MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.
Hatua ya 2b Somo la 17 MSAMALIA MWEMA
SALA – BWANA Mungu, tunaomba utusaidie kuwa wema na tuweze kumsaidia mtu yeyote mwenye matatizo. Tuonyeshe jambo tunalopaswa kufanya ili kuwasaidia. Ni katika jina la Yesu Kristo ninaomba. Amina
SOMA - Luka 10 mstari 30 - 32
SOMO
Somo hili ni mfano mwingine aliousema Yesu. Alikuwa akituonyesha kuwa tusaidie na kumtendea mema mtu yeyote mwenye shida kwamba ni mtu tunayempenda au la. Palikuwa na mtu aliyekuwa anasafiri akitoka Yerusalemu,mji mkuu akielekea mji wa Yeriko,uliokuwa chini bondeni penye kijani kibichi karibu na mto Yordani. Mtu huyu alikuwa na haraka ili afike Yeriko kwa hiyo aliondoka alfajili na mapema akiwa peke yake.
Na kadiri alivyokuwa akisafiri ndivyo njia ile mtelemko wake mkali ulivyozidi kuongezeka na barabara ilipita katikati ya miamba miliwili iliyoinuka juu. Kulikuwa na miamba mikubwa sana iliyoshikamana pande zote mbili. Mtu huyu akafanya haraka ili kupita eneo hili lililokuwa ni la hatari sana.
Na kasha akasikia nyayo za mtu anayetembea akija nyuma yake. Akageuka atazame nyuma, lakini mikono ya watu katili ikamshika na kumwangusha chini na kisha wakamvuta na kumweka kando ya njia. Alijikuta akiwa amezungukwa na wanyang'anyi. Walimwibia mfuko wenye pesa, wakamvua nguo, wakakimbia wakiwacha akiwa anavuja damu mwili mzima na alikuwa amezimia. Yule mtu akajaribu kuinuka, lakini akashindwa maana alikuwa ameumizwa sana na akawa hana nguvu kabisa.Jua likamwakia, likiunguza mwili wa masikini huyu!
Alilala pale masaa yote akiikiria kama kweli atakuja mtu amsaidie. Hatimaye, akasikia kishindo cha nyayo. Kuna mtu anakuja. Huyu alikuwa ni kuhani. Kwa kweli mtu huyu alipaswa kumsaidia kabisa. Lakini kuhani akapita kando tena akapitia upande wa pili wa barabara. Yule mtu akajaribu amwite yule kuhani, kini alishindwa. Kwa kuwa ulimi wake ulikuwa umekwisha kukauka na tena ulikuwa umevimba.
Muda baada ya muda ukawa-unapita tu. Yule mtu hali yake ikawa inaendelea kuwa mbaya zaidi. Na tena akasikia kishindo cha nyayo. Kishindo cha yule mtu kikawa kimemkaribia.Y ule mtu aliyejeruhiwa akatazama, akamwona Mlawi akipita kando. Yule mtu akakoroma, lakini Mlawi akavuka na kupita upande wa pili na akaenda zake.
Yule mtu akawa amelala pale kwa muda mrefu sana.Ikawa sasa inakaribia kuingia giza. Mara hii tena akasikia kishindo cha nyayo. Yule mtu hakutazama tena maana alikuwa mekwisha kukata tamaa ya kupata msaada. Kisha akahisi mikono ya huruma ikimwinua. Alipo kwa mshangao alipofungua macho yake alimwona mtu ambaye ni mgeni, Msamalia. Yule mtu akampaka mafuta na divai majeraha na akamfungamajeraha yake taratibu.
Msamalia alimtumia nguo yake kufunga majeraha ya yule mtu na akamnyanyua na kumweka juu ya punda wake. Wakatembelea polepole kwenye barabara. Msamalia hakuwa amepanda punda tena, kwa kuwa yule mtu alikuwa mahututi asingeweza kukaa peke yake pasipo kushikwa na mtu, hivyo msamalia alikuwa akitembea huku mikono yake imemshikilia. Walipofika nyumba ya wageni, Msamalia alimwita mtunzaji wa nyumba ya wageni aje kumsaidia. Ndipo walipomnyanyua yule mtu nakumlaza kitandani.
Msamalia alikesha usiku wote akimhudumia. Na asubuhi akamwita mtunza nyumba ya wageni, ''Inanipasa niendelee na safari yangu, akamwambia; chukua hizi dinari mbili, naomba umtunze huyu. Na chochote utakachoghariwa zaidi, miimi nitakaporudi nitakulipa''
Yesu akauliza, "ni mtu yupi aliyemhurumia yule mtu aliyekuwa amejeruhiwa?"