Kitabu cha Nabii Obadia MAZINGIRA Kitabu cha Obadia kiliandikwa baada ya kutekwa kwa Yerusalemu na kubomolewa kwake na Wababeli mwaka wa 587 k.K. Hatuna habari zaidi kuhusu huduma ya Obadia kuliko habari zilizoandikwa katika kitabu kifupi kilichopata jina lake. Alikuwa nabii mwaminifu mmojawao aliyeachwa nchini Yuda wakati wa kupinduliwa kwake na wenyeji wake kupelekwa kifungoni. Kitabu chake kinahusu hukumu ya Mungu juu ya Waedomu.