MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.


Hatua 2b Somo la 21 WANAWALI KUMI


SALA – BWANA Mungu mpendwa, ninakushukuru sana kwa ajili ya mambo mema niliyonayo. Ninaomba unisaidie sasa ili niwezekutafakari kwa makini kuhusu habari iliyo ndani ya Biblia yako. Ni katika jina la Yesu Kristo. Amina.


SOMA - Mathayo 25: 1-3


SOMO.

Je, umewahi kwenda arusini? Inafurahisha sana tena unakuwa ni wakati wa furaha. Fundisho hili linahusu arusi na kuhusu wanawali kumi ambao walitakiwa kuhusika katika arusi. Arusi ilikuwa inakwenda kufanyika. Wanawali kumi iliwapasa wawepo na wote walifurahi sana. Bwana arusi angefika muda maalumu na ndipo wote wangekwenda pamoja na bwana arusi ili kuwasha taa zao wamumlikie njia anapopita. Muziki na kucheza vinakuwepo na kila mtu anakuwa ni mwenye furaha.


Lakini huwa wanawali huwa hawafahamu bwana arusi anafika muda gani. Mara nyingi inawapasa kusumsubiri muda mrefu sana, na huwa wanakuwa tayari kuwasha taa zao mara tu bwana arusi anapofika. Wote wanakuwa wamevaa mavazi mazuri maalumu ya arusi, wanakuwa wanakuwa wamemeka maua kuzunguka vichwa vyao nakila mmoja anakuwa na taa il kumumlikia njia bwana arusi anapopita. Wanawali watsno walikuwa wenye busara na walikuwa wamekuja na mafuta ya akiba ikiwa itabidi kusubiri kwa muda mrefu. Lakini wanawali wengine watno walikuwa ni wapumbavu na hawakuwa wameleta mafuta ya akiba.


Na walipokuwa wanasubiri kwa furaha walizungumza kuhusu arusi. Hata ikawa baada mrefu walichoka kuzungumza.Bwana arusi alikuwa hajafika, walikaa chini wakapumzikana, na taa zao zikiwa zimewekwa tayari kkutumika kwa upande wao.


Bwana arusi alipokawia ndipo na wanawali hawa wakalala usingizi mzito sana mmoja mmoja. Ndipo 'waliposikia kelele za shangwe!'. "Bwana arusi anakuja, nendeni nje mkamlaki". Na wanawaali wote wakaamka. Wale wanawali watano wapumbavu wakasema, "Aa! Taa zetu zinazimika. Tupatieni mafuta yenu kidogo. "Wale watano wenye busara wakawajibu "Hapana" maana hayatatutosha sisi na ninyi. Nendeni haraka sasa hivi mkanunue mafuta." Ndipo wale wanawali wapumbavu wakashika njia kwenda kutafuta mahali ili wananunue mafuta.


Kisha wale watano wenye hekima wakaondoka kwa furaha kumlaki bwana arusi,alikuja akiwa amevaa mavazi ya arusi na wale wanawali watano wakaziwasha taa sana zao kumumlikia njia bwana arusi na wakaenda kwa furaha pamoja naye akaingia arusini. Na wote waliokuwa tayari walipokuwa ndani mlango ukafungwa. Na wote wakafurahi maana kulikuwa na muziki na kucheza.


Baada ya muda kupita mlango ukagongwa sana. Wale wanawali watano wapumbavu walikuwa wamerudi, wakasema "uturuhusu tuingie ndani", "Tufungulie mlango," Lakini walikuwa wamechelewa Sauti kutoka ndani ilisema. "Siwajui ninyi,". "ni wale walio tayari ndiyo wanaweza kuwa pamoja nami katika arusi yangu".