MASOMO YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA WAISHIO MBALI NA EKLESIA.
MCHUNGAJI MWEMA
Hatua ya 2b Somo la 16
SALA – BWANA, Mungu, ninakushukuru kwa ajili ya Mwanao Yesu Kristo aliyewapenda wanadamu kupita upeo hata akautoa u hari wake ili kuwaokoa. Nifuraha kubwa kiasi gani kujua kwamba Yesu alitupenda na kutujali na kwa katika jina la Yesu ninaomba, Amina
Soma – Luka 8 mstari 41-42
Somo. Hii ni habari nyingine ambayo Yesu alisema inayohusu Mchungaji. Palikuwa na Mchungaji mwema aliyekuwa na kundi kubwa la Kondoo na akiwa tunzo wanakondoo. Wote walimjua na kumpenda na yeye aliwajua wote kwa majina. Walimfuata kokote alikokwenda. Kama mchungaji mgeni angekuja na kuwaita ili wamfuate, wengemkimbia, lakini kama mchungaji wao angekuja, wote wengemkimbilia na kumfuata popote ambako angekwenda.
Asubuhi huwatangulia kondoo wake mahali penye malisho mazuri, na kwa kawaida huwapeleka penye mito yenye maji mazuri na ya baridi. Huwalinda mchana kutwa akiwalinda wasishambuliwe na wanyama mwitu. Wakati mwingine mnyama mwitu angekuja kuwaiba wanakondoo, lakini hata hivyo asingeweza kupata hata mmoja maana mchungaji mwema alikuwa mwangalifu sana wakati wote na kama angekuja mchungaji angemfukuza au kumwua.
Na endapo mchungaji angetaka kusafiri angemweka mtu mwingine kuwalinda kondoo wake. Wakati mchungaji mwema aliposafiri, mbwa mwitu alikuja na yule aliyeachiwa kondoo badala ya kumfukuza mbwa mwitu, yeye alikimbia kwa sababu aliogopa na kujali zaidi maisha yake kuliko uhai wa kondoo. Mbwa mwitu akawararua baadhi ya kondoo na waliobaki wakakimbi. Haikuwa salama kwa kondoo kuwa porini peke yao usiku. Maana mbwa mwitu wengi walikuwa wakizunguka zunguka usiku eneo lile.Jua lilipoanza kuzama mchungaji huwaiata kondoo na kuwapeleka nyumbani hadi kwenye zizi la kondoo.
Zizi hili lilizungushiwa ukuta mrefu kwenda juu, uliojengwa kwa mawe na juu yake paliwekwa miiba ili kuzuia wezi. Kulikuwa na mlango penye ukuta ambapo mchungaji mwema angepitisha kondoo wake akiwa hesabu wakati wanapoingia. Ndipo wanakondoo hulala chini ya mama zao kwa amani. Mchungaji mwema hulala nje ya mlango akiwalinda kama kuta tokea hatari.
Wakati mwingine kama mwizi angekuja kuiba baadhi ya kondoo. Asingeweza kujaribu kupitia mlangoni kwa sababu mchungaji angemwona na hata kama angejaribu kupanda ukuta pole pole. Hata hivyo kondoo wangemtambua kuwa huyu ni mtu mbaya na kwa sababu hiyo kondoo wangemkimbilia mchungaji wao.
Kwa hiyo mchana na usiku, kondoo walikuwa salama kwa kuwa na mchungaji wao mwema. Yesu akawambia Wanafunzi wake kuwa yeye ni mchungaji mwema na wao na sisi ndiyo kondoo wake.
Yeye anatupenda na anatujua kwa majina yetu. Anatulinda siku zote, aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. ni Furaha kubwa iliyoje kuwa na mchungaji mwema na mwenye upendo mkuu namna hii.