MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.


Hatua ya 2b Somo la 18 SHILINGI ILIYOPOTEA


SALA– BWANA Mungu, tunakushuru kwa ni Baba mwenye upendo, utandelea kutusamehe tunakuomba msamha kwa ajili ya makosa yetu tuliyoyafanya. Ni katika jina la Yesu Kristo tunaomba, Amina.


Soma - Luka 15 mstari 8 – 10


SOMO

Habari hii aliisema Yesu. Mara nyingi tunafanya mambo ambayo ni makosa. Ni sawa na kupotea asiwe na Mungu tena. Na tunapoomba tena msamaha,jisi inavyomfurahisha Mungu kutupata.Anafurahi sana akiwa pamoja na malaika zake mbinguni. Siku moja asubuhi wakati jua lilipokuwa linaangaza sana,mwanamke analikuwa na kazi katika nyumba yake ndogo. Ilikuwa na imeezekwa kwa kuinuliwa sana paa zake.


Nyumba yake ilijengwa kwa mawe na tope na madirisha yake yalikuwa ni madogo kuweza kufanya ndani yake kuwa baridi wakati wa joto sana ilipofika mchana. Na ilifanya chumba kiwe na giza.


Mme na wana wake walikuwa wamekwenda kazini. Ndipo alipofagia na kufuta vumbi.Yule mwanamke alikuwa na shilingi kumi za fedha ambazo alizipenda sana. Alikuwa hajawahi kuwanazo tangu aolewe. Huenda alizifunga kamba pamoja na kuzivaa kama utepe usoni pake. Na mara nyingi alicha kufanya kazi kwa muda ili tu aziangalie sarafu zake hizo ambazo zilinga'aa sana.


Kisha baadaye,akaanza kutayarisha chakula cha mchana. Kwanza ilimpasa asage kwanza ngano apate unga. Unga ulipokuwa tayari alichanganya na maji ili kutengeneza mikate midogo na kisha akaoka kwenye moto.


Kisha aliandaa chakula kwa kuuoka mkate huo kwenye moto.


Ghafla akaangalia zile sarafu zake. Alihuzunika sana alipozikuta zikia nitisa tu! Ah, masikini! Mwanake huyu atakuwa alikuwa ameiangushia chini sarafu hiyo nyingine. Alihuzunika sana kwa kuwa moja kati ya sarafu zake azipendazo ilikuwa imepotea. Marafiki zake walimhurumia na wakatumaini kuwa ataipata upesi shilingi yake.


Ndipo yule mwanamke akainua mkeka na kuangalia chini yake, lakini ile shilingi haikuwepo pale. Alionekana ni mwenye kuhuzunika kwa ajili ya shilingi yake hiyo. Alifagia chumba kizima na akaiinua taa yake juu ili aone vizuri, hata hivyo hakuweza kuiona shilingi.


Akafagia kona zote za chumba. Ndipo mwisho baada ya kutafuta kwa bidii sana na kwa kufagia, akaiona shilingi, ilikuwa imeviringika hadi kwenye kona ya chumba penye giza. Alifurahi sana hata asiweze kuificha furaha yake, akawaita majirani na marafiki zake kwa kuwa ameiona shilingi iliyokuwa imepotea. Akawaabia, "Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena ile sarafu iliyopotea".


Na sisi tunapokuwa tumetenda dhambi ni kwamba tunakuwa tumepotea kwa Mungu. Jinsi Mungu anavyohuzunika. Lakini tunapomwambia Mungu, kuwa tunaomba msamaha, anakuwa ametupata tena. Jinsi Mungu anavyofurahi anapokuwa ametupata tena. Anafurahia sawana yule mwanamke aliyeipata tena shilingi.