MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.


Hatua 2b Somo la 24 YESU ATARUDI TENA


SALA–Baba wa mbinguni mwenye upendo,tunakushuru kwa ahadi yako kuwa Yesu atarudi tena.Baba tunakuomba umtume mapema kuuweka ufalme wako mwema na ambapo kila mmoja atakuwa mwenye furaha. Ni katika jina la Yesu Kristo tunaomba. Amina


Soma - Matendo ya Matendo 1 mstari 9 - 11


SOMO.

Mitume na marafiki wa Yesu walikuwa na furaha kubwa sana kwa sababu ya Mungu kumfufua Yesu. Yesu sasa alikuwa anakwenda kuishi mbinguni akiwa pamoja na Baba yake,Mungu.Lakini kwanza Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwenda kuwaambia wengine habari njema za mwujiza mkubwa ambao Mungu aliufanya wa Yesu kuwa hai tena milele na milele, na kuwa siku moja atauweka ufalme wa Mungu hapa duniani. Yesu aliwaahidi wanafunzi wake kuwasaidia kufanya mapenzi yake ingawaje yeye kwa muda huo hatakuwepo pamoja nao hapa duniani. Siku moja, ambao ulikuwa ni muda wa Yesu kwenda kuishi na pamoja na Mungu mbinguni. Ndipo Yesu akaenda pamoja na wanafunzi wake hadi kwenye mlima wa mizeituni, karibu na Yerusalemu. Akiwa pale mlimani aliwaambia kazi ambayo itawabidi waifanye kwa ajili yake.

Nakisha, ghafula, Yesu akanyanyuliwa kutoka pale mlimani. Akaenda juu mawinguni na kwa ajili ya mawingu Yesu hakuweza kuonekana. Wanafunzi wake wakaendelea kutazama juu mbinguni. Ndipo waliposikia mmoja akizungumza nao, wakageuka wakawaona malaika wawili wakiwa wamevaa mavazi meupe ambao waliwaambia kuhusu ahadi za Mungu. Mungu aliahidi kuwa siku moja Yesu atarudi tena duniani na akiwa kama vile walivyomwona alipokuwa akienda zake mbinguni. Wanafunzi waliposikia ahadi ya Mungu waifurahi sana. Wote walifanya kazi kwa bidii wakiifanya kazi ambayo Yesu aliwaagiza waifanye.Walimwambia kila mtu kuhusu habari za Yesu na kuhusu ufalme mzuri ajabu ambao atauweka hapa dunian.


Tunautazamia muda ambapo Yesu atarudi tena hapa duniani kuwa Mfalme. Yesu atarudi mapema, wakati Yesu ataaporudi ataketi katika kiti cha enzi katika Yerusalemu na atakuwa Mfalme wa dunia yote. Yesu ataifanya dunia hii kuwa mahali pazuri sana kwa ajili ya kuishi.Atawaponya watu wote wagonjwa na kila mmoja atakuwa ni mwenye furaha.Ataleta wingi wa chakula kuweza kustawi ili kil mmoja awe na chakula tele.


Yesu atawafundisha watu kuishi kwa kufuata sheria za Mungu, na kwa hiyo hakutakuwepo vita tena kama ilivyo leo. Hata wanyama wa (mwitu ) porini watakuwa ni marafiki wa binadamu. Hakuna hata mmoja ambaye ataishi kwahofu katika Ufalme wa Mungu. Bwana Yesu, atarudi upesi sana, na anatatutaka sisi tuwe tayari kwa ajili yake. Kama tukimtii Yesu ndipo tutakapokuwa rafiki zake Yesu Kristo na tutaweza kuingia katika Ufalme wake.Ninataka kuwa rafiki wa Yesu na niweze kuishi katika Ufalme mzuri sana wa Mungu, na wewe unapenda?