwa juu ya mlima Gilboa. Waisraeli walikimbia mbele ya wafilisti na askari wengi wa Sauli waliuawa. Kwa huzuni kubwa kuliko zote, shujaa na mwaminifu Jonathani aliuawa pia. Sauli alijeruhiwa vibaya kwa mishale. Wafilisti walikuwa wanamkaribia wakati yeye na mshika / mbebaji silaha zake walikuwa wakikimbia. Sauli alikuwa na dhiki sana (au alidhurika sana). Hakuweza kupona (kutoroka) naye Mungu hangemsaidia angeomba kwake. Alimwomba mshika – silaha wake kumwua, ili asipate dhiki na aibu ya kuuawa na wafilisti, lakini alipokataa, Sauli alichukua upanga wake na kujiua.
Daudi alisikitika mno alipopata habari hizo. Huzuni yake ilikuwa juu ya Sauli na vile vile kwa ajili ya Jonathani (2 Samweli 1: 12 na 17 ).
Jinsi ingelivyokuwa rahisi kufurahia kifo cha adui yake. Lakini Daudi alikuwa mtii kwa mpakwa mafuta wa Mungu na msamehewa sana. Daudi alikuwa amejifunza jinsi zilivyo kuu rehema za Mungu kwake na jinsi anavyotaka sisi tuwe na rehema kwa wengine, hata kama hawastahili (Math. 5: 43 – 48 ). Utaweza kusoma tanzia ya huzuni na nzuri kwa Sauli na Jonathani katika (2 Samweli 1: 17 – 27). Juu ya yote, Daudi alikuwa na huzuni sana kwa kupotea Jonathani, ambaye upendo wake kwake ulikuwa wa vilindi virefu na mtamu kuliko wa mwingine yeyote usingeweza kuwa (2 Samweli 1: 26). Daudi baadae alionyesha upendo kwa Jonathani alipomtunza Mephibosheti, mwana wa Jonathani (2 Samweli 9: 7 ).
MASWALI:
MAJIBU MAFUPI:
Ni yupi katika wana wa Sauli alimpenda Daudi?
Zawadi gani Jonathani alimpatia Daudi kumwonyesha pendo lake?
Mungu alipomchagua Daudi kuwa mfalme Jonathani alifikiria nini juu ya hilo?
Ni wimbo gani ambao Sauli aliusikia ambao ulimfanya awe na wivu kwa Daudi?
Sauli alifanya nini kwa Daudi siku moja Daudi alipokuwa anamchezea nyimbo laini?
Daudi na Jonathani walipokutana shambani, Jonathani alimfanya aahidi nini?
Wakati Jonathani alipomwambia Sauli kwa nini Daudi hakuwepo penye sherehe, Sauli alifanya nini?
Wakati Sauli alikuwa amelala ndani ya pango moja na Daudi, Daudi alifanya nini kwake?
Watu wa Daudi walitaka amwue Sauli. Kwa nini hakuweza kumwua?
Sauli alipoona jinsi ingalivyokuwa rahisi kwa Daudi kumwua ndani ya pango, Sauli alisemaje?
MAJIBU YA KINA.
(a) Ni jinsi gani Bwana Yesu Kristo anatuambia tuwatendee maadui wetu?
(b) Eleza jinsi Daudi alivyolithibitisha hili kwa Sauli.
Sauli na Jonathani walitofautiana kabisa. Mmoja alikuwa adui wa Daudi na mwingine alikuwa rafiki yake.
(a) Ni jambo gani lililosababisha Sauli awe na wivu kwa Daudi? (toa sababu mbili )
(b) Ni kwa nini Jonathani alimpenda Daudi?
Eleza jambo lililotokea wakati Sauli alipopumzika katika pango ambapo Daudi naye alikuwa amejificha katika pango hilo hilo.
MAJIBU YA NYONGEZA.
Eleza jinsi Sauli na Jonathani walivyokufa.
_html_m37b30ab2.jpg)