MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.
Hatua 2b Somo la 23 YESU ALIKUFA NA AKAWA HAI TENA
SALA – BWANA Mungu, tunayo huzuni sana kusikia kuwa alikufa, lakini tunafahamu kwamba ilikuwa ni sehemu ya mpango wako kwa ajili ya dunia. Tunakuomba utusaidie tuweze kukutii wewe, kama vile Yesu alivyokuwa anakutii, na utusaidie ufahamu wetu uweze kukua. Ni katika jina la Yesu Kristo ninaomba. Amina
SOMA - Marko 15 mstari 17 - 19
SOMO,
Yesu kila wakati alikuwa anajitahidi sana kuwafundisha watu wampende Mungu na wapendane pia. Aliwafundisha kuhusu Ufalme wa Mungu ambao atapokurudi atauweks hapa duniani. Naye Yesu ndiye atakuwa Mfalme wa huo Ufalme. Watu wengi sana walimpenda Yesu na pia walipenda kusikiliza maneno yake. Lakini watawala waliopaswa kuwafundisha watu kama vile Yesu alivyokuwa akifundisha, wakamwonea wivu Yesu kwa sababu watu walipenda kumsikiliza badla y kuwasikiliza wao.
Pia Yesu aliwasaidia wagonjwa kwa kuwaponya, na hata kuwafufua watu waliokuwa wamekufa. Masikini walimpenda Yesu, lakini watawala wakafikiria kuwa kamwae hawatapata watu wa kuwasikiliza tena, wakati Yesu akiwa angali anaishi. Kwa hiyo wakafanya shauri la kumwua Yesu. Yesu hakuwa amefanya kosa lolote, lakini baadhi ya watu waovu waliamua kumsingizia maneno ya uongo kuwa ndiye aliyesema.Ndipo wakampeleka Yesu kwa Pilato,ambaye alikuw ni mtawala wa Rumi.Na Pilato akasema kuwa Yesu ni lazima afe.Kwa hiyo maaskari wakampeleka hadi kwenye mlima nje ya mji wa Yerusalemu.
Walimwekwa Yesu juu ya msalabaili afe, pamoja na wahalifu wawili ambapo waliwekwa mmoja mkono wake wa kulia na mwingine mkono wake wa kushoto kwake Yesu. Na ndipo Yesu alipoonyesha jinsi alivyokuwa mtu shupavu na jasiri. Alifahamu kuwa watawala na maaskari kila walilolitaka ili kumuumiza, hata hivyo aliwasamehe. Katika sala yake aliwaombea kwa Mungu, akasema, Baba, uwasamehe dhambi zao, maana hawajui walitendalo. Kisha Yesu akamwangalia mama yake na wanaeunzi wake waliokuwa wamesimama karibu. Alifikiria jinsi mama yake atakavyokuwa na huzuni sana, kwa hiyo akamwambia mmoja wa wanafunzi ili amtunze kama vile ndiye mama yake hasa. Na akamwambia mama yake amtunze huyu mwanafunzi, ili asijisikie upweke na kuwa na huzuni.
Na hatimaye Yesu akafariki, na anwani juu ya msalaba yenye maandishi haya: "MFALME WA WAYAHUDI". Watu hawakuamini kama itakuwa kweli, lakini tunafahamu kabisa kuwa Yesu atakuwa Mfalme wa Ufalme wa Mungu. Rafiki wa Yesu akauchukua mwili wake na kuupaka manukato kisha akauweka mwili wake ndani ya sanda ya kitani safi na kumzika ndani ya kaburi ambalo mtu hajazikwa ndani yake karibu sana na bustani. Kisha akavingirisha jiwe penye mlango wa kaburi.
Siku ya tatu Mungu alituma malaika wake kwenda kumfufua Yesu. Wakarivingirisha jiwe pale penye kaburi na wakamfufua Yesu. Na baadhi ya wanawake walikwenda kaburini alfajiri na mapema ili kuupaka manukato mwili wa Yesu. Ni mshangao ulioje waliokuwanao walipokuta jiwe lilikuwa limewekwa pale kaburini likiwa limeodolewa penye mlango wa kaburi. Malaika wakawaambia, Msiogope. Yesu yu hai. "Enendeni mkawaambie wanafunzi habari hii njema"
Ndipo wanawake walipokwenda mbio kuwajulisha mitume.Ilikua ni habari njema ilioyoje! Jinsi walivyokuwa na kubwa waliposikia kuwa Yesu yu hai tena! Yesu akaenda kuongea na rafiki zake na wot wakafurahi sana kwa kuwa Mungu alikuwa amemfufuka Yesu yu hai milele na milele.Hii bado ni habari njema tena ya kushangaza. Na inatutupatia na sisi furaha pia.