Kitabu cha Nabii Zekaria MAZINGIRA Zekaria alikuwa nabii mwenzi wake Hagai aliyepeleka ujumbe wa Mungu kwa Wayahudi wa Yerusalemu wakati wa mwanzo mpya baada ya kifungo cha Babeli {post-exilic period). Nia yao kuu katika siku zile za kwanza za huduma yao ilikuwa kuwaamsha Wayahudi kutoka uvivu wao wa ubinafsi na kuwahamasisha kujenga hekalu upya. Zekaria aliendelea na kutoa mafundisho juu ya mambo mbalimbali, kama sehemu ya kazi yake ya kuwaandaa watu kwa wakati wa kuja kwake Masihi uliowakabili. Maelezo yaliyotangulia kitabu cha Hagai yanatoa mambo ya mazingira ya watu hao wawili, yaani Hagai na Zekaria. Msomaji anashauriwa kusoma maelezo hayo kabla ya kuendelea na kusoma uchunguzi unaofuata. Maelezo yanayotangulia Hagai pia yanaonyesha alama za huduma ya Zekaria, pia yanayoonyesha aina ya tofauti baina ya vitabu vya Hagai na Zekaria. MUHTASARI 1:1-6:15 Maono ya Zekaria 7:1-8:23 Swali kuhusu vipindi maalumu vya kufunga 9:1-14:21 Ushindi wa Masihi