MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.
Hatua ya 2b SOMO LA 20 ZAKAYO
SALA –BWANA Mungu,tunaomba utusaidie kutambua na kukiri tunapokuwa tumemdanganya mtu kwa sababu sisi ni wachoyo. Tunakuomba utujalie ujasiri wa kusema tumekosa na tuombe msamaha na kisha tujitahidi kufanya vyemanekwa usahihi kwa kadiri tuwezavyo. Ni katika jina la Yesu Kristo tunaomba. Amina.
SOMA - Luka 19 Mstari 2 - 5
SOMO.
Yesu na wanafunzi walikuwa wanatembea katik mji wa Yeriko.Na siku hiyo watu walikuwa wamekusanyika katika mji wa Yeriko. Nahapo aliishi mtu mmoja aliyeitwa Zakayo. Ingawaje Zakayo alikuwa ni tajiri sana hatahivyo alikuwa ni mpweke na asiye kuwa na furaha.Wakati huo Wayahudi hawakuwa na mfalme wao wenyewe ambaye ni mwisraeli kwa maana nchi yao ilikuwa ikitawaliwa na Utawala mkuu wa Rumi katika nchi yao. Na watu walitakiwa walipe fedha, ambayo iliitwa kodi kwa mtawala.
Na katika kila mji alikuwepo mtu ambaye alikuwa akikusanya fedha hii kwa y utawlaa wa Rumi, na Zakayo, amabaye ndiye mtu aliyekusanya fedha ya kodi katika mji wa Yeriko. Na hii ndiyo sababu hakuna mtu aliyekuwa anampenda. Hawakupenda kulipa kodi kwake. Na mara nyingi alidawanganya watu hata akawasababisha wakalipa ushuru mkubwa sana, Kulikuwa na kitu ambacho Zakayo alikitamani sana kuliko kitu chochote. Alitaka kumwona Yesu. Alikuwa amesikia mengi sana kuhusu Yesu, kuhusu miujiza aliyoifanya, uponyaji na upendo wake kwa kutendea mema maskini na waliokuwa wapweke. Mara nyingi alifikiria ni jinsi gani itakuwa vizuri ikiwa ataweza kumwona Yesu siku moja na kuongea naye.
Alikuwa hajawahi kumwona Yesu, kwa hiyo unaweza kuwa nauhakika wa furaha aliyokuwa aliposikia kuwa Yesu anakuja kupitia njia ile. Alikimbia akatanglia mbele mahali ambapo angeweza kuwaona umati wa watu.
Lakini hakuweza kumwona Yesu pamoja na jitihada zote alizozifanya. Maana Zakayo alikuwa ni mfupi sana na watu walikuwa wakimchukia, aliwasukumu watu alipokuwa akijitahidi kupita katikati ya umati wa watu. Na hatimaye alifikiria ajaribu njia nyingine.
Kwa hiyo akakimbia akitangulia mbele ya umati wa watu, kuona kama ataweza kupata kitu ambacho kimeinuka aweze kusimama juu yake ili aweze kuona vichwa vya watu waliokuwa wamemzunguka Yesu na pia amwone Yesu. Ndipo alipouona juu ya mkuyu uliokuwa kando ya njia ile. Matawi yake hayakuwa mbali sana, hivyo akawa amesimama juu ya tawi ambalo lilikuwa ni la kwanza kutoka kwenye shina la mkuyu. Na tawi la pili lilikuwa ni zuri kwake maana lilikuwa na majani mengi ambayo yalisabbisha watu wasimwone, yeye aliweza kuona kila kitu kwa urahisi; lakini kwa ajili ya majani watu wasingeweza kumwona yeye.
Mkutano ukakaribia mahali alipokuwa, kweli, Yesu alikuwepo. Hebu fikiria uso wake Zakayo ulivyofurahi. Kisha umti ule wa watu ukawa unapita ule mkuyu, Yesu akatazama juu akamwambia, "Zakayo, shuka upesi, kwa kuwa leo imenipasa kushinda nyumbani mwako." Ni furaha kubwa iliyoje kwa ajili ya mtu mfupi na mtoza ushuru! Zakayo lishuka chini na kamkaribisha Yesu kwa furaha pamoja na wanafunzi wake nyumbani kwake.
Wakati alipomwona Yesu ameingia ndani na akiwa amekaa kwenye kiti lianz kuhangaika moyoni mwake kama Yesu alimfahmu kuwa yeye ni mtu wa tabia gani. Yesu alikwa ni mtu mwenye huruma na kwa hiyo aitaka Yesu amfikiri mema yeye pia. Hili lilimfanya ahangaike sana kwa kuwa alikuwa ni mchoyo na alipata pesa kwa watu kwa udanganyifu.
Hatimaye akaamua moyoni mwake kuweka wazi makosa yake yote aliyoyafanya. Akamwambia Yesu, "Bwana, nitawapatia nusu ya mali yangu masikini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu kitu kwa hila nitamrudishia mara nne." Ndipo Zakayo akahisi furaha moyoni mwake lipokwisha sema hili. Lakini alikuwa na furaha zaidi alipotambua kuwa Yesu alipendezwa naye.