MASOMO YA SHULE YA JUMAPILI YA WAKRISTADELPHIA KWA NJIA YA BARUA. Hatua ya 2b Somo la 15 BINTI YAIRO. SALA-Bwana Mungu,tunakushukuru kwa kuwa sasa tunaweza kukukaribia nakwa kuwa unaweza unasikia maombi yetu,utusaidie tuweze kuamini na kusadiki.Kwa Jina la Yesu Kristo,Amina. TUNASOMA -Luka 8:41-42 SOMO Siku moja Yesu alivuka Ziwa kwa mtumbwi kwenda katika mji wa Kaperanaumu.Alikuta kundi kubwa la watu wakimsubiri.Alipotoka katika mtumbwi watu wakamzunguka.Miongoni mwa watu hao alikuwemo mtu mhimu.Alikuwa ni mkuu wa sinagogi.Alikuwa na tatizo kubwa sana ,alikuja kwa Yesu ili kupata msaada.Mtu huyu akamkimbilia na kupiga magoti mbele ya Yesu.Jina la mtu huyu anaitwa Yairo. Yairo akamwambia Yesu kuwa binti yangu anaumwa sana.Walikuwa wanahofia kuwa atakufa.Alikuwa amesikia maajabu mengi ambayo Yesu alikuwa ameyatenda,na alikuwa amekuja kwa Yesu kuomba msaada ili aende kumponya binti yake.Yairo hakuwa na furaha kwa sababu binti yake huyo alikuwa ndiye mtoto wa pekee na kama angekufa asingebakia na mtoto yeyote.Yesu akamhurumia Yairo. Yesu akaanza safari ya kwenda pamoja na Yairo nyumbani kwake.Baadhi ya watu wengi wakamfuata na kila mtu alipenda kumkaribia Yesu.Miongoni mwa watu hao alikuwemo mwanamke ambaye alikuwa mgonjwa kwa miaka kumi na miwili.Mwanamke huyu alikuja kwa Yesu ili aponywe.Na baada ya kuponywa Yesu alizungumza naye. Yairo alimwomba Yesu afanye haraka kwa kuwa binti yake alikuwa mgonjwa sana.Yairo aliendelea kumngoja Yesu afike nyumbani kwake.Wakiwa wamekaribia kufika nyumbani mjumbe akaja na kumwambia Yairo kuwa binti yake amekwisha fariki.Yairo akahuzunika sanasana.Kwa kuwa walikuwa wamechelewa sana. Lakini Yesu alipoambiwa kuhusu kufariki kwa mtoto wa Yairo,alimwambia Yairo kuwa asihuzunike kwa sababu ikiwa anaamini mambo yatakuwa mazuri.Walipofika nyumbani kwa Yairo walikuta watu wengi sana pale.Walikuwa wakilia na kuomboleza kwa sababu binti yule alikuwa amekufa. Yesu akawatoa watu wote ndani ya chumba alimokuwa yule maiti.Lakini akawaacha mama na baba wa yule kijana na wanafunzi wake watatu wakabakia mle ndani.Na kisha Yesu akaenda pale alipokuwa yule maiti akamshika mkono na kusema: “Binti,amka”.Binti yule akaamka kama vile aliyekuwa amelala usingizi.Yairo na mke wake wakafurahi sana sana.Na hawakuwa na lakusema. Yesu akamfikiria sana yule binti.Binti alipokuwa mgonjwa alikuwa hajala chakula kwa muda.Na sasa kwa kuwa amekuwa mzima mambo yamekuwa tofauti;Yesu akasema : “Mpeni chakula ale” maana “ana njaa”. Yairo alikuwa na furaha kubwa sana na akamshukuru Yesu kwa yale aliyomtendea. Yesu akawa ameipatia furaha tena familia iliyokuwa na huzuni nyingi.