MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.


Hatua ya 2b Somo la 19 MWANAMKE ALIYEKUWA AMEPINDA MGONGO


SALA – BWANA Mungu,tunaomba utusaidie tukumbuke kukushukuru wewe kwa ajili ya mambo yote katika maisha yetu na hasa kwa jinsi wewe unavyotutunza. Tunakushukuru kwa ajili ya madaktari na wauguzi wanaowasaidia wagonjwa.Baba tunaomba umtume Yesu aje duniani ili maumivu na magonjwa yasiwepo tena.Ni katika jina la Yesu Kristo. Amina.


SOMO - Luka 13 mstari 11 - 13


SOMO.

Katika nchi ya Israeli ,palikuwa na mwanamke wa mzee aliyeishi katika kijiji.Aliweza. kuonekana ndani kila juma ikiwa mtu ataangalia wakati mlango wa nyumba yake ulipokuwa umefunguliwa akifanya kazi zake za nyumbani,wakati mwingine akisaga ngano ili atengeneze mikate midogo au alipokuwa akifagia sakafuni.


Hata hivyo kila alilolifanya,lilichumchukua muda mrefu sana kwa kuwa alifanya polepole. Hakuweza kufanya kwa haraka kama wanawake wengine. Mwanamke huyu alikuwa akiumwa mgongo. Alikuwa na maumivu makali sana ya mgongo na mgongo wake ulikuwa umepinda na alitembea kwa shida sana tena alitembea huku kiwa ameinama. Tatizo hili la mgongo lilikuwa ni miaka mingi na kwa muda wote hakuwezakusimama wima akanyoka. Ikawa siku ya sabato mwanamke huyu alikwenda katika sinagogi,au kanisani kamakawaida yake.Na ingwaje haikuwa mbali na mahali alipoishi,ilimbidi aamke mapema kwakuwa ilimchukua muda mrefu kujitayarisha. na ikiwa ni pamoja na kufika kwa sababu alitembea polepole.


Alipomaliza kula kifungua kinywa (chakula cha kwanza cha asubuhi), aliondoka mapema kuelekea kwenye sinagogi. Tii, tii, tii ndivyo ilivyosikika fimbo yake alipokuwa akitembea katika njia. Maumivu ya mgongo yaliendelea kumuuma na alikuwa akipumzika hapa na pale. Alifurahi sana wakati alipofika lilipokuwa Sinagogi na aliketi akisubiri huduma ianze.Alikupowa ameketi pale, mtu mmoja alimwambia kuwa, Yesu, ambaye ni Mwalimu mkuu ameingia ndani ya Sinagogi.


Na kisha, kwa mshangao alimsikia Yesu akimwita yeye. Hakika hakumaanisha YEYE- mwanamke mwenye kupinda mgongo! Na watu wote waliokuwa karibu naye wakashangaa na wakaanza kumsukuma ili aende mbele. Wakamwaambia "Yesu anakuita wewe," Taratibu, akatembea akielekea Yesu alipokuwa,akamtazama Yesu kwa ajili ya huruma yake na uso wake uliokuwa na tabasamu. Akasema "Mwanamke," akamgusa mgongo wake uliopinda, "Umefunguliwa katika udhaifu wako."


Na saa hiyohiyo akanyoka,akasimama sawasawa. ulemwanamkekasema, "Atukuzwe Mungu," Ni ajabu iliyoje kuweza kusimama kama wengine pasipo maumivu tena.Na watu wote wakamtukuza Mungu, ajili ya wema wake. Ni mtu mmoj tu ambaye hakufurahishwa. Naye alikuwa ni mkuu wa sinagogi aliyekasirishwa na kitendo cha Yesu kuponya siku ya sabato, na kwa kuwa alikuwa karibu,akawaambi makutano; "Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi. Basi njooni mponywe katika siku hizo, wala siyo katika siku ya sabato." Yesu akasema "Enyi wanafiki, "Kama ng'ombe au punda wako anahitaji kunywa maji au anaumwa, unampatia huduma inayotakiwa siku ya sabato.Kwa kweli huyu mwanamke alistahili msaada huu siku ya sabato."


Ndipo yule mkuu akaaibika kutokana na hayo aliyokuwa amesema na watu wote wakamtukuza Mungu kwa sababu ya mambo matukufu ambayo Yesu aliyatenda.