MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.



Hatua ya 2b Somo la 22 YESU ANAINGIA YERUSALEMU



SALA – BWANA Mungu mpendwa,Tunaomba ili ufalme wako uje upesi, wakati ambapo tutaweza kushangilia kwa furaha na kumkaribisha Yesu ambaye ni mfalme wetu, ni katika jina la Yesu Kristo tunaomba haya, Amina.


SOMA - Mathayo 21 mstari 6 - 9


SOMO.

Wakati Yesu na wanafunzi wake walipokuwa wanakwenda kuingia Yerusalemu, mji mkuu. Walipokuwa njiani walifika katika kijiji kidogo. Yesu akawaita wanafunzi wake wawili akawaambia "Enendeni mpaka kijiji kile kinachowakabili na mtamwona punda akiwa amefungwa kando ya barabara, mfungueni, mniletee."


Wanafunzi wale wawili wakaenda haraka mara moja. Na walipoingia katika kijiji kile, walimkuta punda akiwa amefungwa kando kando ya barabara, kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Wakamfungua na kumwongaza njia,na watu wawili waliokuwa wamesimama pembeni, walipowauliza, "Kwanini mnamfungua punda?"


Na Yesu alikuwa amewaambia wanafunzi jinsi ya kuwajibu ikiwa mtu yeyote angewauliza, Kwa hiyo wajibu, "Bwana Yesu anahaja naye," na kama Yesu alivyokuwa amewaambia waseme, basi wale watu wakawaruhusu wanafunzi wamchukue yule punda. Yule punda hakuwa na tandiko juu yake, hivyo badhi ya wanafunzi wakatandika nguo zao juu yake, na Yesu akakaa juu yake na kumwongoza yule mwanapunda kuelekea Yerusalemu. Na alipokaribia kuingia mjini, watu wengi wakatoka mjini ili kumlaki Yesu. Walipomwona Yesu akiwa amepanda mwanapunda kama vile Mfalme, walifurahi sana. Watu wakavunja matawi ya mitende ndipo wakaanza kushangilia kwa furaha. Wakawa wakimzunguka Yesu huku wakishangilia na kusema, "Hosana, Ndiye mbarikiwa, Mfalme ajaye kwa jina la Bwana"


Mkutano uliendelea kuongeza idadi ya watu sana, watu wengi wakaziidi kuongezeka walipokuwa wakisikia kelele za furaha na kuimba nyimbo. Watu wakatupa nguo zao barabarani ili Yesu apite juu yake kana kwamba ni zulia kubwa lililokunjuliwa katika barabara yote. Ilikuwa ni siku iliyo kuu. Nakila mtu alikuwa na furaha kwa jinsi walivyokuwa wakipiga kelele za furaha, "Hosana, Ndiye mbarikiwa, Mfalme ajaye kwa jina la Bwana".


Na hatimaye, Yesu akaingia Yerusalemu. Matawi ya mizeituni yaliinuliwa juu, nguo zenye rangi tofauti zilitandazwa kama zulia, wanaume, wanawake na watoto waliimba nyimbona zaburi. Kila mtu alikuwa ni mwenye furaha na kumshangilia Yesu Mfalme mkuu amekuja Yerusalemu.